Friday, July 26, 2019

Nchi yetu imeudhihirishia ulimwengu kuwa sisi ni Taifa huru - Rais Magufuli


Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema nchi imeudhihirishia ulimwengu kuwaTanzania ni Taifa huru na sio masikini.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo katika hafla ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa bwawa la kufua umeme la mto Rufiji.

"Nchi yetu imeudhihirishia ulimwengu kuwa sisi ni Taifa huru na sio masikini,mradi huu ulipigwa vita ndani na nje ya nchi tangu tulipoonesha nia ya kuujenga, kwakuwa nchi yetu huru na sio masikini tuliamua tuutekeleze kwa fedha zetu wenyewe," amesema Rais Magufuli.

"Mradi huu utazalisha umeme mwingi kuliko umeme wote uliozalishwa nchini tangu tumepata Uhuru, tutakuwa na umeme wa kutosha, wa uhakika na wa bei nafuu, ujenzi wa uchumi wa viwanda kokote Duniani ni lazima uwe na uhakika wa umeme wa bei nafuu, mradi huu ni suluhisho."
Source

Joto Kali Lakumba Ulaya

Joto kali limeendelea kukumba miji kadhaa kaskazini magharibi mwa Ulaya huku viwango vya joto vikizidi kuongezeka na kuweka rekodi mpya nchini Uholanzi, Ubelgiji, Ujerumani na Ufaransa.

Hapo jana Ujerumani ilirekodi kiwango cha juu zaidi cha nyuzi joto 42.6 katika mji wa Lingen, kaskazini magharibi mwa jimbo la Saxony.

Katika mji mkuu wa Ufaransa Paris, viwango vya juu vilifikia nyuzijoto 42.6. Idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini humo Meteo France imesema hicho ni kiwango cha juu zaidi kuwahi kurekodiwa.

Baadhi ya miji ya Uholanzi na Ubelgiji pia imekumbwa na joto kali na maafisa katika nchi kadhaa wametoa tahadhari.

Hata hivyo viwango vya joto, vinatarajiwa kushuka leo Ijumaa na kesho

Thursday, July 25, 2019

MAKONDA APOKEA MIL 23 KUFADHILI MATIBABU YA UPASUAJI WA MOYO KWA WATOTO 60 WENYE UHITAJI


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo Juni 25 amepokea zaidi ya Shilingi Milioni 23 kutoka kwa wadau ambao wameguswa na kampeni aliyoanzisha ya ufadhili wa matibabu ya upasuaji moyo kwa watoto 60 kutoka familia zenye hali duni.


Miongoni mwa Wadau waliomuunga Mkono  Makonda ni Mbunge wa Kibaha Mjini Mhe. Sylvester Koka ambaye amekabidhi hundi ya Shilingi milioni 10 kwa ajili ya matibabu ya watoto 5 huku Mkurugenzi wa Dorka Catering Bi. Dorothy Kansolele akichangia milioni 6 na  mkurugenzi wa kampuni ya Abe Professional Sound Bw. Abraham Ngomko akichangia Milioni 6 kwaajili ya matibabu ya watoto 3.

Akipokea fedha hizo Makonda amezikabidhi kwa uongozi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na kueleza kuwa zitasaidia kugharamia zaidi ya Watoto10 kwenye upasuaji wa awamu ya pili.

Aidha Makonda amewashukuru wadau wote wanaondelea kumuunga mkono kwenye kampeni hiyo inayolenga kuokoa maisha ya watoto ambao wangeweza kupoteza maisha kutokana na wazazi wao kushindwa kumudu gharama za matibabu.

Kwa upande wao wadau waliokabidhi fedha hizo wameeleza kuwa wataendelea kuunga mkono zoezi hilo kwa kuongeza fedha nyingine kwakuwa wanaamini kampeni aliyoanzisha Makonda ni njema na linapaswa kuungwa mkono na wadau mbalimbali ili kuokoa maisha ya watoto.

Itakumbukwa kuwa Makonda alitoa ahadi ya kufadhili matibabu ya upasuaji wa moyo kwa watoto 60 kwa muda wa miezi sita ambapo kila mwezi watatibiwa watoto10 na hadi sasa tayari amefanikisha matibabu ya watoto 30 kati ya 60 alioahidi.








Friday, July 19, 2019

UMEONA PICHA WATU WAKIONEKANA VIJANA AU WAZEE MTANDAONI?? .....SENETA KAAGIZA APP YA 'FACEAPP' ICHUNGUZWE



Seneta mwandamizi wa jiji la New York nchini Marekani    Chuck Schumer amewataka FBI kufanya uchunguzi kuhusu mtandao wa  FaceApp ambao umekuwa ukitumika kubadili picha ya mtu kumuonyesha akiwa mzee au kijana.


Hatua ya Shumer imekuja siku moja baada ya app hiyo kutumiwa na watu maarufu duniani wakiwamo wanamichezo, wasanii na viongozi wa siasa.
Kupitia barua aliyoiweka kwenye mtandao wa Twitter Julai 18, 2019 Schumer alisema kuwa app hiyo inamilikiwa na kampuni ya Urusi ambako ndiko yalipo makao makuu ya kampuni hiyo inachukua data za maelfu ya picha zinazotokana na utumiaji na kuwapo kwa hatari ya kudukuliwa habari zao.
Ikumbukwe kuwa vyombo vya habari vya Magharibi huhusisha chochote chenye historia ya kuwa cha Urusi huwa kinahusishwa na ujasusi.
 Kufuatia barua ya Schumer kampuni ya Wireless Lab ambayo ndiyo wamiliki wa app hiyo wameshatoa ufafanuzi  ikisema ingawa makao makuu ya app hiyo ni Urusi ila servers zinazotumika katika kupokea na kutengeneza picha mpya hazipo nchini Urusi.


Kampuni hiyo imenukuliwa na BBC ikisema kuwa wanachofanya ni kukusanya picha maalumu zilizotumwa kwa ajili ya kuzihariri.

Wednesday, July 17, 2019

Tanzania kuwasilisha Umoja wa Mataifa taarifa ya Mapitio ya Hiyari ya Utekelezaji wa Malengo Endelevu.

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akifuatilia ufunguzi wa mikutano ya Jukwaa la Juu la Kisiasa la Ngazi za  Mawaziri  chini ya Umoja wa Mataifa inayofanyika New York nchini Marekani. Kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt. John Jingu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo.

Waziri Mpango anatarajiwa kuwasilisha kwa mara ya kwanza taarifa ya Tanzania ya  Mapitio ya Hiyari ya Utekelezaji wa Malengo Endelevu.


Monday, July 15, 2019

Waziri Mbarawa Afanya Uteuzi Wa Wakurugenzi Watendaji Wa Mamlaka Za Majisafi Na Usafi Wa Mazingira




WAZIRI WA KILIMO AANZA ZIARA MKOANI SHINYANGA...AKUTANA NA WAKULIMA NA WAMILIKI WA VIWANDA VYA PAMBA


Na Marco Maduhu - Malunde1 blog Shinyanga.
Waziri wa Kilimo,Mhe. Japhet Hasunga amefanya ziara mkoani Shinyanga kwa ajili ya kutatua changamoto ya zao la pamba kwa wakulima ikiwemo ununuaji wa zao hilo ili wakulima waweze kuuza na kupata fedha zao kwa wakati.

Hasunga ameanza ziara yake ya siku tatu mkoani hapa kuanzia leo Julai 15 na atakamilisha ziara hiyo Julai 17, 2019, ambapo ameanza kwa kutembelea wakulima wa zao la pamba, wamiliki wa viwanda wa zao hilo kwa ajili ya kuzungumza nao, na kuwatia moyo kuwa serikali ipo pamoja nao katika kuhakikisha changamoto zilizokuwa zinawakabili hapo awali zinatatuliwa.
Amesema Serikali inatambua changamoto iliyokuwepo awali ya kusuasua ununuzi wa zao hilo pamoja na wakulima kukopwa fedha za mauzo ya zao hilo kupitia kwenye vyama vya msingi vya ushirika AMCOS, lakini kwa sasa tatizo hilo limetatuliwa ambapo hadi kufikia Julai 30 mwaka huu wakulima wote watanunuliwa pamba yao pamoja na kulipwa fedha zao.
"Changamoto iliyojitokeza ni kuwepo kwa mgogoro kati ya nchi ya China na Marekani na kusababisha kushuka kwa dola, hali iliyopelekea bei ambayo tuliipanga ya mkulima kununuliwa pamba yake kwa shilingi 1,200 kuonekana kwa wafanyabiashara kutawatia hasara na hivyo kuacha kununua pamba,"amesema Hasunga.
"Lakini kwenye kikao ambacho tumekaa juzi na waziri mkuu Kasimu Majaliwa mkoani Tabora tumekubaliana kwamba kutokana na kushuka kwa dola, wafanyabiashara waendelee kununua pamba kwa bei hiyo ya 1,200, lakini dola ikiendelea kuwa chini basi serikali italipa fidia ya hasara ambayo wataipata, kuliko kushusha bei ya pamba ambayo itamuumiza mkulima," ameongeza.
Pia amesema kutokana na kusuasua kwa masoko ya nje, serikali imejipanga kufufua viwanda vya ndani ambavyo huwa vinatumia malighafi ya zao hilo la pamba ili kuondoa changamoto hiyo ya kusu sua kwa ununuzi wa zao la pamba.
Katika hatua nyingine amewataka wakulima wa zao la pamba kujikita kulima kilimo chenye tija ambacho kitawapatia mavuno mengi, kuliko kuendelea kulima kwa mazoea na hatimaye kupata mavuno kidogo ambayo yatawapatia fedha kidogo na kushindwa kukua kiuchumi.
Naye Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Albert Msovela akisoma taarifa ya mkoa huo, amesema kwa msimu wa kilimo (2018-19) zao la Pamba mkoani humo limelimwa hekta 97,270 na kutarajia kuvuna Tani 48,435, na kubainisha changamoto iliyopo kuwa ni ukosefu wa fedha ya kununulia pamba kwenye Vyama vya Msingi vya Ushirika AMCOS.
Nao baadhi ya wakulima wa zao la Pamba,akiwemo Peter Samson kutoka kijiji cha Mwaweja wilayani Kishapu, ambao ni miongoni mwa wakulima ambao wamekwenda kuuza pamba yao kwenye kiwanda cha Afrishan Shinyanga Mjini, wamesema wamekwenda kuuza pamba yao hapo kutokana na vyama vya msingi vya ushirika AMCOS kutokuwa na pesa ya kuwalipa na hivyo kuwa azimu kuingia gharama tena ya usafirishaji na kupongeza juhudi hizo za Serikali za kutatua changamoto hiyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Msingi cha Ushirika Uzogole Shinyanga mjini Kulwa Chagu, amekiri kutokuwa na pesa ya kuwalipa wakulima pale wanaponunua pamba yao, na hivyo kushindwa kuendelea na zoezi la ununuaji wa pamba hiyo, ambapo kwa sasa wakulima wanaiuza kwenye kiwanda cha Afrishan  ambacho ndiyo mkombozi wao.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Waziri wa Kilimo,Mhe. Japhet Hasunga akizungumzia lengo la ziara yake mkoani Shinyanga kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack (kulia), kuwa ni kutatua changamoto zinazolikabili zao la Pamba likiwamo na suala la kusuasua kwa ununuzi wa zao hilo.Picha zote na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog
Awali Katibu Tawala wa mkoa wa Shinyanga,Mhe. Albert Msovela akisoma taarifa ya mkoa huo juu ya zao la pamba na kuelezea kuwepo na changamoto juu ya kusuasua kwa ununuaji wa zao hilo kwenye vyama vya Msingi vya Ushirika AMCOS kutokana na ukosefu wa fedha.
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje, akiipongeza Serikali kuitatua changamoto hiyo ya ununuaji wa zao la Pamba kwa wakulima.
Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Shinyanga Mhe. Azza Hilal Hamad akipongeza jitihada za Serikali za utatuzi wa changamoto hiyo ya zao la Pamba, na kuomba pia lifanyiwe kazi suala la kuzuia wafanyabishara wa zao la dengu kutoinunua kwa wakulima hadi AMCOS jambo ambalo litasababisha kutokea kama kwenye kilimo cha pamba, ambapo waziri alifuta agizo la kuzuiwa wafanyabishara hao kutonunua  zao hilo moja kwa moja kwa mkulima.
Waziri wa Kilimo.Mhe. Japhet Hasunga akiwasili kwenye kiwanda cha Afrishan Shinyanga Mjini ambacho kinanunua Pamba kutoka kwa wakulima licha ya wafanyabishara wengine kushindwa kuinunua Pamba hiyo kwa bei ya 1,200 mara baada ya kushuka kwa dola kwenye soko la nje kwa kuhofia ya kupata hasara.

Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga akiwa na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack (mwenye ushungi kichwani) pamoja na viongozi wengine wa mkoa huo, wakiangalia namna ununuaji wa Pamba unavyofanyika kwenye kiwanda hicho cha Afrishan kupitia vyama vya msingi vya ushirika AMCOS ambavyo na viwezeshwa fedha na kisha kuinunua kupitia kwao.

 
 Mkurugenzi mtendaji wa kiwanda cha Afrishan Shinyanga Mjini Ally Habshy, akizungumza ambapo amesema kwa sasa wananunua pamba hiyo kwa mkulima kwa bei ya shilingi 1,200 kupitia fedha zao za ndani, ambapo benki zilisuasua kuwapatia fedha na kupongeza jitihada hizo za Serikali za kutatua changamoto hiyo ya ununuzi wa zao la Pamba pamoja na wao wafanyabiashara kuwa watakopeshwa fedha za ununuaji wa pamba.
Ununuaji wa zao la pamba ukiendelea nje ya kiwanda cha Afrishan Shinyanga mjini.

Wakulima wakiendelea kuleta Pamba yao kuuzwa kwenye kiwanda hicho cha Afrishan Shinyanga mjini ambapo wengine wanatoka Igunga na Mwanza kwa ajili ya kuuza Pamba yao na kupata fedha taslimu.
 
 Pamba ikiwa imemwagwa chini.
 
 Wakulima wa zao la Pamba wakiwa kwenye kiwanda cha Afrishan Shinyanga Mjini wakiuza Pamba yao, mara baada ya vyama vya msingi vya ushirika AMCOS kukosa fedha ya kuwanunulia pamba hiyo.
 
 Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiwataka wakulima hao wa Pamba kutoiweka Pamba chini ambapo inachafuka bali waiweke sehemu ambapo ni pasafi chini ya matulubai na kutoipotezea ubora wake.
 
 Waziri wa Kilimo,Mhe. Japhet Hasunga akiwataka wakulima, kuwa wavumilivu wakati Serikali ikilitatua tatizo la ununuzi wa zao hilo ambapo hadi kufikia Julai 30 fedha zitakuwa zimepatikana na Pamba yote ya mkulima itanunuliwa pamoja na kulipwa pesa zao zote.
 
 Wakulima wa Pamba wakisikiliza ujumbe kutoka serikalini juu ya utatuzi wa changamoto hiyo ya ununuzi wa zao la Pamba kupitia kwenye vyama vya msingi vya ushirika AMCOS.
 
Awali mkuu wa wilaya ya Shinyanga ,Mhe.Jasinta Mboneko mkono wa kulia akimkaribisha Waziri wa Kilimo,Mhe. Japhet Hasunga alipowasili mkoani Shinyanga kwa ajili ya ziara ya siku tatu ya kutatua changamoto ya zao la pamba.

Waziri wa Kilimo,Mhe. Japhet Hasunga akifurahia jambo na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack na mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko mkono wa kulia.


Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog

Yanga Yaleta Beki Spesho wa CAF

UONGOZI wa Yanga umekamilisha taratibu za usajili wa beki wa kushoto wa Rayon Sports ya Rwanda, Ericky Rutanga anayejiunga na timu hiyo kwenye usajili wa dirisha dogo Ligi Kuu Bara maalum kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Awali, Yanga iliwahi kumfuata beki huyo na kuzungumza naye na kushindwa kufikia muafaka mzuri na kusalia Rayon huku Gadiel Michael aliyekuwa akicheza nafasi hiyo, naye akitimkia Simba.

Yanga mara baada ya kushindwana na beki huyo haraka ikakamilisha usajili wa beki wa Singida United, Muharami Salum maarufu kwa jina la Marcelo ambaye tayari yupo kambini mkoani Morogoro.

Yanga msimu ujao itashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika iliyo chini ya Shirikisho la Soka Afrika 'Caf' ambapo itaanzia hatua ya awali iliyopangwa kuanza Agosti 9, mwaka huu na michuano hiyo itamalizika Mei 30, mwakani.

Hivyo basi kama itafanikiwa kushinda mechi za awali za mtoano na kutinga hatua ya makundi, basi itapewa nafasi ya kuongeza wachezaji. Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Jumamosi, Rutanga rasmi atajiunga na Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo akiwa kama mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika.

Habari zinasema kwamba beki huyo atajiunga na Yanga katika usajili huo kuchukua nafasi ya mchezaji wa kigeni, Klaus Kindoki aliyekataa kutolewa kwa mkopo huku akisubiria mkataba wake kumalizika kipindi hicho.

"Rutanga tayari amemalizana na Yanga kwa asilimia 70 na anajiunga nayo kwenye usajili wa ligi na atakuja kuchukua nafasi ya Kindoki ya wachezaji wa kigeni.

"Kama unavyofahamu nafasi za wachezaji wa kigeni tayari zimefikia kumi kama idadi ambao TFF wanaitaka, hivyo wakati Kindoki anaondoka baada ya mkataba wake wa miezi sita kumalizika na Rutanga atakuwa amekuja Yanga.

"Kikubwa uongozi unataka kuwa na mchezaji mwenye uzoefu na uwezo wa michuano ya kimataifa ambayo Yanga watashiriki, mwaka huu," alisema mtoa taarifa huyo.

Sunday, July 14, 2019

Wachezaji wa Yanga wazuiwa kuzungumza

Kocha Msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila amewazuia wachezaji wake kuzungumza chochote na waandishi wa habari.

Mwandila amewazuia wachezaji wake na badala yake amewataka waelekeze nguvu zao zote mazoezini kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Yanga inaendelea na mazoezi kujiandaa na tamasha la Wiki ya Mwananchi litakalofanyika Uwanja wa Taifa August 4 2019.

Tamasha hilo litafanyika ambapo timu hiyo itacheza mchezo wa kirafiki na AS Vita

Saturday, July 13, 2019

Watafiti wabaini mtindo wa Mwanamke kuwa juu ya mwanaume wakati wa tendo la ndoa ni hatari kwa wanaume!


Wanasayansi nchini Brazil wamefanya utafiti ili kubaini ni mtindo upi katika ufanyaji tendo la ndoa ulio hatari zaidi kwa mwanaume.

Kwa mujibu wa utafiti huo, mtindo ambao mwanamke anakuwa juu ya mwanaume ndio hatari zaidi na huwa na risk kubwa zaidi ya kusababisha hata kuvunjika kwa uume.

Wanasayansi hao wanasema:
Pindi mwanamke anapokuwa juu, mara zote hucontrol movement na uzito wote wa mwili wake ukitua kwenye uume uliosimama na kushindwa kuzuia pale uume unapokuwa umeingia vibaya kwasababu madhara huwa ni madogo kwa mwanamke bila maumivu lakini ni mabaya kwa mwanaume.



"…Pindi mwanaume anapokuwa akicontrol movement, ana nafasi kubwa ya kuzuia kutokana na uume wake kuwa sehemu mbaya na hali inayopelekea kusikia maumivu na hivyo kupunguza hatari."

Vanessa Mdee achaguliwa kuwa Jaji East Africa's Got Talent

Msanii wa Muziki, Vanessa Mdee huwa hataki kupitwa na kila fursa inayokatisha mbele yake hasa linapokuja suala la kuingiza mkwanja.

Hit maker huyo wa 'Moyo', amefanikiwa kupata dili la kuwa Jaji kwenye shindano la East Africa's Got Talent  kwa mwaka huu. Shindano hilo linatarajia kuruka hewani tarehe 4 mwezi wa 8.

Akizungumza leo mratibu wa shindano hilo, Lillias Bode, ameseama shindano hilo litaanza kuonyeshwa kuanzia mwanzoni lilipoanza kisha mwezi wa 10 kutakuwa na grand finale na mshindi atachaguliwa na wananchi kupitia kura zao.

Aunguzwa sehemu zake za siri na mkewe

Baba wa watoto kumi huko nchini Nigeria, aitwae Malayu Ibrahim, ameunguzwa sehemu zake za siri na mke wake baada ya kumwambia anataka kuongeza mke wa pili.


Baba huyo alikimbizwa hospitali usiku wa jana Julai 12, 2019, baada ya kurudi nyumbani kwake na kumwagiwa maji ya moto na ameeleza kuwa,

"Nilirudi nyumbani na kumueleza mke wangu nataka kuongeza mke wa pili ambaye tutakuwa pamoja katika maombi na sala, baada ya kumueleza vile alionekana mwenye furaha na tuliishi kwa amani pamoja na sikuona mabadiliko yoyote kwake, lakini kuna siku nilirudi na nyama nyumbani, akaenda kuchemsha kisha alirudi na maji ya moto na kunimwagia sehemu zangu za siri kuanzia mapajani."

Pia Malayu Ibrahim akaongeza kwa kusema yeye kazi yake ni mwalimu wa shule ya msingi, yeye pamoja na mkewe wamebahatika kupata watoto kumi mpaka sasa.

RPC SHINYANGA - 'MSHIRIKI SHINDANO LA MISS SHINYANGA 2019 ALIPIGWA NGUMI,KUCHANIWA NGUO'


Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Richard Abwao

Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limethibitisha taarifa za Mwanamitindo Nicole Emmanuel (19) kupigwa na waandaaji wa Mashindano ya Ulimbwende 'Miss Shinyanga 2019' baada ya mrembo huyo kudai gharama ambazo alitumia katika Shindano la Miss Shinyanga 2019.

Kwa Mujibu wa Taarifa kwa Vyombo vya habari iliyotolewa leo Jumamosi Julai 13,2019 na Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Richard Abwao, tukio hilo la shambulio la kudhuru mwili limetokea Alhamis Julai 11,2019 majira ya 12 jioni katika maeneo ya Nedman hotel iliyopo Tambuka reli katika Manispaa ya Shinyanga.

"Mlalamikaji aitwaye Nicole d/o Emanuel (19),Mwanamitindo, Mkazi wa Dar es salaam, alishambuliwa kwa kupigwa ngumi, mateke na kuburuzwa chini kisha kuchaniwa nguo na kusababishiwa maumivu mwilini na watuhumiwa waliotajwa kuwa ni Mkurugenzi Richard Luhende na Meneja aliyetajwa kwa jina moja la George wote  wa Makumbusho Intertainment",ameeleza Kamanda Abwao.

"Tukio hilo limetokea baada ya mlalamikaji kuwadai watuhumiwa nauli na gharama ambazo alitumia katika Shindano la Miss Shinyanga 2019. Watuhumiwa wawili waliotajwa ni Mkurugenzina Meneja wote wa Makumbusho Intertainment ",amesema Kamanda Abwao. 

Kamanda Abwao amesema watuhumiwa bado hawajakamatwa.

Awali siku ya Alhamis akizungumza na waandishi wa habari Nicole Emmanuel alisema alifikwa na majanga hayo wakati akidai fedha zake nauli shilingi 70,000/= ili arudi Dar es salaam.

Nicole aliwataja waandaji wa Shindano hilo waliompiga kuwa ni Meneja Mkuu wa Makumbusho Entertainment,George Foda na Mkurugenzi wa Makumbusho Entertainment Richard Luhende.

Hata hivyo Meneja Mkuu Makumbusho Entertainment George Foda,aliyekuwa anasimamia mashindano ya Miss Shinyanga 2019 ,alikanusha taarifa za kumpiga mrembo huyo huku akikiri kwamba ni kweli mrembo huyo alikuwa anawadai pesa na katika kudai pesa hizo alianza kuleta fujo hotelini kutumia lugha chafu na kugonga geti ndipo wakamchukua na kumpeleka kituo cha polisi.

Na Kadama Malunde -Malunde1 blog.


Source

News Alert : TAZAMA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2019, UALIMU 2019


Matokeo ya Kidato cha Sita 2019 yametoka....


1.Kutazama matokeo ya Kidato cha Sita  <<BOFYA HAPA>>

2.Kutazama Matokeo Ya Mtihani Wa Ualimu 2019  <<BOFYA HAPA>>



Source

VIDEO: Shule iliyoongoza kidato cha sita , Mwalimu Mkuu afunguka



Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kisimiri, Valentine Tarimo, iliyoshika namba moja katika matokeo ya Kidato cha sita 2019 amesema kujituma na kufanyakazi kwa ari, ikiwa ni pamoja na kuweka mipango thabiti, ndiyo chanzo kikubwa cha kuleta ufaulu huo na matokeo walioyapata siyo malngo yao 

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI...USIKOSE KU-SUBSCRIBE

Afikishwa Mahakakamani Baada ya Kughushi Cheti cha Ndoa

Aliyekuwa mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Wilaya ya Ilala, Norah Waziri maarufu Nora Mzeru amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na shtaka la kughushi cheti cha ndoa.
Wakili wa Serikali, Benson Mwaitenda amedai leo Ijumaa Julai 12, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi, Anifa Mwingira kuwa Februari 4, 1995 jijini Dar, es Salaam kwa nia ya kudanganya mshtakiwa huyo alighushi cheti cha ndoa chenye usajili namba 00040078.

Amedai kuwa alifanya hivyo kwa nia ya kuonesha kuwa alifunga ndoa na Silvanus Mzeru (marehemu) Februari 4, 1995 katika kanisa Katoliki Mburahati wakati akijua si kweli.
Mshtakiwa huyo baada ya kusomewa shtaka lake hilo, amekana na kudai Mzeru ni mumewe.

Upande wa mashtaka umedai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Baada ya kusomewa shtaka hilo mawakili wanaomtetea mshtakiwa, Mtubika Godfrey na Juma Nyamgaruri waliiomba mahakama kumpatia dhamana mteja wao kwa sababu shtaka linalomkabili kwa mujibu wa sheria linadhaminika.

Baada ya kusikiliza hoja hiyo hakimu huyo aliahirisha kesi hiyo namba 365 ya mwaka 2019 hadi Julai 17, 2019 itakapotajwa tena huku mshtakiwa akiachiwa kwa dhamana
Source

Watu wasio na vibali vya kuishi Marekani kuanza kusakwa


Utawala wa Rais Donald Trump unapanga kuanza utekelezaji wa operesheni ya nchi nzima inayolenga familia za wahamiaji, licha ya kupingwa vikali na Democrats.

Operesheni hiyo inasemekana kwamba inaweza kuanza kutekelezwa mwishoni mwa juma hili, baada ya kuahirishwa na Trump mwishoni mwa mwezi uliopita.

Inalenga kuwafuatilia watu walio na amri za mwisho za kurejea katika nchi zao, zikiwemo familia za wahamiaji ambazo kesi zao zilikuwa zikifutiliwa kwa haraka na majaji katika jumla ya miji 10 kama vile Chigaco, Los Angeles, New York na Miami.

Hatua hizo zimeibua hasira na wasiwasi miongoni mwa wanaharakati wa haki za wahamiaji na wabunge.

Operesheni hiyo ni sawa na ile iliyowahi kufanywa mwaka 2003 na kisha kuwakamata watu wengi wasio na vibali.

Trump alitangaza kwenye Twitter mwezi uliopita kwamba operesheni hiyo itakuwa ni mwanzo wa kuwafukuza mamilioni ya watu wanaoishi Marekani kinyume cha sheria.
Source

Siri za kudumu katika mahusiano ya kimapenzi

Watu wengi wanatamani kudumu kwenye uhusiano lakini bahati mbaya huwa inashindikana. Mtu ambaye hadumu kwenye uhusiano, si kwamba anakuwa hapendi bali inatokea tu kutokana na sababu mbalimbali. Inatokea kwa sababu, huenda pengine ni kutokana na tabia zake au za mwenzake. Mfano, yawezekana akawa na 'mdomo' sana, yawezekana akawa mbinafsi. Au ana hulka ya ugomvi lakini mwenzake hana. Yawezekana akawa na tabia za kuchepuka.

Yawezekana tatizo likawa la mwenzake, Akawa ana tabia zisizompendeza mpenzi wake. Yawezekana akawa mbinafsi, yawezekana akawa na hasira kali au akawa na tabia mbaya ambazo mwenzake ameshindwa kuzivumilia. Kikubwa tu, watu hushindwa kudumu penzini kwa kupishana mambo mbalimbali. Kuanzia tabia, mtindo wa maisha na wengine kutoelewana dhumuni la safari yao.

Mara kadhaa nimekuwa nikisisitiza, unapoanzisha uhusiano na mwenzako lazima kwanza mjue lengo au madhumuni ya huo uhusiano wenu. Mwanamke ajue kwamba uhusiano wao ni wa muda mrefu au wa muda mfupi.

Una malengo au hauna? Vivyo hivyo mwanaume, kwa kinywa chake, kutoka moyoni athibitishe lengo na madhumuni ya uhusiano wake ili mwenzake ajue kabisa kwamba yupo kwenye uhusiano wa aina gani. Baada ya hapo ndio muanze safari.

Na hii ndio siri ya maisha. Ndiyo siri ya uhusiano wote. Mkishajua madhumuni ya safari yenu, kinachofauta ni kukipa umuhimu kipaumbele chenu. Pamoja na kujua kwamba mtakumbana na changamoto mbalimbali katika safari yenu lakini mnapokumbuka umuhimu wa safari yenu, mnatiana moyo. Mnapokutana na magumu yasiyokuwa na mfano, hamkati tamaa. Mnainuka na kusimama tena. Kila mmoja anapomuona mwenzake kakosea, anambebea makosa yake na kumsamehe kulingana na uzito wa safari yao.

Ni kama kiapo. Mnaapa kutoachana, mnaapa kuianza safari pamoja na kuimaliza pamoja. Kifo pekee ndicho kitakacho watenganisha kama kweli wote wawili mtakuwa na nia moja, dhumuni moja la kujenga uhusiano wenu hudumu. Wapenda-nao mnapaswa kuzungumza lugha moja. Kwa pamoja mnapaswa kuazimia namna ambavyo safari yenu mnataka iwe. Mathalan, mnataka muishi maisha ya aina gani? Mnataka kufikia hatua au kufunga ndoa ya aina gani?

Ili muweze kufanikisha safari yenu ya ndoa, mnapaswa muishije? Narudia tena, kusikilizana ndio jambo kubwa sana katika safari yenu. Asiwepo mtu wa kumdharau mwenzake. Mwanamke, amthamini mwenzi wake kuliko mtu mwingine yeyote. Mwanaume, amthamini mwanamke wake katika kiwango cha hali ya juu. Asikubali kuyumbishwa na tamaa za kimwili, asirudishwe nyuma na maneno ya watu na kisiwepo kizingiti chochote cha kumkatisha tamaa.

Kwa vyovyote itakavyokuwa, suala lenu la 'utaifa wa uhusiano' ndio mlitangulize mbele. Muishi mkijua kwamba, uhai wa penzi lenu mmeushikilia nyinyi wawili. Mna kila sababu ya kulilinda penzi lenu kwa gharama yoyote kwani mafanikio ya uhusiano wenu, ni mafanikio ya wote wawili.

Mpendane. Mheshimiane katika kiwango cha juu. Kila mmoja atambue majukumu yake. Mwanamke amtii mwanaume, amheshimu. Mwanaume ampende sana mwanamke. Asimdharau, atambue thamani yake katika nyumba licha ya kwamba mwanaume ndio kichwa cha familia.

Mwanaume asivimbe kichwa. Amshirikishe mwenzake katika masuala yanayohusu maisha na uhusiano wao. Hata ikitokea mmepishana kauli, shukeni. Kila mmoja aongozwe na busara kwamba, ipo njia mbadala ya kuwavusha kwenye mabishano hayo bila kusababisha mtafaruku.

Mwanamke usiwe mzungumzaji sana kwa mwanaume. Mpe faraja pale inapobidi. Farijianeni katika vipindi mbalimbali mnavyopitia. Muanguke na kuinuka pamoja. Asiwepo mmoja kati yenu achukulie changamoto ya mwenzake kama si yake.

Kila mmoja aguswe na matatizo ya mwenzake. Mnapokuwa kwenye furaha, kwa pamoja pia mfurahi. Msiwe na tamaa. Tengenezeni maisha yenu mnayoyataka. Kwa pamoja mtakuja kufurahia ushindi wa safari yenu.

Kanuni za kilimo bora cha miwa

Kilimo cha miwa ni kilimo chenye tija kwa mkulima, kilimo hiki kinaweza kufanywa na mtu yeyote yule aidha awe ameajiriwa au laaa! Jambo la msingi ni kuhakikisha anajitoa kikamilifu katika kuhakikisha  unawekeza akili yake katika kulima kilimo hiki.

Kuna aina kuu 2 za miwa katika mbegu za miwa zilizo shamili sana ambazo ni:

1. Bungala

2. Miwa myekundu.

Unachotakiwa kufanya katika kulima kilimo hiki ni, Kwanza kabisa tafuta ekari moja ya shamba kisha anza maandalizi lakini zingatia kupuguza matumizi makubwa ya pesa kadri iwezakanavyo yaani kwa shughuli nyinginezo ambazo unaweza kuzifanya mwenyewe ni vyema ukazifanya ili kupunguza matumizi makubwa ya pesa mfano kulima, kupiga dawa, kupalia n.k

Tafuta mbegu ya miwa ya Bungala miwa hii ni laini sana na ni rahisi kuichana kwa kutumia meno, baada ya kupata miwa hii kata vipande vipande vya pingili tatu tatu .Kumbuka kwamba miwa ni rahisi sana kushambuliwa na mchwa pale tu inapokuwa imepandwa.

Ili kuzuia isiliwe na mchwa nenda katika maduka ya kilimo na ununue moja wapo ya madawa yafuatayo:-

1. TAP 4% GR Tumia gram 100 za dawa kwa lita takribani 20 za maji kisha nyunyizia katika mashina ya miwa.

2. Taniprid 25 WG. Tumia gram 100 za dawa kwa lita takribani 20 za maji au pia unaweza kuweka kijiko kimoja cha chai katika kila shina.

3. Imida Gold Mls 20 kwa lita 20 za maji na unyunyizie shinani.

 4. Gammalin 20. Tumia gram 100 kwa lita takribani 20 za maji. Na unyunyizie katika vipande vya miwa au chovya vipande vya miwa katika maji hayo yaliyo na Gammalin 20 na ndipo uende ukavipande shambani kwako.

5. Gladiator FT.

6. Stom

Mambo yakufanya:
Zingatia kama utatumia aidha Gladiator au Gammalin au Stom, chukua ndoo ya maji ya lita 20 kisha uichanganye na dawa uliyoinunua kisha chukua kipande cha muwa na kukizamisha ndani ya maji hayo na baadae uende kuipanda shambani kwako, hivyo uewezekano wa miwa yako yote kuote utakuwa ni mkubwa sana maana shida kubwa ni mchwa na hapo tayari utakuwa umeidhibiti.

UPANDAJI WA MIWA
Hakikisha unapokuwa unapande miwa yako acha nafasi ya mita moja (1m) kati ya mche na mche pia hakikisha una acha nafasi ya mita moja (1m) kati ya mstari na mstari. Kumbuka awali tulisema katakata muwa wako kupata vipande vilivyo na vipingili vitatu vitatu, hivyo sasa unapokuwa unapande miwa hii hakikisha hizo pingili zote 3 zimezama ndani ya ardhi na kipande kidogo tu ndio kibakie juu ya uso wa ardhi na mche wako huo unapoutumbukiza kwenye ardhi uwe umelala wastani wa nyuzi 30.

Zile pingili katika muwa wako kumbuka ndipo sehemu hasa miwa inamokuwa inachipuka na kuota. Mantiki ya kuacha nafasi kubwa kati ya mche na mche ni kwa sababu hilo shina lako moja ulilolipanda linaweza likachipua vijimiwa vingine zaidi hata ya ishirini kama ukiliacha shina liendelee kuzaa tu kwa kadri linavyotaka na hatimaye shamba lako litakuwa msitu hata usiopitika.

Lakini kibaya zaidi ni kwamba miwa yako itakosa afya njema na mwisho wa siku miwa yako haitakuwa bora hata bei haitakuwa nzuri pindi utakapoamua au wakati wa kuuza utakapofika. Hivyo unashauriwa kuacha miwa kati ya tano mpaka kumi lakini mfano ukiacha miwa mitano katika shina moja ni dhairi hewa na mwanga vitakuwa vya kutosha shambani lakini hata chakula na virutubisho vingine kwa miwa hiyo vitakuwa lukuki na sio vya kung'ang'aniana hivyo mwisho wa siku utapata miwa mirefu na minene ambayo sokoni itakuwa na mvuto mkubwa kwa wateja.

Mfano chukulia kwamba umelima ploti ndogo tu ya upana mita 50 kwa urefu mita 70, kumbukumbu namna ya upandaji miwa kama tulivyozungumza hapo awali umbali wa mita moja moja kwa kila shina. Hivyo kwa ploti ya shamba hili utakuwa na miche au mashina uliyopanda kiasi cha 70×50=3500 (mashina elfu tatu na mia tano) sasa chukulia kwa hesabu rahisi kwamba kila shina umeruhusu miwa mitano tu ndio ikuwe pale maana yake kwa mashina 3500 utazidisha mara 5 ambapo itakuwa 3500×5= 17,500 hiyo ndio itakuwa jumla ya miwa itakayovunwa shambani.

Kwa tafiti zilizofanywa zinaonesha kama hautaki shida na unahitaji pesa ya haraka haraka sana huko huko shamba, basi unaweza ukajumlisha miwa yako kwa bei ya chini sana yaani tukadilie vile kwamba tunahitaji pesa ya haraka so tuuze muwa mmoja kwa bei ya jumla ya 300 hivyo jumla ya pesa utakayoipata itakuwa 17,500 × 300 = 5,250,000 (milioni tano laki mbili na nusu). Hiyo ni pesa ya haraka haraka huko huko shambani .

Ila kama ukiweza kusogea zaidi na kuuza kwa faida maana kama umeweza kupigana mpaka kuweza kuikuza ni dhairi kwamba unastahili kupata faida iliyo njema kwako hivyo ni muhimu kuangalia masoko yamekaaje pande zote za miji, ila kama utaweza kuifikisha Dar es Salaam ambako kiuhalisia soko lake ni kubwa sana .

Kama ukienda Kariakoo bei ya rejareja kwa muwa aina ya bungala wenye wastani wa urefu mita moja na robo bei yake ni 5,000 lakini ukienda mtaani kwa muwa huo huo aina ya bungala mfupi kidogo bei yake inakwenda mpaka 3,500 hivyo chukulia kwamba umeweza kufikisha Dar es Salaam huo mzigo wako wa miwa, hivyo mapato yako kama utaamua uuze kwa bei ya jumla ya 1,500 kwa kila muwa hivyo kiasi cha fedha utakachokipata kitakuwa ni sawa na idadi ya miwa yako zidisha bei ya kujumlishia yaani ingekuwa 17,500 × 1,500= 26,250,000 hii ni pesa utayoipata kwa halali kabisa wala haujamzulumu mtu.

Hapo umelima ploti ndogo tu, sasa chukua pengine umelima ekari moja na kwa shamba la miwa ekari moja kiwango cha chini kabisa cha wewe kuvuma miwa yako ni jumla ya miwa 24,500. Sasa chukulia kama umeweza kuipeleka Dar es Salaam maana yake utapata jumla ya 24,500 × 1,500= 36,750,000. Sasa mfano ndo ukalima ekari 4 hadi 5 hapo ni hakika unatoka katika kundi la uchumi wa chini na kuingia katika uchumi wa kati. Jamani bado hatujachelewa kungali bado fursa ziko kinachohitajika hapa ni kuthubutu tu, Mungu akubariki unapoyatafari haya lakini pia pindi ukifanikiwa usimsahau Mungu maana yeye ndiye nguzo ya mafanikio yako yote.

Friday, July 12, 2019

Bwana MPYA wa Zari Adaiwa Kumdai Mrembo POSHY Qeen, Poshy Afunguka

POSHY QUEEN AFUNGUKA KUDAIWA NA BWANA WA ZARI
July 12, 2019 by Global Publishers


DAR ES SALAAM: Modo matata Bongo ambaye jina lake lilishika kasi ya umaarufu kutokana umbo lake la kiuno cha nyigu, Jacqueline Obeid 'Poshy Queen' amemfungukia anayesemekana ni bwana mpya wa mwanamama mjasiriamali wa Uganda, Zarinah Hassan 'Zari The Boss Lady', King Bae.

Poshy ameliambia Gazeti la Ijumaa kuwa anashangazwa na madai kuwa jamaa huyo anamdai.

Poshy ameweka wazi kuwa, yeye na King Bae waliwekeana dau wakati Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars na Kenya zinacheza kwenye Michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon) hivyo walikubaliana kama Tanzania ingefungwa, Poshy angemlipa jamaa huyo kiasi fulani cha fedha, lakini hakufanya hivyo.

"Unajua ule ulikuwa ni utani tu, watu hata hawakuelewa ananidai nini, basi kila mmoja alishadadia, lakini ni mambo ya mpira na si kitu kingine kwa sababu tuliwekeana dau hivyo watu wasitokwe povu, wakajiuliza ninadaiwa nini mimi mpaka kwenye mitandao," alisema Poshy ambaye hivi karibuni alidaiwa kumpora jamaa huyo kutoka kwa Zari.
Stori: IMELDA MTEMA, IJUMAA

Mpoki Hamnazo KICHWANI Afunguka "Nikiachana na Mwanamke, Nachukua Kila Kitu Changu"


Mchekeshaji maarufu ambaye pia ni mtangazaji wa kipindi cha Ubaoni kinachoruka kupitia Radio Efm, Sylvester Mujuni almaarufu Mpoki amesema akiachana na mwanamke ambaye amekuwa naye kwenye mahusiano basi anamnyang'anya vitu vyote alivyomnunulia.

Mpoki amesema hayo wakati akifanyiwa mahojiano katika kipindi cha Block 89 kinachoruka kupitia Radio Wasafi FM na kuongeza kuwa anafanya hivyo ili mwanaume atakayeingia katika mahusiano na mwanamke mwingine naye aanze upya kama yeye alivyomkuta mwanamke huyo.



Majibu yamekuja baada ya kuulizwa kama anayeweza kurudisha fedha ikiwa ametumiwa kwa bahati mbaya na mwanamke aliyeachana naye, ambapo alisisitiza kuwa huwa hana masihara kwenye masuala ya hela.

"Kwanza mimi sijawahi kuwa na mahusiano na mwanamke ambaye ananipa hela, sana sana wao ndiyo wanataka kutoka kwangu," amesema Mpoki.

Kuhusu sababu ya yeye kukubali kuteuliwa kuwa Mshereheshaji wa hafla ya kusherehekea siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mama Diamond na mpenzi wake Diamond, Tanasha Donna, Mpoki amesema ni heshima aliyopewa na Diamond baada ya kumfuata na kumuomba ahodhi tukio hilo kubwa.
Source

Peter Crouch atangaza kustaafu kucheza soka

Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza Peter Crouch ametangaza kustaafu kucheza soka akiwa na miaka 38.

Crouch ambaye amefunga jumla ya magoli 108 kwenye ligi Kuu ya Uingereza katika michezo 468 akiwa na vilabu saba tofauti na kufanikiwa kucheza timu ya taifa ya Unigereza michezo 42 na kushinda magoli 22.

Vilabu alivyowahi kuchezea ni pamoja na Tottenham, QPR, Portsmouth, Aston Villa, Southampton, Liverpool, Stoke na Burnley.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...