Friday, August 31, 2018

Mwanafunzi Mwingine Apigwa na Mwalimu wake Hadi Kupoteza Fahamu

Takribani wanafunzi 100 wa kidato cha tano na sita  shule ya sekondari Kalangalala mjini Geita   wameandamana kwenda ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Geita kupinga kitendo cha mwenzao kupigwa na mwalimu hadi kupoteza fahamu.

Wanafunzi hao leo Ijumaa Agosti 31, 2018 wametembea umbali wa kilomita 3 kwenda kwa mkuu huyo wa wilaya, Josephat Maganga.

Mwanafunzi huyo Jonathan Mkono amepigwa na mwalimu waliyemtaja kwa jina moja la Lawi jana Alhamisi Agosti 30, 2018  kwa kosa la kuingia bwenini wakati vipindi vikiendelea.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake mbele ya mkuu huyo wa wilaya na kamati ya ulinzi na usalama, mwanafunzi, Aron Mathias amesema hali ya mwenzao aliyelazwa hospitali ya mkoa si nzuri, kwamba hawezi kuzungumza, kukaa wala kusimama.

"Huyu ni kiongozi alikua anasimamia usafi alivyomaliza alirudi bwenini kuchukua vifaa lakini mwalimu Lawi alimwadhibu na sio kwa fimbo alimpiga makofi na marungu," amesema.

Mwanafunzi huyo amedai baada ya kipigo mwenzao alipoteza fahamu na baadaye alizinduka lakini hali yake ilikuwa mbaya na usiku walilazimika kukodi pikipiki kumpeleka hospitali.

"Tulimpeleka hospitali akiwa mahututi tulipofika daktari alikataa kumpokea akishinikiza kupewa taarifa ya polisi , tulivyoipata ndio wakaanza kumtibu majereha yake," amesema.

Kwa upande wake Maganga amewasikiliza na kuwataka kurudi shule ambako ataenda na kufanya kikao na wanafunzi pamoja na walimu.


TAZAMA VIDEO MPYA YA ROSA REE HAPA CHINI ALIYOTOA LEO..
HAYO MAUNO SI YA NCHI HII:



Kwa Sasa Sihitaji Msaada Wowote wa Watanzania:-Wastara

Msanii wa maigizo Wastara Juma ambae hapo awali alikuwa akikaririwa kuomba msaada wa watanzania ili kuweza kufanikisha maswala ya matibabu nje ya nchi amefunguka na kusema kuwa kwa sasa hana mahitahi yoyote ya msaada kutoka watanzania ila maombi yao tu kutokana na magonjwa anayoomba. Wastara ambae alirudi kutoka nchini India kwa matatibabu na msaada huo alipatiwa na watu mbalimbali akiwepo rais wa tanzania, anasema kuwa anaomba watanzania wamuombee sana kwa sababu kwa sasa atakuwa akitumia dawa maisha yake yote. Kwa sasa kwakweli sihitaji msaada wowote kwa watanzania zaidi ya maombi yao ili nizidi kuendelea vizuri,kinachonisumbua kwa sasa ni matatizo ya mgogo na kichwa kuna dawa nimeandikiwa na daktari maisha yangu yote.  

The post Kwa Sasa Sihitaji Msaada Wowote wa Watanzania:-Wastara appeared first on Ghafla!Tanzania.


Source

VIDEO: Movie ya Bahasha yatikisa Dar Dude afunguka kwanini Bongo Movie ilitetereka

Mwigizaji wa Bongo Movie Dude amefunguka kuhusiana na Movie ya Bahasha ambayo ilizinduliwa Mlimani City lakini ameweza kufunguka kuhusiana na tasinia ya Filamu kwa ujumla na kueleza sababu hasa zilizopelekea tasnia ya Bongo Movie kutetereka. Dude amefunguka hayo wakati anapiga stori na Bongo Five na kueleza haya:- By Ally Juma

The post VIDEO: Movie ya Bahasha yatikisa Dar Dude afunguka kwanini Bongo Movie ilitetereka appeared first on Bongo5.com.


Source

Thursday, August 30, 2018

Tanzanian wins major UN award entrepreneurship

A Tanzanian lady, Lucy Odiwa, has emerged the winner of the Women Micro-Entrepreneurs Showcase aimedat helping to achieve Sustainable Development Goals (SDG).
Source

Bila Mimi Hakuna Ebitoke :-Mkali Wenu.

Msanii wa vichekesho Mkali wenu ambae  alipata umaarufu kwake kupitia mitandao ya kijamii amefunguka na kusema kuwa bila uwepo wake basi kusingekuwa na ebitoke anaefahamika katika tasnia ya sanii uapnde wa vichekesho. Ebitoke na Mkali wenu hawajajulikana kuna nini kati yao kwa sababu ebitoke aliwahi kumkana mwenzake hadharani ilhali wawili hao waliwahi kufanya kazi katikakundi moja hapo awali kabla hawajatengana . Hata hivyo Mkali Wenu anasema kuwa kama asingezaliwa na kuamua kuwa mwigizaj basi asingekuwepo ebitoke kama alivyo sasa hivi, ‘kama mimi nisingezaliwa na kuamua kuingi katika vichekesho basi hasingefahamika Ebitoke, Bwana mjeshi wala Mama ashura, kwa sababu hawa wamekuja baada ya mimi kuwa na clip zangu na kuzitambulisha katika kundi la timamu na ndipo wao walipotambulika kupitia kazi zangu hizo.’

The post Bila Mimi Hakuna Ebitoke :-Mkali Wenu. appeared first on Ghafla!Tanzania.


Source

27 Tanzanians arrested in Mombasa crackdown on immigrants

Twenty seven Tanzanians will be deported following their arrest in Mombasa as part of the nationwide crackdown on illegal immigrants.
Source

City pupils administered with bilharzia fighting vaccination

Over 600,000 pupils in 708 public and private schools in the city are set to receive vaccine against bilharzia.
Source

Happy homecoming as Enyimba snatch dramatic win

Wasiu Alalade scored in stoppage time to give Enyimba of Nigeria a 1-0 homecoming victory over CARA of Congo Brazzaville Wednesday and a CAF Confederation Cup quarter-finals place.
Source

MKUU MPYA WA WILAYA YA BAGAMOYO ZAINABU KAWAWA AFUNGUA RASMI MAFUNZO YA AWALI YA JESHI LA AKIBA KWA VIJANA 183 CHALINZE


1
  Mkuu mpya wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa wa kati kati akirukaruka mara baada ya kufungua mafunzo rasmi ya jeshi la akiba kwa vijana wapatao 183 hawapo pichani  kutoka kata ya  Bwilingu katika halmashauri ya Chalinze pembeni yake kulia ni Mshauri wa jeshi la akiba Wilayani Bagamoyo Maj Chinguku.
2
Mkuu mpya wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa wa kati kati akirukaruka mara baada ya kufungua mafunzo rasmi ya jeshi la akiba kwa vijana wapatao 183 hawapo pichani  kutoka kata ya  Bwilingu katika halmashauri ya Chalinze pembeni yake kulia ni Mshauri wa jeshi la akiba Wilayani Bagamoyo Maj Chinguku.
3
Mkuu mpya wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Rashid Kawawa kulia akiwa na  Mshauri wa jeshi la akiba wilayani humo wa kushoto Maj Chinguku wakati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa mafunzo wa jeshi la akiba kwa vijana wapatao 183  ambayo yamefanyika katika  kata ya Bwilingu halmashauri ya Chalinze.

VICTOR MASANGU,  CHALINZE

MKUU mpya wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa amewataka vijana ambao wanahitimu  mafunzo ya jeshi la akiba  kuhakikisha wanakuwa wazalendo na nchi yao na kuachana kabisa na vitendo vya kujiingiza katika matukio ya kihalifu na badala yake wahakikishe wanazingatia sheria na taratibu zote zilizowekwa  kwa lengo la kuweza kulinda hali ya ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao.

Kauli hiyo aliitoa wakati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa mafunzo  ya awali ya  jeshi la akiba ambayo yamefanyika katika kata ya Bwilingu  na kuwajumusiha vipana wapatao 183 kutoka  katika halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

Mkuu huyo pia aliwahimiza vijana hao kuhakikisha wanakuwa na nidhamu ya hali ya juu katika kipindi chote cha mafunzo hayo ya kijeshi na kuzingatia maelekezo ambayo wanapatiwa na walimu wao kwa lengo la kuweza kujifunza   mbinu mbali mbali ambazo zitaweza kuwa ni mkombozi mkubwa katika kulilinda Taifa la Tanzania na kuweza kukabiliana na wimbi la matukio ya uhalifu.

"Napenda kuchukua fursa hii  kuwapongeza vijana ambao mmeweza kujitokeza katika mafunzo haya ya jeshi la akiba,lakini kitu kikukbwa ninawaomba muwe wazalendo na nchi yenu kwa kuhakikisha mnazingatia sheria na taratibu za nchi ikiwa ni sambamba na kuyatumia vizuri mafunzo mliyopatiwa kwa maslahi ya nchi na sio vinginevyo,"alisema

Kwa upande wake Mshauri wa jeshi la akiba  Wilayani Bagamoyo Maj Chinguku alibainisha kuwa  mafunzo hayo yatakuwa ya miezi minne na nusu ambapo vijana hao  wataweza kujifunza mbinu mbali mbali za kivita ambazo zitaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa maslahi ya Taifa.

"Katika mafunzo haya vijana ambao walijitokeza hapo awali walikuwa ni 211 lakini baadhi yao wameshindwa kuendelea kutokana na sababu mbali mbali hivyo ambao wanaendelea kwa sasa na  ni vijana wapatao 183 ambao wametokea katika kata ya bwilingu, ambapo wataweza kupata mafunzo mbali mbali ya kijenzi kwa kipindi cha muda wa wiki 18 alisema Chinguku"

Naye Diwani wa  kata ya Bwilingu Lucas Lufundo alisema  kwamba mafunzo hayo yataweza kuwasaidia vijana kwa kiasi kikubwa kudumisha hali ya ulinzi na usalama katika maeneo mbali mbali  na kwamba kutaweza kupunguza wimbi la vijana wengi  ambao walikuwa wanakaa  vijiweni bila ya kujishughulisha na kazi pamoja na kupunguza na changamoto ya wimbi la  uhalifu.

Source

Kiba kuongeza nguvu Coastal Union

Mshambuliaji mpya wa klabu ya Coastal Union, Ali Kiba Saleh amejiunga na kambi ya timu hiyo huko Tanga.

Kiba anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo kitakachocheza dhidi ya KMC Jumamosi ya Septemba 1 saa katika dimba la Mkwakwani Tanga.

Kiba ambaye amejizolea umaarufu mkubwa zaidi akiwa kama Mwanamuziki kutokana na kufanya vema ikiwa ni pamoja na kutwaa tuzo ya Msanii Bora wa Afrika mwaka 2016, alisaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo.

Mchezaji huyo alikosa mechi mbili za mwanzo kutokana na kukabiliwa na majukumu mengine ambapo alikuwa nchini Canada kwa ajili ya kazi za kimuziki.

VIDEO: Mobetto afunguka sakata la kutukanwa mitandaoni


"Mitandao ya kijamii imenikuza kama brand, mwanamitindo, mfanya biashara na pia ni mmoja ya watu ambao ninapata changamoto nyingi sana kwenye mitandao, vijana wengi hawajui matumizi mazuri ya mitandao mwingine anaamua tu nimtukane kwasababu nina bifu nae lakini siku hizi kuna sheria hivyo vijana watumie vizuri mtandao" Hamisa Mobetto

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.......USISAHAU KUSUBSCRIBE

Uingereza yaanza harakati zake za kibiashara barani Afrika waziri Mkuu atua Kenya

Theresa May na mtihani wa Uingereza kuboresha biashara na Afrika baada ya kujitenga na Umoja wa Ulaya,nchin ya Uingereza ina uhusiano wa kihistoria na mataifa mengi ya Afrika. Uhusiano huo bado unaendelea kuwa na maana, lakini kitu kimoja ambacho Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amekutana nacho katika ziara yake ya Afrika ni kuwa nchi …

The post Uingereza yaanza harakati zake za kibiashara barani Afrika waziri Mkuu atua Kenya appeared first on Bongo5.com.


Source

Gari ya Peter Msechu Balaa!!! “Kila Nikitafuna inajizima”


Staa kutokea kwenye muziki wa Bongo FlevaPeter Msechu ametoa kali ya mwaka Gari ya Peter Msechu balaa!!! "kila nikitafuna inajizima"  kuwaacha mashabiki wake midomo wazi baada ya kumnunulia mke wake gari aina ya Toyota Porte mwaka 2015.

Peter Msechu ametumia ukurasa wake wa instagram na kusema kuwa alimnunulia mke wake gari hilo kutokana na marafiki wa mke wake kumnyali kwa kukosa gari, hivyo akaona sio vibaya kumnunulia usafiri na yeye pia.

Peter Msechu ameandika "Gari langu la tatu mwaka 2015 nilimnunulia Mama Lolo gari hii baada ya kuona mashost zake wanamnyali sana, ila sijui Mama Lolo aligongesha wapi maana lilianza  kuwa bovu balaa ugonjwa wake kila hospitali walishindwa"

"Kuna muda lilikuwa linawasha wiper tu bila sababu mara unashangaa honi inajipiga tu yenyewe bila kubonyezwa Kuna siku ndio nilichoka kabisa ilikuwa haina mafuta kabisa taa imewaka na nikawa sina hela ya mafuta ila nikapita mahali kuchukua chips nilie kwenye gari"

"Kumbe akamaind kila nikitafuna inajizima nisipotafuna inawaka hii ndio gari pekee ambayo imetoka Japan haikuwahi kuzima taa ya mafuta"

'Taa ya mafuta ilikuwa inawaka mpaka dashboard inakua ya moto  vitu kama mayai ya mjusi kuyakuta katikati ya siti za kukalia ilikuwa kawaida tu #KISIRANI story ya gari la nne na la tano zitakujia mnamo kesho jioni kuanzia saa 1 jioni ita wenzako wakae tayari"

Source

UTATA WATAWALA KIFO CHA MTAWA BUGANDO...MAPYA YAIBUKA

Suala kifo cha Mkurugenzi wa Fedha na Mipango wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando (BMC), Mtawa Suzan Bartholomew, limechukua sura mpya baada ya taarifa kusambazwa zikieleza huenda aliuawa.

Juzi, baada ya taarifa kwamba Mtawa huyo alijiua kwa kujirusha kutoka ghorofa ya pili kusambaa, kwenye mitandao ya jamii ulianza kusambaa ujumbe uliokuwa ukieleza kuna uwezekano mtawa huyo aliuawa na kwamba huenda alisukumwa na mtu au watu ambao hawajajulikana.

Akizungumzia suala hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shanna, alisema jana kuwa ameusoma ujumbe huo na kuufanyia kazi.

Alisema ujumbe huo hauna ukweli wowote kwa kuwa vipo vielelezo vingi ukiwamo ushahidi wa maandalizi ya mtawa huyo kujiua.

Kamanda Shanna alisema kabla ya kujirusha, Mtawa huyo alifungasha vitu vyake katika nyumba aliyokuwa akikaa ikiwa ni pamoja na kumkabidhi mmoja wa ndugu zake gari lake na picha zake na baba yake mzazi akimueleza kuwa anakwenda eneo asilolijua.

"Kwenye uchunguzi kuna mambo mengi, picha ya kamera ya CCTV po wazi, inamuonesha mtawa huyo akiwa anapanda ngazi kwenda eneo husika na alipojirusha kuna baadhi ya wafanyakazi wengine na wagonjwa ambao walimuona hivyo hakuna taarifa za kusukumwa wala kurushwa.

"Kabla ya tukio hilo Mtawa huyo alijiandaa na kufunga vitu vyake, aligawa baadhi ya vitu kwa watu ikiwa ni pamoja na kumpatia gari mmoja wa ndugu zake na picha zake na wazazi wake.

"… aliziondoa line za simu zake kutoka ndani ya simu na kuweka simu juu ya kiyoyozi eneo ambalo alijirusha," alifafanua.

Kamanda Shanna alisema yeye binafsi alitembelea eneo alikojirusha Mtawa huyo na kupata maelezo kwa watu mbalimbali.

Alisema aliyesambaza ujumbe kuwa Mtawa huyo kuuawa alikuwa na lengo ambalo litashindana na ushahidi na polisi wanaendelea kuchapa kazi kwa kuwa ukweli wote umebainika.

Mtawa huyo anadaiwa kujirusha usiku wa kuamkia Agosti 27, mwaka huu na kuokotwa.

Alilazwa katika wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) na kuendelea kupatiwa matibabu lakini alifariki dunia usiku wa Agosti 28, mwaka huu wakati akiendelea kupatiwa matibabu.

Wizi wa fedha ulivyotokea:

Habari za ndani zilizopatikana zimedai kuwa Mtawa huyo akiwa mkuu wa kitengo cha fedha katika Hopsitali ya Rufaa Bugando, alikuwa amesimishwa kazi ikiwa ni pamoja na kushushwa cheo na bodi ya hospitali hiyo kutokana na kubainika upotevu wa Sh milioni 380.

Kwa mujibu wa uchunguzi, fedha zilizotoweka ni zile ambazo zilikuwa hazilipiwi katika mfumo wa benki ikiwa ni pamoja na sehemu ya fedha zilizokuwa zikilipwa benki moja kwa moja ambazo zilikuwa zikiinigizwa katika akaunti tofauti na kiasi kingine kikidaiwa kutoroshwa kwa njia ya mtandao.

"Wizi huu wa zaidi ya Sh milioni 300 ni wa kipindi cha miezi miwili tu hivyo ulipogundulika uongozi ulilazimika kufanya ukaguzi maalum.

"Lakini ukaguzi huo ulionyesha kulikuwa na wizi hivyo jukumu la kufuatilia likikabidhiwa kwa maofisa wa Benki ya CRDB, watalaamu wa mtandao, polisi kitengo cha fraud (udanganyifu) na Takukuru.

"Wiki mbili zilizopita baada ya kubainika hali hiyo uongozi wa hospitali ulitutangazia kusimamishwa kazi kwa Mtawa huyo ikiwa ni pamoja na kushushwa cheo.

"Hivyo alitakiwa kukabidhi ofisi lakini alikabidhi na baadhi ya vitu na siku ya kukabidhi ofisi hakutokea na hakuwapo nyumbani na ofisini hakufika mpaka siku iliyofuata ambako alikabidhi na siku moja baadaye kutokoea tukio hilo," alieleza mtoa taarifa.

Akizungumzia kifo hicho, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Bugando (BMC), Dk. Abel Makubi alisema hajabahatika kuona ujumbe ambao umesambazwa katika mitandao ya jamii.

Hata hivyo baada ya kutumiwa na kuusoma alisema anachoamini ni kwamba ujumbe huo umeandaliwa na mmoja wa watu ambao walikuwa na nia ya kutaka kuvuruga upelelezi unaondelea.

"Sikua nimeusoma ujumbe huo, lakini kwa jinsi ulivyonisomea, nauona kama ujumbe huu una lengo fulani.

"Kwanza muandikaji amejificha kwa kutaka kuaminisha yupo ndani ya polisi na anaongea kama polisi, lakini unaona anataka kuhamisha tatizo lionekane kuwa kauawa na ananijua mkurugenzi… hebu tuwaachie polisi wafanye uchunguzi wa haya, hata juu ya ujumbe huu," alisema.

Alikizungumzia suala la kamera za usalama hospitalini hapo, alieleza kuwa zipo lakini kutokana na ukubwa wa jengo hilo hazijawekwa jengo lote kwa asilimia 100 isipokuwa katika maeneo muhimu na yale ya njia za wanaoingia na kutoka.

"Kweli kuna kamera (CCTV camera), lakini hazitoshelezi jengo zima la hospitali, hivyo siyo rahisi kwa jengo lote kuwa nazo," alisema.
Chanzo - Mtanzania

Majaliwa wants locals to play role in mega projects

Prime Minister Kassim Majaliwa has instructed the ministry of Works, Transport and Communication to find ways that will see increased participation of private sector players in mega construction projects currently being implemented in the country.
Source

Video: Mwanamke wa kwanza kuiba gari Saudi Arabia anaswa na kamera ya CCTV

Mwanamke mmoja nchini Saudi Arabia ameonekana kwenye kipande cha video akiiba gari lililo egeshwa kando ya barabara. Tukio hilo lanamfanya mwanamke huyo kuwa mwizi wa kwanza magari Saudi Arabia tangu kupitishwa kwa sheria inayo waruhusu wanawake kuendesha chombo hicho cha usafiri miezi miwili iliyopita. CCTV iliyokuwa maeneo hayo ilinasa kipande cha video huko Al Dammam …

The post Video: Mwanamke wa kwanza kuiba gari Saudi Arabia anaswa na kamera ya CCTV appeared first on Bongo5.com.


Source

Jinsi ya kudumisha uhusiano wa mbali ( Long Distance Relationship)


Kuweza Kudumisha Uhusiano wa Mbali wa Kimapenzi (Distance Relationship)' kwa wapenzi wanaoishi mbalimbali.

Ni sehemu ndogo sana ya wapenzi wanaoishi mbalimbali ambao hudumu katika uhusiano wao kwa muda mrefu. Hiki kinaonekana kuwa ni kitendawili kigumu sana kwa wapenzi wengi kuvumiliana kwenye uhusiano bila kusalitiana.

Ninapozungumzia umbali namaanisha wilaya na wilaya, wilaya na mkoa au mkoa na mkoa au nchi na nchi au bara na bara.

Ninaamini miongoni mwetu ama tumeshuhudia au kusikia au kuona au kuadithiwa kuwa kuna mwanaume au mwanamke ambaye alikuwa na mpenzi, mara mpenzi wake akapata nafasi ya kwenda kusoma mkoa mwingine au nchi nyingine lakini mwisho wa siku ukasikia wapenzi wale wamemwagana baada ya mmoja kupata mpenzi mwingine huko aliko.

Inawezekana mpenzi wako alihamishwa kikazi nje ya wilaya uliyopo lakini mwisho wa siku ukabaini kuwa mwenzio amepata mtu mwingine na mapenzi kwako yameanza kupungua au yamepungua kama siyo kwisha kabisa.
Najua wengi huwa mnajiuliza ni nini huwa kinachangia? Zifuatazo ni baadhi ya sababu;

UAMINIFU
Kutokuwa na uaminifu miongoni mwenu, kama wapenzi mtakuwa ni waaminifu katika uhusiano wenu basi kila unapoingiwa na pepo wa usaliti unakumbuka uzuri wa mpenzi wako basi unaacha na kujizuia kumshinda pepo huyo.

UZALENDO
Kutokuwa mzalendo kwa mpenzi wako. Jaribu kumpenda kwa kuwa ndiye uliyemchagua kuwa naye, kila siku Tanzania inasema watumishi wake wawe wazalendo, siyo wao tu hata mapenzi yanahitaji uzalendo.

Uzalendo wa kupenda kitu chako, kumpenda mpenzi wako, mkeo, mumeo au mchumba wako. Lazima ujivunie, ujisifie kuwa naye kisha mthamini.

SUBIRA
Kutokuwa na subira au uvumilivu. Hili nalo huchangia mapenzi ya mbali kuvunjika. Kama ilivyo subira ya kila mtu kuamini kuwa ipo siku ataondoka kwenye shida na ugumu wa maisha alio nao, basi amini na kuwa na subira au uvumilivu kwa mpenzi wako ili mfikie ndoto zenu.
MAZINGIRA
Jiepushe sana na mazingira ambayo yanaonekana kabisa yanaweza kukusababisha ukaingia kwenye uhusiano usio rasmi tena, pengine kwa mtu ambaye huna ndoto naye.
Tatizo la kujiingiza kwenye uhusiano kwa sababu za kimazingira linaweza kukufanya ukajikuta umezama kwenye huba na mtu ambaye hana mapenzi na wewe na mwisho wa siku ukajikuta unaumia sana.

MAWASILIANO
Kutokuwa na mawasiliano ya mara kwa mara nayo huchangia sana kuvunjika kwa mapenzi ya mbali au kupoteza ladha, lakini kama mtu anakupenda, anakupenda tu, anaweza kukupigia simu na kukutumia SMS kibao lakini akawa bado ni tatizo.

TAMAA
Kama utaishi kwa kutamani vitu usivyokuwa na uwezo navyo ni dhahiri utajikuta unamsaliti mpenzi wako kwa kuwa tu uko mbali na unaona hawezi kukubana wala kukufuatilia. Ingawa ningeshauri ufanye kitu kwa kujiongoza na siyo kwa kuongozwa na tamaa au kwa kuwa mpenzi wako hayuko karibu nawe.

MKUMBO
Acha maisha ya kufuata mkumbo kama mwenzako amefanya kitu f'lani basi eti na wewe unataka ukifanye au ukipate ili uonekane wa kisasa au mjanja.
Kumbuka kuwa mwisho wa siku mtamaliza chuo na mengineyo, kila mtu atasambaa, kama uliharibu kwa mpenzi wako, mwenzio hatokuwepo.
Source

Picha : AFISA MIRADI UMOJA WA ULAYA AFANYA ZIARA SHINYANGA KUKAGUA UTEKELEZAJI WA MRADI WA KUTOKOMEZA MILA NA DESTURI KANDAMIZI KWA WATOTO


Afisa Miradi 'Afisa Programu' kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) John Villier amefanya ziara ya kutembelea na kujionea maendeleo ya mradi wa Kutokomeza Mila na Desturi Kandamizi zinachochangia ndoa na mimba za utotoni mkoani Shinyanga unaotekelezwa na Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Watoto la Save The Children.

Ziara hiyo imeanza leo Jumatano Agosti 29,2018 kwa Afisa Miradi huyo kukutana na wadau wanaoshiriki katika kutekeleza mradi huo wakiwemo viongozi wa serikali ya mkoa wa Shinyanga, Shirika la Save The Children na Shirika la Agape Aids Control Programme (AACP) ambao kwa pamoja wanaendelea kushirikiana katika kufanikisha mradi huo.

Akiwa katika ziara yake, John Villier pia amekutana na wanafunzi wa shule ya Msingi Mwamashele iliyopo kata ya Mwamashele kupitia "Tuseme Club" pamoja na kikundi cha watu wazima katika kijiji cha Itilima kata ya Itilima halmashauri ya wilaya ya Kishapu ambao hukutana na kujadili namna ya kukabiliana na mila na desturi kandamizi.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo,Villier alieleza kufurahishwa na jinsi mradi huo wa kutokomeza mila na desturi kandamizi unavyotekelezwa kwani umesaidia kupunguza mimba na ndoa za utotoni mkoani Shinyanga.

"Nimefurahi kuona kazi kubwa inayofanywa na Save The Children na AGAPE kwa kuwa na ushirikiano wa karibu na serikali pamoja na jamii katika kupiga vita mila na desturi kandamizi ambazo zinasababisha watoto wakose haki zao na kushindwa kutimiza ndoto zao,naomba tuendelee kushirikiana zaidi ili kuwakomboa watoto wanaopewa mimba na kuolewa katika umri usiotakiwa",aliongeza Villier.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga George Andrew aliushukuru Umoja wa Ulaya kwa kufadhili mradi huo unaotekelezwa na Shirika la Save The Children na kueleza kuwa kumekuwepo mafanikio makubwa akibainisha kuwa sasa jamii imebadilika na imeanza kuachana na mila na desturi kandamizi.

"Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na sekta binafsi,Umoja wa Ulaya na Save The Children tunatambua mchango wenu,kwa kweli sasa mila na desturi potofu zimeanza kupungua katika baadhi ya maeneo,mafanikio haya yanatokana na nyinyi kuwa karibu na serikali na wadau wengine",alieleza

Aidha alisema mradi huo umekuwa chachu kwa maafisa maendeleo ya jamii kuwajibika zaidi kwa kuyafikia maeneo ya pembezoni ambayo haikuwa rahisi kuyafikia na kuwapa elimu wananchi.

Naye Naibu Mkurugenzi Uendeshaji Miradi Kutoka Shirika la Save The Children nchini Tanzania, Jesse Orgenes alisema shirika hilo litaendelea kushirikiana na serikali na wadau wote wa maendeleo katika kupiga vita mila na desturi potofu katika jamii.

NIMEKUWEKEA HAPA PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI YALIYOJIRI WAKATI WA ZIARA YA AFISA PROGRAMU WA UMOJA WA ULAYA JOHN VILLIER
Afisa Miradi 'Afisa Programu' kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) John Villier akifanya mazungumzo na viongozi wa Shirika la Save The Children katika ofisi za Shirika hilo Mjini Shinyanga leo Jumatano Agosti 29,2018 - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde
Afisa Miradi 'Afisa Programu' kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) John Villier akizungumza na viongozi wa Shirika la Save The Children na kuhoji masuala mbalimbali kuhusu Mradi wa Kutokomeza Mila na Desturi Kandamizi zinachochangia ndoa na mimba za utotoni unaotekelezwa na Shirika la Save The Children kwa kushirikiana na Shirika la Agape Aids Control Programme (AACP) la Mjini Shinyanga wilaya ya Kishapu na Kahama mkoani Shinyanga.
Naibu Mkurugenzi Uendeshaji Miradi Kutoka Shirika la Save The Children nchini Tanzania, Jesse Orgenes akifafanua namna wanavyotekeleza mradi wa Mradi wa Kutokomeza Mila na Desturi Kandamizi katika mkoa wa Shinyanga.
Kushoto ni Naibu Mkurugenzi Uendeshaji Miradi Kutoka Shirika la Save The Children nchini Tanzania, Jesse Orgenes akielezea namna jamii inavyoshirikishwa katika mradi huo ili kuufanya uonekane ni wa jamii na siyo wa shirika.
Katikati ni Meneja wa Shirika la Save The Children Mkoa wa Shinyanga Benety Malima akielezea namna wanavyoshirikiana na shirika la AGAPE katika kutekeleza mradi wa Mila na Desturi Kandamizi katika mkoa wa Shinyanga. 
Meneja wa Shirika la Save The Children Mkoa wa Shinyanga Benety Malima akizungumza katika kikao hicho na kubainisha kuwa serikali ya mkoa wa Shinyanga imekuwa ikitoa ushirikiano mkubwa katika kufanikisha mradi wa kutokomeza mila na desturi kandamizi mkoani Shinyanga.
Wa pili Kulia ni Mratibu wa Mradi wa Kutokomeza Mila na Desturi Kandamizi zinachochangia ndoa na mimba za utotoni ,Mary Zabron akisisitiza jambo katika kikao hicho.
Hapa ni katika Ofisi ya Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga : Kulia ni Afisa Miradi 'Afisa Programu' kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) John Villier akisalimiana na Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga George Andrew.
Afisa Miradi 'Afisa Programu' kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) John Villier akifurahia jambo wakati akisalimiana na Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga George Andrew.
Wa pili kushoto ni Afisa Miradi 'Afisa Programu' kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) John Villier akielezea lengo la ziara yake mkoani Shinyanga kwa Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga George Andrew (katikati).
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga George Andrew akielezea mchango unaotolewa na Umoja wa Ulaya na Shirika la Save The Children katika kutetea haki za watoto ikiwa ni pamoja na kupiga vita mila na desturi kandamizi zinazochangia kuwepo kwa ndoa na mimba za utotoni.
Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Shinyanga George Andrew akiwaomba wadau wa maendeleo kuendelea kushirikiana na serikali katika mapambano dhidi ya ndoa na mimba za utotoni.
Hapa ni katika Ofisi za Shirika la AGAPE Mjini Shinyanga : Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la AGAPE John Myola akimwelezea Afisa Miradi 'Afisa Programu' kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) John Villier jinsi wanavyoshirikiana na shirika la Save The Children katika kutekeleza mradi wa Kutokomeza Mila na Desturi Kandamizi zinachochangia ndoa na mimba za utotoni mkoani Shinyanga.
Afisa Miradi 'Afisa Programu' kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) John Villier akisaini kitabu cha wageni katika ofisi za shirika la AGAPE.
Hapa ni katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Kishapu : Kushoto ni Meneja wa Shirika la Save The Children Mkoa wa Shinyanga Benety Malima akimtambulisha Afisa Miradi 'Afisa Programu' kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) John Villier. Katikati ni Mkurungezi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Mang'era Mang'era.
Wa pili kushoto ni Afisa Miradi 'Afisa Programu' kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) John Villier akieleza malengo ya ziara yake katika wilaya ya Kishapu.
Mkurungezi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Mang'era Mang'era akiushukuru Umoja wa Ulaya kwa kufadhili mradi wa Kutokomeza Mila na Desturi Kandamizi zinachochangia ndoa na mimba za utotoni ambao unatekelezwa na shirika la Save The Children kwa kushirikiana na shirika la AGAPE.
Ndani ya Ofisi ya Mwalimu Mkuu shule ya Msingi Mwamashele wilayani Kishapu : Kushoto ni Afisa Miradi 'Afisa Programu' kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) John Villier akiuliza swali kwa Mwalimu mku wa shule hiyo Justin Claud (wa kwanza kushoto) kuhusu changamoto zinazojitokeza kwenye 'Tuseme Club' ya wanafunzi wa shule hiyo. Jumla ya Tuseme Club 12 zipo katika shule 12 wilayani Kishapu. Klabu hizo zinasimamiwa na shirika la AGAPE kwa kushirikiana na Shirika la Save The Children.
Wanafunzi katika shule ya Msingi Mwamashele ambao wanaunda 'Tuseme Club' wakicheza mchezo ikiwa ni sehemu ni ya kupeana elimu juu ya madhara ya mimba na ndoa za utotoni.
Afisa Miradi kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) John Villier na viongozi wa shirika la Save The Children wakishuhudia elimu iliyokuwa inatolewa na walimu wa shule ya msingi Mwamashele kwa Klabu ya wanafunzi 'Tuseme Club'.
Kushoto ni Mwalimu Kalunde Majid akiendelea na kipindi kwa wanafunzi wa 'Tuseme Club'.
Afisa Miradi kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) John Villier akifuatilia kwa makini kilichokuwa kinaendelea darasani.
Wanafunzi wakionesha kwa vitendo kazi ya kuosha vyombo kuwa inafanywa na watu wa jinsi zote zote yaani kiume na kike na siyo kazi ya wanawake/wasichana tu.
Mratibu wa Mradi wa Kutokomeza Mila na Desturi Kandamizi zinachochangia ndoa na mimba za utotoni nchini ,Mary Zabron akiuliza swali kwa wanafunzi wa shule ya msingi Mwamashele.
Mwanafunzi akinyoosha mkono ili ajibu swali kuhusu madhara ya ndoa na mimba za utotoni.
Hapa ni katika kijiji cha Itilima kata ya Itilima wilayani Kishapu : Afisa Miradi kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) John Villier akijitambulisha kwa kikundi cha wananchi wa rika mbalimbali katika kijiji cha Itilima waliokuwa wanaendelea na mdahalo kujadili namna ya kuondokana na mila na desturi kandamizi ili kupiga vita ndoa na mimba za utotoni. 
Afisa Miradi kutoka Umoja wa Ulaya (European Union) John Villier alisema alifarijika kuona namna wananchi wa kata ya Itilima walivyohamasika kujitoa kupiga vita mila na desturi kandamizi kwa watoto.
Wakazi wa Itilima wakiendelea na mdahalo kuhusu mila na desturi kandamizi.
Mdahalo unaendelea.
Mkazi wa Itilima akichangia hoja wakati wa mdahalo huo.
Wa pili kulia ni Mratibu wa Mradi wa Kutokomeza Mila na Desturi Kandamizi zinachochangia ndoa na mimba za utotoni nchini ,Mary Zabron akiwaomba wananchi kuacha kufumbia macho mila na desturi zinazomkandamiza mtoto na kusababisha akose haki zake.
Mkazi wa Itilima Peter Mulwano 'Mzee Goma' akilishukuru shirika la Save The Children na AGAPE kuwafikia wananchi wa Kishapu kupitia mradi huo.
Afisa Mradi wa Kutokomeza Mila na Desturi Kandamizi zinachochangia ndoa na mimba za utotoni kutoka shirika la AGAPE, Peter Amani akizungumza wakati wa mdahalo huo.
Naibu Mkurugenzi Uendeshaji Miradi Kutoka Shirika la Save The Children nchini Tanzania, Jesse Orgenes akiwataka wananchi kubadilika na kuachana na mila na desturi potofu zinachochangia kuwepo kwa mimba na ndoa za utotoni.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

TB healthcare services brought closer to people

The government through the ministry of Health has decentralised Tuberculosis (TB) healthcare services to local authorities so to reduce inconveniences of covering long distances by people to health centres that number 78 countrywide.
Source

Ufahamu ugonjwa wa Saratani ya Ubungo


Kupambana na ugonjwa huu ni vigumu na unatisha.Kuna aina nyingi ya saratani jambo linalofanya kuwa gumu kukabiliana nao.

Saratani ya ubongo 
Ubongo ni mojawapo ya kiungo kitovu cha mtandao wa mishipa ya kusafirisha damu mwilini.Ubongo na uti wa mgongo huweza kuwa na uvimbe wa saratani ingawa ni nadra sana, ugonjwa huu ni hatari sana ikiwa hautatibiwa mapema.

Kisababishacho saratani ya ubongo haijulikani, lakini kuna mambo mengi yanayoweza kusababisha ugonjwa huu:

Ukiwa na saratani katika sehemu zengine za mwili huweza kusambaa hadi katika ubongo

Kufanya kazi katika kampuni za kusafisha mafuta, bidhaa za mipira , zinazotengeza madawa.

Dalili
Uvimbe unaweza kujitokeza katika sehemu yoyote ya ubongo,kwa hivyo dalili zitatofautiana.

Sehemu ya mbele (frontal)

Kuumwa na kichwa

Ulegevu mwilini

Kufa ganzi sehemu moja ya mwili

Mabadiliko ya haraka mwilini,hisia ,moyo na tabia

Kuchanganyikiwa na akili


Sehemu sawia (parietal)

Kuumwa na kichwa

Kushikwa na kifafa

Kufa ganzi

Shida unapoandika hati

Shida unapojaribu kusonga kwa namna Fulani

Shida kufanya hesabu rahisi


Sehemu ya nyuma (occipital)

Kuumwa na kichwa

Kushindwa kuona vizuri

Kuona mazingaumbwe yako tu

Kushikwa na kifafa


Kwa muda mfupi (temporal)

Kuumwa na kichwa

Kushikwa na kifafa

Shida ya kufuata maagizo kwa pamoja

Kutong'amua usumbufu wa hali ya anga.

Uvimbe katika mtandao wa mishipa huweza kumfanya mtu ashindwe kusimama wima, kutapika,na kubadilika kwa ghafla kwa hisia.


Saratani ya Matiti Wanawake walio hatarini kuupata ugonjwa huu ni:

Ajuza

Wenye asili ya kihindi au kizungu

Wanawake ambao washaugua saratani ya matiti mbeleni

Walio na jamaa wa karibu ( mama,dada,binti) ambao washawahi kuuguwa ugonjwa huu

Wanawake wenye hitilafu ya kinasaba kutoka kwa mzazi aliyeugua ugonjwa huu

Wanawake tasa au waliowapata watoto baada ya umri wa miaka 30.

Wanawake waliopata damu yao ya hedhi wakiwa na umri mdogo kabla miaka 12.

Wanawake waliokatika hedhi wakiwa wamechelewa baada ya miaka 50.

Wanawake wenye matiti makubwa(daktari anaweza kukuelezea baada ya uchunguzi wa mammogram)

Wanawake waliotumia tembe za uzazi,waliokosa kunyonyesha, wanaokunywa pombe kila siku,wanaonenepa sana baada ya kukatika hedhi,wanaomeza vidonge vya kubadilisha nasaba,na wale ambao hawakunyonyesha.


Dalili ya saratani ya Matiti:

Uvimbe kwenye matiti au kwapa

Mabadiliko katika umbo la matiti

Chuchu kutoa usaa ama titi kuwa nyororo

Chuchu kupotelea ndani ya matiti badala ya kujitokeza nje

Madutamaduta kwenye matiti kama yale ya maganda ya machungwa

Kubadilika kwa ngozi ya matiti na chuchu kuonekana zimefura

Ukiwa na mojawapo ya dalili hizi muone daktari,ni vyema kufanyiwa uchunguzi wa mammograms.

Fanyiwa uchunguzi wa matiti mapema ili kutambua saratani ya matiti mapema.Kujichunguza kila mwezi na kufanyiwa uchunguzi wa mammograms mara moja kwa mwaka hasa wanaozidi miaka 40 in bora.

Wednesday, August 29, 2018

Yanga sio wa Kimataifa Tena...Washika Mkia Kombe la Shirikisho


BAADA ya kumalizika kwa michezo ya kundi D, ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika hatimaye klabu za Yanga na Gor Mahia zimeaga rasmi michuano hiyo baada ya kupoteza katika michezo yao ya mwisho. Anaripoti Kelvin Mwaipungu …. (endelea).

Yanga ilipoteza mchezo wake mbele ya Rayol Sport ya Rwanda kwa kukubali kipigo cha bao moja kwa bila lililofungwa dakika 19, ya mchezo na mshambuliaji Bimenyimana baada kutumia vizuri makosa yaliyofanywa na Nahodha wa klabu hiyo Kelvin Yondani.

Kwa upande wa Gor Mahia ambayo ilikuwa ugenini mbele ya USM Alger ilikubali kipigo cha mabao mawili kwa moja, mabao ya mchezo huo kwa upande wa wenyeji yalifungwa na Price Ibara dakika ya 36 na Sayoud aliyefunga dakika ya 81 ya mchezo huku bao pekee la wakenya hao lilifungwa na Tuyisenge 83.

Kwa matokeo hayo, USM Alger ikiwa na pointi 11 kileleni, na Rayon Sports yenye pointi 9, zinafuzu hatua ya robo fainali, huku Gor Mahia ikipata alama 8, na kushika nafasi ya tatu na Klabu ya Yanga iliambulia alama nne na kushika mkia kwenye kundi hilo.

Ripoti: Zifahamu sumu zinazoweza kusababisha tatizo kama la Ommy Dimpoz la kushindwa kumeza (Audio/Picha)

Baada ya kusikia tatizo la muimbaji Ommy Dimpoz la kushindwa kumeza chakula limesababishwa na sumu, mtandao wa Bongo5 umeamua kufutilia suala hilo kwa ukaribu na kukuletea ripoti maalumu ambayo inaeleza ni sumu ya aina gani ambayo huwenda ikawa imesababisha tatizo kwa muimbaji huyo ambaye tayari ameshafanyiwa upasuaji na kuwekewa mfumo mpya wa chakula baada ya …

The post Ripoti: Zifahamu sumu zinazoweza kusababisha tatizo kama la Ommy Dimpoz la kushindwa kumeza (Audio/Picha) appeared first on Bongo5.com.


Source

Tuesday, August 28, 2018

Watumishi wa Umma Wapigwa Marufuku Kutumia Mitandao ya Kijamii


Serikali imezuia matumizi ya mitandao ya kijamii kwa watumishi wa umma wakati wa kazi kwa madai yanaathiri kasi ya mtandao wa intaneti ya serikali, na kudai kuwa watumishi wengi wanapoteza muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii kuliko kutekeleza majukumu yao. 

Taarifa iliyotolewa leo na katibu mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro kwa taasisi zote za umma, imeonya juu ya matumizi mabaya ya mitandao ya mawasiliano ya serikali na kwamba, hatua hiyo imelenga kudhibiti matumizi ya mitandao. 

"Kasi ya mtandao wa serikali inapungua kutokana na matumizi makubwa ya mitandao ya kijamii hususan inayopakua video, mfano 'YouTube' na hivyo kusababisha watumishi wengine wanaotumia mtandao wa intaneti wa Serikali katika kutekeleza majukumu yao kuathirika," imesema barua hiyo. 

Aidha,  Menejimenti ya Utumishi imezitaka taasisi zenye mahitaji maalumu ya matumizi ya mitandao ya kijamii wakati wa saa za kazi, kuwasilisha maombi yao kwa katibu mkuu wa utumishi yakiambatana na sababu za maombi hayo. 

Kwa mara kadhaa, serikali imekuwa ikitoa miongozo ya matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano kwa taasisi za serikali ikiwemo kukataza matumizi ya mitandao kupitia intaneti ya serikali muda wa kazi. 

MTAWA AJIUA KWA KUJIRUSHA GHOROFANI HOSPITALI YA RUFAA BUGANDO MWANZA


Mkurugenzi wa Fedha na Mipango katika Hospitali ya Rufaa Bugando, jijini Mwanza, Mtawa Suzan Bathlomeo (Pichani) amefariki dunia baada ya kujirusha kutoka gorofani muda mfupi baada ya kutoka kusali misa ya saa 12:00 asubuhi, leo Jumanne Agosti 28, 2018.

Habari zilizomkariri Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shana akithibitisha kutokea kwa tukio hilo zimesema kuwa taarifa kamili zitatolewa na Polisi kwa Kamanda huyo kuzungumza na waandishi wa habari baadaye.

Kwa mjibu wa ofisa uhusiano wa Bugando, Lucy Mogele Mtawa huyo amefariki dunia leo alfajiri, huku akibainisha kuwa hospitali hiyo haina mamlaka ya kuzungumziwa suala hilo na kutaka litafutwe shirika la watawa la Kagera, ambalo makao makuu yake yapo mjini Bukoba mkoani Kagera.

"Ni kweli Sister Suzan amefariki dunia baada ya kujirusha kutoka ghorofani lakini Bugando hatuna mamlaka ya kuzungumzia suala hilo," amesema Lucy.

Gigy Money Amtolea Uvivu Irene Uwoya.

Msanii wa bongo fleva na ‘video vixen’ nchini, Gigy Money amefunguka na kumchana muigizaji wa filamu, Irene Uwoya kuwa umri wake umeshaisha wa kutengeneza ‘skendo’ za kuvaa na kupiga picha za nusu utupu na ndio maana anawasii watu wengine kuwa kama yeye. Gigy ametoa kauli hiyo alipokuwa anazungumza na www.eatv.tv baada ya kupita takribani siku tano tokea mwanadada Irene Uwoya alipotoa kauli yake, ya kuwataka ma-star wenzake kuacha kutumia ‘skendo’ za kupiga picha nusu utupu kwa madai vitendo hivyo vinamchukiza hadi Mungu. “Ana haki ya kuongea hivyo Irene, kwasababu ameshamaliza ujana wake wa kufanya vitu vya hivyo na anajua faida na hasara zake, ila sisi bado tutaendelea hadi pale tutakapoona imefikia tamati, ndio nasi tutaacha na kuwa kama yeye”, amesema Gigy. Mbali na hilo, Gigy Money amesema mitandao ya kijamii imewasaidia kwa kiasi kikubwa kuwatambulisha katika jamii, jambo ambalo likapelekea na wao kuonyesha kipaji chao cha uimbaji walichokuwa nacho baadhi ya watu. “Kinachoimba sio mavazi, mimi ninaamini kwenye kipaji zaidi kuliko kitu chochote. Lakini kama tungeanza kwenye muziki wasingetufahamu hadi hii leo na ndio maana kila mtu ana njia yake ya kujisogeza pahali fulani. Kwa hiyo waangalie u-serious wa mtu, vitu vingine ni ‘brand’ tu”, amesisitiza Gigy. Gigy Money ni miongoni mwa wanadada walioweza kujipatia umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, kwa vituko vyake anavyovifanya kila kukicha bila ya kuhofia kitu chochote kilichopo mbele yake.

The post Gigy Money Amtolea Uvivu Irene Uwoya. appeared first on Ghafla!Tanzania.


Source

Jackline Mengi Akerwa na Watumiaji Vibaya Mitandao ya Kijamii.


Mwanadada mrembo Jackline Mengi amekerwa na wale wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii huku wakitumia mitandao hiyo vibaya na kuifanya kama mwamvuli ya kufanya mambo maovu ambayo wasingeweza kifanya wakiwa mbele ya watu.

Jackline Mengi amesema kuwa watu hao wapo wengi katika jamii tunazoishi kiasi kwamba watu wanatakiwa wafikirie kuwa unapoamua kufanya jambo la kumtukana au kumuumiza mtu mwingien kwa makusudi unatakiwa kuja kabisa kwamba hata yeye anaumia .

Kupitia instagramu yake aliandika hivi'' Ndugu zangu watumiaji wa mitandao ya kijamii tukumbuke kuwa ubinadamu wetu unabaki pale pale hata wakati tunatumia mitandao. Ukimtukana,kumkejeli au kumbeza mwenzio mtu anaumia kama ambavyo ungemwambia mbele ya uso wake. Wapo wengi wanaotumia mitandao kama mwamvuli wakidhani kwenye mitandao wana haki ya kufanya vitendo au maneno ambayo wasingeweza kufanya wazi mbele ya jamii.Tukumbuke tu mitandao haitupi haki ya kujivua utu wetu, tujiheshimu na kuheshimu wengine.''
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...