Sunday, February 28, 2021

Uso kwa Uso ROSA REE na wasanii wachanga wenye unyama wa hatari Aliowachagua Kufanya Collabo Nao


Uso kwa Uso ROSA REE na wasanii wachanga wenye unyama wa hatari, Wafunguka baada ya kufanya NGOMA

VIDEO:


Tanzia : MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AFARIKI DUNIA


Andrew Mollel enzi za uhai wake

Na Mussa Juma - Arusha
 Mfanyabiashara maarufu mkoani Arusha, Andrew Mollel ambaye alikuwa mwanzilishi na Mkurugenzi wa kampuni mbalimbali mkoani Arusha amefariki dunia na kuibua simanzi kwa wakazi wengi wa jiji hilo.

Akizungumza na Mwananchi leo, Februari 28, Mbunge wa jimbo la Monduli , Fredrick Lowassa amesema kifo cha Mollel ni pigo kubwa katika jiji la Arusha kutokana na mchango wake.

Lowassa amesema taratibu za mazishi wa Mollel zinaendelea kufanywa na wanafamilia lakini, kubwa ambalo Arusha watamkumbuka ni kuandaa michoro ya mradi mkubwa wa nyumba za PPF zilizopo eneo la Kijenge jijini hapa ambalo lilikuwa ni eneo lake.

Mollel alikuwa pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Happy Sausages ,Kijenge Animal Products Limited, Georges Center Ltd na AGM Holding na pia mjumbe wa bodi mbalimbali hapa nchini.

Via Mwananchi

Wanaharakati 47 wakamatwa kwa makosa ya kufanya uasi Hong Kong


Polisi mjini Hong Kong imewakamata wanaharakati 47 wa kutetea demokrasia kwa makosa ya njama ya kufanya uasi ikitumia sheria iliyo na utata ya usalama wa kitaifa iliyopitishwa mwaka uliopita.


Wanaharakati hao wakiwemo wabunge wa zamani waliwahi kukamatwa mwezi Januari lakini baadae wakaachiliwa huru. Kulingana na taarifa ya polisi watu hao walikamatwa tena hivi karibuni na watafikishwa mahakamani Jumatatu. 


Wanadaiwa kukiuka sheria mpya ya usalama wa kitaifa iliyowekwa na China kwa kuhudhuria uchaguzi wa bunge ambao haukuwa rasmi katika eneo hilo lililo na utawala wa ndani. Kwa mujibu wa polisi mjini Hong Kong, washtakiwa hao wanajumuisha wanaume 39 na wanawake wanane walio kati ya umri wa miaka 23 na 64

Shambulizi la bomu Somalia


Watu watatu wameuawa wawili kati yao wakiwa wanajeshi katika shambulizi la bomu kwenye msafara wa jeshi Mogadishu, mji mkuu wa Somalia, Imetangazwa kuwa shambulizi hilo lililenga afisa mkuu wa jeshi.


Imeripotiwa kuwa afisa huyo amesema alinusurika tukio hilo bila kujeruhiwa, lakini wanajeshi 2 na raia 1 walifariki katika mlipuko huo, Hakuna mtu aliyedai kuhusika na shambulizi hilo bado.


Wafungwa watoroka gerezani Haiti: 25 wafariki

 


Watu 25 wameripotiwa kufariki wakiwemo wafungwa 6 kufuatia ghasia zilizotokea wakati wafungwa walipokuwa wakijaribu kutoroka gerezani nchini Haiti.


Kulingana na taarifa za vyombo vya habari, wafungwa ambao walianzisha ghasia katika Gereza la Croix-des-Bouquets karibu na mji mkuu wa Port-au-Prince na kujaribu kutoroka, walipambana na polisi.


Wakati wa makabiliano na vikosi vya usalama, watu 25, wakiwemo wafungwa 6 kati walipoteza maisha, na zaidi ya wafungwa 200 wakatoroka gerezani.


Mamlaka ilitangaza kuwa wafungwa walishambulia raia wakati wa kutoroka gerezani, na kusababisha raia kadhaa kufariki.


Imebainika kuwa polisi wamewakamata wafungwa 69 hadi sasa katika operesheni iliyoanzishwa dhidi ya wafungwa waliotoroka gerezani.


Kwa upande mwingine, inasemekana kwamba mmoja wa viongozi wa magenge yenye silaha huko Haiti alikuwa miongoni mwa wafungwa waliotoroka gerezani.


Rais Jovenel Moise alitoa taarifa kwenye akaunti yake ya Twitter kuhusu tukio hilo na kusema,


"Tunalaani wale waliokimbia kutoka gereza la Croix-des-Bouquets na tunawasihi watu wawe na utulivu. Nimetoa maagizo yote muhimu kwa Polisi wa Kitaifa kudhibiti hali hiyo."


Gereza la Croix-des-Bouquets linatajwa kama mahali pa mfano kwa wapinzani wanaotuhumiwa kujaribu kutekeleza mapinduzi dhidi ya Rais Moise mnamo 7 Februari.


MKURUGENZI WA SHIRIKA LA AGRI THAMANI FOUNDATION MH NEEMA LUGANGIRA AONGOZA ZOEZI LA KUGAWA TAULO ZA KIKE WANAFUNZI 1,800 MANISPAA YA BUKOBA

 

MKURUGENZI wa Agri Thamani ambaye Pia ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia NGOs Mh Neema Lugangira akigawa taulo za kike kwa wanafunzi wa shule za Sekondari
WANAFUNZI wa kike wa shule za Sekondari wakifurahia kupokea mfuko wao uliojaa taulo za kike za kutosha mwaka mzima kwa kila mmoja
FUSO lililokuwa limejaa Taulo za kike za wanafunzi wa kike 1800 wa Bukoba Manispaa likiingia kwenye uwanja wa Kaitaba Bukoba mjini likitokea Dar es Salaam
Mabox ya Taulo za kike ambazo zote zilikuwa zimeandikwa Jina la Shule ya Sekondari kwa Idadi Kamili ya Wanafunzi wa Kike

Hivi ndivyo kila mwanafunzi wa kike alivyoondoka uwanja wa Kaitaba na Furaha



Mkurugenzi wa Agri Thamani; Mhe Neema Lugangiea (Mb.) ambae pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) kupitia Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Mh.Neema Lugangira ametoa msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi 1800 kutoka kwenye shule 16 za Manispaa ya Bukoba .

 

Ambapo kila mwanafunzi mmoja ataweza kutumia taulo alizopewa kwa kipindi cha mwaka mmoja katika zoezi ambalo iliyofanyika kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Kwa Manispaa ya Bukoba jumla ya packet 25,200 za Taulo za Kike ziligawiwa kwa Wanafunzi wa Kike 1,800 kutoka Sekondari 16 za Kata zote 14 za Manispaa ya Bukoba.


Akizungumza wakati wa ugawaji wa taulo hizo katika zoezi ambalo liliratibiwa na Idara ya Elimu Sekondari Bukoba Manispaa na Afisa Elimu Taaluma Sekondari alishiriki zoezi zima.

 

Mhe Neema Lugangira amesema ameamua kufanya hivyo ili kuwasaidia wanafunzi hao kuweza kujihifadhi na kuweza kuendelea na masomo yao wakati wa  kipindi cha hedhi.

 

Alisema wanafunzi ambao watanufaika na msaada huo ni kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne ambao kwa sasa wataondoka na adha ambayo walikuwa wakikumbana nao wakati wakiwe kwenye kipundi cha hedhi.

 

"Naamini msaada huo utakuwa na manufaa makubwa kwao kutokana na kwamba watatumia muda mwingi kusoma hata wakiwa kwenye kipindi chao cha hedhi kutokana na kuwa na taulo ambazo zitawasaidia" Alisema Mbunge huyo.

 

Akizungumzia kuhusu msaada huo wa Taulo za Kike, Afisa Elimu Sekondari Manispaa ya Bukoba Mjini Emanuele Ebeneza alimshukuru Mbunge Neema kwa msaada wake wa taulo za wasichana ambao utakuwa chachu ya kupunguza utoro shuleni.

 

Alisema kupitia msaada huo wanafunzi wengi watajua namna ya kujihifadhi na kupunguza utoro shuleni kwa sababu ya kutokujisikia vizuri kwenye kipindi cha hedhi.

 

"Niseme tu kwamba licha ya kutoa msaada huo lakini pia Mbunge Neema anafundisha wanafunzi juu ya hedhi salama,  anawaandaa kisaikolojia kupita kwenye kipindi cha hedhi na hivyo kuwaondolea hofu na anawapa elimu ya lishe bora inayowasaidia waepukane na changamoto ya upungufu wa damu (anemia) "Alisema Afisa Elimu Sekondari Bukoba Manispaa. 

 

Afisa Elimu Sekondari huyo alisema kwamba pia Mbunge Neema Lugangira anawafundisha usafi hatua ambayo inasaidia kupunguza utoro ambao ungetokana na wanafunzi kushindwa kuhudhuria masomo wakati wa mzunguko wa hedhi.

 

"Kama unavyojua mzunguko wa wasichana unatokea kila mwezi mara moja na wakati mwengine wakishindwa kuhudhuria masomo hivyo alilolifanya ni kitu cha muhimu sana sana kwa maana ya wanasichana "Alisema Ndg Ebeneza

 

Mmoja wa wanafunzi hao Alisema kwamba changamoto kubwa ni kubwa pale pedi zinapokuwa zimekwisha wanashindwa kuishi kwa amani kabisa wakati wakiwa wanaendelea na masomo

 

Naye mwanafunzi mwengine amesema wanashukuru kwa msaada huo kutokana na kwamba wakati mwengine wamekuwa wakikosa shule kutokana na kutokuwa na taulo za kujihifadhi wakati wakiwa kwenye kipindi cha hedhi.

 

Hata hivyo Avitha Faustini ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari  Hamugumbe alimshukuru Mbunge Neema kwa msaada huo ambao amewapatia ambao umekuwa ni faraja kubwa kwao na kuwaondolea changamoto walizokuwa wakikumbana nazo.

 

Alisema wamepata ujasiri wa kuendele na masomo kwani kabla ya kupata Taulo  hizo walikuwa wakitokewa na hali hiyo wanakuwa wanyonge na wakati mwengine hulazimika kurudi nyumbani na  kukosa masomo. Aliongezea kwamba sasa hivi hawana haja ya kuwaomba wazazi pesa ya kununua pedi.

Mwanafunzi mwingine alikiri kwamba wengi hawajawahi kuziona taulo za kike na alielezea njia ambazo wengi wao wanatumia ambazo kwakweli hata sisi tunashindwa kuziandika maana sio salama kabisa. Mwanafunzi huyu alionyesha furaha ya aina yake kuona kwamba wamekumbukwa na kuthaminiwa hata kama wao ni watoto wa kimaskini.

Mradi huo wa Taulo za Kike umeshawanufaisha  Watoto wa Kike katika mikoa ya Dodoma, Tabora, Pwani, Tanga, Kigoma, Mtwara na Kagera na mikoa inayofuata kwa awamu hii ya kwanza ni Ruvuma na Lindi

Mbunge Neema Lugangira alimalizia kwa kusema kwamba Jumla ya Wanafunzi wa Kike 5,500 nchini watakuwa wamenufika ifikapo mwezi Mei 2021 ambapo Taulo za Kike zote zimetengenezwa na Kiwanda cha Tanzania ambacho kinauzoefu wa zaidi ya miaka 40 kwenye eneo hili. 

 


Tumeshampendekeza Mrithi Wa Maalim Seif


Sehemu ya hotuba ya kiongozi wa chama Cha ACT Wazalendo Ndg, Zitto Kabwe kwenye khitima ya kumuombea Maalim Seif iliyofanyika Dar-es-salaam.


"Tayari tumeshapendekeza jina kwa rais wa Zanzibar la mtu Ambaye atarithi Majukumu Ambayo Maalim Seif alikuwa anafanya.


Bahati nzuri Maalim alikuwa ni kiongozi bora na alijua kuna siku mwenyezi mungu atamchukua kwasababu sisi sote lazima turejee kwa Mwenyezi mungu kama kama tulivyoambiwa na mafunzo ya dini zetu.


Kwa hiyo aliacha  Ametupa maelekezo ya nini kitokee endapo atatangulia Mbele ya Haki.


Namshukuru mwenyezi mungu kwamba viongozi wa chama wamsfuata yale Maelekezo yake kwa namna ambayo kiongozi wetu alituelekeza. Sasa umebaki wajibu wa Rais wa zanzibar kuyatekeleza hayo.


Sisi tunaamini kabisa kuwa huyo Ambaye amependekezwa ataweza kusimamia Maridhiano na haki za wazanzibar kama ambavyo Maalim seif alisimamia.


Tunawaomba muendelee kutuombea duwa ili tusitoke kwenye mstari, tuendelee kupigania demokrasia, haki na kuhakikisha kuwa nchi yetu inaendelea kuwa ya Amani ya Amani iliniweze kupata Maendeleo ya Watu"


Source

Saturday, February 27, 2021

Iran yasema mashambulizi ya Marekani nchini Syria yachochea ugaidi


Katibu wa baraza kuu la usalama wa kitaifa nchini Iran Ali Shamkhani amesema leo kuwa mashambulizi ya angani yaliofanywa Ijumaa na Marekani dhidi ya wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran katika eneo la Mashariki mwa Syria yanachochea ugaidi. 


Marekani imesema kuwa mashambulizi hayo katika ngome za wanamgambo hao wa Kataib Hezbollah katika mpaka na Iraq ni kujibu mashambulizi ya roketi dhidi ya malengo ya Marekani nchini Iraq.


Shamkhani amemwambia waziri wa mambo ya nje wa Iraq aliyeko ziarani nchini humo Fuad Hussein kwamba vitendo hivyo Marekani vinaimarisha na kupanua vitendo vya kigaidi vya kundi la itikadi kali la Daesh katika eneo hilo. 


Mashambulio hayo ya anga yalilenga maeneo ya wanamgambo katika upande wa Syria katika mpaka kati ya Iraqi na Syria ambapo makundi yanayoungwa mkono na Iran yanadhibiti njia muhimu ya kuvukishwa kwa silaha, wafanyakazi na bidhaa.

SABABU Zinazopelekea Wasichana wa Kileo Mpigwe Chini na Wanaume Kimapenzi


Kumekuwa na ulalamishi sana miaka ya karibuni kuwa wanaume sijui tupoje,tunawaacha bila sababu ila kumbe sababu zipo tu ila wengi hawajazijuaga tu.Nimeona nibainishe sababu zangu kadhaa ambazo ni hizi hapa:

1. Hufanyi chaguo sahihi
Marazote unapenda mtu mwenye swaga,status ambaye kila msichana anamtaka bila kujali kuwa swaga si jambo la msingi katika mahusiano ila penzi la kweli na utu.80% ya wale mnaowadiss ndio wana mapenzi ya kweli na utu uliotukuka!Wenye swaga huwa hawana future wanasuuza rungu tu wakati wakiskilizia kali mara nyingi akitokea mkali zaidi ujue ushalia!

2. Kupenda ready made
Jaribuni kuanza mapenzi na mtu sahihi tokea akiwa chini ili mfurahie mafanikio badae.Mara nyingi mwanaume ulieanza nae kwenye msoto hana jeuri ya kukuacha.Unakurupuka kwa mtu mwenye life lake tayari hujui kahaso vipi kuupata mchomoko unaleta shobo za kujitia unamjua sana.Utaumia maana ukizingua kidogo anapita hivi!

3. Kuendekeza uzungu mwingi
Kina dada wengi siku hizi hampendi kuwa chini,hutaki kuishi uhalisia ila unaendekeza u-instagram na tamthilia nyingi kitu ambacho sio sahihi.Ni nani ambaye kila 24/7 kwake sikukuu na jua lilivyo kali hapa bongo.Kila siku shopping kweli? Niwape cheat,wanaume wengi wanalijua hilo so wana row with the tide.Mlume ndago hawezi kuwekeza kwenye bidhaa feki ndio maana mnaona tunaoa midemu mikauzu yenye full uhasilia na ina akili za maisha baada ya miaka miwili/mitatu ya huduma wanakuwa bomba ile mbaya watu wanabaki midomo wazi.Hivyo basi be real jameni...

4.Tamaa tamaa
Hii inaweza isiwe kwa mademu wote ila wengi siku hizi mnamaindisha mapene,mizinga mingi bila kujali kipato cha ME ili yasapoti pointi namba 3 apo juu.Hii itakufanya uwe na mibwana mingi kitu ambacho sio rahisi mwanaume mwenye akili timamu na anayejua thamani ya penzi kukivumilia.Ukimwi upo na unaua jamani! Hamna mwanaume atayependa umchanganyie kimaisha na akigundua tu anatoka baru.

5. Personal traits
Je una akili za maisha(mipango)? ni msafi,msikivu,mvumilivu,unajia mini,mwaminifu,mkweli,huna choyo,sio mswahili kwa sana,unapendeka n.k hivi ni baadhi vitu muhimu sana ambavyo inabidi mwanamke avibalansishe na mbele ya mwanaume sahihi atajitwalia upendo wa kweli.

6. Sex
Inakubidi uwe fresh pia hapa ili uweze kuwa mtamu zaidi.Kuna wanaume ambao wamefanikiwa kutulizwa tuli baada ya kukutana na mashine nzuri sana ukijumlisha na yaliomo kwenye point 5 apo juu wakaamua kuoa kabisa.Wapo! Kwahiyo nafikiri pia umahiri wa kitandani una nafasi kubwa zaidi ya kumtuliza mwanaume sahihi! Ukiwa legelege utaachwa tu maana hamna namna nyingine.

NB: HUU NI MTAZAMO TU WAKUU MSIJENGE CHUKI

Naomba na wengine muongeze sababu nyingine ili wapate majibu kwa nini wanaachwa bila sababu!

Kajala Avunja Ukimya Kubeba Mimba ya Harmo




KAJALA Masanja ameendelea kutikisa vyombo vya habari, safari hii amefunguka mambo mengi ikiwemo suala la kumbebea mimba mpenzi wake, Rajabu Abdul 'Harmonize', RISASI limezungumza naye.

 

 

Mwanamama huyo ambaye ni 'pisi' kali kutoka kiwanda cha Bongo Muvi, amesema kuwa ametukanwa sana kwenye mitandao ya kijamii kuhusu uhusiano wake huo mpya lakini ukweli utabaki palepale kuwa moyo hauendeshwi na hisia za mtu mwingine hivyo wamuache aendelee na mambo yake.

 

 

Mazungumzo yake na RISASI yalikuwa kama ifuatavyo:

Risasi: Kajala naona mambo ya mabodigadi na jeshi siku hizi… Kajala: (Kicheko) nimebidi nicheke.

 

 

Risasi: Vipi lakini unaendeleaje kwenye penzi lako jipya?

Kajala: Niko poa kabisa naendelea kama kawaida na ninafurahi sana penzi langu na sidhani kama kuna anayenidai mimi.

Risasi: Vipi kuhusu maneno ya waja mitandaoni.

 

 

Kajala: Nilishatukanwa sana toka huko nyuma na kwa mambo mengi, hivyo waendelee tu kufanya wawezavyo au kutukana wanavyotaka kwa maana hakuna mtu ambaye anabeba hisia za moyo wangu, waache maisha ya watu wengine yaendelee.

 

 

Risasi: Mna mpango wowote kuhusiana na kufunga ndoa?

Kajala: Kila jambo lina mpangilio na taratibu zake kwa hiyo kama hilo lipo basi litakuja tu.

Risasi: Lakini nakumbuka kama bado ile ndoa ya Katoliki uliyofunga na Chambo kidini bado ipo, maana ndoa za Katoliki hazifunjiki?

Kajala: Ndoa hiyo tulishakamilisha taratibu zote na talaka ilishatoka hivyo sina ninachodaiwa.

 

 

Risasi: Una mpango wa kumbebea mimba na kumzalia Harmonize?

Kajala: Mungu akipenda maana kila kitu ni mpango wa Mungu.

Risasi: Lakini nasikia kama kuna ugomvi wa chinichini wewe na Wolper (Jacqueline)?

 

 

Kajala: Mimi sijajua hilo maana naangalia zaidi mambo yangu, kama kuna mtu ana tatizo na mimi sawa ila mimi niko sawa kabisa.

Risasi: Vipi kuhusu Paula, ishu yake inaendeleaje?

Kajala: Hii ishu iko kwenye mikono ya sheria ndio maana sitaki kuiongelea kabisa kwa sasa.

 

 

Risasi: Unawaambiaje ambao wanakuchamba kuhusiana na malezi ya Paula?

Kajala: Ni ngumu sana kubishana nao kwa sababu mimi ndio ninayejua namleaje mtoto wangu hivyo sitaki kupoteza muda wangu kwenye hilo hata kidogo.

Risasi: Vipi kuhusu shule Paula?

 

 

Kajala: Anaenda hivi karibuni.

Risasi: Haya shukrani.

Kajala: Asante na karibu tena!

Baba Mzazi wa Young Killer afunguka mazito


Baba mzazi wa msanii wa HipHop Young Killer, anayefahamika kwa jina la Mzee Msodoki ambaye amesema chanzo cha kutokuwa sawa na mwanaye huyo ni mama yake kumwambia kwamba baba yake amefariki tangu utotoni.


Mzee Msodoki amesema mama Young Killer aliamua kumwambia hivyo mtoto wao kwa sababu aliumizwa na kitendo cha Mzee Msodoki kuukimbia ujauzito wa msanii huyo kabla hajazaliwa na kwenda kuishi nchini Congo DR.


"Mama Young Killer nilikuwa nakaa naye jirani kule Mwanza, wakati huo nilikuwa nafanya kazi Saloon, tukawa kwenye mahusiano ambayo yalidumu kama miezi 6 na baadaye akaniambia ana ujauzito, sasa kwa wakati huo mimi nilikuwa sijajiandaa kulea na majukumu hivyo nikapata safari ya kwenda Congo nilivyorudi sikumkuta" ameeleza Mzee Msodoki 


"Nimekuja kugundua kama mtoto yupo na ameshakuwa mkubwa ila mama yake alishamwambia kwamba baba yake ameshakufa wakati mimi nipo, ndiyo maana hata yeye haamini kama mimi ndiyo baba yake kweli" ameongeza 


Mzee Msodoki amesema aliwahi kukutana na Young Killer na alimwambia kama yeye ndiyo baba yake lakini alijibiwa kwamba hana shida lakini mpaka mama yake amdhibitishie.

Saudia yakanusha Bin Salman kuhusika na kifo cha Khashoggi

 


Saudi Arabia imekanusha vikali ripoti ya kijasusi iliyotolewa na Marekani ikifichua kuwa mrithi wa kiti cha ufalme wa nchi hiyo Mohammed bin Salman aliidhinisha mauaji ya mwandishi habari Jamal Khashoggi mwaka 2018.


Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya kigeni ya Saudi Arabia imesema serikali mjini Riyadh inaipinga vikali ripoti hiyo ikisema imejaa taarifa za uzushi na tathmini isiyokubalika kuhusu utawala wa falme hiyo ya eneo la Ghuba.


Tathmini hiyo ya Marekani iliyotolewa na utawala wa rais Joe Biden kutoka ripoti pana ya kijasusi imehitimisha kuwa Bin Salman aliidhinisha operesheni ya kumkamata au kumuua Khashoggi mjini Istanbul, nchini Uturuki.


Hapo kabla Saudi Arabia ilisema mauaji ya Khashoggi kwenye ubalozi mdogo wa Saudi Arabia nchini Uturuki yalifanywa katika operesheni ya kihalifu na kukanusha kuhusika kwa mwanamfalme Salman.


"Kwa bahati mbaya kuwa ni kweli kwamba ripoti hii, ikiwa na hitimisho lisilo sahihi, imetolewa wakati falme hii imekwisha kosoa uhalifu huo wa kutisha, na uongozi wa Saudia ulichukua hatua zinazohitajika kuhakikisha kisa kama hicho hakitokei tena" imesema sehemu ya taarifa ya wizara hiyo ya mambo ya kigeni.


Taarifa hiyo pia imeongeza kusema Saudi Arabia inapinga kile imeikiita uingiliaji wa utawala wake na uhuru wa mfumo wake wa kutoa haki.


Kwa mujibu wa ripoti ya Marekani, kutokana na ushawishi wa mwanamfalme Salman siyo rahisi kuwa mauaji ya Khashoggi yalitokea bila kuyaidhinisha.


Jamal Khashoggi aliyekuwa uhamishoni Marekani akiandika ripoti zinazomkosoa Mohammed Salman na serikali ya Saudi Arabia, aliuwawa tarehe 2 mwezi Oktoba mwaka 2018.


Muandishi huyo aliyekuwa na umri wa miaka 59 wakati wa mauaji yake, aliambiwa na balozi wa Saudia afike katika ubalozi wa taifa hilo mjini Istanbul, ili kupata nyaraka kadhaa alizohitaji ili aweze kufunga ndoa na mpenzi wake raia wa Uturuki, Hatice Cengiz.


wezi mmoja baada ya mauaji hayo, shirika la Ujasusi la Marekani, CIA lilisema kwa kujiamini kuwa mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman, ndiye aliyeamuru mauaji hayo.


Mwenyewe Bin Salman anakanusha madai hayo 


Mrithi huyo wa kiti cha ufalme, Mohammed bin Salman, ameendelea kukanusha kuhusika na mauaji hayo hata baada ya washauri wake wa karibu kutiwa hatiani na mamlaka za sheria nchini mwake kuwa kuhusika nayo.


Kufuatia kutolewa kwa ripoti hiyo, waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani, Antony Blinken amesema Washington inalenga kuchukua mwelekeo mpya wa kisera lakini siyo kuvuruga mahusiano yake na Saudi Arabia ambayo ni mshirika wa karibu wa usalama kwenye eneo la Mashariki ya Kati.


Licha ya hasira iliyoelezwa na Saudi Arabia, nchi hiyo imesisitiza nia yake ya kuendeleza uhusiano na Marekani.


"Ushirika baina ya Marekani na Saudi Arabia ni imara na stahamilivu" imesema taarifa kutoka Saudia.

Fei Toto: Tutashinda leo mechi yetu na Kengold ya Mbeya



FEISAL Salum, kiungo wa Klabu ya Yanga amesema kuwa wana amini kwamba watapata ushindi kwenye mchezo wa leo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 32 bora dhidi ya Kengold ya Mbeya.

Uwanja wa Uhuru saa 10:00 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa ambapo timu ambayo itashindwa kupata matokeo itatolewa jumlajumla.


Feisal amesema kwa namna ambavyo wamejiandaa inawapa nafasi kupata ushindi ndani ya uwanja kwenye mchezo huo muhimu.


"Tupo sawa na tunaamini kwamba kila mchezaji anahitaji kuona timu ikishinda hivyo tutapambana kupata matokeo ndani ya uwanja.


"Inawezekana kupata ushindi na nafasi yetu ipo pia tunawaheshimu wapinzani wetu hilo lipo wazi kwa kuwa nao pia wanahitaji ushindi," .

Marekani inasema Mwanamfalme wa Saudia aliidhinisha mauaji ya Khashoggi




 Ripoti ya kijasusi ya Marekani imebaini kuwa Mwnamfalme wa Saudia Arabia Mohammed bin Salman aliidhinisha mauaji ya mwandishi wa habari wa nchi hiyo aliyekuwa ukimbizini Jamal mwaka 2018.



Ripoti iliyotolewa na utawala wa Bw Biden inasema mwanamfalme aliidhinisha mpango wa "kumkamata au kumuua" Khashoggi.



Marekani ilitangaza vikwazo kwa makumi kadhaa ya Wasaudia lakini sio dhidi ya mwanamfalme mwenyewe.



Saudi Arabia ilipinga ripoti hiyo ikiitaja kuwa "hasi, uongo na isiyokubalika ".





Mwanamfalme Mohammed, ambaye anatambuliwa kama mtawala wa ufalme, amekanusha kuhusika kwa namna yoyote ile katika mauaji hayo.


Khashoggi aliuawa alipokuwa akiutembelea ubalozi mdogo mjini Instanbul , Uturuki , na mwili wake ulikatwa katwa.



Mwandishi huyo wa habari aliyekuwa na umri wa miaka 59 wakati mmoja aliwahi kuwa mshauri wa serikali ya Saudi Arabia na alikuwa karibu sana na utawala wa Ufalme , lakini alikosana nao na kwenda nchini Marekani mwaka 2017.



Akiwa nchini Marekani, aliandika waraka wa kila mwezi katika gazeti la Washington Post ambapo alikosoa sera za Mwanamfalme Prince Mohammed.

FURAHIA HUDUMA ZA KIBENKI UKIWA NA 'SIMBANKING' MZIGO ULIOBORESHWA

Benki ya CRDB imeboresha huduma yake ya SimBanking na kuipa jina la Benki ni SimBanking 'Mzigo Ulioboreshwa' . Maboresho haya makubwa yanampa uhuru mkubwa mteja kufanya miamala yote kupitia SimBanking na ndiyo maana sasa inaitwa Benki ni SimBanking.

Benki ni SimBanking inawawezesha wateja kufungua akaunti wenyewe bure popote walipo na kupata huduma za kibenki mbalimbali ili kuhakikisha Benki ya CRDB inakuwa kinara wa teknolojia katika utoaji wa huduma za kibenki.


Ridhiwani Kikwete ‘afagilia’ Ujenzi Wa Jengo La Huduma Za Matibabu Ya Dharura Chalinze


NA ANDREW CHALE, CHALINZE

JIMBO la Chalinze  linatarajiwa kujengwa jengo la kituo cha huduma za Matibabu ya Dharura 'Emergency Department'  litakalosaidia Watanzania mbalimbali ikiwemo wa wanaotoka Mikoa jirani ikiwemo ya Tanga, Morogoro, Dar es Salaam pamoja na Pwani kupatiwa huduma za haraka na za  kibingwa pindi wapatapo shida za ajali ama majanga.


Hayo ameyasema Mbunge wa Jimbo hilo, Mhe. Ridhiwani Kikwete  wakati wa kukagua eneo litakalojengwa jengo hilo la mradi huo kwa udhamini wa Shirika la About Fund Tanzania, 


ujenzi unaotarajiwa kujengwa eneo la viunga vya  Hospitali ya Msoga, Halmshauri ya Chalinze.


"Niwashukuru sana Abbott Fund Tanzania   kwa jambo kubwa ambalo wamekuja kutufanyia hapa.


Imekuwa ni kilio cha muda mrefu, kama mnavyofahamu watanzania wengi hasa wanaotoka njia hii ya Tanga, lakini pia wanaotoka njia ya Morogoro kwa namna moja ama nyingine wamekuwa wakipata tabu sana hasa wanapopata matatizo ya kiafya au hata ajali kwa mfano watu wa Tanga wanapopita Kabuku na watu wa upande wa Morogoro wanapoondoka Morogoro,  wanapopata shida ya kiafya, Hospitali za karibu zimekuwa mbali sana kwao. 


Kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, Serikali ilielekeza Halmashauri ya Chalinze, pamoja na kujiandaa kupokea Wilaya lakini ijiandae kuwa sehemu ya 'center'  itakayotoa huduma hizo,


hivyo Serikali ilianza kwa kutupatia pesa, kama mnakumbuka zamani hapa kulikuwa na kituo cha afya, lakini serikali ikatoa pesa kukiongeza hadhi kituo hiki kiwe Hospitali. 


Majengo mengi yamejengwa, lakini katika jengo ambalo ni muhimu sana ambalo lilikuwa linasubiriwa kwa hamu ni lile la Huduma za Dharura 'Emergency Department' ambalo sasa leo tumekuja kuangalia na tumekutana na Wakandarasi na Mshauri ambao wamekuja kusimamia ujenzi huo.


Abbott Fund Tanzania wametuhakikishia kwamba watakuwa tayari kutoa pesa za ujenzi wa majengo hayo, pamoja na kuweka vifaa na mahitaji mengine ikiwemo huduma za maji zitakuwepo pale.


Pamoja na jengo lakini wataweka tanki la kuhifadhi maji lita Laki moja, lakini pia wataweka magari ya Wagonjwa 'Ambulance' ambayo yatakuwa yakifika sehemu itakayotokea ajali na kufika kutoa msaada wa haraka". Alisema Ridhiwani Kikwete.


Aidha, Ridhiwani Kikwete aliongeza kuwa;

"Kwangu mimi nisimame kwanza kuishukuru sana Serikali yetu chini ya Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kutusaidia kutupa mwanga ule wa nini ambacho kipo katika hili, kwa sababu kwa muda mrefu watu wa Chalinze walikuwa wanahitaji huduma hii lakini leo katika awamu ya tano tunakuja kuipata, 


Lakini pili kuishukuru pia Abbott Fund Tanzania kwa msaada huu wanaokuja kutupa.... Siku zote usione vyaelea, vimeundwa, waundaji wenyewe wapo, ili jambo nimshukuru sana Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, ambaye yeye ndiye alitufungulia milango ya kuonana nao Abbott Fund na kutupa fursa ya kukutana na leo wamefika kufanya jambo hili". Alisema Ridhiwani Kikwete.


Mbunge pia alitumia fursa ya kuwaasa Wananchi wa Chalinze, kwamba serikali yao inafanya kazi kubwa kuhakikisha wananchi wanapatiwa huduma ya afya lakini kwao wao ni kuona vifaa ama huduma hizo  wanazienzi na kuzitunza.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmshauri ya Chalinze, Ramadhani Possi, alishukuru Serikali pamoja na Wadau hao, Abbott Fund Tanzania kwa kuweza kutenga fedha za ujenzi wa jengo hilo la dharura katika Halmashauri hiyo.


"Kwa niaba ya Halmashauri ya Chalinze, tunawashukuru sana wadau wetu, Abbott Fund Tanzania, kwa kuja kutujengea jengo hili la dharura hapa kwetu Chalinze.


 Hii itatoa suluhisho la matatizo ambalo tulikuwa tunakabiriana nayo kwa upande wa huduma za dharura. Kwa hii ndio itakuwa Halmashauri ya kwanza ya Wilaya kuwa na jengo hili la huduma za Dharura.


Wadau hawa tayari wameshajenga  majengo kama hayo ya dharura kwenye mikoa ya Mbeya,  Dodoma, Arusha, Tanga na sasa wanakuja hapa kwetu ambapo wametuhakikishia mpaka mwezi Disemba mwaka huu litakuwa limekamilika". alisema Mkurugenzi huyo Ramadhani Possi.


Nae Msanifu wa majengo hayo ya Dharura kutoka Abbott Fund, Bwana. Vasco Bokera alisema ujenzi huo utaanza mara moja ambapo utachukua kuanzia miezi Saba hadi 12  hadi kukamilika kwake kulingana na hali ya hewa na mazingira.

4A9 NI SULUHISHO LA KINGA MWILINI


T.R. Msigwa anatoa msaada kwa watu wa sukari, HIV, kansa na maradhi mengine yenye kupunguza Kinga za mwili wao watachangia asilimia 45 TR. Msigwa atachangia asilimia zilizobaki na wale wenye matatizo ya kuchoka choka mwili na maradhi ya homa kali za vipindi tofauti tofauti  na ukosefu wa Kinga wasikose kutumia CHAMMY  TEA kwa mawasiliano zaidi zungumza na T.R.Msigwa Ili upate msaada huu 0713646691 au 0773149272


ANGALIA VIDEO HII.



Huyu Hapa Muuguzi Aliyenusurika Ajali Tatu za Meli Ikiwemo Titanic

 


Violet Constance Jessop alikuwa Nesi akihudumu kwenye Meli na anajulikana zaidi kwa kunusurika ajali tatu zilizowahi kutokea ikiwemo meli ya #Titanic ambayo ilitokea April 1912, akiwa na miaka 24


Ajali yake ya kwanza kunusurika ilikuwa 1911 ambapo ndio alikuwa anaanza kazi kwenye Meli ya Olympic ambayo kimsingi haikusababisha vifo


Ajali yake ya mwisho ilikuwa kipindi cha Vita ya Kwanza ya Dunia, Novemba 1916 akiwa ndani ya Meli ya #Britannic ambayo ilizama katika Bahari ya Aegean kutokana na mlipuko


Violet Constance Jessop alizaliwa Oktoba 2, 1887 na alifariki Mei 5, 1971 Nchini Uingereza akiwa na miaka 83

Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo February 27, 2021



















 

Friday, February 26, 2021

Amber Lulu: Pigeni Kelele, Nasubiri Kujifungua



AMBER Lulu ni bonge moja la msanii wa Bongo Fleva ambaye alianza kama muuza sura (video queen) kwenye video. Alianza kupata umaarufu baada ya kupiga picha za utupu na kuzisambaza mitandaoni huku Serikali ikishindwa kumchukulia hatua kutokana na kutokuwepo kwa sheria za kumbana wakati huo.

 

 

Amber Lulu anasema maisha yake ya nyuma yalikuwa yenye sarakasi nyingi akiwa na umri mdogo ambapo alilazimika kujitafutia hadi pesa ya shule.

 

 

Anasema wakati akiwa mdogo akisoma, mama yake alikuwa na tatizo na lililomfanya ashindwe kutimiza majukumu mengi ya kifamilia, hivyo akaamua kujiingiza kwenye masuala mbalimbali ya kujitafutia riziki ili aweze kumudu gharama za maisha.

 

 

Itoshe kusema kwamba unapozungumzia wasanii ambao wamepigana vilivyo mpaka kufikia hatua aliyopo bila kujali Dunia itawaonaje, basi mwanadada Amber Lulu anaweza akawa kwenye tano bora.

 

 

Leo amekuwa ni msanii mzuri wa Bongo Fleva akiwa na sifa ya ziada ya kuweza kumiliki vyema jukwaa.

Jina lake halisi ni Lulu Euggen ambaye kwa sasa ni mjamzito.

 

 

Katika mahojiano maalum (exclusive interview) na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, Amber Lulu anasema kuwa, watu wengi wanamshangaa na kuona amebeba ujauzito ni kama kitu cha ajabu au kimewashangaza hivyo anawaomba watulize kelele kwanza, yeye anasuburi kujifungua mtoto wake kisha maisha yaendelee. Amber Lulu, alizungumza hayo alipokuwa akifanya mahojiano na Ijumaa Wikienda kama ifuatavyo:



Wikienda: Habari Amber,na hongera naona mambo ni mazuri

Amber Lulu: Asante, Mungu akipanga lake amepanga kwakweli.

Wikienda: Ila umejificha sana watu wengi walikuwa hawajui kama ni mjazito, kwanini umejificha hivyo?

 

 

Amber Lulu: Macho ya watu nayaogopa kwasababu kipindi kama hiki lazima usiweke kila kuitu kwenye mitandao kwasababu hujui nani mzuri kwako,hivyo niliamua kujikalia tu.

Wikienda: Maana huko mitandaoni kila mtu anaongea lake na kutaka kujua baba wa mtoto.

 

 

Amber: Jamani hebu waniache nizae zangu,kelele wazipeleke huko mbele kwasababu hata wakimjua baba wa mtoto watanisaidia kuleta nepi au maziwa, lakini pia itawasaidia nini.

Wikienda: Unajua mastaa wengi wamekuwa na tabia ya kuwaweka wazi wapenzi wao na hata wewe kipindi cha nyuma ulikuwa unafanya hivyo sasa hapa nashangaa kwanini?

 

 

Amber: Kila kitu kinabadilika kutokana na mazingira,lakini pia nimejifunza mengi sana kuhusiana na kuweka wapenzi mitandaoni na tulikuwa hatujui tu kuwa hayo ni maisha binafsi ya mtu,tulikuwa tunakosema sana, mii hayo mambo sipendi kabisa,wasubiri tu mtoto watamuona kwasababu sio wa kuficha.

 

 

Wikienda: Sasa hivi huko kwenye hali hiyo,na ukiangalia maisha yako unategemea muziki kwa maana ufanye shoo ili chochote kiingie kinywani, hii inakuaje?

 

 

Amber: Nikipata shoo nafanya tu mbona kwasababu, hakuna kinachonizuia kabisa,kwasababu kuna wengine wanapanda jukwaani kuimba, wakishuka wanaenda kujifungua basi hata mimi napiga kazi kama kawaida hakuna shida maana mimi nimpambanaji toka kitambo sana.

 

 

Wikienda :Hivi ulishawahi kuzaa mtoto huko nyuma,au huyu utakayejifungua ndio kwanza?

Amber: Huyu Mungu, akinisaidia kujifungua salama ndio mtoto wa kwanza sikuwahi kuzaa mwingine kabla, wala sijawahi kuficha mtoto kama watu wengine wanavyofanya.

 

 

Wikienda: Ungependelea upate mtoto gani?

Amber: Mimi yeyote tu ambaye mwenyezui Mungu,atanichagulia nitashukuru.

Wikienda: Ni kitu gani ambacho utokipenda mtoto wako asikione akija kuwa mkubwa kuhusu wewe?

 

 

Amber: Kwanza kabisa natamani akikua asikute mitandao ya kijamii hii,tuliopitia wala asijue kilichowahi kutokea kuhusu mimi huko nyuma,yaani sitaki kabisa.

Wikienda: Haya asante sana Amber.

Amber: Shukurani sana.


Jafo aeleza chanzo shule za bweni kuteketea kwa moto

 


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Selemani Jafo amesema chanzo cha mabweni kuteketea kwa moto ni ubovu na uchakavu wa miundombinu.


Ameeleza hayo leo Ijumaa Februari 26, 2021 jijini Dodoma wakati akizindua ushirikiano wa programu ya mafunzo kati ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na chama cha skauti Tanzania.


Amesema maeneo mengi kunaporipotiwa majanga ya moto imekuwa ni ubovu wa miundombinu licha ya kuwa zipo sababu nyingine.


Amebainisha kuwa ili  kudhibiti tatizo hilo, Serikali imeamua kufanya ukarabati wa shule kongwe zote nchini, kwamba zilizoanishwa ni 89 lakini hadi sasa wamefikia 86.


"Kuna uzembe ndani yake, hujuma na mambo mengine lakini kikubwa ni uchakavu wa miundombinu unaotokana na ukongwe wa majengo yetu, lazima tubadilike na kutoka huko sasa maana si wakati wa kurudi nyuma," amesema Jafo.


Jafo ameziagiza shule binafsi kupitia mifuko ya majengo yao upya ili waweze kuchukua tahadhari kabla ya majanga kuwakuta kwani moto umekuwa ukisababisha madhara makubwa kwa shule za Serikali na binafsi.


Amewaagiza wakuu wa shule kutoa ushirikiano kwa mamlaka za uchunguzi ili waliosababisha majanga ya moto wachukuliwe hatua.

Kocha Simba Aigeukia Yanga, Ligi Kuu na Kombe la FA





KOCHA Mkuu wa Simba, Mfaransa Didier Gomes ameweka kando maandalizi ya mchezo unaofuatia wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al-Merrikh ya nchini Sudan na badala yake nguvu amezirudisha katika Ligi Kuu Bara na Kombe la FA.

 

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu awafunge mabingwa wa Afrika Al Ahly ya nchini Misri bao 1-0 mchezo uliopigwa Jumanne kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.



Simba hivi sasa ipo katika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi wakiwa na pointi 42 wakiongozwa na Yanga wenye 49 ambao wamepanga kubeba mataji yote wanayoshindania ligi na FA kwenye msimu huu.

 

Kwa maana hiyo ni wazi sasa Gomes akili yake kwa kipindi hiki anawaza ushindi katika ligi za ndani ikiwemo Ligi Kuu ili kuifukuzia Yanga ambao ndio wanapambana nao katika mbio za ubingwa msimu huu.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Gomes alisema kuwa wamepanga kuanza maandalizi ya mchezo dhidi ya Merrikh wiki mbili zijazo na hivi sasa nguvu na akili zake amezielekeza katika ligi kuu na FA.



Gomes alisema ndani ya wakati mmoja anataka kuona anaipa mataji timu hiyo na kubwa ligi, hivyo hivi sasa yupo katika maandalizi ya kukiimarisha kikosi chake kuhakikisha wanaondoa Yanga kileleni kwa kushinda michezo yote iliyokuwepo mbele yao.

 

Aliongeza kuwa anaamini atafanikiwa katika hilo kutokana na ubora wa kikosi chake ambao wameuonyesha katika mchezo wa kimataifa waliocheza dhidi ya Al Ahly uliomalizika kwa Simba kushinda bao 1-0.



"Tumeshinda mechi mbili na tunaongoza Kundi A, ni matokeo muhimu sana kwetu.

Tunaanza maandalizi ya mchezo unaofuata wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Al-Merrikh wiki mbili zijazo."Mchezo wetu wa Merreikh hautakuwa mwepesi hii ni timu ninayoifahamu vizuri kutokana na kuwahi kuifundisha, hivyo sina hofu nayo na zaidi hivi sasa nguvu na akili nazihamishia katika ligi na FA.

 

"Hatutakuwa na utani katika michezo inayofuatia ya ligi na kikubwa tunataka kukaa kileleni kwenye msimamo wa ligi na mwisho wa siku tuwe mabingwa, hilo sina hofu nalo kutokana na ubora wa vijana wangu," alisema Gomes.


DC MBONEKO AMUAGIZA MENEJA TANESCO KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO YA UKATAJI UMEME SHINYANGA



Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (juu pichani)

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Shinyanga kuwaomba Radhi wananchi kutokana na kukata umeme mara kwa mara bila kutoa taarifa ili wafahamu kinachoendelea.

Mkuu huyo wa wilaya ametoa agizo hilo leo Ijumaa Februari 26,2021 baada ya kukerwa kitendo cha TANESCO kukata umeme bila kutoa taarifa kwa wananchi kwani inaathiri biashara na shughuli za kijamii.

"Namuagiza Meneja wa TANESCO mkoa wa Shinyanga Mhandisi Narrowil Sabaya awaombe radhi wananchi kwa kutotoa taarifa kuhusu kukatika kwa umeme na aeleze kwanini umeme unakuwa hivi, kwanini umeme unakatika mara kwa mara Shinyanga",amesema Mboneko.

Mboneko ameyataja maeneo yanayolalamikiwa zaidi kwa kukatiwa umeme katika Manispaa ya Shinyanga kuwa ni Kitangiri, Ndala, Ibinzamata, Mwawaza na Masekelo pamoja na maeneo mengine Mjini Shinyanga ambapo umeme umekuwa ukikatwa.

Aidha amemtaka Meneja huyo wa TANESCO kusimamia kikamilifu Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja ya TANESCO  iwe inatoa taarifa kwa wananchi kuhusu kukatika kwa umeme kupitia vyombo vya habari zikiwemo Redio za Kijamii na Mitandao ya kijamii ili wananchi wafahamu nini kinaendelea badala ya kukaa tu kimya.

"Meneja wa TANESCO akae na maafisa habari wa TANESCO wawe wanatoa taarifa kuhusu kukatika kwa umeme kwenye vyombo vya habari zikiwemo Redio za Kijamii kama vile Radio Faraja,mitandao ya kijamii yakiwemo magroup ya Whatsapp ama watume Ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) kwa wananchi ili wajue kinachoendelea kama inavyofanya Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA)",amesema Mboneko.

"Tofauti na changamoto ya Gridi ya Taifa ambapo umeme hukatika nchi nzima, hapa Shinyanga tupewe taarifa za kukatika kwa umeme. Haiwezekani maeneo mengine yawe na umeme halafu Shinyanga umeme unakatika na hakuna taarifa yoyote inatolewa",ameeleza Mboneko.

Katika hatua nyingine, Mboneko ameiagiza TANESCO mkoa wa Shinyanga kuboresha Kitengo cha Huduma za Dharura (Emergency) kwani kuna malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa wanapopigiwa simu kuhusu matatizo ya umeme hawafiki kwa wakati na inafikia wakati wanaenda baada ya hata siku tatu hadi wiki moja.

Pia amewataka kuondoa nguzo zilizokuwa zinatumika kupitishia umeme kuziondoa kwenye baadhi ya maeneo baada ya kuweka nguzo mpya baada ya kufanya maboresho na kuhakikisha maeneo yasiyo na huduma ya umeme yanapelekewa umeme.

 "Kata za Mwamalili na Masengwa ziingizwe kwenye miradi ya REA lakini maeneo mengine ambayo hayana umeme katika Manispaa ya Shinyanga TANESCO wafanye survey na makisio wapeleke Wizarani, sisi tufuatilie kuomba hizo fedha",amesema Mboneko.

Hali kadhalika ameitaka TANESCO ifuatilie na kuwajua wananchi waliolipia huduma ya umeme na hawajafungiwa umeme mpaka leo kama vile Kolandoto na viwanja vya Mwadui kata ya Ngokolo na kuhakikisha wanatoa Control Number kwa wakati.

Nao wananchi wamesema wanakerwa na kitendo cha kukatwa umeme mara kwa mara hususani inapofika saa moja usiku umeme unakatwa kusababisha vifaa vya umeme kuungua lakini pia kulipotezea taifa mapato hivyo kuiomba TANESCO kuwa inatoa taarifa kwa wananchi na kuacha kukata umeme.

"Ni matengenezo gani wanafanya kila siku wanakata umeme?.. wakati mwingine wakata umeme kisha wanarudisha ndani ya sekunde 30. Kama ni mgao wa umeme ni mgao gani huu, huu mtindo wa kukata umeme kwa sekunde nao unaitwaje",wamehoji wananchi.

Tayari Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Shinyanga limewaomba radhi wateja wake wilayani Shinyanga kwa kukosa huduma ya umeme kwa nyakati tofauti tofauti.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Februari 26, 2021 jioni na Ofisi ya Uhusiano na huduma kwa wateja mkoa wa Shinyanga imeeleza sababu ya makatizo haya ni hitilafu ambayo imekuwa ikijitokeza kwenye mfumo wa umeme na kusababisha baadhi ya njia za kusambazia umeme mkoani Shinyanga kukata umeme Kama kinga ya mfumo wa kusafirishia umeme. 

Taarifa hiyo imebainisha kuwa maeneo yanayoathirika ni njia zote za kusambazia umeme zinazotoka kwenye vituo vyetu vya kusambazia umeme vya Ibadakuli na Matanda.

"Aidha katizo hili ni kinga ya mfumo wa usafirishaji wa umeme na Wala siyo mgao au katizo  lilopangwa kama wateja wengi wanavyosema. 

Shirika linaendelea kuomba radhi wateja wake kwa kipindi hiki ambapo juhudi mbalimbali zinaendelea kufanywa na  Shirika ili kutatua hitilafu hii katika mfumo wake wa umeme",imesema taarifa hiyo. 

Hospitali ya KCMC yafuta sherehe za jubilee ya miaka 50

 


Hospitali ya Rufaa ya KCMC inayomilikiwa na Shirika la Msamaria Mwema (GSF) imefuta sherehe za maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwake zilizokuwa zifanyike Machi mosi hadi  6, 2021.


Sherehe hizo zilikuwa ziambatane na utoaji wa huduma 15 bure kwa wahitaji 5,000 kutoka maeneo mbalimbali Tanzania ikiwa ni pamoja na upimaji wa magonjwa na ushauri bure kwa watakaobainika kuwa na matatizo.


Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Februari 26, 2021 na ofisa uhusiano wa KCMC, Gabriel Chisseo inasema huduma hizo 15 za matibabu zilizokuwa zitolewe bure nazo zimefutwa kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa KCMC.


"Huduma za matibabu bure na huduma za maonyesho zilizokuwa zimepangwa kutolewa na idara mbalimbali na mashirika alikwa hazitaweza kufanyika kama ilivyokuwa imepangwa kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu," inasema.


Ofisa huyo amesema huduma za kawaida za kitabibu pamoja na kliniki zitaendelea kutolewa kama ilivyo utaratibu wa hospitali na Chisseo kupitia taarifa hiyo amesema uongozi unaomba radhi umma kwa usumbufu utakaojitokeza.


Huduma ambazo KCMC ilikuwa imepanga kuzitoa bure kama sehemu ya maadhimisho hayo ni upimaji mkojo kwa utambuzi wa shida ya figo na pia wangepima maambukizi ya virusi ya Ukimwi na saratani ya shingo ya kizazi.


"KCMC ilikuwa imepanga kupima bure saratani ya matiti na kutoa elimu ya afya ya mama na mtoto na kutoa elimu pia ya magonjwa ya upasuaji, tezi dume, elimu ya magonjwa ya njia ya mkojo, chakula na lishe na elimu ya uzazi," inaeleza taarifa hiyo.


Hospitali hiyo ilikuwa itumie maadhimisho hayo pia kufanya harambee ya uchangiaji wa taasisi ya moyo kanda ya Kaskazini inayojengwa KCMC kwa gharama ya Sh16 bilioni ambayo ni muhimu kwa kanda ya Kaskazini.


KCMC anayotegemewa na watu zaidi ya milioni 15 wa mikoa ya Kaskazini ilianzishwa mwaka 1971 ikiwa na vitanda 300 tu vya kulaza wagonjwa, lakini sasa ina vitanda 686 ikipokea wagonjwa wa nje 1,000 kila siku.

DC MBONEKO AMWAGIZA MENEJA TANESCO KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO YA UKATAJI UMEME SHINYANGA



Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko (juu pichani)

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Shinyanga kuwaomba Radhi wananchi kutokana na kukata umeme mara kwa mara bila kutoa taarifa ili wafahamu kinachoendelea.

Mkuu huyo wa wilaya ametoa agizo hilo leo Ijumaa Februari 26,2021 baada ya kukerwa kitendo cha TANESCO kukata umeme bila kutoa taarifa kwa wananchi kwani inaathiri biashara na shughuli za kijamii.

"Namuagiza Meneja wa TANESCO mkoa wa Shinyanga awaombe radhi wananchi kwa kutotoa taarifa kuhusu kukatika kwa umeme na aeleze kwanini umeme unakuwa hivi, kwanini umeme unakatika mara kwa mara Shinyanga",amesema Mboneko.

Mboneko ameyataja maeneo yanayolalamikiwa zaidi kwa kukatiwa umeme katika Manispaa ya Shinyanga kuwa ni Kitangiri, Ndala, Ibinzamata, Mwawaza na Masekelo pamoja na maeneo mengine Mjini Shinyanga ambapo umeme umekuwa ukikatwa.

Aidha amemtaka Meneja huyo wa TANESCO kusimamia kikamilifu Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja ya TANESCO  iwe inatoa taarifa kwa wananchi kuhusu kukatika kwa umeme kupitia vyombo vya habari zikiwemo Redio za Kijamii na Mitandao ya kijamii ili wananchi wafahamu nini kinaendelea badala ya kukaa tu kimya.

"Meneja wa TANESCO akae na maafisa habari wa TANESCO wawe wanatoa taarifa kuhusu kukatika kwa umeme kwenye vyombo vya habari zikiwemo Redio za Kijamii kama vile Radio Faraja,mitandao ya kijamii yakiwemo magroup ya Whatsapp ama watume Ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) kwa wananchi ili wajue kinachoendelea kama inavyofanya Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mjini Shinyanga (SHUWASA)",amesema Mboneko.

"Tofauti na changamoto ya Gridi ya Taifa ambapo umeme hukatika nchi nzima, hapa Shinyanga tupewe taarifa za kukatika kwa umeme. Haiwezekani maeneo mengine yawe na umeme halafu Shinyanga umeme unakatika na hakuna taarifa yoyote inatolewa",ameeleza Mboneko.

Katika hatua nyingine, Mboneko ameiagiza TANESCO mkoa wa Shinyanga kuboresha Kitengo cha Huduma za Dharura (Emergency) kwani kuna malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa wanapopigiwa simu kuhusu matatizo ya umeme hawafiki kwa wakati na inafikia wakati wanaenda baada ya hata siku tatu hadi wiki moja.

Pia amewataka kuondoa nguzo zilizokuwa zinatumika kupitishia umeme kuziondoa kwenye baadhi ya maeneo baada ya kuweka nguzo mpya baada ya kufanya maboresho na kuhakikisha maeneo yasiyo na huduma ya umeme yanapelekewa umeme.

 "Kata za Mwamalili na Masengwa ziingizwe kwenye miradi ya REA lakini maeneo mengine ambayo hayana umeme katika Manispaa ya Shinyanga TANESCO wafanye survey na makisio wapeleke Wizarani, sisi tufuatilie kuomba hizo fedha",amesema Mboneko.

Hali kadhalika ametaka TANESCO ifuatilie na kuwajua wananchi waliolipia huduma ya umeme na hawajafungiwa umeme mpaka leo kama vile Kolandoto na viwanja vya Mwadui kata ya Ngokolo na kuhakikisha wanatoa Control Number kwa wakati.

Nao wananchi wamesema wanakerwa na kitendo cha kukatwa umeme mara kwa mara hususani inapofika saa moja usiku umeme unakatwa kusababisha vifaa vya umeme kuungua,hivyo kuiomba TANESCO kuwa inatoa taarifa kwa wananchi.

"Ni matengenezo gani wanafanya kila siku wanakata umeme?.. wakati mwingine wakata umeme kisha wanarudisha ndani ya sekunde 30. Kama ni mgao wa umeme ni mgao gani huu, huu mtindo wa kukata umeme kwa sekunde nao unaitwaje",wamehoji wananchi.


Hata hivyo Mwandishi wa habari hizi alipomtafuta Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Narrowil Sabaya kuzungumzia malalamiko ya wananchi kuhusu ukataji umeme na chanzo cha umeme kukatika mara kwa mara amesema atatoa taarifa.





Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...