Thursday, October 31, 2019

Jiji La Dodoma Latozwa Faini Kutokana Na Uchafu Wa Machinjio

Na Lulu Mussa
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) hii leo imefunga machinjio ndogo ya Msalato kwa muda usiojulikana na kupiga faini kwa kosa la kukithiri kwa uchafu wa mazingira na miundombinu chakavu.
 
Hatua hiyo imefikiwa mara baada ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira kufanya ziara ya kushtukiza katika eneo hilo na kujionea Mazingira yasiyoridhisha kwa usalama wa afya za binadamu. 
 
Katika ziara hiyo, wabunge wamejionea mazingira yasiyoridhisha na kuhatarisha afya za watumiaji wa nyama inayochinjwa machinjioni hapo ikiwa ni pamoja na kurundikana kwa samadi, kukithiri kwa harufu kali na kukosekana kwa maji safi.
 
Bw. Gratius Mwesiga, Afisa Mifugo wa Jiji la Dodoma ameieleza Kamati hiyo kuwa ukarabati katika eneo hilo umeanza na unaendelea kwa awamu, ikiwa ni pamoja na ukarabati wa mifumo ya maji taka.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Mussa Sima amesema lazima hatua kali za kisheria zichukuliwe kwa manufaa ya afya za walaji. "Sisi watu wa Mazingira afya za binadamu ni kipaumbele namba moja, hali hii haikubaliki" Sima alisisitiza. 
 
Waziri Sima amemuagiza Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Nchini (NEMC) Dkt. Samwel Gwamaka kufanya tathmini ya haraka na kina na kuhakikisha kuwa machinjio yanazingatia taratibu zilizopo katika Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004.
 
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bunge Viwanda, Biashara na Mazingira Kanali Mstaafu Masoud Ali amesema hali ya usafi katika machinjio hiyo haidhirishi na kuwataka NEMC kuchukua hatua. "NEMC msingechukua hatua, sisi Kamati tungechukua, haiwezekani hali hii haikubaliki" Alisisitiza Mhe. Masoud Ali.
 
Wakati huo huo, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC amelitoza faini Jiji la Dodoma ya kiasi cha Shilingi Milioni tano (5) kwa mujibu wa kifungu namba 194 cha sheria ya usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004 na kutakiwa kuilipa ndani ya wiki mbili.


Treni Yawaka Moto, 62 Wafariki Dunia...Kisa Mtungi wa Gesi Kulipuka


WATU 16 wamefariki baada ya treni ya mwendokasi kuwaka moto na wengine 13 wamejeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea mapema leo huko Liaqatpur karibu na mji wa Rahim Yar Khan.



Waziri wa Masuala ya Usafirishaji wa reli, Sheikh Rashid Ahmad amesema moto umesababishwa na jiko la gesi lililopuka wakati abiria wakipika chai, jambo ambalo ni kinyume na sheria.





Treni hiyo ilikuwa inatokea Lahore kwenda Karachi. Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya karibu huku shughuli za uokoaji zikiendelea.

Viongozi Ubungo Wananenepeana' - Paul Makonda



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, amewaonea huruma wakazi wa Ubungo kwa kile alichokieleza kuwa hawakuchagua viongozi sahihi, ambao wangeweza kutatua kero zao hii ni baada ya kufika katika eneo maalumu lililotengwa kwaajili ya ujenzi wa Hospitali ya wilaya, bila kuwaona wabunge,


Hayo ameyabainisha leo Oktoba 29, 2019, alipotembelea eneo ambalo litajengwa hospitali hiyo inayotarajiwa kukamilika ndani ya miezi mitatu, ujenzi utakaosimamiwa na Jeshi la kujenga Taifa (JKT), utakaogharimu kiasi cha Shilingi bilioni 1.5.

''Kama nilivyosema juzi, Ubungo hatujapata viongozi kwa ajili ya maendeleo ya wananchi, tumepata kwa ajili ya matumbo yao na ndio maana nimefika hapa nikawa nawatafuta, Meya, Mbunge wa Kibamba na Ubungo yuko wapi, hayupo,sasa niwasihi wakati mwingine msiwaonee haya walafi na wanaonenepa kupitia pesa zenu, wakati wao wameshindwa hata kupaza sauti ili ninyi muweze kupata huduma bora, nafahamu kuna baadhi ya maeneo Ubungo yana changamoto ya barabara, lakini wabunge wenu wala Meya wenu hawana chochote cha kuongea lakini utawakuta wamehamia twitter'' amesema Makonda.

Kufuatia hali hiyo Makonda amewaomba wakazi wa Ubungo, katika kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa, wahakikishe wanachagua viongozi wanaojitambua na watakaoweza kuwasilisha vyema kero zao ngazi za juu.

Oktoba 26, 2019, wakati wa upokeaji wa ndege mpya Dreamline ya pili, Makonda aliwasilisha ombi la kutengewa fedha hizo, ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, aliridhia ombi hilo na kuagiza zitengwe shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo.

Source

Wednesday, October 30, 2019

PICHA YA RAIS MAGUFULI YAMPONZA IDRIS SULTAN ....MAKONDA AMTAKA AJISALIMISHE POLISI...KIGWANGALLA KUWEKA DHAMANA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, amemtaka mchekeshaji na muigizaji hapa nchini, Idris Sultan, kuripoti katika kituo chochote cha polisi, hii ni baada ya msanii huyo ku 'post' picha katika ukurasa wake wa Instagram, akiwa amehariri picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na kuweka sura yake.

Makonda ametoa agizo hilo leo Oktoba 30, 2019, kupitia ukurasa wake wa Instagramu.

"Naona mipaka ya kazi yako huijui, nenda sasa hivi kituo chochote cha Polisi, uwaambie Makonda kaniambia nije utakuta ujumbe wako" ameandika Makonda.

Idris aliweka picha hizo ikiwa ni siku moja tu imepita tangu Rais Magufuli, atimize umri wa miaka 60, ambapo msanii huyo aliandika kuwa.

 "Kwa siku moja tukabadilishana kazi ili a-enjoy birthday yake kwa amani".

Makonda amesema, "nimesema kweli aende polisi sina utani na watu wa aina hiyo."

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla amesema atamuwekea dhamana mchekeshaji Idris Sultan ikiwa ataripoti polisi na kukamatwa baada ya kutakiwa kufanya hivyo na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

 Dk Kigwangalla aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, "nimeambiwa kuna msanii wa vichekesho anatafutwa na polisi."

"Mniambie nitajitolea mwanasheria wa kwenda kumuwekea dhamana na kumtetea. Rais wetu ni mtu wa watu na imejidhihirisha kwa jinsi wananchi walivyojitolea kumuombea dua siku ya kuzaliwa kwake. Wameonesha upendo."

Monday, October 28, 2019

MZEE SOMBI : VIJANA WANAOGOPA KUOA KWA SABABU HAWANA KAZI....HAWATAKI USUMBUFU



Mzee James Makungu Sombi (85) akizungumza na Malunde1 blog leo Jumatatu Oktoba 28,2019 

Wimbi la vijana kutooa ama kuolewa limekuwa likiongezeka kila kukicha kutokana na vijana kutofanya kazi za kuwaingizia kipato hivyo kuona jambo la kuwa na familia ni mzigo na usumbufu katika maisha yao.

Hayo yamesemwa na Mzee maarufu wa Kabila la Kisukuma James Makungu Sombi (85) mkazi wa Kisesa mkoani Mwanza wakati akizungumza na Malunde1 blog ambapo amesema kutokana na vijana kuwa wazembe,kutaka kula tu na kuzurura ndiyo maana suala la kuoa au kuolewa linakuwa gumu. 

"Msichana hana kazi,mvulana hana kazi unadhani wakianza kuishi pamoja nyumba itakalika?.Kijana hana kazi atamlisha nini mke wake?,pesa za kumvalisha zitatoka wapi?,ndiyo maana vijana hawaoi ili kukwepa majukumu ya familia kwani akioa atakosa raha akiwaza atapata wapi pesa za kutunza familia",amesema Mzee Sombi. 

"Zamani kilimo ndiyo ilikuwa ngao nzuri ya kumuweka mtu katika maisha mazuri,lakini siku hizi vijana hawataki kulima,hata kufanya kazi nzito nzito hawataki,ukimwambia kijana akalime unakuwa kama umemfukuza, wanakimbilia mjini,wao wanataka kula na kuzurura tu,sasa mtu wa namna hiyo ataoa kweli?",alihoji Mzee Sombi. 

"Zamani huku kwetu tulikuwa na Shikome,hii ilikuwa kama ofisi ya mambo mbalimbali,wazazi walitumia shikome kuongea na vijana wao,lakini siku hizi hakuna shikome,wazazi hawana muda wa kuzungumza na watoto wao na watoto nao hawataki kushauriwa na wazazi, matokeo yake tunakuwa na vijana wa hovyo kweli kweli",amesema. 

Anasema tofauti na sasa zamani wazazi walikuwa wanawatafutia vijana wachumba wa kuoa kisha kijana anaenda kuhakikisha kama mchumba anafaa ndipo anaoa lakini siku hizi vijana wanajiamulia wao wenyewe ndiyo maana hata ndoa hazidumu. 

"Kijana kajiamulia mwenyewe kuoa,msichana kakubali kuolewa,msichana yupo ndani ya ndoa akiona kijana huyo hana kazi anafikiri ataishije,mwisho wa siku kwa kuwa naye hana kazi anaamua kuondoka kwenda kutafuta pesa mahali pengine, na kama walibahatika kuzaa basi mtoto anajikuta analelewa na mzazi mmoja na mara nyingi mtoto atakuwa hana maadili na huo ndiyo mwendelezo wa kuwa na vijana wasio na maadili",ameelza 

Mzee Sombi anasema zamani wanandoa walikuwa wanavumiliana kwa sababu hawakuwa na tamaa ya kupata pesa wao nia yao ilikuwa ni kupata familia na kuzaa na kulea watoto wao. 

"Wasichana wetu siku hizi wakiona wamepata mtoto wanawaza kwamba huyu mtoto atamlisha nini ndiyo maana wengine wanaamua kuwatupa ili wapate nafasi ya kwenda kutafuta pesa kwa wanaume wengine,nawashauri wanawake wawe wanajishughulisha ili wapate kipato badala ya kutegemea wanaume ambao mara nyingi wamekuwa wakiwakimbia na kujikuta tunakuwa na Single Mother wengi 'familia ya mama na mtoto'",alisema Mzee Sombi.

Mzee James Makungu Sombi ambaye ni mkazi wa Kisesa Mwanza Manju Mstaafu wa ngoma za Kisukuma na ni miongoni mwa waanzilishi wa Makumbusho ya Kisukuma ya Bujora yaliyopo Kisesa jijini Mwanza

Mzee Sombi ni Mtaalamu wa Masuala ya Utamaduni wa Kabila la Kisukuma,Wasiliana naye kwa namba 0755903972

KUFANYA SANA MAPENZI KUNAPUNGUZA SIKU ZA KUISHI....BABU WA MIAKA 85 ATOA USHAURI

Mkutano wa kuvutia uwekezaji SADC kutoka China wafunguliwa

Mkutano wa kuvutia uwekezaji katika nchi za SADC kutoka Jimbo la Jiangsu umefunguliwa leo jijini Nanjing na Naibu Gavana wa Jimbo hilo Ndugu Ma Qiulin.

Mkutano huo umehudhuriwa na Mabalozi 11 wa nchi za SADC na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa SADC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Miundombinu wa Sekretariat ua SADC, Mapolao Mokoena.

Katika hafla ya ufunguzi wa mkutano huo Balozi wa Tanzania Mbelwa Kairuki alitoa hotuba kwa niaba ya Jumuiya ya Mabalozi wa Nchi za SADC nchini China ambapo pamoja na mambo mengine aliyakaribisha makampuni ya SADC kuchangamkia fursa za uwekezaji katika nchi za SADC kutokana na fursa za soko kubwa lenye idadi ya watu milioni 345 na uchumi wa GDP 600 Billioni.
Source

RC MNYETI : WANANCHI DONGOBESH WAPOKEENI WAFANYAKAZI WA HALMASHAURI YA MBULU


Na Beatrice Mosses - Malunde 1 blog 
WANANCHI wa kata ya Dongobesh wilaya ya Mbulu mkoani Manyara wametakiwa kuwapokea na kuwakaribisha wafanyakazi wa halmashauri hiyo ambapo wanatarajia kuhamishia makao makuu ya halmashauri hiyo ndani ya wiki hii.

Kauli hiyo imetolewa juzi na mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti alipotembelea na kukagua jengo jipya la halmashauri ya wilaya ya Mbulu linalojengwa kwenye kata hiyo. 

Mnyeti alisema  ujio wa watumishi hao wa halmashauri kwenye kata ya Dongobesh utaleta mabadiliko ya haraka lakini pia mji utachangamka na maendeleo yataonekana kwa haraka zaidi. 

"Sasa nikuombe Mwenyekiti  uwahamasishe wananchi wa Dongobesh wawapokea watumishi kwa sababu tunaambiwa hapa kuna Ka Ukoo fulani ambako ndiko kana dominate kila kitu sasa kama mkifanya hivyo shauri yenu. 

"Lakini mkitaka maendeleo muwapokee watumishi, msiwafanye watumishi usiku wamelala wanaamka  wanajikuta wapo barabarani maana tunasikia kwamba hapa Dongobesh ni wataalamu sana wa sekta hiyo. 

"Niwaombe muwapokee watumishi na kuwafanya kama watoto wenu, sio tukileta hapa watumishi halafu mkawa mnawafanyia mambo ya namna hiyo tutawaondoa, tutajenga nyumba za halmashauri maeneo mengine watakuwa wanakuja kufanya kazi wanaondoka", Alieleza Mnyeti. 

Hata hivyo Mnyeti alishauri kwamba pindi watumishi wa halmashauri hiyo watakapohamia kwenye eneo hilo uitishwe mkutano wa wazee wa kimila wawapokee na kuwapa ulinzi wa kimila asidhurike mtu hata mmoja. 

Pamoja na hayo Mnyeti alipongeza kazi ya ujenzi unaoendelea kwenye jengo la halmashauri hiyo ambalo linajengwa na kampuni ya kijeshi ya Mzinga ambapo alidai kuwa fedha iliyotolewa inaendana na kazi inayofanyika. 

"Ingelikuwa tumetoa pesa halafu hakuna kinachofanyika tungesikitika sana, mwanzoni nilipita hapa nilimkuta mzee mmoja  tu na hapakuwa na mtu mwingine, nilisikitika sana   kwa sababu Mzinga tunaowaamini ni makampuni ya kijeshi ambayo tunaamini kwamba kazi zao zinakwenda kijeshi tulitoa mawazo yetu,  tulitoa ushauri na mmetekeleza tunawapongeza sana. 

"Sasa mlichonishawishi ni kitu kimoja tu kikubwa kwenda kuwatafutia pesa ili ije pesa nyingine muweze kuendelea na ujenzi huu na kwa spidi hii kwa kweli mmetufurahisha kwani hakuna kitu kibaya kama kuletewa pesa halafu miradi inakuwa haiendi",alisema.  

Kwa upande wake Mwenyekiti  wa halmashauri ya wilaya ya Mbulu Joseph Mandoo alipongeza kazi kubwa inayofanywa na Rais Magufuli kwa kusimamia fedha za watanzania kutokana na huko nyuma kutokuwa na historia nzuri. 

"Sisi wana Mbulu niseme ametupendelea sana kwa sababu ametupa miradi mikubwa ya maendeleo kwenye shule za sekondari na msingi lakini kubwa zaidi ni kutuletea fedha bilioni mbili na milioni Mia tano kwa ajili ya ujenzi wa jengo la halmashauri ya wilaya katika mji wa Dongobesh lakini pia ametuletea fedha zaidi ya bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa hospitali ya wilaya", alieleza Mandoo. 

KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA OFISI YA WAZIRI MKUU KWA MKAKATI WA AJIRA NA UWEZESHAJI VIKUNDI VYA VIJANA


Na; Mwandishi Wetu
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria imeipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu kwa mikakati iliyoweka katika kuwajengea uwezo vijana kujiajiri na uwezeshwaji kiuchumi kwa vijana kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana "Youth Development Fund" na Mikopo kupitia mapato ya ndani ya halmashauri.

Akizungumza wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya vijana katika Mkoa wa Morogoro, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Najma Giga ameipongeza Serikali kwa mikakati iliyokuja nayo katika kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana kwa kuwajengea mazingira wezeshi na yanayowahamasisha kuanzisha miradi mbalimbali ya kiuchumi.

"Matokeo ya utekelezaji wa mikakati hiyo tumeona kwa kiasi kikubwa imewawezesha vijana kutambua taratibu rasmi za kupata mikopo yenye riba nafuu na ambayo imewasaidia kuazisha miradi ya kiuchumi," alisema Mheshimiwa Giga.

Aliongeza kuwa Serikali iendelee kutenga bajeti zaidi ya uwezeshwaji wa vikundi vya vijana kwa kuwa vina tija na vinapunguza tatizo la ajira kwa vijana kwa kiasi kikubwa.

Sambamba na hayo Kamati hiyo iliitaka Ofisi ya Waziri Mkuu kuendelea kutoa maelekezo katika halmashauri zote kuelimisha vijana zaidi ili waweze kutambua taratibu za kupata mikopo kupitia mfuko wa maendeleo ya vijana na asilimia 10 ya mikopo ambayo utolewa kwa Vijana 4%, Wanawake 4% na Wenye Ulemavu 2% kupitia mapato ya ndani ya halmashauri.

Akitoa maelezo ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde ameihakikishia Kamati ya Bunge kwamba Serikali itaendelea kuviwezesha kiuchumi vikundi vya vijana katika mkakati wa kuhamasisha vijana kujiajiri lakini pia kuwajengea uwezo wa kiuchumi vijana ili nao pia washiriki kikamilifu katika mnyororo mzima wa uchumi wa viwanda ambapo matarajio ni kwamba ifikapo mwaka 2025 zaidi ya asilimia 40 ya nguvukazi iwe imeajiriwa kwenye sekta ya viwanda.

"Serikali iliazisha mfuko wa maendeleo ya vijana na programu mbalimbali ili kuwawezesha wananchi hususan vijana kuweza kupata mahitaji ya mitaji ya kuanzisha shughuli za kiuchumi zitakazo waingizia kipato," alisema Mavunde

Akitolea mfano mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vijana kutumia teknolojia ya kitalu nyumba ni mkakati mzuri ambao Serikali imekuja nao katika kutatua tatizo la ajira kwa vijana kupitia sekta ya kilimo.

Aidha, Naibu Waziri Mavunde aliwahamasisha vijana kuandaa maandiko ambayo yataelezea shughuli zenye tija wanazotaka kuzifanya katika kujileta maendeleo ili waweze kupata mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya vijana na Mikopo kupitia mapato ya ndani ya halmashauri itakayowasaidia kuendesha shughuli zao. 

Kwa nyakati tofauti vijana wa Mkoa wa Morogoro wameishukuru Serikali kwa uwezeshaji kupitia Mfuko wa maendeleo ya vijana na kuomba kuwezeshwa zaidi ili kukidhi matarajio yao ya uanzishwaji wa viwanda katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya Tano katika uchumi wa viwanda.


Sunday, October 27, 2019

Meseji nzuri za mapenzi zitakazomfanya mpenzi wako akupende zaidi

Hutakiwi kwenda kwa waganga wa kienyeji ili kumfanya mpenzi wako akupende bali unahitaji mbwembwe ndogo ndogo ambazo zitamfanya mwenza wako huyo akupende zaidi. Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na kumtumia meseji mwenza wako, mfano wa meseji hizo ni:

1. Moyo wangu umekupenda wewe peke yako, kamwe sifikirii kwenda kwa mwingine. I luv you honey…

2. Hata kama nitajidanganya kwamba sikupendi, moyo wangu umeganda kwako na hakuna dalili za kukuacha, wewe ni wangu peke yako dear…

3. Hata kama watasema mengi kiasi gani, kwako wewe nitaendelea kuwa mpole, maana nakupenda sana…

4. Siyo rahisi kuishi bila wewe, maana wewe maishani mwangu ni sawa na maji katika maisha ya binadamu. Mwaaaaa

5. Ni kweli nakiri ndani ya nafsi yangu kwamba nilikukosea mpenzi wangu, naomba unisamehe na unipe nafasi nyingine katika moyo wako mpenzi wangu. Nakupenda sana, pokea busu mwanana kutoka kwanngu….mwaaaaaaaa…

Ujue mchango wa marafiki katika kuyabadili maisha yako


Kuna aina mbili za marafiki ambao tunaishi nao katika maisha yetu ya kila siku.  Aina ya kwanza ni marafiki ambao ni wema na aina ya pili ni marafiki wabaya.

Tukianza na kuangalia aina hiyo ya kwanza, marafiki wema hao ni marafiki ambao ni watu ambao wana mawazo chanya katika kukushauri hata kutenda mambo mbalimbal yenye mchango mkubwa wa kuyabadili maisha yako kwa kiwango cha juu sana. Pia katika kundi hili la marafiki wapo marafiki wa aina hii wachache sana.

 Aina ya pili,marafiki wabaya hawa ni  marafiki ambao ni watu ambao hawana msaada wowote katika safari yako ya mafanikio zaidi ya kukukatisha tamaa tu.

Watu wengi tunafeli kimaisha hii ni kutokana na kufanya uchaguzi mbaya wa marafiki. Wengi wetu tunaambatana na marafiki wabaya hata sehemu ambazo hatustili kuishi na watu hao .

Vile vile wengi wetu tumekuwa tukiomba ushauri kwa watu ambao siyo sahihi hata kidogo. Kwa mfano leo hii tumeona marafiki wabaya huwa na mtazamo mmoja wa kushindwa kufikia malengo yao.

Tumekuwa tukushuhudia  baadhi ya wanafunzi ambao pindi waendapo  masomoni baada ya kufika huko wamekuwa na tabia za ajabu hii ni kutokana wamekutana na marafiki ambao sio sahihi.

Tumeona baadhi ya vijana hao wamekuwa wakijingingiza kwenye wimbi la ulevi,  utumiaji wa madawa ya kulevya na hata kuuza miili yao hii ni kutokana watu hao wameshindwa kuchagua marafiki sahihi.

Mpenzi msomaji wa makala haya naendelea tena juu ya somo hii la marafiki. Wapo baadhi ya watu wameshindwa kuwa sehemu fulani kwa sababu ya marafiki walio nao. Wapo baadhi ya watu wamekuwa wakipata baadhi ya mawazo mazuri na kuwashirikisha marafiki zao, na marafiki hao wamekuwa wanazidi kuwakatisha tamaa tu.

 Kwa mfano unaweza ukamshirikisha rafiki yako na kumwambia nataka kufanya biashara ya fulani. Baada ya kumwambia rafiki uliyenaye utamsikia akisema Biashara hiyo hatatoka kwa sabubu fulani anaifanya au fulani kaliteka soko la biahara hiyo, hivyo hatuweza ni bora utafute kitu kingine cha kufanya. Ukichunguza kwa umakini juu ya marafiki wabaya huwa hawana sababu ya msingi ya jambo ambalo anakwambia kwa nini usifanye.

Wapo baadhi ya marafiki ambo wao ukiwashirikisha jambo lako na wao huchukua jukumu la kuwashirikisha wengine. Marafiki wa aina hiyo hawafai hata kidogo.

Kimsingi ni kwamba watu wengi walio fanikiwa leo hii walichagua marafiki sahihi wa kuwashauri juu ya mambo yao. Hivyo na wewe chagua marafiki sahihi ambao unahisi wewe wanamsaada mkubwa katika maisha yako, pia ukumbuke wanasema ndege wafananao huruka pamoja hivyo ni wasaa wako mzuri wa kuchagua marafiki wema. Marafiki wabaya ambao hawana mchango na msaada wowote juu ya maisha yao wafute na wala usijali watesema nini.

Marafiki hao wabaya wakianza kukuliza kwanini siku hizi umebadilika jibu la kuwajibu ni rahisi ni kwamba utawaambia "always forward, backward never" ikiwa na maana ya daima mbele, nyuma mwiko. Marafiki sahihi wao ukiwaambia juu ya jambo lako zuri tegemea kupata majibu sahihi kwa kile ulichowashirikisha na sababu za msingi.

Swali dogo la kujiuliza marafiki ulio nao ni wema au wabaya? kama ni wabaya unachukua jukumu gani baada ya kukupa somo hili?  ni muda wako mzuri wa kufikiri juu ya jambo hili na kuchukua uamuzi sahihi.

Pia kumbuka usemi usemao ya kwamba kila gumu unalokutana nalo mbele yako limebeba siri ya mafanikio yako, usinung'unike kutokana na magumu unayokutana nayo katika mizunguko yako lakini ifundishe akili yako, usingalie nani kasema nini? nani kasema kipi juu yako. Jambo la msingi ni fanya kazi kwa bidii zote na simamia mipango yako . Siku moja utakuwa mtu wa thamani sana mbele ya jamii.

Na. Benson Chonya

Saturday, October 26, 2019

Rais Magufuli Na Mkewe Watoa Pole Kwa Familia Ya Mmoja Wa Waasisi Wa Vyama Vingi Nchini Marehemu Mzee James Mapalala

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mwanasiasa Mkongwe na mmoja wa Waasisi wa Mfumo wa Vyama vingi nchini Marehemu James Mapalala Osterbay jijini Dar es salaam aliyefariki dunia Oktoba 23,2019 katika Hospital ya Kairuki jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsalimia Bi. Hannah Mapalala Mke wa Marehemu James Mapalala alipokwenda na Mkewe Mama Janeth Magufuli kutoa pole nyumbani kwa Mwanasiasa Mkongwe na mmoja wa Waasisi wa Mfumo wa Vyama vingi nchini Osterbay jijini Dar es salaam aliyefariki dunia Oktoba 23,2019 katika Hospital ya Kairuki jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.


Thursday, October 24, 2019

Namna sahihi za kukabiliana na changamoto za kimafanikio katika maisha


Nafahamu ya kuwa kila mmoja wetu anahitaji mafanikio makubwa sana kwa kile anchokifanya siku zote, ila tatizo  kuna baadhi  changamoto mbalimbali zinasomsonga na kufanya eidha kefeli kabisa kwa jambo anolifanya au kufanikiwa kwa asilimia chache tofauti na alizokuwa anategemea mwanzoni mwa kuanza jambo.

Kuna wakati mwingine tunajikuta tunakata tamaa baada ya kuona baadhi ya changamoto zinatokea na kuzuia mafanikio ambayo tumejipangia. Changamoto hizi zinaweza zikajitokeza katika biashara, elimu, kazi kwa mfano kufukuzwa kazi ambayo ulikuwa unaitegemea, kufiwa na mtu ambaye ulikuwa unamtegemea na changamoto zinginezo.

Pia kuna wakati mwingine changamoto zikitokea tulio wengi  hukataa tamaa na muda mwingine na kujiona  hutafai kuendelea kuishi ,pia wakati mwingine huwa hata tunakufuru kwa kusema baadhi ya maneno kama vile Mungu kampendelea na mengineyo mengi.

Lakini ndugu msomaji wa makala hii tukumbuke ya siku zote changamoto ni njia ya kufikia mafanikio tunayoyahitaji. Pia changamoto hutokea ili kupima imani yako je wewe ni mtu wa aina gani katika kakabilana na changamoto?

Zifutato ni baadhi ya njia ya jinsi ya kukabilaiana na changamoto.

Kubali changamoto zinajitokeza.
Kama nilivyoeleza hapo awali ya kwamba changamoto ni lazima zitokee katika safari yako ya mafanikio, hivyo basi hakikisha ya kwamba unakua ni mtu kwa kuzikubali  changamoto hizo na ujue ni jinsi gani unaweza kupambana nazo ili uweze kutimiza malengo yako, mfano huenda ukawa unafanya biashara mahali fulani ila mwanzoni mwa biashara yako wateja walikuwa wengi ila kwa sasa wamepungua jaribu kufanya taathimini juu hili uone ni sababu zipi zilizochangia kutokea kwa hili na siyokuwa  ni mtu wa kukataa taamaa maana hakuna dhambi kubwa kama kukaata tama.

Tafuta washauri
Nafahamu ya kuwa baadhi yetu huwa tuna watu wa karibu ambao huwa tunaweelezea shida zetu ili kupata ushauri. Mfano wa  watu wa karibu wanaweza kuwa ndugu, marafiki na watu wengine. Pia unaweza kuwatumia viongozi wa dini kwa jambo linalolokukatiza kwani ni watu ambao ni washauri wazuri kwa  jambo linalokukatiza  na kukuzuia kukamilisha malengo yako.

Pia katika utautizi wa changamoto watu wengi huwa tunakosea sana. Huwa tunaangalia effect (madhara) ya jambo fulani kutokea badala ya kualia causes (sababu) ya jambo Fulani kutokea. Huenda ukawa hujanielewa ngoja nikupe mfano ufutao; katika baadhi ya maeneo hapa nchini kuna ugonjwa wa mlipuko ambao umetokea unaitwa kipundupindu lakini katika utatutizi juu ya ugonjwa huu watu huenda kuatibu madhara (effects) sawa ni jambo nzuri lakini ni vyema kuanza kuangalia ni nini chanzo (causes) cha ugonjwa huu kutokea ndipo tuje tuangalie madhara (effect).

Ukifuata kanunu hii ya kuangalia chanzo yaani (causes)  harafu uje kuangalia effect (madhara) itasaidia kupunguza changamoto zingine zinazokutatiza katika kufanikisha malengo yako.

Mwisho naomba nimalize kwa kusema "usizibe ufa kabla ya kujua chanzo cha ufa kutokea''

Na. Benson Chonya.

RC Sanare agiza Sokoine Memorial High School kupokea wanafunzi

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Loata Ole Sanare amewaagiza Afisa Elimu wa Mkoa huo na Viongozi wa Wilaya ya Mvomero na Halmashauri ya Wilaya hiyo kuhakikisha Sekondari ya Sokoine Memorial High School iliyopo Wilayani humo inapokea wanafunzi kwa ajili ya kuanza masomo mwaka huu bila kukosa.

Mkuu huyo wa Mkoa ametoa agizo hilo leo Oktoba 24 alipofanya ziara ya kuangalia utekelezaji wa Ujenzi wa mradi huo pamoja na majengo ya Mama na Mtoto yanayojengwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mvomero.

"miaka saba mradi unajengwa mmoja, sasa naomba tubadilishe staili, Mkurugenzi, lazima sasa hivi tuwachukue watoto sasa hawa wanaokuja, hakuna tena mjadala …….tuanze tufanye finishing (umaliziaji) wa majengo yale ya muhimu…tuanze sasa kuchukua watoto" amesisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.

Ole Sanare amesema sio busara kusubiri fedha kiasi cha shilingi Bilioni 12 zinazohitajika kukamilisha ujenzi wa majengo hayo ndipo tuanze kuwapokea wanafunzi hao kwa ajili ya kuanza masomo bali fedha zilizobaki zaidi ya shilingi milioni mia moja zitumike kumalizia majengo yaliyopo mwishoni kumalizika ili wanafunzi waanze masomo mwaka huu.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wananchi wa Wilaya ya Mvomero kumpa ushirikiano ili kufanya kazi ya kuwaletea maendeleo wananchi Wilayani humo huku akiwaahidi kurudi tena ili kukaa nao na kujadili changamoto ya Migogoro ya Ardhi baina ya wakulima na wafugaji inayoendelea kujitokeza ili kuipatia ufumbuzi wa kudumu.

Hata hivyo amewataka wananchi wa Halmashauri hiyo kuishi kama ndugu na kujikita kwenye masuala ya maendeleo ikiwemo suala la Elimu badala ya kuendekeza Migogoro isiyo na tija kwao.

Awali akitembelea majengo yanayojengwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mvomero yatakayotoa huduma ya mama na Mtoto, Mhe. Ole Sanare aliwapongeza Viongozi wa Halmashauri hiyo kwa kusimamia fedha za Serikali zaidi ya shilingi 500 Mil.

Amesema katika mradi huo sio tu unakamilika kwa wakati lakini pia kwa kiwango bora kinachoendana na fedha zilizotolewa na Serikali.

Naye Mkuu wa Wilaya hiyo Mwl. Mohamed Utali pamoja na kupokea maagizo ya Mkuu huyo wa Mkoa alieleza sababu inayopelekea kiasi cha shilingi milioni mia moja kinachotakiwa kutumika katika kujenga njia ya kupita wagonjwa kutoka jengo moja hadi jingine (Walk way).

Akitoa taarifa ya ujenzi wa Sekondanri ya Sokoine Memorial High School, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mvomero Florent Kyombo amemueleza Mkuu wa Mkoa kuwa mradi huo awali ulitengewa fedha Bil. 12 lakini baada ya uamuzi wa Serikali wa Kutumia Force akaunti, mradi huo sasa utakamilisha ujenzi wake kwa shilingi Bil. 7 pekee.

Waziri Lukuvi Aagiza Wananchi Wote Waliodhurumiwa Kulipwa Fidia.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ameziagiza Halmashauri za Miji pamoja na watu wenye mashamba makubwa wahakikishe wanawalipa fidia Wananchi wote ambao hawajalipwa kwa muda mrefu tangu kufanyika kwa tathmini kwani wananchi wengi wamekuwa wakiishi ndani ya mashamba yao kwa muda mrefu na wakiamishwa hawalipwi fidia zao kwa miaka mingi na wengine kuondolewa bila kulipwa kabisa.

Waziri Lukuvi meyasema hayo alipofanya ziara Wilayani Handeni Mkoani Tanga wakati wa kusikiliza kero za wananchi katika uwanja wa Soko la zamani Chanika maarufu Nyerere Squre Katika mkutano huo Waziri wa Ardhi aliongozana na Mkuu wa Wilaya hiyo Godwin Gondwe akiwa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Handeni Mhe. Omari Abdallah Kigoda na watendaji mbalimbali wa Halmashauri ya wilaya hiyo.

Kupitia kampeni yake ya "FUNGUKA KWA WAZIRI"   Mhe. Lukuvi amesikiliza kero za ardhi za wananchi zaidi ya 200 wa wilaya ya Handeni zilizowasilishwa kwake. Kampeni hiyo iliyoanza saa 4 asubuhi hadi saa 12 jioni ambapo wakazi wengi wa mji huo wamelalamikia suala la kulipwa fidia ndogo au kutokulipwa fidia zao kabisa.

Mh. Lukuvi amesema Halmashauri nyingi zimekuwa na pupa za kupanga viwanja bila kuwalipa wananchi fidia na hata ikitokea wakalipa fidia basi fidia itakuwa ndogo sana kwani kwa kufanya hivyo kutazidisha migogoro mingi ya ardhi isiyo ya lazima, hivyo amezitaka halmashauri kupitia upya madai ya wananchi na kuwalipa stahiki zao.

"Kwa kuwa hapa sasa mashamba mengi ya mji huu yamegeuka kuwa ni miji, lazima hawa watu muwafidie viwanja zaidi kuliko pesa kama wanataka pesa basi wauze wenyewe hivyo viwanja, hamuwezi kuwapa shilingi milioni tatu wakati nyinyi mnauza viwanja milioni kumi. Kumekuwepo na unyang'anyi na kuwalazimisha watu kupima viwanja kwa fidia kidogo. Na kwa mujibu wa sheria ya fidia kama hujamlipa mwananchi kwa miaka zaidi ya miwili basi inatakiwa ufanye tathmini upya".   

Hata hivyo Mh.Lukuvi ameshangazwa na wingi wa migogoro ya Ardhi ambayo ilikwisha patiwa ufumbuzi wake na mingine ilikwisha tolewa hukumu na Mahakama lakini cha kushangaza bado wananchi wanacheleweshewa haki zao hivyo kuwaamuru Maafisa ardhi kuhakikisha wanashughulikia swala hilo haraka iwezekanavyo kwani asingependa kuona swala hilo likijirudia tena.

Mhe. Lukuvi amesema kuwa amebaini 90% ya Wananchi wa Handeni hawana uwelewa juu ya hatimiliki ya ardhi zao wanazomiliki kwani ameshangazwa sana kuona wengi wao hawafahamu mipaka ya maeneo yao hali inayopelekea kuzuka kwa migogoro ya mipaka hivyo amewaasa wananchi kuyafatilia maeneo yao na kuyapatia hati miliki ili kuyalinda na wavamizi kwani Hati ndio kielelezo namba moja kinachotambulika kisheria.

"Mimi kama Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ipo migogoro ambayo nina uwezo wa kuitafutia ufumbuzi kutokana na mamlaka niliyonayo na ndio maana nimeamua kuwa na kampeni ya Funguka kwa Waziri ili kusikiliza kero mbalimbali za Ardhi lakini hii migogoro ya mtu na mtu inatakiwa kutafutiwa ufumbuzi ndani ya ofisi zenu za ardhi au wilaya" Amesema Waziri Lukuvi.

Hata hivyo baada ya kusikiliza kero za wananchi Waziri Lukuvi ameahidi kuanzisha Baraza jipya la Ardhi na Nyumba la Wilayani Handeni kwani wananchi wamekuwa wakisafiri hadi Wilayani Korogwe kusikiliza mashauri yao jambo ambalo limekuwa na ucheleweshaji wa kusikiliza na kutatua kero za ardhi kwa wakati kwani ndio chanzo cha migogoro mingi Wilayani hapo.

Aidha, akifunguka mbele ya Waziri Bi. Telessa Petro Gumbo ambae ni mkazi wa Handeni amelalamikia uvamizi wa uliofanywa katika shamba lake ambapo amemuomba Waziri Lukuvi kuingilia kati swala lake la kutolulipwa fidia baada ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kulimega eneo lake na kupitisha barabara hali inayomlazimu kulipwa fidia ya eneo hilo.

Naye, Bi. Amina Ali Kiale ambae pia ni mkazi wa Handeni amemlalamikia Waziri lukuvi kwa baadhi ya watendaji wa Ardhi ambao sio waaminifu kushiriki katika vitendo vya kudhurumu ardhi kwa kuwacheleweshea hati zao kwa muda mrefu wanapokuwa wanazifatilia.

Katika kutoa shukurani kwa Mhe. Waziri, Mkuu wa Wilaya ya Handeni Godwin Gondwe amemshukuru Mh. Lukuvi kwa kitendo cha kuifanya programu hiyo ya FUNGUKA KWA WAZIRI katika Wilaya yake ya Handeni kwani imeweza kutatua migogoro ya ardhi iliyodumu muda mrefu na kuahidi kushughurikia migogoro iliyobaki katika ofisi yake ya Wilaya.


Wednesday, October 23, 2019

VIDEO: Tazama goli la Meddie Kagere alilowafunga Azam FC (1-0)


Klabu ya soka ya Simba SC imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara. Bao hilo la ushindi la Simba limefungwa na Meddie Kagere.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI....USISAHAU KUSUBSCRIBE

Tuesday, October 22, 2019

Ogopa Sana Mida ya Saa TISA Usiku Mpaka Saa Kumi na Moja Alfajiri ni Hatari..Majini Wapo Kazini


Unambiwa kuanzia mida ya saa tisa usiku mpaka saa kumi na mbili alfajiri ,ni mida ya shetani,ghosts na wachawi ,na mambo mengi sana mabaya hutokea mida hiyo kama vifo ,pia ghosts ndomana kuanzia mida hiyo mbwa,paka,bundi na kuku ,huwa wana piga kelele sana kwasababu wana uwezo mkubwa wa kuona vitu visivyo onekana.

Unambiwa endapo kama sehemu unayo ishi(nyumbani kwako) ikifika usiku ,kuna kuwa na mazingira ya ajabu mfano

Baridi kali,upepo, harufu ambazo hazina chanzo,unasikia sauti zisizo elezeka,pia unaweza ukakuta mapazia yana pepea bila chanzo kama upepo

Jua basi kuna uwezekano mkubwa sana apo ni makazi ya ghosts/mizimu..au pia hiyo sehemu ulio jenga yalikuwa makaburi ya watu.

Pia unambiwa siku ambayo unajikuta unakuwa muoga sana haswa wakati wa usiku unapoenda kulala ,basi jua kwamba siku hiyo ni rahisi sana kutembelewa na ghosts/mizimu kwasababu unakuwa una wapa uhuru wakukutawala.

Serikali Yashtukia Kusuasua Kwa Uendeshaji Kiwanda Cha Tanga Fresh.

Na. Edward Kondela
Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeshtukia kusuasua kwa uendeshaji wa kiwanda cha Tanga Fresh hali iliyolazimu kuundwa tume kufanya uchunguzi wa namna kiwanda kinavyofanya kazi ikiwemo kuchunguza mtambo unaotumika kusindika maziwa ya muda mrefu ambao unadaiwa umekuwa ukiongeza gharama ya uendeshaji wa kiwanda hicho.

Akizungumza jana (21.10.2019) katika kiwanda cha Tanga Fresh mjini Tanga, kwenye kikao kilichohusisha menejimenti ya kiwanda pamoja na wanachama wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Wafugaji wa Ng'ombe wa Maziwa Mkoa wa Tanga (TDCU) kinachomiliki asilimia 43 ya kiwanda hicho.

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amefafanua kuwa serikali itahakikisha inachukua hatua kunusuru kiwanda kufuatia ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli alipotembelea kiwanda hicho mwaka 2017 na kuahidiwa na menejimenti kusindika maziwa lita laki moja kwa siku ambapo katika ziara hiyo Rais Magufuli aliwasaidia kupata hati iliyokuwa imekwama kwa miaka mingi, kuondoa changamoto ya wanahisa juu ya hisa zao Tume ya Ushindani (FCC) hali iliyopelekea kiwanda  kuanza kujitanua na kuongeza uzalishaji wa maziwa ya muda mrefu (UHT) ingawa kiwanda kiliamua kuchukua mkopo Benki ya Biashara (NMB), unaoonekana kuwalemea na kutofanya vizuri sawa na ahadi kwa Rais Magufuli.

"Kwanza serikali imebaini manunuzi ya mtambo wa kusindika maziwa ya muda mrefu kuwa ni mtambo uliyokwishatumika na umenunuliwa kwa zaidi ya Shilingi Bilioni Sita, pia riba ya mkopo kuwa ni kubwa na kuwa mzigo, hivyo nimeagiza iundwe tume ambayo tayari Mkuu wa Mkoa wa Tanga ameiunda kuanzia leo kufanya uchunguzi wa mtambo ulionunuliwa ikiwemo fedha ya kununulia mtambo huo na utaratibu uliotumika kununulia mtambo." Amesema Mhe. Ulega

Aidha Mhe. Ulega ameitaka bodi ya wakurugenzi wa kiwanda pamoja na wamiliki wakae pamoja na Benki ya Kilimo (TADB) kuitaka benki hiyo kununua deni hilo ili kutoa nafuu kwa kiwanda na kuondoa mzigo kwa wafugaji na kuinua kipato chao.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw. Martine Shigella amesema tayari timu ya wataalamu wakiwemo kutoka Taasisi ya Utafiti wa Viwanda na Maendeleo (TIRDO) imeshaundwa ili kubaini hali ya mtambo wa kusindika maziwa. 

Bw. Shigella amefafanua kuwa serikali itachukua hatua kwa yeyote atakayebainika kukihujumu Kiwanda cha Tanga Fresh ikiwemo kununua mtambo wa kusindika maziwa usio na tija kwa kiwanda hicho.

Nao baadhi ya wanachama wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Wafugaji wa Ng'ombe wa Maziwa Mkoa wa Tanga (TDCU) wamepongeza hatua zilizochukuliwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi pamoja na uongozi wa Mkoa wa Tanga kutafuta suluhu ya namna ya kuboresha Kiwanda cha Tanga Fresh ili kiweze kuongeza uzalishaji na kuwanufaisha wafugaji ambao wamekuwa wakiuza maziwa katika kiwanda hicho pamoja na kutaka kiwanda hicho kiongeze bei ya kununua maziwa kutoka kwa wafugaji hao ambao hawaridhiki na bei ya Shilingi 700 kwa lita moja.

Kikao baina ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi chini ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, uongozi wa mkoa wa Tanga, menejimenti ya kiwanda cha Tanga Fresh, bodi na wamiliki wa kiwanda kinatarajiwa kuendelea hii leo (22.10.2019) ili kutafuta suluhu ya kunusuru kiwanda hicho baada ya kupata hasara kwa miaka mitatu mfululizo.

Mwisho.


Makubwa...Amuua Mwenzake Kwa KISU Wakigombea Kumbikumbi



MURIUNGI KIYOGERE (35), mkazi wa Kaunti ya Tharaka-Nithi nchini Kenya, anadaiwa kumchoma kisu mara nne Daniel Mutiria Cece (36) kutokana na mzozo wa kugombea kumbikumbi Jumapili jioni.

Kamanda wa Polisi wa Tharaka Kusini, Kiprop Rutto,  alisema mshukiwa alikimbilia katika Kituo cha Polisi cha Marimanti kuwakwepa wanakijiji waliokuwa wakitaka kumuua.

Mshukiwa alizuiliwa kituoni hapo baada ya kukiri kuua na  polisi walipokwenda eneo la tukio walikuta mwili wa Daniel ukiwa umelowa damu.

Inadaiwa wanaume hao walikuwa marafiki wa miaka mingi na kabla ya ugomvi kutokea walikuwa pamoja wakinywa pombe.

Top 5 ya Wasanii Matajiri Africa, Diamond Hayupo...Why?



Mimi sio shabiki wa mambo ya muziki wa Tanzania, ila napenda sana kuingia mitandaoni na sifa anazopewa Diamond ni nyingi sana.

Ila nimejiuliza, baada ya pitapita zangu nimekutana jarida maarufu Marekani la Forbes limetaja wasanii matajiri zaidi Barani Africa ila cha kushangaza Diamond sijamuona kabisa, shida nini?

Nikaendelea kucheki hadi Top-Ten jamaa hayupo ila Wizkid & Davido wapo. Au uwa ni kiki tu na maisha ya kuigiza

Monday, October 21, 2019

Mke Wangu Anachat na li Mtu Wanaitana "MY"



Aisee huwa naichunia simu ya mke wangu kwa kuogopa bp na pia namuamini maana ana kautulivu kimuonekano na maisha tulioishi hajawahi kuniletea mazombie mpaka yanitishe na kuhisi sio mwaminifu sasa leo week end nipo kitandani nimeshika simu yake aisee kucheki video za whatsapp nikajikuta nimeingia inbox yake Kuna li mtu anachat nalo linaonesha linamcare huku linamuita "My" na yeye anajibu na neno "My".HAPA NILIPO NIMESHAPANIC JAPOKUWA WANASALIMIANA TU NA KUTAKIANA CHAKULA CHEMA ILA KIMENISHANGAZA HICHO KIBWAGIZO CHAO CHA KUITANA "MY" Nataka niuwashe moto maana sijaelewa kabisa hiyo term "My".
Naogopa kuianzisha hii vita kabla sijajua wenzangu hii issue mnaichukuliaje maana nisije itwa Complicator wa term kumbe ni term ya kawaida tu.

NATAKA USHAURI SIO MATUSI.

By Billie

Friday, October 18, 2019

Mechi ya FC Barcelona dhidi ya Real Madrid yaahirishwa

Mechi ya El Clasico iliyokuwa inazikutanisha timu za FC Barcelona dhidi ya Real Madrid iliyotarajiwa kuchezwa Octobe 26 2019 katika uwanja wa Nou Camp Catalunya jijini Barcelona imeahirishwa kwa sababu za kiusalama.

Game hiyo ya El Clasico imeahirishwa kwa sababu za machafuko ya kisiasa yanayoendelea katika jimbo la Catalunya, club za Real Madrid na FC Barcelona zimepanga kukutana na Jumatatu na kujadiliana ni lini itachezwa mechi hiyo.

Mwanzo ilipendekezwa mchezo huo ukachezwe katika dimba la Santiago Bernabeu katika jiji la Madrid, ila kocha wa Barcelona Ernest Valverde amekataa mchezo huo kuamishiwa Madrid kwa sababu itakuwa inaenda kuchezwa siku 3 ikiwa wametoka October 23 kucheza dhidi ya Slavia Prague hivyo wachezaji watakuwa wamechoka.

Meneja was Diamond Salam Sk Naye Aamua Kuimba Kuachia Ngoma Yake Hivi Karibuni

Maneja wa msanii wa muziki wa Bongo Fleva Diamond Platnumz, Sallam SK huwenda naye akatumbukia kwenye muziki huo pendwa hapa nchini.

Ni baada ya Meneja huyo kutoa taarifa kuwa ataachia wimbo wake mpya hivi karibuni. Sallam SK
alitoa taarifa hiyo kupitia mtandao wa Insta Story.


Source

AUAWA KWA KUPIGWA RISASI YA MAKALIO KAHAMA

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kijana aliyekutwa na Kitambulisho chenye jina la Mishael Masatu (29) amefariki dunia baada ya kupigwa risasi kwenye makalio na mlinzi wa Kampuni ya Ulinzi Serengeti Security Services Ltd, mkazi wa mtaa wa Malunga kwenye yard ya magari katika kisima cha mafuta cha PetroAfrica mtaa wa Mbulu Mjini Kahama.

Kwa Mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Richard Abwao tukio hilo limetokea Oktoba 16,2019 majira ya tisa alfajiri.

"Mlinzi wa kampuni ya Ulinzi ya Serengeti Security Services LTD  Isumail Hassan (20) mkazi wa mtaa wa Malunga akiwa kazini hapo kisimani, alifyatua risasi moja kutoka kwenye bunduki aina ya Shortgun yenye namba HP.9-1.  007710112 mali ya Kampuni ya Serengeti Security Services LTD na kumjeruhi matakoni mtu aliyekutwa na kitambulisho chenye jina la Mishael Z. Masatu(29), mkazi wa Nyihogo mtaa wa Sazia ambaye aliingia kwenye yard hiyo bila kibali",ameeleza Kamanda Abwao.

 "Chanzo cha tukio ni majeruhi kuingia kwenye yard bila kibali na kudhaniwa kuwa ni mwizi. majeruhi alianza kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Halmashauri Mji wa Kahama na baadaye alifariki dunia",amesema Kamanda Abwao.

Amesema askari mlinzi  anashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Wilaya Kahama wakati upelelezi unaendelea.

Wednesday, October 16, 2019

Breaking : ANGALIA HAPA MATOKEO YA MTIHANI DARASA LA SABA MWAKA 2019



Matokeo ya darasa la saba 2019, yametangazwa. NECTA imeeleza ufaulu umeongezeka kwa asilimia 3.78. Waliofaulu ni asilimia 81.50 ya watahiniwa 933,369. Pia Watahiniwa 909 wamefutiwa matokeo kwa sababu mbalimbali ikiwemo udanganyifu.




Source

Breking : ANGALIA HAPA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2019...Yanafunguka Fastaa



Matokeo ya darasa la saba 2019, yametangazwa. NECTA imeeleza ufaulu umeongezeka kwa asilimia 3.78. Waliofaulu ni asilimia 81.50 ya watahiniwa 933,369. Pia Watahiniwa 909 wamefutiwa matokeo kwa sababu mbalimbali ikiwemo udanganyifu.



Katibu Mtendaji wa NECTA Dkt Charles Msonde
amesema mwanafunzi aliyeongoza Kitaifa ni Grace Manga kutoka Shule ya Msingi Graiyaki Mara, akifuatiwa na Francis Gwagi kutoka Shule ya Msingi Paradise ya Geita.



Amesema kuwa aliyeshika nafasi ya tatu ni Loi Kitundu kutoka Shule ya Msingi Mbezi ya Dar es Salaam, na Victor Godfrey kutoka Graiyaki ameshika nafasi ya nne.



"Katika ufaulu wa masomo, somo la Kiswahili, Kiingereza na Sayansi katika mtihani huo ufaulu wake umepanda na somo la Hisabati umeshuka,"

Tuesday, October 15, 2019

Breking News : HAYA HAPA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2019...Yanafunguka Fastaa



Matokeo ya darasa la saba 2019, yametangazwa. NECTA imeeleza ufaulu umeongezeka kwa asilimia 3.78. Waliofaulu ni asilimia 81.50 ya watahiniwa 933,369. Pia Watahiniwa 909 wamefutiwa matokeo kwa sababu mbalimbali ikiwemo udanganyifu.



Katibu Mtendaji wa NECTA Dkt Charles Msonde
amesema mwanafunzi aliyeongoza Kitaifa ni Grace Manga kutoka Shule ya Msingi Graiyaki Mara, akifuatiwa na Francis Gwagi kutoka Shule ya Msingi Paradise ya Geita.


Amesema kuwa aliyeshika nafasi ya tatu ni Loi Kitundu kutoka Shule ya Msingi Mbezi ya Dar es Salaam, na Victor Godfrey kutoka Graiyaki ameshika nafasi ya nne.

"Katika ufaulu wa masomo, somo la Kiswahili, Kiingereza na Sayansi katika mtihani huo ufaulu wake umepanda na somo la Hisabati umeshuka,"

Wednesday, October 9, 2019

Mambo 5 ambayo wanawake wanatamani mwanaume ajue wakati wa kufanya mapenzi


Hivi ni baadhi ya vitu ambavyo wanawake hutamani sana wanaume zao wawe wanajua katika mapenzi, ili wasipate shida ya kumwambia mara kwa mara, jambo ambalo si wanawake wengi huwa uwezo wa kumwambia mtu, hapo ndipo unakuta mara nyingi mwanamke anaanza kuchepuka na kwenda kwa mtu mwingine wa kawaida tu kupata mahitaji yake baada ya kuona kile anachokitaka hakipati kwa mpenzi wake.

Yafuatayo ni mambo matano ambayo wanawake wanapenda waume zao wayafanye:

1. Wanawake wanapenda ufuate wanayoyataka
Katika mapenzi wanawake wanapenda ufanye kile wanachokitaka japo ni vigumu kujua mwanamke anapenda nini. Kwa hiyo kama ni vigumu kujua kitu gani anapenda basi ni vizuri kuwa makini na kugundua ni kitu gani hapendi ili usimfanyie ambacho hapendi na ufanye anachopenda. Japokuwa si wanawake wote wanaweza kukwambia ni nini hasa kinawauzi, kuogopa kukuudhi, hivyo inawafanya wapate shida sana na kuweka maisha yao yawe magumu. Kwa sababu hiyo wewe kama mwanaume unapaswa kuwa makini na matendo yao ili kujua tofauti ya vitu ambavyo hawapendi na vile vinavyowapa furaha. Kisha fanya vile wanavyovipenda.

2. Hupendelea tendo la ndoa lidumu muda mrefu
Wanawake hupenda tendo la ndoa lidumu walau kwa dakika mbili. Na wanatamani ikiwezekana hata ikibidi ifanyike siku nzima. Sio muda tuu ndio muhimu bali hata kile unachofanya. Wanaume wengi kujali kujizuia, ilimradi wakae muda mrefu katika tendo, lakini kutokana na tafiti hili sio sababu, wanawake wengi hupenda zaidi ya muda mrefu, hupenda kuungana na wewe kihisia kupitia kushikana, kubusu nakadhalika. Wakati wanaume wengi huwa hawafanyi na kukazania tu kukaa muda mrefu kujua kuwa ndio wanawake wanachotaka. Kwa hiyo wanapenda tendo la ndoa lidumu lakini lisichoshe.

3. Wanataka mwanaume jasiri sio anayetumia nguvu
Wanawake wanataka wanaume walio jasiri wa kufanya nasio wanaotumia nguvu na ubabe. Wanaume wengi huwa hawajui tofauti ya ujasiri na kutumia nguvu, hivyo wasikiapo kuwa inabidi uwe na ujasiri wanadhani kuwa kuna kutumia nguvu na mwisho kuwaumiza wapenzi wao, wanawake wengi wamekuwa wakikerwa na kuogopeshwa na mambo ambayo hufanyiwa na wanaume zao, kipindi ambacho wanaume wakufikiri kufanya hivyo ni kuwa na ujasiri. Wanawake hutamani sana wanaume wangejirekebisha na kujua maana halisi ya kuwa na ujasiri kwamba sio kutumia nguvu na ubabe.

4. Wanawake hawafanani
Wanawake wanapenda wanaume wajue kuwa sio wanawake wote hupenda vitu sawa. Wanaume wengine hufikiri kuwa kwa sababu mpenzi wake wa zamani alikua anapenda kufanyiwa alikuwa basi na huyu wa sasa atakuwa hivyo hivyo, hii inatokea kuwachanganya sana wanawake, na kukereka kwa baadhi ya mambo, huku mwanamke akiwa hana jinsi bali kuvumilia tu, na mwisho wa siku ndio unakuta, ananza kutafuta njia ya kukukwepa. Kwa hiyo mwanamme anatakiwa amjue mpenzi wake kibinafsi yeye kama yeye na sio kumjua kwa kumfananisha na wanawake wengine. Mwanamme amfanyie mpenzi wake kama anavyopendelea na sio kama anavyofikiri wanawake wanapendelea.

5. Kumfurahisha mwanamke sio ufundi tu bali ni mapenzi ya dhati
Wanawake wanapenda kuonyeshwa upendo au mapenzi ya dhati. Wanawake wengi hukubali kuwa kuna wanume wenye ufundi na uzoefu katika haya mapenzi, ila wanasema hiyo sio kitu bora zaidi, wanachokitaka ni mapenzi, kuonyesha mapenzi na dalili zote za kumjali ndio jambo muhimu sana. Mapenzi ni kichocheo kikubwa cha kumridhisha mwanamke.


Tuesday, October 8, 2019

Simba Watangaza Mechi Tatu Za Kirafiki


Timu ya Simba SC itacheza mechi tatu za kirafiki dhidi ya Bandari FC ya Kenya, Aigle Noir ya Burundi pamoja na Mashujaa ya Kigoma kabla ya kukutana na Azam FC Oktoba 23.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...