Wednesday, February 27, 2019

Je Unajua Kwanini Wazungu Wanasema Life Begins at 40 Years Old? Majibu Haya Hapa

Watu wengi hawajui kwa nini wazungu huwa wanasema LIFE BEGINS AT 40. Yaani maisha yako ya kweli yataanza ukifika umri wa Miaka 40. Wakati ambapo unatakiwa uwe na elimu uliyoihitaji.. Uwe na familia yako tayari.. Uwe na kwako tayari siyo umepanga bado.. Uwe na usafiri binafsi.. Uwe na kitu chako cha kukuingizia pesa na si kutegemea ajira peke yake. At 40!!

At 40 inabidi uwe unaishi. Siyo ndo unaanza kujaribu hiki na kile. At 40 inabidi uwe unasomesha zaidi kuliko kusoma wewe japo kuongeza maarifa ni vizuri.
At 40 unatakiwa uwe umeshapata exposure kwa kusafiri huku na kule dunia hii kujua wengine walioendelea zaidi wanaishi vipi na wewe ufanyeje?
At 40 utakuwa bado unaomba nauli kwa baba na mama kwani?

Sasa hivi vitu haviji ukiwa upoupo tu hutafuti fursa za kukusaidia kuwa na maisha tofauti upo tu una LIKE kila kitu facebook na Instagram unatuma tu picha za ajali za mabasi zikikosekana unatuma za migomo ya madereva mgomo ukiisha unatuma za mafuriko kama mvua zimeisha unatuma picha za Lowassa yaani umekuwa mtumwa wa simu. Ikikosa network unalalamikia kampuni ya simu utafikiri hiyo network unafanyia kitu cha maana. Gallery yako imejaa vitu vya ajabuajabu tu. Havikufikishi popote na umri unazidi kwenda unazidi kusogea miaka 40 hivi hivi. Maisha ya kweli yataanza ukiwa na miaka 40. Wakati ambapo watoto wako hawatakula LIKES zako za instagram bali wanahitaji chakula. Wanahitaji ada. Wanahitaji maisha bora. Wewe inasubiri maisha bora CCM ndo wakupe. Wasipokupa unataka UKAWA waje wakupe ukiwa umekaa Instagram unaLIKE picha za Wema Sepetu. Umeshajua wema akifika miaka 40 atakuwaje? Ulishajiuliza wanamuziki waliovuma miaka 15 iliyopita wakiwa na umri wa miaka 25 hivi au 30 wakati huo wana miaka mingapi na wako wapi sasa hivi. You see? Unayemfuatilia kila siku kavaaje kaamkaje katembea na nani hakusaidii kuwa na maisha mazuri. Maisha bora hayaji ukiwa unafatilia nyimbo gani zimetoka udownload. Maisha bora hayaji kwa KU-ENTERTAIN brain yako bali kwa kuifikirisha akili na kufanya mambo ambayo wachache tu ndo wanafanya.

Kwani wanasoka wangapi wako kama Beckham
Wnamuziki wangapi wako kama Kirk Franklin
Wacheza Tennis wangapu wako kama Roger Federer? Unadhani amekuwa champion akiwa amekaa na TECNO chumbani ana comment kuhusu migomo? No. Alikuwa ana-hussle wakati wengine wanachat.

Seriously. Diamond unayemfollow anafanya kazi hivyo. Anatoka studio saa saba usikuwewe uko kwenye page yake unaLIKE. Huwezi kuona kuwa uko tofauti. Anaandaa maisha akifika miaka 40 awe na kila kitu wewe utakuwa unalalamikia network ya tigo tu na kutuma picha  za sijui gari limegonga treni. Kwa hiyo wewe ndo NIPASHE sasa hivi?

Anyway. Kuwa serious na maisha yako angalau basi kwa ajili ya watoto wako na wajukuu zako. Aise huyu mzazi wetu alifanya jambo la maana. Au unadhani watazikuta hizo comments na LIKES zako? No. Wanapaswa wakute nyumba, viwanja, account za benki zinazopumua. Siyo account inaingiaga mshahara tu halafu by tarehe 10 iko empty ushakomba kila kitu!!!! Wanatakiwa wakute assets za maana angalau. Siyo rundo la CD za bongo movie ambazo hazikusaidii wewe wala wao.

Siku zilizobaki kumaliza mwaka huu umeeka mikakati gani kuweka msingi wa maisha tofauti sana na kuhakikisha ufikapo umri wa miaka 40?
Au bado unategemea mshahara wa laki 8 (tena hapo kabla ya makato) uje ubadili maisha yako).
Kwa waajiriwa, Microsoft ya Bill Gates inapunguza wafanyakazi 800. Kama ulikuwa hujui. Unadhani kampuni yako ndo utakaa hapo milele?
Be careful my friend.

" KUZALIWA MASIKINI SI KOSA BUT KUFA MASIKINI NI DHAMBI"
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...