Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania amepatikana akiwa hai leo Jumanne Julai 2, 2019 Mombasa, Kenya.
Raphael anadaiwa kutekwa na watu hao Juni 24, 2019 akiwa na mke wake Veronica Kundya walizuiwa kwa mbele na kuwatolea silaha aina ya bastola na kuwachukua wote wawili kabla ya kumwachia mkewe na kuondoka na Raphael.
Veronica ameandika:
"Nipo hapa leo nikiwa na furaha kubwa sana sana kuushuhudia UKUU WA MUNGU 🙏🙏🙏. My Raphael AMEPATIKANA leo Mombasa na yupo salama, sina taarifa ingine zaidi ya hio ila hio pia INATOSHA sana kwangu 🙏🙏🙏 .
"Sina mengi ya kusema zaidi ya KUMSHUKURU MUNGU sana sana kwa kuwa yeye ni Mungu wa miujiza maana ametenda 🙏🙏🙏. Napenda KUWASHUKURU WOTE kwa moyo wangu wote kwa niaba ya familia yangu kwa sala na kujitoa kwenu kwa hali na mali kwenye kipindi hiki kigumu.
"Mimi na familia yangu tutaishi kutangaza ukuu wa Mungu 💃💃💃💃💃 Mungu azidi kutubariki sisi sote na familia zetu 🙏🙏🙏