Naibu waziri wa TAMISEMI Mwita Waitara amewataka viongozi kutoka ngazi mbalimbali kujenga Mahusiano Mazuri na waandishi wa habari kwani ndio nguzo muhimu kwa maendeleo ya Taifa.
Waitara amesema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na wadau wa elimu katika kikao cha Maandalizi ya Mashindano ya Umoja wa Michezo shule za Sekondari ,Tanzania [UMISETA] unaodhaminiwa na Coca cola.
Mhe.Waitara amesema waandishi wa habari wanatakiwa kupewa kipaumbele katika mambo ya Msingi ya Serikali vivyo hivyo katika mashindano hayo ya UMISETA ni vyema vyombo vya habari vikatumika kuibua vipaji vya wachezaji mbalimbali na serikali za mitaa kuwawezesha wanahabari katika kutekeleza majukumu yao kwani ni nguzo muhimu.
"Sio kwamba mpaka aje Mkurugenzi,Waziri No.hata wewe unaweza ,mwanafunzi kafanya vizuri tangaza hiyo,shule za kata zinatoa matokeo mazuri tangaza hiyo.Kuna Ofisi zingine zina pwaya ni mzigo akimwona mwanahabari hata ushirikiano hatoi yeye yupoyupo tu.
"Hivyo katika Mashindano haya tumieni vyombo vya habari,kupitia blogs,redio,magazeti ,vyombo vya habari vyote kuhamasisha michezo."
Aidha waitara ameagiza Maafisa elimu wilaya ni mikoa kufuatilia somo la michezo kufundishwa kwa nadharia na vitendo,viwanja vya michezo kufufuliwa,kusimamia makusanyo ya fedha za michezo na nyimbo za uzalendo ikiwa ni pamoja na wimbo wa Taifa na wimbo wa Afrika Mashariki kuimbwa hasa kwenye mashindano hayo.
"Unakuta mtu mzima na ofisi yake ukimwambia imba anasingizia ana kikohozi ,tatizo sio kikohozi bali haujui huo wimbo.hivyo tuhamasishe nyimbo za uzalendo kwa Taifa Letu."
Katika kuboresha na Kutunza Mazingira Mhe.Waitara ameagiza kila mwalimu apande mti mmoja wake shuleni na kila mwanafunzi miti miwili nyumbani na shuleni.
Mkurugenzi Idara ya Elimu Tanzania,Julius Nestory amesema watashirikiana na wadau mbalimbali katika kukuza vipaji vya wanafunzi shuleni huku akipongoza Copa Coca Cola kwa kudhamini Mashindano ya UMISETA.
Kwa Upande wake ,Mkurugenzi wa Mambo ya Umma na Mawasilino ,Coca Cola Haji Mzee Ally amezitaja mikoa atakayoanza katika kuzindua Mashindano ya UMISETA 2019 ni Tabora,Manyara na Ruvuma huku akisema kuwa kutakuwa na mkakati kabambe wa kuzipa zawadi shule zitakazokusanya takataka za plastiki za kampuni yoyote katika kuhakikisha utunzaji wa Mazingira .
Mwenyeji wa Mashindano UMISETA 2019 ni Mkoa wa Mtwara na yanatarajia kuanza mwezi ujao.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Bongo Deco wauzai wa vifaa mbalimbali vya umeme kama TV, Subwoofer, Hometheator, Majiko madogo na makubwa ya Gesi, Friji, Generator nk leo w...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia)akimsikiliza Waziri wa Maliasili na Utalii wa Jamhuri ya ...
-
Kuongezeka kwa ghasia za hivi majuzi kumesababisha idadi kubwa ya raia wa Lebanon kukimbia kutoka Beirut huku milipuko ikitikisa jiji hilo...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 15, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekagua ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi) ...