Monday, April 7, 2025
Msaada wa kisheria wawafikia wakazi wa Tanga (Mama Samia leagal Aid)
NA REBECA DUWE TANGA
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batlida Burian amewataka wananchi wenye migogoro mbalimbali ikiwemo ya ndoa na ardhi kujitokeza kwa katika kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia ambayo itafanyika kwa siku tisa katika kata zaidi ya 100 zilipo katika Halmshauri zote 11 za mkoani hapa.
Kampeni hiyo, ambayo tayari imeshafanyika katika mikoa 22 ya Tanzania Bara, imeweza kuwafikia wananchi zaidi ya milioni 2.2 na kushughulikia jumla ya migogoro elfu 20,000, ambapo migogoro zaidi ya 4000 imeweza kutatuliwa na kumalizika kabisa.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mkuu wa mkoa huyo amesema kuwa kampeni hiyo si yalele mama hivyo amewataka wananchi watoe taarifa za ukweli na za uhakika ili waweze kupatiwa msaada wa kisheria.
Kwa upande wake Laurent Burilo ambaye ni Afisa Uchunguzi Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria na Mratibu wa kampeni hiyo alisema kuwa changamoto zote walizokutana nazo katika mikoa hiyo 22 ambayo tayari wamepita kuzitatua kisheria.
Alisema miongoni mwa Migogoro ya Ardhi, Mirathi na ndoa ambayo inahatarisha amani na usalama wa familia na jamii, na wakati mwingine husababisha mivutano isiyokwisha, ambayo inazuia maendeleo na ushirikiano.
Burilo aliongeza kusema kuwa ni muhimu kwa jamii kuhamasika kutatua migogoro hii kwa njia ya amani ili kudumisha umoja na ushirikiano.
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kusikiliza wimbo wake mpya 2021 un...