Sunday, March 31, 2019
Waziri Hamisi Kigwangala Afunguka Kumtetea Pierre Liquid Dhidi ya Maneno ya Makonda " Pierre ni mtu huru kwenye nchi yake"
Reposted from @hamisi_kigwangalla - It's ok! It's ok! It's ok, very ok kwa Pierre Liquid kufanya anachofanya na kufurahisha wanaoona 'anachekesha'. Nchi haiwezi kujengwa na watu wanaofanya mambo magumu magumu pekee. Kila mmoja wetu anafanya sehemu yake. Pierre anatuchekesha na kutukumbusha kufurahia maisha tunapopata nafasi, haswa tunapotoka kufanya hayo mambo yetu magumu magumu! Jamani maisha ni magumu, yana mitihani mingi na ni mafupi sana. Katika kuleta furaha na shangwe kwenye maisha ndiyo maana 'wachekeshaji' wakapata ajira! Wengine tusome udaktari, uhandisi na tufanye uvumbuzi na utatuzi wa changamoto na wengine watutetemeshe, watuvuruge akili, watupe raha na furaha, watuchekeshe, siku zisogee. Maisha ndiyo haya haya! Zaidi ya yote, Pierre ni mtu huru kwenye nchi yake. Tunapaswa kuulinda uhuru wa Pierre kama ambavyo Katiba ya nchi yetu inavyoelekeza. Let him be. Tumuache apate riziki yake. Mungu anajua zaidi kwa nini hatukumjua miaka 5 iliyopita na kwa nini sasa anazua mjadala.
Hata kwa mimi binafsi, Mungu anajua zaidi kwa nini sikuwa Waziri miaka mitano iliyopita, na leo ni Waziri. Mungu anatupangia maisha yetu. Anatugawia mafungu yetu. Pengine hii inaweza kuwa sababu ya Pierre kuwa mtu bora zaidi leo kuliko ile siku aliyopiga ukelele wa raha na kubembea pale Liquid! Pengine hii ndiyo nyota yake ya jaha. Kwa hakika, Pierre atabaki kuwa juu! Pierre atabaki kuwa kileleni! Everebade sey yeeh! #HK
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025 Msimamo Ligi Kuu Bara 2024/2025, NBC Premier League Tanzania Msimamo Ligi Kuu NBC 2024/2025 Tanzania Premier...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...
-
Na Mbuke Shilagi Kagera. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mradi wa umeme wa maji ya maporomoko wa Rusumo...
-
Msanii wa nyimbo za asili Nyanda Madirisha Obhado 'Maliganya' maarufu Shikomba Bhulolo anakualika kusikiliza wimbo wake mpya 2021 un...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...