Wednesday, February 27, 2019
Msiba Hautakuwa wa majonzi kama Bali Itakuwa ni kusherehekea maisha yake kama ambavyo mwenyewe alitaka Iwe- Kusaga
Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group Joseph Kusaga amesema kwamba msiba wa Ruge hautakuwa wa majonzi kama ilivyozoeleka, bali itakuwa ni kusherehekea maisha yake kama ambavyo mwenyewe alitaka iwe.
Kusaga amezungumza hayo akisema kwamba kabla Ruge hajafariki, aliwahi kusema kuwa ikitokea siku amekufa, basi watu wasihuzunike sana, bali washerehekee maisha yake na vile alivyo vifanya wakati yupo hai.
"Kuna kitu alikuwa akisisitiza, kwamba ikitokea bahati mbaya Mwenyezi Mungu amemchukua, tu-'celebrate' maisha yake, tu-'celebrate' alivyovifanya, kwa hiyo tutaanza maombolezo lakini yatakuwa ku-'celebrate' mazuri aliyoyafanya, hii alisisitiza wazi kabisa, na mimi kumpa heshima hiyo ni lazima tu-'celebrate' mengi mazuri aliyoyafanya", amesema Kusaga.
Akiendelea kuzungumzia hilo Joseph Kusaga amesema kwamba Ruge amefanya mengi mazuri ambayo yalifaa kutunukiwa, huku akitoa shukrani kwa serikali kwa kuwa nao bega kwa bega, kwenye kipindi hiki kigumu kwao.
"Inaweza ikawa sio wakati mzuri wa kusema mengi, lakini Watanzania inabidi tujifunze kutoa tuzo au kitu chochote kizuri kwa mtu aliyefanya mambo mazuri, amefanya mengi mazuri kwenye tasnia hii na burudani, naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa serikali na viongozi wote ambao wamekuwa kwa kiasi kikubwa wamekuwa wako karibu sana kutu suport, ili kuhakikisha tunamponya na maisha yake yanaendelea", amesema Kusaga.
Ruge Mutahaba amefariki jioni ya Februari 26 huko Afrika Kusini, akipatiwa matibabu ya figo aliyokuwa akisumbuliwa nayo.
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...