Wednesday, April 16, 2025

NYONGO : SEKTA BINAFSI INA MCHANGO MKUBWA KWA TAIFA

Na Mwandishi Wetu, Mwanza 

NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Mipango na Uwekezaji, Stanislaus Nyongo, ametoa wito kwa sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika kupanga na kutekeleza mikakati mbalimbali ya nchi kwani zina mchango mkubwa kwa taifa.

Ameyasema hayo leo Aprili 16, 2025 wakati akifungua Mdahalo wa Kitaifa ulioandaliwa na Media Brains kwa kushirikiana na Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC)
wenye Mada Kuu ya Ubia wa Sekta ya umma na Sekta Binafsi katika Muktadha wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 akimwakilisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo.

Amesema ushiriki wa sekta binafsi ni muhimu katika maeneo mbalimbali kama vile sekta ya usafirishaji ikiwemo bandari, sekta ya nishati na usafiri wa umma pamoja na huduma za kijamii.

"Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia, Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuweka mazingira bora, wezeshi na shindani kwa sekta binafsi ili kufanya kazi kwa ufanisi.

"Na ili tufanikiwe katika jambo hili, lazima tujipange na kuandaa midahalo kama hii ili kubadilisha fikra zetu na kujipanga vizuri. Kwa hiyo nitoe wito kwa sekta binafsi kushiriki kikamilifu katika kupanga na kutekeleza mikakati ya nchi," amesema.

Amefafanua kuwa, katika kuandaa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, sekta binafsi imepewa kipaumbele katika kuchangia kwenye Dira hiyo.

"Mdahalo huu umekuja wakati ambapo Taifa letu limeingia katika hatua muhimu ya kupanga mustakabali wa Maendeleo yake kwa miongo ijayo kupitia maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050.

"Tunampongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu kutumia wananchi kukusanya maoni ya Dira hii. Tunatambua kuwa safari ya maendeleo ni endelevu kwa kuwa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 iko katika hatua za utekelezaji na serikali imeanza katika maandalizi ya Dira mpya," amesema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa PPPC, David Kafulila amesema uchumi wa nchi hauwezi kujengwa bila kuzishirikisha sekta binafsi.

Amesema dunia nzima inafanya ubia na masuala hayo yamekuwa ni ajenda kubwa kwenye mijadala ya uchumi duniani.

"Duniani kote imekuwa ni ngumu kwa serikali hizi kutekeleza matarajio ya wananchi kwa kutumia kodi na mikopo... na ushahidi wake ni takwimu za hali ya uchumi wa dunia. Uchumi wa dunia kufika mwaka jana Novemba ulikuwa takribani Trilioni Dola za Marekani 115, lakini deni la serikali zote duniani ilikuwa takribani Trilioni Dola za Marekani 102.

"Deni la dunia yote kwa maana ya serikali, sekta binafsi na kaya ilikuwa ni zaidi ya Dola Trilioni 315... tafsiri yake ni kwamba uchumi wa dunia unaendeshwa kwa mikopo," amesema.

Kafulila amefafanua kuwa uchumi wa Dunia zaidi ya asilimia 90 ni mikopo ambapo kwenye upande wa Afrika mikopo ya serikali kwa uchumi ni takribani asilimia 67 na kwa Tanzania ni asilimia 47.

"Unaweza ukaona pamoja na maneno kwamba deni la serikali linaongezeka, lakini utaona Tanzania kuna utofauti mkubwa, na hii ni kielelezo kuwa serikali ya awamu ya sita inasimamia vizuri hali ya uchumi," amesema.

Amebainisha kuwa mdahalo huo ni sehemu ya kujenga uelewa kwa wananchi kuhusu masuala ya ubia na kuweza kutafakari kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

"Hii ni fursa kubwa ya kujadili namna ambavyo tunataka kuwa na uchumi wa nchi yetu kwenda mwaka 2050. Lazima kufungua uchumi kwa kuongeza ubia sekta za ndani na nje kushiriki katika kujenga uchumi na serikali ipo tayari kushirikiana na sekta binafsi katika kuimarisha uchumi wa nchi," ameongeza.

Awali akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Chagu Nghoma, kuna fursa nyingi ya uwekezaji za kukuza uchumi katika mkoa huo, ikiwamo sekta ya uchumi wa buluu ukilenga ufugaji wa samaki na shughuli nyingine zinazofanyika katika Ziwa Victoria.

Amesema pamoja na hayo pia kuna maeneo mengi yanayofaa kwa ufugaji wa mifungo kama vile ng'ombe, mbuzi.

Ameeleza kuwa kuhusu uchumi wa buluu kuna ufugaji wa samaki ambayo inahitaji kwa kiasi kikubwa uwekezaji wa viwanda na kuwekeza katika chakula cha samaki, pia viwanda vya nyama vinahitajika zaidi.

"Mkoa wa Mwanza una maeneo mengi ya uwekezaji na upo tayari kuyatoa maeneo hayo kwa watu binafsi na serikali. Uchumi wa mtu unaanza na mtu binafsi, ni lazima kufikiria nini unataka kufanya katika kuboresha uchumi binafsi na nchi," amesema.


DKT. JINGU ATOA MKONO WA PASAKA KWA WAZEE NUNGE


πŸ“Œ Akagua Huduma Makazi ya Wazee Nunge - Kigamboni Dar es Salaam 

πŸ“Œ Asikiliza changamoto za watumishi

Na WMJJWM- Kigamboni Dar eS Salaam 

Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu ametoa mkono wa Pasaka kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa wazee wanaoishi katika Makazi ya Wazee Nunge Kigamboni Dar es Salaam. 

Akizungumza katika Makazi hayo Aprili 16, 2025 Dkt. Jingu amesema  Serikali ya awamu ya sita ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan inawathamini sana wazee, inawajali na ndio maana iko tayari kuwatunza na kuhakikisha maisha yao yanakuwa bora na yenye usalama.

Amesema Serikali itaendelea kuwekeza katika kuwahudumia wazee wasiojiweza hasa katika kuwapatia huduma muhimu za malazi, chakula na huduma za Afya ili kuwaenzi kwa mchango wao kwa maendeleo ya taifa.

"Mhe. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anawapenda na kuwajali sana ndio maana mnaona huduma zote mnapatiwa kwa wakati ili kuenzi mchango wenu kwa taifa lenu mlioutoa katika sekta mbalimbali" amesema Dkt. Jingu

Akisoma taarifa ya Makazi ya Wazee Nunge Afisa Mfawidhi wa Makao hayo Jacklina Kanyamwenge amesema Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imekuwa ikitoa huduma zote muhimu kwa wazee katika Makazi hayo kila mwezi pamoja na kuboresha miundo mbinu mbalimbali iliyopo ili kuendelea kutoa huduma kwa wazee hao.

"Watumishi tunashukuru kwa kupatiwa mafunzo ya Afya ya Akili na Msaada wa Kisaikolojia na Kijamii kuongeza weledi wa kuwahudumia Wazee wenye shida ya saikoloji,  afya ya akili na wenye mahitaji maalum ya kihisia na uzee" amesema Jackilina.

Akizungumza kwa niaba ya Wazee  Katibu wa Wazee hao Mzee Mussa Juma Muna ameishukuru  Serikali inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa upendo mkubwa kwao kwa kuhakikisha kila mmoja wao anapata mahitaji yote muhimu na kikubwa zaidi Bima za Afya ambazo zinawapa matibabu  na yenye viwango vya juu. 

 

MSIMU WA NNE MBIO ZA RUN FOR BINTI KUFANYIKA MEI 24, 2025 DSM


SHIRIKA lisilo la kiserikali la Smile for Community (S4C) kwa kushirikiana na LSF leo limetangaza msimu wa nne wa mbio za Run for Binti zinazotarajiwa kufanyika tarehe 24 Mei 2025 katika viwanja vya Farasi,Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Mbio hizi hufanyika kila mwaka kwa lengo la kuweka nguvu na rasilimali za pamoja katika kuwawezesha watoto wa kike kupata haki ya elimu na afya ya uzazi, kwa kuhakikisha wanapata hedhi salama na mazingira bora ya kusoma.

Kupitia Run for Binti ya mwaka jana, wanafunzi wa shule za sekondari Nanyamba na Chawi katika Halmashauri ya Mji Nanyamba walinufaika kwa kujengewa vyoo bora na vya kisasa, huku wanafunzi wa kike wakipata taulo za kike kwa ajili ya kuwalinda kiafya na kuwawezesha kuhudhuria vipindi bila kukosa.

Akizungumza wakati wa kutangaza mbio hizo, Afisa Mtendaji Mkuu wa LSF, Lulu Ng'wanakilala amesema "Katika utekelezaji wa mradi wetu wa Sauti ya Mwanamke nchini, tumeona dhahiri kwamba wasichana na mabinti wanakumbana na vizuizi vinavyozuilika na visivyoweza kuzuilika katika kupata elimu, huduma za afya, na haki zao za msingi. Ndiyo maana ushirikiano wetu na Smile for Community pamoja na wadau mbalimbali ni muhimu sana. Kupitia mbio hizi, tunapunguza vikwazo na kutengeneza njia mpya zitakazochochea jamii yenye usawa hususan kwa mtoto wa kike."

Aidha amesema mbio hizo zimeendelea kuwa jukwaa la kuwaleta wadau pamoja na kuweka nguvu ya pamoja kutatua changamoto za watoto wa kike.

"Mwaka jana, zaidi ya wanafunzi 2,500 walinufaika kupitia ujenzi na ukarabati wa vyoo, usambazaji wa taulo za kike, upandaji wa miti mashuleni na utoaji wa elimu ya hedhi salama na haki za mtoto wa kike". Amesema

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Smile for Community, Bi Flora Njelekela amesema "Smile for Community kwa kushirikiana na LSF tuna furaha kubwa kutangaza kuwa mbio za msimu huu wa nne zitafanyika tarehe 24 Mei 2025. Wakimbiaji watahusika katika mbio za KM 21, KM 10, KM 5."

Bi Njelekela ameongeza kuwa, "Lengo letu mwaka huu ni kufikia watoto wa kike 1,000 kutoka shule tatu, hasa mikoa ya Geita na Dar es Salaam. Katika tukio la makabidhiano, msaada utakao tolewa utahusisha: Usambazaji wa taulo za kike 7,000, Ujenzi wa vyoo bora mashuleni, Upandaji wa miti 500 katika shule tatu kwa ajili ya hifadhi ya mazingira, Elimu ya ukatili wa kijinsia na mbinu za kuzuia na kushughulikia matukio hayo, Elimu ya fedha (financial literacy) na Uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi ya kupikia (clean cooking), lakini pia Shughuli za mazingira zitafanyika Ukonga, Dar es Salaam na shughuli za afya ya hedhi, elimu ya fedha na miundombinu Geita."

CCM Inafurahia Kususa kwa Vyama Vya Upinzani - Semu

CCM Inafurahia Kususa kwa Vyama Vya Upinzani - Semu


Kiongozi wa Chama Cha ACT Wazalendo Doroth Semu ameeleza kuwa Chama hicho kitashiriki kikamilifu uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba mwaka huu kwenye nafasi zote za Udiwani, Ubunge, Uwakilishi na Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ule wa Zanzibar.


Akizungumza na wanahabari leo Aprili 16, 2025, Vuga visiwani Zanzibar, Semu ameeleza kuwa maamuzi hayo yametokana na tafakuri waliyoifanya, wakibaini kuwa kususia uchaguzi huo Mkuu kutatoa fursa ya kuimarisha hujuma zaidi za dola dhidi ya Demokrasia, akisema uchaguzi huu utakuwa sehemu ya mapambano dhidi ya mageuzi ya mifumo ya uchaguzi nchini.


"Baada ya tafakuri ya kina, Chama chetu ACT Wazalendo kimejiridhisha kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kinahitaji na kwa hakika kitafurahia iwapo vyama makini vya upinzani vitasusia uchaguzi ili kiendeleze hujuma kwa demokrasia nchini. ACT Wazalendo tumegoma kutoa fursa hiyo kwa CCM.


"Uchambuzi wetu pia unaonesha kuwa katika nchi mbalimbali duniani, kususia uchaguzi kumeimarisha hujuma zaidi za dola dhidi ya demokrasia kwa kutoa mwanya wa kupora kwa urahisi sauti ya wananchi. Mifano ya hili inaweza kupatikana kwenye nchi za Kenya (2017), Misri (2018), Ivory Coast (2020), Zanzibar (2015), Venezuela (2018)." Amesema Doroth Semu.


Aidha katika hotuba yake, Semu ameeleza kuwa ACT Wazalendo inashiriki kwenye uchaguzi huo kutokana na kubaini kuwa CCM imeshindwa kuwakomboa watanzania kiuchumi, kisiasa na Kijamii, hivyo ushiriki wao ni jukwaa la vijana, wakulima na wafanyakazi wanaonyonywa, wananchi wanaokandamizwa na wale wanaopuuzwa na kuonewa katika kuiondoa @ccmtanzania madarakani.


Katika hatua nyingine, Chama hicho kimeeleza kuwa bado kinaendeleza mapambano ya kupigania mageuzi ya mifumo ya uchaguzu nchini, akieleza kuwa Viongozi na wanachama wa Chama hicho wapo tayari kulipa gharama za mapambano hayo bila ya kukata tamaa mpaka pale kutakapokuwa na chaguzi za haki, uhuru na zenye kuaminika.

Jambo TV

🌸🐣 PENDEZA KIPASAKA !! MZIGO MPYA UMETUA! πŸ›οΈβœ¨

🌸🐣 PENDEZA KIPASAKA !! MZIGO MPYA UMETUA! πŸ›οΈβœ¨

Sikukuu ya Pasaka imefika! Madera Fashion tunakukaribisha kwa mavazi mapya ya kisasa! 

Tumedhamiria ung'are na kupendeza kipindi hiki maalum na siku zote!

πŸ‘— Magauni ya kisasa kwa wanawake – kwa mitoko ya kanisani na sherehe
πŸŽ’ Nguo mpya za watoto (kike & kiume) – zenye rangi, ubora na mvuto
πŸ‘• Suruali, Tisheti, na Mashati ya wanaume – smart casual & classic styles
πŸ‘œ Mikoba mipya na vipochi vya kisasa – kwa kumalizia muonekano wako

πŸ§• Pia tunazo abaya, Vijora na madera  yenye hadhi!

🌍 Mzigo mpya umetoka: Oman, China, India, Uganda, na Tanzania.

πŸŽ‰ Usikubali kupitwa na mitindo hii mipya – kwa bei nafuu na ubora wa kipekee!

πŸ“ Tupo: Jirani na Katamba Lodge, hatua chache kutoka Daraja la Upongoji – Ndala, Shinyanga Mjini
πŸ“ž Wasiliana nasi sasa: 0652 882 061

🌟 MADERA FASHION – Pasaka hii, pendeza kwa mtindo wa tofauti!


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...