Tuesday, August 28, 2018

MTAWA AJIUA KWA KUJIRUSHA GHOROFANI HOSPITALI YA RUFAA BUGANDO MWANZA


Mkurugenzi wa Fedha na Mipango katika Hospitali ya Rufaa Bugando, jijini Mwanza, Mtawa Suzan Bathlomeo (Pichani) amefariki dunia baada ya kujirusha kutoka gorofani muda mfupi baada ya kutoka kusali misa ya saa 12:00 asubuhi, leo Jumanne Agosti 28, 2018.

Habari zilizomkariri Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shana akithibitisha kutokea kwa tukio hilo zimesema kuwa taarifa kamili zitatolewa na Polisi kwa Kamanda huyo kuzungumza na waandishi wa habari baadaye.

Kwa mjibu wa ofisa uhusiano wa Bugando, Lucy Mogele Mtawa huyo amefariki dunia leo alfajiri, huku akibainisha kuwa hospitali hiyo haina mamlaka ya kuzungumziwa suala hilo na kutaka litafutwe shirika la watawa la Kagera, ambalo makao makuu yake yapo mjini Bukoba mkoani Kagera.

"Ni kweli Sister Suzan amefariki dunia baada ya kujirusha kutoka ghorofani lakini Bugando hatuna mamlaka ya kuzungumzia suala hilo," amesema Lucy.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...