Wednesday, January 30, 2019

Video: Baadhi ya viongozi Yanga watuhumiwa kwa upigaji wa mabilioni, Ten ahusishwa, Uongozi Mkuu walaani taarifa hizo

Uongozi wa klabu ya Yanga umemtaka mtu yoyote mwenye ushahidi kuwa baadhi ya viongozi wao wamehusika katika kuchukua mabilioni ya fedha, hayo yamejiri baada ya gazeti moja kuandika habari hiyo ambayo wamesema siyo ya kweli.

The post Video: Baadhi ya viongozi Yanga watuhumiwa kwa upigaji wa mabilioni, Ten ahusishwa, Uongozi Mkuu walaani taarifa hizo appeared first on Bongo5.com.


Source

Monday, January 28, 2019

WAKUU WA MIKOA WAKABIDHIWA VITAMBULISHO VYA WAFANYABISHARA AWAMU YA PILI


Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mgwhira vitambulisho


Wakuu wa Mikoa yote nchini wamekabidhiwa vitambulisho vya awamu ya pili vya wafanyabiashara wadogowadogo leo Jumatatu, Januari 28, 2019, Ikulu Jijini Dar es salaam.

Jumla ya vitambulisho milioni moja na laki moja vimekabidhiwa kwa wakuu hao wa mikoa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, ambavyo viliasisiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli mwishoni mwa mwaka uliopita.

Balozi Kijazi amekabidhi vitambulisho hivyo na kuwataka wakuu wa mikoa hiyo kuhakikisha vitambulisho hivyo vinatolewa kwa wahusika na kwa wakati kwa wahusika na kuongeza kuwa tayari kuna taarifa za baadhi ya watumishi wa halmashauri ambao wanaviuza vitambulisho hivyo kwa zaidi ya bei elekezi iliyotolea na Rais.

Pia amewataka wakuu hao wa mikoa kuwachukulia hatua za kinidhamu wale wote wanaokiuka agizo hilo.

Amewataka wakuu hao wa mikoa kusimamia kikamilifu zoezi hilo la ugawaji wa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo wadogo huku akitaja idadi ya vitambulisho ambavyo kila mkoa utakabidhiwa.

Saturday, January 26, 2019

Tanzia : MUIGIZAJI WA FILAMU TANZANIA AFARIKI DUNIA


Marehemu Mama Abdul enzi za uhai wake.

Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifamba, amesema msiba wa muigizaji Mama Abdul ni msiba ni pigo kwenye kiwanda kizima cha filamu Tanzania na wasanii wanatakiwa kuungana kuifariji familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu.

Akiongea kwa njia ya simu Mwakifamba amesema amepokea taarifa za msiba huo akiwa safarini hivyo hajaongea na familia juu ya chanzo cha msiba huo lakini anafanya mawasiliano usiku huu ili kujua undani wake.

''Nipo safarini ndio nimefika usiku huu, kuhusu chanzo cha kifo chake bado sijawasiliana na familia lakini niwaombe tu wasanii wenzangu tuungane katika kipindi hiki kigumu cha kumhifadhi mwenzetu kisha mimi nafanya mawasiliano na familia na nitatoa taarifa rasmi'', amesema.

Kwa mujibu wa taarifa ya mapema iliyotolewa na Kamati ya Matukio Maadili na mikataba ya Chama cha waigizaji TDFAA (M) Kinondoni na Ubungo ilieleza kuwa msiba huo umetokea mchana leo nyumbani kwake Mburahati na msiba upo hapo nyumbani.

Aidha ilifananua kuwa taarifa juu ya taratibu za mazishi itatolewa baadaye baada ya kikao na familia, huku wasanii pia wakiombwa kushirikiana.

Baadhi ya wasanii walioonesha kusikitishwa na msiba huo ni pamoja na JB, Riyama Ally, Johari, Monalisa na wengine.
Mtangazaji, Zamaradi kupitia ukurasa wake wa Instagramu ameandika "Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa SALOME NONGE maarufu kama MAMA ABDUL."

"Kwa wasiomfahamu kama uliwahi kuangalia filamu ya KIGODORO 'kantangaze' nilibahatika kufanya nae kazi enzi za uhai wake, lakini pia kwa ambao hawajabahatika kuona filamu hiyo unaweza kumuona kupitia tamthilia ya MWANTUM kwenye stesheni ya Magic Swahili DSTV," aliandika Zamaradi huku akimalizia hiv; MUNGU amuweke mahala pema peponi Mama Abdul' Inalillahi wainailaihi Rajiun'

Kwa upande wake mama yake mzazi Monalisa ambaye anajulikana kama Natasha Mamvi ameandika TANZIA;RAFIKI YANGU KIPENZI.MZAZI MWENZANGU.MWIGIZAJI MWENZANGU SALOME NONGE (MAMA ABDUL) AMEFARIKI. NI PENGO AMBALO HALITAZIBIKA KAMWE.RIP MAMA ABDUL.

Naye Monalisa ameandika," Mama Abdul Jamani, Pumzika kwa amani tutakukumbuka daima."

Joti naye ameandika R.I.P Mama Abdull.Mimi mwanao Sina cha kuongea zaidi ya kukuombea upate mwanga wa milele, Pumzika kwa amani mama."

Kuwa Mjanja..Download App mpya ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari za michezo moja kwa moja Kwenye Simu yako

Friday, January 25, 2019

Mapenzi Hayana Nafasi kwa Diana

Mwanadada Diana Kimari amefunguka na kusema kuwa moja kati ya vitu ambavyo kwake sio muhimu sana ni kufanya mapenzi kuwa sehemu ya maisha yake  hata kama yuko katika mahusiano . Diana anasema kuwa kitedno cha kuwa katika mahusiano na kuyaweka mbele sana kunaweza kufanya kushindwa kufanya vitu vingine  vya maana ambavyo anahisi vinaweza kumpa faida zaidi kuliko kile anachokifanya. siyo kwamba sina mapenzi, ni kwamba sijamchukulia kihivyo huyo mwanaume kwa sababu naona kuna vitu vingine ninaona nina vitu vingi sana vya kufanya kwa sababu  nikijikita huko naona nitaharibu mambo mengi sana,  na ndio maana sitaki kumuonyesha mahali popote kwa sasa.  

The post Mapenzi Hayana Nafasi kwa Diana appeared first on Ghafla! Tanzania.


Source

Hawa Asimulia Alivyonusurika Kifo

Afya ya Hawa kwa sasa imeimarika na kurudi katika hali yake ya kawaida baada ya kuchungulia kaburi, jambo ambalo hata yeye mwenyewe hakulitegemea kwani alishakata tamaa ya kuishi. Mwishoni mwa mwaka jana, Hawa alipelekwa kwenye matibabu nchini India kutokana na tatizo lake la tumbo kujaa maji. Jitihada hizo za matibabu ya Hawa zilifanywa na mwanamuziki Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' aliyeshirikiana naye kwenye Wimbo wa Nitarejea. Baada ya kurejea Bongo, Hawa aliwekwa mafichoni kwenye hoteli moja jijini Dar kutokana na maelekezo kutoka kwa madaktari ambao walitaka iwe hivyo kwa miezi mitatu. Baada ya miezi hiyo mitatu, Hawa alirejea nyumbani kwao, Buguruni-Rozana jijini Dar kuendelea na maisha yake kama kawaida. Risasi Mchanganyiko lilimuibukia nyumbani hapo ili kufanya naye mahojiano kuhusu hali yake kwa sasa na mambo aliyoyapitia. "Kwa kweli ninamshukuru sana Mungu maana bila yeye, huenda nisingekuwepo, leo hii naweka tabasamu usoni, lakini niliteseka mimi jamani. Hadi ninasafiri kwenda India nilikuwa na maumivu makali hadi nilihisi kama nataka kuchanganyikiwa, yaani hadi kumsimulia mtu nahisi kama nitampunja kwa sababu hayaelezeki, yalikuwa makali sana. 

The post Hawa Asimulia Alivyonusurika Kifo appeared first on Ghafla! Tanzania.


Source

Mr Blue afunguka historia ya maisha yake na kuhusu kutokupata tuzo yeyote mpaka sasa hivi (+ Video)

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Henry Samir alimaarufu Mr Blue amefunguka mwanzo mwisho kuhusu historia ya maisha yake Msanii huyo wakati akipiga stori na Bongo5 amesema haya:- By Ally Juma.

The post Mr Blue afunguka historia ya maisha yake na kuhusu kutokupata tuzo yeyote mpaka sasa hivi (+ Video) appeared first on Bongo5.com.


Source

Thursday, January 24, 2019

Bi. Hindu Amtaka diamond kuiga mfano wa Alikiba kwenye Kuoa

Moja ya watnagzaji na wasanii wakongwe katika snaa Bi hindu amefunguka na kuwafunda wasanii huku akimtaka msanii Daimond platinumz kufanya uamuzi wa kuoa kwa sasa kwa sababu umri wake umeenda na anazidi kuongeza watoto. Bi hindu amemtaka Diamond kuiga mfano wa msanii mwenzake Alikiba mabe aliamua kuoa kimya kimya baada ya kuona kuwa muda wake wa kuoa umefika na ndoa yake imekuwa ya heshima sana. Bi hindu pia nasema kuwa kwa umri wake kwa sasa angeacha taba yake ya kuimba nyimoz za matusi kwa sababu pa ya jina lake ambalo lmekuwa kubwa na kutunza heshima yake, maneno haya yanakuja  baada ya mfululizo wa matukioa ya adhabu na pia kufungiwa kwa msanii huyo kutokana na utovu wa nidhamu katika nyimbo anazotunga.

The post Bi. Hindu Amtaka diamond kuiga mfano wa Alikiba kwenye Kuoa appeared first on Ghafla! Tanzania.


Source

Friday, January 18, 2019

Tazama A-Z ya mazishi ya baba yake Alikiba, Waziri Kigwangalla, Mwana FA, Dully Sykes na mastaa kibao wahudhuria (+video)

Tazama full video ya mazishi ya mwili wa baba yake msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Alikiba marehemu, Mzee Saleh Kiba yaliyofanyika katika makaburi ya Kisutu jijini Dar Es Salaam. Kwenye mazishi hayo, yamehudhuriwa na watu wakiwemo viongozi wa Serikali na wasanii wa muziki.

The post Tazama A-Z ya mazishi ya baba yake Alikiba, Waziri Kigwangalla, Mwana FA, Dully Sykes na mastaa kibao wahudhuria (+video) appeared first on Bongo5.com.


Source

Serikali: Tundu Lissu alishindwa kujibu maswali ya BBC, aliishia kubabaika tu



Msemaji wa Serikali, Dk Hassan Abbas amemjibu mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu, akidai kuwa mwakilishi huyo wa wananchi anazungumza uongo kuhusu maendeleo ya Tanzania.

Dk Abbas amesema kwamba licha ya kuulizwa mazuri ya Serikali lakini Lissu alishindwa kujibu na badala yake aliishia kubabaika.

Akihojiwa na kituo cha Utangazaji Uingereza (BBC) jana Januari 16, 2019, Lissu amezungumza masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na maoni yake kuhusu maendeleo ya nchi, utawala wa katiba na mpango wake wa kugombea urais.

"Unakwenda Ulaya unaponda nchi yako eti haifuati Katiba wakati wewe mwenyewe kuanzia ubunge wako, sifa za ubunge wako na taratibu za uchaguzi wa ubunge wako vyote vipo kwenye Katiba na ndio maana ukawa mbunge," amesema Dk Abbas.

Dk Abbas amedai Lissu hata alipoulizwa mazuri aliyoyaona licha ya changamoto zilizopo, alishindwa kujibu vyema.

"Angalia alivyoshindwa si tu kueleza jema moja la nchi yake baada ya kupewa fursa hiyo, bali kashindwa hata kueleza jema moja alilofanya yeye binafsi jimboni kwake, kaishia kubabaika tu," amedai Dk Abbas.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano ina dhamira tofauti na ile waliyonayo watu wa aina ya Lissu, hivyo itaendelea kutekeleza wajibu wake katika kuwaletea Watanzania maendeleo ya kweli.

"Sisi tunapigania maendeleo na Watanzania wanaona kazi kubwa inayofanyika kote nchini iwe reli, maji, viwanda, umeme na mambo mengine. Hakuna wa kutuzuia katika kuiletea Tanzania maendeleo. Hakuna," amesisitiza.

Source: Mwananchi

Tuesday, January 15, 2019

Msanii wa Afrika Kusini Atoa Siri ya Kuimba Kiswahili na Kufikisha Viewers Milion 3 Youtube


Msanii wa kike wa muziki nchini Afrika Kusini, Sho Madjozi ambaye anatamba na wimbo wa Kiswahili unaojulikana kwa jina la 'Huku', ameitaja siri iliyomfanya hadi kuimba wimbo huo.

Madjozi ameimba wimbo huo kwa mashairi ya Kiswahili, hali iliyopelekea watu wengi kushangazwa na uwezo wake wa matamshi ilhali sio raia wa nchi za Afrika Mashariki ambazo zinatumia zaidi lugha hiyo.

Kupitia ukurasa wake katika mtandao wa Twitter, Madjozi ameandika kuwa familia yake ilihamia kuishi nchini Tanzania mwaka 2008, jambo liliomsaidia kukuza ujuzi wa lugha hiyo na kutoa wimbo wake mwaka uliopita.


Wimbo huo uliachiwa mwezi Mei, 2018 ambapo katika Youtube umetazamwa mara milioni 3.3 na kuufanya kuwa maarufu nchini Afrika Kusini.

Monday, January 14, 2019

Njia za kuepukana na madeni


Hakuna mtu anayependa kuwa na madeni, lakini mara nyingi watu hujikuta katika madeni makubwa. Kwa kiasi kikubwa watu wengi huingia kwenye madeni kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha matumizi kuliko kipato.

Madeni siyo kitu kizuri hasa ikiwa hayatalipwa kwa wakati. Swala la kuepuka madeni ni swala linalohitaji maamuzi sahihi ya kifikra pamoja na mikakati stahiki.

Je unapenda kuepuka au kupunguza kiwango chako cha madeni? Karibu nikufahamishe njia  za kuepuka madeni.

1. Jiwekee bajeti binafsi
Utawasikia watu wakikosoa bajeti ya serekali lakini hawana bajeti zao binafsi. Bajeti binafsi ni muhimu kwani hukuwezesha kupanga juu ya mapato na matumizi yako.

Ili kuepuka madeni, ni muhimu kuweka bajeti binafsi ambayo itakuongoza juu ya matumizi yako ya pesa ili usije ukatumia kuliko kipato chako.

2. Epuka matumizi yasiyo ya lazima
Kuna matumizi chungu nzima ya pesa, lakini matumizi ya lazima ni machache. Ikiwa kipato chako ni kidogo hakuna haja ya kufanya mambo kama vile kununua simu au nguo za gharama kubwa.

Nimeshuhudia baadhi ya watu wakikopa mikopo kwa ajili ya sherehe na matumizi mengine ya anasa. Mambo kama haya huwaingiza watu wengi kwenye madeni makubwa, hivyo yakupasa kuyaepuka.

3. Epuka kukopa bila mpango
Watu wengi hushindwa kurejesha mikopo kutokana na kukopa bila mpango. Inatakiwa kabla ya kukopa uhakikishe una mpango mzuri unaoonyesha jinsi utakavyotumia na kurejesha mkopo huo.

Kumbuka pesa ya mkopo hasa kutoka kwenye taasisi za kifedha inatakiwa irejeshwe kwa wakati tena kwa riba. Hivyo epuka kutumia pesa za mkopo bila mpango unaoeleweka vyema.

4. Epuka ushawishi wa marafiki kwenye matumizi
Watu wengi hutumbukia kwenye matumizi makubwa au yasiyo na ulazima kutokana na ushawishi wa marafiki kwenye matumizi yao ya pesa.

Hakikisha kila unachokinunua au kutumia pesa yako kina maana kwako na hakitakupotezea pesa zako. Kumbuka mrejeshaji wa mkopo ni wewe na wala siyo rafiki yako


5. Tumia kidogo kuliko unachopata
Mara nyingi matumizi huwa makubwa kuliko kipato; na hii ndiyo sababu kubwa ya watu kukopa pesa. Hakikisha unajitahidi kutumia pesa kidogo kuliko zile unazozipata ili ujiwekee akiba na uweze kukidhi mahitaji yako ya msingi.

6. Weka akiba
Kuna kipindi cha shibe na njaa kwenye uchumi; hivyo unahitaji kujiandaa kwa vipindi vyote. Mara nyingi watu hukopa pindi wawapo na uhitaji.

Kwa njia ya kujiwekea akiba utaweza kuwa na pesa hata wakati huna kipato. Kumbuka! Kuweka akiba siyo kuwa na pesa nyingi bali ni maamuzi tu.

Kwa hakika nidhamu ya matumizi ya pesa ni jambo muhimu sana katika kuepuka madeni. Naamini pia kama utazingatia hoja jadiliwa hapo juu huku ukihakikisha unakuwa na matumizi mazuri ya pesa, utaweza kupunguza kama siyo kuepuka madeni maishani mwako.
Source

Friday, January 11, 2019

Uongozi wa Airport Wajibu Tuhuma za Ray Kuibiwa Mizigo

Uongozi wa uwanja wa ndege  wa mwl julius kambarage nyerere wamejibu tuhuma za kuibiwa kwa msanii ray kigosi baada ya msanii huyu kulalamika sana kuwa aliibiwa mizigo yake baadhi akiwa uwanja wa ndege. Uongozi wa uwanja wa ndege unasema kuwa mtu yoyote anapopata tatizo lolote ni vizuri zaidi kama watatoa taarifa moja kwa moja kwa uongozi na sio kuandika katika mitandao ya kijamii kama ambavyo wamekuwa wakifanya baadhi ya watu. katika ukurasa wa insta wa msanii Ray kigosi aliandika ”

The post Uongozi wa Airport Wajibu Tuhuma za Ray Kuibiwa Mizigo appeared first on Ghafla! Tanzania.


Source

Wednesday, January 9, 2019

Flaviana Matata Foundation Yatoa Vifaa Mashuleni.

Mwanadada ambae amefanikiwa sana katika kazi zake za mitindo Flaviana matata kupitia foundation yake wameweza kufanikiwa kutoa misaada kwa watoto wa shule ya msingi mzinune kwa kuwapa vifaa vya shule kwa mwaka 2019. katika ukurasa wake wa instagram, Flaviana amenadika kuwa amefanikiwa kuwapa wanafunzi 284 wa shule hiyo ili waweze kwenda shuleni kwa mwaka mpya wa masomo. Flaviana ameandika >>>"Leo muhula mpya wa masomo kwa mwaka 2019 umeanza. Taasisi yetu @flavianamatatafoundation ambayo ni walezi wa Shule ya Msingi Msinune tunaendelea na utaratibu wetu wa kugawa vifaa vya kujifunzia kwa wanafunzi na vifaa vya kufundishia kwa walimu vitakavyotumika kwa mwaka mzima" "Kwa mwaka 2019, watoto 284 wa Shule ya Msingi Msinune kila mmoja kapata begi la shule, kalamu za wino 50 , kalamu za risasi 50 na vifutio ambavyo vitakidhi mahitaji yao kielimu kwa mwaka huku wazazi wakitimiza mahitaji mengine yaliyobaki. Upande wa walimu taasisi imetoa kalamu, chaki, rejista za masomo na karatasi (reams) kwa ajili ya kudurufu (copy) mitihani na kazi za masomo"      

The post Flaviana Matata Foundation Yatoa Vifaa Mashuleni. appeared first on Ghafla! Tanzania.


Source

Tuesday, January 8, 2019

Slim Sosa afunguka kuhusu muziki wake, kutoswa na wasanii na mengine (Video)

Msanii wa muziki wa Hip Hip ambaye anafanya vizuri na wimbo Control, Slim Sosa amefunguka mengi kuhusu muziki wake pamoja na mtindo wa baadhi ya wasanii wa muziki kushindwa kuwasupport wasanii wenzao pale wanapohitaji msaada.

The post Slim Sosa afunguka kuhusu muziki wake, kutoswa na wasanii na mengine (Video) appeared first on Bongo5.com.


Source

Monday, January 7, 2019

Hatugusani Mpaka Ndoa :-Mc pilipili

Wikiedn iliyopita , mchekeshaji mc pilipili amemvisha pete ya uchumba , mchumba wake wa siku nyingi tayari kwa ajili ya ndoa , lakini kutokana na sherai na taratibu za dini, mchekeshaji huyo anasema kuwa hawako tayari kufanya mapenzi maka pale watakapofunga ndoa . Mc pilipili aliweka wazi kuwa alitoa mahali ya binti huyo kiasi cha shilingi milioni 8,  na wala haoni shida kusubiri mpaka atakapofunga ndoa na binti huyo ambae ni chaguo lake. ni kweli nimeokoka na ndioa maana kwenye sherehe ya mahaki hakukuwa na vinywaji vikali, hatyuishi pamoja na mpenzi wangu ila anaweza kuja nyumbani kupika, hatutagusana na mpenzi wangu mpaka tutakapofunga ndoa. Mc ilipili anasema kuwa waliweza kukubaliana na mshenga kiasi cha shilingi milioni 8 lakini waliweza kuongea na kulipa milion 5 , mpaka sasa anadaiwa milioni 3.

The post Hatugusani Mpaka Ndoa :-Mc pilipili appeared first on Ghafla! Tanzania.


Source

Thursday, January 3, 2019

Clouds Fm Yashika Nafasi ya Tatu Afrika

Moja ya Radio maarufu Tanzania clouds fm chii ya Clouds Media wameshika nafasi ya  tatu afrika ikiwa kama moja ya changamoto kubwa kwa radio nyingine  kubwa tanzania hasa kutokana na ukubwa wa radio hiyo na wafanyakazi pia. Radio hiyo ambayo imetajwa kati ya aradio kubwa afrika,  imekuwa moja ya radio inayisikiliza sana maoni ya wasikilizaji na hata kujali sana kile kinachotoka kwa mashabiki na ndio maana imekuwa moja ya radio zinazosikilizwa sana na watu. Mahabiki wameipongeza sana radio hiyo pamoja na kwamba kwa sasa kumekuwa na sintofahamu kuhusu hali ya bosi ya media hiyo bwana RUGE MUTAHABA kutokana na kuwa amekuwa akiripotiwa kuumwa.  

The post Clouds Fm Yashika Nafasi ya Tatu Afrika appeared first on Ghafla! Tanzania.


Source

Wednesday, January 2, 2019

VIDEO: Diamond Ashikwa Makalio Jukwaani Mombasa!

Diamond Platnumz, ameshikwa makalio na mashabiki akiwa jukwaani, baada ya kuwageukia na kuanza kukata mauno kihasarahasara, jambo lililozua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii. Video:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...