Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu.
Aidha Sillo Vijana kuendelea kuiunga mkono Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuyasema na kuyatangaza mazuri yanayofanywa katika kila mkoa, wilaya, kata na kwenye vijiji.
Wito huo umetolewa na Naibu waziri wa Mambo ya ndani ya nchi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Babati vijijini Mheshimiwa Daniel Sillo wakati akifunga Mashindano ya mpira wa miguu (SILLO CUP) katika kata ya Ayasanda fainali iliyowakutanisha Kipanga FC na Dughai FC uwanja wa shule ya Sekondari Ghorowa Oktoba 22,2024.
Mheshimiwa Sillo amesema kuwa kupitia michezo ataendeleza mshikamano na mahusiano kati ya Vijana na Serikali kwani michezo ni ajira, afya.
Bingwa wa michuano hiyo kata ya Ayasanda Kipanga FC wamekabidhiwa mpira na jezi full set, wa Pili Dughai nafasi ya pili mipira miwili na mshindi wa tatu ni Ayasanda wamepatiwa mpira mmoja.
Kaulimbiu ya Mashindano hayo "alipo Sillo, Vijana tupo".