Thursday, August 30, 2018
Ufahamu ugonjwa wa Saratani ya Ubungo
Kupambana na ugonjwa huu ni vigumu na unatisha.Kuna aina nyingi ya saratani jambo linalofanya kuwa gumu kukabiliana nao.
Saratani ya ubongo
Ubongo ni mojawapo ya kiungo kitovu cha mtandao wa mishipa ya kusafirisha damu mwilini.Ubongo na uti wa mgongo huweza kuwa na uvimbe wa saratani ingawa ni nadra sana, ugonjwa huu ni hatari sana ikiwa hautatibiwa mapema.
Kisababishacho saratani ya ubongo haijulikani, lakini kuna mambo mengi yanayoweza kusababisha ugonjwa huu:
Ukiwa na saratani katika sehemu zengine za mwili huweza kusambaa hadi katika ubongo
Kufanya kazi katika kampuni za kusafisha mafuta, bidhaa za mipira , zinazotengeza madawa.
Dalili
Uvimbe unaweza kujitokeza katika sehemu yoyote ya ubongo,kwa hivyo dalili zitatofautiana.
Sehemu ya mbele (frontal)
Kuumwa na kichwa
Ulegevu mwilini
Kufa ganzi sehemu moja ya mwili
Mabadiliko ya haraka mwilini,hisia ,moyo na tabia
Kuchanganyikiwa na akili
Sehemu sawia (parietal)
Kuumwa na kichwa
Kushikwa na kifafa
Kufa ganzi
Shida unapoandika hati
Shida unapojaribu kusonga kwa namna Fulani
Shida kufanya hesabu rahisi
Sehemu ya nyuma (occipital)
Kuumwa na kichwa
Kushindwa kuona vizuri
Kuona mazingaumbwe yako tu
Kushikwa na kifafa
Kwa muda mfupi (temporal)
Kuumwa na kichwa
Kushikwa na kifafa
Shida ya kufuata maagizo kwa pamoja
Kutong'amua usumbufu wa hali ya anga.
Uvimbe katika mtandao wa mishipa huweza kumfanya mtu ashindwe kusimama wima, kutapika,na kubadilika kwa ghafla kwa hisia.
Saratani ya Matiti Wanawake walio hatarini kuupata ugonjwa huu ni:
Ajuza
Wenye asili ya kihindi au kizungu
Wanawake ambao washaugua saratani ya matiti mbeleni
Walio na jamaa wa karibu ( mama,dada,binti) ambao washawahi kuuguwa ugonjwa huu
Wanawake wenye hitilafu ya kinasaba kutoka kwa mzazi aliyeugua ugonjwa huu
Wanawake tasa au waliowapata watoto baada ya umri wa miaka 30.
Wanawake waliopata damu yao ya hedhi wakiwa na umri mdogo kabla miaka 12.
Wanawake waliokatika hedhi wakiwa wamechelewa baada ya miaka 50.
Wanawake wenye matiti makubwa(daktari anaweza kukuelezea baada ya uchunguzi wa mammogram)
Wanawake waliotumia tembe za uzazi,waliokosa kunyonyesha, wanaokunywa pombe kila siku,wanaonenepa sana baada ya kukatika hedhi,wanaomeza vidonge vya kubadilisha nasaba,na wale ambao hawakunyonyesha.
Dalili ya saratani ya Matiti:
Uvimbe kwenye matiti au kwapa
Mabadiliko katika umbo la matiti
Chuchu kutoa usaa ama titi kuwa nyororo
Chuchu kupotelea ndani ya matiti badala ya kujitokeza nje
Madutamaduta kwenye matiti kama yale ya maganda ya machungwa
Kubadilika kwa ngozi ya matiti na chuchu kuonekana zimefura
Ukiwa na mojawapo ya dalili hizi muone daktari,ni vyema kufanyiwa uchunguzi wa mammograms.
Fanyiwa uchunguzi wa matiti mapema ili kutambua saratani ya matiti mapema.Kujichunguza kila mwezi na kufanyiwa uchunguzi wa mammograms mara moja kwa mwaka hasa wanaozidi miaka 40 in bora.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 15, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekagua ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi) ...