Monday, November 30, 2020

Diamond Avunja Rekodi ya Kufikisha 1 Milioni Viewers Ndani ya Masaa Manane


Video Ya Wimbo Wa 'WAAH!' Ya Msanii @diamondplatnumz Aliyomshikirisha Legend Wa Muziki Barani Africa @koffiolomide_officiel Imeweka Rekodi Mpya Afrika Baada Ya Kufikisha Watazamaji Million 1 Kwenye Mtandao Wa YouTube Ndani Ya Masaa 8, Inaingia Kwenye Rekodi Kufikisha Watazamaji Hao Huku Ikivunja Rekodi Ya DAVIDO Aliyekuwa Akishikiria Katika Wimbo Wake Wa FEM Ambayo Ilifikisha 1 M Kwa Ndani Ya Masaa 9.

Kupitia Ukurasa Wa Instagram Wa DIAMOND Ameandika... ''Thank you so much my beloved fans for the Record of 1 Million Youtube Viewers within 8 hours...it means alot to me🙏🏼....#WAAH! full Video link in BIO! (Asanteni sana kwa Rekodi hii ya Viewers Milioni 1 Youtube ndani ya Masaa Manane, Daima nitaendelea Kuwashukuru🙏🏼) ''


Serikali Kuinua Sekta ya Sanaa-Dkt. Abbasi





KATIBU Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ambaye pia ni msemaji mkuu  wa Serikali Dkt.Hassan Abassi leo Novemba 30, 2020, jijini Dar es Salaam, ameanza ziara ya kukutana na wadau wa sanaa kwa kukutana na Wakuu wa Taasisi za Wizara hiyo zinazoratibu masuala ya sanaa nchini.

Dkt. Abbasi ameelekeza taasisi hizo kuwa kiungo kati ya wadau wa sanaa na Serikali na amezitaka ziwe karibu na wadau hao, ziwahudumie kwa karibu na zaidi zibuni mambo mapya ya kuishauri Serikali katika kutekeleza azma ya kuiinua sekta ya sanaa nchini.

"Serikali imeahidi kuinua sekta ya sanaa na dhamira kubwa ipo; ni juu yenu kushirikisha wadau ili kupata mrejesho sekta inataka kufanyiwa nini na Serikali ili ikue; zama za wanatasnia na taasisi za sanaa kuwa mbali na kila mmoja anakwenda na lake zimekwisha," alisema Dkt. Abbasi.


Serikali yasema walioajiriwa ualimu sio 13,000, yaonya waliodanganya masomo


Makatibu wakuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ofisi ya Rais Tamisemi na Ofisi ya Rais Utumishi wametoa ufafanuzi kuhusu ajira za walimu nchini.


 Hata hivyo, Katibu Mkuu Utumishi Dk Laurence Ndumbaro amesema ajira zilizotolewa ni 13,000 lakini waliopata vibali ni walimu 8000.


Dk Ndumbaro amesema pengo la walimu 5000 litazibwa wakati wowote kabla ya mwaka wa fedha 2020/21 haujaisha hivyo Watanzania hawapaswi kuwa na hofu kwa kuwa muda wa kuajiri bado upo.


"Ni kweli tulipokea maelekezo kutoka kwa Rais kuwa tuajiri walimu 13,000, lakini mfumo hauruhusu kupata ajira nyingi kwa wakati mmoja,hivyo tunakwenda kwa awamu mbili," amesema Dk Ndumbaro.


Hata hivyo,  Katibu huyo amekiri kulikuwa na makosa kwa baadhi ya maeneo ikiwemo katika mfumo hata kupelekea baadhi ya majina kujirudia mara nyingi kwenye orodha na tatizo hilo limefanyiwa kazi.


Katika hatua nyingine, Katibu ameonya walimu waliodanganya kwamba wanakwenda kufundisha masomo fulani na kupata ajira wakati wamesomea masomo mengine, watahakikiwa na watakaobainika kufanya vitendo hivyo watafukuzwa kazi mara moja na kuchukuliwa hatua zaidi ikiwemo kuzuiwa wasiingie tena katika mfumo wa ajira.

Madaktari waliotoa figo na maini ya marehemu wahukumiwa

Watu sita wakiwemo Madaktari wamefungwa gerezani nchini China kwa kutoa viungo vya mwili kinyume cha sheria kwa watu waliofariki kutokana na ajali, vyombo vya habari vya nchini humo vimeripoti juu ya hukumu hiyo.


Kundi hilo lilikuwa limelaghai familia za waliofariki kuwa wanachangia rasmi viungo vya mwili katika mashirika husika.


Kati ya mwaka 2017 na 2018 walitoa maini na figo kutoka kwa watu 11 katika hospitali ya Anhui.


Watuhumiwa hao sita wakiwemo Madaktari wanaohusika na ulanguzi huo wa viungo vya binadamu walisomewa mashtaka yao Julai mwaka huu kwa kosa la "kuharibu miili ya wafu kimaksudi" na kuhukumiwa kifungo cha kati ya miezi 10 na 28 gerezani.


China inakabiliana na upungufu wa viungo vya mwili na imekuwa na wakati mgumu kukidhi mahitaji ya raia.

Waziri Mkuu Amaliza Mgogoro Wa Ardhi Kilosa


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemaliza mgogoro wa ardhi katika shamba la Chanzuru lenye ukubwa wa ekari 1,598 lililopo wilayani Kilosa, Morogoro kati ya Laizer Maumbi na Ameir Nahad kwa kuagiza likabidhiwe kwa Laizer ili aweze kuliendeleza kwa kulima mkonge.

Hata hivyo, Waziri Mkuu ameagiza eneo wanaloishi wananchi ndani ya shamba hilo kikiwemo kitongoji cha viwanja 60 na Chekeleni lihakikiwe na kupimwa ukubwa wake na kisha mkulima huyo akafidiwe eneo jingine na wananchi hao wasibugudhiwe.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Novemba 30, 2020) katika kikao chake na Makatibu Wakuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Ardhi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Viongozi wa mkoa wa Morogoro, wilaya ya Kilosa pamoja na Laizer. Kikao hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma.

"Viongozi wa Serikali simamieni na mratibu vizuri ili wananchi wanaoishi katika vitongoji vilivyomo ndani ya shamba hilo wasibugudhiwe waachwe waendelee kuishi na eneo lililobaki lisilokuwa na mgogoro apewe Laizer. Sehemu hiyo iliyopungua Laizer atafutiwe shamba jingine ili kufidia."

Amesema awali shamba hilo lilikuwa linamilikiwa na Sadruddin Rajabali ambaye alimuuzia Laizer ambaye aliamua kuachana na shughuli za ufugaji na kuanza kulima mkonge, na alipokuwa katika harakati za kubadilisha umiliki shamba hilo liliuzwa kwa mtu mwingine.

Waziri Mkuu amewataka watumishi wa sekta ya ardhi wilayani Kilosa wahakikishe suala hilo wanalisimamia vizuri ili haki itendeke kwa mkulima huyo kukabidhiwa shamba lake na watumishi waliohusika katika mgogoro huo wachukuliwe hatua.

Pia, Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa mkoa wa Morogoro uhakikishe inabainisha maeneo makubwa yote ambayo hayajaendelezwa na kutoa mapendekezo Serikalini.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Loatha Sanare ametumia fursa hiyo kumshukuru Waziri Mkuu kwa kumaliza mgogoro huo na kuahidi kwamba atasimamia utekelezaji wa maagizo na maelekezo yaliyotolewa.

Naye, Laizer ameishukuru Serikali kwa hatua iliyofikiwa ya yeye kukabidhiwa shamba hilo ambalo ndilo tegemeo lake kwa sasa, kwani aliuza mifugo yake yote na kununua shamba hilo ambalo amepanda mkonge
.

KMC FC yajipanga katika mchezo dhidi ya Dodoma Jiji Disemba Nne

Timu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC inaendelea kujifua kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Timu ya Dodoma Jiji utakaopigwa Disemba Nne mwaka huu katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo, KMC FC ambao ni wenyeji, wanafanya maandalizi  katika uwanja wa White Sand Hotel ikiwa ni katika kuhakikisha kwamba mipango na mikakati ya kupata ushindi huo unafanikiwa kwa asilimia kubwa ilikuendelea kujiweka katika nafasi nzuri ya msimamo wa ligi Kuu Soka Tanzania Bara  msimu wa 2020/2021.

Kikosi cha KMC FC ambacho kinanolewa na makocha wawili wa zawa ambao ni John Simkoko pamoja na Habibu Kondo, kimejipanga kuhakikisha kwamba kinaendeleza ushindi ikiwa ni baada ya kumfunga Azamu goli moja kwa bila na hivyo kupata alama tatu katika uwanja wa Uhuru Novemba 22 mwaka huu.

" Kikosi chetu kipo imara, hatuna majeruhi, tunaimani kwamba maandalizi ambayo yanaendelea kufanyika yataleta matokeo mazuri katika mchezo huo,na mingine ambayo tutacheza pia, hatujiandai kwa ajili ya mechi moja,ila ni kwa kila mechi ambazo zipo mbele yetu".

 Hatujacheza michezo miwili dhidi ya Namungo pamoja na Simba, kwa hiyo tumekuwa na wakati mzuri zaii  wakufanya maandalizi yetu, hivyo mashabiki wategemeekuona Pira Spana tukiliendeleza kwa wapinzani wetu.

Hata hivyo KMC FC mbali na kucheza na Dodoma Jiji, pia itakutana na Mtibwa Suger mchezo ambao utapigwa mkoani Morogoro,  Ihefu Mbeya pamoja na JKT Tanzania katika uwanja Samora Iringa.

Mbali na michezo hiyo, KMC FC bado itakuwa na viporo vya michezo miwili ambayo ni dhidi ya Namungo pamoja na Simba timu hizo kwa sasa zinashiriki michuano ya kimataifa.

Mike Tyson Amevuta Mkwanja Huu Kwenye Pambano Lake na Roy Jones Jr


Jumamosi ya Novemba 28 mwaka huu, mkongwe wa masumbwi na bingwa wa zamani wa uzito wa juu Mike Tyson alirejea ulingoni mara baada ya kustaafu mchezo huo miaka 15 iliyopita.


Tyson (54) alirejea ulingoni kuzichapa kwenye pambano la maonesho akizichapa na Roy Jones Jr (51) pambano ambalo lilimalizika kwa sare. Kubwa kwenye pambano hilo lililoteka hisia za watu wengi hasa baada ya kumuona Tyson ulingoni, ni mkwanja ambao ameingiza kwa dakika hizo alizopigana katika round 8.


Imeelezwa kuwa Mike Tyson pamoja na Roy Jones Jr, waliingiza kiasi cha ($1million) sawa na TSH. Bilioni 2.3 kwenye pambano hilo ambalo Tyson ameliita la hisani na si kwa ajili ya kutengeneza pesa.

 

Video Mpya: Diamond Platnumz Ft. Koffie Olomide – Waah


Video Mpya: Diamond Platnumz Ft. Koffie Olomide – Waah


Biden kupewa taarifa ya kwanza ya ujasusi


Rais mteule wa Marekani, Joe Biden leo anatarajiwa kupokea taarifa ya kila siku ya rais kwa mara ya kwanza, wiki kadhaa baada ya utawala wa Rais Donald Trump kukataa kutoa taarifa hizo. 

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya Biden, inaeleza kuwa baada ya kupokea taarifa hiyo, rais huyo mteule atakutana na washauri wake. 

Wakati huo huo, Biden ameitangaza timu yake ya mawasiliano ambayo yote inawajumuisha wanawake. Hii itakuwa ni mara ya kwanza katika historia ya Marekani timu ya mawasiliano ya rais kuwa na wanawake watupu.

 Miongoni mwa walioteuliwa ni Jen Psaki, ambaye atakuwa katibu wa habari wa Ikulu ya Marekani. Kate Bedingfield ameteuliwa kuwa mkurugenzi wa mawasiliano wa Ikulu ya Marekani. 

Wanawake wengine walioteuliwa ni Ashley Etienne, Symone Sanders, Pili Tobar, Karine Jean Pierre na Elizabeth Alexander.

Roberto Carlos afunguka dili la kusaini Chelsea



Legendary, nyota wa Brazil, Roberto Carlos amezungumzia namna alivyokaribia kujiunga na klabu ya Chelsea kutoka nchini England mwaka 2007.



'Icon' huyo wa Brazil aliyeitumikia Real Madrid kwa mafanikio makubwa akicheza jumla ya michezo 527, makombe 13 akiwa na umri wa miaka 34 akitangaza kustaafu huku watu wengi walikuwa bado wakimuhitaji kwakuwa walikuwa wakiamini bado anacho kitu cha kufanya uwanjani.

Carlos amesema alikuwa katika nafasi ya mwisho kujiunga na Chelsea chini ya mipango ya kocha wake kwa wakati huo Jose Mourinho.

Roberto Carlos: What stopped me from Joining Chelsea | TrueNEWS Sports

Kwa wakati huo Kocha huyo raia wa Ureno alikuwa tayari na Ashley Cole, ambaye amekuwa anamhakikishia matokeo mazuri kunako uwanja na beki huyo wa kushoto Carlos akiwa bora kweli kweli duniani

Kwa sasa Carlos ana umri wa miaka 47, wakati ambao anagusia namna alivyonukia kutua Blues. Akiiambia Goal mchezaji huyo aliyekuwa katika ubora wa dunia amesema "Nilikuwa na mapendekezo kutoka klabu mbili, Fenerbahce na Chelsea. Chelsea haikufanya kazi hivyo nikasaini Fenerbahce."

"Lakini nilikaribia sana kujiunga na Chelsea. Nilibidi niende huko hivyo nikaamua kusaini. Ilikuwa ni wiki moja tu kabla ya kusaini Fenerbahce na nilikuwa Paris nilikwenda kukutana na Roman Abramovich na Peter Kenyon.


Museveni ashutumu wanasiasa wa upinzani kupotosha vijana

Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameshutumu waandamanaji na wanasiasa wa upinzani kwa kuwapotosha vijana kujiingiza katika vitendo vya uhalifu.

Bwana Museveni amesema wazo la kuwa mheshimiwa Bobi Wine akikamatwa kutakuwa na ghasia lisirejee tena.

''Hakuna mwanasiasa ambaye ana mamlaka kuliko sheria'', Museveni alisema.

Aliongeza kuwa wanasiasa wanalipa magenge ya uhalifu ambao wametangaza baadhi ya sehemu za mji wa Kampala eti hazitawaliki na hata kuvamia maafisa wa polisi wanaoshika doria.

Bwana Museveniameshutumu watu waliorekodiwa wakivamia maafisa wa usalama na waliokuwa wamevaa mavazi ya rangi ya njano inayoashiria chama tawala.

''Hili, halitawahi kutokea tena, kwasababu waliotekeleza hayo wameona matokeo ya kucheza na moto'', amesema rais Museveni.

Bwana Museveni pia alisema kuwa ajenda za wanasiasa wa upinzani ni kupata uungwaji mkono kutoka nje ya nchi ambao nia yao ni kukosesha uthabiti nchi ya Uganda.

Rais Museveni aliongeza kuwa makosa makubwa ni wagombea urais walikiuka hatua zilizowekwa za kukabiliana na virusi vya corona na kutojali utekelezaji wa sheria.

Pia, alitoa risala zake za rambirambi kwa raia wa Uganda waliopoteza wapendwa wao wakati wa ghasia hizo na kuongeza kwamba serikali itawalipa fidia.

Bobi Wine anatafuta kumuondoa madarakani Museveni ambaye ametawala nchi hiyo kwa miaka 34 - katika uchaguzi utakaofanyika Januari 2021.

Sunday, November 29, 2020

SIMBA SC YAWAZIMA WA NIGERIA KWAO, YAWACHAPA PLATEAU UNITED 1-0


SIMBA SC imetanguliza mguu mmoja mbele Raundi ya Pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Plateau United jioni ya leo Uwanja wa Kimataifa wa Jos International, Jijini Jos nchini Nigeria.

Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo Mzambia Clatous Chota Chama dakika ya 53 akimalizia kazi nzuri ya winga kutoka Msumbiji, Luis Jose Miquissone.

Sasa mabingwa wa Tanzania watakuwa na kazi nyepesi kwenye mchezo wa marudiano Jumapili ijayo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Wakifanikiwa kuitoa Plateau United, SImba SC watakutana na mshindi kati ya Costa do Sol ya Msumbiji na Platinum FC ya Zimbabwe kuwania kuingia Hatua ya 16 Bora inayochezwa kwa mtindo wa makundi.

Mechi ya kwanza jana, Platinum FC walishinda 2-1 ugenini Uwanja wa Taifa wa Zimpeto Jijini Maputo, Msumbiji na timu hizo zitarudiana Desemba 5 Uwanja wa Taifa wa Michezo wa Harare, Zimbabwe. 
Kikosi cha Plateau United kilikuwa; Adamu Abubakar, Ibrahim Babawo, Dennis Nya, Andrew Ikefe, Gabriel Wassa, Isah Ndala, Oche Ochewechi/Sunday Anthony, Sunday Adetunji, Abba Umar, Uche Onuasonya na Saheed Jibrin.
Simba SC; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein 'Tshabalala', Joash Onyango, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Hassan Dilunga, Erasto Nyoni, John Bocco, Clatous Chama nba Luis Miquissone.

CHANZO- BINZUBEIRY

Chadema wapiga shangwe baada ya diwani wao wa pekee jijini Arusha kuapa


Licha ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwa na diwani mmoja wa Kata ya Olorieni, Laurence Kombe katika Halmashauri ya Jiji la Arusha, haikuwazuia wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa chama hicho kujitokeza kwa wingi wakati na baada ya kuapishwa kumshangilia.


 Shughuli za kiapo zimefanyika leo Jumapili, Novemba 29, 2020 kwa madiwani 33 wa Kata 25 na wa Viti Maalumu wanane katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa mkoa na kuhudhuriwa na wafuasi wa vyama vya CCM, Chadema na ndugu na marafiki.


Matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020 yamekua kinyume na matokeo ya mwaka 2015 ambayo Chadema ilipata ushindi wa madiwani 24 isipokua kata moja ya Kati pekee iliyoenda CCM.


Baada ya madiwani wote kuapa na kumchagua Meya wa Jiji hilo, Maxmillian Iranqhe na Naibu wake, Veronica Mwelange, vifijo na nderemo kutoka kwa wafuasi wa vyama hivyo viwili zilifunika viunga vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa.


Jitihada za kuwatuliza wafuasi wanaodaiwa kuwa ni wa Chadema ili kumruhusu Mkurugenzi wa Jiji, Dk John Pima kuendelea na shughuli za kumkabidhi Meya gari atakalokua akilitumia kwa ajili ya shughuli za serikali, hazikufaulu na ndipo walipoamua kutoka nje ya uzio na kuondoka na diwani huyo kwenye msafara wa magari na pikipiki.


Mmoja wa wafuasi wa CCM ambaye jina lake halikupatikana mara moja alisikika akikejeli shamrashamra za hao wanaodaiwa ni wafuasi wa Chadema kuwa hazina maana kwa kuwa wana diwani mmoja pekee kati ya madiwani 33 hivyo hawakupaswa kushangilia.


Katibu wa CCM wilaya ya Arusha, Denis Mwita alisema wamewakabidhi madiwani halmashauri hiyo ili washirikiane na watumishi wa halmashauri hiyo kuwaletea wananchi maendeleo.

Wanawake wa Shoka Upinzani Karibuni CCM-Dkt. Bashiru





Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Dkt. Bashiru Ally  amewakaribisha wanawake kutoka vyama vya upinzania kujiunga na CCM kwa kile alichodai kuwa milango iko wazi kupokea wanawake wapambanaji na wenye nia ya kulitumikia taifa.

 

 

Dkt. Bashiru ametoa kauli hiyo wakati akifungua mkutano wa Kamati za Jumuiya za Chama hicho uliofanyika leo Novemba 29, 2020 jijini Dodoma ambapo amesema kuwa, vyama vya upinzani vilikuwa na wagombea wengi wanawake majimboni na walikuwa na ushahidi.

 

 

"Upinzani walikuwa na wakina Mama wenye ushawishi sana na wametusumbua sana huko majimboni haikuwa rahisi. Lakini nasikitika sana vyama vyao haviwathamini na havitaki kuitambua nguvu yao, Wanawake wa shoka wote wa Upinzani karibuni CCM milango iko wazi", amesema Dkt. Bashiru.

 

 

Akizungumzia suala la ushindi wa Chama, "Hatuna mitambo ya kuiba Kura sisi kama Marekani, sisi mitambo yetu ni mabalozi wetu ambao walifanya kazi Usiku na mchana sababu tulikuwa tunashindana na vyama vilivyoishiwa sera. Vyama vimeshindwa kwa halali vinatafuta sababu kuna Watu wametukana siku 60 za kampeni badala ya kumwaga sera, niwapongeze sana Vijana wa Chama cha Mapinduzi mmeonesha uvumilivu sana kipindi chote cha kampeni"

 

Serikali yasisitiza uwepo wa miradi kwa wafugaji


Serikali imesema katika kuboresha na kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Mkoa wa Morogoro, inasisitiza uwepo wa miradi ambayo itakuwa na manufaa makubwa kwa makundi yote mawili.


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel amesema hayo katika Wilaya ya Mvomero, Morogoro alipotembelea ujenzi wa mradi wa kiwanda cha nyama katika Ranchi ya Nguru Hills na kubainisha kuwa mradi huo unaotarajia kukamilika mwezi Aprili mwaka 2021 utakuwa na manufaa makubwa kwa wafugaji na wakazi wa Morogoro.


"Tumekuja kuangalia shughuli zinazoendelea kutokana na kikao ambacho tulikuwa nacho katika ofisi ya katibu tawala wa mkoa na mkuu wa Mkoa wa Morogoro katika kuboresha shughuli za mifugo kwenye mkoa huo na kuondoa changamoto za migogoro ya wafugaji ambapo uongozi wa mkoa waliniambia juu ya mradi huu ambao utakuwa na msaada mkubwa sana kwa wakulima na wafugaji wa mkoa wa Morogoro na nchi kwa ujumla." Amesema Prof. Gabriel


Prof. Gabriel amebainisha kuwa mradi huo wa kipekee ambao mara baada ya kiwanda hicho kukamilika kitakuwa na uwezo wa kuchinja mbuzi zaidi ya 200 na ng'ombe zaidi ya 1,000 kwa siku, kumejengwa mabwawa makubwa ambayo yatakuwa yanakusanya maji yanayotoka kwenye machinjio, kisha kutibiwa kabla ya kutumika tena kwa shughuli za kilimo cha umwagiliaji.


"Mradi huu una jambo mahsusi kuliko mingine, maji haya ya mabwawa yatatumika kwa ajili ya umwagiliaji huu ni moja kati ya miradi ambapo wafugaji na wakulima watanufaika ili wote waone huu mradi ni wa kwao kwa ajili ya uchumi wetu." Ameongeza Prof. Gabriel


Aidha amesema mradi huo wenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 25, ambao unashirikisha wabia mbalimbali ukiwemo Mfuko wa Pesheni kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), ni azma ya serikali katika kuzidi kuboresha mazingira ya uwekezaji hapa nchini kwenye sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya Mifugo hivyo kuwataka wafugaji kuboresha mifugo yao kwa kufuga ng'ombe bora wa kisasa na kupitia miradi ya kunenepesha mifugo ili waweze kuuza mifugo yenye ubora katika viwanda vya kusindika mazao ya mifugo hapa nchini ili sekta izidi kukua na kuchangia pato la taifa kupitia uchumi wa viwanda.

CCM yawakaribishwa waliofukuzwa upinzani



Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi, Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amewakaribisha wanawake kutoka vyama vya upinzania kujiunga na CCM kwa kile alichodai kuwa milango iko wazi kupokea wanawake wapambanaji na wenye nia ya kulitumikia taifa.
Dkt. Bashiru ametoa kauli hiyo wakati akifungua mkutano wa Kamati za Jumuiya za Chama hicho uliofanyika leo Novemba 29, 2020 jijini Dodoma ambapo amesema kuwa, vyama vya upinzani vilikuwa na wagombea wengi wanawake majimboni na walikuwa na ushahidi.

"Upinzani walikuwa na wakina Mama wenye ushawishi sana na wametusumbua sana huko majimboni haikuwa rahisi. Lakini nasikitika sana vyama vyao haviwathamini na havitaki kuitambua nguvu yao, Wanawake wa shoka wote wa Upinzani karibuni CCM milango iko wazi", amesema Dkt. Bashiru.

Akizungumzia suala la ushindi wa Chama, "Hatuna mitambo ya kuiba Kura sisi kama Marekani, sisi mitambo yetu ni mabalozi wetu ambao walifanya kazi Usiku na mchana sababu tulikuwa tunashindana na vyama vilivyoishiwa sera. Vyama vimeshindwa kwa halali vinatafuta sababu kuna Watu wametukana siku 60 za kampeni badala ya kumwaga sera, niwapongeze sana Vijana wa Chama cha Mapinduzi mmeonesha uvumilivu sana kipindi chote cha kampeni".


Jenerali Mabeyo Atunukiwa Nishani Maalum Ya Mlima Kilimanjaro


Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi akipokea Nishani Maalum ya juu ya Mlima Kilimanjaro kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa, Baba Askofu Mstaafu Elinaza Sendoro wakati wa Mahafali ya 23 ya Chuo hicho Mjini Iringa.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi akionesha Nishani Maalum ya juu ya Mlima Kilimanjaro aliyopokea kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa, Baba Askofu Mstaafu Elinaza Sendoro wakati wa Mahafali ya 23 ya Chuo hicho Mjini Iringa.


Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Julius Mbungo akionesha Nishani Maalum ya juu ya Mlima Kilimanjaro aliyopokea kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa, Baba Askofu Mstaafu Elinaza Sendoro wakati wa Mahafali ya 23 ya Chuo hicho Mjini Iringa.

…………………………

Na Kanali Juma Nkangaa SIPE, Iringa

Chuo Kikuu cha Iringa (zamani Tumaini University) kimemtunukia Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Salvatory Venance Mabeyo Nishani Maalum ya Mlima Kilimanjaro (University of Iringa Miunt Kilimanjaro Award) ambayo hutolewa kwa Viongozi wa juu Serikalini ambao wametoa mchango wa kutukuka kwa Chuo au Tasnia ya Elimu kwa ujumla. Tukio hilo limefanyika wakati wa Mahafali ya 23 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika "campus" ya Chuo Mjini Iringa tarehe 28 Nov 20.

Mwingine aliyetunukiwa Nishani hiyo Maalum ya juu wakati wa Mahafali hiyo ni Mkurugenzi wa TAKUKURU, Brigedia jenerali John Julius Mbungo. Kwa mara ya kwanza Nishani hiyo ilitunukiwa kwa aliyekuwa Rais (Mstaafu) wa Awamu ya Tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Benjamin William Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa wakati wa Mahafali ya 22 ya Chuo hicho mwaka 2019.




Messi kutua Chelsea ?



Klabu ya Chelsea imeripotiowa kufuatilia kwa karibu mno hali ya mchezaji Lionel Messi ndani ya Barcelona kama inaweza kumsajili nyota huyo msimu ujao wa majira ya joto.

Lionel Messi to Chelsea? Blues fans spot interesting development on  Instagram

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari Hispania, Guillem Balague amedai Chelsea imekuwa ikifuatilia kwa karibu kila kinachoendelea ndani ya Barcelona baina ya Messi na klabu yake.

Muargentina siku za hivi karibuni ameripotiwa kushinikiza kwa uongozi wa Barcelona akihitaji kuondoka jambo ambalo liligonga mwamba, ikumbukwe kuwa mnamo mwezi Agosti aliwahi kuutumia ujumbe uongozi wake akiweka wazi dhamira yake hiyo ya kutimka.

Hayo yote yalijiri mara baada ya Barcelona kushushiwa gharika ya mabao 8 – 2 dhidi ya Bayern Munich katika hatua ya robo fainali ya Champions League.

Ukiachana na Chelsea klabu ya Manchester City nayo imeonekana ikifukuzia saini ya Messi lakini hata hivyo nyota huyo amewahi kusikika akidai kuwa ataendelea kusalia Barcelona licha ya kutambua hatakuwa na furaha.

Messi mwenye umri wa miaka 33, ameonekana kutokuwa vema msimu huu hasa ukizingatia amefunga jumla ya magoli matatu tu kwenye michezo 10 aliyocheza ligi kuu Hispania La Liga.



Source

KIKAO CHA SEKRETARIETI YA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM NA KAMATI ZA UTEKELEZAJI ZA JUMUIYA ZA CCM CAFANYIKA JIJINI DODOMA

KATIBU Mkuu CCM Dkt Bashiru Ally akizungumza wakati wa Kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na Kamati za Utekelezaji za Jumuiya za Chama - UVCCM, UWT NA WAZAZI ukumbi wa White House jijini Dodoma leo



Katibu Mkuu Wizara ya Maji atoa siku 60 kwa SOUWASA


Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga ametoa Siku 60 kwa Mamlaka ya Majisafi  na Usafi wa Mazingira Songea (SOUWASA) kukamilisha ujenzi wa mradi wa maji wa kijiji cha Litisha katika Halmashauri ya wilaya ya Songea.

Mhandisi Sanga ameelekeza hayo Novemba 28, 2020 wakati wa ziara yake ya kukagua na kujionea hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa miradi ya maji inayotekelezwa wilayani humo akiwa ameambatana na Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama.

Akiwa kwenye mradi wa maji wa Litisha unaotekelezwa na wataalam wa ndani kutoka SOUWASA, Mhandisi Sanga alijionea hali halisi ya ujenzi wake ambapo alisema amefarijika kuona kisima kilichochimbwa kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wa kijiji hicho kikitoa maji mengi.

Hata hivyo alisisitiza ukamilishwe haraka na huku akikumbushia dhamira ya Serikali ya kuwasogezea huduma ya maji wananchi wakehasa wanyonge ili kuwapunguzia usumbufu wa kutembea umbali mrefu kufuatilia huduma ya magi.

"Nimefurahi kuonakisima kinatoa maji mengi sana na tenki tayari limekamilika lakini bado miundombinu ya kuwafikishia wananchi maji haijakamilika; maelekezo yangu ni kuwa, ndani ya siku 60 mradi huu uwe umekamilika na wananchi wawe wamepata huduma ya maji," alielekeza Mhandisi Sanga.

Mhandisi Sanga aliwahakikishia wananchi wa Songea kwamba Serikali haitowaangusha, itahakikisha huduma ya majisafi na salama inawafikia wananchi mapema iwezekanavyo kama ilivyoahidiwa kwenye Ilani ya Chama cha Mapinduzi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu.

"Ninawahakikishia Serikali mliyoichagua kwa kura nyingi haitowaangusha, iliahidi na sasa inatekeleza, ni suala la muda tu, kero ya maji hapa Litisha na maeneo mengine ya jimbo hili la Peramiho tunakwenda kuimaliza," alisisitiza Mhandisi Sanga.

Mhandisi Sanga alibainisha kwamba kabla ya mwezi huu kumalizika Wizara ya Maji itapeleka kiasi cha shilingi milioni 200 ili kuiwezesha SOUWASA kununua mabomba sambamba na kuhakikisha huduma ya nishati ya umeme imefika kwenye mradi ili wananchi wapate huduma.

"Tutaleta milioni 200 kwa ajili ya kununua mabomba na kujenga miundombinu ya kuwasogezea huduma wananchi wanyonge ili ndani ya siku 60, wawe wamefikishiwa maji," alisisitiza Mhandisi Sanga.

Mhandisi Sanga alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama kwa jitihada zake za kufuatilia utekelezwaji wa miradi ya maji jimboni humo.

Akizungumzia utekelezaji wa miradi kwenye halmashauri ya wilaya ya Songea, Mkurugenzi Mtendaji wa SOUWASA, Mhandisi Patrick Kibasa alisema inatekelezwa kupitia Fedha za Mfuko wa Maji na inahusisha uchimbaji wa visima virefu na ujenzi wa miundombinu ya maji.

Kibasa alisema miradi inatekelezwa kwa awamu mbili tofauti na kwamba awamu ya kwanza inatekelezwa kupitia Mkandarasi Drilling and Dam Construction Agency (DDCA) na inahusisha uchimbaji wa visima virefu 39 katika vijiji 20 vya Halmashauri ya Wilaya ya Songea na kwamba tayari visima 19 vimechimbwa na shughuli inaendelea.

Aidha, aliongeza kuwa awamu ya pili inatekelezwa na wataalam wa ndani na inahusisha ujenzi wa miundombinu ya maji kwenye vijiji nane vilivyothibitika kuwa na maji ya kutosha na kwamba ujenzi umeanza katika vijiji vinne ambavyo ni Litisha, Litowa, Nakahuga na Peramiho B kwa gharama ya shilingi bilioni 2.4

Kamwe Usiolewe na Mwanaume Asiyeweza Kukulipia Mahari

  


Kamwe usiolewe na mwanaume ambaye hawezi kukulipia mahari. Sikuwahi kuona kwenye Biblia mwanaume aliyepewa mke bure.


Tena wengine mnajifanya kupenda sana, unalazimisha kuolewa na mwanaume ambaye hawezi kukulipia mahari. Wengine mnaenda mbali zaidi na kuwasaidia kulipa hizo mahari.


Ukiona umemsaidia kulipa mahari usishangae na huko ndani akakuachia majukumu yote ya familia.


Kama unampenda msaidie mambo mengine lakini ikifika muda wa kulipa mahari hiyo ngoma mwache aicheze mwenyewe, ikimshinda basi huyo hakufai.


Kwanini hakufai?


Hakufai kwa sababu suala la kuoa siyo surprise ni suala la kujiandaa. Kama mchumba ameweza kununua mahitaji yake yote, atashindwaje kukulipia mahari!?


Binti nakwambia usije thubutu kujifanya unamsaidia mwanaume kulipa mahari, hilo ni lake. Ukimpa mahari ujue umejioa mwenyewe dada.


Na wale vijana mnaolipiwa mahari na wazazi wenu pia siwaelewi jamani. Usije ukashangaa mke anakuwa wa ukoo, wao ndiyo wanamcontrol na hauwezi kufanya jambo bila wao.


Na Winnie Kilemo

MIZIZI 29 POWAR NI DAWA YANYE UBORA WA ALI YA JUU YENYE UWEZO WA KUBORESHA AFYA YA MWANAUME


1. kushindwa kushiliki vyema tendo la ndoa

2. kushindwa kurudia tendo la ndoa dawa hii itakufanya uludie zaidi ya mala tatu

3. kufika kileleni haraka kabra mwenzi wako ajafika dawa hii itakufanya uchelewe kukojoa

4. uume kulegea na kuwa mfupi dawa hii itauboresha

5. ngiri ya kupanda na kushuka

6. tumbo kuunguruma na kukosa choo


ISENYE hii ni dawa ya kisukari  dawa hii hahina masharti endapo Kama Kuna dawa nyingine unatumia ni dawa ya tofauti kabasi na inakupa matokeo ya haraka Sana


MWITA hii ni dawa mvuto wa mpenzi mme ,mke au mpenzi aliyekuacha au unayemtaka wewe, pia nidawa zuri kwa wafanya biashara ,


Pia Kuna dawa za presha, vidonda vya tumbo,uzazi,miguu ,mgongo,na kiuno kuuma, magonjwa ya moyo,


Je unasumbuliwa na magonjwa sugu ambayo umehangahika bira mafanikio onana na TABIBU AGU atakusaidia


kwa nini uhangahike bila sababu okoa afya yako na ndoa yako Sasa, kumbuka  magonjwa  haya sio mageni kigeni ni tiba ipi sahihi ya kukupa furaha


Wasiliana nami 0782794980 Whatsapp +255782794980 uduma hizi utapata popote ulipo ata Kama upo nnje ya nchi

Saturday, November 28, 2020

TAMWA YAONESHA NJIA YA KUMALIZA UDHALILISHAJI ZANZIBAR

Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali kisiwani Pemba wakionesha bango lenye ujumbe wa kukataa kupinga vitendo vya udhalilishaji katika viwanja vya Gombani ya kale Pemba.
***

Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa kusini Pemba  Rashid Khadid Rashid ameelezea kutoridhishwa na baadhi ya watendaji wa vyombo vya mahakama, polisi pamoja na wanaharakati wanaoshiriki kufanya suluhu dhidi ya kesi za udhalilishaji na kusema hali hiyo inachangia kukwamisha juhudi za serikali za kuyatokomeza matendo hayo.

Akizungumza kwenye maadhimisho ya siku kumi na sita za kupinga ukatili wa kijinsia katika viwanja wa Gombani kisiwani Pemba yaliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA Zanzibar).

Mkuu huyo wa Wilaya amezitaka kamati za kupinga udhalilishaji za wilaya kushirikiana na Ofisi ya Mufti kutoa elimu ya ndoa kwa wanandoa  pamoja na sehemu zenye mikusanyiko ya watu ikiwemo maskulini.

Amesema kesi nyingi za udhalilishaji zinashindwa kupatiwa ufumbuzi wa haraka kutokana na kuwepo na baadhi ya watumishi wa vyombo vinavyosomamia sheria kukosa uadilifu.

"Miongoni mwa mambo yanayochangia kesi hizi ziendelee kutokea ni uwepo wa baadhi ya watumishi ambao sio waadilifu wanaoshiriki kufanya suluhu, pamoja na hukumu ndogo zinazotolewa dhidi ya watuhumiwa,"alisema.

Akizungumzia kuhusu mwenendo wa matukio hayo Kisiwani Pemba amesema bado tatizo hilo lipo kwa kiwango kikubwa katika jamii licha ya matukio hayo kuanza kupungua ikilinganishwa na miaka iliyopita ikiwa ni kutokana na juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na wanaharakati mbalimbali wakiwemo TAMWA Zanzibar.

"Naomba niiambie hadhira hii kuwa vitendo vya udhalishaji bado ni tatizo kubwa na matukio haya yanaripotiwa kila siku katika jamii zetu, kwa mwaka huu hadi sasa tuna  kesi 218 ambazo zinafanyiwa kazi ktika ngazi mbalimbali ambapo kwa wilaya ya Wete ni 57, Micheweni 30, Chake Chake 84, na Mkoani 47 ambapo kesi za ubakaji ndizo zinazoongoza kwa wingi katika kesi hizi." alisema.

Mratibu wa TAMWA Pemba Fat-hiya Mussa Said amesema lengo la kuandaliwa kwa mazoezi hayo ya hiari ya siku moja ni kubadilisha tabia hasa za vijana dhidi ya fikra potofu za kubaka na kudhalilisha kwa ujumla kupitia ufanyaji wa mazoezi.

"TAMWA Zanzibar kwa kuwa ni wadau wakubwa wa kupambana na udhalilishaji wa wanawake na watoto tumeamua kuadhimisha siku hii kwa kufanya mazoezi ya hiari ili kupaza sauti za wanyonge kupitia kampeni  ya siku 16 za  kuhamasisha  jamii  kubadili tabia juu ya ukatili wa mtoto wa kike.''

Katika hatua nyingien Mratibu huyo amesema, TAMWA itaendelea kushirikiana wadau mbali mbali, ili kuhakikisha wanawake na watoto wanaishi bila ya ukatili na udhalilishaji.

Akitoa salama za wanawake, Mkuu wa Idara ya wanawake Pemba, Mwanaisha Ali Massoud, alisema siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto wa kike ni muhimu kwa jamii, ili kutafakari namna ya kuyakinga makundi hayo dhidi ya ukatili.

Alisema, udhalilishaji na ukatili huathiri sana wanaofanyiwa ikiwa ni pamoja na kukatisha ndoto zao ziwe na kielimu au biashara kutokana athari zake.

Alisema, "njia rahisi ya kupambana na matendo hayo ni kwa jamii kuondoa muhali na kushirikiana na vyombo vya sheria ikiwa ni pamoja Polisi na mahakama."

Tatu Abdalla Msellem kutoka jumuiya ya Tumaini Jipya Pemba (TUJIPE)ametoa wito kwa taassi na idara za serikali kuongoeza ushirikiano na asasi za kiraia hasa suala la upatikanaji wa takwimu ili kufanikisha mapambano dhidi ya vitendo hivyo.

"Ili kufanikisha kupiga vita matendo hayo, wakati mwengine tunapoomba miradi huhitaji takwimu, ili kupata ithibati, lakini huwa vigumu, sasa lazima hili lionekane na liondolewe,''aliesema.

Awali kwenye mkutano huo ulinogeshwa na kikundi cha mazoezi cha Gombani, usomaji wa utenzi pamoja na mchezo wa kuigiza kutoka kundi cha 'Thesode' la Ngwachani wilaya ya Mkoani Pemba.

Maadhimisho ya siku kumi na sita za kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto huadhimishwa kila ifikapo tarehe 25 Novemba hadi tarehe 10 Desemba ya kila mwaka ambapo Ujumbe wa mwaka huu ni TUPINGE UKATILI WA KIJINSIA , MABADILIKO YAANZE NA MIMI. Sambamba na ujumbe maalum wa TAMWA ZNZ 'Fanya mazoezi zuia mihemuko: Muache mtoto wakike salama.


MBUNGE RIDHIWANI KIKWETE AFANYA ZIARA TARURA-CHALINZE, AAHIDI KUPIGANIA KUONGEZA BAJETI ZAIDI


Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akizungumza na Meneja wa TARURA- Chalinze, Mhandisi Enrico Shauri (kulia).
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete ameendelea na ziara maalum ambapo leo ametembelea ofisi za Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini-Tanzania (TARURA)- Chalinze ili kuona namna wanavyofanya kuendelea kuboresha miundombinu ya barabara korofi za Halmashauri hiyo.

Awali akifanya mazungumzo na Meneja wa TARURA- Chalinze, Mhandisi Enrico Shauri leo, Mbunge Ridhiwani alitaka kufahamu mpango mkakati wa namna ya kuboresha baadhi ya barabara zilizo katika Kata hiyo ambazo zimekuwa kero kwa kipindi kirefu.

"Chalinze tuna barabara nyingi lakini baadhi ya barabara hizo zina usumbufu mkubwa hasa baada ya wakati wa mvua hazipitiki kirahisi; je Tarura tumejipangaje na ni kwa namna zitakavyokuwa zinapitika muda wote.?"

Pamoja na hoja hiyo Mheshimiwa Mbunge alitamani kujua wamejipangaje kufungua baadhi ya barabara ambazo zikifunguliwa zitakuwa msaada mkubwa kwa Wananchi wa Chalinze kufikia malengo.

Kwa upande wake Meneja wa TARURA- Chalinze, Mhandisi Enrico Shauri alianza kwa kupongeza ziara hiyo ya Mbunge ambapo pia aliahidi kuyafanyia kazi maagizo na ushauri wote  uliotolewa kayoka mazungumzo yao.

Mhandisi Shauri alieleza changamoto kubwa wanayokabili ni ufinyu wa Bajeti ambao unasababisha ufanisi wa kazi zao kusuasua" akifafamua Muhandisi Shauri alisema kuwa TARURA- Chalinze ina kilometa (KM) 679 ambazo ni nyingi sana kwa bejeti inayotengwa ya mfuko wa barabara ni  Milioni 700.44. 

Kwa mwaka huu 2020-2021 tumeshapewa milioni 200 na zingine zitaendelea kutolewa kwa awamu.utolewaji wa haraka wa mafungu ndiyo utawezesha kukamilika kwa kazi mapema.

Mh. Mbunge alimuahidi Meneja wa Tarura kwenda kushauriana na madiwani wenzake kwa kujenga hoja ili aongezewe mafungu ili kuwezesha ujenzi wa Miundo mbinu ya Halmashauri ufanyike haraka kwa faida ya Maendeleo ya Chalinze na Tanzania kwa jumla.

Kwa upande wa Mh. Mbunge alimshukuru Mkandarasi na Tarura kwa jinsi walivyojitahidi kujenga miundombinu pamoja na changamoto hiyo ya kibajeti.

Pamoja na kusikia toka Tarura, Mh.Mbunge alitumia nafasi hiyo kuhimiza maandalizi ya marekebisho na ujenzi wa barabara korofi zote za halmashauri zikiwemo zile za kata ya Kimange, Miono, Mkange, Vigwaza, Ubena, Talawanda, Mandela, Mji wa Chalinze na maeneo mengine kama sehemu za kutolewa macho sana kutokana na shughuli za kimaendeleo na kuchangia uchumi katika Halmashauri hiyo.

Mheshimiwa Mbunge alimaliza kwa kuwaahidi Ushirikiano mkubwa ili kufikia malengo makubwa waliyopanga kuyasimamia kwa pamoja wakishirikiana na Wananchi.

Ziara ya Kata kwa kata inaanza Jumatatu tarehe 30 ambapo Mbunge anatarajia kwenda kata Kata kukagua miradi ya Maendeleo na kuzungumza na Wananchi kusikia kero na matarajio waliyonayo kwa Serikali yao inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli.

Picha: MAONYESHO YA BIASHARA NA TEKNOLOJIA YA MADINI SHINYANGA YAZINDULIWA RASMI

 

Mkuu wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel, (watatu kutoka kulia) akizindua maonyesho ya Biashara na Teknolojia ya madini mkoani Shinyanga, wa pili kulia ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack, wakwanza kushoto ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Zainab Telack, akifuatiwa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi.



Na Marco Maduhu -Shinyanga. 

MKUU wa mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel, amezindua rasmi maonyesho ya biashara na Teknolojia ya madini mkoani Shinyanga, na kuwataka wawekezaji wa madini kwenda kuwekeza mkoani humo, ili kuunyanyua mkoa huo kichumi na kukua kimaendeleo.

RC Mbeya aagiza walioghushi sahihi za marehemu kukamatwa


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila ameamuru watu sita kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kughushi sahihi za watu waliofariki dunia  kisha Serikali kuwalipa fidia ya Sh108 milioni  katika eneo lenye mradi wa soko.


Chalamila amesema hivyo leo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Iyunga jijini hapa ambako kuliibuka mgogoro wa eneo la soko   huku watuhumiwa hao wakidai ni mali yao.


"Hawa wazee walifika ofisini kwangu na kuandika barua ofisi ya Rais na Waziri Mkuu waidai fidia ya Sh 108 milioni huku halmashauri ikiwa imewalipa fidia ya Sh 17 milioni ambazo ni halali  na walipisha eneo hilo "amesema.


Chalamila anasema baada ya kuwasikiliza malalamiko yao amelazimika kuchunguza kwa kina na kubaini  kuwa watuhumiwa hao ni matapeli tayari walilipwa fidia na kwamba kiwanja hicho chenye mradi wa soko ni eneo la urithi wa Wazazi wao ambao walipewa bure na kiongozi wa kimila na hivyo kufanya utapeli kwa serikali.


Mmoja wa watuhumiwa hao,   Philimon Chapanga amekiri mbele ya umati wa watu kuwa walilipwa  Sh 17 milioni na kwamba hawajaridhishwa na kiwango hicho cha fedha kwa kuwa eneo hilo la mradi wa soko lilikuwa kwa ajili ya kilabu cha wazee kujiliwaza jioni.


Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Jiji la Mbeya, Amude Ng'wanidako amesema watuhumiwa hao walilipwa  Sh17 milioni  ikiwa ni fidia ya mradi wa soko ambalo kwa sasa ni mali ya serikali .


Amesema kimsingi madai hayo si ya kweli ni suala la kuihujumu  Serikali kwa madai ya fidia Sh 108 milioni.


"Mgogoro huu ni wa miaka mingi baada ya kufualia nyaraka na kamati zilizoundwa kufuatilia nimebaini wahusika hawaidai halmashauri na kwamba eneo la soko ni mali ya Serikali," amesema.


Akizungumza katika mkutano huo, Nelson Mayena mzee wa mila aliyetoa eneo hilo (chifu Mayena) amesema lilitolewa bure kwa watuhumiwa na walijenga klabu cha wazee kwa ajili ya maongezi ya jioni na kwamba awali walikubaliana na Serikali kulipwa fidia na kupisha mradi wa soko. 


Amesema mwaka 2010 walikabidhi eneo hilo kwa Serikali na kulipwa fidia ya Sh17milioni  suala na madai mengine silielewi.

Ujerumani yasema vizuizi vya corona vitakuwepo hadi Machi



Waziri wa Uchumi wa Ujerumani Peter Altmaier, amesema vikwazo vilivyowekwa kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona vitaendelea kuwepo hadi majira ya kuchipua yanyoanza mwezi Machi 2021. 


Altmaier ameliambia gazeti la Ujerumni la Die Welt lilochapishwa hii leo kwamba haiwezekani kuviondoa vikwazi hivyo wakati bado kunashuhudiwa maambukizi ya watu 50 katika kila wakazi 100,000 kwenye maeneo mengi ya Ujerumani. 



Hapo Jumatano iliyopita, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alikubaliana na viongozi wa majimbo yote16 nchini kuongeza vikwazo na kuviendeleza hadi mnamo Desemba 20. 



Ujerumani ilitangaza kwa mara nyingine tena masharti ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona mwanzoni mwa Mwezi Novemba. Kwa sasa migahawa na baa zimefungwa lakini shule na maduka bado ziko wazi.


Yanga Yaichapa JKT Taifa, Wazidi Kupaa Kileleni



Timu ya Yanga leo Novemba 28 imefanikiwa kuondoka na pointi zote tatu kwenye Uwanja wa Mkapa  jijini Dar, baada ya kuifunga JKT Tanzania ya Dodoma kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara.

 

Goli pekee la timu ya Wananchi limewekwa Nyavuni na Deus Kaseke ambaye amefunga mabao mawili kwenye mechi mbili mfulululizo akiwatungua Azam na leo akiwaadhibu JKT.

 



 

Licha ya kumkosa Nahodha wao Lamine Moro bado Yanga wameendelea kuwa ukuta ngumu kufungika, japokuwa safu ya ushambuliaji inaonekana kukosa makali ya kufamania nyavu hii ikiwa ni mwendelezo wa kushinda magoli yasiozidi mawili.

Kwa ushindi huo kiduchu Yanga imezidi kujikita Kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 31.


Msekwa "Wale 19 sio Wabunge Tena Katiba ya Nchi Inasema Hivyo"




"Siyo sheria ya Bunge hiyo ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inasema kuwa mbunge akiacha kuwa mwanachama wa chama kilichompeleka Bungeni na ubunge wake unakwisha" Spika mstaafu Msekwa

"Spika Ndugai, hapati ugumu wowote wanapoondolewa yeye ni mpokeaji tu, ni kama mganga wa hospitali anapokea wagonjwa akiwatibu wanaondoka na wakifa wanaondoka na hakuna anayeweza kuvunja katiba" Spika Mstaafu, Msekwa


Usiku wa kuamkia leo Novemba 28, 2020, kupitia kikao cha kamati kuu ya chama cha CHADEMA chini ya Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, iliazimia kuwavua uanachama wanachama wake 19 waliokula kiapo cha ubunge bila ridhaa ya chama hicho.


Madini kuchangia 10% ya pato la Taifa hadi 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amewataka wataalamu wa jiolojia nchini kutekeleza wajibu wao kwa weledi ili kuongeza mchango wa sekta ya madini kwenye pato la Taifa kutoka 5.2% mwaka 2019 hadi kufikia 10% mwaka 2025.

Mongella ametoa wito huo katika mkutano mkuu wa mwaka wa chama cha wanajiolojia nchini, unaofanyika jijini Mwanza na kushirikisha wataalamu pamoja na wadau wa jiolojia kutoka sekta mbalimbali zikiwemo za madini na nishati.

Rais wa Chama cha Wanajiolojia Tanzania, Prof. Abdulkarim Mruma, amesema ongezeko la mchango wa sekta ya madini katika pato la Taifa kutoka 3.2% mwaka 2012 hadi 5.2% mwaka jana, limetokana na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Serikali ikiwemo mabadiliko ya sheria zinazosimamia maliasili na rasilimali za Taifa ya mwaka 2017.

Prof. Mruma amesema usimamizi makini utawezesha sekta ya madini kuchangia 10% ya pato la Taifa ifikapo mwaka 2025.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini, James Mataragio, amesema Serikali imejipanga kusambaza nishati ya gesi asilia ili kukidhi ongezeko la mahitaji ya nishati hiyo ndani na nje ya nchi.

Kupitia mkutano huo utakaofikia tamati Novemba 29, baadhi ya wachimbaji wadogo watapata mafunzo kuhusu namna ya kuendesha uchimbaji wenye tija
.

TFF yatoa muongozo huu kumuenzi Maradona

 


Shirikisho la soka Tanzania (TFF)  limetoa mwongozo kwa michezo yote itakayochezwa leo kusimama kwa dakika moja ya ukima ikiwa ni maombolezo a msiba wa gwiji la soka Diego Armando Maradona.



EX wa GINIMBI, Zodwa, afunguka MAZITO kuhusu tetesi za tajiri huyo kufuga JOKA linalotema HELA

 


EX wa GINIMBI, Zodwa, afunguka MAZITO kuhusu tetesi za tajiri huyo kufuga JOKA linalotema HELA

VIDEO:

VIDEO: Hivi ndivyo Halima Mdee na wenzake walivyovuliwa uachama CHADEMA, Mbowe awaonya

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema Kamati Kuu ya Chama hicho iliyoketi leo Nov 27,2020 imeazimia kuwavua uanachama Halima Mdee na wenzake 18 waliopishwa juzi kuwa Wabunge Viti Maalum "wamekinajisi Chama na wamekataa kuja kwenye Kamati Kuu"

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI......USISAHAU KUSUBSCRIBE

Friday, November 27, 2020

Serikali ya Ujerumani yaweka marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki



Ujerumani imetangaza kuchukuwa hatua ya kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki kuanzia Januari 2022.

Kwa mujibu wa kanuni iliyopitishwa na bunge la serikali, mifuko ya plastiki yenye unene wa kati ya mikromita 15 hadi 50 itapigwa marufuku ispokuwa mifuko membamba inayotumika kwa ajili ya mboga.

Waziri wa Mazingira Svenja Schulze alisema kuwa badala ya mifuko ya plastiki, vikapu vya ununuzi na mifuko ya nguo inayoweza kuoshwa ni njia inaweza kutumika kama njia mbadala.

Wakfu wa Kulinda Mazingira Asili WWF, umesisitiza kuwa mifuko ni ishara inayoleta maana ya marufuku kwa mtazamo wao.

WWF inadai kwamba mifuko ya plastiki inayotumika katika ununuzi nchini Ujerumani inachukua asilimia moja ya matumizi yote ya plastiki, kwa hivyo matumizi ya plastiki yanapaswa kupunguzwa katika maeneo yote.

Matumizi ya mifuko ya plastiki yalipungua kwa asilimia 64 nchini Ujerumani baada kuanza kuuzwa mwaka 2015.

Mtu mmoja hutumia mifuko ya plastiki 24 ndani ya mwaka kwa kipimo cha wastani.

Plastiki huchukuwa miaka 400 kutoweka majini na miaka 800 kutoweka ardhini.  

 


Mbunge Sanga awanunulia wananchi wake gari kwa ajili ya kazi mbalimbali za kijamii Jimboni humo

Mbunge wa jimbo la Makete Mh Festo Richard Sanga amewanunulia wananchi wake gari kwa ajili ya kazi mbalimbali za kijamii Jimboni humo.

Aidha kwa upande mwingine mheshimiwa Amesema Ameaumua kutekeleza Baadhi ya ahadi Zake kwa Wananchi wake alizowaahidi wakati anawaomba kura kwa kuanza kuwanunulia Gari Mahususi kwa ajili ya Wananchi wa Jimbo lake ili kuweza kuwasaidia katika shughuli Mbalimbali za kijamii kama vile Misiba, dharula na kuzungukia miradi mbalimbali na utekelezaji wa ilani Kijiji kwa Kijiji.


 

ORODHA YA WALIMU 13,000 WALIOPANGIWA VITUO VYA KAZI


Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Joseph Nyamhanga ,ametangaza ajira za walimu wa shule za msingi na Sekondari zipatazo 13,000 huku akiwataka wote walioweza kupata ajira hizo kuripoti ndani ya muda uliopangwa.
Akitangaza mbele ya waandishi wa habari jijini Dodoma Mhandisi Nyamhanga amesema kuwa walimu hao wanapaswa kuripoti ndani ya siku 14 kuanzia Desemba Mosi hadi 14 na wale ambao watashindwa kuripoti ndani ya muda huo nafasi zao zitachukuliwa na walimu wengine.
 





MAJINA YA WALIMU WOTE WALIOPANGIWA SHULE ==> TAZAMA HAPA



VIDEO: Kinochoendelea CHADEMA kuitwa kwa Halima Mdee na wenzake kuhojiwa

Baadhi ya wanachama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema leo Novemba 27 wamejitokeza makao makuu ya chama hicho kushinikiza uongozi kuwachukulia hatua Wabunge 19 wa Viti maalum walioapishwa huku kukiwa kuna sintofahama.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.....USISAHAU KUSUBSCRIBE 

Kenya yapunguza idadi ya wageni wanaohudhuria harusi kutokana na corona



Idadi ya wageni watakaoruhusiwa kuhudhuria harusi nchini Kenya imepunguzwa hadi kufikia watu 50 pekee kutokana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona nchini humo.

Baraza linalojumuisha dini mbali mbali nchini humo limesema kuwa chakula kinachotolewa katika harusi kitakuwa kikitilewa kwa wazazi na ndugu wa damu wa maharusi pekee.

Mwezi Agosti Rais Uhuru Kenyatta aliongeza idadi ya wageni wanaoweza kuhudhuria harusihadi watu 100 alipolegeza masharti ya kudhibiti maambukizi ya Covid-19.

Katika masharti mapya yaliyotangazwa Alhamisi wiki hii, chakula kimepigwa marufuku katika mazishi na idadi ya watu wanaoruhusiwa kuhudhuria mazishi imepunguzwa hadi watu 100 pekee.

Muda wa mazishi pia umerekebishwa kwa kupunguzwa hadi saa moja pekee.

Huduma za kanisa pia hazitatolewa kwa zaidi ya dakika 90.

Wiki iliyopita mwenyekiti wa baraza la dini mbali mbali nchini Kenya, Anthony Muheria, alitibiwa virusi vya corona katika hospitali moja mjini Nairobi.


Tume ya uchaguzi Uganda yawataka polisi kutowazuwia wagombea urais





Tume ya uchaguzi nchini Uganda imewatahadharisha polisi nchini humo dhidi ya kuwazuia wagombea wa urais kuendesha kampeni zao.
Tume hiyo imesema kuwa imepokea baadhi ya malalamiko kutoka kwa wagombea wa urais na pia kuona taarifa zavyombo vya habari kwamba polisi inazuia na kuvuruga kampeni zao .

Wakati huo huo katika taarifa ya pamoja ya mabalozi wa nchi za Muungano wa Ulaya nchini humo, wameeleza kutofurahishwa kwao na ghasia zilizotawala kampeni ya uchaguzi tarehe 18 na 19, Novemba nchini humo.

Wamesema Uganda ilishuhudia ghasia na maandamano pamoja na matumizi yasiyofaa ya vikosi vya usalama dhidi ya raia na kuvitaka vyama vyote vya kisiasa na wagombea wake kuwataka wafuasi wao kuacha ghasia na matumizi ya lugha mbaya.

Wametoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua kali za kisheria kumaliza uchokozi unaolenga kuleta ghasia au kusababisha ukiukaji wa sheria.

Hii inajiri huku Kiongozi wa upinzani nchini huo Robert Kyagulanyi al maarufu Bobi Wine alilalamikia kuzuiwa kuendesha kampeni zake katika mji wa Hoima magharibi mwa nchi hiyo.

Katika ujumbe wake wa twitter Bobi Wine amesema kuwa polis walifunga barabara za kuelekea katika mji huo ili kumzuwia kufika katika hoteli aliyotarajia kupata malazi na kuziamuru hoteli zaote katika mji huo zisimpokee na timu yake, na hivyo kuwalazimisha kulala ndani ya magari:


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...