Sunday, February 24, 2019
Namna Sahihi ya Kupunguza Matumizi ya Mafuta ya Gari yako
Matumizi ya gari ni mojawapo ya matumizi makubwa kwa familia nyingi hasa zinazoishi mjini.
Inasemekana kwa wale wanaomiliki magari kuwa inawezekana nyumbani kukakosekana baadhi ya mahitaji mengine muhimu lakini gari ni lazima liwekwe mafuta na litembee. Je kuna ukweli wowote? Jaribu kufanya utafiti utaona. Watu wanalalamika uchumi mbaya lakini magari yanatembea.
Hii inamaanisha kuwa kwa maisha ya kisasa tunayoishi gari limekuwa mojawapo ya nyenzo muhimu na ya lazima. Lakini pia ni mojawapo ya kitu ambacho kinakula fedha nyingi toka mifukoni mwetu.
Kila mtu anatakiwa kutafuta jinsi ya kupunguza matumizi yanayotokana na gari. Mafuta ni sehemu mojawapo ya matumizi makubwa katika kumiliki na kuendesha gari.
Katika mada hii tunaangalia mbinu za kupunguza matumizi ya mafuta ya gari hivyo kuboresha uchumi wa wamiliki.
Mbinu za Uendeshaji Zinazosaidia Kupunguza Matumizi ya Mafuta ya Gari
Madereva wengi wanaendesha magari kwa namna ambayo inasababisha injini kula mafuta mengi sana. Kama utaendesha gari kwa kufuata mbinu hizi tu unaweza kupunguza matumizi yako ya mfuta kwa asilimia 10-20.
Zingatia Mwendo Kasi Sahihi
Kila gari linatumia mafuta katika namna tofauti, lakini katika spidi juu ya 90 Km/Saa mpaka 100 Km/Saa gari lolote huwa linatumia mafuta kidogo kuliko likiwa katika spidi nyingine. Kwa mjini huwezi kufikia spidi hii lakini jitahidi kuendesha juu ya 30 Km/Saa.
Pia fahamu kuwa spidi ikizidi 50Km/Saa mafuta yatatumika zaidi kwa kuwa gari linahitaji nguvu zaidi kushindana ukinzani wa hewa.
Zingatia: Zuia mwendo kasi kati ya 60-90 Km/Saa kwakuwa hutumia mafuta mengi
Usiongeze Mwendo Kwa Haraka
Kukanyaga mafuta kwa haraka ilikuongeza spidi kunachangia ulaji mkubwa wa mafuta. Unashauriwa kukanyaga mafuta taratibu unapoongeza mwendo kasi.
Unaweza ukasikiliza gari lako wakati unaendesha,ukisikia sauti kubwa unapoongeza mwendo ujue unachoma mafuta mengi na hivyo unaongeza gharama.
Usipunguze Mwendo Kwa Haraka- Acha Ukanyagaji Breki za Kushitukiza
Kama ilivyo katika kuongeza mwendo,unatakiwa kupunguza mwendo taratibu. Hakikisha kuna umbali wa kutosha kati yako na gari la mbele yako vinginevyo utajikuta ni lazima ukanyage breki kwa haraka na kwa kushitukiza ambako kunasababisha injini kula mafuta zaidi.
Kutobeba Mizigo Mizito Kwenye Gari
Uzito unapoongezeka katika gari hufanya injini kutumia nguvu nyingi kusukuma gari na hivyo kuhitaji mafuta mengi zaidi. Punguza mizigo isiyo ya lazima katika gari ukiwa unaendesha.
Kutoacha Gari Likiwa Linawaka Bila Kutembea
Utafiti unaonesha kuwa kwa wastani gari linatumia lita zipatazo 2 kwa saa kama likiwa linawaka bila kutembea. Sababu ni kuwa katika hali hii injini huwa inatembea na inahitaji mafuta kuzunguka.
Kama gari halitembei unashauriwa kuzima injini ili kupunguza matumizi ya mafuta.
Zingatia: Usiache gari likiwa linawaka zaidi ya dakika 1 bila kutembea
Zima Kiyoyozi (AC) Katika Mwendo Mdogo
Katika mwendo kasi wa chini ya 90 km/saa zima kiyoyozi na fungua madirisha. Kiyoyozi kinazungushwa na injini hivyo kutumia mafuta zaidi. Kukiwa unaenda spidi zaidi ya 90km/saa unatatumia mafuta kidogo ukifunga madirisha na kuwasha kiyoyozi.
Endesha Gari Likiwa na Matairi Yenye Upepo wa Kutosha
Matairi yenye upepo mdogo yanasababisha kuongezeka kwa eneo linalokanyaga barabara na hivyo nguvu nyingi inahitajika kusukuma gari.
Hakikisha matairi ya gari lako yana upepo katika viwango sahihi.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...