Friday, November 30, 2018

VIDEO: Full Video Kilichotokea Mbowe, Matiko kukosa dhamana


Mahakama Kuu ya Tanzania imesitisha kusikiliza rufaa ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini,Esther Matiko hadi rufaa ya upande wa mashtaka itakaposikilizwa Mahakama ya Rufani ya kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu ya kusikiliza rufaa hiyo.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI..........USISAHAU KUSUBSCRIBE............ 

Ali Kiba Kupiga Shoo na Yvonne Chakachaka

Mwanamuziki katika tasnia ya Bongo movie Ali Kiba amefunguka kwamba atafanya shoo mbili za kufanga mwaka jijini Dar es Salaam ambapo atakuwa na muimbaji mkongwe, Yvonne Chakachaka kutoka Afrika Kusini. Kupitia ukurasa wa Instagram, Ali Kiba amesema atafanya shoo hizo kabla ya mwaka haujaisha: Ikiwa leo ni siku yangu ya kuzaliwa namshukuru Mungu kwa kuendelea kunibariki katika kila jambo na namshukuru kwa kunipa mashabiki wanaonipa support ya dhati kabisa. Shukrani zangu kwa mashabiki mwaka huu katika Funga mwaka na King Kiba zinakuja na show mbili kubwa ndani ya Desemba 2018. 1st Edition ya Funga Mwaka Na King Kiba nitakuwa na Princess of Africa Mama Yvonne_ ChakaChaka itafanyika Serena Hotel Dar es Salaam 22. December. 2018. Halafu 2nd Edition ya Funga Mwaka Na KingKiba itatukutanisha pale Next Door Arena, Dar es Salaam tarehe 29. December.2018." Hii haikuwa mara ya kwanza Msanii kwa Ali Kiba kumleta Yvonne Chakachaka na kupiga naye shoo, ameshawahi kumleta na Kuperfom naye katika siku ya wanawake.

The post Ali Kiba Kupiga Shoo na Yvonne Chakachaka appeared first on Ghafla! Tanzania.


Source

Mbunge nchini Uingereza atangaza kuwa anaishi na virusi vya UKIMWI ‘nimejificha kwa miaka 10’

Mbunge wa Chama cha Leba cha nchini Uingereza, Lloyd Russell-Moyle ametangaza hadharani kuwa anaishi na virusi vya UKIMWI. Moyle alitoa taarifa hizo jana Novemba 29, 2018 bungeni kwenye hotuba yake iliyokuwa yenye hisia nzito kuhusu Ugonjwa wa Ukimwi. “Ninakaribia miaka 10 sasa tangu nipimwe na nikutwe na virusi vya UKIMWI nikiwa na miaka 22, lakini kwa …

The post Mbunge nchini Uingereza atangaza kuwa anaishi na virusi vya UKIMWI ‘nimejificha kwa miaka 10’ appeared first on Bongo5.com.


Source

Picha : VIONGOZI WA HALMASHAURI WILAYA YA SHINYANGA WAFANYA ZIARA RAFIKI SDO

Viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga leo wamefanya ziara kutembelea Shirika lisilo la kiserikali la Rafiki Social Development Organization (Rafiki SDO) kwa ajili ya kujionea shughuli zinazotekelezwa na shirika hilo kwenye halmashauri hiyo katika kuhakikisha wananchi wenye hali ya chini wanajikwamua kimaisha.

Ziara hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Ngasa Mboje aliyekuwa ameambatana na Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Thomas Tukay na maafisa wengine imefanyika leo Ijumaa Novemba 30,2018.

Awali viongozi hao walipokea taarifa ya shughuli zinazofanywa na shirika hilo kisha kukutana na watoto 10 kutoka kata ya Mwakitolyo waliokuwa vibarua katika mgodi wa Mwakitolyo wanaosoma kwa ufadhili wa Rafiki SDO katika Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi Buhangija mjini Shinyanga

Akizungumza wakati wa ziara hiyo,Mboje alisema lengo la ziara ni kujionea kwa vitendo shughuli zinazofanywa na shirika la Rafiki SDO ikiwa ni sehemu ya kujiridhisha badala ya kupeana taarifa za kwenye makaratasi ili kujenga ushirikiano na uwazi katika utendaji.

"Tunawashukuru sana kwa kuendelea kushirikiana na serikali katika kuwasaidia wananchi,tunatambua shughuli zenu nzuri za kuwakwamua kiuchumi wananchi",alisema.

Mboje alitumia fursa kuwataka watendaji wa vijiji na kata kushirikiana na wadau wa maendeleo yakiwemo mashirika kwa lengo ni moja tu kuwatumikia wananchi.

Aliyataka mashirika kutoa taarifa kwa viongozi wa serikali pale wanapokosa ushirikiano ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la Rafiki SDO,Gerald Ng'ong'a alizitaja baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo kwenye maeneo wanayotekeleza miradi kuwa ni ushirikiano mdogo wa viongozi wa serikali mfano Mtendaji wa kata ya Mwakitolyo hali inayosababisha kushindwa kufikia malengo ya mradi wa kupinga ajira za utotoni.

Aliitaja miradi sita inayotekelezwa na shirika hilo kuwa ni mradi wa kupinga ajira za utotoni,Tulonge afya,Ulinzi wa haki za mtoto na utawala,Kupinga ukatili wa kijinsia,Kupinga mimba na ndoa za utotoni na mradi wa Sauti.

Aidha aliishukuru serikali kwa ushirikiano inaotoa katika kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa na kwamba ziara hiyo ya viongozi wa halmashauri itakuwa chachu ya mabadiliko zaidi ili kuwainua wananchi kiuchumi.

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Rafiki SDO,Gerald Ng'ong'a akiwakaribisha viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga katika ofisi za shirika hilo Mjini Shinyanga. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngasa Mboje akifuatiwa na Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Thomas Tukay,Kaimu Mganga mkuu wa halmashauri,Bashiri Salum,kaimu Afisa Maendeleo ya jamii,Edmund Ardon na Mratibu wa Ukimwi halmashauri hiyo, Happiness Misael - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkurugenzi wa Shirika la Rafiki SDO,Gerald Ng'ong'a akizungumza wakati viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga walipotembelea shirika hilo kujionea shughuli zinazofanywa na shirika hilo.
Mkurugenzi wa Shirika la Rafiki SDO,Gerald Ng'ong'a akizungumza wakati wa ziara hiyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Ngasa Mboje akizungumza wakati wa ziara yao kwenye shirika la Rafiki SDO.
Kushoto ni Mratibu wa Ukimwi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Happiness Misael akizungumza wakati ziara hiyo.
Afisa Mradi wa Ulinzi wa mtoto,haki na utawala wa shirika la Rafiki,Tangi Clement akielezea shughuli zinazofanywa na shirika katika maeneo ya afya,elimu,uwezeshaji kiuchumi,ulinzi wa mtoto,haki na utawala na ujasiriamali.
Viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakifuatilia taarifa ya shirika la Rafiki SD wakati Tangi Clement akisoma taarifa kwao.
Viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na viongozi wa shirika la Rafiki SDO wakiwa katika picha ya pamoja nje ya ofisi za Rafiki SDO.
Kijana Chalo Adam ambaye ni miongoni mwa watoto 8 kati ya 10 ambao wamesomea ufundi umeme kwa ufadhili wa shirika la Rafiki katika chuo cha Maendeleo ya Wananchi Buhangija akionesha jinsi wanafanya ufundi umeme majumbani wakati viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga walipotembelea chuo hicho kujionea shughuli zinazotekelezwa na Rafiki SDO.
Vijana ambao awali walikuwa vibarua migodini kisha kuchukuliwa na shirika la Rafiki SDO na kusomeshwa katika chuo cha Maendeleo ya Wananchi Buhangija kusomea masuala ya umeme wakionesha jinsi wanavyounganisha umeme majumbani.
Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Thomas Tukay akiwapongeza vijana hao kwa ujuzi walioupata kwenye chuo cha Maendeleo ya Wananchi Buhangija.
Kijana Benjamin Clement akitoa maelezo kwa viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga jinsi wanavyounganisha umeme.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Ngasa Mboje akiangalia batiki katika darasa la fani ya ushonaji nguo katika Chuo Cha Maendeleo ya Wananchi. Wanafunzi wawili wa kike ambao walikuwa wanasaidia mama lishe kwenye mgodi wa Mwakitolyo wamesomeshwa na shirika la Rafiki SDO.
Katikati ni Kaimu Afisa Maendeleo ya jamii,Edmund Ardon akiangalia nguo zilizotengenezwa na vijana katika Chuo cha Maendeleo ya jamii. 
Kijana Jefta Eziel akilishukuru shirika la Rafiki SDO kwa kusomesha watoto/vijana 10 waliokuwa vibarua katika mgodi wa Mwakitolyo na sasa vijana wa kiume 8 wamehitimu mafunzo fani ya umeme na wawili wa kike fani ya ushonaji.
Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Buhangija Maria Mkanwa akimweleza jambo Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngasa Mboje na Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Thomas Tukay walipotembelea chuo hicho kukutana na wanafunzi waliosomeshwa na shirika la Rafiki SDO.Kulia ni Mkurugenzi wa shirika la Rafiki SDO,Gerald Ng'ong'a
Viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,viongozi wa shirika la Rafiki SDO  na vijana waliosomeshwa na shirika la Rafiki katika Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Buhangija wakiwa katika picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Wema Sepetu Afunguka Baada Ya Skendo Yake Nzito

Muigizaji wa Bongo movie mrembo Wema Sepetu amefunguka na kuelezeawmaisha yake yanavyoenda tangu akumbwe na ile fedheha ya mwaka Baada ya picha na video zake chafu kuvuja mtandaoni.

Wiki chache zilizopita Wema aliwadhangaza watu wengi Baada ya kuamua kuwanika video na picha zake kwenye mitandao ya kijamii zilizomuonyesha akiwa anakumbatiana kubusiana na aliyekuwa Mpenzi Wake kwa kipindi hiko PCK.

Baada ya sakata hilo Wema amefunguka na kusema kuwa maisha yake ya sasa  anapenda yawe ya siri zaidi na kama ana shida ya kuzungumza vitu ambavyo vinamsibu ni vyema amtafute mtu sahihi ambaye anamuamini kwa asilimia zote.

Katika mahojiano yake na Gazeti la Ijumaa, Wema alisema kuwa, kwa sasa amekuwa makini kwa kila kitu anachofanya ili kumuweka salama tofauti na zamani ambapo mambo yake mengi yalikuwa yakivuja hovyo.

Kwa kweli sasa hivi niko makini sana na kila jambo hivyo nimepitia kipindi kigumu sana mpaka sasa hivi nimeamua kujituliza kufanya vitu vyangu kiakili".

Baada ya kusambaza picha hizo Wema alifunguliwa kesi mahakamani ambayo inaendelea kusikilizwa.

Picha : BENKI YA NMB YATOA MAFUNZO KWA MAWAKALA WA NMB MKOA WA SHINYANGA

Benki ya NMB imeendesha mafunzo kwa Mawakala NMB mkoa wa Shinyanga kwa ajili kuwajengea uwezo wa kiutendaji wafahamu mbinu za kudhibiti fedha haramu pamoja na mbinu za kukuza biashara zao kwa kuongeza wateja.

Mafunzo hayo yamefanyika leo Alhamis Novemba 29,2018 katika ukumbi wa Empire Hotel Mjini Shinyanga ambapo mgeni alikuwa Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Lembris Melusori.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo,Melusori alisema mafunzo hayo yana lengo la kuwawezesha mawakala kukuza kipato chao lakini pia namna ya kudhibiti fedha chafu/haramu 'Money laundering'.

"Lengo jingine ni kuwasilisha na kuzipatia ufumbuzi changamoto zinazowakabili mawakala hawa,kuwapongeza/kutambua mchango wa mawakala wanaofanya kazi vizuri na kuwaeleza kuhusu maboresho yanayofanywa na NMB",alisema Melusori.

Hata hivyo aliwataka mawakala wa NMB kufanya kazi kwa umakini na kuzingatia maadili katika utendaji kazi wao na kuhakikisha wanafuata taratibu na sheria halali za fedha.

"Asilimia ya watanzania wanaotumia benki ipo chini ya asilimia 20 kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni hivyo shirikiane na benki kuhakikisha kuwa watanzania ambao hawajaanza kutumia huduma ya benki kwani benki ni sehemu salama zaidi",aliongeza.

Kwa upande wake Meneja Mahusiano na Wakala na Mauzo NMB makao makuu, Nehemiah alisema benki ya NMB yenye matawi 228,ATM mashine 715 ina mawakala 7000 wa NMB nchini kati yao 75 ni wa mkoa wa Shinyanga.

"Nawapongeza mawakala wa Shinyanga kwa kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa NMB,tunajivunia sana kuwa na mawakala waadilifu,tumeamua kuwafikia kwani tunajali wateja wetu kwani lengo letu ni kutoa huduma bora,salama na zenye ufanisi",alisema.

Alisema katika mafunzo hayo,miongoni mwa mada zilizotolewa ni pamoja na huduma zinazotolewa na NMB,Mawakala wa NMB,matumizi sahihi ya mashine za kutolea huduma,namna ya kupata mikopo na mbinu za kutambua na kudhibiti watakatishaji wa fedha 'watu wabaya'.

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI

Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Lembris Melusori akizungumza wakati wa kufungua mafunzo kwa Mawakala wa Benki ya NMB mkoa wa Shinyanga leo Alhamis Novemba 29,2018 katika ukumbi wa Empire Hotel mjini Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Lembris Melusori akizungumza wakati wa kufungua mafunzo kwa Mawakala wa Benki ya NMB mkoa wa Shinyanga.

Meneja Mahusiano na Wakala na Mauzo NMB makao makuu, Nehemiah Simba akizungumza wakati wa mafunzo hayo.

Meneja wa Uwakala Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Tabora,Ngarami Urassa akizungumza wakati wa mafunzo kwa mawakala wa NMB mkoa wa Shinyanga.

Mawakala wa NMB wakiwa ukumbini.

Mawakala wa NMB wakiwa ukumbini.

Mawakala wa NMB wakifuatilia mada ukumbini.

Meneja Mahusiano na Wakala na Mauzo NMB makao makuu, Nehemiah Simba akitoa mada kuhusu huduma zinazotolewa na benki ya NMB.

Meneja Mahusiano na Wakala na Mauzo NMB makao makuu, Nehemiah Simba akiendelea kutoa mada ukumbini.

Mawakala wa NMB wakifuatilia mada ukumbini.

Mafunzo yakiendelea.

Meneja wa Uwakala Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Tabora,Ngarami Urassa akitoa mada kuhusu huduma zinazotolewa na wakala wa NMB.

Mawakala wakiwa ukumbini.

Mafunzo yanaendelea.

Wakala wa NMB,Johari Ibrahimu akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo.

Meneja wa Uwakala Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Tabora,Ngarami Urassa akitoa mada wakati wa mafunzo hayo.

Afisa Mikopo benki ya NMB Manonga,Magreth Mbuduka akitoa ufafanuzi kuhusu masuala ya mikopo katika benki hiyo.

Mawakala wa NMB wakifuatilia mafunzo hayo.

Mafunzo yanaendelea.

Mafunzo yanaendelea.

Wakala wa NMB Kasiano Kicho akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo.

Meneja Mahusiano na Wakala na Mauzo NMB makao makuu, Nehemiah Simba akielezea kuhusu mambo ya kuzingatia katika biashara ya uwakala.

Afisa wa Benki ya NMB Richard Paul akielezea kuhusu huduma zinazotolewa na mawakala wa NMB .

Msimamizi wa Sheria,Taratibu na Kanuni benki ya NMB Kanda ya Tabora, Janeth Uiso akitoa mada jinsi ya kuzuia vitendo vya kutakatisha fedha na kuwezesha kifedha vikundi vya kigaidi.

Msimamizi wa Sheria,Taratibu na Kanuni benki ya NMB Kanda ya Tabora, Janeth Uiso akiwataka mawakala wa NMB kujiepusha na vitendo vya kutakatisha fedha.

Wakala wa NMB Joeli Fanueli Moshi akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo.

Afisa Mauzo/Huduma Mbadala benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Trifon Melkiory akitoa mada kuhusu matumizi ya mashine za kutolea huduma
Afisa Mauzo/Huduma Mbadala benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Trifon Melkiory akitoa mada kuhusu matumizi ya mashine za kutolea huduma.

Mawakala wa NMB wakifuatilia mada ukumbini.
Kushoto ni Meneja wa mauzo benki ya NMB Manonga, Thadei Mhengilolo na Afisa Mdhibiti ubora wa benki ya NMB,Timotheo Elias wakiwa ukumbini.
Wakala wa NMB,Juliana Shilatu wa mjini Shinyanga akiuliza swali wakati wa mafunzo hayo.

Wakala wa NMB,Magese Lusambagula Shagembe kutoka Solwa akiuliza swali wakati wa mafunzo hayo.

Afisa Mdhibiti ubora wa benki ya NMB,Timotheo Elias akizungumza wakati wa mafunzo hayo.

Wa pili kushoto ni Meneja Mahusiano na Wakala na Mauzo NMB makao makuu, Nehemiah Simba akimtangaza Juliana Shilatu (wa kwanza kulia) kuwa ni Wakala Bora wa NMB mkoa wa Shinyanga wakati wa kutangaza mawakala 10 bora wa NMB mkoa wa Shinyanga kwa mwaka 2018.

Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Lembris Melusori akimkabidhi zawadi ya cheti na fedha taslimu 100,000/- bi Juliana Shilatu aliyetangazwa kuwa Wakala bora wa NMB mkoa wa Shinyanga.

Wakala bora wa NMB mkoa wa Shinyanga,Juliana Shilatu akielezea mbinu mbalimbali anazotumia kufanya kazi ya uwakala.

Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Lembris Melusori akimkabidhi Saha Dachi and Company shilingi 75,000 mshindi wa nafasi ya pili ya wakala bora wa NMB.

Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Lembris Melusori akimkabidhi Amos Francis Ndila shilingi 60,000 mshindi wa nafasi ya tatu ya wakala bora wa NMB.

Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Lembris Melusori akimkabidhi Ngenda Mabula Hamis shilingi 50,000 mshindi wa nafasi ya nne ya wakala bora wa NMB.

Mwakilishi wa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi,Lembris Melusori akimkabidhi Hamis Ahmad mwakilishi wa Micatel Tanzania Ltd shilingi 50,000 mshindi wa nafasi ya tano ya wakala bora wa NMB.

Mawakala wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea ukumbini.


Mawakala wa NMB wakiwa ukumbini.

Mafunzo yanaendelea.

Picha ya pamoja baada ya mafunzo kumalizika.

Picha ya pamoja baada ya mafunzo kumalizika.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...