Friday, January 31, 2020

VIDEO: Spika Ndugai amlipua Zitto, sakata lake latinga kwa mwanasheria mkuu ''kaisaliti nchi''


Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai ameliambia Bunge kuwa watahitaji maelezo ya Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kwa nini aliandika barua kwenda Benki ya Dunia ili Tanzania ikose mkopo ambao lengo lake ni elimu kwa sababu za utofauti wa kisera.

"Mbunge mwenzetu atakaporudi labda anaweza akatufafanulia, Mhe. Zitto kuandika barua World Bank nchi yetu ikose fursa ya mkopo ,kwasababu ya tofauti za sera..lakini na ku-block Tanzania isipate fursa fulani nadhani ni kwenda mbali,Sijui mbunge unafaidika nini," amesema Job Ndugai.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI..,.....USISAHAU KUSUBSCRIBE


Source

Saturday, January 18, 2020

BABA AMPA UJAUZITO BINTI YAKE WA DARASA LA NNE...ATOWEKA NAYE KUSIKOJULIKANA


Mkazi wa kijiji cha Milala Kata ya Misunkumilo Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi aitwaye Deus Richard (40) anadaiwa kumpa ujauzito binti yake wa Darasa la Nne (jina linahifadhiwa) na kumtelekeza mkewe na watoto wadogo watano na kutoweka kusikojulika na mtoto wake aliyempa mimba.

Bi Mariam Masanja ambaye ndiye Mke aliyetelekezwa, amesema kuwa alipobaini uhusiano wa kimapenzi baina ya mwanae na Baba yake aliwaeleza viongozi wa Dini, kitendo ambacho kilimkasirisha bwana huyo na kuanza kuonesha bayana mapenzi yake na mtoto wake.

Aidha Mariam ameongeza kuwa licha ya ugumu wa maisha anaopitia kwa sasa, kutokana na kutelekezwa akiwa na watoto wadogo na pia ndani kukiwa hakuna chakula, anaiomba Serikali kumkamata mumewe na kumchukulia hatua kali za kisheria.

Friday, January 17, 2020

Monday, January 13, 2020

Chama Cha Wamiliki wa Mabasi (TABOA) mbioni kuanza kukatisha tiketi Kielectroniki



Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma

Chama cha wamiliki wa mabasi nchini (TABOA)kimesema kipo katika hatua nzuri kukamilisha zoezi la  kuanza kukatisha tiketi kwa njia ya kielektroniki  ili kupunguza msongamano na usumbufu kwa abiria hasa wakati wa msimu wa sikukuu.

Akizungumza na Muungwana blog Katibu wa TABOA Enea Mruto amesema baada ya kikao chao na mamlaka ya mapato nchini TRA kufikia makubaliano  taratibu za ukatishaji tiketi kwa njia ya elektroniki unaarajia kuanza mwezi ujao kwa mabasi yote.

"Kama TRA hawatatuangusha kile tulichokubaliana nao basi mpango huo utaanza rasmi mwezi ujao tunahitaji kufanya kazi kwa kwenda na teknolojia mpya kuondoa usumbufu kwa wateja wetu "amesema Mruto.

Amesema wakakamilisha baadhi ya taratibu mpango huo utazinduliwa rasmi na kuwekwa agizo kwa mabasi kuanza kutumia njia hiyo ambayo inawarahisishia wateja kupata tiketi rahisi au kuweka booking kwa njia ya mtandao.

Amesema licha ya kuwa baadhi ya kampuni zimejaribu kuanza mpango huo ila rasmi itakuwa mwezi ujao kwa mabasi yote kuanza kutumia mfumo huo utakao warahisishia wateja wao kupata tiketi kwa njia salama.

Akizungumzia agizo la Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye,  kuhakikisha mabasi yote yasiyokuwa na vibali kusafirisha vifurushi.

Amesema hata katika mkutano wao wamiliki walisisitiza agizo hilo ili kuendana na Sheria zinavyohitaji na kwenda sambamba na Serikali inavyoagiza.

"TABOA tunatekeleza agizo hilo atakayekiuka atakupambana na mkono wa sheria hivyo kila mmoja anapaswa kutekeleza sheria, "amesema.

Katika hatua nyingine Mrutu amesema moja ya mikakati waliojiwekea ni kuhakikisha wanapunguza ajali za barabarani kwa kuhimiza umakini katika kampuni za mabasi hususa ni kwa madereva kutii Sheria na taratibu zilizowekwa.

Amesema wao kama TABOA watakuwa wakisisitiza wamiliki wa mabasi kufanya ukaguzi katika vyombo vyao vya moto ili kunusuru ajali zinazotokea mara kwa mara.

WAZIRI DKT. KALEMANI AKAGUA TENA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UMEME WA MAJI WA JULIUS NYERERE MW 2115, AAGIZA WAKANDARASI KUHAKIKISHA WAFANYAKAZI WAO WOTE WANAHAMIA ENEO LA MRAD



NA MWANDISHI WETU, RUFIJI

WAZIRI wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, amefanya ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius Nyerere Mw 2115 (JNHPP) uliotimiza mwaka mmoja tangu kuanza kwa utekelezaji wake.

 Dkt. Kalemani ameridhishwa na hatua mbalimbali ambazo mradi huo unaotekelezwa kwenye mto Rufiji kwenye mpaka wa mikoa ya Pwani na Morogoro umefikia tangu kuanza kwa ujenzi wa mradi. 

Aidha, alitoa maagizo kwa Wakandarasi kuhakikisha Wafanyakazi wao wote wanahamia eneo la mradi, huku akitoa mwezi mmoja kwa wafanyakazi wengine wa mradi wawe wamehamia. 

"Wafanyakazi wote wakae eneo la mradi, hii itaharakisha mradi kukamilika mapema na haraka", alisema Dkt. Kalemani. Pia, alisisitiza kazi zote zinazohusu utoaji huduma zifanywe na Makampuni ya kitanzania ikiwemo Wakandarasi wasaidizi. 

Mkataba wa ujenzi mradi wa Julius Nyerere ulisainiwa Desemba 12, 2018 Ikulu Jijini Dar ea Salaam ambapo Mkandarasi alikabidhiwa eneo la mradi Februari 14, 2019 na kuanza kazi za maandalizi ya ujenzi kwa kipindi cha miezi sita, ambapo mwezi Juni 2019 alianza rasmi kazi za ujenzi. Mradi wa Julius Nyerere unatarajiwa kukamilika 14 Juni 2022
 Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani, (kushoto), akimsikiliza Mratibu wa ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius NyerereMw 2115 (JNHPP) wa mto Rufiji mkoani Pwani, Mhandisi Steven Manda wakati alipofanya ziara ya kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa mradi  huo.
 Dkt. Kalemani (kulia) akitoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka (kushoto kwa waziri), wakati wa ziara hiyo leo Januari 12, 2019.





Sunday, January 12, 2020

VIDEO: Nyalandu alipuka, asimulia alivyopigiwa simu na Rais mstaafu Kikwete


Mwenyekiti wa Chama cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA Kanda ya kati Lazaro Nyarandu amesema kama Chama Kanda ya kati wamejiimarisha kuhakikisha wanashinda ubunge katika jimbo la Dodoma Mjini, na miji yote iliyokatika kanda hiyo na hawatakubali kuyumbishwa na kitu chochote.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI........USISAHAU KUSUBSCRIBE

Saturday, January 11, 2020

Upendo unahitaji mambo haya

Upendo unahitaji mambo yafuatayo ambayo ndio msingi wa upendo. Kuna vitu ambavyo upendo unahitaji;

1. Tumaini (Hope)
Upendo unahitaji Tumaini, kwa lugha ya Kiyunani 'elpis' lenye maana ya
(a) Favourable
(b) Confident, expectation

2. Uvumilivu (patience)
Upendo unahitaji uvumilivu kuvumiliana. Hakuna mwanadamu aliyekamilika katika mambo yote, unajua Waswahili wanasema "mvumilivu hula mbivu " mvumilivu katika upendo maana yake hii ni shule ya kila siku, tunajifunza kutokana na makosa. Uvumilivu unatakiwa sana katika upendo - unajua kumfanya mwenzi wako kuwa kama wewe unavyotaka awe inahitaji uvumilivu. Hilo ni kweli, maana mmetoka mazingira tofauti na malezi tofauti; hivyo kumbadilisha inahitaji uvumilivu.

3. Kiasi
Kiasi ni kitu muhimu. Chochote kinachofinywa zaidi ni hatari, unatakiwa uwe na kiasi katika mambo yako ili uweze kudumu katika upendo maana upendo unahitaji kiasi. Usijifanye uko (busy) sana unakosa hata nafasi/muda wa kukaa na mwenzi wako, lakini wewe unarudi usiku, huo sio upendo. Nakuombea uwe na kiasi ili uenzi katika maisha yako.

4. Kutiwa moyo
Upendo unahitaji kutiwa moyo. Mtie moyo mwenzi wako ukimwambia pole asali wangu wa moyo, Unafanya vizuri sana, umefanya vizuri sana, unapoweza kumtia moyo mwenzi wako kwa yale anayofanya yanamuhamasisha kutenda zaidi na kukupenda zaidi. Kutiwa moyo ni kufarijiwa, moyo unahitaji kutiwa moyo, kuthaminiwa. Hivyo katika upendo unahitaji kumtia moyo mwenzi wako ili upendo huo udumu maishani mwako. Ikiwa hauna tabia ya kumtia moyo mwenzi wako ipo siku utampoteza, akipata watu wanaothamini mambo anayoyafanya na kumfariji. Atulie badilika uuteke upendo kwa kufuata masharti yake.

5. Kutambuliwa
Upendo unahitaji kutambuliwa katika maisha yako na kujua umuhimu wake. Kutambuliwa ni kitu muhimu sana katika maisha, kumtambua mpenzi wako na umuhimu wake kwako. Atambulike toka moyoni mwako kuwa anafaa kuwa mumeo au mke wako, hivyo upendo unahitaji sana utambuliwe na wewe mwenyewe. Umfahamu na umuelewe kiundani.

6. Uaminifu
Upendo unahitaji uaminifu kwa mwenzio sio msaliti wenye kujitunza na kujiheshimu mtu asiye na hila ndani yake uaminifu ni dawa ya upendo katika maisha yetu tukikosa uaminifu sisi kwa sisi upendo hautaweza kukaa pamoja nasi.

7. Usawa
Upendo unahitaji usawa unajua mapenzi ni kusaidiana hakuna kiongozi wa mapenzi bali tunasaidiana hivyo huo ndio usawa katika mapenzi upendo unahitaji usawa huo wewe unawajibu kwa mwenzi wako na mwenzi wako anawajibu kwako.

8. Urafiki
Upendo unahitaji urafiki upendo hujenga urafiki mwenzi wako ni rafiki yako kuliko marafiki ulionao katika maisha yako- Mapenzi wako sio adui yako mficha siri wako usimuogope maana upendo hauna hofu unatakiwa kuzungumza na rafiki yako kirafiki ili upendo uwezo kudumu na kushamili.

9. Kukubalika
Upendo unahitaji kukubalika, kupokelewa toka moyoni mkubali mwenzi wako apate kibali moyoni na maishani mwako ukimkubali hautamuumiza hivyo upendo unataka kukubalika hapo utafurahia maisha yako.

10. Ukweli
Upendo unahitaji ukweli,upendo ni adui wa uongo unatakiwa uwe mkweli katika mapenzi yenu,ukweli hujenga upendo, ukweli huimarisha mahusiano,upendo unahitaji mtu ambaye ni mkweli kwa mwenzi wake,ukweli ndio upendo wenyewe unatakiwa uwe mkweli ili upendo uchukue nafasi moyoni mwako.

11. Imani
Upendo unahitaji imani na imani ni kuwa na uhakika wa mambo yatarajiwayo ,ni bayana ya mambo yasio onekana. Unatakiwa kuwa na imani na mwenzi wako, imani katika mahusiano ni muhimu sana kuaminiana ,toa wasiwasi kwa mwenzi wako, mwamini kuwa amekuchagua wewe na hakuna mwinginen wewe uko peke yako.

12. Penzi
Upendo unahitaji penzi la kweli linalotoka moyoni ,penzi kwa mpenzi wako ni muhimu sana kama litatumika kwa utaratibu na kwa uaminifu kabisa maana penzi linahitaji muda hivyo hivyo unatakiwa uwe na muda wa kutosha ili uweze kupata pendo la kweli.

13. Ujasiri
Upendo unahitaji uwe jasiri katika hali zote ujasiri katika kunena ,ujasiri kutenda, ujasiri katika kuuzungumzia upendo kwa mwenzi wako upendo unamhitaji mtu jasiri sio kitu rahisi kama wengine wanavyozungumzia.

14. Mawasiliano
Upendo unahitaji mawasiliano maana mawasiliano hutengeneza mahusiano ,bila mawasiliano hakuna mahusiano imara na ili ujenge msingi mzuri wa mahusiano yako unahitaji uwe mtu mzuri katika mawasiliano- mawasiliano yana uwezo mkubwa sana wa kutunza mahusiano hivyo upendo unahitaji mawasiliano.

15. Asante
Upendo unahitaji neno asante kwa mwenzi wako kwa lolote atakalo litenda kwako kama atakupa zawadi asante hasa kwa mpenzi wako ni neno muhimu sana na linaongeza nguvu ya mapendo
Uwe unatumia neno hili asante kwa mpenzi wako maana upendo unahitaji neno hili ASANTE.
Hata baada ya kutoka katika tendo la ndoa sema asante maana ni tendo la ndoa ni matokeo ya mapendo. Hivyo upendo unahitaji ASANTE.

16. Haki
Upendo unahitaji haki ,unatakiwa umtendee haki mwenzi wako usimyime haki yake ya msingi kumtunza kumpenda na kumtimizia haki zake zote, najua unajua haki za mpenzi wako- upendo ili ukomae unahitaji haki iwepo katika mahusiano yenu.

17. Sifa
Upendo unahitaji sifa ,unatakiwa kumsifia mwenzi wako kuwa umependeza sana mpenzi wangu, unapika vizuri kuliko wengine, mpenzi wangu umevaa vizuri, unavutia mpenzi wangu, umeumbika vizuri, unatabasamu zuri , kwakila anachokifanya kizuri kwako msifu usiache wengine wamsifu mume wako au mke wako utampoteza maana sifa inanguvu sana katika kuimarisha upendo.

18. Upole
Upendo unahitaji upole ,upendo hauwezi kudumu katika ukali, upendo unajengwa na upole maana upole hujenga lakini hasira hubomo,uwe mpole unapozungumza na mwenzi wako upole hugeuza hasira kuwa furaha.

Hivyo ili ufanikiwe katika kutunza mahusiano yenu unatakiwa uwe mpole hata kama umesikia kitu kibaya kwa mwenzi wako unatakiwa uwe mpole ili uweze kufanikiwa kujua unachotaka kujua ,Upole ni mlezi wa upendo.

19. Kutetea (Defending)
Upendo unahitaji utetezi, Unajua unavyoamua kumpenda mtu unatakiwa umtetee unapoona ananenewa mabaya, usichangie kunena mabaya juu ya mpenzi wako usimchafue mpenzi wako, hatua uliyofanya kumpenda tayari umefanyika mtetezi wa mpenzi wako, usikubali dada, mama, baba, mjomba,na marafiki zako wanamnena mabaya mpenzi wako mtotoe kwa bidii ficha aibu ya mwenzi wako .

Ukitaka Upendo usiharibike na uimarike unatakiwa uwe mtetezi mzuri kwa mwenzi wako. Hivyo upendo unahitaji mtetezi.

20. Kutoshelezwa (satisfication)
Upendo unahitaji kutosheleza, upendo hauhitaji kulipuliwa, unahitaji utoshelezwe, unatakiwa kumtosheleza mwenzi wako sawa sawa, usiwe kama kuku upendo hauhitaji kilipuliwa unahitaji kutoshelezwa.

21. Furahi (Enjoyment)
Upendo unahitaji furaha ,unatakiwa umfurahishe mpenzi wako kwa kila kitu ,mfanye afurahi na kufurahia upendo wako unaompa.

22. Hisia (Fellings)
Upendo unahitaji hisia, unatakiwa kuonyesha hisia kali za mapenzi kwa mwenzi wako ,unajua kuwa upendo ni hisia kali?

Muonyeshe mpenzi wako hisia kali za mapenzi ulizonazo kwake –maana upendo ili ukuwe unahitaji mtu mwenye hisia za mapenzi.

23. Adabu (Discipline)
Upendo unahitaji adabu, Upendo unamtafuta mtu mwenye adabu, mtiifu, mnyenyekevu upendo unakaa kwa mtu mwenye adabu ukiwa na adabu hutatoka nje ya ndoa yako, hutaweza kumsaliti mumeo wako au mwenzi wako lakini kama humpi anachostahili akitoka kutafuta faraja nje basi jilaumu wewe maana nae anataka furaha.

24. Kujali (Caring)
Upendo unahitaji kujali, unatakiwa kuonyesha kuwa unajari kwa mpenzi wako,unamjari,muonyeshe kuwa unamjari,Unamheshimu,unamdhamini hauko tayari kumpoteza mteende mema mwenzi wako,ukijali utatunza upendo wako usipotee-mpendezeshe mwenzi wako,mfanye aingie mtaani,n.k. akilinga cheka pamoja naye, lia pamoja naye.

25. Kupenda (Love)
Upendo unahitaji kupendwa unajua unatakiwa kupenda unapopendwa maana upendo unaishi mahali unapopendwa unatakiwa kuonyesha ni jinsi gani unavyompenda.

Upendo wa kweli hauna hofu muonyeshe mapendo mwenzi wako bila hofu na watu watajua jinsi uanvyompenda usiwape maadui nafasi ya kuonyesha upendo wao kwa mwenzi wako.
Mpende mpenzi wako kutoka ndani ya moyo wako maana upendo unahitaji kupendwa.

26. Msamaha (Appologizing/argrivment)
Upendo unahitaji msamaha, msamaha ndio upendo wenyewe rafiki ningependa kukwambia
kuwa unapojua umemkosea mpenzi wako ninakusihi uwe mwepesi kuomba msamaha, hakuna mwanadamu aliyekamilika wote huwa tunakosea ila neno msamaha liwe karibu naomba unisamehe na wewe unayeombwa msamaha unatakiwa uwe na moyo wa kusamehe na ukisamehe hutakiwa kukumbuka tena kama tutakuwa watu wa kuomba msamaha na kutorudi tena waliyofanya na kusamehe na kutokumbuka tena ,msamehe mwenzi wako toka moyoni.

27. Kukumbatia (Hagging)
Upendo unahitaji kukumbatiwa, unajua hapa ni eneo muhimu sana kwa wapendanao,kuna utofauti wa kumkumbatia rafiki,mzazi na mpenzi wako- unapomkumbatia mpenzi wako lazima watu waone utofauti mkubwa na jinsi unavyomkumbatia mpenzi wako unatakiwa umkumbatie vizuri sana hadi utakaposikia mapigo yake ya moyo. Unatakiwa umsogeze karibu sana na wakati yupo kifuani mwako unatakiwa uwe na maneno matamu ukimnong'oneza masikioni mwake yanayowakalisha upendo wako kwake hadi anayekumbatiwa ajue kuwa amependwa na mtu Fulani wala hatakiwi kuona aibu ni mali yako-Hivyo upendo unahitaji kukumbatiwa kama Ishara ya kukubaliwa.

28. Ushauri (advising)
Upendo unahitaji kushauriwa ,mashauri hujenga taifa mashauri hujenga mahusiano.
Unatakiwa uwe mtu mwenye ushauri mzuri kwa mwenzi wako, mshauri unapomuona anaenda kinyume na wewe, mshauri anapokosea, kubali kushauriana na mwenzako, muweke chini na kumshauriana na jinsi mtakavyoweza kuendesha familia yenu.

Mshauriane kabla ya kufanya kitu usiwe mwenye amri kwa mwenzi wako hapana upendo wa kweli umejaa mashauri ili uwe mtu mwenye mafanikio unatakiwa uwe na mshauri mzuri – mshauri wa kwanza kabla ya yote ni mwenzi wako – maana upendo unahitaji ushauri ukiwa mtu usiyetaka kushauriwa hutaweza kufika mbali.

Nlyumba nzuri na yenye mafanikio imejaa ushauri mzuri na wenye matokeo chanya.

29. Majadiliano (Discussion)
Upendo unahitaji majadiliano ya amani, unajua kuwa majadiliano ya amani ni mazuri sana maana wewe unaweza kuwaza kuuza nyumba kwa sababu ya hasira lakini majadiliano yatakukumbusha wapi umetoka, wapi ulipo na wapi unakwenda ……?

Majadiliano kwa wapendanao ni kitu muhimu sana maana yanaimarisha upendo wenu na yana nguvu ya kuwapeleka katika kiwango kikubwa cha mahusiano yenu, usiwe mtu wa kujiamulia mambo katika familia.

Acha ubinafsi badilika wewe mwenyewe huwezi kuipeleka familia katika mafanikio kama una wadharau wa nyumbani mwako.

Hivyo upendo ili udumu unahitaji majadiliano.

30. Uwazi (Openly)
Upendo unahitaji uwazi ,unatakiwa uwe muwazi kwa mwenzi wako mwambie kweli nini unataka na nini hutaki, nini ulifanya na kama ulikosea mwambie.

Jaribu kuwa muwazi kwa mwenzi wako, kwa nini unamficha mambo yako, mapenzi ya kweli hayana maficho, kama unapesa Benki mwambie unamficha kwanini, kama ulizaa nje ya ndoa mwambie usimfiche….. Utasababisha matatizo makubwa sana wakati mwenzi wako atakapo tambua kuwa ulimdanganya.

31. Kubembelezwa (Pamper)
Upendo unahitaji kubembelezwa, unatakiwa kumbembeleza Mwenzi wako.

Acha mpenzi wako adeke kwako, na unatakiwa umdekeze mwenzi wako kwa kumpakata, mbemebeleze, muimbie nyimbo nzuri za mapenzi, cheza naye, mbebe mwenzi wako, cheka na mpenzi wako, muache ajiachie kwako, huyo ndiye mwanao wazazi wake wamekukabidhi; umlee na kumtunza, mfute machozi, muogshe, mpake mafuta.

Mabembelezo yanafaa sana kwa mtu na mpenzi wake, deka kwake naye adeke kwako na hapo ndipo upendo utakapodumu katika maisha yenu.
Maana upendo unahitaji kubembelezwa.

32. Kuvuta ukaribu na umakini (Splash)
Upendo unahitaji ukaribu na umakini sana, unatakiwa utengeneze ukaribu na umakini na mwenzi wako asiwe mbali nawe. Jaribu kumsogeza karibu nawe kwa kumuonyesha kuwa upo makini sana na yeye, utaona jinsi upendo utakavyozidi kuongezeka katika maisha yenu.

Upendo wa kweli unahitaji uvute ukaribu na umakini kumsikiliza mwenzi wako, kumtia moyo, kumuelewa anachosema na kutenda hapo upendo hautakimbia katika maisha yenu.

Thursday, January 9, 2020

Gharama za Mafuta Zapanda Baada ya Shambulio la Iran


Gharama za mafuta zimepanda baada ya kambi mbili za majeshi ya Marekani nchini Iraq kushambuliwa na makombora.

Tokeo la picha la oil increase cost after iran attack

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Gharama za mafuta ghafi zimepanda kwa 1.4% kwa dola 69.21 za Marekani kwa pipa moja. Wakati huo huo gharama za mafuta kwenye soko la dunia zilishuka kutokana na mzozo wa Mashariki ya kati.

Televisheni ya Taifa ya Iran ilisema kuwa shambulio lilikuwa ni kisasi baada ya kuuawa kwa kamanda wa juu wa jeshi la nchi hiyo Qasem Soleimani.

Shambulio lilitokea saa chache baada ya shughuli za mazishi ya Soleimani, aliyeuawa na shambulio la Marekani siku ya Ijumaa.

Kifo chake kilisababisha wasiwasi kuwa mzozo kati ya Marekani na Iran unaweza kuwa mkubwa zaidi.

Hali hii inaelezwa kuwa inaweza kuathiri usafirishaji wa mafuta kupitia lango la Hormuz linalotenganisha ghuba ya uajemi na ghuba ya Oman. Takribani moja ya tano ya mafuta duniani husafirishwa kupitia lango hilo linalounganisha eneo la ghuba na bahari ya Arabia.

Mlango wa Hormuz ni muhimu kwa wasafirishaji wakubwa wa mafuta katika eneo la ghuba – Saudi Arabia, Iraq, Umoja wa falme za kiarabu na Kuwait- ambao uchumi wao unajengwa kutokana na uzalishaji wa mafuta na gesi.

Iran pia inategemea kwa kiasi kikubwa njia hiyo kwa ajili ya kusafirisha mafuta. Qatar, mzalishaji mkubwa duniani wa gesi, husafirisha karibu gesi yake yote kupitia lango hilo.

Baada ya mashambulio, mamlaka ya anga ya Marekani imezuia ndege za Marekani kuruka kwenye anga ya Iraq, Iran na nchi jirani. Marufuku hiyo pia inahusisha ghuba ya Oman na maji ya kati ya Iran na Saudi Arabia.

Mamlaka hiyo imesema uamuzi umechukuliwa baada ya kuwepo kwa mvutano wa kisiasa na shughuli za kijeshi katika eneo hilo.

Kabla ya muongozo wa hivi karibuni, mamlaka hiyo ilishazuia ndege za Marekani kupaa umbali wa chini ya futi 26,000 katika anga la Iraq na kutopita kwenye eneo la anga ya Iran eneo la ghuba ya Oman tangu Iran ilipoidungua ndege isiyo na rubani ya Marekani mwezi Juni mwaka 2019.

Wakati huo huo shirika la ndege la Singapore limesema ndege zake zote hazitapita kwenye anga ya Iran.


Wednesday, January 8, 2020

Maelfu ya Ngamia kuuawa kwa kupigwa risasi kutoka angani


Maelfu ya Ngamia kusini mwa Australia watauawa kwa risasi kutoka kwenye helikopta kutokana na kuwepo kwa joto kali na ukame.


Zoezi hilo la siku tano limeanza Jumatano, jamii ya eneo hilo imeripoti kuwepo kwa makundi makubwa ya ngamia kuharibu miji na majengo.

"Wanaambaa mitaani wakitafuta maji ya kunywa. Tunahofukuhusu usalama wa watoto", anasema Marita Baker, ambao wanaishi kwenye jamii ya Kanypi.

Baadhi ya wanyama pori pia watauawa.Ngamia

Kwa mujibu wa BBC, Maafisa watakaofanya kazi hiyo wanatoka katika idara ya mazingira na idara ya maji.

Imeelezwa kuwa kutokana na hali ya ukame ngamia wamekuwa tishio kwenye jamii hivyo unahitajika udhibiti wa haraka.

Jamii zinazoishi karibu na makazi ya ngamia hao wamesema wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu, kwa sababu ngamia hubomoa uzio, huzunguka nyumba wakijaribu kupata maji kupitia maji yanayodondoka kutoka kwenye viyoyozi.

Joto kali na ukame kumesababisha moto wa nyika nchini Australia kwa kipindi cha miezi kadhaa, lakini hali ya ukame ya nchi hiyo imekuwepo kwa miaka kadhaa.

Ngamia hawana asili ya Australia- walipelekwa nchini humo na walowezi kutoka India, Afghanistan na mashariki ya kati katika karne ya 19.

Ngamia hao huharibu uzio, huharibu vifaa vya shamba na makazi, na pia hunywa maji yanayohitajika kwa matumizi ya watu katika eneo hilo.

Pia hutoa gesi ya methane, gesi ambayo inachangia mabadiliko ya hali ya hewa.Maafisa wa zima motoKaribu makazi 2,000 yameharibiwa kutokana na moto uliodumu kwa miezi kadhaa.

Karibu watu 25 wameuawa tangu mwezi Septemba.

Maeneo ya mashariki na kusini mwa Australia yameharibiwa vibaya- na wanyama wengi wameuawa kwa moto.

Nchi hiyo imekuwa ikikumbwa na joto kali katika kipindi cha miongo ya hivi karibuni na hali inatarajiwa kuendelea.

Wanasayansi wametahadharisha kuwa hali ya joto kali, na ukame utachangia matukio ya moto mara kwa mara na wenye madhara .Binti wa afisa wa zima moto akiwa karibu na jeneza la baba yake


Tuesday, January 7, 2020

Mfanyabiashara Kutoka India Yuko Nchini Kuangalia Fursa Za Uwekezaji

Mfanyabiashara kutoka nchini India, Bw.Vivek Agarwala yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku saba kuanzia tarehe 6 hadi 12 Januari 2020. Bw. Agwarala ambaye amekuja kuangalia fursa za uwekezaji nchini, atafanya mazungumzo na Uongozi wa Benki ya CRDB, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) pamoja na kutembelea maeneo kadhaa kwa lengo la kupata maelezo kuhusu taratibu na fursa za uwekezaji zinazopatikana nchini.

Maeneo yatakayotembelewa na mfanyabiashara huyo ni Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji (EPZA) Dar es Salaam, Mkoa wa Simiyu ambapo ataangalia uwezekano wa kupata eneo la ekari elfu mbili (2,000) kwa ajili ya kuanzisha kilimo cha mpunga na ujenzi wa kiwanda zao hilo. Bw. Agarwala atatembelea maghala ya pamba ili kujiridhisha kabla ya kununua kiasi cha robota laki moja (100,000) ambayo aliahidi kununua wakati alipofanya mazungumzo na Uongozi wa Benki ya CRDB mwezi Desemba 2019.

Bw. Agarwala pia atatembelea machimbo ya Tanzanite, mkoani Manyara, Kiwanda cha Karatasi cha Mufindi kilichopo mkoani Iringa na kuangalia uzalishaji maparachichi ili kujenga kiwanda cha kusindika zao hilo kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi.

Ujio wa mfanyabiashara huyo ni matokeo ya juhudi za Ubalozi wa Tanzania nchini India ambao uliratibu ziara ya kikazi iliyofanywa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji-Uendeshaji na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts iliyofanyika nchini India mwezi Desemba mwaka jana. Ziara hiyo ililenga kutafuta wawekezaji kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo soko la pamba nchini humo.

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali.



Source

BASATA YAMFUTIA USAJILI MSANII DUDUBAYA ...SASA MARUFUKU KUJIHUSISHA NA SANAA


Msanii wa muziki wa Bongo Flava nchini, Dudubaya amefutiwa usajili na baraza la sanaa la Taifa (BASATA) ambapo  baraza hilo pia limetoa onyo kwa taasisi, kampuni na mtu yeyote kutofanya kazi na msanii huyo. Hatua hiyo imekuja baada ya msanii huyo kukataa wito wa baraza hilo.





Dudubaya ambaye jina lake halisi ni Godfrey Tumaini alitakiwa kufika ofisi za Basata leo Januari 7, 2020 saa 4:00 asubuhi baada ya kusambaa kwa video zake kwenye mitandao ya kijamii akizungumzia mambo mbalimbali, ambapo Basata imeeleza ametumia kauli zisizokuwa na maadili wala staha.


Hata hivyo, Dudubaya aliukataa wito huo kwa kulijibu baraza hilo kuhangaikia kwanza na migogoro iliyopo kati ya baadhi ya vyombo vya habari na wasanii ili kuufanya muziki usonge mbele huku maneno aliyoyatumia katika video zake akieleza kuwa ni ya kawaida.

Kutokana na kutoitikia wito huo, Katibu Mtendaji, wa baraza hilo, Godfrey Mngereza katika tamko lake hilo amesema baraza limechukua hatua ya kumfutia usajili wake kuanzia leo Januari 7,2020.



Meddie Kagere Afunguka Kuhusu HIRIZI Aliyovuliwa Uwanjani 'Ni Cheni Yangu ya Dhahabu Siyo Hirizi Jamani"




HUKO mitani na hata kwenye mitandao ya kijamii, mashabiki wa Yanga wamemzulia kitu straika wa Simba, Meddie Kagere baada ya sakata lake na beki Kelvin Yondani, lakini mwenyewe amewasikia na kuwaambia "acheni hizo, ile ni cheni yangu ya dhahabu tu".

Katika pambano la juzi lililoisha kwa sare ya 2-2, Ally Mtoni 'Sonso' aliyekuwa anakabana na Kagere aliiona cheni shingoni mwa straika huyo na kumtonya Yondani ambaye aliikata kijanja kabla ya kukimbilia kwa mwamuzi Jonesia Rukyaa kulalamikia kuvaa kwake cheni hiyo.

Hata hivyo, kulitokea purukushani kidogo na mashabiki kuzua eti ili 'busta', lakini Kagere amesema hana mambo hayo ya kipuuzi na kwamba ile ni cheni ya dhahabu na alipitiwa tu kuivua kabla ya kuingia uwanjani, lakini imechukuliwa sivyo ndivyo.

Alisema alikuwa amevaa cheni hiyo kabla ya mchezo kuanza na hata alipokwenda kupasha misuli alikuwa nayo na alijisahau kuivua walipoenda vyumba vya kubadilishia nguo, alisahau kuvua na akaingia nayo uwanjani.

"Nilijikuta nimeingia nayo uwanjani na kuanza kucheza, lakini wakati Yondani ananikaba aliivuta na kuikata, huku akienda kumueleza mwamuzi nacheza nikiwa na cheni jambo ambalo aliichukua na kuipeleka katika benchi letu," alisema na kuongeza:

"Huwa naivaa muda mwingi kwani hata nikiwa nimelala nakuwa nayo, ndio maana nilijisahau kuivua na nilijikuta nipo nayo uwanjani na muda ambao nilijua kuwa ninayo ni ule Yondani alivyoikata, lakini hakuna kingine cha ziada na mlipoona natafuta kitu ni kidani cha herufi K."

Naye beki wa kulia wa Simba, Shomary Kapombe aliyeshuhudia sakata hilo alisema hakuona kitu chochote tofauti na cheni ya Kagere ambayo Yondani akiwa katika harakati zake za kumkaba aliivuta na kuikata.

"Ni cheni yake ya dhahabu iliyokatwa na Yondani na pale tulipokuwa tunashangaa ilikuwa tunatafuta kidani chenye herufi ya jina lake, lakini tulishindwa kukipata kwa vile mechi ilikuwa ikiendelea," alisema Kapombe.

Source

VIDEO: Mapya kesi ya Tito Magoti na mwenzake, taarifa ya upelelezi yaelezwa mahakamani


Upande wa utetezi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili ofisa wa Programu kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) nchini Tanzania, Tito Magoti (26) na mtaalamu wa Tehama, Theodory Giyama (36) wameuomba upande wa mashtaka kuhakikisha wanakamilisha upelelezi wa kesi kwa wakati ili haki iweze kutendeka

Magoti na Giyani wanakabiliwa na makosa matatu likiwamo la utakatishaji fedha kiasi cha Sh 17 milioni, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam hata hivyo hawana dhamana kutokana na shtaka la utakatishaji fedha linalowakabili kutokuwa na dhamana kwa mujibu wa sheria.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE

Saturday, January 4, 2020

VIDEO: Mkwasa ailipua Simba, tuligundua madhaifu yao ''tumecheza na timu inayoongoza kupewa penati''


Kocha Mkuu wa Yanga SC, Charles Boniface Mkwasa amefunguka kuhusiana na mchezo wao dhidi Simba ambapo uliomalizika jioni hii ambapo amesema wametumia madhaifu ya wapinzani wao na ndio maana kipindi cha pili wamefanya vizuri

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI........USISAHAU KUSUBSCRIBE


Source

Mwanahabari wa DW Adaiwa Kulishwa Sumu



Deokaji Makomba ambaye ni Mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili ya DW amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma baada ya kufikishwa Hospitalini hapo akiwa hajitambui.

Alikutwa akiwa amepoteza fahamu ndani ya basi la Ally's. Imeelezwa kuwa alikuwa umelala usingizi mzito na ikabainika kuwa ameibiwa mizigo yake.

Mwandishi huyo alitoka Jijini Mwanza kwa basi hilo na ameeleza kuwa alipewa vipande vya Biskuti na abiria aliyepandia njiani na ndipo akapoteza fahamu.

Mwanahabari huyo licha ya kueleza kuwa anaendelea vizuri lakini amekiri kuwa hana nguvu na bado anahitaji kulala zaidi ili kupumzisha mwili wake.

Mwanaume unapaswa kukumbuka hili katika mahusiano yako

Mwanaume acha ubahiri kwa sababu ni maagizo ya Mungu mwenyewe. In fact ni furaha ya mwanamke yeyote yule kuwa na mwanaume anaeweza kumhudumia mahitaji yake licha ya mwanamke nae kujikwamua kiuchumi kama ziada na nyongeza tu lakini sio wajibu wake.

Mwanaume Mungu anapokubariki na kipato sio vibaya ukamfanyia vitu vizuri mwanamke wako anataka manicure au pedicure.

Mpe fedha akaweke mwili katika mwonekano bomba! Mfanyie hata suprise ya shopping mara moja moja. Tuache ubahili, tusihonge pembeni tutafilisika, vichenchede vya nje huwa vinakamua mpaka unabaki na sharubu tu! tujifunze kuwahonga wake zetu!

Anataka vacation, peleka Ngorongoro huko huyo baby wako akashangae tembo. Anataka kula vitu vizuri, give her the treat. Kazi yako kama mwanaume ni kuhakikisha mwanamke wako anaridhika na anafurahia uwepo wako.

Kila mwanamke ni mzuri, inategemeana na wewe utakavyompa kipaumbele!

Mwanamke nae asibweteke, Mumewe anaporudi nyumbani huku akiwa na furaha ya kufanikisha dili kadhaa au huzuni ya kufeli kwa dili zake ampe mumewe maneno matamu ya kutia moyo pamoja na vitu adimu kitandani afurahie uwepo wako.

Thursday, January 2, 2020

Upande wa Jamhuri wakataa Kabendera kumzika Mama yake...Mahakama Kuamua

Upande wa Serikali umempa pole Mwandishi wa Habari, Erick Kabendera kwa kufiwa na Mama yake mzazi, Verdiana Mujwahuzi huku ukipinga maombi yake ya kutaka ashiriki Ibada ya mazishi ya mama yake.

Hayo yamebainika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati Kabendera anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha alipofikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kesi yake.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amemueleza Hakimu Mkazi, Janeth Mtega kwamba Jamhuri inampa pole Kabendera kwa kufiwa na Mama yake mzazi.

"Hata sisi tuna masikitiko makubwa na tunampa pole nyingi Kabendera kwa kufiwa na Mama yake mzazi, lakini mahakama isifungwe mikono kwa maombi yaliyowasilishwa ya kutaka kushiriki msiba,"amesema Wankyo.

Wankyo amedai kuwa maombi ya Kabendera kupitia mawakili wake yamewasilishwa wakati ambao si sahihi kwa sababu mahakama haina mamlaka na pia Mkurugenzi wa Mashitaka hajaipa kibali ya kusikiliza kesi hiyo.

"Katika macho ya kisheria mahakama yako haina mamlaka, hata sisi tuna masikitiko makubwa lakini mahakama isifungwe mikono," amesema.

Kuhusu mwenendo wa kesi, upelelezi unaendelea na shauri limefika hatua nzuri ya maelewano baina ya mshitakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka (DPP).

Kukataliwa kwa Kabendera kushiriki mazishi ya Mama yake, kumeibuka kutokana na maombi aliyoyatoa Kabendera kupitia Mawakili wake akiwemo Jebra Kambole.

Wakili Kambole amedai wanaiomba mahakama hiyo imruhusu Kabendera akashiriki Ibada ya Mazishi ya Mama yake mzazi katika Kanisa la Roman Katoliki lilipo Changombe majira ya mchana.

Kambole ameieleza mahakama kuwa suala la kushiriki sala ya mwisho ya msiba ni haki ya Binadamu, suala la faragha.

"Kushindwa kuudhuria maziko ya Mama yake tutakuwa tumemuadhibu adhabu kubwa tena kwa kuangalia uhusiano wa mshitakiwa na mama yake mzazi kwani alikuwa akimuuguza na ni vizuri akatoa heshima ya mwisho,"ameeleza.

Wakili Jebra amedai kuwa ni muhimu kwa Kabendera kushiriki kwa sababu Mama mzazi ni mmoja, akifa anaagwa mara moja.

"Jamhuri haitaathirika kwa lolote kwa sababu mshitakiwa atakuwa chini ya ulinzi na ibada itakuwa mchana kanisani na Temeke sio mbali na gerezani, tunaomba akatoe heshima ya mwisho," ameomba.

Baada ya kutoa hoja hizo, Hakimu Mtega ameahirisha kesi hiyo hadi saa 8:45 mchana kwa ajili ya kutoa uamuzi kama Kabendera ashiriki Ibada ya mazishi ya Mama yake mzazi ama lah.


Wednesday, January 1, 2020

Mahakama ya Angola imeagiza mali za mtoto wa rais zikamatwe



MAHAKAMA ya Angola imeagiza kukamatwa kwa mali na akaunti za benki za bilionea ambaye ni binti wa rais wa zamani wa Angola, Jose Eduardo Dos Santos, Bi Isabel Dos Santos.

Kukamatwa kwa mali hizo kunatokana na mipango ya serikali iliyopo kukabiliana na ufisadi katika taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta.

Utawala wa Rais Joao Lourenco unataka kuchukua takriban dola bilioni moja ambazo umekuwa ukimdai Bi Isabel Dos Santos na washirika wake.

Amepinga madai hayo na kusema kwamba hajafanya makosa yoyote wakati babake alipokuwa mamlakani.

Akidaiwa kuwa mwanamke tajiri zaidi barani Afrika, Bi Dos Santos anakadiriwa na jarida la Forbes kuwa na mali yenye thamani ya dola bilioni 2.2.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 46 anaishi ughaibuni, akisema kwamba aliondoka Angola kwa kuwa maisha yake yalitishiwa.

Anaendesha biashara kubwa akiwa na kampuni nchini Angola na Portugal ambapo anamiliki hisa katika kampuni ya Nos SGPS.

Mahakama iliagiza mali ya Bi Santos kupigwa kuchukuliwa ikiwemo akaunti zake za benki mbali na hisa zake katika kampuni nchini Angola, ikiwemo ile ya Unitel na Benki ya Fomento de Angola (BFA) kilisema chombo kimoja cha habari cha serikali ambapo naye alisema anashutumu kile alichokitaja kuwa shambulio linaloshinikizwa kisiasa.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...