Mwanadada mrembo Jackline Mengi amekerwa na wale wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii huku wakitumia mitandao hiyo vibaya na kuifanya kama mwamvuli ya kufanya mambo maovu ambayo wasingeweza kifanya wakiwa mbele ya watu.
Jackline Mengi amesema kuwa watu hao wapo wengi katika jamii tunazoishi kiasi kwamba watu wanatakiwa wafikirie kuwa unapoamua kufanya jambo la kumtukana au kumuumiza mtu mwingien kwa makusudi unatakiwa kuja kabisa kwamba hata yeye anaumia .
Kupitia instagramu yake aliandika hivi'' Ndugu zangu watumiaji wa mitandao ya kijamii tukumbuke kuwa ubinadamu wetu unabaki pale pale hata wakati tunatumia mitandao. Ukimtukana,kumkejeli au kumbeza mwenzio mtu anaumia kama ambavyo ungemwambia mbele ya uso wake. Wapo wengi wanaotumia mitandao kama mwamvuli wakidhani kwenye mitandao wana haki ya kufanya vitendo au maneno ambayo wasingeweza kufanya wazi mbele ya jamii.Tukumbuke tu mitandao haitupi haki ya kujivua utu wetu, tujiheshimu na kuheshimu wengine.''