Thursday, December 27, 2018

Makosa yanayofanywa na wajasiriamali wengi

Wajasiriamali wengi wamekuwa wanafanaya makosa Fulani fualani yanayowafanya washindwe kusonga mbele katika sula la kupata mafanaikio. Baadhi ya makosa hayo ni pamoja na;

Kupuuza maoni ya wateja
"Mteja ni mfalme"; je unalifahamu hili? Wajasiriamali wengi hupuuzia maoni ya wateja bila kujua kuwa maoni ya wateja ndiyo huwawezesha kujirekebisha na kuweza kuwapa wateja wao kile wanachokihitaji. Kosa hili lisiposhughulikiwa litakupotezea kiasi kikubwa cha wateja na kuleta matokeo mabaya kwenye biashara au mradi wako.

Kuacha fursa zipite
Wajasiriamali wengi hupenda kungojea mazingira yawe mazuri bila hata kujali fursa zinazopotea. Ni dhahiri kuwa hakuna mtu atakaye kutengenezea mazingira unayotaka; ukiona fursa itumie na mambo yatakaa vyema mbele ya safari. Inawezekana fursa unayoiona leo kesho isiwepo tena.

Kukataa ushauri wa kitaalamu
Kila kitu kizuri kinahitaji maarifa stahiki ili kiweze kutokea. Ni dhahiri kuwa wajasiriamali wengi wanafanya kosa la kupuuza ushauri wa kitaalamu katika kazi zao kwa kuona kuwa hauna nafasi. Kwa mfano kama unafuga kuku au unalima mazao fulani kwanini usimwite mtaalamu wa kilimo au mifugo ili akushauri? Ni dhahiri kuwa ukipata ushauri wa kitaalamu utakuwa mwenye tija zaidi.

Kutokwenda na soko linavyotaka
Mjasiriamali mzuri ni yule anayefahamu kuwa kwa sasa soko linataka nini. Ni lazima uweze kuepuka kosa la kutokutazama mahitaji ya soko, ili uhakikishe mauzo ya bidhaa au huduma yako hayaathiriki. Kwa mfano zamani watu walinunua zaidi kuku walio hai, lakini leo soko la kuku waliochinjwa ni kubwa pia; kwanini wewe bado unauza tu kuku walio hai? Ni dhahiri ukitazama mfano huu utaona jinsi kosa hili linavyowaathiri wajasiriamali wengi katika maeneo mbalimbali.

Kushindwa kubaini wateja lengwa
Ni lazima wewe kama mjasiriamali uwabaini wateja wako ili huduma au bidhaa yako iuzike. Kwa mfano umetengeneza dawa ya kuua mbu, kisha unaiuza mikoa ya baridi badala ya mikoa yenye joto (kwenye mbu wengi); ni dhahiri kuwa hutoweza kupata wateja wa bidhaa yako sawa sawa. Chukua hatua leo watafute na uwafuate wateja sahihi wa huduma au mradi unaoufanya.

Mbinu duni za masoko
Maswala ya masoko ni taaluma kamili ambayo watu hujifunza katika shule na vyuo mbalimbali. Hivyo ni muhimu wewe kama mjasiriamali kutokupuuzia taaluma hii kwani ndiyo itakayokuwezesha kubaini njia bora na sahihi za kuuza huduma au bidhaa yako. Hakikisha mbinu za masoko unazifahamu vyema tena zinaendana na soko husika la bidhaa yako. Hakikisha pia mbinu zako zinabadilika kulingana na mazingira na hali ya soko.

Maarifa sahihi ni msingi wa kufanya vitu kwa ubora. Ni dhahiri kuwa makosa mengi yaliyoelezwa hapa yanatokana na ukosefu wa maarifa stahiki ya ujasiriamali. Nakushauri ujifunze kila siku ili kupanua uwezo na uzoefu wako wa kiujasiriamali. Pia usisahau kuweka kwenye matendo yale yote unayojifunza.

Tuesday, December 25, 2018

Good News : Pakua Upya App ya Malunde 1 blog ...Imeboreshwa Kukupa Raha zaidi ...Bonyeza HAPA SASA

Kuwa wa Kwanza kupata habari na matukio yanayojiri Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kupakua/ kudownload App ya Malunde 1 blog tukuhabarishe masaa 24.

Tembea na dunia kiganjani mwako sasa.

Pakua App mpya ya Malunde 1 blog imeboreshwa zaidi ili kukidhi mahitaji ya wasomaji wetu. Hii ndiyo mpya kabisa,ina alama hii ↡↡
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Ni rahisi sana : Ingia Play store kisha Andika Malunde 1 blog halafu bonyeza Install

https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog

NB: App uliyokuwa unatumia mwanzo tumeifuta na kuleta mpya ya kisasa zaidi..Tafadhali fuata maelekezo hapo juu... Usikubali kukosa habari kizembe..Pakua app yetu Mpya ya Malunde1 blog Sasa

Monday, December 24, 2018

MBUNGE WA CHADEMA APATA AJALI YA GARI..KUNA TAARIFA YA VIFO



Mbunge wa Viti Maalum, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kunti Yusuf Majala, amejeruhiwa vibaya baada ya gari alilokuwa akisafiria kupata ajali. Anaripoti Yusuph Katimba.

Ajali hiyo imetokea leo Jumatatu, tarehe 24 Desemba, maeneo ya Kilema, katikati ya wilaya za Chemba na Kondoa.

Taarifa zilizothibitishwa na ofisa mmoja wa Bunge mjini Dodoma, ambaye hata hivyo, hakupenda kutajwa jina lake, zinaeleza kuwa katika ajali hiyo, watu wengine wanne wamefariki dunia.

Afisa huyo ambaye anasema siyo msemaji wa Bunge, anaeleza kuwa gari ambalo mbunge alikuwa akilitumia lilianguka baada ya kuchomoka tairi la mbele mkono wa kushoto wa dereva.

Anasema, "gari hili lilikuwa na watu 11 (kumi na moja), watoto saba na wakubwa wanne. Mhe. Kunti ana maumivu makali sana ya kiuno na shingo."

Anasema, kufuatia hali ya mbunge huyo kuwa mbaya, ofisi ya Spika, imeanza kufanya utaratibu wa haraka wa kuhakikisha mara atakapofikishwa kwenye hospitali ya mkoa wa Dodoma, aweze kusafirishwa yeye na majeruhi wengine, kupelekwa jijini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi."

Hata hivyo, afisa huyo hakuweza kuwafahamu mara moja majina ya wale waliofariki dunia; na au kujeruhiwa. Bali, taarifa kutoka maofisa wa Chadema zinasema, baadhi yao waliofariki, sehemu kubwa watakuwa familia ya mbunge huyo.

Kwa mashuhuda, gari lililokuwa limembeba Kunti na ambalo limepata ajali, lilikuwa na namba za usajili, T 624 DPE. Lilikuwa likitokea Dodoma mjini kuelekea Kondoa.

Dereva wa gari hilo alikuwa ni Stephano Masawe, ambaye ni dereva wa Katibu wa Chadema, Kanda ya Kati.

Chanzo - Mwanahalisi online

Yanga Wakifikisha Nusu ya Mashabiki Tuliokua Nao Jana Najiuzulu Nafasi Yangu- Haji Manara

Yanga Wakifikisha Nusu ya Mashabiki Tuliokua Nao Jana Najiuzulu Nafasi Yangu- Haji Manara
Afisa Habari wa Simba SC, Haji Manara ameendelea na majigambo yake hasa kwa watani wake Yanga, ambapo amesema kuwa endapo watani zake wa jadi Yanga katika mchezo wake na Tukuyu Stars leo, wakifikisha nusu ya mashabiki waliohudhuria kwenye mchezo wao dhidi ya Nkana FC, yuko yatari kujiuzulua nafasie ya usemaji, ndani ya klabu.

Manara amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameandika kuwa Simba haiwezi kufananishwa na timu zingine Tanzania wakiwemo watani wake, Yanga.

"Yanga leo wanacheza na Tukuyu Stars, wakijaza asilimia kumi kama jana najiuzulu usemaji wa Simba, halafu yupo mswahili anaweza kuthubutu kunifananisha De la boss na wasemaji wengine?", ameandika Manara.

Yanga inacheza na Tukuyu stars katika dimba la taifa, jijini Dar es salaam katika michuano ya shirikisho (AFC), huku watani wao Simba wakiwa  wamefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Klabu Bingwa Afrika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 15, wakiichapa Nkana FC ya Zambia.



Friday, December 21, 2018

SAED KUBENEA : SINA MPANGO WA KUHAMIA CCM..MAKONDA ATAONDOKA KWA AIBU

Mbunge wa Ubungo (CHADEMA) Saed Kubenea amesema kuwa kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kusema kuwa yeye na Mbunge wa Kibamba John Mnyika walitaka kujiunga na CCM, si kweli.

Kubenea amesema kuwa hawakuongea vile na Rais bali walikuwa wakizungumza mambo mengine, na Makonda amesema yale ili kuwafurahisha wanachama wa chama cha mapinduzi waliokuwepo kwenye hafla ile.

Kubenea amesema kuwa uchaguzi ujao watahakikisha kuwa wanashinda kwa kishindo hadi serikali inayoongozwa na CCM ishangae.

"Nataka nimwambie tu RC Makonda kwamba katika uchaguzi unaokuja upinzani tutashinda zaidi kuliko ilivyo kawaida, na ataondoka kwa aibu", amesema Kubenea.

Kubenea ameongeza, "Nchi yetu inajenga matabaka, mtu akionekana anaikosoa serikali wanasema huyu mpinzani na siku hizi wametupatia jina jipya wanatuita mawakala wa mabeberu".

Kubenea amesema kuwa, wale wanaomuunga mkono Rais Magufuli wengi wao ndio wanaompinga kimya kimya wakishirikiana na wanachama wengine ndani ya chama ambao wanajiandaa kumpinga katika uchaguzi ujao.

Hayo yamejiri baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, kudai kuwa, amepokea maombi ya wanachama mbalimbali wanaotaka kujiunga na CCM, wakiwemo wabunge wawili wa CHADEMA, Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na wa Kibamba, John Mnyika, wakati akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa daraja la kisasa la Selander na barabara unganishi jijini Dar es salaam.

Thursday, December 20, 2018

“Sina Habari na Mambo Ya Ndoa”- Linah Sanga

Mwanamuziki wa Bongo fleva mrembo Linah Sanga amefunguka na kuweka wazi kuwa hivi sasa hana mpango wa kuolewa na wala hawazi kuhusu mambo ya ndoa. Linah amefunguka kuwa maisha ya ndoa kwa sasa hayafikirii na badala yake anatamani kuona muziki wake unampa heshima kwanza. Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la DIMBA, Linah alisema, licha ya wanawake wengi kutamani ndoa lakini kwake inekuwa tofauti na badala yake ameelekeza nguvu zaidi kwenye kazi zake. Mimi ukiniuliza mambo ya ndoa kwa sasa ni ngumu kueleza.. niulize muziki wangu unakwendaje au kuhusu mwanangu". Linah amezaa Mtoto mmoja na mwanaume ambaye alikuwa kwenye mahusiano naye ya muda mrefu aitwaye Shaban Mchomvu ambaye amezaa naye Mtoto mmoja wa kike anayeitwa Tracey Paris.

The post "Sina Habari na Mambo Ya Ndoa"- Linah Sanga appeared first on Ghafla! Tanzania.


Source

Tuesday, December 18, 2018

Tambua umuhimu wa kuvaa soksi


Miguu ni sehemu mojawapo inayotoa jasho  sana hivvo ni vema kuiweka mikavu kuzuia ukuaji wa bacteria au fungus.Wakaka tunajua umuhimu wa soksi au tunavaa bila kujua na wengine hatuvai? Hii ni kwa wadada pia wanaovaa viatu kama raba au hata nyumbani. Ni vema sana kufahamu kwanini tunavaa soksi na mda mwingine soksi gani tuvae.

1.KUZUIA MAGONJWA YA NGOZI MIGUUNI.

Tumia sekunde tatu tu kuvaa soksi na ujikinge na maradhi haya ya fungus na bacteria, kama sio mpenzi was soksi nashauri ufikirie tena maamuzi yako ya kutovaa soksi.

2.EPUKA HARUFU MBAYA YA MIGUU
Image result for atletes foot
Kwa kweli hii ni kero kwako na wanaokuzunguka.Usipovaa soksi jasho lote la miguu litaenda kwenye viatu na ivo viatu kutoa harufu.Soksi hunyonya lile jasho na huzuia harufu iyo. Aya basi tushtuke aibu hii ya nini katika karne ya watanashati sisi.Tuvae soksi na kubadili kila siku.

3.LAINISHA NGOZI YA MIGUU YA YAKO

Nani hapendi miguu soft?? wadada kutwa kusugua miguu saloon.Simple ukirud nyumban kama sakafu ni ngumu vaa soksi zako nyepesi safi miguu iwe laini.Baadhi ya viatu pia vina surface ngumu kwa chini (wakaka) ukiweka soksi zako safi hamna maneno.

4.KUPUNGUZA MAUMIVU MIGUUNI

Hii hasa kwa watoto wadogo ..tuwazoeze mapema kuvaa soksi.Mtoto anatembea ndani Mara akanyage maji mara vitu vya ncha Kali....Pia kuna viatu ukivaa bila soksi lazima upate maumivu na kupata zile sugu nyeusi.

5.KUPATA JOTO NYAKATI ZA BARIDI 

Wale was mikoa iliyo na baridi kwa sasa naamini tuna soksi za kutosha za miguuni na mikono.Kama kuna sehemu inayongoza kutoa joto ni miguuni na mikononi.Basi vaa soksi ili kuzuia joto lisipotee.

6.MVUTO

Ili sio geni, mi mtu akivaa viatu bila soksi kwa kweli napunguza maksi za utanashati...wengine wanasema kuna viatu vya kutovaa soksi. .hakuna kitu kama icho kuna soksi ndogo ambazo hazionekani kwa juu zimejaa tele madukani tutafte.Ebu mtu kavaa kiatu chake safi akiweka na soksi safi inaonekana mvuto lazima uwepo....Nani hapendi kuvutia??basi sote tunapenda tuvae soksi


Siandiki mengi sana, soksi sio jambo geni, tubadilike tujijali,.Ok unavaa soksi Je?unavaa soksi pea moja mara ngapi, unafua na kukausha vizuri maana soksi mbichi ni janga jingine la uchafu na maradhi.Kitu kingine ujue aina ya soksi nyakati za joto usivae soksi ambazo  ni nzito sana vaa nyepesi, ambazo ni nzito vaa nyakati za baridi. Na soksi za watoto tununue ambazo hazibani sana.

Monday, December 17, 2018

Baada ya Jana Kuachwa na Ndege ya Air Tanzania...Leo Aipanda Ndege hiyo na Kuandika Yafuatayo


Fom #diamondplatnumz - Telling my Wifey we jus Ordered another 2 Airbus for Our AirTanzania Airline, so KQ Better be Ready and she was Like "Ooh Really?" i said Oooh Yes😋!!!...
(Nimemwambia Mke, Tumeagiza Ndege Zingine Airbus Mbili kwajili ya Shirika letu la Air Tanzania, Hivyo KQ zijiandae... akasema "Ooh kweli?" nikamwambia Pigia Mstari😋!!!).... Asante @airtanzania_atcl
leo Huduma Zimeboreka barabara!!!

Source

VIDEO: Tuliowanyanganya watakuwa wamechukia / naomba mniombee kwa Mola - Rais Magufuli


Rais Magufuli awataka Waislamu kuzitunza mali walizodhulumiwa ambazo zimerejeshwa.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA, PIA SUBSCRIBE 

DIAMOND AZOZANA NA SHIRIKA LA NDEGE TANZANIA KISA KUACHWA NA NDEGE UWANJANI

Mwanamuziki nyota kutoka Tanzania Diamond Platnumz ametofautiana na Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kuhusu kilichotokea hadi akaachwa na ndege uwanjani Mwanza.

Mwanamuziki huyo anasema tamko lililotolewa na shirika hilo kwamba alichelewa kufika uwanjani si za kweli.

ATCL kupitia taarifa wamesema Diamond , ambaye wamemrejelea kama Isaack Nasibu, alikuwa miongoni mwa abiria waliopaswa kusafiri na ndege ya shirika hilo Jumapili 16 Desemba, 2018 hakuachwa kama inavyodaiwa bali alichelewa kufika uwanjani kwa muda unaotakikana.

Anadaiwa kufika dirishani robo saa baada ya dirisha kufungwa.

Jina rasmi la mwanamuziki huyo ni Nasibu Abdul Juma Issaack.

"Kampuni inapenda kutoa ufafanuzi kuwa abiria huyo alifika uwanjani kwa kuchelewa na hivyo kuzuiliwa na mamlaka zinazosimamia uwanja kwa mujibu na taratibu," ATCL wamesema.

Aidha, shirika hilo la serikali limepuuzilia mbali madai ya msanii huyo kwamba tiketi yake iliuzwa kwa abiria wengine.

"Kampuni inapenda kutoa ufafanuzi kwamba, tuhuma hizo si za kweli kwani tiketi za kampuni yetu zinamruhusu mteja wetu kuitumia tiketi yake ambayo haijatumika kwa siku nyingine ambapo atakuwa tayari kusafiri nasi.

"Hata hivyo mteja wetu aliyelalamika ameiomba kampuni kutumia tiketi yake siku ya leo.

"Kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) imesikitishwa na tuhuma na malalamiko yaliyotolewa na ndugu Issaack Nasibu na wenzake kwa kupitia video waliyojirekodi na kuirusha kwenye mitandao ya kijamii wakati kampuni inazo taratibu za namna ya kuwasilisha malalamiko pindi mteja asiporidhika na huduma zetu."

ATCL wametoa wito kwa abiria "kuzingatia muda unaoonyeshwa katika tiketi zao ili kuepuka usumbufu usiokuwa wa lazima."

Mkuu wa mawasiliano wa shirika hilo Josephat Kagirwa amesema shirika lililazimika kutoa ufafanuzi kwa umma baada ya kuona malalamiko ya Diamond yakisambaa katika mitandao ya kijamii.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond amesema hakuchelewa kamwe na badala yake akadai kuna mchezo ulifanyika ikiwa ni pamoja na tiketi za abiria kuuzwa kwa abiria wengine, ambapo anasema miongoni mwa waliokuwa wanauziwa ni baadhi ya wafanyakazi wa kampuni yake ya Wasafi Media.

Licha ya kwamba ujumbe ni wa kulalamika, kwenye picha yake ameweka picha ya ndege ya Air Tanzania na kitambulisha mada #WakwanzaAfrika, kuashiria kwamba shirika hilo litakuwa la kwanza Afrika kupokea ndege aina ya Airbus A220-300.

"Sikuchelewa ndege Kabisa..Nilifika muda sawia kama usafiri wa ndege za ndani unavyotaka, na kulidhihirisha hilo.. nikiwa niko pale kuna hata abiria wengine waliingia nusu saa baadae, tena nikiwepo nimesimama palepale..." ameandika kwenye Instagram.
".. na mmoja ya watu waloingia nikiwepo nimesimama ni @Harmonize_tz ..."

"Kilichotokea ni kuwa Mmoja ya watu wenye dhamana pale, siti zetu (viti vyetu) aliziuza kwa abilia (abiria) wa fastjet...kwa abiria watalii wazungu, na walichokuwa hawajajua pia waliwauzia na baadhi ya watu ambao ni wafanyakazi wetu wa Wasafi Media..."

"Na Kuthibitisha tena kuwa hatukuchelewa, alikuja tena mtu wa Air Tanzania na kutuambia kuwa siti zimebaki mbili...Hivyo tuchague watu wawili tu wasafiri....

"Kama kweli tulichelewa, sasa hao wawili, sasa wangewezaje ingia??? tukasema hatuwezi safiri wawili lazima tuwe wote kama tulivyokata... hivyo ni dhahiri kuwa hatukuchelewa....ila kutokana na Ndege nyingi za kuja mwanza zilicancel trip zao, ikiwepo Fastjet hivyo tickets zikawa ni dili sana na ndio yote kutokea...."

Ametetea msimamo wake na kusema „ kama Mtanzania Mzalendo Mwenye akili Timamu, siwezi tu kukurupuka kusema jambo kwani ni jukumu langu kuhakikisha nalilinda shirika hili."

"Nikiwa kama Mtanzania mwenye uchungu siwezi kuona mtu alopewa dhamana ya kuzisimamia ndege hizo anafanya vitu tofauti halafu eti nikakaa kimya..."

Harmonize, mwanamuziki mwenzake, ameandika maoni kwenye ujumbe wa Diamond na kusema 'Fact', kwa Kiingereza kwa maana ya kweli kabisa.
ATCL wanasema nini kilitokea?

Kwa mujibu wa shirika hilo la ndege, abiria Issaack Nasib aliyekuwa na tiketi namba- 197 2400458865 ya kampuni ya ndege ya Tanzania alikuwa katika safari ya kutoka Mwanza kwenda Dar Es Salaam, ndege nambari TC103 ya jioni tarehe 16 Disemba 2018. Kwa kawaida shirika hilo linasema abiria hutakiwa kufika uwanjani masaa mawili kabla ya ndege kuruka.

ATCL wanasema afisi yao ya Mwanza ilifungua dirisha kwa ajili ya kuwahudumia wateja (wasafiri) majira ya 17:45 na kulifunga majira ya 20:00.

Ndege hiyo iliruka kutoka Mwanza kuja Dar Es Salaam majira ya saa 20:45 na kuwasili Dar Es Salaam saa 22:00.

"Kwa kumbukumbu zilizopo kwa kutumia vyanzo mbalimbali, zikiwemo Camera (CCTV) za uwanjani inaonekana abiria tajwa hapo juu alifika majira ya 20:15 ambapo dirisha lilikuwa limeshafungwa. "

Bw Kagirwa, akizungumza na wanahabari alisema: "Tiketi ya mteja haiwezi kuuzwa. Ila asipoonekana uwanjani na akawepo mtu mwingine anahitaji huduma tutampa nafasi maana nafasi katika ndege thamani yake inaisha ndege inaporuka lakini tiketi baada ya hapo inabadilishwa."

Tumesikitishwa sana, Diamond alichelewa masaa matatu kufika Airport Mwanza – ATCL

Kampuni ya ndege Tanzania (ATCL ) limetoa taarifa rasmi kuhusu sakata la Msanii wa muziki,  Diamond Platnumz kuchelewa Airport Jijini Mwanza usiku wa jana.   Taarifa hiyo imeeleza kuwa Diamond alitakiwa kufika saa 11:45 jioni lakini yeye alifika saa 2:15 usiku. Ikiwa tayari ndege ilibakiza dakika 30 kuondoka kuelekea Dar Es Salaam .

The post Tumesikitishwa sana, Diamond alichelewa masaa matatu kufika Airport Mwanza – ATCL appeared first on Bongo5.com.


Source

Dogo Janja Amponda Bilnass na Style Yake ya Nywele.

Msanii kutoka Arusha Dogo Janja amemtupia msanii mwenzake Billnass,  Dongo baada ya msanii huyo kuonekana akiwa na style mpya ya nywele akiwa ametengeneza dread, style ambayo wasanii weng ka sasa wamekuwa wakiweka kichwani. Dogo Janja amefunguka na kusema kuwa style hiyo haijampndeza kabisa msanii mwenzake huyo na kumwambia kuwa  hata waliupokutana katika After school bash wikiend iliyopita hakumtambua mara moja kwa sababu ya  upya huo. Dogo janja amefunguka na kumwambia kuwa msanii mwenzake huyo hajapendeza kabisa na kuamua kubadili style hiyo. Wasanii hasa wa kiume kwa sasa wengi wamekuwa wakivutiwa na kutengeneza nywele style ya nywele ndefu yaan dread , ingawa wengi hupendelea kusuka lakini  sio kichwa kizima, vado haijafahamika kama dogo janja alikuwa akitania kuhusu swala hili au lakwa sababu wawili hao ni marafiki pia.  

The post Dogo Janja Amponda Bilnass na Style Yake ya Nywele. appeared first on Ghafla! Tanzania.


Source

Kauli ya Dogo Janja baada ya Billnass kubadili staili ya nywele


Baada ya mkali Billnass kutuonesha style mpya ya nywele ya kusuka rasta style ya Dreads, Dogo Janja ameiponda style hiyo na kudai haijampendeza hata kidogo na istoshe alikutana naye kwenye After School Bash lakini hakumgundua haraka kutokana na muonekano wake.

MOYO WASAHAULIKA KWENYE NDEGE,YALAZIMIKA KUKATIZA SAFARI YAKE

Ndege ya abiria ya Marekani iliyokuwa ikisafiri kutoka mji wa Seattle kuenda Dallas ililazimika kukatiza safari baada ya moyo wa binadamu kusahaulika ndani yake.

Shirika la ndege la Southwest linasema kuwa kiungo hicho kilisafirishwa Seattle kutoka California, ambako ilitarajiwa kutolewa mishipa ambayo ingetumiwa baadaye kwa utaratibu wa tiba ya upandikizaji.

Lakini kisanduku ambacho kilikuwa kimehifadhi moyo huo kilisahaulika ndani ya ndege hiyo na hilo lilifahamika baada ya ndege kuanza safari kuelekea Dallas.

Kisa hicho kilitokea siku ya Jumapili lakini kiliangaziwa katika vyombo vya habari siku ya Alhamisi.

Abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo wanasemakana kushutuka sana wakata rubani alipowaambia kuhusiana na mzigo huo na kwamba hana budi kugeuza mkondo na kurejea walikotoka.

Baadhi yao walitumia simu zao kujifahamisha kuhusu muda ambao moyo unaweza kuhifadhiwa kabla ya itumike kwa upasuaji- kwa mujiu wa wataalamu, moyo wa binadamu huchukuwa kati ya saa nne na sita kuharibika.

Chanzo:Bbc

DIAMOND AONESHA JEURI..AIMBA WIMBO WA NYEGEZI ULIOKATAZWA...BASATA KUKOMAA NAE

Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limesema kitendo cha mwanamuziki Diamond Platnumz kuimba wimbo wa Mwanza uliofungiwa na baraza hilo ni dharau na kubainisha kuwa litatoa tamko kuhusu kitendo hicho.

Diamond aliimba wimbo huo alioshirikishwa na Rayvanny jana Desemba 15, 2018 katika tamasha la Wasafi lililofanyika jijini Mwanza, huku maelfu ya mashabiki wakimshangilia na kumfuatisha alivyokuwa akiimba.

Mkali huyo wa Bongo Fleva aliimba wimbo huo jukwaani akiwa pamoja na Rayvanny.

Akizungumzia na Mwananchi kuhusu kitendo hicho leo Jumapili Desemba 16, 2018 katibu mtendaji wa Basata Godfrey Mngereza amesema, "Nimepigiwa simu kuhusu hii kitu. Niko Arusha kikazi nimeshawasiliana na mwenyekiti wa bodi (ya Basata)."

"Basata itakuja na majibu muafaka kwani hapa (Diamond) kaonyesha kiwango cha juu cha dharau kwa baraza, bodi, wizara (Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo) na Serikali kwa ujumla."

Wimbo huo ulifungiwa Novemba 12, 2018 na baraza hilo kwa maelezo kuwa unahamasisha masuala yasiyokubalika katika jamii.

Akizungumza wakati akitoa tamko la kufungiwa kwa wimbo huo Mngereza alisema hautakiwi kuchezwa mahali popote.


Alipoulizwa kama ni ruksa wimbo huo kupigwa katika tamasha la Wasafi lililoanza Novemba 24, 2018 likifanyika mikoa mbalimbali nchini Tanzania, alisema nalo watalifungia iwapo watautumia wimbo huo.

Sunday, December 16, 2018

Kanuni za Kilimo bora cha Tangawizi


Asili ya zao hili ni maeneo ya kitropiki ya bara la Asia na hasa katika nchi za India na China. Zao hili linazalishwa kwa wingi kutoka katika nchi ya Jamaica. Hapa nchini zao hili hulimwa katika mikoa ya Kigoma, Tanga, Morogoro, Pwani, Mbeya na Kilimanjaro.

Tangawizi hutumika kama kiungo katika kuongeza ladha, harufu na kuchangamsha katika vinywaji (kama chai, soda, juisi, vilevi n.k) na vyakula mbalimbali kama mikate, biskuti, keki, nyama za kusaga, achari n.k.

Hutumika pia katika viwanda vinavyotengeneza madawa ya tiba mbalimbali kama dawa za meno, kikohozi, tumbo na muwasho wa ngozi n.k. pia hutumika katika vipodozi kama poda n.k).

Aina ya Tangawizi.
Hakuna uthibitisho wa aina za tangawizi ambazo hulimwa hapa nchini ila kuna dalili ya kuwa na aina za White Africa (Jamaica) na Cochin (flint); hii huwa na tunguu ngumu zenye nyuzi.


Tabia ya Mmea.
Tangawizi ni mmea unaotambaa chini ya ardhi, wakati wa masika hutoa majani juu ya ardhi. Jamaica ina rangi hafifu ya kahawia na tunguu fupi wakati Cochin ina tunguu fupi zaidi lenye ngozi ya rangi iliyo kati ya kijivu na nyekundu.

Mmea una urefu wa futi mbili na majani yake ni membamba marefu ambayo hufa kila mwaka yakiacha tunguu ardhini likiwa hai. Maua ya mmea huu yana rangi nyeupe au manjano.


Hali ya Hewa na Udongo.
Zao hili hustawi katika maeneo yenye hali ya kitropiki, kutoka usawa wa bahari hadi mwinuko wa mita 1,500 au zaidi. Huhitaji mvua kiasi cha mm.1,200-1,800 na joto la wastani wa nyuzi za sentigredi 20-25. Hustawi vema katika udongo tifutifu wenye rutuba na usiotuamisha maji.

Upandaji
Zao la tangawizi hupandwa kwa kutumia vipande vya tunguu vyenye kichipukizi kizuri angalau kimoja na huweza kukatwa katika urefu wa sm.2.5-5. Wakati mwingine, vichipukizi vinavyopatikana katika kumenya tangawizi huweza kuhifadhiwa na kutumika kwa kupanda. Kiasi cha kilo 840-1700 cha vipande vya tunguu huweza kutumika kwa kupanda katika hekta moja. Nafasi inayotumika kupanda ni kati ya sentimita.23-30 kwa 15-23 na kina cha sentimita.5-10 na mara nyingi hupandwa katika matuta. Baadhi ya mazao huweza kupandwa katika shamba la tangawizi ili kuweka kivuli chepesi ingawa si lazima kivuli kiwepo. Inashauriwa kumwagilia maji endapo mvua inakosekana.

Wiki 1-2 kabla ya kupanda weka mbolea ya samadi au mboji kiasi cha tani 25-30 kwa hekta na kwa kukuzia weka kiasi cha NPK kwa uwiano wa kilo 36:36:80. Tandaza nyasi shambani kuhifadhi unyevunyevu hasa pale kivuli kinapokosekana. Palizi hufanywa mara magugu yanapoota, dawa ya kuua magugu, kama simazine au round up hutumika.

Magonjwa na wadudu
Madoa ya majani yanayosababishwa na viini vya magonjwa viitwavyo Colletotrichum zingiberis na Phyllosticta zingiberi.
Kuoza kwa tunguu; kunasababishwa na viini viitwavyo Pithium spp
Mizizi fundo; inasababishwa na Meloidegyne spp.

Uvunaji
Tangawizi huweza kuwa tayari kwa kuvuna kati ya miezi 9-10 baada ya kupanda, wakati majani yake yanapogeuka rangi kuwa njano na mashina kusinyaa. Tangawizi inayohitajika kwa kuhifadhi kwenye kemikali (preserved ginger in brine) huvunwa kabla haijakomaa kabisa, wakati ile iliyokomaa kabisa huwa kali zaidi na huwa na nyuzi hivyo hufaa kwa kukausha na kusaga. Mavuno hutofautiana kulinganana na huduma ya zao, mavuno yanaweza kuwa kiasi cha tani 20-30 cha tangawizi mbichi huweza kupatikana.

Usindikaji.
Tangawizi ikisindikwa utapata unga, mafuta maalum (essential oils) n.k. Tangawizi iliyovunwa huweza kumenywa, kukatwa na kukaushwa juani au mara nyingine huchovywa katika maji yaliyochemka kwanza na ndipo kukaushwa au hukamuliwa mafuta. Pia tangawizi husindikwa na kuhifadhiwa kwenye chupa zikiwa zimechanganywa na sukari na/au chumvi au bila kuweka kitu chochote. Hata hivyo tangawizi ina Kiasi cha mafuta cha 16.0-18.0%.


Source

Rammy Galis atinga kijeshi uzinduzi wa Movie ya ‘Hukumu’ aliyomshirikisha Agnes Masogange, amchana Duma(+video)

Muigizaji wa filamu Bongo Rammy Gallis usiku wa leo wa Desemba 15 amezindua rasmi movie yake ya Hukumu ambayo amemshirikisha marehemu Agnes Masogange. Katika uzinduzi huo ameonekana kutinga na vazi la kipekee huku akielezesa sababu ya kuvalia nguo hizo na huku akizungumzia kilichopeleka kufanya uzinduzi wa filamu zao siku moja na msanii mwenzake maarufu kama …

The post Rammy Galis atinga kijeshi uzinduzi wa Movie ya ‘Hukumu’ aliyomshirikisha Agnes Masogange, amchana Duma(+video) appeared first on Bongo5.com.


Source

Thursday, December 13, 2018

MAHAKAMA YA MAFISADI TANZANIA YAMTUPA JELA MAISHA RAIA WA ETHIOPIA

Mahakama Kuu Kitengo cha Uhujumu Uchumi 'Mahakama ya Mafisadi' imemuhukumu kifungo cha maisha jela raia wa Ethiopia, Ana Moises Chissano baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya aina ya Cocaine Kg 3.03.

Hukumu hiyo imetolewa na Jaji Lilian Mashaka ambapo amesema mshtakiwa huyo amefungwa chini ya kifungu cha sheria cha 15(1)(b) cha sheria namba 5 ya 2015 cha sheria ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya.


Mahakama imeamuru dawa hizo ziteketezwe.

Tuesday, December 11, 2018

Kimnana Adakwa na Otile

Mwanadada ambae alisifika na kuta umaarufu wa muda mfui sana hao nyakati za nyuma  kimnana ambae alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Diamond platinum anasemekana kuwa katika penzi zito na mwanakaka kutoka kenya Otile brown ambae na yeye pia ametoka katika kiumizwa kichwa baada ya kuachwa na mpenzi wake. Wawili hao wanasemwa kuoneka apamona baadhi ya maeneo huku Otile akiweka baadhi ya pichakatika mitandao za mwanadada huyo.ikumbukwe kuwa otile alikuwa na mahusiano na mtu maarufu sana uganda, vera sidika na hata kim alikuwa na mahusiano na mtu maarufu sana Diamond  platinum, Otile na kim wote kwa sasa wamekuwa wakiugulia mauivu ya mapenzi. Hata hivyo , msanii harmonize pia alimtuia ujumbe wa kum-miss kimnana , ujumbe unaomtaka kurudi huko alipokuwa huku ikisaidkiwa kuwa ni kweli mwanadada huyo atakuwa nje ya tanzania na mpeniz wake huyo

The post Kimnana Adakwa na Otile appeared first on Ghafla! Tanzania.


Source

Sunday, December 9, 2018

Kikosi cha Coastal Union dhidi ya Mbeya City hiki hapa


Kikosi cha Coastal Union kitakachoanza dhidi ya Mbeya City

1. Hussein Shariff
2. Mbwana Hamis
3. Abdalah Wazir
4. Bakari Mwamnyeto
5. Ibrahim Mohamed
6. Athuman Chuji
7. Issa Abushehe
8. Mtenje Albino
9. Andrew Simchimba
10. Ali Kiba
11. Ayoub Lyanga

Kikosi cha akiba

12. Abubakar Abbas
13. Abubakar Kinanda
14. Kenedy Kipepe
17. Hassan Mangayamba
18. Deo Anthony
19. Muhsim Makame
20. Mohamed Mussa


Friday, December 7, 2018

Mo j Atoa Sababu ya kumiga Gigy Money

Mtangazaji wa clouds media, Mo Jay amefunguka  baada ya mwanadada Gigy Money kusema katika mitandao ya kijamii kuwa baba wa mtoto wake huyo ndio aliempiga na wala sio mpenzi wake mpya. Katika moja ya post yake wiki hii Gigy Money alieleza mengi na mwishoni alisema kuwa hata makovu hayo yaliyo mwilini mwake hivi karibuni ni baba mzazi wa mtoto wake ndio aliesababisha kwa kumpiga. Hata baada ya maneno mengi katika kitandao, shabiki mmoja aliamua kum-attack mo jay kwa kuwambia kua aache kuiga mama wa mtoto wake na ndipo mwanaue huyo alipoamua kumjibu shabiki huyo kwa kusema “shortly alikuja kwangu kunifanyia fujo, na sio mara moja nitawaeleza ilivyokuwa :‘

The post Mo j Atoa Sababu ya kumiga Gigy Money appeared first on Ghafla! Tanzania.


Source

Tuesday, December 4, 2018

Hizi ndio post zilizopata likes nyingi zaidi Instagram

Katika mitandao yote ya kijamii Instagram imekuwa ni sehemu ambao watu wanaufuatili na wanajifunza vitu vingi sana na hata kwa mastaa ni sehemu ambayo inamuonyes staa yupi ana fuatiliwa zaidi. katika post ambazo kila mtu anapost huwa zinapata ushawishi wa watu kuifuatilia post hiyo, ikiwa ni video au picha na ktokana na tukio maalumu la …

The post Hizi ndio post zilizopata likes nyingi zaidi Instagram appeared first on Bongo5.com.


Source

CHINA YAPIGA MARUFUKU HARUSI

Mamlaka za China zipo mbioni kudhibiti ongezeko la harusi za kifahari amabazo zimekuwa zikishamiri katika miaka ya karibuni.

Kwamujibu wa maafisa wa serikali, harusi za kisasa si tu ni za gharama kubwa bali zinaenda kinyume na misingi ya kijamaa ya nchi hiyo.

Harusi za Kichina ambazo hufungwa kimila, hauambatana na sherehe ambazo kwa sasa mamlaka zinadai kuwa zimekuwa kubwa mno.

Sasa serikali ya Beijing inajipanga kuja na namna ya kuzifanya ziwe sawa kwa kufanyika kwa sherehe zenye kiasi.

Wachina kama ilivyo kwa raia wa nchi nyengine duniani wamekuwa wakishindana na jirani, marafiki na jamaa katika kuandaa sherehe kubwa na za kupendeza za harusi. Na harusi kubwa tayari zimeshakuwa fasheni nchini humo.

Harusi hizo huambatana na karamu kubwa, nguo za kifahari na safari za ughaibuni kupiga picha za harusi.

Chanzo:Bbc

Video 20 za muziki za Tanzania zilizoangaliwa zaidi YouTube kwa muda wote

Zikiwa zimebaki siku chache mwaka 2018 umalizike, Bongo5 imekuandali list ya video za muziki za Tanzania zilizoangaliwa zaidi kupitia mtandao wa YouTube kwa moja wote. List hii ni kwa mujibu wa mtandao wa dbase.tube ambao unatoa data na takwimu mbalimbali kuhusu kazi za wasanii zinazopakiwa kupitia mtandao huo duniani. Angalia list hiyo. 1. Diamond Platnumz …

The post Video 20 za muziki za Tanzania zilizoangaliwa zaidi YouTube kwa muda wote appeared first on Bongo5.com.


Source

SERIKALI YAFUTA MITIHANI YA KIDATO CHA PILI


Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imefuta mitihani ya kidato cha pili visiwano humo iliyokuwa ikiendelea na kusema kuwa tarehe ya mitihani hiyo itatangazwa tena.

Akizungumza na wanahabari leo Disemba 3, 2018, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Aamali Zanzibar, Riziki Pembe amesema kuwa mitihani hiyo ifutwe na wanafunzi waendelee na masomo yao kama kawaida.

"Wizara imefuta mitihani hiyo na itatangaza tena tarehe ya kurudiwa, mara tu taratibu zitakapo kamilika", amesema Bi. Pembe.

Mitihani hiyo imeahirishwa ikiwa ni muda mfupi tangu kwa upande wa Tanzania bara, kukamilisha mitihani hiyo Novemba 24,2018.
Chanzo - EATV

Jinsi ya kumtambua mpenzi ambaye ni tapeli



KWENYE ulimwengu wa mahaba, wengi wanaumizwa. Wengi hufikia hatua ya kukata tamaa na kusema hawatapenda tena. Hawaoni umuhimu, wameambulia karaha za kutosha. Yote hayo hutokea kwa sababu gani? Kuingia kwenye uhusiano na mtu ambaye si sahihi. Asikwambie mtu, mapenzi ni matamu kama utakuwa na mtu sahihi. Inawezekana. Kwenye dunia hiihii ya matapeli wa mapenzi, wapo ambao wanajielewa. Wana nia ya dhati kabisa ya kufika mbali katika safari ya uhusiano.

Kama wewe unahitaji kufika mbali, wapo pia wanaotamani kama wewe. Wapo wanaume wanaohitaji wanawake wa kufika nao mbali, wapo pia wanawake wanaohitaji wanaume wa kufika nao mbali. Tatizo kubwa ni watu hao kupishana. Mwanaume anapishana na mke mwema, mwanamke anapishana na mume mwema. Bahati mbaya sana, mapenzi huhifadhiwa moyoni. Ni vigumu kujua mwenzi wako anawaza nini kwenye moyo wake. Ana siri gani, anawaza nini juu yako.

Wengi wamekuwa wajanja sana. Wanaishi na lao moyoni. Unakuwa na mtu ukiamini mpo pamoja kumbe mwenzako hayupo na wewe. Ana agenda yake binafsi. Pengine ana mtu mwingine, anampenda zaidi na wewe anakufanya kama bosheni tu. Ni hatari sana kuishi na mtu wa aina hii. Yeye anajua kupanga karata zake, anakuwa na mtu mwingine mwisho wa siku anakuja kukuacha solemba. Aliyeachwa ataumia sana. Atajutia muda alioupoteza, anayachukia mapenzi.

UTAJUAJE ULIYE NAYE SI SAHIHI?
Pamoja na kwamba ni ngumu sana kujua lililopo moyoni mwa mwenzako lakini kuna viashiria ambavyo unapaswa kuwa navyo makini pindi unapoviona kwa mwenzi wako. Ukiviona hivyo, fanya majaribio ya kujiridhisha, akili yako pekee inatosha kung'amua ukweli.

KIASHIRIA CHA KWANZA
Namna mtu anavyokutana na wewe siku ya kwanza, wakati wa mazungumzo yake ya awali utagundua ni mtu wa aina gani. Ana uharaka wa mambo? Anatumia lugha za aina gani katika mazungumzo yake? Lugha pia huweza kutoa picha ya mtu alivyo.

Kupitia mazungumzo yake, unaweza kugundua kama ni mtu mpole. Unaweza kujua ana hekima, ana busara? Kupitia mazungumzo yake, waweza pia kujua kama ni mhuni? Waweza pia kumtambua kama hana malengo marefu.

KIASHIRIA CHA PILI
Baada ya kumpitisha kwenye hatua ya kiashiria cha kwanza, unashauriwa umweke karibu ili uweze kumsoma zaidi. Yawezekana akawa ameficha baadhi ya mambo katika kiashiria cha kwanza, ukamnasa katika kiashiria hiki.

Mazungumzo yake kila wakati yanalenga kwenye hitaji fulani tu muhimu. Yawezekana akawa anahitaji fedha, anahitaji mapenzi na mambo mengine yanayofanana na hayo. Ukiona mtu wa hivyo, jua kuna walakini na unaweza kumuingiza kwenye kipimo haraka na ukamtoa kabla hata moyo wako haujazama penzini.

KIASHIRIA CHA TATU
Hazungumzii maendeleo. Kila unapoanzisha mada ya maendeleo hususan ya uhusiano wenu, unamuona mwenzako anakupiga chenga kwa kuhamisha mada. Anatoa kipaumbele katika vitu ambavyo havina manufaa ya baadaye.

Mambo kama matembezi, kujirusha au kwenda gesti au hotelini ndiyo anayotaka kuyasikia. Sisemi kwamba kufanya hivyo ni vibaya lakini vyote hivyo kwa mtu ambaye yupo serious, huambatana na mazungumzo ya maendeleo ya uhusiano wenu.

KIASHIRIA CHA NNE
Hajali. Unakuta wewe unajitoa kwa hali na mali kuhakikisha unaufanya uhusiano unakuwa hai, mwenzako hakupi ushirikiano. Yeye anakuwa na hitaji fulani tu kwako. Utahangaika kumpa zawadi mbalimbali, utamuonesha upendo wako lakini vyote hivyo mwenzako anachukulia kawaida tu.

CHUKUA HATUA
Ukiona mambo yanakuwa hivyo kwa muda mrefu, umeviona viashiria vyote nilivyoviainisha kwa mwenzi wako basi anza kuchukua hatua ya kumweka pembeni. Ondoa mawazo taratibu kwake, kama aliteleza bahati mbaya atarudi lakini akiendelea, jiengue utampata mwingine.

Monday, December 3, 2018

Klabu ya Barcelona yapatwa na pigo

Klabu ya Barcelona leo Jumatatu imepatwa na msiba mzito wa kuondokewa na aliyekuwa Rais wa klabu hiyo mwaka 1978-2000, Josep Lluís Nuñez. Nunez anatajwa kuwa ndiye Rais aliyeleta mabadiliko makubwa ndani ya klabu hiyo kwenye sekta ya kiuchumi na ushawishi. Nunez ndiye Rais aliyepata kuongoza klabu hiyo kwa muda mrefu miaka 22 katika historia ya klabu …

The post Klabu ya Barcelona yapatwa na pigo appeared first on Bongo5.com.


Source

HAYA NDIO MATUNDA YA VITA DHIDI YA UJANGILI

Vita dhidi ya Ujangili wa Tembo katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha imeanza kuzaa  matunda, kutokana na mikakati  mbalimbali inayoendelea kuwekwa na na kutekelezwa na  mamlaka zinazosimamia hifadhi hiyo kwa kushirikiana na wananchi wanaozunguka hifadhi hiyo. Imeelezwa kuwa hifadhi ya Taifa ya Ruaha imezungukwa na vijiji 21 vinavyounganisha Tarafa ya Pawaga na Idodi ambavyo kwa […]
Source

Harmonize na Wolper Mapenzi Moto Moto

Msanii wa Bongo fleva nchini kutoka WCB Harmonize na msanii wa Bongo movie Jacqueline Wolper wamezidi kutengeneza headline kwa tetesi za kurudisha Penzi Lao Kama zamani. Wawili hao wameendelea kuzua gumzo baada ya Harmonize kutangaza kurudi kwa Wolper wake ambaye alimwagana naye miezi kadhaa iliyopita. Ishu nzima ilijiri usiku wa kuamkia juzi Jumamosi katika shoo ya Wasafi Festival iliyofanyika mjini Iringa na kusababisha mji huo kutikisika. Gazeti la Ijumaa Wikienda linaripoti kuwa Wikiend iliyopita katika Uwanja wa Samora, Harmonize alimpandisha stejini Wolper kama 'sapraizi' na kumwangukia akimuomba warudiane, jambo ambalo Wolper alilikubali mbele ya maelfu ya mashabiki wao. Naomba niseme wazi hapa hadharani kuwa nimerudi kwa Wolper wangu". Kufuatia kile kilichojiri mjini Mtwara ambapo Wolper alieleza nia yake ya kumrudisha Harmonize kwenye himaya yake ambapo wengi waliamini kuwa wawili hao wamerudiana maana wahenga walisema kiporo hakihitaji kupashwa na moto mwingi. Pamoja na kuwepo kwa tetesi za wawili kurudiana Mpenzi wa siku nyingi wa Harmonize, Sarah ambaye kwa sasa yupo nyumbani kwao nchini Italy lakini amesema wazi kuwa yeye na mpenzi wake Harmonize bado wako wote na anategemea kurudi Tanzania muda wowote.

The post Harmonize na Wolper Mapenzi Moto Moto appeared first on Ghafla! Tanzania.


Source

Tazama maswali 7 ambayo Rayvanny, Harmonize, Lavalava, Dudu Baya, Queen Darleen na Khadija Kopa hawajawahi kuulizwa Bongo (+video)

Leo usiku Desemba 02, 2018 Wasanii kibao wa muziki wa Bongo Fleva watatumbuiza mjini Morogoro kwenye tamasha la Wasafi Festival, na hapa tumekuwekea maswali 6 ambayo Harmonize, Rayvanny, Nikki Mbishi, Dudu Baya, Lava Lava na Queen Darleen.

The post Tazama maswali 7 ambayo Rayvanny, Harmonize, Lavalava, Dudu Baya, Queen Darleen na Khadija Kopa hawajawahi kuulizwa Bongo (+video) appeared first on Bongo5.com.


Source

Sunday, December 2, 2018

DC Jerry Muro atoa ahadi nzito kwa Rais Magufuli (+video)

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Jerry Muro amempa ahadi ya ushindi Rais Magufuli kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2020, ambapo amedai kuwa atapata kura bila hata kufanya kampeni kwenye Wilaya hiyo. DC Muro ametoa ahadi hiyo leo Desemba 2, 2018 kwenye hotuba yake mbele ya Rais Magufuli, katika shughuli za uwekaji wa jiwe la msingi la …

The post DC Jerry Muro atoa ahadi nzito kwa Rais Magufuli (+video) appeared first on Bongo5.com.


Source

KATIBU MKUU WA CCM : 'MEMBE HANA NGUVU ZAIDI YA CHAMA'

Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally amekataa masharti yaliyotolewa na kada wa chama hicho, Bernad Membe katika ujumbe wake kupitia kitandao ya kijamii na kusema huo siyo utaratibu wa kukutana na wanachama wake.

Dk Bashiru amesema hayo jana Jumamosi Desemba 1, 2018 wakati akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM wilaya ya Bukombe mkoani Geita.

Amesema katika miaka 10 iliyopita CCM haikufanya vizuri kutokana kikundi cha wachache kujifanya ndiyo wenye nguvu na kudharau jambo lililosababisha chama kisipendwe na wapiga kura.

Amesema tangu achaguliwe kuwa katibu mkuu hajawahi kuonana na Membe na licha ya chaguzi zote zinazofanyika za kurudisha wabunge, Membe aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje hajawahi kutoa mchango wowote wa mawazo.

Amesema Membe kama mwanachama mwingine hana nguvu zaidi ya chama hivyo bado anamhitaji afike kwake bila masharti yoyote.

"Sikumsema Membe kama mtu maarufu au mwenye nguvu bali nimemsema kama mwanachama wa kawaida, hana tofauti kabisa na wanachama walioingia leo, ila ana tofauti kwa kuwa amekuwa waziri na mbunge" amesema Dk Bashiru

"Namuhitaji sana (Membe), ningekuwa na namba yake ya simu ningempigia," ameongeza.

Amesema CCM kipindi cha nyuma imeumizwa na makundi, fitina, uongo na nguvu ya pesa mambo ambayo sasa hawapo tayari kuyaendeleza.

Dk Bashiru ametoa kauli hiyo kujibu ujumbe unaodaiwa kuwa wa Membe aliyeutoa kupitia mitandao ya kijamii akijibu wito wa katibu mkuu huyo wa CCM kumtaka kufika ofisini kwake kujibu tuhuma zinazodaiwa kutaka kumkwamisha Rais John Magufuli.

Katika ujumbe huo ulioandikwa na mtu aliyejiita Bernard Membe unasema; Kufuatia taarifa za kwenye mitandao jioni (jana) hii na ujumbe mfupi unaotumwa kwake "Nimeamua kutoa ujumbe huu kwa wote wanaonitakia mema."

"Usiku huu nimempelekea Katibu Mkuu wa chama chetu ndugu Bashiru ujumbe wa kukubali kumwona mara nitakaporejea kutoka nje ya nchi."

"Nimeshangazwa kidogo na utaratibu uliotumika kuniita, lakini kwa sababu ya ugeni kazini na kwa sababu ninamheshimu, nitakwenda kumwona ofisini kwake," amesema.

Simba wakwea pipa Leo kuwafata Mbabane FC


Kikosi cha Simba ambacho kitacheza mchezo wa marudiano na timu ya Mbabane Swalows FC ya Eswatini kimepaa leo kuwafuata wapinzani wake kikiwa na tahadhari ya kulinda heshima ambayo walijiwekea katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba walifanikiwa kupata ushindi wa mabao 4-1 kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo wanatakiwa wasifungwe zaidi ya mabao 2 watakapocheza Desemba 4 kwenye mchezo wa marudio ili kusonga mbele.

Ofisa habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wanatambua wanakwenda kucheza na timu bora na kubwa, kazi yao ni moja kuweza kupata matokeo mazuri.

"Tunatambua tunakwenda kucheza na timu kubwa na bora, ila tuna kazi ya kulinda heshima yetu, tunajua sisi ni mabingwa wa Taifa na tunaliwakilisha, matokeo mabaya ni kujifedhehesha na kufuzu kwa Simba ni kujiweka sokoni kwa wachezaji kwenye rada za soka," alisema.

Safari yao ya leo watapitia Johannseburg, Afrika Kusini kisha  watabadili ndege na kuelekea Manzini, Eswatini kwa ajili ya mchezo wao marudiano wa Ligi ya Mbaingwa Afrika dhidi ya Mbabane Swallows.

Saturday, December 1, 2018

Herieth Paul apata shavu kwa mara nyingine kwenye Victoria’s Secret

Mtanzania, Herieth Paul anaendelea kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika masula ya mitindo baada ya Ijumaa hii kupokea mualiko wa kuwa miongoni mwa warembo ambao watatembea kwenye maonyesho makubwa ya mitindo duniani, Victoria’s Secret. Kwa sasa mrembo huyo anapata nafasi hiyo kwa mara ya tatu toka mwaka 2016 ambapo alichaguliwa kwa mara ya kwanza. “I …

The post Herieth Paul apata shavu kwa mara nyingine kwenye Victoria’s Secret appeared first on Bongo5.com.


Source

Esma Platnumz Amuweka Wazi Mpenzi Wake Mpya (picha)

Dada wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Esma Platnumz amemuanika mpenzi wake  Mpya kwa Mara kwanza kwenye mitandao ya kijamii tangu Atangaze mahusiano mapya.

Miezi michache iliyopita Esma aliachana rasmi na aliyekuwa mume Wake ndoa Petit Man Wakuache Baada ya kukaa kwenye ndoa kwa miaka kadhaa.

Esma aliweka wazi kuwa sababu ya kuvunja ndoa yao ni pale alipogundua kuwa baba watoto wake huyo amechepuka na mwanamke mwingine na ameishia kumpa mimba.

Esma ametumia social media kumuanika Mpenzi Wake Mpya ambapo ameweka picha zake na kusindika na maneno matamu ya kimahaba akiwa ameandika:

Roho yangu furaha yangu kipenzi changu umeniambukiza ugonjwa wa mapenzi naona Kama dunia nzima tuko wawili tu".




AGAPE : MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI ZINACHANGIA MAAMBUKIZI YA VVU...; DAS 'MSIOGOPE KUPIMA'


Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi akikabidhi sare za shule zilizotolewa na shirika la Agape kwa ajili ya watoto yatima/wanaoishi katika mazingira wanaosoma katika shule ya msingi Pandagichiza wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
****
Jamii imetakiwa kupiga vita mila potofu, mimba na ndoa za utotoni kwani zinachangia uwepo wa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa vijana na watoto mkoani Shinyanga.

Rai hiyo imetolewa leo Jumamosi Desemba 1,2018 na Afisa Mradi wa Afya ya Uzazi na Ujinsia kwa Vijana wa Shirika la Agape AIDS Control Program la Mjini Shinyanga Lucy Maganga wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani ambapo katika wilaya ya Shinyanga yamefanyika katika kijiji cha Shilabela kata ya Pandagichiza.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko.

Maganga alisema ili kutokomeza Maambukizi ya VVU ni lazima jamii ipewe elimu ya afya uzazi na madhara ya mila potofu, mimba na ndoa za utotoni kwani vinachangia maambukizi ya VVU na Ukimwi hasa kwa vijana na watoto.

Alisema katika kuhakikisha maambukizi ya VVU kwa watoto yanatokomezwa mkoani Shinyanga,shirika la Agape limekuwa likitoa elimu ya afya uzazi kupitia mradi wake wa wa Afya ya Uzazi na Ujinsia kwa Vijana katika wilaya ya Shinyanga.

Maganga alisema lengo la mradi huo unaotekelezwa na Agape kwa ufadhili wa Shirika la Kimataifa la Sida la nchini Sweden, ni kuwajengea uwezo watoto na vijana kujitambua,kujithamini na kujitunza dhidi ya tabia hatarishi zinazoweza kuwasababishia mimba za utotoni na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi pamoja na magonjwa ya zinaaa.

"Tupo hapa kuungana na wadau wengine kuadhimisha siku ya Ukimwi Duniani kwani, kwetu Ukimwi ni suala mtambuka,Ukimwi upo, siku ya leo inatukumbusha kuwa ni jukumu letu sote kujilinda na kuwalinda wengine dhidi ya maambukizi ya VVU",alieleza Maganga.

"Katika kuadhimisha siku ya Ukimwi duniani mwaka huu,Agape tumetoa elimu kuhusu VVU na Ukimwi kwa njia ya sinema katika vijiji vya kata ya Shilabela,Sayu na Pandagichiza tukilenga makundi yote katika jamii wakiwemo watoto na vijana",alisema.

Kwa upande wake,Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi aliwataka wananchi kutoogopa kupima na kutumia ARVs hivyo wajitokeze kupima afya zao ili kuhakikisha malengo ya 90 tatu yanafikiwa.

"Tunataka ifikapo 2020, asilimia 90% ya watu wenye maambukizi ya VVU wawe wamefikiwa na kupimwa,kati yao asilimia 90% ya walioathirika watapewa dawa za kufubaza virusi (antiretroviral treatment) na asilimia 90% ya watakaotumia dawa hizo hawataweza kuwaambukiza wenza watakaojamiiana nao kwasababu virusi vitakuwa vimefubazwa na tiba hiy",alisema Chambi.

Naye Mganga Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Dkt.Amos Mwenda alisema wanaendelea kushirikiana na wadau waliopo katika halmashauri hiyo ili kuongeza nguvu kwenye huduma za upimaji VVU,uanzishaji wa dawa za kufubaza VVU na kutoa huduma stahiki kwa watu waishio na VVU.

Hata hivyo alizitaja changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni ushiriki duni wa jamii hasa wanaume katika suala la upimaji VVU na huduma ya afya ya baba,mama na mtoto pamoja na upungufu wa wataalamu wa afya kwa ajili ya utoaji huduma shirikishi za UKIMWI.

Shirika la Agape limetumia fursa ya maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani kutoa msaada wa sare za shule kwa wanafunzi yatima 10 wanaosoma katika shule ya msingi Pandagichiza kwa ajili ya kuwapa hamasa wapende shule na kufanya vizuri kwenye masomo yao.

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA
Mgeni rasmi Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani wilaya ya Shinyanga ambayo yamefanyika katika kijiji cha Shilabela kata ya Pandagichiza.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Afisa Mradi wa Afya ya Uzazi na Ujinsia kwa Vijana wa Shirika la Agape AIDS Control Program la Mjini Shinyanga Lucy Maganga akizungumzawakati wa Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani ambapo katika wilaya ya Shinyanga ambayo yamefanyika katika kijiji cha Shilabela kata ya Pandagichiza.

Wanafunzi na wananchi wa Pandagichiza wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba 1,2018.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Ngasa Mboje akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani katika wilaya ya Shinyanga.
Mganga Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Dkt.Amos Mwenda akisoma taarifa kuhusu maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani Desemba 1,2018.
Mgeni rasmi Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko akikabidhi sare za shule kwa mmoja wa wanafunzi/watoto yatima 10 wanaosoma katika shule ya msingi Pandagichiza iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.Sare hizo zimetolewa na Shirika la Agape ambalo linatekeleza Mradi wa Afya ya Uzazi na Ujinsia kwa Vijana katika halmashauri hiyo. 
Mwanafunzi wa shule ya msingi Pandagichiza akipokea sare ya shule.
Wanafunzi wa shule mbalimbali katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakisubiri kupewa zawadi mbalimbali ikiwemo ya sare za shule,madaftari na kalamu.
Katibu Tawala wilaya ya Shinyanga,Boniface Chambi akikabidhi zawadi ya madaftari na kalamu kwa mwanafunzi.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba 1,2018.
Wanafunzi na wananchi wa Pandagichiza wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani Desemba 1,2018.

Wanafunzi wa shule ya msingi Pandagichiza wakifurahia zawadi ya sare za shule walizopewa na shirika la Agape.Kulia ni Mwalimu wa shule hiyo,Lucia Maungo.
Wanafunzi wanaosoma katika shule ya msingi Pandagichiza halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa wameshikilia zawadi ya sare za shule zilizotolewa na shirika la Agape.
Wanafunzi wanaosoma katika shule ya msingi Pandagichiza halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,walimu wa shule ya msingi Pandagichiza na wafanyakazi wa shirika la Agape wakiwa katika picha ya pamoja.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...