Thursday, August 30, 2018

MKUU MPYA WA WILAYA YA BAGAMOYO ZAINABU KAWAWA AFUNGUA RASMI MAFUNZO YA AWALI YA JESHI LA AKIBA KWA VIJANA 183 CHALINZE


1
  Mkuu mpya wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa wa kati kati akirukaruka mara baada ya kufungua mafunzo rasmi ya jeshi la akiba kwa vijana wapatao 183 hawapo pichani  kutoka kata ya  Bwilingu katika halmashauri ya Chalinze pembeni yake kulia ni Mshauri wa jeshi la akiba Wilayani Bagamoyo Maj Chinguku.
2
Mkuu mpya wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa wa kati kati akirukaruka mara baada ya kufungua mafunzo rasmi ya jeshi la akiba kwa vijana wapatao 183 hawapo pichani  kutoka kata ya  Bwilingu katika halmashauri ya Chalinze pembeni yake kulia ni Mshauri wa jeshi la akiba Wilayani Bagamoyo Maj Chinguku.
3
Mkuu mpya wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Rashid Kawawa kulia akiwa na  Mshauri wa jeshi la akiba wilayani humo wa kushoto Maj Chinguku wakati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa mafunzo wa jeshi la akiba kwa vijana wapatao 183  ambayo yamefanyika katika  kata ya Bwilingu halmashauri ya Chalinze.

VICTOR MASANGU,  CHALINZE

MKUU mpya wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa amewataka vijana ambao wanahitimu  mafunzo ya jeshi la akiba  kuhakikisha wanakuwa wazalendo na nchi yao na kuachana kabisa na vitendo vya kujiingiza katika matukio ya kihalifu na badala yake wahakikishe wanazingatia sheria na taratibu zote zilizowekwa  kwa lengo la kuweza kulinda hali ya ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao.

Kauli hiyo aliitoa wakati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa mafunzo  ya awali ya  jeshi la akiba ambayo yamefanyika katika kata ya Bwilingu  na kuwajumusiha vipana wapatao 183 kutoka  katika halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani.

Mkuu huyo pia aliwahimiza vijana hao kuhakikisha wanakuwa na nidhamu ya hali ya juu katika kipindi chote cha mafunzo hayo ya kijeshi na kuzingatia maelekezo ambayo wanapatiwa na walimu wao kwa lengo la kuweza kujifunza   mbinu mbali mbali ambazo zitaweza kuwa ni mkombozi mkubwa katika kulilinda Taifa la Tanzania na kuweza kukabiliana na wimbi la matukio ya uhalifu.

"Napenda kuchukua fursa hii  kuwapongeza vijana ambao mmeweza kujitokeza katika mafunzo haya ya jeshi la akiba,lakini kitu kikukbwa ninawaomba muwe wazalendo na nchi yenu kwa kuhakikisha mnazingatia sheria na taratibu za nchi ikiwa ni sambamba na kuyatumia vizuri mafunzo mliyopatiwa kwa maslahi ya nchi na sio vinginevyo,"alisema

Kwa upande wake Mshauri wa jeshi la akiba  Wilayani Bagamoyo Maj Chinguku alibainisha kuwa  mafunzo hayo yatakuwa ya miezi minne na nusu ambapo vijana hao  wataweza kujifunza mbinu mbali mbali za kivita ambazo zitaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa maslahi ya Taifa.

"Katika mafunzo haya vijana ambao walijitokeza hapo awali walikuwa ni 211 lakini baadhi yao wameshindwa kuendelea kutokana na sababu mbali mbali hivyo ambao wanaendelea kwa sasa na  ni vijana wapatao 183 ambao wametokea katika kata ya bwilingu, ambapo wataweza kupata mafunzo mbali mbali ya kijenzi kwa kipindi cha muda wa wiki 18 alisema Chinguku"

Naye Diwani wa  kata ya Bwilingu Lucas Lufundo alisema  kwamba mafunzo hayo yataweza kuwasaidia vijana kwa kiasi kikubwa kudumisha hali ya ulinzi na usalama katika maeneo mbali mbali  na kwamba kutaweza kupunguza wimbi la vijana wengi  ambao walikuwa wanakaa  vijiweni bila ya kujishughulisha na kazi pamoja na kupunguza na changamoto ya wimbi la  uhalifu.

Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...