Thursday, February 28, 2019

Kanuni 15 za Ujasiriamali ambazo ni lazima uzifahamu

Ikizingatiwa kuwa upatikanaji wa ajira umekuwa wa shida sana, watu wengi hujikuta wakiwa na chaguo la kuwa wajasiriamali pekee kwenye maisha yao.

Wengi hutamani au hata kujiingiza kwenye ujasiriamali, lakini siyo wote wanaofanikiwa kutokana na kutokufahamu kanuni muhimu za ujasiriamali. Ni wazi kuwa ili uanzishe kitu chochote chenye mafanikio, ni lazima ufahamu kanuni za kukifanya kitu hicho jinsi ipasavyo.

Ikiwa wewe ni mjasiriamali, au unataka kuwa mjasiriamali, basi fuatilia makala hii ili nikufahamishe kanuni 15 za ujasiriamali.

1. Kuwa mtatuzi wa matatizo
Ujasiriamali ni zaidi ya kupata pesa, ni lazima kwanza utatue changamoto ya mtu ndipo utaweza kupata pesa kutoka kwa mtu husika. Ni muhimu ukafahamu kanuni hii kama mjasiriamali kwani hutojikita kutafuta pesa bali utajikita kutatua matatizo ya watu.

Kwa mfano kama kuna tatizo la upatikanaji wa mboga katika mji au eneo unalokaa, ikiwa wewe utaleta mboga katika eneo hilo ni wazi kuwa watu watakupa pesa ili uwape mboga. Hivyo ni muhimu kila mara ukatafuta changamoto ukaitatua, nawe bila shaka utapata pesa za uhakika.

"Pesa ni matokeo ya kutatua shida ya mtu"

2. Kuwa na maono
Hakuna ujasiriamali bila maono. Kuwa mjasiriamali bila maono ni sawa na kuendesha gari isiyokuwa na usukani. Maono katika ujasiriamali yatakuwezesha kukuongoza ufanye nini na kwa muda gani. Ni lazima ujiulize kuwa unataka kuwa nani, lini na unataka kufanya nini baadaye? Jonathan Swift alisema maono ni sanaa ya kuona kile ambacho wengine hawaoni. Ni lazima uwe na lengo na ufanye bidii kulifikia.

"Wajasiriamali waliofanikiwa ni wale walioweza kubadili maono yao kuwa uhalisia"

3. Chagua washirika au timu sahihi
Wakati mwingine utahitaji kufanya kazi na watu au mtu fulani. Ni muhimu kuwa makini wakati wa kuchagua washirika au timu ya kufanya nayo kazi ili kuhakikisha maono yako hayakwamishwi. Kamwe usichukue mtu tu kwa kigezo kuwa ni rafiki au ndugu yako, bali chukua mtu ambaye unaamini anaweza kufanya kitu chenye tija kwa ajili ya kufanikisha malengo yako kama mjasiriamali.

4. Toa huduma au bidhaa yenye tija
Hivi leo sokoni kuna bidhaa na huduma nyingi ambazo ni za aina moja, lakini siyo zote zinafanya vizuri. Hii ni kutokana na baadhi ya bidhaa au huduma kutozingatia kuwa na tija kwa wateja wake. Ikiwa unatengeneza bidhaa au huduma fulani hakikisha itakuwa na manufaa makubwa na ya uhakika kwa wateja wako.

Kwa mfano nimewahi kuona vitafunwa vilivyoandaliwa katika mazingira duni na kuwa na dosari mbalimbali kama vile marashi, vipande vya nywele, mchanga n.k. Ni wazi kuwa bidhaa za namna hii zitakosa wateja kutokana na kuwa na ubora duni.

Kila mara kumbuka kuwa ushindani ni mkubwa, hivyo jitahidi kuongeza tija na ubora wa huduma na bidhaa zako.

5. Fahamu na jali wateja
Ikiwa wewe ni mjasiriamali, basi futa mawazo kuwa wateja wanakuhitaji wewe. Fahamu kuwa wewe kama mjasiriamali, ndiye unaye wahitaji wateja ili ukuze biashara au huduma yako. Hakikisha mambo haya kuhusu wateja:


  • Fahamu wanataka nini.
  • Sikiliza maoni na ushauri wao.
  • Hakikisha unakamilisha mahitaji yao.
  • Tumia lugha nzuri na rafiki kwa wateja.
  • Mfanye mteja aone unamthamini.
  • Mfanye mteja aone kuwa umetanguliza huduma kabla ya pesa.

Naamini kwa kufanya hivi utaweza kujijengea msingi mzuri wa wateja kwa ajili ya huduma au bidhaa zako kila siku.

6. Tumia pesa vyema
Changamoto ya matumizi mabaya ya pesa inawakabili watu wengi kuanzia kwenye matumizi yao binafsi ya pesa. Watu wengi wanapata pesa lakini zinaisha bila ya kufahamu wamezitumiaje au wamefanya kipi chenye tija.

Ni wazi kuwa matumizi mazuri ya pesa ni kanuni muhimu sana kwa mjasiriamali, kwani kwa njia hii utaweza kukuza biashara yako kila siku. Jifunze kufahamu hii ni pesa kwa ajili ya nini, na uitumie kwa mambo ya msingi pekee. Epuka tabia za kibadhirifu na anasa. Ikiwa biashara au uwekezaji wako ni mkubwa, basi unaweza kumwajiri mtu aliye na taaluma ya utunzaji na usimamizi wa pesa.

Unaweza pia kujifunza wewe mwenyewe jinsi ya kutunza na kutumia pesa vyema; unaweza pia kutumia programu za bure za kompyuta kama vile Wave app kutunza mahesabu yako.

7. Jifunze kusema hapana
"Hapana" ni jibu dogo lakini lenye manufaa makubwa. Ikiwa wewe ni mjasiriamali ni muhimu kuzingatia kanuni hii ya kusema hapana kwani itakutenga na mambo au mipango isiyokuwa na ulazima.

Kuna watu, mipango, vitu au hata tabia ambazo zinaweza kukuathiri vibaya sana kwenye ujasiriamali wako. Hivyo kusema hapana kutakuepusha kwa kiasi kikubwa na mambo haya.

8. Usipuuze nafasi ya teknolojia
Tunaishi kwenye ulimwengu wa sayansi na teknolojia, hivyo wewe kama mjasiriamali huwezi kujitenga nao. Kwa kupitia teknolojia kama vile simu na mtandao wa intaneti, unaweza kuwafikia watu wengi zaidi na kuongeza mauzo ya huduma au bidhaa zako.

Hakikisha wewe kama mjasiriamali unakuwa karibu na wateja wako ili kutatua shida na mahitaji yao; pia hakikisha unajifunza mbinu bora za kufanya biashara kupitia mtandao.

Soma pia: Makosa 8 ya Kuepuka Unapofanya Biashara Kwenye Mtandao.

9. Fahamu soko
Kanuni mojawapo ya kuongeza mauzo yako kama mjasiriamali ni kulifahamu soko vyema. Hakikisha huduma au bidhaa unayoitoa inakidhi mahitaji na inafika kwenye soko stahiki.

Kwa mfano ikiwa wewe ni mzalishaji wa mayai, lakini eneo ulilopo soko ni duni, basi tafuta eneo jingine ambalo soko la bidhaa hii ni nzuri. Ikiwa wewe huwezi kwenda, unaweza kutafuta mtu kwenye eneo lenye soko zuri akakuuzia bidhaa yako na ukampa gawio fulani.

Kwa kufanya hivi utaweza kulenga soko na kujiongezea faida zaidi wewe kama mjasiriamali.

10. Ongeza maarifa
Kwanza nikupongeze kwa kusoma makala hii, ni wajasiriamali wachache sana ndiyo hupenda kusoma makala na vitabu mbalimbali ili kuongeza maarifa. Ni muhimu sana kila mara ukajizoesha kujiongezea maarifa, hasa ya ujasiriamali pamoja na kile unachokifanya; hili liitakuwezesha kuwa na tija na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Unaweza kusoma vitabu, majarida na tovuti mbalimbali (kama fahamuhili.com) ili kuongeza maarifa yako.

11. Jifunze kutokana na makosa
Moja ya kanuni inayozingatiwa na wajasiriamali waliofanikiwa ni kujifunza kutokana na makosa. Makosa ni shule nzuri sana kwa kila mtu hasa wajasiriamali. Ikiwa uliwekeza ukapata hasara, basi jifunze nini hasa kilikuwa chanzo cha hasara ili mbeleni uweze kukiepuka. Usikubali kukwamishwa na makosa, bali yawe ni hamasa kwako ya kuendelea mbele zaidi.

"Uzoefu ni kufanya makosa na kujifunza kutokana na makosa hayo"

Bill Ackman
12. Jifunze kwa waliofanikiwa
Watu wengi wameshindwa kufanikiwa kwenye maisha yao kwa sababu wanajifunza kwa walioshindwa. Walioshindwa wana maneno mengi, hasa ya kukatisha tamaa kama vile hili haliwezekani, hili linahitaji pesa nyingi sana, mimi lilinishinda, linachosha, lina faida ndogo, kuna wengi wanaolifanya, fulani alishindwa n.k.

Wewe kama mjasiriamali, epuka watu hawa na ujifunze kwa waliofanikiwa, fahamu walitatua vipi changamoto walizokabiliana nazo pamoja na mipango waliyoitumia hadi wakafika hapo walipo.

13. Tumia muda vizuri
Hakuna mtu mwenye zaidi ya saa 24 duniani; lakini mwingine muda unamtosha wakati mwingine analalamika  muda haumtoshi. Ni wazi kuwa mpangilio au matumizi mabaya ya muda ndiyo husababisha changamoto hii. Wewe kama mjasiriamali ni muhimu ukaondoa mambo yasiyokuwa na ulazima kwenye ratiba yako. Tambua ni kitu gani ni cha muhimu zaidi na ukifanye kwa wakati.

14. Weka vipaumbele
Wewe kama mjasiriamali, ni muhimu kuzingatia kanuni hii ya kujiwekea vipaumbele; vipaumbele vitakuwezesha kubaini ni kipi kianze na ni kipi kifuate kutokana na umuhimu wake.

Kwa mfano ikiwa kuna wateja walipata shida kupata huduma au bidhaa yako, maliza kwanza swala hili kabla ya kuendelea kuweka jitihada za kuuza bidhaa mpya. Kwa kufanya hivi utaweza kufanya mambo kutokana na umuhimu wake, jambo ambalo litakuwezesha kukua.

15. Usikate tamaa
Ni wazi kuwa katika safari ya ujasiriamali utakutana na changamoto mbalimbali. Jambo la msingi ni kukumbuka kanuni hii kuwa usikate tamaa. Tumia changamoto kama chachu ya kukuhamasisha kufanya bidii zaidi na usirudi nyuma.

Changamoto zipo leo na kesho lakini keshokutwa hazitakuwepo tena; jambo unalotakiwa kufanya ni kutazama lengo lako na kufanya bidii kila kukikucha kuzikabili changamoto husika ili ufikie lengo lako.

"Siri ya mafanikio yetu ni kutokukata tamaa"

Wilma Mankiller

Hitimisho

Naamini umefahamu kuwa kuna kanuni muhimu ambazo wewe kama mjasiriamali unatakiwa kuzizingatia ili uweze kufanikiwa. Ni wazi kuwa bidii, mipango mizuri na kutokukata tamaa kutakuwezesha kufikia lengo lako la kufanikiwa kama mjasiriamali.

Rais mstaafu Jakaya Kikwete na aliyekuwa waziri mkuu Edward Lowasa walivyowasili kwenye msiba wa Ruge (+ Video)

Ikiwa ni siku ya pili tangu Tanzania iondokewe na mtu muhimu sana, Viongozi mbalimbali wa Serikali wameendelea kuhudhuria nyumbani kwa wazazi wake marehemu Ruge Mutahaba ambaye amefariki dunia akiwa anapokea matibabu nchini Afrika ya Kusini. Na leo wameweza kuhudhuria baadhi ya viongozi wastaafu wakiongozwa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana …

The post Rais mstaafu Jakaya Kikwete na aliyekuwa waziri mkuu Edward Lowasa walivyowasili kwenye msiba wa Ruge (+ Video) appeared first on Bongo5.com.


Source

WENYE MAKALIO MAKUBWA WATUA KWA SPIKA KULALAMIKA SHINDANO LAO KUZUIWA


Waandaaji wa shindano la wanawake walio na maumbo makubwa nchini Uganda wamewasilisha malalamiko yao kwa spika wa bunge kufafanua madhumuni yao.

Wamesema kuwa lengo lao sio kutumia shindano la 'Miss Curvy Uganda'' kuvutia watalii kuja nchini humo.

''Haya ni mashindano ya urembo wa wanawake wanene''alisema Annie Mungoma, mkurugenzi mkuu wa mashindano hayo.

Bi. Mugoma aliongeza kuwa mtazamo wao itaondosha fikra za kimagharibi kuwa urembo unamaanisha mtu kuwa mwembamba.

''Tunataka kuwapatia motisha wanawake wenye maumbo makubwa kujiamini kwamba wao pia ni warembo''.Baadhi ya waandalizi wa Miss Curvy Uganda wakizungumza na Spika wa Bunge la Uganda Rebecca Kadaga

Siku mbili zilizopita spika wa bunge Rebecca Kadaga aliyepinga vikali mashindano hayo amebadili msimamo wake baada ya kupokea ufafanuzi huo.

Ameahidi mkono juhudi zao na kutoa ufafanuzi kwa bunge ili kuondoa fikra kwamba mashindano hayo ni ya aibu kwa jinsia ya mwanamke.

Tangu shindano shindano hilo lilipozinduliwa mapema mwezi huu, wanasiasa,wanaharakati wa haki za wanawake na viongozi wa kidini wamejitokeza na kulishtumu vikali.
Waziri wa utalii nchini Uganda Godfrey Kiwanda alipendekeza kuwe na onyesho la wanawake wenye maumbo makubwa ili kuvutia wageni zaidi wanaoitembelea nchi hiyo.

Akizungumza katika uzinduzi wa shindano hilo , waziri huyo alisema kuwa itakuwa "tukio la kipekee ambalo litawaonesha mabanati wakionesha maumbo yao mazuri yaliyo nona"

Kauli hiyo ilizua mjadala mkali hasa katika mitandao ya kijamii huku baadhi ya watu wakimshutumu bwana Kiwanda kwa kuzungumza juu ya wanawake wanene kama wananyama huku mwanamke mmoja akihoji kama ingewezekana basi wawekwe bustanini ili watazamwe kama wanayama watendewavyo ".
Licha ya mjadala huo kufikia sasa washiriki 200 kutoka sehemu mbalimbali za Uganda pamoja na nchi jirani ya Rwanda wamejisajili kushiriki shindano la Miss Curvy Uganda linalotarajiwa kufanyika mwezi wa June mwaka huu.
Chanzo- BBC

Alikiba apata mtoto wa kiume (+ Video)

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na mkurugenzi wa Rockstar, Alikiba amethibitisha kupata mtoto. kupitia ukurasa wa Snapchat msanii huyo amepost picha zikionesha sura na miguu ya mtoto. ikidaiwa mke wake Amina amejifunua jana. Baada ya muda kidogo msanii huyo alipost clip fupi ya video ikiwaonyesha watoto wakituma salamu kwa msanii huyo wakimwambi “Hongera kwa …

The post Alikiba apata mtoto wa kiume (+ Video) appeared first on Bongo5.com.


Source

Waandaaji wa shindano la wanawake wenye makalio makubwa watua kwa spika wa bunge Uganda, ni baada ya kupingwa vikali, zaidi ya washiriki 200 wajitokeza

Waandaajii wa shindano la wanawake walio na maumbo makubwa nchini Uganda wamewasilisha malalamiko yao kwa spika wa bunge kufafanua madhumuni yao. Wamesema kuwa lengo lao sio kutumia shindano la ‘Miss Curvy Uganda” kuvutia watalii kuja nchini humo. ”Haya ni mashindano ya urembo wa wanawake wanene”alisema Annie Mungoma, mkurugenzi mkuu wa mashindano hayo. Bi. Mugoma aliongeza …

The post Waandaaji wa shindano la wanawake wenye makalio makubwa watua kwa spika wa bunge Uganda, ni baada ya kupingwa vikali, zaidi ya washiriki 200 wajitokeza appeared first on Bongo5.com.


Source

Picha : MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU AKIWA MKOANI SHINYANGA LEO


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa haamini macho yake kuona uchafu uliokithiri mara baada ya kutembelea jiko la kupikia chakula cha wanafunzi wa Chuo Cha Ualimu SHYCOM wengine pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Taleck (kushoto) na Mkuu wa Chuo hicho John Nandi. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais 
Mwanafunzi wa Chuo Cha Ualimu SHYCOM Happyness Kasuku akimueleza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) changamoto ya maktaba ya kusomea ambayo ni ndogo na ina vitabu vichache. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akkizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ualimu SHYCOM mkoani Shinyanga mara baada ya kutembelea chuo hicho na kukagua ukarabati na ujenzi wa miundombinu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Edward K. Mulumba (kulia) wa Wizara ya Maji yanayohusu maendeleo ya ujenzi wa mradi wa ofisi ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji taka Shinyanga (KASHWASA).
Picha ya Jengo la Madarasa ya Chuo cha Ualimu SHYCOM ambalo Makamu wa Rais alitembelea na kutaka kujua kwa nini ujenzi wake umesimama. Makamu wa Rais yupo mkoani Shinyanga katika ziara ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wanafunzi wa shule ya Msingi Jumuishi Buhangija (hawapo pichani) mkoani Shinyanga.
Wanafunzi Nchambi Nsile (kulia) anayesoma darasa la 7 akiwa amempakata mwenzake Nyazobe Sembe darasa la 4 wa Shule ya Msingi Jumuishi Buhangija wakati wa kumsikiliza Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye alitembelea shule hiyo na kufungua Bwalo.Makamu wa Rais yupo ziara ya kikazi mkoani Shinyanga. 
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga (CCM) Mhe. Azza Hilal Hamad akiwa amempakata mmoja wa wanafunzi Shule ya Msingi Jumuishi Buhangija wakati wakimsikiliza Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) ambaye alitembelea shule hiyo na kufungua Bwalo. Makamu wa Rais yupo ziara ya kikazi mkoani Shinyanga. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna kutoka kwa Msanifu wa Pamba Bi. Sharifa Salum (kushoto) mara baada ya kutembelea maabara ya pamba katika Ofisi ya Bodi ya Pamba mkoani Shinyanga. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna kutoka kwa Msanifu wa Pamba Bw. Dotto Ntumba (kushoto) mara baada ya kutembelea maabara ya pamba katika Ofisi ya Bodi ya Pamba mkoani Shinyanga. Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais

Wednesday, February 27, 2019

Picha : KIGWANGALLA AHANI MSIBA WA RUGE

Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla amefika nyumbani kwa familia ya Ruge Mutahaba na kutoa pole za msiba ambapo pia ameweza kumwelezea marehemu Ruge kama mtu mwenye uthubutu kwa jamii.

Dk. Kigwangalla ameweza kuonana na kutoa pole kwa wafiwa ndugu,jamaa na marafiki akiwemo Baba mzazi Mzee Mutahaba pamoja Mama wa Ruge Bi. Cristina Mutahaba na kutoa pole zake hizo pamoja na rambirambi alizokabidhi kwa Mama mzazi.

Dk.  Kigwangalla amemuelezea marehemu kama mtu wa kuigwa kwani alijituma katika kuhakikisha anatimiza malengo yake aliyopangiwa ama kujipangia. 

"Ruge alikuwa mtu wa watu na alisimama katika mipango sahihi hata nikamchagua kwenye Kamati za kuendeleza masuala ya Utalii ikiwemo ile ya Tanzania Unforgettable." alieleza Dk Kigwangalla. 

Aidha, Dk Kigwangalla ameweza kuungana na viongozi wengine pamoja na ndugu na jamaa.

Awali taaifa ya Msemaji wa Familia Bw. Anic Kashasha amesema kama mipango itakwenda kama ilivyopangwa mwili wa marehemu Ruge Mutahaba utawasili Ijumaa na utaagwa rasmi siku ya Jumamosi jijini Dar es salaam, Baada ya kuagwa utasafirishwa kwenda Bukoba siku ya jumapili na kuzikwa siku ya jumatatu huko Bukoba mkoani Kagera.

Na Andrew Chale  - Dar es salaam
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamisi Andrea Kigwangalla akitoa pole kwa Mama mzazi wa Ruge Mutahaba alipoenda kutoa pole mapema leo Februari 27.2019.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Hamisi Andrea Kigwangalla akiteta jambo na Mbunge pole wa Kigoma Zitto Kabwe katika msiba wa Ruge Mutahaba alipoenda kutoa pole mapema leo Februari 27.2019.

Source

Steve Nyerere: Dudubaya Anapaswa Kuomba Msamaha

Steve Nyerere: Dudubaya Anapaswa Kuomba Msamaha
Muigizaji nguli wa filamu nchini, Steve Nyerere, amesema kama kuna msanii anamzungumzia vibaya marehemu Ruge Mutahaba kwa sasa jkama anavyofanya Rapa Dudu Baya basi anapaswa kutengwa kwani hakuna binadamu aliye mkamilifu.


  • Steve amesema Ruge amefungua milango kwa vijana wengi na kutoa fursa waweze kufanikiwa huku akiweka wazi kuwa atamkumbuka milele.

Nafasi ya Manchester United ni ipi kwenye ligi baada ya kuwakosa wachezaji zaidi ya 7 katika kikosi cha kwanza wakiwa ni majeruhi

Wachambuzi wana tathmini kwamba kujeruhiwa kwa wachezaji wa Manchester uniyted kunaweza kutoa nafasi na faida kwa Crystal Palace hatimaye leo kufanikiwa kushinda mechi ya ligi kuu England dhidi ya mashetani wekundu. Ushindi wao mkubwa dhidi ya Leicester mara ya mwisho haikufua matumaini ya timu hiyo ya Wanamwewe lakini pia kuondosha hofu ya kuanguaka chini ya …

The post Nafasi ya Manchester United ni ipi kwenye ligi baada ya kuwakosa wachezaji zaidi ya 7 katika kikosi cha kwanza wakiwa ni majeruhi appeared first on Bongo5.com.


Source

Msiba Hautakuwa wa majonzi kama Bali Itakuwa ni kusherehekea maisha yake kama ambavyo mwenyewe alitaka Iwe- Kusaga

Msiba Hautakuwa wa majonzi kama Bali Itakuwa ni kusherehekea maisha yake kama ambavyo mwenyewe alitaka Iwe- Kusaga

Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group Joseph Kusaga amesema kwamba msiba wa Ruge hautakuwa wa majonzi kama ilivyozoeleka, bali itakuwa ni kusherehekea maisha yake kama ambavyo mwenyewe alitaka iwe.


Kusaga amezungumza hayo akisema kwamba kabla Ruge hajafariki, aliwahi kusema kuwa ikitokea siku amekufa, basi watu wasihuzunike sana, bali washerehekee maisha yake na vile alivyo vifanya wakati yupo hai.

"Kuna kitu alikuwa akisisitiza, kwamba ikitokea bahati mbaya Mwenyezi Mungu amemchukua, tu-'celebrate' maisha yake, tu-'celebrate' alivyovifanya,  kwa hiyo tutaanza maombolezo lakini yatakuwa ku-'celebrate' mazuri aliyoyafanya, hii alisisitiza wazi kabisa, na mimi kumpa heshima hiyo ni lazima tu-'celebrate' mengi mazuri aliyoyafanya", amesema Kusaga.

Akiendelea kuzungumzia hilo Joseph Kusaga amesema kwamba Ruge amefanya mengi mazuri ambayo yalifaa kutunukiwa, huku akitoa shukrani kwa serikali kwa kuwa nao bega kwa bega, kwenye kipindi hiki kigumu kwao.

"Inaweza ikawa sio wakati mzuri wa kusema mengi, lakini Watanzania inabidi tujifunze kutoa tuzo au kitu chochote kizuri kwa mtu aliyefanya mambo mazuri, amefanya mengi mazuri kwenye tasnia hii na burudani, naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa serikali na viongozi wote ambao wamekuwa kwa kiasi kikubwa wamekuwa wako karibu sana kutu suport, ili kuhakikisha tunamponya na maisha yake yanaendelea", amesema Kusaga.

Ruge Mutahaba amefariki jioni ya Februari 26 huko Afrika Kusini, akipatiwa matibabu ya figo aliyokuwa akisumbuliwa nayo.



Mh Mwakyembe Aagiza Dudubaya Kukamatwa

Waziri anaeshughulikia maswala ya michezo nchini amefunguka na kutoa amri kukamatwa kwa msanii Dudubaya ambae alianza kutoa maneno ya kashaf kwa marehemu Ruge Mutahaba ambae amefariki siku ya jana jioni,. Marehemu Ruge alifariki akiwa katika matibabu yake nchi Afrika ya Kusini , huku msanii Dudubaya akiwa ameanza kurusha maneno ya kejeli na matuzi kwa mkurugenzi huyo ambae  alikuwa akipigania afya yake tangu akiwa hai. Hata baada ya kifo, msanii dudubaya aliendelea kutuma maneno ya kejeli katika mitandao ya kijamii na kukwaza watu wengi na hata kuanza kumlili awaziri mwenye  dhamana hiyo kutaka kumchukulia hatau msanii huyo. Hata hivyo baada ya saa chache tangu kuripotiwa kwa msanii huyo , tayari msanii huyo ameamuriwa kukamatwa na kuwekwa ndani ili  kuthibiti hali hiyo. Taarifa hiyo ambayo imetolewa na naibu waziri wa habari ,sanaa na micheoz mh juliana shonza anasema kuwa kwa kushirikiana na BASATA  na polisi wanatakiwa kumkamata msanii DUDUBAYA.

The post Mh Mwakyembe Aagiza Dudubaya Kukamatwa appeared first on Ghafla! Tanzania.


Source

MWANAFUNZI AUAWA KWA KUPIGWA NA KIRANJA SHULENI


 Hali ya majonzi imeikumba Shule ya Sekondari St Joseph Nyabigena iliyopo Gucha Kusini, Kaunti ya Kisii nchini Kenya kufuatia kifo cha mwanafunzi mwenzao anayedaiwa kupigwa na kiranja.


 Mwanafunzi huyo wa kidato cha tatu anadaiwa kuaga dunia baada ya kukimbizwa katika Hospitali ya Wamisionari ya Tabaka.

Kwa mujibu wa ripoti ya Nation, marehemu alianguka na kuzimia baada ya kupigwa na kiranja, na inadaiwa walizozana kabla ya kisa hicho asubuhi ya Jumanne 26,2019.

 "Marehemu alikuwa akisoma Bibilia kuelekea saa moja asubuhi. Baada ya mgogoro kidogo kati yao kiranja alimpiga kofi kisha teke la tumbo na hapo alianguka na kuzimia," mmoja wa wanafunzi alisema.

 Usimamizi wa hospitali ulikataa kusema na wanahabari kuhusu kilichosababisha kifo cha mwanafunzi huyo.

 Kamanda wa Polisi wa Kaunti Martin Kibet alithibitisha kutokea kisa hicho na kusema tayari uchunguzi wa polisi umeanzishwa. 

"Tunafahamu kuhusu kisa hicho na tumewaruhusu polisi kufanya uchunguzi wao kabla ya kutoa taarifa." Kibet alisema.

 Mwalimu Mkuu Mathew Simiyu alitoweka katika shule hiyo mara baada ya tukio hilo na wanahabari hawakupata fursa ya kusema naye.

 Mwalimu ambaye hakutaka jina lake kutajwa alisema, mwalimu mkuu alizungumza na wanafunzi na kuwataka kuwa watulivu kabla ya kuondoka.

 Baadhi ya walimu waliozungumza na wanahabari waliwalaumu walimu wakuu kwa kuwapa mamlaka mengi viranja.

 "Waliohusika wakamatwe na kusema kilichotokea. Ni makosa kwa wanafunzi kupewa idhini ya kuwaadhibu wanafunzi wengine," mmoja wa walimu alisema.

 Wanafunzi walisusia chakula cha mchana na kulalamika kuhusu viranja kuwafanyia ukatili shuleni. 

Maafisa wa Polisi kutoka Kituo cha Polisi cha Nyamarambe walimhoji mwalimu aliyekuwa zamu kuhusu tukio hilo lakini haikubainika iwapo yeyote ametiwa nguvuni kuhusiana na kifo cha mwanafunzi huyo.

Muhammadu Buhari amefanikiwa kumbwaga mpinzani wake kwa asilimia 56, Sasa kuiongoza Nigeria kwa mara nyingine

Tume ya taifa ya uchaguzi ya Nigeria imemtangaza rais Muhammadu Buhari kuwa mshindi wa urais kwa muhula wa pili katika taifa hilo lenye nguvu kiuchumi barani afrika na mzalishaji mkubwa wa mafuta. Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi amemtangaza Buhari mapema leo kuwa mshindi wa uchaguzi uliocheleweshwa na kugubikwa na kasoro kadhaa za maandalizi pamoja na …

The post Muhammadu Buhari amefanikiwa kumbwaga mpinzani wake kwa asilimia 56, Sasa kuiongoza Nigeria kwa mara nyingine appeared first on Bongo5.com.


Source

Je Unajua Kwanini Wazungu Wanasema Life Begins at 40 Years Old? Majibu Haya Hapa

Watu wengi hawajui kwa nini wazungu huwa wanasema LIFE BEGINS AT 40. Yaani maisha yako ya kweli yataanza ukifika umri wa Miaka 40. Wakati ambapo unatakiwa uwe na elimu uliyoihitaji.. Uwe na familia yako tayari.. Uwe na kwako tayari siyo umepanga bado.. Uwe na usafiri binafsi.. Uwe na kitu chako cha kukuingizia pesa na si kutegemea ajira peke yake. At 40!!

At 40 inabidi uwe unaishi. Siyo ndo unaanza kujaribu hiki na kile. At 40 inabidi uwe unasomesha zaidi kuliko kusoma wewe japo kuongeza maarifa ni vizuri.
At 40 unatakiwa uwe umeshapata exposure kwa kusafiri huku na kule dunia hii kujua wengine walioendelea zaidi wanaishi vipi na wewe ufanyeje?
At 40 utakuwa bado unaomba nauli kwa baba na mama kwani?

Sasa hivi vitu haviji ukiwa upoupo tu hutafuti fursa za kukusaidia kuwa na maisha tofauti upo tu una LIKE kila kitu facebook na Instagram unatuma tu picha za ajali za mabasi zikikosekana unatuma za migomo ya madereva mgomo ukiisha unatuma za mafuriko kama mvua zimeisha unatuma picha za Lowassa yaani umekuwa mtumwa wa simu. Ikikosa network unalalamikia kampuni ya simu utafikiri hiyo network unafanyia kitu cha maana. Gallery yako imejaa vitu vya ajabuajabu tu. Havikufikishi popote na umri unazidi kwenda unazidi kusogea miaka 40 hivi hivi. Maisha ya kweli yataanza ukiwa na miaka 40. Wakati ambapo watoto wako hawatakula LIKES zako za instagram bali wanahitaji chakula. Wanahitaji ada. Wanahitaji maisha bora. Wewe inasubiri maisha bora CCM ndo wakupe. Wasipokupa unataka UKAWA waje wakupe ukiwa umekaa Instagram unaLIKE picha za Wema Sepetu. Umeshajua wema akifika miaka 40 atakuwaje? Ulishajiuliza wanamuziki waliovuma miaka 15 iliyopita wakiwa na umri wa miaka 25 hivi au 30 wakati huo wana miaka mingapi na wako wapi sasa hivi. You see? Unayemfuatilia kila siku kavaaje kaamkaje katembea na nani hakusaidii kuwa na maisha mazuri. Maisha bora hayaji ukiwa unafatilia nyimbo gani zimetoka udownload. Maisha bora hayaji kwa KU-ENTERTAIN brain yako bali kwa kuifikirisha akili na kufanya mambo ambayo wachache tu ndo wanafanya.

Kwani wanasoka wangapi wako kama Beckham
Wnamuziki wangapi wako kama Kirk Franklin
Wacheza Tennis wangapu wako kama Roger Federer? Unadhani amekuwa champion akiwa amekaa na TECNO chumbani ana comment kuhusu migomo? No. Alikuwa ana-hussle wakati wengine wanachat.

Seriously. Diamond unayemfollow anafanya kazi hivyo. Anatoka studio saa saba usikuwewe uko kwenye page yake unaLIKE. Huwezi kuona kuwa uko tofauti. Anaandaa maisha akifika miaka 40 awe na kila kitu wewe utakuwa unalalamikia network ya tigo tu na kutuma picha  za sijui gari limegonga treni. Kwa hiyo wewe ndo NIPASHE sasa hivi?

Anyway. Kuwa serious na maisha yako angalau basi kwa ajili ya watoto wako na wajukuu zako. Aise huyu mzazi wetu alifanya jambo la maana. Au unadhani watazikuta hizo comments na LIKES zako? No. Wanapaswa wakute nyumba, viwanja, account za benki zinazopumua. Siyo account inaingiaga mshahara tu halafu by tarehe 10 iko empty ushakomba kila kitu!!!! Wanatakiwa wakute assets za maana angalau. Siyo rundo la CD za bongo movie ambazo hazikusaidii wewe wala wao.

Siku zilizobaki kumaliza mwaka huu umeeka mikakati gani kuweka msingi wa maisha tofauti sana na kuhakikisha ufikapo umri wa miaka 40?
Au bado unategemea mshahara wa laki 8 (tena hapo kabla ya makato) uje ubadili maisha yako).
Kwa waajiriwa, Microsoft ya Bill Gates inapunguza wafanyakazi 800. Kama ulikuwa hujui. Unadhani kampuni yako ndo utakaa hapo milele?
Be careful my friend.

" KUZALIWA MASIKINI SI KOSA BUT KUFA MASIKINI NI DHAMBI"

“Diamond Anapendeza na Tanasha Zaidi”- Shilole

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole ameibuka na kuwamwagia sifa kibao staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na Mpenzi wake Tanasha Donna. Siku za nyuma Shilole hakuficha hisia zake za Jinsi gani alikuwa anamkubali Mama Watoto wa Diamond, Zari na hata kumuomba Diamond arudiane naye Baada ya kuachana. Lakini Hivi sasa Zari anaoenekana kumsahau Zari na kuhamisha majeshi yake kwa wifi yake Mpya Tanasha kwani ameshindwa kujizuia na kumwagia sifa kibao mrembo huyo. Kwenye mahojiano aliyofanya na Times Fm, Shilole ameweka wazi kuwa Tanasha anapendezana na Diamond na hata kudai tangu amekuwa naye amekuwa akipendeza zaidi hasa Baada ya kunyoa. Diamond na Tanasha wanapendezana sana, siku hizi naona hata Diamond ananyoa vizuri kusema Ukweli wapo kizazi sana". Stori za chini chini zinadai kuwa Shilole alikoromewa na Diamond Baada ya kumtaka arudiane na Zari kwenye mkutano na waandishi wa habari Wiki chache zilizopita.

The post "Diamond Anapendeza na Tanasha Zaidi"- Shilole appeared first on Ghafla! Tanzania.


Source

Mzee Kikwete alizwa na kifo cha Ruge ‘nakosa maneno ya kuelezea’

Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete ameeleza maumivu aliyonayo kufuatia  kifo cha Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba. Dkt. Kikwete na Marehemu Ruge Mzee Kikwete kupitia ukurasa wake wa Twitter, Kameandika ujumbe  maneno yaliyosomeka. "Nimelemewa! Nakosa maneno ya kuelezea huzuni na majonzi niliyonayo kwa kifo …

The post Mzee Kikwete alizwa na kifo cha Ruge ‘nakosa maneno ya kuelezea’ appeared first on Bongo5.com.


Source

CCM YAMLILIA RUGE MUTAHABA



Rayvanny Awashangaa Wanaomtuhumu Kujichubua

Msani Ray Vanny amekanusha taarifa za mitandao na kurasa za udaku kuwa kwa sasa ameanza kujichubua. Akiongea na waandishi wa habari wa  Ijumaa Wikienda, Rayvanny alisema kuwa anashangaa maneno hayo yanatoka wapi kwani katika maisha yake haja­wahi kuwaza kufanya hivyo na anachoamini yeye watu watakuwa wanaongea kwa sababu ya muonekano wake kwenye picha. "Jamani mimi hizo tabia nimezianza lini tena? Yaani walimwengu hawakosagi cha kusema, unajua kuna picha ambazo zikitupiwa mtandao­ni naonekana mweupe sana na nyingine zinakuwa zime­toka vibaya, hapo watu ndiyo huanza kusema nimejichibua, kitu ambacho siyo kweli," alisema Rayvanny. Hivi karibuni msanii huyo aliposti picha kwenye akaunti yake ya Instagram akiwa ana­toka kwenye mahojiano na moja ya vyombo vya habari hapa nchini, ambapo picha hiyo ilionesha magoti yake ni meusi tofauti na sehemu nyingine za mwili wake hivyo kuwafanya wadau kudhani amejichubua.

The post Rayvanny Awashangaa Wanaomtuhumu Kujichubua appeared first on Ghafla! Tanzania.


Source

Breaking NEWS: Ruge Mutahaba ametutoka....This is beyond sad

Ruge Mutahaba ametutoka....This is beyond sad. Dah roho inaniuma sana

Mungu awatie nguvu ndugu zake, watoto wake na wafanyakazi wa clouds....

Tanzania has lost its biggest entertainment genius. R.I.P legend. R.I.P Creator and founder of Tanzania's entertainment industry. Tanzania and its people will miss you Ruge..


Source

Hatua muhimu zitakazosaidia kudumu katika mahusiano yako ya kimapenzi

Mahusiano ya mapenzi yenye kudumu ni sharti yapandwe katika udongo wenye rutuba kama ulivyo mmea,yatahitaji maji ya kumwagilia na mbolea ya kukuzia.  Na zaidi ya yote yanahitaji muda wa kukua kabla matunda kuonekana.

 Hizi ndizo  hatua muhimu zitakazokusaidia kudumu katika mahusiano yako ya mapenzi.

Mawasiliano
Mawasiliano ni muhimu sana baina ya wapenzi. Hata kama umebanwa na kazi pata dakika chache za kuongea na mpezi wako na kumtaka hali. Andika hata ujumbe wa maneno au barua pepe. Mwambie mpenzi wako ulipo kila mara inapobidi ili kumjengea imani na wewe na kumpa amani moyoni. Tuma ramani ya mahali ulipo kama unatumia simu ya "Smart phone" (Tuma location kwenye whatsapp)

Mawasiliano ni ufunguo wa kudumisha upendo. Wakati kuwasiliana na mpendwa wako, kumbuka kwamba upendo ni muhimu. Ongea toka moyoni na si kwa ajili ya kutimiza wajibu tu,kwani mpezi wako atajua tu kama hakuna mahaba katika mawasiliano yenu hivyo kutoleta faida ile inayotegemewa.

Mawasiliano mengine ni yale ya kuelezana yaliyo moyoni. Mweleze mwenza wako linalokusibu ili kupata ufumbuzi wa pamoja. Wapenzi wanaoongea kwa utulivu siku zote watakuwa pamoja.

Zawadi
Tafuta kitu cha kumpa mpenzi wako. Si lazima kiwe na thamani kubwa  .Inaweza ikawa pipi au matunda tu. Mnunulie zawadi kila inapowezekana hasa unaposafiri au katika siku yake ya kuzaliwa.

Onyesha Upendo Wako
Kila mtu anajinsi yake tofauti ya kuonyesha upendo, lakini vyovyote itavyokuwa ni jambo la muhimu sana kuonyesha hisia zako kwa mpenzi wako. Mara nyingi wapenzi wa muda mrefu wanasahau juu ya hili. Maneno kama "Nakupenda"au majina ya mahaba kama "Mpenzi" au "La-azizi" yanachangia sana kuonyesha mapenzi na kumfanya mwenza wako kujisikia vizuri.

Maneno haya yanaposemwa kwa hisia halisi na toka moyoni yana mchango mkubwa katika kuboresha mahusiano.

Tuesday, February 26, 2019

Matokeo ya Ligi Kuu Tanzania Bara leo

Ligi Kuu ya Tanzania Bara imeendelea leo kwenye viwanja viwili Somara Mkoani Iringa na Manungu Mkoani Morogoro na matokeo ni kama yafuatayo;

FT: Lipuli FC 1-3 Simba SC

FT: Mtibwa Sugar 3-1 Coastal Union


Monday, February 25, 2019

Safari ya Pascal wa BSS ya kwenda kutibiwa India yakwama kisa passport (Video)

Safari ya Pascal wa BSS kwenda India kwa matibabu kwa msaada wa RC Makonda yakwama kisa mgonjwa kukosa passport ya kusafiria, arudi tena kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kuomba amfanyie mchakato wa hati ya kusafiria. Kwa upande wa familia wamesema kwa sasa ndio wanaanza mchakato wa passport ili kuhakikisha ndugu yao anapata msaada …

The post Safari ya Pascal wa BSS ya kwenda kutibiwa India yakwama kisa passport (Video) appeared first on Bongo5.com.


Source

BABA MZAZI AFURAHIA MTOTO WAKE KUFUNGWA JELA MIAKA 30 MTWARA


Mzee Musa Katambo, baba mzazi wa Ally Katambo (30), ambaye amehukumiwa kwenda jela miaka 30 baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara kumkuta na hatia ya kumbaka mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 11, amefurahia kifungo cha mwanawe. 

Ally alitiwa hatiani na kupewa adhabu hiyo kutokana na kumfanyia binti yake huyo mwanafunzi wa darasa la nne kitendo cha kinyama.

Mzee huyo alishangilia na kuipongeza mahakama kwa kutoa hukumu hiyo ya kifungo cha miaka 30 jela dhidi ya mwanae, akisema kosa alilolifanya la ubakaji ni kinyume cha sheria za nchi.

Katambo ambaye anaishi kijijini kwake Ndanda wilayani Masasi Mkoani Mtwara, alisema kwamba hajutii maamuzi ya mahakama dhidi ya mtoto wake huyo kufungwa miaka 30 jela, na kwamba serikali imetenda haki katika kusimamia sheria hasa juu ya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.

Mzee Katambo aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipokuwa akizungumza na gazeti hili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Masasi, baada ya mtoto wake huyo kuuhukumiwa kwenda jela miaka 30.

Alisema amefurahishwa na hukumu hiyo kwa sababu itatoa fundisho kwa vijana wengine wenye tabia kama ya mtoto wake kwa kuwa watakaposikia wataacha kufanya vitendo hivyo, ambavyo vinaonekana kuchochewa na imani za kishirikina, badala yake vijana wafanye kazi kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao.

Alisema serikali ya sasa inasimamia haki kuhusiana na vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto hasa pale wanapofanyiwa vitendo hivyo na wazazi wao.

Alisema kitendo alichofanya mtoto wake dhidi ya mjukuu wake ni cha kikatili na kimeiletea aibu familia yake.

"Kwa kweli enzi zetu sisi yaani ile miaka ya zamani hakukuwa na mambo kama haya ya ajabu, mzazi kumbaka mwanawe wa kumzaa kisa kaambiwa na mganga ili apate utajiri," alisema na kuongeza:

"Mambo kama haya sisi ndio kwanza tunayaona siku hizi zamani hayakuwapo kabisa kwa hili mimi naipongeza serikali imetenda haki kabisa." 

Mzee Katembo alisema siku ya kwanza alipopata taarifa ya kuwa mjukuu wake amebakwa na baba yake mzazi na binti huyo kulazwa katika hospitali ya Mision ya Ndanda mjini Masasi, alipoteza fahamu kwa vile katika maisha yake hakuwahi kusikia jambo kama hilo la baba kumbaka mtoto wake wa kumzaa.

Aliongeza kuwa hata alipokuwa akifunga safari ya kwenda hospitalini Ndanda kwa ajili ya kumuona mjukuu wake anaendeleaje baada ya kulazwa pia alipokuwa akiingia ndani ya hospitali hiyo, alikuwa akianguka na kupoteza fahamu kwa mara mbili mpaka tatu ndipo anapata fahamu.

Na Hamisi Nasiri - Nipashe

Wadau mbalimbali wa sanaa watoa maoni yao kuhusu tuzo na kukosekana kwa tuzo za Bongo Fleva zinavyoathiri tasnia (+ Video)

Wadau mbali mbali napa nchini wameweza kutoa maoni yao kuhus tuzo zinazotolewa hapa nchini lakini pia kuhusu kukosekana kwa tuzo za muziki wa Bongo Fleva kunavyoathiri tasnia kwa ujumla. Wakipiga stori na Bongo 5 wadau hao wamefunga kama ifuatavyo:- Msanii Ruck Baby alivyotoa maoni yake. Patrick Kanumba alivyotoa maoni yake hasa kukosekana kwa kanumba na …

The post Wadau mbalimbali wa sanaa watoa maoni yao kuhusu tuzo na kukosekana kwa tuzo za Bongo Fleva zinavyoathiri tasnia (+ Video) appeared first on Bongo5.com.


Source

Hatimaye Halima Mdee Aachiwa kwa Dhamama

Hatimaye Halima Mdee Aachiwa kwa Dhamama
Halima Mdee ambaye ni Mbunge wa Kawe (Chadema),  jana Jumapili Februari 24, 2019 saa 10 jioni alipata dhamana baada kushikiliwa kituo cha polisi Oysterbay kwa zaidi ya saa 24.

Mdee  alikuwa akishikiliwa kituoni hapo baada ya kuitikia wito wa mkuu wa upelelezi mkoa wa kipolisi Kinondoni (RCO) Jumamosi Februari 23, 2019.

Hekima Mwasipu ambaye ni wakili wa Mdee amesema;"Tumehangaika tangu juzi lakini tunashukuru jana amepata dhamana ya polisi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili na kutakiwa kuripoti kwa mkuu wa upelelezi Februari 26"

Halima Mdee alidhaminiwa na Hekima na mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Anatropia Theonest.

Mdee anadaiwa kutoa kauli ya uchochezi alipokuwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kata ya Mikocheni, tarehe 21 Februari 2019.

Sunday, February 24, 2019

Ndege yatua kwa dharura baada ya jaribio la kuiteka nyara


Ndege iliyokuwa inafanya safari kutoka mji mkuu wa Bangladesh, Dhaka kuelekea Dubai, ililazimika kutua kwa dharura baada ya kutokea jaribio la kuteka nyara ndege, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.

Ndege ya shirika la Binman, ikiwa na abiria 142, ilizungukwa na vikosi vya usalama katika uwanja wa ndege wa mji wa pwani wa Chittagong.

Abiria wa ndege BG 147 walitoka ndani ya ndege hiyo wakiwa salama, ripoti zilieleza zikinukuu polisi.

Mtu mmoja aliyekisiwa kujaribu kuvamia chumba cha rubani alikamatwa, Shirika la habari la Ufaransa limeeleza.

Ndege hiyo iliwekwa kwenye uangalizi mara moja ilipotua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Shah Amanat wakati polisi wakizungumza na mshukiwa huyo.

Picha zilizowekwa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha watu wakiwa katika makundi makundi huku ndege aina ya Boeing 737 ikionekana kwa nyuma.

Haijafahamika kwa nini mshukiwa huyo anayeaminika kuwa na umri wa miaka 25, alijaribu kuteka nyara ndege.

YANGA SC YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA TFF BAADA YA KUICHAPA RUANGWA



 Yanga SC wamefanikiwa kuingia Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Namungo FC jioni ya leo Uwanja wa Kassim Majaliwa wilayani Ruangwa mkoani Lindi.

Shujaa wa Yanga SC kwa mara nyingine amekuwa mshambuliaji wake, Heritier Ebenezer Makambo raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 82 kwa kichwa cha kuparaza akimalizia krosi ya kiungo Deus Kaseke kutoka upande wa kulia.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Abubakar Mturo aliyesaidiwa na washika vibendera Khalfan Sika na Kassim Safisha, Namungo FC walifanikiwa vizuri kuibana Yanga kipindi cha kwanza. 

Na kipindi cha Yanga ilikianza na mabadiliko, kocha Mkongo Mwinyi Zahera akimpumzisha beki wa kushoto mwinyi Hajji Mngwali na Gardiel Michael Mbaga.

Na hiyo ni baada ya Mngwali kunusurika kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 43 baada ya kucheza rafu aliyostahili kuonyeshwa kadi ya njano akiwa tayari ameonyeshwa kadi hiyo awali, lakini refa Mturo akamuacha. 

Namungo FC ilipoteza nafasi nzuri ya kupata bao dakika ya 60 baada ya mshambuliaji wake, Reliant Lusajo kumpelekea mpira mkononi kipa Mkongo, Klaus Kindoki akiwa kwenye boksi baada ya pasi ya kutanguliwa na mtokea benchi, Kelvin John.

Dakika ya 76 Hashim Manyanya naye akafumua shuti kali akiwa umbali wa mita 18, lakini kipa Kindoki aliyekuwa katika ubora leo, akapangua ikatoka nje.

Kikosi cha Namungo FC kilikuwa; Adam Oseja, Miza Chirtom, Jukumu Kibanda, Freddy Mlelwa, Hamisi Fakhi, Daniel Joram, Hashim Manyanya, John Mbise, Ramadhani Hussein/Abeid Athumani dk73, Lucas Kikoti/Kelvin John dk60 na Reliants Lusajo.

Yanga SC; Klaus Kindoki, Paul Godfrey, Mwinyi Mngwali/Gardiel Michael dk46, Andrew Vincent 'Dante', Abdallah Shaibu 'Ninja', Feisal Salum, Mrisho Ngassa/Amissi Tambwe dk73, Papy Kabamba Tshishimbi, Heritier Makambo, Mohammed Issa 'Banka' na Ibrahim Ajibu/Deus Kaseke dk59.

Kura za uchaguzi mkuu Nigeria bado zinahesabiwa, Harmonize aandaa show ya kuwapoza machungu mashabiki wake nchini humo

Jana Februari 23, 2019 mamilioni ya watu nchini Nigeria walishiriki katika zoezi la kupiga kura kwenye uchaguzi mkuu baada ya shughuli hiyo kuahirishwa ghafla wiki iliyopita. Mpaka sasa bado shughuli shughuli ya kuhesabu kura inaendelea na matokeo ya awali yanatarajiwa kuanza kutangazwa kesho Jumatatu. Kwenye uchaguzi huo, Wagombea wawili wakuu ni Rais Muhammadu Buhari, (76) …

The post Kura za uchaguzi mkuu Nigeria bado zinahesabiwa, Harmonize aandaa show ya kuwapoza machungu mashabiki wake nchini humo appeared first on Bongo5.com.


Source

Namna Sahihi ya Kupunguza Matumizi ya Mafuta ya Gari yako


Matumizi ya gari ni mojawapo ya matumizi makubwa kwa familia nyingi hasa zinazoishi mjini.

Inasemekana kwa wale wanaomiliki magari kuwa inawezekana nyumbani kukakosekana baadhi ya mahitaji mengine muhimu lakini gari ni lazima liwekwe mafuta na litembee. Je kuna ukweli wowote? Jaribu kufanya utafiti utaona. Watu wanalalamika uchumi mbaya lakini magari yanatembea.

Hii inamaanisha kuwa kwa maisha ya kisasa tunayoishi gari limekuwa mojawapo ya nyenzo muhimu na ya lazima. Lakini pia ni mojawapo ya kitu ambacho kinakula fedha nyingi toka mifukoni mwetu.

Kila mtu anatakiwa kutafuta jinsi ya kupunguza matumizi yanayotokana na gari. Mafuta ni sehemu mojawapo ya matumizi makubwa katika kumiliki na kuendesha gari.

Katika mada hii tunaangalia mbinu za kupunguza matumizi ya mafuta ya gari hivyo kuboresha uchumi wa wamiliki.

Mbinu za Uendeshaji Zinazosaidia Kupunguza Matumizi ya Mafuta ya Gari
Madereva wengi wanaendesha magari kwa namna ambayo inasababisha injini kula mafuta mengi sana. Kama utaendesha gari kwa kufuata mbinu hizi tu unaweza kupunguza matumizi yako ya mfuta kwa asilimia 10-20.

Zingatia Mwendo Kasi Sahihi
Kila gari linatumia mafuta katika namna tofauti, lakini katika spidi juu ya 90 Km/Saa mpaka 100 Km/Saa gari lolote huwa linatumia mafuta kidogo kuliko likiwa katika spidi nyingine. Kwa mjini huwezi kufikia spidi hii lakini jitahidi kuendesha juu ya 30 Km/Saa.

Pia fahamu kuwa spidi ikizidi 50Km/Saa mafuta yatatumika zaidi kwa kuwa gari linahitaji nguvu zaidi kushindana ukinzani wa hewa.

Zingatia: Zuia mwendo kasi kati ya 60-90 Km/Saa kwakuwa hutumia mafuta mengi

Usiongeze Mwendo Kwa Haraka
Kukanyaga mafuta kwa haraka ilikuongeza spidi kunachangia ulaji mkubwa wa mafuta. Unashauriwa kukanyaga mafuta taratibu unapoongeza mwendo kasi.

Unaweza ukasikiliza gari lako wakati unaendesha,ukisikia sauti kubwa unapoongeza mwendo ujue unachoma mafuta mengi na hivyo unaongeza gharama.

Usipunguze Mwendo Kwa Haraka- Acha Ukanyagaji Breki za Kushitukiza
Kama ilivyo katika kuongeza mwendo,unatakiwa kupunguza mwendo taratibu. Hakikisha kuna umbali wa kutosha kati yako na gari la mbele yako vinginevyo utajikuta ni lazima ukanyage breki kwa haraka na kwa kushitukiza ambako kunasababisha injini kula mafuta zaidi.

Kutobeba Mizigo Mizito Kwenye Gari
Uzito unapoongezeka katika gari hufanya injini kutumia nguvu nyingi kusukuma gari na hivyo kuhitaji mafuta mengi zaidi. Punguza mizigo isiyo ya lazima katika gari ukiwa unaendesha.


Kutoacha Gari Likiwa Linawaka Bila Kutembea
Utafiti unaonesha kuwa kwa wastani gari linatumia lita zipatazo 2 kwa saa kama likiwa linawaka bila kutembea. Sababu ni kuwa katika hali hii injini huwa inatembea na inahitaji mafuta kuzunguka.

Kama gari halitembei unashauriwa kuzima injini ili kupunguza matumizi ya mafuta.

Zingatia: Usiache gari likiwa linawaka zaidi ya dakika 1 bila kutembea

Zima Kiyoyozi (AC) Katika Mwendo Mdogo
Katika mwendo kasi wa chini ya 90 km/saa zima kiyoyozi na fungua madirisha. Kiyoyozi kinazungushwa na injini hivyo kutumia mafuta zaidi. Kukiwa unaenda spidi zaidi ya 90km/saa unatatumia mafuta kidogo ukifunga madirisha na kuwasha kiyoyozi.

Endesha Gari Likiwa na Matairi Yenye Upepo wa Kutosha
Matairi yenye upepo mdogo yanasababisha kuongezeka kwa eneo linalokanyaga barabara na hivyo nguvu nyingi inahitajika kusukuma gari.

Hakikisha matairi ya gari lako yana upepo katika viwango sahihi.

DEREVA ALIYEKUFA KWENYE AJALI ILIYOUA 19 MBOZI KUSHTAKIWA


 Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini, kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi, Fortunatus Muslim ameagiza dereva wa gari lililosababisha ajali iliyoua watu 19 akiwamo yeye mwenyewe katika Mlima Senjele wilayani Mbozi mkoa wa Songwe ashtakiwe.

Aidha, ametoa maagizo matatu ya kutekelezwa haraka ili kukomesha ajali zinazojitokeza mara kwa mara na kuua watu wengi katika eneo hilo.

Alitoa maagizo hayo jana siku moja baada ya kutokea ajali ya lori kugongana na basi aina ya Coaster na kusababisha vifo vya watu 19 katika mlima Senjele Mbozi mkoa wa Songwe.

Akizungumza katika eneo ajali hiyo iliyotokea Februari 21 mwaka huu saa 3:15 usiku, kamanda Muslim alitaja jambo la kwanza ni polisi kufanya uchunguzi wa kina ili kupata chanzo cha ajali hiyo na hatua kuchukuliwa kwa dereva na mmiliki wa gari hilo.

"Hata kama dereva wa gari hilo amefariki lakini ipo sheria inayotumika kumshitaki na pia mmiliki wa lori hilo amekwishajulikana na askari wa usalama barabarani wanamfuatilia ili naye aje ajibu tuhuma za kuruhusu gari lake kutembea barabarani likiwa bovu," alisema.

Na Stephano Simbeye, Mwananchi

Picha: Mtendaji Mkuu TEMESA afanya ziara Mkoani Iringa, Njombe na Mbeya



Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle amefanya Ziara ya Utendaji kazi Mkoani Njombe











Abdu Kiba afunguka ishu kupigwa chini kwenye show za Alikiba ‘hawanilipi siwezi kwenda nae’ (+video)

Msanii wa muziki kutoka Kings Music Records, Abdu Kiba amefunguka sababu za yeye kutotumbuiza na alikiba kwenye show zake za nje, ile hali wasanii wenzake kutoka kwenye lebo hiyo wanasafiri na Alikiba kwenda kupiga show.

The post Abdu Kiba afunguka ishu kupigwa chini kwenye show za Alikiba ‘hawanilipi siwezi kwenda nae’ (+video) appeared first on Bongo5.com.


Source

Waandaaji wa SZIFF washambuliwa mitandaoni, Johari ashangazwa na washindi wa tuzo ya muigizaji bora wa kike na kiume (+video)

Jana usiku kulikuwa na ugawaji wa tuzo za filamu za SZIFF, ambapo tulishuhudia waigizaji wa filamu wa ndani wakiibuka kidedea. Ugawaji wa tuzo hizo, umezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii hususani kwenye kipengele cha muigizaji bora wa kike na kiume, ambapo washindi walikuwa ni Flora Kihombo na Rashid Msigala kupitia filamu yao ya KESHO. Kiufupi …

The post Waandaaji wa SZIFF washambuliwa mitandaoni, Johari ashangazwa na washindi wa tuzo ya muigizaji bora wa kike na kiume (+video) appeared first on Bongo5.com.


Source

Saturday, February 23, 2019

Yanga yapata pigo kwa kufiwa na kiongozi wake

Yanga yapata pigo kwa kufiwa na kiongozi wake
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Mustapha Urungu, amefariki dunia mchana wa leo Jumamosi Februari 23, 2019 nyumbani kwake Temeke.

Msemaji wa Yanga Dismas Ten amethibitisha taarifa hizo kwa kusema Urungu amefariki dunia akiwa nyumbani kwake na chanzo ni presha kushuka.

Ten ameongeza kuwa kwa mujibu wa familia ya marehemu Urungu ni kwamba aliamka akiwa sawa lakini ghafla mchana leo alizidiwa na kufariki dunia.

Mwili wa Urungu utasafirishwa kwenda kwao Wilayani Rufiji mkoani Pwani kwaajili ya mazishi ambayo yatafanyika kesho Jumapili.

Ndani ya Yanga Urungu alikuwa na nafasi mbili ambazo ni makamu mwenyekiti wa kamati ya mashindano pamoja na makamu mwenyekiti wa kamati ya usajili.


How to learn a language in 2019? Here is the '15 min method'
Babbel
|
Sponsored
This Natural Weight Loss Fruit Can Easily Help You Drop Pounds
Purple Mangosteen | Supplement
|
Sponsored
15 Emotional LGBTQ Wedding Pictures That Will Melt Your Heart
Beauty Secondly
|
Sponsored

7 Insider Secrets to Booking Cheap Flights
Relocation Target
|
Sponsored
If You Eat Ginger Root Every Day, This is What Happens To Your Body
Health & Human Research
|
Sponsored
Afikishwa mahakamani kwa kuvamia msafara wa Rais | East Africa Television
Mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina la Adriunus Landnam (34) mkazi wa Mkunazini, Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, amefikishwa mahakamani kwa kosa la kuingilia msafara wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dr Alli Mohamed Shein.
EATV

TOP STORIES

SPORT
"Shughuli ya Lechantre imekwisha"-Manara

SPORT
Ngoma ashindwa kuichezea Azam, Kagame

CURRENT AFFAIRS
Amuua mke mwenza na kumzika shambani

CURRENT AFFAIRS
Mbunge wa CHADEMA, ajiuzulu na kujiunga CCM


MOST POPULAR

CURRENT AFFAIRS
Makamu wa Rais asikitikia rufaa ya kina Mbowe

CURRENT AFFAIRS
Afikishwa mahakamani kwa kuvamia msafara wa Rais

ENTERTAINMENT
Fid Q awataja walioiba fedha za rambirambi

SPORT
Meddie Kagere sasa ni wa pili Afrika

ENTERTAINMENT
Mfahamu Mtanzania aliyeigiza kwenye Game of Throne
ABOUT US
ABOUT USADVERTISEJOBSTERMS & CONDITIONSCONTACT USFREQUENTLY ASKED QUESTIONS
NETWORK
IPP MEDIAEAST AFRICA RADIOITVRADIO ONECAPITAL RADIOLOKOPROMO
© 2019 East Africa Television Limited. All Rights Reserved


Watu waanza kupora mali za Godzilla | East
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...