Sunday, March 31, 2019

SIMBA SC WAITWANGA MBAO FC 3 - 0...BOCCO ATUPIA 2,KAGERE 1



Simba SC imeendeleza furaha kwa mashabiki wake baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mbao FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Ushindi huo uliotokana na mabao mawili ya Nahodha John Raphael Bocco na Mnyarwanda Meddie Kagere unaifanya Simba SC ifikishe pointi 57 baada ya kucheza mechi 22, lakini inabaki nafasi ya tatu nyuma ya Azam FC yenye pointi 59 na Yanga SC pointi 67 baada ya wote kucheza mechi 28.

Bocco, mmoja wa wachezaji waliokuwemo kwenye kikosi cha Tanzania kilichokata tiketi ya Fainali za Kombe la Mataifa uya Afrika mwaka huu nchini Misri wiki iliyopita, alifunga bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 25 akimalizia krosi ya beki wa kushoto Mohammed Hussein 'Tshabalala'.

Bao hilo lilidumu hadi mapumziko na kipindi cha pili Bocco akafunga bao la pili kwa penalti dakika ya 59 baada ya beki Peter Mwangosi kuanguka na kuunawa mpira uliopigwa na kiungo Muzamil Yassin.

Kagere, mwenye asili ya Uganda na kinara wa mabao wa Simba SC msimu huu, akafunga bao la tatu kwa penalti pia dakika ya 79 baada ya yeye mwenyewe kuangushwa na Hamimu Abdulkarim wa Mbao FC.

Kipa Deogratius Munishi 'Dida' aliyeanza badala ya majeruhi Aishi Manula alidaka kwa ustadi mkubwa na kumaliza dakika 90 bila kuruhusu hata bao la kuotea. 

Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Deogratius Munishi 'Dida', Zana Coulibaly, Mohammed Hussein 'Tshabalala', Erasto Nyoni, Pascal Wawa, James Kotei, Haruna Nioyonzima, Muzamil Yassin, John Bocco/Said Ndemla dk73, Meddie Kagere/Adam Salamba dk86 na Mohamed 'Mo' Ibrahim/Hassan Dilunga dk61.

Mbao FC; Metacha Mnata, Erick Murilo, Amos Charles, David Mwassa, Peter Mwangosi, Said Said, Ally Mussa, Herbert Lukindo/Robert Ndaki dk63, Ibrahim Njohole/Zamfuko Elias dk75, Hamim Abdulkarim na Pastory Athanas.

Chanzo -Binzubeiry blog

Mtanzania ateuliwa na kiongozi mkuu wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis kuwa balozi wake nchini New Zealand

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amemteua Askofu Novatus Rugambwa mzaliwa wa Parokia ya Ishwandimi, Bukoba vijijini, Jimbo katoliki la Bukoba kuwa balozi wa Papa nchini New Zealand. Askofu Novatus Rugambwa Awali Askofu Novatus Rugambwa alikuwa balozi wa Papa Francis nchini Honduras. Askofu Rugambwa ni moja ya Watanzania wakatoliki ambao wamewahi kupata cheo kikubwa …

The post Mtanzania ateuliwa na kiongozi mkuu wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis kuwa balozi wake nchini New Zealand appeared first on Bongo5.com.


Source

Haya ndio Madhara ya Kufanya Mapenzi Kupita Kiasi


Katika hali ya kawaida kufanya mapenzi kuna faida nyingi, lakini linapokuja suala la kuzidi kiasi tunapata matatizo ya msingi ambayo huleta madhara kwa watu wanaoendekeza sana ngono.

Kuna watu ambao hawezi kulala bila kufanya mapenzi na huku wengine wakikosa uwezo wa kuvumilia hata kwa siku mbili au tatu.

Hilo linaweza kuwa jambo jema kwa upande mwingine, lakini uchunguzi unaonyesha kuwa watu wengi kati ya watu wanaolalamika kupoteza hisia za kimapenzi hutoka katika kundi la watu wapenda ngono.

Pamoja na tatizo hilo, yapo madhara mengine mengi ambayo mtu asiyekuwa na kiasi katika tendo la ndoa anaweza kukabiliana nayo, hivyo ni vema tukajifunza ili tusiwe watu wa kuendekeza miili kiasi cha kulazimika kufanya mapenzi kila tunapokutana.

Yafuatayo ndio madhara yenyewe;

1. Kupoteza hamu ya tendo la ndoa.
Watu wenye pupa za kufanya mapenzi hupoteza haraka hisia za kimapenzi kwa wapenzi wao kutokana na sababu za kisaikolojia zinazoweza kujitokeza wakati wa ufanyaji wa tendo la ndoa mara kwa mara.

Sababu hizo zinaweza kuwa ni pamoja na zile za kumzoea mwenza kiasi cha kukosa msisimko hata anapomuona akiwa mtupu.

Aidha kukinai haraka staili za kimapenzi kunatajwa kujitokeza kutokana na kukutana mara kwa mara kwa aina zile zile za mapenzi na pengine sehemu moja, kitanda kimoja na chumba kile kile, jambo ambalo linaweza kumfanya mhusika asione jipya kutoka kwa mwenza wake na hivyo kupoteza hamu naye na kuhisi kama hawezi tena kushiriki tendo la ndoa kikamilifu.

2. Kuujaza mwili tamaa kubwa.
Tabia ya kufanya mapenzi mara kwa mara huongeza uzalishaji wa homoni mwilini na kuufanya mwili uwe na msukumo mkubwa wa kutaka kuridhishwa kwa tendo la ndoa bila kukosa na hivyo kumfanya mhusika asiwe mtu mwenye uwezo wa kuzuia tamaa na kukosa chaguo la nani wa kufanya naye mapenzi na kwa wakati gani?

Watu wanaojiendekeza katika kufanya mapenzi mara kwa mara ndiyo wale ambao kila wanayemtazama barabarani humtamani bila kujali hadhi yake.

Hawa ndiyo wanaobaka, kusaliti ndoa zao hata kwa watumishi wa ndani au kufanya mapenzi na watoto wao wa kuwazaa kwa vile akili zao huwa zimeathirika kwa tamaa ya mapenzi.

Unapokuwa mtu wa kufanya mapenzi mara kwa mara huwezi kuwa na uwezo wa kuzuia tamaa yako. Mumeo akiondoka siku mbili unatamani kuwa hata na houseboy ili akukate kiu ya penzi.

3. Kupoteza raha kamili ya tendo.
Raha ya tendo hutegemea sana hisia iliyokuzwa kutokana na mapenzi sahihi na kiu ya kufanya mapenzi, hivyo basi ukiwa mtu wa kufanya mapenzi kila mara unaweza kupoteza msisimko wa tendo na kujikuta unapata furaha ambayo haikutoshi kumaliza tamaa yako.

Kama ni mapenzi utakuwa unayafanya kwa mazoea tu na msisimko wako utakuwa mdogo!

4. Kupoteza nguvu ya mwili.
Madhara mengine yanayoweza kupatikana kwa kufanya mapenzi mara kwa mara ni pamoja na kupoteza nguvu nyingi za mwili.

 Kama tujuavyo tendo la ndoa hasa kwa wanaume huwafanya watumie nguvu nyingi, hivyo kuufanya mwili uchoke. Aidha lishe inapokuwa ndogo kwa wafanya mapenzi mwili hukosa nguvu za kutosha kuhimili misukosuko ya kimaisha.

Sambamba na hilo mbegu za uzazi zinazotoka kwa wanaume wanaofanya mapenzi mara kwa mara huwa dhaifu.

5. Kupatwa na magonjwa.
Kama tulivyojifunza kuwa watu wanaofanya mapenzi mara kwa mara huwa na tamaa na hujikuta wanafanya mapenzi holela ambayo huweza kuwasababishia magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi, lakini ufanyaji wa mapenzi usiokuwa na msukumo wa kutosha hasa kwa wanawake huwafanya waishiwe msisimko na kuzifanya sehemu zao za siri kutotoa ute unaoweza kuwakinga na michubuko wakati wa kujamiiana na hivyo kuwasababishia michubuko itakayoweza kuleta maambukizi ya haraka ya magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi.
 Facebook  Twitter  Google+  Pinterest  Linkedin

Mkurugenzi TAMWA Awasihi Wazazi Kuacha Kuwahamasisha Watoto Kujifelisha Mitihani Kwa Makusudi.


Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Wanahabari  Wanawake Tanzania (TAMWA) Bi Rose Reuben, amewataka wanawake wa Ruangwa kubadilika na waweke juhudi katika kupinga kuishi kwenye maisha ya ukatili wa kijinsia.

Aidha amewataka wazazi kuacha kuwanyima watoto haki ya kupata elimu, kwani ni jukumu la mzazi kumpatia mtoto elimu na si kumshawishi afanye vibaya katika mitihani yake ya mwisho.

Mkurugenzi huyo, ameyasema hayo  Machi 29 March 2019, wakati wa mkutano wa wadau wa kujadili mbinu mkakati ya  kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika ukumbi wa Rutesco uliopo  Ruangwa mjini,katika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

Bi Rose alisema lengo la TAMWA ni kusaidia jamii kuondokana na changamoto za ukatili wa kijinsia hivyo wataendelea kuhakikisha changamoto hizo zinaisha katika jamii ya Ruangwa

"Suala la kupinga ukatili wa kijinsia si la TAMWA pekee yake ni jukumu la kila mwananchi hivyo tusaidiane kubainisha changamoto hizo na sisi tutasimamia kutoa elimu katika kuhakikisha tunatokomeza hizo changamoto"alisema Bi Rose.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa, Hashim Mgandilwa, ametoa rai kwa wananchi wa Ruangwa kuacha kuwahamasisha watoto kufanya vibaya katika mitihani yao ya mwisho ya darasa saba na kidato nne kwa makusudi.

Mheshimiwa Mgandilwa  alisema mzazi atakayebainika anafanya jambo la kushawishi mtoto kufeli kwa kisingizo cha kukosa uwezo wa kusomesha atamchukulia hatua za kisheria.

Pia aliwataka wazazi wa Ruangwa kubeba majukumu yao kama wazazi kwa kuwasimamia watoto wao katika mienendo iliyobora na kuwahamasisha watoto hao kufanya vizur katika masomo yao.

Mgandilwa ametoa rai kwa uongozi wa TAMWA kusaidia kutatua changamoto zilizobainishwa na wadau ili kumaliza matatizo yanayowakabili watoto na wanawake.

"Nitoe shukurani za dhati kwa jitihada mnazozifanya TAMWA na nitapenda sana siku mkiniambia nije nizindue bweni mlilojenga kwa ajili ya kusaidia watoto wanaotembea umbali mrefu hasa wa kike" alisema Mgandilwa.

Mjumbe wa mkutuno huo Esha Issa, amesema wanaochangia mmomonyoko wa maadili kwa watoto ni wamama wenyewe kwani wamekuwa ndiyo watu wenye sauti kubwa katika familia na wanaitumia sauti hiyo vibaya.

"Wamama hatutaki watoto wetu wasemwe wakikosea hata ukiletewa mashitaka ya mtoto anafanya uhuni unakuwa mkali utaki kuamini na hata akipata mimba unaishia kusema acha aongeze dunia"alisema na kuongeza;

"Hili ni tatizo sana kwani watoto wetu wanakuwa hawana adabu na wanapata nguvu ya kufanya mambo ya ajabu kwasababu anaona mzazi mwenyewe unafurahia ujinga anaoufanya".

Mjumbe huyo amewashukuru uongozi wa TAMWA na  aliuomba uongozi huo kutoa elimu ya madhara ya unyanyasaji wa kijinsia kwa watu wa ngazi ya kata na vijiji mara kwa mara ili kumaliza matatizo hayo katika jamii ya Ruangwa.

Jimbo la Arumeru kufanya Uchaguzi mdogo Mei 19


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Semistocles Kaijage ametangaza uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki utafanyika Mei 19 mwaka huu.

Jaji Kaijage ameitoa taarifa hiyo leo akiwa mkoani Morogoro ambapo ameeleza kwamba tume ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Tanzania.

"Nafasi ya jimbo la Arumeru ipo wazi na imetokana na aliyekuwa mbunge Joshua Samwel Nassari kupoteza sifa ya kuwa mbunge kutokana na kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge mfululizo bila ruhusa ya Spika," amesema Jaji Kaijage

Machi 14, 2019 Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai alimuandikia barua Mwenyekiti wa NEC, Jaji Kaijage kumtaarifu jimbo la Arumeru Mashariki lipo wazi kutokana na kutohudhuria vikao vya mikutano mitatu mfululizo.

Aidha Mwenyekiti Kaijage amevitaka vyama vya siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia sheria, kanuni, maadili ya uchaguzi, taratibu, miongozo na maelekezo ya uchaguzi wakati wa kipindi cha uchaguzi mdogo.

Nassari anadaiwa kutohudhuria, mkutano wa 12 wa Septemba 4 hadi 14 mwaka 2018, mkutano wa 13 wa Novemba 6 hadi 16 mwaka 2018 na mkutano wa 14 wa 29 Januari hadi Februari 9 mwaka 2019.

Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru kufanyika Mei 19


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Semistocles Kaijage ametangaza uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki utafanyika Mei 19 mwaka huu.

Jaji Kaijage ameitoa taarifa hiyo leo akiwa mkoani Morogoro ambapo ameeleza kwamba tume ilipokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge la Tanzania.

"Nafasi ya jimbo la Arumeru ipo wazi na imetokana na aliyekuwa mbunge Joshua Samwel Nassari kupoteza sifa ya kuwa mbunge kutokana na kutohudhuria mikutano mitatu ya Bunge mfululizo bila ruhusa ya Spika," amesema Jaji Kaijage

Machi 14, 2019 Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai alimuandikia barua Mwenyekiti wa NEC, Jaji Kaijage kumtaarifu jimbo la Arumeru Mashariki lipo wazi kutokana na kutohudhuria vikao vya mikutano mitatu mfululizo.

Aidha Mwenyekiti Kaijage amevitaka vyama vya siasa na wadau wote wa uchaguzi kuzingatia sheria, kanuni, maadili ya uchaguzi, taratibu, miongozo na maelekezo ya uchaguzi wakati wa kipindi cha uchaguzi mdogo.

Nassari anadaiwa kutohudhuria, mkutano wa 12 wa Septemba 4 hadi 14 mwaka 2018, mkutano wa 13 wa Novemba 6 hadi 16 mwaka 2018 na mkutano wa 14 wa 29 Januari hadi Februari 9 mwaka 2019.


Shilole ampigia magoti Pierre Liquid ‘Akili yangu ndogo, nilishindwa kusoma mazingira nisamehe’

Baada ya kuunga mkono kauli ya RC Mkaonda kuwa Media zinawapa muda mwingi watu wanaofanya mambo ya kipuuzi na kuwafanya wawe maarufu badala ya kufanya hivyo kwa watu wanaofanya mambo ya msingi, hatimaye Shilole ameamua kumuomba radhi mlevi maarufu Tanzania Konki Liquid juu ya kauli yake ya jana usiku. Shilole kwenye maelezo yake ya msamaha …

The post Shilole ampigia magoti Pierre Liquid ‘Akili yangu ndogo, nilishindwa kusoma mazingira nisamehe’ appeared first on Bongo5.com.


Source

CAG amkabidhi Rais Magufuli ripoti 17 za ukaguzi wa mwaka wa fedha 2018/19

Ripoti 17 za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad, kwa mwaka wa fedha unaoishia mwezi Juni 30, 2019 zimekabidhiwa rasmi kwa Rais Dk. John Magufuli. Prof. Mussa Assad Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana Machi 30, 2019 jijini Dar es Salaam na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT), ripoti …

The post CAG amkabidhi Rais Magufuli ripoti 17 za ukaguzi wa mwaka wa fedha 2018/19 appeared first on Bongo5.com.


Source

Yanga SC yatua Dar


Kikosi cha Yanga SC kimewasili jijini Dar es Salaam kikitokea Mwaza ambako kilicheza mchezo wa robo fainali wa kombe la Azam Sports Federation Cup na kushinda kwa penati 4-3 baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya mabao 1-1.

Baada ya kurejea Kocha mkuu Mwinyi Zahera amewapa mapumziko wachezaji wake kwa leo na kesho asubuhi wataendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Chuo cha Polisi kurasini.

Mazoezi hayo yataanza kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Ndanda FC April 04 katika dimba la Nagwanda Sijaona Mtwara.

Yanga ilitinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho jana na sasa itacheza dhidi ya Lipuli FC kwenye mchezo ujao utakaopigwa kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa.
Source

Waziri Hamisi Kigwangala Afunguka Kumtetea Pierre Liquid Dhidi ya Maneno ya Makonda " Pierre ni mtu huru kwenye nchi yake"


Reposted from @hamisi_kigwangalla  -  It's ok! It's ok! It's ok, very ok kwa Pierre Liquid kufanya anachofanya na kufurahisha wanaoona 'anachekesha'. Nchi haiwezi kujengwa na watu wanaofanya mambo magumu magumu pekee. Kila mmoja wetu anafanya sehemu yake. Pierre anatuchekesha na kutukumbusha kufurahia maisha tunapopata nafasi, haswa tunapotoka kufanya hayo mambo yetu magumu magumu! Jamani maisha ni magumu, yana mitihani mingi na ni mafupi sana. Katika kuleta furaha na shangwe kwenye maisha ndiyo maana 'wachekeshaji' wakapata ajira! Wengine tusome udaktari, uhandisi na tufanye uvumbuzi na utatuzi wa changamoto na wengine watutetemeshe, watuvuruge akili, watupe raha na furaha, watuchekeshe, siku zisogee. Maisha ndiyo haya haya! Zaidi ya yote, Pierre ni mtu huru kwenye nchi yake. Tunapaswa kuulinda uhuru wa Pierre kama ambavyo Katiba ya nchi yetu inavyoelekeza. Let him be. Tumuache apate riziki yake. Mungu anajua zaidi kwa nini hatukumjua miaka 5 iliyopita na kwa nini sasa anazua mjadala.

Hata kwa mimi binafsi, Mungu anajua zaidi kwa nini sikuwa Waziri miaka mitano iliyopita, na leo ni Waziri. Mungu anatupangia maisha yetu. Anatugawia mafungu yetu. Pengine hii inaweza kuwa sababu ya Pierre kuwa mtu bora zaidi leo kuliko ile siku aliyopiga ukelele wa raha na kubembea pale Liquid! Pengine hii ndiyo nyota yake ya jaha. Kwa hakika, Pierre atabaki kuwa juu! Pierre atabaki kuwa kileleni! Everebade sey yeeh! #HK

Uteuzi Mpya Uliofanywa na Rais Magufuli Lro Jumapili March 31

Rais wa Tanzania, John Magufuli amemteua Adolf Ndunguru kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango anayeshughulikia sera.

Taarifa  iliyotolewa leo Jumapili Machi 31, 2019 na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imesema Ndunguru ameteuliwa kushika nafasi hiyo kujaza nafasi iliyokuwa wazi.

Imesema kabla ya uteuzi huo, Ndunguru alikuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kufuatia Uteuzi huo, Rais Magufuli amemteua Msafiri Lameck Mbibo kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa TRA.

Kabla ya uteuzi huo, Mbibo alikuwa Meneja wa TRA Mkoa wa Kilimanjaro.

Uteuzi wa viongozi hao umeanza leo Jumapili Machi 31, 2019.



Nedy Music atangaza ujio wa tamasha lake la ‘Welcome Home’, ampigia saluti Ommy Dimpoz (+video)

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Nedy Music ametangaza kuwa mwaka huu ameandaa tamasha ka lake la muziki la Welcome Home ambalo atazunguuka visiwani Zanzibar akiwa na wasanii tofauti tofauti. Nedy akiongea na Bongo5, amesema kuwa lengo la tamasha hilo ni kunyanyua wasanii wachanga kutoka visiwani Zanzibar. Kwa upande mwingine, Nedy amempongeza Ommy Dimpoz kwa …

The post Nedy Music atangaza ujio wa tamasha lake la ‘Welcome Home’, ampigia saluti Ommy Dimpoz (+video) appeared first on Bongo5.com.


Source

Kukumbatiana ni njia nzuri sana ya kumaliza migogoro katika mahusiano

Kuna siku fulani nilipata wasaa mzuri wa kusoma kitabu fulani hivi cha saikolojia, katika kitabu hicho yapo mambo mengi sana ambayo yameandikwa hususani tabia za mwanadamu kiujumla. Moja kati ya vitu ambavyo vilinishangaza ni pamoja ya kwamba mgusano wa mtu mmoja na mwingine ni dawa tosha kwa watu wenye tofauti.

Nilipokuwa nikiendela kusoma kitabu hicho nikaleta fikra zangu katika maisha ya kawaida nikaja nikagundua ya kwamba watu wengi wakikosana katika jamii zetu watu ambao wakitokea kwa lengo la kuwapatanisha basi huwa uwamuliwa watu hao wapeane mikono ikiwa ni ishara ya wazi kwamba kila mmoja moyo wake ni safi na hauna kinyongo na mtu  mwingine.

Nikaendelea kusoma kitabu hicho ambapo tena nikakutana na faida kadha wa kadha la kumbatio katika mahusiano hasa pale inapotokea watu fulani wamekwazana katika mahusiano ya kimapenzi.

 Ambapo nilikuja kugunundua ya kwamba kukumbatiana katika mahusiano ya kimapenzi inaweza kuwa ni njia nzuri sana ya kumaliza tofauti za wapendanao katika mahusiano, hii ni kwasababu watu waligombana pindi wanapokumbatiana basi huzalisha joto na hisia za Upendo ambapo kila mmoja wao hujikuta anamsemehe yule ambaye amemkosea.

Kitu kingine  ambacho nimekigundua katika kukumbatiana,  kumkumbatia mwenza wako wakati mnapokuwa katika malumbano ya hoja yenu taratibu  inabadilisha hali  yote ya machafuko.

 ukimkumbatia mwenza wako wakati wa malumbano huwa inaleta hali tofauti, haiwezi kuwa kama siku zote ambazo umezoea, imegundulika kuwa inakuwa na hisia za kweli, mtu anaweza kujisikia vizuri zaidi kuliko ile kawaida ya siku zote, inaondoa  hali ya kuwa na shaka lolote.

Mpaka kufikia hapo sina la ziada nakutakia utumiaji mwema wa njia hii ya kumbatio hasa pale unapokuwa umegombana na mwenza wako.

Na. Benson Chonya.

KINDOKI AGEUKA SHUJAA!! APANGUA PENALTI MBILI KUIPELEKA YANGA NUSU FAINALI


Kipa Klaus Kindoki amepangua penalti mbili na kuiwezesha Yanga SC kwenda Nusu Fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), au Azam Sports Federation Cup (ASFC) kwa ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya wenyeji, Alliance FC kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.

Kindoki, mlinda mlango kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), alipangua penalti za Dickson Ambundo na Nahodha wa Alliance FC, Siraj Juma, wakati kinda Martin Kiggi aligongesha mwamba wa kushoto.

Waliofanikiwa kumfunga penalti zao upande wa Alliance FC ni Joseph James, Geofrey Luseke na Samir Vincent, wakati za Yanga zilifungwa na beki Paul Godfrey 'Boxer', viungo Mzimbabwe Thabani Kamusoko, Haruna Moshi 'Boban' na Deus Kaseke.

Vijana wazaliwa wa Mwanza na walioibukia mkoani hapa kisoka ndiyo waliokosa penalti zote za Yanga, beki Kelvin Patrick Yondan akigongesha mwamba na kiungo Mrisho Khalfan Ngassa mkwaju wake ukipanguliwa na kipa John Mwanda. 

Katika dakika 90 za mchezo huo, Yanga SC walitangulia kwa bao la mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Heritier Ebenezer Makambo dakika ya 38 kwa shuti la kitaalamu baada ya pasi ya kiungo Pius Charles Buswita.

Alliance FC walisawazisha bao hilo dakika ya 62, kupitia kwa kiungo wake wa ulinzi, Joseph James aliyemalizia kwa kichwa mpira wa adhabu uliopigwa na Mapinduzi Balama kutoka upande wa kulia.

Sasa Yanga itasafiri kuwafuata Lipuli FC Uwanja wa Samora mjini Iringa mwishoni mwa mwezi Aprili katika mchezo wa Nusu wa Fainali.

Nusu Fainali nyingine itafanyika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam ikiwakutanisha Azam FC walioitoa Kagera Sugar kwa kuichapa 1-0 jana Bukoba na KMC ya Kinondoni walioitupa nje African Lyon kwa kuipiga 2-0 Jumatano Mbweni. 

Kikosi cha Alliance FC leo kilikuwa; John Mwanda, Godlove Mdumule, Siraj Juma, Wema Sadoki, Geoffrey Luseke, Joseph James, Michael Chinedu/Samir Vincent dk58, Paul Maona/ Hussein Javu dk55, Bigirimana Blaise/Martin Kiggi dk90+3, Balama Mapinduzi na Dickson Ambundo.

Yanga SC; Klaus Kindoki, Paul Godfrey, Gustapha Simon, Said Juma 'Makapu', Kelvin Yondan, Feisal Salum 'Fei Toto'/Thabani Kamusoko dk77, Mrisho Ngassa, Papy Kabamba Tshishimbi, Heritier Makambo, Amissi Tambwe/Haruna Moshi 'Boban' dk61 na Pius Buswita/Deus Kaseke dk77.

Chanzo- Binzubeiry 

Daktari Awaonya Wanaume na Wanawake Kunyoa Nywele za Sehemu ya Siri

Daktari wa wanawake ameonya dhidi ya kunyoa sehemu za siri eti kama njia moja kudumisha usafi

Kulingana na Dkt Ignitius Kibe, Mungu aliumba binadumu awe na nywele hizo anapobalehe kwa sababu kadhaa na pia zina umuhimu sana hasa wakati wapenzi waposhiriki kitendo cha ndoa.

Akiwa kwenye mahojiano na runinga ya Citizen Jumatano Machi 27, daktari huyo alisema nywele hizo husaidia sana wakati wa kitendo cha ndoa.

Aidha, daktari huyo alisema sio salama kuzinyoa kwani mtu anaweza pata vipele na michubuko kwenye sehemu za siri

" Mimi kwangu binafsi napendelea hizo nywele ziwepo, zina umuhimu sana wakati wapenzi wanaposhiriki kitendo cha ndoa," Dkt Kibe alisema.


Daktari huyo alisema wale ambao hunyoa nywele hizo wanahatarisha maisha yao kwani ni rahisi kuambukiwa magonjwa ya zinaa.


Messi ashindwa kujizuia aeleza namna anavyommisi Ronaldo kwenye La Liga ‘Nammisi sana Cristiano’

Mchezaji bora duniani, Lionel Messi amesema kuwa anatamani mpinzani weke mkubwa, Cristiano Ronaldo angelikuwa bado yupo kwenye ligi kuu nchini Hispania, La Liga. Ronaldo ameondoka Real Madrid na kujiunga na miamba ya soka nchini Italia klabu ya Juventus kwa dau la pauni milioni 100 na kuhitimisha safari yake ya miaka tisa ndani ya La Liga. …

The post Messi ashindwa kujizuia aeleza namna anavyommisi Ronaldo kwenye La Liga ‘Nammisi sana Cristiano’ appeared first on Bongo5.com.


Source

Saturday, March 30, 2019

VIDEO: Waziri Lugola atoa onyo kwa Polisi. "Ripoti ipo mezani kwangu inapumua"


Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, ametoa onyo kwa polisi na watu ambao wanasimamia sheria kuhusu suala mla rushwa. Waziri Lugola amesema uchunguzi ambao ulikuwa unafanywa na watu aliowaagiza tayari umeshakamilika na ripoti ipo mezani kwake.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI....USISAHAU KUSUBSCRIBE

Source

Mwanamke aliyefariki toka mwaka jana ajifungua, azikwa siku moja baada ya kupatikana kwa mtoto huyo

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 26 nchini Ureno, amejifungua mtoto wa kiume siku ya Alhamisi licha ya kutangazwa kuwa ni mfu toka mwezi Disemba mwaka jana. Mwanamichezo wa kimataifa, Bi Catarina Sequeira alipatwa na shambulio kali la pumu akiwa nyumbani kwake. Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Bi Sequeira mwenye umri wa …

The post Mwanamke aliyefariki toka mwaka jana ajifungua, azikwa siku moja baada ya kupatikana kwa mtoto huyo appeared first on Bongo5.com.


Source

Live | Magufuli Akiwatunuku Kamisheni Maofisa Wapya JWTZ

Live | Magufuli Akiwatunuku Kamisheni Maofisa Wapya JWTZ


Kuna Vingi Tumefanya na Uwoya Ila Nimemiss Kumpiga Makofi -Dogo Janja

Kuna Vingi Tumefanya na Uwoya Ila Nimemiss Kumpiga Makofi -Dogo Janja
Mume wa zamani wa Irene Uwoya, Dogo Janja amefunguka vitu anavyovbimiss kwa aliyekuwa Mke wake huyo.

Dogo Janja amesema kuwa baada ya kutengana amesema kuwa kitu anachokimiss ni kumpiga makofi.

"Namiss kumpiga makofi" . Kuna vitu vingi ambavyo tumefanya pamoja na Irene Uwoya moment ni nyingi kikubwa namiss kumpiga, nafurahi kuona jinsi anavyopambana na toka zamani nilikuwa natamani kuona akifanya vitu vyake na kumtofautisha na watu wengine," Dogo Janja ameiambia XXL ya Clouds FM.

Mtanzania mwenye taaluma ya Maendeleo ya Jamii atengeneza ndege isiyo na rubani, akosa kibali cha kuirusha (Video)

Kijana wa Kitanzania aitwaye, BoneLove ambaye ana taaluma ya Maendeleo ya Jamii, jana katika maonyesho ya Innovation Week aliushangaza umati watu baada ya kuonyesha ndege isiyo na rubani ambayo amaeiunda mwenyewe huku akidai kukosa vibali kwaajili ya kurusha kwaajili ya majaribio.

The post Mtanzania mwenye taaluma ya Maendeleo ya Jamii atengeneza ndege isiyo na rubani, akosa kibali cha kuirusha (Video) appeared first on Bongo5.com.


Source

Mambo yatakayokusaidia kudumu katika mahusiano ya kimapenzi

kikubwa kinachotafutwa na wapendanao huwa ni furaha ya moyo. Wapendanao wanapaswa kuishi kwa furaha, amani na upendo. Uhusiano wao uwe sehemu ya kudumisha urafiki, udugu na kwa pamoja muweze kuishi vizuri.

Wapendanao wanatengeneza umoja wao ambao ni wa kutiana moyo pale mambo yanapokuwa si mazuri. Wakati wa matatizo na wakati wa furaha wanakuwa pamoja, wanategemeana katika kuifanya safari yao ya hapa duniani iweze kutimia sawasawa na mpango wa Mungu.

Kwa kuzingatia hilo, kila mmoja anapaswa kuwa furaha ya mwenzake. Anapaswa kumtendea mambo mazuri ili aweze kuwa na furaha na amani muda wote. Mwanaume anapaswa kushughulikia amani na furaha ya mwanamke wake, vivyo hivyo mwanamke ashughulikie furaha na amani ya mwanaume wake. Kuna vitu ambavyo mara nyingi huwa tunaviona ni vidogo lakini kimsingi huwa vina maana kubwa sana katika suala zima la uhusiano wa kimapenzi kwa mchumba au hata hatua ya ndoa.

Vitu hivyo ni pamoja na:

Mitoko ya hapa na pale.
Mara nyingi wapendanao huwa wanajisahau sana katika suala zima la mitoko ya hapa na pale. Mara nyingi kila mtu anajua kutoka kivyake na marafiki zake.

Mwanaume anatoka kwenda hoteli au sehemu mbalimbali za burudani na rafiki zake na mwanamke naye anatoka na mashoga zake. Ndugu zangu, hata kama kweli kila mtu ana mitoko yake lakini ni vyema kujiwekea utaratibu siku moja moja wapendanao mkatoka pamoja, ina maana kubwa sana katika suala la kujenga mahusiano yenu ya kimapenzi.

Kupeana zawadi.
Lingine ni la vizawadi. Hata kama unajua kwamba mwenzako ana uwezo wa kununua kile ambacho wewe utamnunulia lakini fanya hivyo kama ishara ya upendo, inaleta maana kubwa sana katika uhusiano.

Toa kipaumbele kwa mwenzako.
Unapokuwa unawaza juu ya jambo fulani, mpe kipaumbele mwenzi wako kwa kuomba hata ushauri badala ya kuomba ushauri kwa marafiki zako, wafanyabiashara au wafanyakazi wenzako. Mwenzi wako anapoona humpi kipaumbele hususani katika masuala ya msingi, anaweza kuona ni kama unamdharau na hivyo kupunguza hamu ya kuwa na wewe.

Msaidie katika kufanya mambo mbalimbali.
Kuna wakati mwenzi wako anaweza kuwa anaweza kufanya jambo fulani lakini anapokuwa na wewe, anatamani wewe umsaidie, hilo nalo lina maana kubwa lifanye kadiri uwezavyo.

Mjali kwa hali na mali.
Hili ni la muhimu sana, unaweza kuona kama halina maana sana lakini unapokuwa unamkumbusha mwenzi wako kuhusu suala la kula au kumuamsha asubuhi awahi kazini na mambo mengine kama hayo, yanaleta chachu na hamasa kubwa katika uhusiano.

Ukiyazingatia haya yawezekana ukaona kana kwamba hii dunia mmeumbiwa watu wawili tu yaani wewe nay eye kwa sababu hatua na mtu mwingine zaidi ya huyo mwenza wako katika suala la mafanikio.


Source

Friday, March 29, 2019

Mfahamu Charlie Chaplin kiundani zaidi

Siku ya leo nilipata bahati ya kusoma historia ya muigizaji maarafu wa vicheko vya kimya kimya, naomba nawe ukae mkao wa kula ili uweze kumjua Charlie Chaplin kama ifutavyo:

Vyanzo vingi vinasema kwamba Charlie Chaplin alikuwa ni muigizaji na pia ni mtayarishaji  wa filamu maarafu wa kingereza.

Pia Charlie Chaplin alizaliwa mnamo tarehe 16 mwezi wanne mwaka 1889 na alifariki mnamo mwezi wa 12 mwaka 1977.

Umaarufu wake ulitokana na uwigizaji wa video zake  za kuchekesha ambazo zilikuwa ni za kimya kimya ambazo zilikuwa hamna kuongea wala kutoa sauti na watazamaji walikuwa wanafurahi, kwa miaka ya hivi karibuni tunaweza kumfananisha mchekeshaji huyo na Mr. bean japo Mr. bean yeye hafanyi vichekesho vya kimya kimya pekee kama ambavyo alifanya Charlie Chaplin.

Kama nilivyosema hapo awali kwamba Charlie Chaplin alikuwa ni muigizaji pia muongozaji wa filamu  zote zinazomhusu. Charlie Chaplin alifanya kazi hiyo kwa takribani kwa miaka 70.

Sehemu kubwa za filamu  ambazo alikuwa akicheza Charlie Chaplin mara nyingi ilikuwa  ikiitwa "the Tramp".  Uhusika huu ulikuwa ukimuonesha Charlie Chaplin kwamba ni mtu mwenye heshima zake, ambaye alikuwa akivaa koti, suruali kubwa kofia pamoja viatu huku akichekesha.

Huyo ndiye Charlie Chaplin muigizaji maarafu kuwahi kutokea katika sayari hii.

Asante na endelea kutembelea Muungwana Blog kila wakati.

Picha: Simba SC waanza mazoezi Morogoro kuwakabili Mbao FC


 Kikosi cha Simba SC leo jioni kimeanza mazoezi mkoani Morogoro kujiandaa kuwakabili Mbao FC katika mchezo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (TPL) ambao utapigwa  siku ya Jumapili

Bondia aliyemkisi mwandishi kwenye interview baada ya ushindi kufunguliwa kesi (+video)

Mwandishi wa kike wa habari za michezo, Jenny Sushe amejikuta akikisiwa bila ya ridhaa yake na bondia wa uzito wa juu, Kubrat Pulev wakati akimfanyia mahojiano hali iliyopelekea mwanaharakati wa haki za wanawake kukusudia kumfungulia kesi. Mwanaharakati wa haki za wanawake nchini Marekani, Bi Gloria Allred ameamua kulikomalia swala hilo na kukusudia kufanya mkutano na …

The post Bondia aliyemkisi mwandishi kwenye interview baada ya ushindi kufunguliwa kesi (+video) appeared first on Bongo5.com.


Source

Simba Yatua Moro Yapokelewa na Mamia ya Mashabiki

Simba Yatua Moro Yapokelewa na Mamia ya  Mashabiki
Klabu ya Simba imewasili salama mjini Morogoro tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mbao FC wikiendi hii.


Simba ambayo imetoka asubuhi ya leo jijini Dar es salaam na kuwasili Morogoro majira ya mchana, imepokelewa na mamia ya mashabiki katika hoteli waliyofikia ambao muda wote wameonekana kutaja majina ya wachezaji.

Jina la mshambuliaji John Bocco ndilo lilliloibua shangwe kubwa zaidi baada ya kushuka kutoka kwenye basi, ikionesha kuwa mashabiki wamekubali kiwango alichokionesha katika mechi mbili kubwa na muhimu za mwisho.

Mechi hizo ni ili iliyoipeleka Simba robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika baada ya kuifunga AS Vita mabao 2-1 katika Uwanja wa Taifa pamoja na mechi iliyoipeleka Taifa Stars kwenye fainali za AFCON kwa kuichapa Uganda kwa mabao 3-0, ambapo katika mechi zote mshambuliaji huyo ameonesha kiwango kikubwa.

Makamanda wetu walivyopokelewa mji kasoro bahari (Morogoro). Siku ya Jumapili watakuwa uwanja wa Jamhuri kuwapa burudani Wanasimba wote. #NguvuMoja pic.twitter.com/ziQwF7cSni

— Simba Sports Club (@SimbaSCTanzania) March 29, 2019

Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu wanatarajia kupambana na Mbao FC katika Uwanja wa Jamhuri kutokana na Uwanja wa Taifa kuwa katika maandalizi ya michezo ya AFCON ya vijana chini ya miaka 17 inayoratajia kuanza mwezi ujao nchini Tanzania.

Nafasi ya Simba katika msimamo wa ligi


Katika msimamo wa Ligi Kuu, Simba inakamata nafasi ya tatu ikiwa na pointi 54 baada ya kushuka dimbani michezo 21 huku Mbao FC ikiwa katika nafasi ya 14 kwa pointi 36 baada ya kushuka dimbani michezo 30.


Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) yatoa tahadhari ya mvua nchini

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya siku tano ya kunyesha mvua kubwa inayoweza kusababisha athari ikiwemo mafuriko.

 Kwa mujibu wa taarifa ya TMA, mvua hizo zinatarajiwa kuanza kunyesha leo Ijumaa Machi 29 hadi Aprili 2, 2019 na kwamba zinaweza kuleta athari kwenye makazi ya watu.

Mvua hiyo inatarajiwa kunyesha katika mikoa ya Rukwa, Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe, Ruvuma, Lindi, Mtwara, Morogoro, Dar es Salaam, Tanga, Pwani na Zanzibar.

Pia zinaweza kuleta shida katika usafiri na kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii. Mamlaka hiyo imesema kuanzia leo hadi Machi 31, 2019 mvua hizo zitanyesha katika mikoa ya Rukwa, Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe, Ruvuma, Lindi, Mtwara na Morogoro.

Imeeleza kuwa Aprili Mosi hadi Aprili 2, 2019 mvua hizo zitanyesha katika mikoa ya Rukwa, Mbeya, Iringa, Njombe, Songwe, Ruvuma, Lindi, Mtwara, Morogoro, Dar es Salaam, Tanga, Pwani na Zanzibar.

TMA imeshauri Menejimenti ya Maafa na watoa huduma za dharura pamoja na wadau wengine kuchukua hatua za kuweka mipango stahiki kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza.


KAULI YA BUNGE BAADA YA MAHAKAMA KUU KUTUPILIA MBALI KESI YA JOSHUA NASSARI



Waitara: Viongozi Jenganeni Mahusiano Mazuri Na Waandishi Wa Habari Kwani Ni Nguzo Muhimu Kwa Maendeleo Ya Taifa

Naibu waziri wa TAMISEMI Mwita Waitara amewataka viongozi kutoka ngazi mbalimbali  kujenga Mahusiano Mazuri na waandishi wa habari kwani ndio nguzo muhimu kwa maendeleo ya Taifa.

Waitara amesema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na wadau wa elimu   katika kikao  cha Maandalizi ya Mashindano ya Umoja wa Michezo  shule za Sekondari ,Tanzania [UMISETA] unaodhaminiwa na Coca cola.

Mhe.Waitara amesema waandishi wa habari wanatakiwa kupewa kipaumbele katika mambo  ya  Msingi ya Serikali vivyo hivyo katika mashindano hayo ya UMISETA ni vyema vyombo vya habari vikatumika kuibua vipaji vya wachezaji mbalimbali na serikali za mitaa  kuwawezesha wanahabari katika kutekeleza majukumu yao kwani ni nguzo muhimu.

"Sio kwamba mpaka aje Mkurugenzi,Waziri  No.hata wewe unaweza ,mwanafunzi kafanya vizuri tangaza hiyo,shule za kata zinatoa matokeo mazuri tangaza hiyo.Kuna Ofisi zingine zina pwaya  ni mzigo  akimwona mwanahabari hata  ushirikiano hatoi yeye yupoyupo tu.

"Hivyo katika Mashindano haya tumieni vyombo vya habari,kupitia blogs,redio,magazeti ,vyombo vya habari vyote kuhamasisha michezo."

Aidha waitara ameagiza Maafisa elimu wilaya ni mikoa kufuatilia somo la michezo kufundishwa kwa nadharia na vitendo,viwanja vya michezo kufufuliwa,kusimamia makusanyo ya fedha za michezo  na nyimbo za uzalendo ikiwa ni pamoja na wimbo wa Taifa na wimbo wa Afrika Mashariki kuimbwa hasa kwenye mashindano hayo.

"Unakuta mtu mzima na ofisi yake ukimwambia imba anasingizia ana kikohozi ,tatizo  sio kikohozi bali haujui huo wimbo.hivyo tuhamasishe nyimbo za uzalendo kwa Taifa Letu."

Katika kuboresha na Kutunza Mazingira Mhe.Waitara ameagiza kila mwalimu apande mti  mmoja wake shuleni na kila mwanafunzi miti miwili nyumbani na shuleni.

Mkurugenzi Idara ya Elimu Tanzania,Julius Nestory amesema watashirikiana na wadau mbalimbali katika kukuza vipaji vya wanafunzi shuleni huku akipongoza Copa  Coca Cola kwa  kudhamini Mashindano ya UMISETA.

Kwa Upande wake ,Mkurugenzi wa Mambo ya Umma na Mawasilino ,Coca Cola  Haji Mzee Ally amezitaja mikoa atakayoanza katika kuzindua Mashindano ya UMISETA 2019 ni Tabora,Manyara na Ruvuma huku akisema kuwa kutakuwa na mkakati kabambe wa kuzipa zawadi shule zitakazokusanya  takataka  za plastiki  za kampuni yoyote katika kuhakikisha utunzaji wa Mazingira .

Mwenyeji wa Mashindano UMISETA 2019 ni Mkoa wa Mtwara na yanatarajia kuanza mwezi ujao.

Audio: Mjukuu wa Mbaraka Mwinshehee Marissa, aendelea kufuata nyayo za babu yake, aachia wimbo ‘Safarini’

Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye pia ni mjukuu wa msanii wa zamani ambaye ni marehemu kwa sasa Mzee wetu Mbaraka Mwinshehe, Marissa ambaye yuko chini ya THT ameachia Audio ya wimbo wake ‘Safarini’ Wimbo huu wa Safarini ambao ni wimbo wake wa pili kuachia na audio ya wimbo huu ukifanywa na Producer Eliasi …

The post Audio: Mjukuu wa Mbaraka Mwinshehee Marissa, aendelea kufuata nyayo za babu yake, aachia wimbo ‘Safarini’ appeared first on Bongo5.com.


Source

Ukaribu wa Willy Paul na Nandy wahimarika, amwagia sifa


Baada ya mwimbaji Nandy 'African Princess'  kufanya kolabo na Willy Paul kutokea +254 Kenya kwenye ngoma ya Njiwa ambayo iliachiwa rasmi June 27,2018 kaaika mtandao wa You Tube na kufanya vizuri ndani na nje ya nchi ya Tanzania, sasa wawili hao wanaonekana kuileta ngoma nyingine pamoja.

Kupitia ukurasa wa instagram wa  Nandy ametuonyesha kipande kifupi cha video na kuandika caption ikisema 'Hallelujah" ambapo imetabiriwa kuwa ndio jina la ngoma inayofata na kisha akamtaja mwimbaji Willy Paul. Endapo ngoma hiyo ikitoka basi itakua ni track ya pili kutoka kwa mwimbaji Nandy na Willy Paul.

Inaelezwa kuwa ngoma hii inakuja baada ya kilio cha Willy Paul kutamani kufanya kazi tena na Nandy baada ya ngoma yao ya Njiwa kufanya vizuri huku akiwa ameshusha sifa kibao kwa mwanadada Nandy na kushukuru kwa kufanya nae project hiyo ya njiwa.

"Nandy ni mmoja wa wasanii wa kike wenye sauti Tanzania na Afrika kwa ujumla, ninafuraha kufanya nae kazi kwenye project ya njiwa, sitojali kufanya nae wimbo mwingine, kufuatia mafanikio ya njiwa sitojali kufanya nae nyingine tafadhali mwambieni sitojali kufanya nae nyingine, kama unatamani sisi kufanya wimbo mwingine basi andika neno ndio" >>>Willy Paul

Thursday, March 28, 2019

Vazi la kitenge linavyokuweka 'smart'


Ni miaka mingi sana sasa, Afrika imekuwa ikitengeneza malighafi hii ya Kitenge. Mataifa mengi kama Nigeria, Ghana, DR Congo na kwingineko, tulizoea kuwaona wakivaa vitenge vilivyoshonwa kwa mitindo anuai na ya kuvuatia.

Hapa nchini Tanzania, Kitenge, naweza kusema kimechelewa sana kupewa nafasi ingawa tulikuwa na viwanda vilivyozalisha aina hii ya malighafi kama Sunguratex, Urafiki nk. Nyakati zile ilikuwa ukimwona mwanamama kavaa vazi hilo basi moja kwa moja watu watasema 'kavaa vazi la taifa'.

Halikuwa vazi la kawaida, kwa sababu tulitekwa na mitindo mingi ya kigeni. Wanaume ni wachache sana ambao walivaa vazi hili miaka hiyo.

Lakini sasa mambo yamegeuka, Kitenge kimekuwa vazi la gharama na kinashonwa katika mitindo mbalimbali ya kuvutia kama magauni, mashati, kaptula, suruali, suti, mikoba na ushishangae ukikutana na viatu vya aina hii.

Hakika ukivaa muonekano wako hubadilika, urembo au ushababi wako huwa dhahiri shahiri hasa ukimpata fundi anayejua vyema kucheza na 'body' na kukufyatulia kitu kifaacho. Vijana watasema 'Amazing!'

Wednesday, March 27, 2019

Mbao FC yaahidi kuifunga Simba tena katika ligi kuu


Kuelekea mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara kati ya Simba SC na Mbao FC ya Jijini Mwanza utakaochezwa Machi 31 mwaka huu katika Uwanja wa Jamuhuri Mkoani Morogoro, Meneja wa Klabu ya Mbao FC Almas Moshi amesema kuwa wanauhakika wataifunga tena Simba SC katika mchezo huo.

Moshi amesema kutokana na Waalimu walionao kwa sasa ambao ni aliyekuwa Kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa stars" Salum Mayanga na msaidizi wake Novatus Fulgence,wanaamini watafanya vizuri katika mechi zao kutokana na uzoefu mkubwa walionao waalimu hao.
.
"Kutokana na waalimu tulionao kwa sasa tutafanya vizuri katika mchezo wetu na Simba japo Simba kwa sasa amekuwa akifanya vizuri katika Ligi kuu na mechi za kimataifa pia,lakini kwa uwezo walionao walimu wetu kwa mechi za kitaifa na kimataifa pia tutafanya vizuri na kuwafunga Simba tena" amesema Moshi

Klabu ya Simba SC sasa wanaotumia Uwanja huo Jamhuri kama Uwanja wao wa nyumbani baada ya Uwanja wa Taifa,Uhuru na Azam complex kufungwa ili kupisha maandalizi ya fainali za AFCON U17 ambapo Tanzania ndio mwenyeji.

Ikumbukwe kuwa Simba SC alifungwa bao 1-0 Septemba 20 mwaka jana na Mbao FC katika Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Source

Fursa Za Ufadhili Wa Masomo Kwa Watanzania kutoka Serikali ya Thailand.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imepokea fursa za ufadhili wa masomo ya muda mrefu katika fani mbalimbali kutoka Serikali ya Thailand.

Kozi hizo zitakazotolewa kwenye Vyuo mbalimbali nchini humo, zitajikita katika fani za Filosofia ya Uchumi Timilifu; Mabadaliko ya Tabianchi, Usalama wa Chakula; Afya ya Jamii na Malengo ya Maendeleo Endelevu.

Wizara inawahimiza Watanzania wenye sifa kuomba nafasi hizo za mafunzo zilizotangazwa na Serikali ya Thailand kwa mwaka 2019.

Mwisho wa kuomba nafasi hizo ni tarehe 31 Machi 2019. Kwa maelezo zaidi kuhusu kozi hizo na namna ya kuomba, tafadhali tembelea tovuti  ifuatayo: http://www.tica.thaigov.net

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje Na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam
27 Machi 2019


Waziri Mhagama amkumbuka Mwl. Julius Nyerere


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amewahimiza vijana kuwa wazalendo na kuithamini nchi yao.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga vijana waliopanda Mlima Kilimanjaro jana Machi, 2019 Mkoani Kilimanjaro ikiwa ni kuaadhimisha kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Waziri Mhagama alisema kuwa, Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere alikuwa kiongozi mzalendo kwa nchi yake na alijali utu na usawa, hivyo ni vyema vijana na vizazi vijavyo wakarithishwa falsafa za Baba wa Taifa.

"Vijana mna kila sababu kuyaenzi matendo ya Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere na Mhasisi wa Mapinduzi ya Zanzibar, Abeid Amani Karume kwa vitendo kwa kuwa ninyi ndio nguzo ya Taifa na mnaelewa vema tulipotoka, tulipo na tunapoenda," alisema Mhagama.

Aliongeza kuwa, Viongozi hawa hawakuwa wabinafsi kwa kujilimbikizia mali na hawakubagua mtu kwa rangi wala kabila bali walijenga Taifa na kudumisha amani na moja.

Aliendele kwa kuwapongeza vijana kwa azma yao ya kuenzi historia na mazuri yaliyofanywa na viongozi hao kwa kupanda mlima Kilimanjaro na kuwatakia baraka waende na kurudi salama.

"Kitendo hiki ni cha kishujaa na uzalendo wa hali ya juu kwa Taifa ikiwa ishara ya kumuenzi Baba wa Taifa," alieleza Mhagama

Aidha Waziri Mhagama alitoa rai kwa vijana kuwa wazalendo na kuwasihi wafanye kazi kwa bidii ili kujenga Taifa kupitia uchumi wa viwanda utakao ifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Alifafanua kuwa uzalendo lazima ujengwe sambamba na ujenzi wa uchumi wa Taifa, ulinzi na usalama wa Taifa na utunzaji wa tunu za Taifa.

Pamoja na hayo, aliwapongeza na kuwashukuru Viongozi wa Mkoa wa Songwe na Lindi pamoja na uongozi wa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) kwa ushirikiano mkubwa na Ofisi yake katika kuwashirikisha vijana kwenye suala hilo.

Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba alisema kuwa tukio hili ni muhimu kwa vijana kutambua historia na mchango wa Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere katika Taifa.

"Tumieni fursa hii kupitia vitabu mbalimbali vya kihistoria ili mjifunze mipango, mwenendo na malengo ya Baba wa Taifa itawasaidia na kuwajengea nafasi nzuri ya kujitambua na kuelewa historia ya Taifa," alisema Warioba.

Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana, Bw. James Kajugusi alieleza kuwa Baba wa Taifa alianza harakati za kulikomboa Taifa akiwa kijana na aliendelea kufanya hivyo kwa kuwa hamasisha vijana kujenga Taifa lao baada ya kupata uhuru.


TETESI: Gadiel Michael kufanya majaribio ya soka kwenye klabu hii kubwa Afrika Kusini

Tetesi zilizopo katika usajili ni kuwa beki wa pembeni wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, Gadiel Michael imedaiwa kuondoka nchini kuelekea nchini Afrika Kusini kwaajili ya majaribio. Gadiel Michael ambaye anakipiga kwenye klabu ya mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu soka Tanzania Bara Yanga imedaiwa amekwenda kufanya majaribio kwenye klabu ya Bidvest West ya …

The post TETESI: Gadiel Michael kufanya majaribio ya soka kwenye klabu hii kubwa Afrika Kusini appeared first on Bongo5.com.


Source

BREAKING: Lukumay na Nyika wajiengua Yanga SC


Kaimu Mwenyekiti Yanga SC Samuel Lukumay na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika wametangaza kujiuzulu nafasi zao.

Wawili hao wameamua kuachia ngazi mapema ili kupisha mchakato wa uchaguzi mkuu wa klabu ambao utafanyika hivi karibuni.

Nyika na Lukumay wameamua kujiondoa ili kutoa mwanya mzuri kwa mchakato wa uchaguzi kwenda vizuri ili kuja kupata warithi wa nafasi hizo.

Licha ya kujiuzulu, Nyika amewamba msamaha wale wote aliowakosea pindi akiwa madarakani ndani ya klabu.

''Ninajiuzulu nafasi zangu zote nikiwa kama Mjumbe wa kamati ya utendaji.

"Lakini pia Mwenyekiti wa kamati ya usajili na kamati ya mashindano na niombe msamaha kwa wale niliowakosea katika utekelezaji wangu wa majukumu''.

Ikumbukwe hivi karibuni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Yanga, George Mkuchika, alitangaza kuwa watakuwa na mkutano mkuu maalum utakaoenda kuamua kama klabu inahitaji kufanya uchaguzi mkuu ama wa kujaza nafasi.


Jamal wa The Empire Afutiwa Kesi ya Kutoa Ushahidi wa Uongo

Staa wa Tamthilia ya Empire @jussiesmollett amefutiwa mashtaka yote kwenye kesi yake ya kutoa ushahidi wa uongo na kudanganya kuhusu shambulio la kibaguzi.

#Jussiesmollett ambaye alikuwa amefunguliwa mashtaka 16 ya jinai kutokana na kitendo cha kutoa ushahidi wa uongo na kupanga shambaulio lake mwenyewe hapa akizungumza na waandishi wa habari muda mchache baada ya kitangazwa kufutiwa mashtaka yote.

Kwasasa #JussieSmollett atatakiwa kulipa Tsh. Millioni 25 ya dhamana tu.

Louis van Gaal aichambua Manchester, ataja tofauti ya Solskjaer na Mourinho ‘United inaendelea na style yake ya kupaki basi’

Aliyewahi kuwa kocha wa Manchester United, Louis van Gaal amesema kuwa staili ya uchezaji wa klabu hiyo haijabadilika chini ya Ole Gunnar Solskjaer. Aliyewahi kuwa kocha wa Manchester United, Louis van Gaal Wakati vyombo vya habari vikiripoti siku ya Jumatatu kuwa Ole Gunnar Solskjaer anatarajiwa kukabidhiwa jumla jumla United kwa kandarasi ya muda mrefu Van …

The post Louis van Gaal aichambua Manchester, ataja tofauti ya Solskjaer na Mourinho ‘United inaendelea na style yake ya kupaki basi’ appeared first on Bongo5.com.


Source

JISHINDIE MPAKA MILLIONI 23 UKIWA NA Infinix ZERO 6


Kwa mara nyingine tena kampuni ya simu ya Infinix kutikisa soko la simu barani Afrika baada ya ujio wa Infinix ZERO 6, ikiwa ni muendelezo wa toleo la ZERO linalowakilisha kampuni ya Infinix. Infinix ZERO 6 inathibitika kuwa na uwezo mkubwa wa kupiga picha nzuri kutokana na megapixel 12+24 ultra-resolution dual camera iliyoambatanishwa na teknologia ya AI.

Infinix ZERO 6 inapatikana katika maduka ya Infinix na Vodacom ikiwa na ofa ya GB 12 kwa miezi mitatu na zawadi nyingine. na Kutokana na ubora wa camera ya ZERO6, Infinix wanawapa wateja wao nafasi ya kujishindia Dola 10,000 (Sawa na Millioni 23 za Tanzania) kupitia kampeni yao ya "Beautiful Pictures". Kufahamu zaidi namna ya kushiriki, tembelea kurasa zao za Facebook Infinix Mobile Tanzania.

Kwa maelezo Zaidi kuhusiana na bidhaa za Infinix tembelea:
http://www.infinixmobility.com/

Tuesday, March 26, 2019

Faida ya kula Tufaa (Apple) kiafya

Tunda asili yake ni sehemu za Mashariki mwa Europe na pia Magharibi mwa Asia, na tunda hili linajulikana kwa miaka ya zamani mno katika miji ya Old China,  Babulon na Egypt.

Tunda hili hutumiwa na lina faida kubwa katika mwili wa mwanaadamu. Lina dawa ya maradhi tofauti:

Apple hutibu Anaemia
Apple lina wingi wa iron, arsenic na phosphorus, kwa mtu mwenywe ugonjwa huu inafaa kufanya juice ya apple iwe fresh. Ni vizuri kunywa juice hiyo glass moja kabla kula chakula (nusu saa kabla) na pia kabla ya kwenda kulala usiku.

Hutibu tatizo la kuharisha na kutapika
Mwenye kutokezewa na ugonjwa huu ni vizuri sana kutumia tunda hili (iwe bivu). Kila siku ale 2 pia kama yatapikwa au kuchomwa ni mazuri zaidi kwani hulainisha cellulose.

Hutibu matatizo ya tumbo.
Kuna matatizo tofauti ya tumbo, kwahivo tunda hili limekusanya matatizo yote ya tumbo na kuondoa matatizo hayo. Changanya apple, asali kidogo na ufura kidogo na kula kabla chakula hii husaidia kuondoa matatizo ya tumbo kama vile usagaji mdogo wa chakula na mengine.

Kuumwa na kichwa.
Tunda hili lina faida katika maradhi yote ya kichwa. Apple lilowiva limenye maganda yake, halafu ule kwa kutia chumvi kidogo kila siku asubugi kabla ya kula kitu chochote, na uendelee kufanya hivi kwa muda wa wiki 2.

Matatizo ya moyo
Apple ya wingi wa potassium na phosphorus lakini sodium inapatikana kidogo sana.Kwa wakai wa zamani watu walikuwa wakila matunda haya na asali, kwa ajili ya maradhi ya moyo na research imefanyika imeonekana kwa wale watu wanotumia vyakula venye potassium kwa wingi huepukana na maradhi ya moyo. Kwahili ni uzuri kula tunda hili pamoja na asali.

High Blood Pressure 
Apple linasaidia katika kuongeza kutoa (secreation) mkojo ambayo hii inasaidia kurudisha blood pressure katika hali ya kawaida, pia inasaidia kupungua kwa sodium chloride katika figo..

Hutibu matatizo ya meno
Matunda haya yanasaidia sana meno katika kuyasafisha na kuyaepusha na vijidudu na kuoza, kila baada chakula kula apple moja.

FULL VIDEO: A-Z sababu za kutaka kufutwa ACT Wazalendo! ''msajili afanye mambo anayoyajua'' Zitto


Mbunge wa Kigoma Mjini ambaye pia ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amefunguka kuhusiana na barua iliyowafikia kutoka kwa msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mutungi ambapo ametishia kukifutia usajili Chama hicho kutokana na kukiuka Sheria ya Vyama vya Siasa ikiwamo kuchoma moto bendera ya Chama cha Wananchi (CUF).

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE 

Bobi Wine amtumia salamu za vitisho Rais Museveni ‘siku zako zinahesabika za kukaa madarakani’

Msanii wa muziki nchini Uganda ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kyadondo, Bobi Wine amesema kuwa siku za Rais wa Taifa hilo, Yoweri Museveni za kukaa madarakani zinahesabika.


Bobi Wine
Bobi Wine akihutubia maelfu ya watu waliojitokeza katika ziara yake ya kutoa shukrani mjini Arua Jumapili iliyopita, amesema kuwa 2021 hana imani kama Museveni atasalia madarakani kwani amekuwa akiminya demokrasia hata ndani ya chama chake cha NRM, hivyo hawezi kushinda uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2021.

"Nakwambia (Rais Museveni) siku zako za kukaa madarakani zinahesabika. Inaingiaje akilini kutwambia uliingia msituni kutafuta Demokrasia ile hali unashindwa hata kuonesha Demokrasia ndani ya chama chako cha NRM, Tena ukiwa tayari umefikisha miaka 33 madarakani,". amesema Bobi Wine.

Ziara hiyo ya Bobi Wine, ililenga kuwapongeza wananchi wa jimbo la Arua kwa kumchagua Mbunge Kassiano Wadri ambaye alikuwa anampigia upatu kwenye kampeni za uchaguzi mwaka jana, kabla ya kukamatwa na kupigwa na jeshi la polisi kwa kuhusishwa na vurugu za kuzuia msafara wa Rais Museveni.

Kauli hiyo, inakuja ikiwa ni siku chache zimepita tangu chama cha NRM kumtangaza kuwa, Rais Museveni ndiye atakayegombea urais mwaka 2021 kupitia chama hicho tawala.

Rais Museveni baada ya kupitishwa na chama chake, alisikika akimuonya Bobi Wine kuwa ni vyema angeendelea kwenye muziki na aachane na siasa.

Bobi Wine amejibu kauli hiyo kwenye ziara hiyo kwa kusema "Wakati yeye alivyokuwa na umri kama wangu alikuwa mchungaji, kwanini hakuendelea kuchunga na akaamua kuingia kwenye siasa?, nawambieni tuitafanya kama tulivyofanya mwaka jana hapa Arua.".

Bobi Wine amejipanga mwaka 2021 kugombea urais kama mgombea huru na tayari wanasiasa wengi wakongwe wamemtabiria kuwa atakuwa mpinzani mkubwa wa Rais Museveni.

MKUU WA MAJESHI AMTAKA RAIS ATANGAZE KUWA HANA UWEZO WA KUONGOZA NCHI


Kiongozi wa jeshi nchini Algeria ametaka rais wa taifa hilo Abdelaziz Bouteflika kutangazwa kuwa hawezi kuongoza tena taifa hilo kutokana na sababu za kiafya.

''Ni sharti tutafute suluhu ya tatizo hili baada ya wiki ya maandamano dhidi yake. Tutafute suluhu ya tatizo hili haraka iwezekanavyo, ndani ya katiba'' , alisema Luteni jenerali Gaed Salah katika hotuba yake ya runinga.

Rais huyo tayari amekubali kwamba hatowania muhula wa tano katika uchaguzi ujao ambao umecheleweshwa.

Lakini wanaandamanaji wanamshutumu kuwa na njama ya kuongeza utawala wake wa miaka 20.

Mazungumzo yameanzishwa kujadili hatma ya siku za baadaye ya Algeria ambayo yataongozwa na mwanadiplomasia wa muda mrefu wa Umoja wa mataifa Lakhdar Brahimi.

Maandamano yalianza mwezi mmoja uliopita wakati rais huyo mwenye umri wa miaka 82 aliposema kuwa anapanga kuwania urais kwa muhula mwengine .

Lakini watu waliendelea kuandamana hata baada ya kusema kuwa hatowania tena muhula mwingine na badala yake wakataka kufanyika kwa mabadiliko ya haraka.

Luteni jenerali Gaed Salah awali alinukuliwa akisema kuwa jeshi na raia wanafikiria kuhusu hatma ya taifa hilo akitoa ishara kwamba jeshi linaunga mkono maandamano hayo.

Ni nini haswa alichosema mkuu huyo wa jeshi?

Katika hotuba yake iliopeperushwa hewani na kituo cha umma, kiongozi huyo wa jeshi na naibu wa wizara ya ulinzi alisema kuwa ''katiba ndio njia pekee ya kuleta uthabiti wa kisiasa'' .

Ametoa wito wa kutumika kwa kifungu 102 ambacho kinaliruhusu baraza la kikatiba nchini Algeria kutangaza wadhfa wa urais kuwa uko wazi iwapo kiongozi huyo hawezi kuongoza.

''Suluhu hii itavutia uungwaji mkono na lazima iungwe mkono na kila mtu'' , aliaesma Luteni jenarali Gaed Salah ambaye alipongezwa na maafisa waliokuwa wakitazama hotuba yake.

Tangazo hilo la jeshi la Algeria ni muhimu sana.
Hata hivyo, hali ya afya ya rais Bouteflika, na mgogoro wa kikatiba kuhusu utawala wake hadi uchaguzi mwengine utakapofanyika mbali na wito wa waandamanaji ambao wanasalia katika barabara za Algeria, hatua hiyo haitarajiwa kufanikiwa.

Bado kutakuwa na maswali kuhusu uamuzi huo wa mkuu wa jeshi.

Katika miaka ya hivi karibuni, ni wandani wa kisiasa na wale wa kijeshi wa rais huyo ambao wamekuwa wakizungumza kwa niaba yake huku uwepo wake ukipingua kutokana na hali yake ya kiafya.

Luteni jenerali Ahmad Gaed Salah anaonekana kuwa mtiifu sana kwa rais Bouteflika na nguzo muhimu ya utawala wa rais huyo nchini Algeria ambapo wikendi iliopita gazeti moja la kibinafsi lilitaka atimuliwe madarakani pamoja na rais huyo.

Baraza la kikatiba la taifa ilo litalazimika kuunga mkono wito wake wa hivi karibuni na baadaye itasalia kwa bunge kuamua kuhusu hatma ya rais huyo.
Chanzo - BBC

Source

CUF YAFUNGUA KESI MAHAKAMANI DHIDI YA WALIOCHOMA MOTO BENDERA NA KUBADILISHA RANGI ZA OFISI YA CUF

Katibu mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Khalifa Suleiman Khalifa amesema wamefungua kesi ya kiraia mahakama kuu ya Vuga visiwani Zanzibar dhidi ya wote waliofanya vitendo vya kijinai kwa kuchoma moto bendera na kubadilisha rangi za ofisi ya chama hicho.

Katibu mkuu huyo ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua walizochukua kwa wanachama wa chama hicho waliohamia ACT Wazalendo kwa kuharibu mali za CUF ikiwemo bendera na ofisi za chama hicho.

Amesema takribani ofisi 100 za chama cha CUF zimepakwa rangi ya ACT Wazalendo hivyo hawawezi kufumbia macho hujuma hizo dhidi ya chama chao.

Katika hatua nyingine khalifa amesema wabunge wa CUF waliokuwa wanamuunga mokono maalim Seif Sharif Hamad wanatakiwa kushirikiana na chama hicho pekee na wale watakaobainika kuimarisha vyama vingine hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.

Kesi hiyo ya kiraia namba 19 ya mwaka 2019,imefunguliwa dhidi ya waliokuwa wanachama wa chama hicho kwa kuchoma bendera pamoja na kubadilisha rangi za ofisi za chama cha CUF visiwani Zanzibar,baada ya kuhamia chama cha ACT Wazalendo.

Mahakama ya Rufaa nchini Kenya, Imependekeza umri wa kufanya ngono uwe ni miaka 16 badala ya 18

Mahakama ya Rufaa nchini Kenya imependekeza umri wa kuruhusiwa kujihusisha na ngono nchini Kenya upunguzwe kwa miaka miwili. Kwa sasa, sheria za Kenya zinaruhusu vijana wa miaka 18 na kuendelea kufanya ngono. Kwa mujibu wa BBC. Gazeti binafsi la The Standard la nchini Kenya linaripoti kuwa majaji watatu wa mahakama hiyo wapendekeza maboresho ya sheria …

The post Mahakama ya Rufaa nchini Kenya, Imependekeza umri wa kufanya ngono uwe ni miaka 16 badala ya 18 appeared first on Bongo5.com.


Source

Kapteni wa Taifa Stars Mbwana Samatta, aiomba TFF kumjumuisha Shomari Kapombe katika zawadi watakazopewa wachezaji wa Stars

Mshambuliaji wa Tanzania na klabu ya KRC Genk, Mbwana Samatta ametumia ukurasa wake wa Twitter kuliomba shirikisho la soka Tanzania TFF kumjumuisha beki wa taifa stars Shomari Kampombe katika zawadi zao ambazo waliahidiwa a mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda . Shomari kapombe.kama captain ningeomba tff imuangalie katika zawadi ambazo wachezaji watapata,ikishindikana …

The post Kapteni wa Taifa Stars Mbwana Samatta, aiomba TFF kumjumuisha Shomari Kapombe katika zawadi watakazopewa wachezaji wa Stars appeared first on Bongo5.com.


Source

Rais wa Zanzibar Aipongeza Taifa Starts kwa Ushindi

Rais wa Zanzibar Aipongeza Taifa Starts kwa Ushindi
Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein ameipongeza timu ya soka ya taifa, Taifa Stars kwa kuifunga Uganda na kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika Afcon 2019.

Stars imefuzu fainali hizo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 39 kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Uganda kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam juzi.

Katika salamu zake hizo za pongezi, Rais Shein alisema wananchi wa Zanzibar na Tanzania nzima wamefarijika na ushindi huo ambao utaendelea kuipa hadhi kubwa Tanzania Kitaifa na Kimataifa katika anga za michezo.

Alieleza kuwa wananchi wa Zanzibar na Tanzania nzima wataendelea kuiunga mkono Timu yao hiyo kutokana na jitihada kubwa inazozichukua katika kuhakikisha inailetea ushindi Tanzania.

Aidha, Rais Shein alitumia fursa hiyo kuwapongeza wananchi wote kwa kuishangilia timu yao.

Alilipongeza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Kocha mkuu wa Stars, Emmanuel Amunike, watendaji na viongozi wote waliofanikisha ushindi huo kwa kuonesha kiwango cha hali ya juu.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...