Sunday, January 31, 2021

Mkuu wa polisi nchini Ujerumani azituhumu kampuni za ndege kwa kuvunja sheria za corona

 


Mkuu wa polisi nchini Ujerumani Dieter Romann amezishutumu kampuni za ndege kwa kushindwa kuzingatia sheria za kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona . 


Katika mahaojiano na gazeti la Ujerumani la Bild am Sonntag yaliyochapishwa leo, Romann amesema katika muda wa siku sita zilizopita, polisi nchini humo wamegundua karibu matukio 600 ambapo kampuni za ndege zimekiuka masharti ya kupambana na COVID-19. 


Ameongeza kuwa abiria kutoka maeneo yalio na viwango vya juu vya maambukizi ya virusi hivyo ama yale ambayo aina mpya ya virusi hivyo imegunduliwa, wameingia nchini Ujerumani bila ya kusajiliwa kidigitali ama kuonesha vyeti vya ushahidi wa kutokuwa na maambukizi ya virusi hivyo jambo ambalo ni kinyume na sheria. 


Romann amesema kuwa kampuni za ndege sasa zinakabiliwa na hatari ya kutozwa faini kutoka kwa mamlaka ya afya ya dola takriban elfu 30 kwa ukiukaji huo wa kanuni.

Pentagon yasimamisha utoaji chanjo kwa wafungwa wa Guantanamo

 


Wizara ya ulinzi ya Marekani imesema itasimamisha mpango wake wa kuwapa chanjo dhidi ya COVID-19 wafungwa wa makosa ya ugaidi wanaozuiwa kwenye kambi ya Guantanamo kufuatia kuongezeka kwa malalamiko katika wakati ambapo nchi hiyo inajikakamua kuwachanja kwanza watumishi wa afya na wazee. 


Msemaji wa wizara hiyo John Kirby ameandika hayo kupitia ukurasa wa twitter akisema hakuna mfungwa yoyote kwenye kambi hiyo ambaye tayari amechanjwa. 


Kirby amekiri akisema ni kweli rais Joe Biden amesema ana mpango wa kutokomeza virusi vya corona katika siku yake ya kwanza ofisini lakini hakusema atawapa chanjo magaidi kwanza kabla ya Wamarekani. 


Kambi ya Guantanamo iliyoko Cuba inawazuia washukiwa wa makosa ya ugaidi ikiwa ni pamoja na Khalid Sheikh Mohammed, mfuasi wa kundi la Al-Qaeda anayedaiwa kupanga shambulizi la Septemba 11.

Wakamatwa Kwa Madai Ya Wizi Wa Fedha Kwa Njia Ya Simu


Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Ialla jijini Dar es Salaam linawashikilia watu 10 kwa tuhuma za wizi wa mtandaoni na utapeli.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa Ilala, Janeth Magomi imeeleza kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa katika tarehe tofauti ya mwezi Januari mwaka huu katika maeneo tofauti ya Jiji la Dar es Salaam na wilayani Mkuranga mkoani Pwani.

Aidha, Mgomi ameeleza kuwa watuhumiwa hao wamekamatwa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) baada ya wananchi kadhaa kutapeliwa fedha zao. Wananchi hao walitoa taarifa kwa jeshi hilo ndipo ukafanyika msako pamoja na kuweka mtego wa kubaini mtandao wa watuhumiwa hao.

Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi Mkoa wa Ilala limewatahadhariasha watumiaji wa huduma za mitandao kuwa makini na watu ambao mara nyingi wanajifanya ni watoa huduma za mitandao husika na kuwalaghai wananchi ili kuwaibia.

Miongoni mwa watuhumiwa waliotiwa mbaroni ni pamoja na Baraka Makwaya, Fatuma Ayoub, Teddy Njauz, Modesta Njauz pamoja na Gift Makwaya.


IGP Sirro Awataka Polisi Wasaidizi Kufuata Sheria


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka Polisi Wasaidizi waliopo kwenye taasisi mbalimbali nchini kuhakikisha wanaheshimu na kuzingatia sheria sambamba na nidhamu wakati wanapotekeleza majukumu yao ya kazi za kila siku katika kubaini, kuzuia na kupambana na uhalifu.

IGP Sirro amesema hayo jana  jijini Dar es salaam, wakati alipofanya kikao kazi na Polisi Wasaidizi waliopo Kanda Maalum ya Dar es salaam ambapo amesema kuwa, weledi, ufanisi na kujituma kutasaidia kupunguza malalamiko miongoni mwa jamii wanayoihudumia.

Naye Kamishna wa Kamisheni ya Ushirikishwaji wa Jamii Dkt. Mussa Ali Mussa amesema kuwa, uwepo wa Polisi Wasaidizi umesaidia kuwezesha mamlaka na Halmashauri mbalimbali zilizopo nchini kuendelea kuimarika.


Tutatenga Fedha Kwa Ajili Ya Huduma Za Ugani- Prof. Mkenda


Wizara ya Kilimo imesema katika bajeti ya mwaka 2021/22 inatarajia kutenga fedha mahsusi kwa ajili kugharimia huduma za ugani ili kuondoa changamoto zinazotatiza ukuaji wa tija kwenye uzalishaji mazao nchini ikiwemo maslahi ya maafisa kilimo ugani.


Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda ametoa kauli hiyo jana (30.01.2021) jijini Dodoma wakati akifunga kikao kazi baina ya wizara yake na maafisa kilimo toka mikoa 26 na halmashauri zote 185 za Tanzania bara uliojadili hali ya upatikanaji huduma za ugani kwenye kilimo.


"Kilimo kimekuwa na maneno mengi utasikia kilimo ni uti wa mgongo ama kilimo cha kufa na kupona.Sasa tunasema maneno yametosha hebu tuanze hatua moja mbele kwa vitendo tuboreshe utoaji huduma za ugani nchini ili wakulima wahudumiwe kwa vitendo" alisema Prof. Mkenda.


Prof. Mkenda alibainisha kuwa wizara yake imeitisha kikao hicho cha siku mbili ili kujadiliana na wataalam wa kilimo wote pamoja na wadau wa sekta binafsi hali ya kuboresha utoaji huduma za ugani na kuweka mikakati ya kuondoa changamoto za ugani


Alisema kuwa suala la kutokuwepo bajeti mahsusi kwa ajili ya watoa huduma za ugani kwenye ngazi za mikoa, halmashauri na vijiji imekuwa ikiathiri utoaji huduma kwa wakulima kushindwa kulima kwa tija.


Katika kikao hicho Waziri wa Kilimo alirejea kueleza dira ya wizara yake kwa sasa na kutaja mambo manne ya kipaumbele ili kilimo kichangie zaidi ukuaji wa uchumi  kwanza ni kuongeza utafiti na uzalishaji mbegu bora za mazao.


Pili, kutoa elimu bora ya kilimo ,tatu kutafuta masoko ya mazao ya wakulima na nne kuhakikisha wakulima na wawekezaji wanapata mitaji yenye riba nafuu toka kwenye taasisi za kifedha nchini.


"Tutawekeza fedha bajeti ijayo na nguvu kukuza utafiti ili tupate mbegu bora zaidi zenye kutoa mavuno bora na tija kwa wakulima" alisisitiza Prof. Mkenda.


Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Charles Mwijage alisema anawapongeza wakulima wa Tanzania pamoja na wataalam wa kilimo kwa kuhakikisha katika kipindi cha miaka mitano ya kwanza ya serikali ya awamu ya tano Tanzania haikupata tatizo la njaa.


" Kipindi chote kuanzia mwaka 2015 hadi 2020 nchi hii haikupata njaa, tunawashukuru maafisa ugani na wakulima wote wa Tanzania kwa kazi kubwa ya kuhakikisha taifa lina chakula cha kutosha" alisema Mwijage ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.


Mwijage aliiomba serikali kuweka mikakati mizuri na kuongeza bajeti ya kuhudumua watoa huduma za ugani wa serikali waliopo chini ya Ofisi ya Rais Tamisemi na Wizara ya Kilimo ili watatue changamoto za wakulima.


Naye Mwenyekiti wa umoja wa Maafisa Kilimo Halmashauri (DAICOs) Enock Ndunguru aliomba serikali kupitia Wizara ya Kilimo kuwa na mkakati wa kuwahamishia maafisa ugani waliopo halmashauri zote nchini kutoka Mamlaka za Serikali za Mitaa na sasa wawe chini ya Wizara ya Kilimo.


Katika hatua nyingine Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya alisema kwa sasa kuna maafisa ugani kilimo 6700 ambao wanahitaji kuwezeshwa vitendea kazi ili watekeleze majukumu yao ya kusimamia kilimo


Kusaya alisema kwa kuanzia wizara ya kilimo itaendeleza mkakati wa kuwapatia pikipiki maafisa ugani wote 67000 kwa awamu pamoja na kupeleka kifaa maalum cha kupima afya ya udongo (Extension Kit).


Akizungumza kwenye kikao hicho Mbunge wa Musoma Vijijini Prof. Sospeter Muhongo alitoa wito kwa serikali kufanya jitihada za kukifanya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Mwalimu Nyerere (Mwalimu Nyerere University of Agriculture) kilichopo Butiama Mara kianze kudahili wanafunzi mwaka 2021/22 ili kifundishwe maafisa ugani.


"Chuo hiki cha Kilimo cha Mwalimu Nyerere  cha Butiama kimekusudiwa kufundisha wataalam wa ugani ,tunaomba kianze mapema mwaka huu 2021 ili tatizo la upatikanaji wataalam wa kilimo hususan vijijini litatuliwe" alisema Prof. Muhongo.


Mwisho
Imeandaliwa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Kilimo
DODOMA
31.01.2021




Updates : PAKUA APP YA MALUNDE 1 BLOG ....IMEFANYIWA MABORESHO 2021

Kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kupakua/ kudownload App ya Malunde 1 blog tukuhabarishe masaa 24.

Usikubali kupitwa na habari na Matukio yanayotoke… Pakua Aplikesheni ya Malunde 1 blog


Tembea na dunia kiganjani kiulaini kabisa.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡


Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://bit.ly/2Qb7qyF

Tafadhali fuata maelekezo hapo juu... Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa




Saturday, January 30, 2021

AKAMATWA BAADA YA KUNASWA AMEFICHA MWILI WA MAREHEMU MIAKA 10 NYUMBANI


Polisi nchini Japan wamemkamata mwanamke mmoja baada ya mwili wa mama yake kukutwa kwenye jokofu nyumbani kwake.

Yumi Yoshino, 48, amesema kuwa alimkuta mama yake akiwa amefariki dunia kisha aliuficha mwili wake miaka 10 iliyopita kwa sababu '' hakutaka kuhama'' katika nyumba waliokuwa wakiishi mjini Tokyo, vyombo vya habari vimewanukuu maafisa polisi ambao hawakutajwa majina yao.

Hakukuonekana majeraha yoyote kwenye mwili ulioganda barafu, polisi wameeleza.

Mamlaka hawakuweza kuthibitisha muda na sababu ya kifo cha mwanamke huyo.

Mwili uliripotiwa kugundulika na mfanya usafi baada ya Bi. Yoshino kulazimishwa kuondoka katika nyumba hiyo kwa sababu ya kukosa kodi.

Mwili ulikuwa umekunjwa kiasi cha kutosha kuingia kwenye jokofu lenye barafu, polisi walisema.

Bi Yoshino alikamatwa katika hoteli mjini Chiba karibu na jiji la Tokyo, siku ya Ijumaa.

CHANZO - BBC SWAHILI

Wazee walioondolewa bandarini kwa kukosa sifa wamuangukia Magufuli

 


Mzee Omary Said ameamua kujikita katika kilimo wilayani Rufiji mkoani Pwani, baada ya kuondolewa kazini miaka miwili iliyopita kwa sababu ya kuwa na elimu ya darasa la saba.


Saidi alikuwa akifanya kazi kama kibarua katika bandari ya Dar es Salaam tangu mwaka 1994, ilipofika mwaka 2007 aliajiriwa rasmi katika bandari hiyo na kufanya kazi mpaka mwaka 2018 alipoondolewa kwa kukosa sifa.


Alikuwa amebakisha miaka miwili astaafu kazi yake kama msimamizi katika shughuli ya kushusha mizigo kwenye meli (foreman), hivyo amepoteza mafao yake ambayo angepata baada ya kustaafu.


"Lazima maisha yaendelee, ukikosa plani A, unatafuta plan B. Ndiyo maana nimejikita kwenye kilimo ili niendelee kuihudumia familia yangu," anasema Said.


Said anasimulia jinsi alivyoanza kazi katika bandari hiyo kwamba alianza kama kibarua wa kupakia na kupakua mizigo na kwamba kadri siku zilivyozidi kwenda, Mamlaka ya Bandari nchni (TPA) ilianza kuwapatia mikataba ya muda mfupi; miezi mitatu, sita mpaka mwaka.


Anasema mwaka 2007, alifanikiwa kupata ajira ya kudumu katika bandari hiyo na wakati huo hakuwahi kusikia chochote kuhusu waraka wa ajira wa mwaka 2004 ambao unataka watumishi wa umma kuajiriwa kwa elimu ya kidato cha nne.


Mkulima huyo anasema makosa yalifanywa na viongozi waliopita kwa kuwaajiri wakati wakijua hawakuwa na sifa, hivyo anaiomba Serikali iwapatie stahiki zao kwa sababu walijitoa kwa muda mrefu kufanya kazi katika bandari hiyo.


"Tumekubali kuondoka, lakini tunaiomba Serikali itusaidie tupate stahiki zetu. Tuna haki zetu ambazo tuliziacha, tunastahili kulipwa," anasema Said na kuongeza kuwa Serikali iwahurumie kama watoto wake.


Anasisitiza kwamba kuwa darasa la saba haina maana kwamba hawana akili, wanaweza kuwa na akili pengine kuliko hata waliosoma mpaka sekondari.


Anasema waliokuwa darasa la saba wengi walipatiwa mafunzo mbalimbali kama vile ushonaji na udereva wa winch na focal.


"Katika hili kundi la walioishia darasa la saba, tupo sisi pia ambao tulifika kidato cha nne lakini hatuna cheti, yaani wale form four failure kabisa," anasema mzee huyo na kusisitiza kwamba maslahi yao yazingatiwe.


Kilio cha Said kinawakilisha waliokuwa wafanyakazi wa bandari zaidi ya 100 ambao walipunguzwa kazini kwa sababu wana vyeti vya darasa la saba, jambo ambalo ni kinyume na waraka wa ajira wa mwaka 2004.


Wafanyakazi hao wameshusha kilio chao kwa Rais John Magufuli wakitaka awaonee huruma na kuwalipa stahiki zao baada ya kuondolewa kazini mwaka 2018 kwa sababu wana elimu ya darasa saba.


Akizungumza na gazeti hili, kiongozi wa wafanyakazi hao, Fahki Athuman alisema wamekwenda kwa viongozi mbalimbali wa Serikali kutaka kupatiwa msaada ili wapate stahiki zao, hata hivyo, hawajapata msaada wowote.


"Suala hili bado liko Mahakamani, lakini sisi tunaamini kwamba tunaweza kulimaliza kwa mazungumzo na Serikali, ndiyo maana tumekwenda kwa Katibu mkuu wa Utumishi, tumekwenda Dodoma kwa Spika wa Bunge, tumekwenda kwa Waziri Mkuu mpaka Ikulu.


"Pamoja na jitihada hizo za kutafuta suluhisho, jambo letu limekwama. Tunamuomba Rais Magufuli asikie kilio chetu, tunahangaika sana tangu tuondolewe kazini, hatukulipwa chochote, wenzetu wengine walikuwa wanakaribia kustaafu," alisema Athuman.


Kiongozi huyo alibainisha kwamba kwa sasa wanachotaka ni kulipwa stahiki zao kwa sababu wamefanya kazi kwa muda mrefu katika bandari hiyo kama vibarua na baadaye wakaajiriwa rasmi kwa elimu hiyo hiyo waliyonayo. "Sisi hatukuwa na vyeti feki, tuna vyeti vya darasa la saba na tulikuwa tunafanya kazi za kubeba mizigo, wengine walipata mafunzo katika Chuo cha Bandari wakaanza kuendesha mitambo. Tunataka tupewe stahiki zetu," alisema.


Mwathirika mwingine katika kundi hilo, Kassimu Mnyani alisema waraka wa mwaka 2004 unaoelekeza ajira kutolewa kwa wenye elimu ya kuanzia kidato cha nne haukuwafikia, lakini wanashangaa kwanini waliajiriwa wakati kulikuwa na waraka huo.


Alisema baada ya kufanya kazi kama kibarua kwa muda mrefu, mamlaka ya bandari ilitaka kuajiri watu kwa sharti la kuwa na ujuzi. Alisema baadhi ya watu walijiendeleza kwa kupata ujuzi tofauti, ndipo wakaajiriwa.


"TPA ilikuwa inaajiri kwa kuzingatia mahitaji yake yenyewe na huo waraka wa ajira wa mwaka 2004 haukuwahi kutufikia, tusingeweza kuajiriwa," alisema Mnyani na kusisitiza kwamba wanaomba Rais Magufuli awasaidie.


Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), Deusdedit Kakoko alisema wafanyakazi hao waliondolewa kihalali kwa kufuata sheria kama ilivyokuwa kwa wafanyakazi katika taasisi nyingine za umma.


Alisema anashangaa kuona wafanyakazi hao wa zamani wakiendelea kulalamika kila siku, wakati wenzao wa maeneo mengine wamekubaliana na hali na hawazunguki kila kona kulalamika kwamba wameonewa.


"Sheria inapopitishwa, lazima wote tuiheshimu. Sheria ya ajira ya mwaka 2004 inaelekeza kwamba Serikali haitaajiri mtu wa kiwango cha elimu chini ya kidato cha nne, sasa sheria ikisema hivyo walitaka sisi tufanyaje?" alihoji Kakoko.


Kuhusu waliokuwa na elimu ya darasa la saba kabla ya mwaka 2004, Kakoko alisema hao hawakuguswa na mpaka sasa wapo wanaendelea na kazi zao na kusisitiza kwamba walioondolewa ni wale walioajiriwa baada ya mwaka 2004.


"Kama wangekuwa wameajiriwa kabla ya mwaka 2004 malalamiko yao yangekuwa sawa, lakini hao ni baada ya mwaka 2004, wamekwenda mpaka Ikulu lakini walirudishwa, hawana hoja," alisema Kakoko.


Mkurugenzi huyo alibainisha kwamba wapo wengine katika kundi hilo waliondolewa kwa kuwa cheti feki cha kidato cha nne, baada ya kuona wameguswa wakatoa cheti hicho na kubaki na cheti cha darasa la saba kisha wanalalamika kuonewa.


Alipotafutwa Katibu mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Meli na Bandari Tanzania (Dowuta), Jonathan Msoma kuzungumzia suala hilo, hakutaka kuzungumza lakini akaelekeza suala hilo kwa kiongozi wa wafanyakazi hao.

Jafo atangaza wiki nzima ya kupiga nyungu

 


Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo, ametangaza siku saba za kupiga nyungu kwa Watanzania huku wakiendelea kumuomba Mungu, alizozipa jina la 'One week season Three' ili watu wajifukize huku wakiendelea kuchapa kazi na Corona ikose nafasi.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 30, 2021, wakati akizungumza na wananchi wa mkoa wa Tabora mara baada ya Rais Dkt. John Magufuli, kumaliza kuweka jiwe la msingi katika jengo la wagonjwa wa dharura katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora pamoja kuzindua mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda maeneo ya Tabora, Nzega na Igunga.

"Hapa Corona haina nafasi, Mh Rais tutaendelea kumuomba Mungu kama ulivyoelekeza na umesema watu wajifukize sana na Rais naomba nikuambie Jumatatu tunaanza kampeni nyingine ya one week season three, nyungu kama kawaida tunajifukiza, tunakula matunda tunaanza tarehe 1 hadi tarehe 7 hatupoi kazi inaendelea, uchumi wetu lazima usimame", amesema Waziri Jafo


Source

WAFUGAJI NCHINI WATAKIWA KUFUGA KISASA

Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki akizungumza wakati
wakati wa hafla ya kukabidhi malori na vifaa vya maziwa kutoka shirika la Heifer International kupitia mradi wa usindikaji maziwa Tanzania (TMPP) iliyofanyika katika kiwanda cha Tanga Fresh kilichopo Jijini Tanga kushoto aliyekaa ni Meneja wa Kanda ya Mashariki Benki ya Maendeleo ya kilimo TADB Jeremiah Mhada

Mkurugenzi wa mradi wa usindikaji wa maziwa Tanzania kutoka shirika la Helfer Mark Tsoxoakizungumza wakati wa halfa hiyo
Meneja wa Kanda ya Mashariki Benki ya Maendeleo ya kilimo TADB Jeremiah Mhada akieleza jambo wakati wa halfa hiyo
Kaimu Msajili bodi ya maziwa Noely Byamunguakizungumza wakati wa halfa hiyo
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki kushoto akikata utepe wakati wa hafla ya kukabidhi malori na vifaa vya maziwa kutoka shirika la Heifer International kupitia mradi wa usindikaji maziwa Tanzania (TMPP) iliyofanyika katika kiwanda cha Tanga Fresh kilichopo Jijini Tanga kulia ni Mkurugenzi wa mradi wa usindikaji wa maziwa Tanzania kutoka shirika la Helfer Mark Tsoxo

Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki kushoto akimshukuru Mkurugenzi wa mradi wa usindikaji wa maziwa Tanzania kutoka shirika la Helfer Mark Tsoxo mara baada ya makabidhiano hayo kulia anayeshuhudia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ambaye pia alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga katika halfa hiyo
Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki akiwasha moja ya magari hayo

WAFUGAJI  nchini wametakiwa kubadilika na kuachana na ufugaji wa mazoea bali wafuge kisasa kwa ajili ya kupata mazao mengi lakini yenye ubora ambayo yataweza kuuzika kwa faida na hivyo kuongeza mchango wa pato la Taifa.

Ushauri huo umetolewa na Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki wakati wa hafla ya kukabidhi malori na vifaa vya maziwa kutoka shirika la Heifer International kupitia mradi wa usindikaji maziwa Tanzania (TMPP) iliyofanyika katika kiwanda cha Tanga Fresh kilichopo Jijini Tanga.

Alisema kuwa licha ya Tanzania kuwa na mifugo mingi lakini sekta hiyo mchango wake kwenye pato la taifa ni asilimia 7.9% pekee  kutokana na ufugaji wa kimazoea  ambao hautoi matokeo bora.

Akizungumzia uzalishaji wa maziwa nchini Waziri Ndaki alisema ni lita Bil 3.01 huku kati ya hizo lita Mil 2.1 zinatokana na ng'ombe wa asili Mil 31 huku ng'ombe wa kisasa Mil 2 wanatoa lita bil 0.9. 

"Kutokana na uzalishaji mdogo wa maziwa hata kiwango cha unywaji wa maziwa kwa mwananchi mmoja mmoja kimekuwa kidogo kwani kwa mujibu wa takwimu ni lita 54 kwa mwaka sawa na kijiko kimoja kwa siku" alisema Waziri Ndaki.

Nae Kaimu Msajili bodi ya maziwa Noely Byamungu alisema kuwa uwepo wa mradi umesaidia kuongeza kasi ys uanzishwaji wa viwanda vya maziwa hadi kufikia vitano ambavyo vinazalisha maziwa kwa kutumia teknolojia ya UHT.

Alisema kuwa bado kumekuwepo na changamoto katika eneo la ukusanyaji wa maziwa kwani kuna kiasi kikubwa yanakuwa hana kosa ubora kabla ya kufika soko hivyo kuwa hasara kwa mfugaji.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uzalishaji na masoko kutoka wizara ya mifugo na uvuvi Steven  Maiko alisema kuwa kutokana na tathimini waliyoifanya 2016/17 inaonyesha kuwa ifikapo mwala 2030/31 sekts hiyo itakabiliwa na upungufu mkubwa raslimali zake za nyama na maziwa kutokana na ongezeko la idadi ya watu.

Hivyo kutokana na changamoto hiyo serikali kwa kushirikiana na wahisani waliamua kuja na mradi huo ili  kuongezs uzalishaji, kudhibiti magonjwa ya mifugo lakini.na kuongeza mnyororo wa thamani wa maziwa ikiwemo kuweka mazingira safi ya kufanyabiashara.

Nae  Mkurugenzi wa mradi wa usindikaji wa maziwa Tanzania kutoka shirika la Helfer Mark Tsoxo alisema kuwa lengo la mradi wa TMPP kuongeza kipato kwa wafugaji wapatao 50, 000 nchi nzima na kwa kipindi cha miezi mitatu pekee tayari wameweza kuwafikia wafugaji 45, 000 kwa kuwapa mafunzo ya ufugaji wa kisasa ili waweze kupata mazao bora na ambayo yataweza kuuza kwa urahisi.

Alisema kwa upande wa wasindikaji waweze kuwawezesha vifaa ili kuhakikisha wanaboresha ukusanyaji wa maziwa na kudhibiti ubotevu wake ili kumuhakikishia mfugaji  soko lenye uhakika.

Nae Meneja wa Kanda ya Mashariki Benki ya Maendeleo ya kilimo TADB Jeremiah Mhada alisema kuwa benki hiyo imewawezesha wafugaji mkopo wa zaidi ya sh Mil 396 pamoja na mitamba bora.

"Ili kuongeza kipato kwa wafugaji wadogo tumewawezesha kupata mitamba ya kisasa na kiwaunganisha ns masoko ili kuongeza thamani na kuchoches kuongeza uzalishaji wa maziwa nchini" alisema Mhada.


Zuchu – Sukari (Official Music Video)



SECOND lady kutoka lebo kubwa ya muziki Bongo, Wasafi Classic Baby 'WCB', Zuhura Othman 'Zuchu' leo Januari 30, 2021 ameachia video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Sukari.

VIDEO:


WAZIRI JAFO ATANGAZA SIKU 7 ZA WATANZANIA KUPIGA NYUNGU KUCHUKUA TAHADHARI YA CORONA


Waziri wa Tamisemi, Seleman Jafo ametangaza kuanzia Februari mosi hadi 7, 2021 zitakuwa siku saba za kupiga nyungu kwa Watanzania ili kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa corona.

Akizungumza mkoani Tabora leo Jumamosi Januari 30, 2021 katika ziara ya Rais John Magufuli, waziri huyo amesema wananchi wanatakiwa kuendelea na majukumu ya kujenga Taifa bila hofu sambamba na kuchukua tahadhari kwa kupiga nyungu akimaanisha kujifukiza.

"Hakuna Mtanzania atajifungia ndani kwa ajili ya hofu ya ugonjwa huu wote tutapiga nyungu kuanzia Februari moja mpaka saba baada ya hapo shughuli nyingine ziendelee kama kawaida," amesema Waziri Jafo.

Amesema hakuna hofu ya kuacha kufanya shughuli za maendeleo na nyungu ni shughuli inayotakiwa kufanyika mara kwa mara.



DC Sabaya aibukia mochwari apiga marufuku maiti kuzuiwa kisa madeni

 


Serkali Wilayani Hai imepiga marufuku masharti yanayowekwa na Hospitali ya kuzuia miili ya watu waliofariki hadi Ndugu zao watakapomaliza madeni yanayotokana na matibabu wakati wa uhai wake.

Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya ameelekeza kutowekwa sharti lolote wakati wa kuchukua mwili na kuongeza kwamba utaratibu huo unaongeza huzuni na majonzi kwa wafiwa.


Amesema inashangaza kuona huu utaratibu unakita mizizi huku ukiwa hauendani na Mila na Desturi za kibinadamu.


Sabaya pia ameonya Watumishi wa Afya kuacha kuwekeza katika kufitiniana na majungu kwani kunaua na kuondoa Watu wenye uwezo katika Taasisi na kubakiza Watu ambao wamewekeza katika maneno tu.


MIGODI YA BUZWAGI NA BULYANHULU YALIPA USHURU BIL 2.3 KWA AJILI YA MAENDELEO MANISPAA YA KAHAMA NA HALMASHAURI YA MSALALA

Viongozi wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu na Manispaa ya Kahama,halmashauri ya Msalala na Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha (wa tatu kushoto) baada ya makabidhiano ya hundi zenye thamani ya shilingi Bilioni 2.387 kwa Manispaa ya Kahama na Halmashauri ya wilaya ya Msalala ikiwa ni malipo ya ushuru wa huduma 'Service Levy'

 Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Twiga Minerals kupitia Migodi yake ya Buzwagi na Bulyanhulu imekabidhi hundi zenye thamani ya shilingi Bilioni 2.387 ( Tsh. 2,387,745,061.23/=) kwa Manispaa ya Kahama na Halmashauri ya wilaya ya Msalala ikiwa ni malipo ya ushuru wa huduma 'Service Levy' kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai hadi Desemba mwaka 2020.

Hafla fupi ya makabidhiano imefanyika leo Jumamosi Januari 30, 2021 katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Kahama na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu na viongozi wa Manispaa ya Kahama na halmashauri ya Msalala wakiongozwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha.

Akikabidhi hundi hizo, Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi,Benedict Busunzu amesema mgodi wa Buzwagi umelipa kiasi cha shilingi 1,642,815,335.45/= kwa Manispaa ya Kahama huku Mgodi wa Bulyanhulu ukilipa shilingi 744,929,725.78/= ambazo ni malipo ya ushuru kwa ajili ya maendeleo.

"Kampuni ya Twiga Minerals ambayo ni Kampuni inayoundwa ka ushirikiano baina ya Kampuni ya madini ya Barrick na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia migodi yake ya Buzwagi na Bulyanhulu leo tunakabidhi jumla ya shilingi Bilioni 2.387 kwa ajili ya shughuli za maendeleo katika Manispaa ya Kahama na halmashauri ya Msalala",amesema Busunzu.

"Tunapokabidhi fedha hizi tunaona Fahari kubwa kwa kuwa tunaendelea kuona matunda ya matumizi sahihi ya fedha hizi katika uboreshaji wa  miundo miundombinu mbalimbali inayoimarisha uchumi na huduma muhimu kwa ajili ya wananchi",ameeleza Buzunzu.

Busunzu amesema Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu inafurahi kuwa sehemu ya mafanikio ya maendeleo ya Kahama na Msalala na mkoa wa Shinyanga kwa ujumla aambapo kipimo  cha mafanikio hayo ni matokeo chanya na endelevu yanayotokana na mchango wa fedha ambazo wamekuwa wakitoa.

"Tumeshuhudia mafanikio mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupadishwa hadhi Halmashauri ya Mji wa Kahama kuwa Manispaa ya Kahama.Tunapenda kuwapongeza sana viongozi wetu wa serikali na wananchi kuanzia ngazi ya kijiji tunakochimbia madini hadi mkoa kwa ushirikiano na juhudi tunazoziona za kusimamia vizuri matumizi ya fedha za ushuru wa huduma ambazo tunalipa kila baada ya miezi sita",ameongeza Busunzu.

"Juhudi hizo zinatuhamasisha kufanya kazi zaidi ili tuzalishe zaidi na tulipe ushuru mkubwa na kuendelea kuchangia zaidi maendeleo chanya katika Manispaa ya Kahama,halmashauri ya Msalala na mkoa wa Shinyanga kwa ujumla",amesema Busunzu.

Amesema Kampuni ya Twiga Minerals kwa kushirikiana na serikali na wadau wengine wa maendeleo wa ndani na nje ya nchi itaendelea kujenga jamii endelevu ili kuendana na Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano na Dira ya Taifa 2025.

Akipokea Hundi hizo, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha ameishukuru Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu kwa kulipa ushuru wa huduma kwa wakati na hivyo kuongeza mapato ya ndani ya Manispaa ya Kahama na halmashauri ya Msalala akibainisha kuwa fedha hizo kiasi cha shilingi Bilioni 2.3 zitatumika kwa ajili ya mahitaji ya wananchi.

"Migodi hii inatusaidia sana kupata fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo na imekuwa na mchango mkubwa sana katika kuifanya Halmashauri ya Mji wa Kahama ipandishwe hadhi na kuwa Manispaa ya Kahama",amesema Macha.

Mkuu huyo wa wilaya ya Kahama amewaelekeza Wakurugenzi wa Manispaa ya Kahama na halmashauri ya Msalal kutumia fedha katika sekta ya elimu na afya ili kuondokana na changamoto zilizopo kwenye baadhi ya maeneo.

Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi, Benedict Busunzu (wa tatu kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha ( wa pili kushoto) hundi ya shilingi 744,929,725.78  kwa ajili ya Halmashauri ya Msalala ambazo ni malipo ya ushuru kwa ajili ya maendeleo leo Jumamosi Januari 30,2021. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala, Simon Berege. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi,Benedict Busunzu (wa tatu kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha ( wa pili kushoto) hundi ya shilingi 744,929,725.78  kwa ajili ya Halmashauri ya Msalala ambazo ni malipo ya ushuru kwa ajili ya maendeleo. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala, Simon Berege.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha ( wa pili kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala, Simon Berege hundi ya shilingi 744,929,725.78 zilizotolewa na mgodi wa Bulyanhulu kwa ajili ya Halmashauri ya Msalala ambazo ni malipo ya ushuru kwa ajili ya maendeleo
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha ( wa pili kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala, Simon Berege hundi ya shilingi 744,929,725.78 zilizotolewa na mgodi wa Bulyanhulu kwa ajili ya Halmashauri ya Msalala ambazo ni malipo ya ushuru kwa ajili ya maendeleo
Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi, Benedict Busunzu (wa pili kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha (wa tatu kushoto) hundi ya shilingi 1,642,815,335.45/=  kwa ajili ya Manispaa ya Kahama ambazo ni malipo ya ushuru kwa ajili ya maendeleo. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Anderson Msumba, akifuatiwa na Meya wa Manispaa ya Kahama, Yahaya Ramadhani Bundala.
Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi, Benedict Busunzu (wa pili kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha (wa tatu kushoto) hundi ya shilingi 1,642,815,335.45/=  kwa ajili ya Manispaa ya Kahama ambazo ni malipo ya ushuru kwa ajili ya maendeleo.
Meya wa Manispaa ya Kahama, Yahaya Ramadhani Bundala akimkabidhi Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama, Anderson Msumba hundi ya shilingi 1,642,815,335.45/= zilizotolewa na mgodi wa Buzwagi kwa ajili ya Manispaa ya Kahama ambazo ni malipo ya ushuru kwa ajili ya maendeleo.
Meneja Mkuu wa Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi, Benedict Busunzu akizungumza wakati akikabidhi hundi za shilingi Bilioni 2.3 ambapo amesema mgodi wa Buzwagi umelipa kiasi cha shilingi 1,642,815,335.45/= kwa Manispaa ya Kahama huku Mgodi wa Bulyanhulu ukilipa shilingi 744,929,725.78 ambazo ni malipo ya ushuru kwa ajili ya maendeleo.
Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha akiushukuru mgodi wa Buzwagi kwa kulipa kiasi cha shilingi 1,642,815,335.45/= kwa Manispaa ya Kahama na Mgodi wa Bulyanhulu kulipa shilingi 744,929,725.78 ambazo ni malipo ya ushuru kwa ajili ya maendeleo.
Meya wa Manispaa ya Kahama, Yahaya Ramadhani Bundala akiishukuru Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu kwa kuendelea kutoa ushuru wa huduma kwa wakati na kuahidi kutumia fedha zilizotolewa kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Viongozi wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu na Manispaa ya Kahama,halmashauri ya Msalala na Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha (wa tatu kushoto) baada ya makabidhiano ya hundi hundi zenye thamani ya shilingi Bilioni 2.387 kwa Manispaa ya Kahama na Halmashauri ya wilaya ya Msalala ikiwa ni malipo ya ushuru wa huduma 'Service Levy'
Viongozi wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu na Manispaa ya Kahama,halmashauri ya Msalala na Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha (wa tatu kushoto) baada ya makabidhiano ya hundi zenye thamani ya shilingi Bilioni 2.387 kwa Manispaa ya Kahama na Halmashauri ya wilaya ya Msalala ikiwa ni malipo ya ushuru wa huduma 'Service Levy'
Viongozi wa Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu na Manispaa ya Kahama,halmashauri ya Msalala na Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha (wa tatu kushoto) baada ya makabidhiano ya hundi zenye thamani ya shilingi Bilioni 2.387 kwa Manispaa ya Kahama na Halmashauri ya wilaya ya Msalala ikiwa ni malipo ya ushuru wa huduma 'Service Levy'
Muonekano hundi zenye thamani ya shilingi Bilioni 2.387 kwa Manispaa ya Kahama na Halmashauri ya wilaya ya Msalala zilizotolewa na Migodi ya Buzwagi na Bulyanhulu ikiwa ni malipo ya ushuru wa huduma 'Service Levy'
Muonekano wa Hundi ya shilingi 744,929,725.78/= ambazo zimetolewa na Mgodi wa Bulyanhulu kama ushuru wa malipo ya ushuru kwa ajili ya maendeleo.
Muonekano wa hundi ya shilingi 1,642,815,335.45/= iliyotolewa na mgodi wa Buzwagi kwa Manispaa ya Kahamaambazo ni malipo ya ushuru kwa ajili ya maendeleo.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Diamond aibuka na sakata mtoto wake kupewa mwanaume mwingine

Dar es Salaam. Wakati sakata la yupi baba mzazi wa msanii wa muziki, Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz likiwa bado vichwani mwa watu, msanii huyo ameibuka na kufunguka kuwa hata yeye ana mtoto ambaye mzazi mwenzie amegoma kumpatia na huenda ameshapewa baba mwingine.


Diamond alisema hayo kupitia mahojiano aliyoyafanya na kipindi cha The Switch cha Wasafi FM, Januari 28 baada ya kuulizwa anadhani ana watoto wangapi.


Akijibu, Diamond alisema anachojua ana watoto sita, tofauti na watu wengi wanavyofahamu kwamba ana watoto wanne ambao ni Tiffah na Nillan aliozaa na Zarina Hassan "Zari", Dylan aliyezaa na mwanamitindo Hamisa Mobetto na Naseeb Junior aliyezaa na mwimbaji kutoka Kenya, Tanasha Donna.


"Watu wengi wanafahamu mtoto wangu wa kwanza ni Tiffah, lakini ninao wengine wawili ambao walizaliwa kabla yake. Kuna mmoja yuko Mwanza, mama yake amegoma kunipa, pia juzi kati nimeletewa mtoto mwingine wa kike hapa hapa Dar es Salaam, lakini sijawahi kumuona.


"Mama wa huyo mtoto yuko katika mahusiano mengine na mwenye mahusiano naye anajua ni mwanae. Mambo yale...kwa hiyo yule mama anaogopa kuniletea mtoto kwa sababu akikutana na mimi mtoto ataenda kusema kwa baba yake tumeenda kwa Diamond. Kwa hiyo mtoto yupo, inatafutwa timing siku moja kumuona, lakini mama yangu amemuona na akaniambia, mwanangu, yule mtoto ni wako, mmefanana sana," alisema mkali huyo wa wimbo "Waah".


Alisema ikiwa watoto hao wawili ni wa kweli, Tiffah atakuwa mtoto wa tatu kwa kuzaliwa.



Sakata la nani baba mzazi wa msanii huyo lilipoanza kuvuma mapema mwezi huu, mama mzazi wa Diamond aliweka bayana baba wa msanii huyo ni mzee anayefahamika kwa jina la Salum Iddi Nyange na sio Abdul Juma kama ilivyokuwa inafahamika awali.


Jambo hilo liliibua mjadala kwa mashabiki na wafuatiliaji wa matukio ya kuvutia ya familia hiyo ikiwemo huenda hakukuwa na uhusiano mzuri kati ya mama Diamond na baba mzazi wa msanii huyo ndiyo maana akamkabidhi mtoto kwa baba mwingine ambaye ndiye huyu mzee Abdul.


Hii inamaanisha matukio yanajirudia ukilinganisha na hiki kinachotokea sasa kwa Diamond kutopewa mtoto wake ambaye anadai yupo Dar es Salaam.


Diamond alifafanua kuwa "Mama akiniambia kitu huwa hadanganyi kwa sababu macho yake ni kama teknolojia inayotumika viwanjani kuhakiki usahihi wa mpira ulipo (VAR), alipomuona aliniambia ni wangu, nasubiri nimuone," alisema.


Diamond pia alielezea kuhusu sakata la nani baba yake halisi kwa kusema kuwa "Nimefahamu kuwa mzee Abdul siyo baba yangu tangu mwaka 2000, alienieleza ukweli alikuwa mama yangu mkubwa (mama yake Rommy Jones).


"Nilikuwa napenda sana kumtajataja baba yangu, kipindi hicho alikuwa ameshaondoka nyumbani, ametuacha Tandale. Sasa ilikuwa inawaudhi watu akiwemo mama mkubwa kwa sababu alikuwa hatuhudumii wakati alikuwa vizuri kiuchumi. Enzi hizo alikuwa na magari na pesa za kutosha."


Hilo siku moja lilimkera mama yangu mkubwa na ndipo kwa hasira akamueleza ukweli kuwa baba yake mzazi sio Abdul anayemtajataja kila kukicha, bali ni mtu mwingine anayeitwa Salum Iddi au Salum Bubu kwa jina la utani.


"Ndipo akaniambia kama unakata kuthibitisha nenda pale Tandale sokoni wanapouza mchele wa jumla. Kamuulize mtu anayeitwa Salum Bubu, halafu mwambie mimi mwanao." alisema.


Diamond alisimulia kwamba alienda huko na kweli akakutana na baba yake.


"Baba akanipa mchele na shilingi mia mbili. Nikapeleka mchele nyumbani mia mbili nikatumia. Na tangu hapo huo ndiyo ukawa mchezo wangu. Nikawa naenda kazini kwa baba mara kwa mara." Alisema ile kwenda mara kwa mara kwake ikarudisha ukaribu wa mama yake na Salim Nyange na baadaye mzee huyo akampeleka Diamond nyumbani kwake Kariakoo alipokuwa akiishi kwenda kumkutanisha na ndugu zake.


Diamond alifafanua kuwa hata shughuli zake za muziki alianza akiwa Kariakoo alipokuwa akienda na kuishi mara kwa mara kwa baba yake.

WAZIRI MKUU WA DRC AJIUZULU

Sylvestre Ilunga Ilunkamba amejiuzulu rasmi kama waziri mkuu wa Jamuhuri ya kidemokrasi ya Congo, na kuwasilisha barua yake kwa Rais Félix Tshisekedi.

Bw Ilunga, ambaye ni mshirika mkuu wa mtangulizi wa Rais Tshisekedi, Joseph Kabila, ameongoza baraza la mawaziri la serikali ya Muungano kwa miezi 15.

Hata hivyo wabunge walipitisha kura ya kutokuwa na Imani na serikali yake Jumatano wiki hii na akapewa saa 24 awe amejiuzulu.

Kujiuzulu kwake kunatoa fursa kwa Rais Tshisekedi ya kuwateua washirika wake kama mawaziri.

Hadi sasa, utendaji wa Bw Tshisekedi umekuwa ukidhibitiwa na, muungano alionao na Bw Kabila ambao uliafikiwa wakati alipoingia madarakani miaka miwili iliyopita.

Ushindi wake katika uchaguzi mwezi Disemba 2018 ulisifiwa kama wa kihistoria-ambapo kulikuwa na makabidhiano ya kwanza ya utawala kwa njia ya amani ambayo hayakuwahi kushuhudiwa katika historia ya miongo sita nchini humo.

Bw Tshisekedi bado hajamchagua waziri mkuu mpya,ambaye ataunda serikali ijayo.

 CHANZO - BBC SWAHILI

NI MTAFITI NA MGUNDUZI WA TIBA ASILI YENYE KUTIBU MAGONJWA SUGU NA MWENYE OFU YA MUNGU ANATOBU NA KUPONA KABISA UNABAKI NA ISTORIA

 


DOCTOR MBOJE,


NI MTAFITI NA MGUNDUZI WA TIBA ASILI YENYE KUTIBU MAGONJWA SUGU NA MWENYE OFU YA MUNGU ANATOBU NA KUPONA KABISA UNABAKI NA ISTORIA


MAGONJWA NINAYO TIBU NI 


A,_KISUKARI na tibu kwa miti shamba  kunywa na kupona kabisa


B,_TEZI DUME_natibu kwa miti  kunywa na kupona kabisa bila kufanyiwa upasuaji


C,_NGUVU ZA KIUME 

  Kwa wale wenye upungufu wa nguvu za kiume na wasio kua nazo kabisa natibu kwa miti shamba na kupona kabisa


D,_kutibu magonjwa mbalimbali Kama uzazi) (miguu kuvimba na kuwaka Moto) (Tumbo kujaa gesi na kupata choo ngumu) (mgongo,   kiuno)


MHERA JIGURHU ni dawa ya miti shamba inatibu kisukari na kupona kabisa kwa mda wa siku 16 

Sukari iwe kubwa kabisa lakini iwe normal 5.1  


NNKOROBHIJE ,ni dawa ya miti shamba inayotibu  TEZI DUME bila kufanyiwa operation na kupona kabisa kwa siku 14 na kibaki history 


NHUNGHU MAPANDO Kwa wale wenye upungufu wa nguvu za kiume na wasio kua nazo kabisa au kama unahisi kupungukiwa tumia nhunghu mapando ni dawa inatibu na kupona kabisa tatizo kwa mda wa siku 4 tu


 NTURURU ni dawa ya miti shamba inayotibu uzazi chango kwa wakina mama wasio kua na watoto inatibu na kumaliza tatizo kabisa na mfumo wako wa Heath Kama umevulugika inatibu kwa mda wa siku 18


MWICHE,ni dawa ya miti shamba inayotibu Tumbo kujaa gesi na kupata choo ngumu kurunguia kiuno kuuma mgongo na kupona kabisa kwa mda wa siku 7


PIIA UNAWEZA KUNIPATA KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA 

CALL AND WHAT SAAP

+255744922982

+255737585753 


HUDUMA ZANGU ZINAPATIKANA DUNIA NZIMA KWA OFISI NI DAR ES SALAAM NA MOROGORO KWA ULIE MBALI DAWA NAKUSAFIRISHIA MPAKA INAKUFIKIA KWA WALE WA DAR NA MOROGORO KAMA HUWEZI KUFIKA OFISINI NAKUAGIZIA DAWA INAKUFIKIA MPAKA ULIPO

Zijue athari za kuvaa viatu virefu wakati wa ujauzito

 

Kipindi cha ujauzito ni wakati wa kubadili mambo mengi katika mfumo wa maisha wa mjamzito. Moja ya mambo makubwa ni pamoja na tabia ya kuvaa viatu vyenye visigino virefu. Mjamzito hashauriwi kuvaa viatu vyenye visigino virefu kutokana na athari zinazoweza kutokana na aina hizi za viatu.

Zifuatazo ni athari za kuvaa viatu vyenye visigino virefu wakati wa ujauzito:

Maumivu ya misuli ya mapaja.
Wadada hupenda kuvaa "high heels" husababisha misuli ya mapaja kukaza na kuwa na muonekano mzuri. Katika ujauzito, mabadiliko ya homoni huweza kupelekea misuli hii kuwa na maumivu tofauti na ilivyokua kabla ya ujauzito.

Maumivu ya mgongo.
Wakati wa ujauzito, uzito mkubwa huhamia mbele na misuli ya nyonga hulegea. Mabadiliko haya ya kimsawazo huweza kusababisha maumivu ya sehemu ya chini ya mgongo na kiuno.

Hatari ya kuanguka.
Ni wazi kuwa uzito huongezeka wakati wa ujauzito na mabadiliko ya vichocheo vya mwili huweza kupelekea kizunguzungu cha hapa na pale. Hii huongeza hatari ya kuanguka iwapo utavaa "high heels" na kupelekea majeraha kwako na kwa mtoto aliyeko tumboni.

Uvimbe miguuni.
Ni jambo la kawaida miguu kuvimba wakati wa ujauzito. Kuvaa viatu vyenye visigino virefu na vyenye kubana huweza kuongeza tatizo hilo na kupelekea maumivu.

Mimba kutoka.
Mjamzito akivaa viatu vyenye visigino virefu anakua katika hatari kubwa ya kuanguka. Hii huweza kusababisha majeraha makubwa kwa mtoto aliyeko tumboni hali inayoweza kusababisha mimba kutoka.

Lakini, iwapo kuna ulazima sana wa kuvaa viatu hivyo, unapaswa kuzingatia yafuatayo:
Ni salama kuvaa viatu hivi katika muhula wa kwanza wa ujauzito (Miezi mitatu ya mwanzo).
Viatu visiwe virefu sana na visigino viwe imara.
Vaa viatu visivyo na bugdha na usivikaze sana.
Epuka visigino vyembamba sana.
Usivae siku nzima. Vitoe mara kwa mara kupumzisha miguu.
Epuka kutembea au kusimama muda mrefu ukiwa umevivaa.
Ukihisi maumivu kwenye misuli ya mapaja jaribu kufanya mazoezi ya kujinyoosha na kujikanda.

Faida za limao au ndimu kilishe na afya

 


Zifuatazo ndizo faida zitokanazo na utumiaji wa limao na ndimu kilishe na kiafya;
Kusaidia uwiano sahihi wa pH ya mwili kuuwezesha kufanya shughuli mbalimbali.

Ina vitamin C na kemikali mimea ambayo husaidia kutibu mafua na mfumo wa upumuaji. Pia kuboresha afya ya ngozi, fizi (kuzuia fizi kutoka damu, ukavu wa ngozi ikiwemo kuchanika midomi na pua kavu), moyo, figo, misuli, maini na ubongo kwa kupambana na sumu mbalimbali mwilini. Pia husaidia kukata uchovu wa mazoezi au marathon.

Husaidia mfumo wa mmeng'enyo wa chakula, kunywa sharubati yenye mchanganyiko wa limao au ndimu, au bilauli ya maji ya limao au ndimu nusu saa kabla ya kula.

Pia tindikali zilizonazo husaidia kuzuia au kupambana na vijiwe vya figo, gout (mlundiknoi wa uric acid kwenye viungo na mwili). Husaidia kufyonzwa na kubadilisha madini ya chuma kwenye vyakula jamii ya mimea na kufanya iweze kutumika kutengeneza damu (ferrous iron).

Ganda la limao pia lina virutubisho, kemikali mimea na mafuta kwa wingi. Ganda lake au mafuta husaidia kutibu mafua, kuchua misuli au hutumika kwenye vinywaji kuleta ladha au kama tiba mvuke kwa magonjwa ya msongo wa mawazo, au magonjwa ya mifumo ya fahamu.

Matumizi ya mara kwa mara Husaidia kupambana na kisukari, shinikizo la damu (kutokana na wingi wa potassium) na ulemavu wa macho.

Matumizi ya kila siku kwa muda mrefu Husaidia kuzuia saratani mbalimbali mwilini.
Husaidia mchakato wa kuzalisha nguvu mwilini.

 Mambo muhimu ya kuzingatia.
Inashauriwa kuongeza limao/ndimu kwenye mboga za majani kama tembele na chai ili kusaidia ufyonzwaji na utumiwaji wa madini ya chuma mwilini toka kwenye mboga hizo.

Faida hizi pia zafanana na jamii zote za malimao yakiwemo machungwa, madalansi, machenza nk japo baadhi ya faida zinaweza kuwa kwa wingi au kidogo kwa kila tunda

Inashauriwa kutumia moja ya matunda hayo kila siku ili kuboresha lishe na afya zetu.

Angalizo
Wapo wanaotumia limao kuondoa kichefuchefu au kuzuia kutapika, ila limao halizuii kutapika, bali inapelekea kutapika kutokana na uchachu wake. Hivyo waweza tumia parachichi au tunda baridi (lisilo chachu) kuzuia kutapika.

Friday, January 29, 2021

RC Mbeya aunda tume kuchunguza kifo cha dereva



MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila ameunda tume ndogo ya watu wanne na kuipa jukumu la kuchunguza kifo cha dereva wa Lori aliyefahamika kwa jina la Abdulhman Issa anayedaiwa kufia mikononi mwa polisi katika eneo la Shamwengo wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.



Chalamila amefikia hatua hiyo  baada ya kuwepo kwa taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikiwaonyesha askari polisi wakimshusha kwenye gari dereva huyo na hatimaye kubainika amefariki na mwili wake kuhifadhiwa katika hospitali ya Igawilo jijini Mbeya.


Akizungumza na wanahabari hii leo Chalamila amesema Tume aliyoiunda itampa majibu ndani ya siku tatu kuanzia leo na endapo itabinika kuwa dereva huyo amefia kwenye mikono ya vyombo vya dola wahusika watawajibishwa kwa mujibu wa sheria.


Tukio hilo limetokea January 27 mwaka huu majira ya saa 12 jioni huku mkuu wa mkoa wa Mkoa akizuia mwili wa marehemu kuzikwa hadi atakapopewa ripoti ya tume aliyoiunda.

Mkuu wa Usalama bara barani aipongeza TANROADS Manyara kwa kuweka alama Maeneo hatarishi

 Na John Walter Manyara

Kamishna msaidizi Mwandamizi wa jeshi la Polisi ambaye pia ni Mkuu wa  Usalama bara barani nchini Tanzania Wilbroad Mutafungwa,  amepongeza wakala wa bara bara mkoa wa Manyara (TANRODS) kwa kazi kubwa walioifanya ya kuweka alama zote zinazohitajika katika maeneo hatarishi ya bara bara.


Amesema kuwepo kwa alama hizo kunasaidia kutoa ishara kwa madereva na watembea kwa miguu pindi wawapo bara barani na kupunguza ajali.


Mutafungwa ameyazungumza hayo wakati  akizungumza na kituo hiki  akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Manyara na kanda ya kaskazini kwa ujumla.


"Kama mnavyofahamu bara bara hizi za mkoa wa Manyara zina Mlima, Kona kali na miteremko, tumepita kuona namna ambavyo magari yanatembea na madereva wanavyozingatia sheria za usalama bara barani" alisema Mutafungwa.


"Kusema kweli nichukue nafasi hii kuwapongeza wenzetu wa Tanroads ambao wamefanya kazi kubwa kuhakikisha kwamba wameweka alama kwenye maeneo yote ambayo ni hatarishi katika bara bara za mkoa huu" alisema Mutafungwa.


Amesema katika ukaguzi wao walifika katika eneo hatarishi lenye kona kali lijulikanalo kama  Logia katika bara bara ya  Babati Singida ambapo wamejionea madereva wakizingatia sheria kwa kufuata alama zilizowekwa na Tanroads.


Museveni akataa maridhiano na wapinzani

 


Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amewaonya watu wenye lengo la kumpatanisha na wapinzani baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu uliompa ushindi na kuongoza muhula wa sita.


Upande wa upinzani unaoongozwa na msanii Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine aliyeshika nafasi ya pili, unapinga vikali kuyatambua matokeo hayo.


Kauli hiyo ya Museveni imekuja baada ya kuibuka wasiwasi kwa Taifa na baadhi ya viongozi wa dini kuomba maridhiano kwa Serikali na upinzani na kumuachia Bobi Wine aliyekuwa amezuiliwa nyumbani kwake.


Rais Museveni aliwajibu akisema Serikali ya NRM tayari ilianza maridhiano miaka mingi iliyopita ndiyo sababu katika Serikali yake kuna mtoto wa aliyekuwa Rais wa Uganda, Idi Amin, mtoto wa Rais wa zamani, Tito Lutwa Okello na wengine wengi.


Kiongozi wa chama cha NUP, Bobi Wine alipokutana na wabunge wake wateule kwa mara ya kwanza, aliwataka wapinge matokeo ya uchaguzi mkuu.

Picha : THUBUTU AFRICA YATAMBULISHA MRADI WA 'UTU WA MSICHANA' KUJENGA CHOO CHA KISASA SHULE YA WANAFUNZI NA WALIMU WANACHANGIA CHOO KIMOJA

Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives, Jonathan Manyama akisaini Mkataba wa kazi ya ujenzi wa choo cha shule ya msingi Mwamagunguli 'A' iliyopo katika kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga itakayofanywa na fundi ujenzi Robert Kayange mkazi wa kijiji cha Galamba kata ya Kolandoto.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Shirika la Thubutu Africa Initiaves (TAI) limetambulisha mradi wa 'Utu wa Msichana' wenye lengo la kujenga choo cha kisasa chenye matundu 8 na sehemu ya kujistiri kwa wanafunzi wa kike katika shule ya Msingi Mwamangunguli 'A' iliyopo katika kijiji cha Mwamagunguli kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.

Ujenzi huo wa vyoo kwa ajili ya wanafunzi wa kike ni sehemu ya utatuzi wa changamoto iliyopo katika shule ya Msingi Mwamagunguli 'A' yenye jumla ya wanafunzi 400 ambapo kati yao wasichana ni 200 ambao wamekuwa wakilazimika kutumia tundu moja la choo na wavulana 200 wakitumia matundu mawili na walimu katika tundu moja ndani ya choo kimoja.

Uzinduzi na utambulisho huo wa mradi wa 'Utu wa Msichana' ambao umeenda sanjari na kuanzisha rasmi ujenzi wa choo cha kisasa umefanyika leo Ijumaa Januari 29,2021 katika shule hiyo.

Akitambulisha mradi wa 'Utu wa Msichana', Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives, Jonathan Manyama amesema tayari ujenzi wa choo cha kisasa katika shule ya Mwamagunguli "A" umeanza ambapo tayari shimo la choo limechimbwa, matofali yameshafyatuliwa na shirika hilo limesaini mkataba na Fundi Ujenzi Robert Kayange kwa ajili ya kazi ya ujenzi.

"Mradi huu wa ujenzi wa choo cha kisasa katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A' unaotekelezwa na shirika la Thubutu Africa Initiaves, unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi mitatu kuanzia Januari ukigharimu shilingi milioni 16.5 ambazo tumefadhiliwa na Balozi wa Marekani nchini Tanzania",ameeleza Manyama.

"Tulipata kilio cha changamoto ya vyoo katika shule hii ofisini kwetu kupitia kwa Moses Mshagatila aliyesoma katika shule hii akituomba tusaidie ujenzi wa vyoo kwani hali ni mbaya katika shule hii nasi tukaanza kutafuta mdau wa kutushika mkono ndiyo tukampata Balozi wa Marekani nchini akakubali kutusaidia",ameongeza.

Akielezea kuhusu sifa za choo cha kisasa chenye vigae wanachojenga, amesema kitakuwa na matundu 8 ya vyoo kwa ajili ya wanafunzi wa kike,chumba maalum cha kujistri watoto kike,choo maalumu kwa watu wenye ulemavu,sehemu ya kunawia mikono,masinki yenye koki na tanki kwa ajili ya maji ya dharura.

Manyama amesema tayari shirika hilo limepeleka matofali 1,500,mifuko 120 ya saruji na litaendelea kupeleka mahitaji mengine kwa ajili ya ujenzi wa choo na kwa upande wa wananchi watashiriki kwa kuongeza nguvu kazi ikiwemo kupeleka maji.

Amefafanua kuwa lengo la shirika lake ni kuhakikisha linaunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha mazingira shuleni.

Manyama ametumia fursa hiyo kuwasihi wananchi ,wanafunzi na walimu kutunza miundo mbinu ya choo hicho cha kisasa ili idumu kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji wa kata ya Kolandoto, Mwakaluba Wilson alilishukuru shirika la Thubutu Afric Initiatives kwa msaada huo wa choo huku akiwaomba wadau wengine kusaidia kutatua changamoto zingine zilizopo katika shule hiyo.

Mwenyekiti wa kijiji cha Mwamagunguli Makoye Shindayi ameahidi kusimamia kikamilifu ujenzi wa choo hicho huku akimpongeza Kijana Moses Mshagatila kwa kutoa kilio cha changamoto ya vyoo kwa shirika la Thubutu Africa Initiatives ambalo bila kusita limejitokeza kusaidia ujenzi huo.

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mwamagunguli 'A' Adam Mbega amesema kujengwa kwa choo hicho kutapunguza adha ya wanafunzi kutumia muda mrefu kupanga foleni kwenda kujisaidia wakati wa mapumziko lakini pia kuwaondoa katika hatari ya kupata magonjwa kutokana na kutumia choo kimoja kujisaidia.

"Shule hii iliyopata usajili mwaka 1993 ina walimu 7, wanafunzi 400. Tunatumia choo kimoja walimu na wanafunzi kwani tuna choo kimoja chenye matundu manne, mawili wanatumia wavulana 200, tundu moja wanatumia wanafunzi wa kike 200 na tundu moja tunatumia walimu. Kawaida tundu moja la choo linapaswa kutumiwa na wanafunzi 20 wa kike na kwa upande wa wavulana 25 kwa tundu moja",ameeleza Mwalimu Mbega.

Naye aliyekuwa mwanafunzi wa shule hiyo, Moses Mshagatila aliyeanza kusoma darasa la kwanza mwaka 1999 wakitumia choo cha mabua na mwaka 2000 kikajengwa choo chenye matundu manne kinachotumika sasa, amelishukuru shirika la Thubutu Africa Initiatives kwa kuanzisha ujenzi wa choo cha kisasa katika shule hiyo ambapo ndoto yake kubwa ilikuwa ni kuona wanafunzi wanasoma katika mazingira rafiki ndiyo maana akaamua kupiga hodi katika shirika hilo ili lisaidie.

Nao wanafunzi wa shule hiyo wameeleza kufurahishwa na ujio wa choo cha kisasa wakibainisha kuwa wakati mwingine wanachelewa kuingia darasani baada ya kipindi cha mapumziko kutokana na foleni kubwa lakini pia afya zao zinakuwa hatarini kutokana na kutumia choo kimoja tu.
Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives, Jonathan Manyama (aliyesimama) akitambulisha Mradi wa 'Utu wa Msichana' leo Januari 29,2021 katika shule ya Msingi Mwamagunguli 'A' iliyopo katika kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga. Mradi huo una lengo la kujenga choo cha kisasa  katika shule hiyo.  Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives, Jonathan Manyama (aliyesimama) akitambulisha Mradi wa 'Utu wa Msichana' leo Januari 29,2021 katika shule ya Msingi Mwamagunguli 'A' iliyopo katika kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives, Jonathan Manyama (aliyesimama) akitambulisha Mradi wa 'Utu wa Msichana' leo Januari 29,2021 katika shule ya Msingi Mwamagunguli 'A' iliyopo katika kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives, Jonathan Manyama akisaini Mkataba wa kazi ya ujenzi wa choo cha shule ya msingi Mwamagunguli 'A' iliyopo katika kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga itakayofanywa na fundi ujenzi Robert Kayange mkazi wa kijiji cha Galamba kata ya Kolandoto ( wa kwanza kushoto). Wa pili kushoto ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Kolandoto Mwakaluba Wilson akishuhudia zoezi la kusaini mkataba wa ujenzi. 
Robert Kayange mkazi wa kijiji cha Galamba kata ya Kolandoto akisaini Mkataba wa kazi ya ujenzi wa choo cha shule ya msingi Mwamagunguli 'A' iliyopo katika kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mwamagunguli, Makoye Shindayi akisaini Mkataba wa kazi ya ujenzi wa choo cha shule ya msingi Mwamagunguli 'A' iliyopo katika kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga itakayofanywa na fundi ujenzi Robert Kayange mkazi wa kijiji cha Galamba kata ya Kolandoto.
Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives, Jonathan Manyama akimkabidhi Mkataba wa kazi ya ujenzi wa choo cha shule ya msingi Mwamagunguli 'A' iliyopo katika kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga fundi ujenzi Robert Kayange (kushoto).
Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives, Jonathan Manyama akimkabidhi Mkataba wa kazi ya ujenzi wa choo cha shule ya msingi Mwamagunguli 'A' iliyopo katika kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga fundi ujenzi Robert Kayange mkazi wa kijiji cha Galamba kata ya Kolandoto.
Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives, Jonathan Manyama (katikati) akiangalia shimo la choo lililochimbwa na wananchi kwa ajili ya ujenzi wa choo cha kisasa kwa wanafunzi wa kike katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A' kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Muonekano wa choo chenye matundu manne kinachotumiwa na walimu na wanafunzi katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A' kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga. Kulia ni sehemu inayotumiwa na wanafunzi wa kike 200, kushoto ni choo kinachotumiwa na walimu.
Muonekano wa choo chenye matundu manne kinachotumiwa na walimu na wanafunzi katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A' na eneo panapojengwa choo kipya cha kisasa na Shirika la Thubutu Africa Initiatives.
Shughuli ya kusafisha eneo la ujenzi wa choo cha kisasa katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A' ikiendelea.
Shughuli ya kusafisha eneo la ujenzi wa choo cha kisasa katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A' ikiendelea.
Mchanga ukiwa eneo la ujenzi wa choo cha kisasa katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A'.
Shughuli ya kuleta matofali eneo la ujenzi wa choo cha kisasa katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A' ikiendelea.
Muoenekano wa sehemu ya matofali
Shughuli ya kusoma matofali eneo la ujenzi wa choo cha kisasa katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A' ikiendelea.
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mwamagunguli 'A' Adam Mbega akizungumza ambapo amesema kujengwa kwa choo hicho kutapunguza adha ya wanafunzi kutumia muda mrefu kupanga foleni kwenda kujisaidia wakati wa mapumziko lakini pia kuwaondoa katika hatari ya kupata magonjwa kutokana na kutumia choo kimoja kujisaidia.
Afisa Mtendaji wa kata ya Kolandoto, Mwakaluba Wilson akilishukuru shirika la Thubutu Afric Initiatives kwa msaada wa ujenzi wa choo katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A' huku akiwaomba wadau wengine kusaidia kutatua changamoto zingine zilizopo katika shule hiyo.
Diwani wa kata ya Kolandoto, Musa Elias akilishukuru shirika la Thubutu Afric Initiatives kwa msaada wa ujenzi wa choo katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A'.
Afisa Mtendaji wa kijiji cha Mwamagunguli, Godfrey Majija akizungumza wakati Shirika la Thubutu Africa Initiatives likitambulisha mradi wa Utu wa Msichana katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A' iliyopo katika kijiji hicho kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti  wa kijiji cha Mwamagunguli Makoye Shindayi akizungumza wakati Shirika la Thubutu Africa Initiatives likitambulisha mradi wa Utu wa Msichana katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A' iliyopo katika kijiji hicho kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti  wa kijiji cha Mwamagunguli Makoye Shindayi akimpongeza Moses Mshagatila (kulia) kwa kupeleka kilio cha changamoto ya vyoo katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A' na kuamua kuanzisha ujenzi wa choo cha kisasa.
Aliyekuwa mwafunzi wa shule ya msingi Mwamagunguli 'A' Moses Mshagatila mkazi wa kijiji cha Mwamagunguli, akizungumza wakati Shirika la Thubutu Africa Initiatives likitambulisha mradi wa Utu wa Msichana katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A' iliyopo katika kijiji hicho kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Sehemu ya wanafunzi wa kike wakifuatilia matukio wakati Shirika la Thubutu Africa Initiatives likitambulisha mradi wa Utu wa Msichana katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A' iliyopo katika kijiji hicho kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Sehemu ya wananchi wakifuatilia matukio wakati Shirika la Thubutu Africa Initiatives likitambulisha mradi wa Utu wa Msichana katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A' iliyopo katika kijiji hicho kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.
Sehemu ya wananchi wakifuatilia matukio wakati Shirika la Thubutu Africa Initiatives likitambulisha mradi wa Utu wa Msichana katika shule ya msingi Mwamagunguli 'A' iliyopo katika kijiji hicho kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...