Kampuni ya KILIMANJARO BIOCHEM LIMITED inazindua kinywaji kipya aina ya pombe kali ya KIWINGU. Kinywaji hichi kitazalishwa katika kiwanda chao kilicho katika kijiji cha Kifaru, wilaya ya Mwanga mkoa wa Kilimanjaro na kitasambazwa kuanzia Dar es Salaam na Mwanza. Kinywaji hichi kipya kimetengenezwa kwa kuzingatia mahitaji ya wanywaji na kwa utaalamu wa hali ya juu.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Naibu waziri wa viwanda Mhe. Exaud Kigahe, ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema kuwa serikali itaeendelea kuunga mkono wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ili kufanikisha mikakati wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda akiongea na waandishi wa habari na wafanya biashara katika sekta ya usambazaji wa pombe Dar es Salaam
"Nawapongeza Kilimanjaro Biochem Limited, kwa kuzindua kinywaji chao kipya kiitwacho Kiwingu, kuingia sokoni, sambamba na mikakati yao ya kuyateka masoko zaidi.
Tumejumuika siku ya leo pamoja na wafanya biashara katika sekta ya usambazaji, na ni ishara kwamba mnatambua manufaa ya bidhaa hii mpya katika biashara zenu na pia mngependa kuwa sehemu ya mafanikio na ukuzaji wa uchumi. "
Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Kilimanjaro Biochem, Bw. Mehul Patel alisema "Soko la vinywaji nchini Tanzania lina ushindani mkubwa. Tunajali ubora na kuhakisha viwango katika kila hatua ya utengenezaji wa kinywaji chetu kipya kinacho itwa Kiwingu.
Katika ubora wetu tunatumia ethanol yenye viwango vya juu isiyo sababisha uchovu baada ya kunywa na yenye kiwango cha juu cha pombe."
Kampuni ya Kilimanjaro Biochem imewekeza takribani TZS. 11.5 Billioni, kwa ajili ya uwezeshaji na uzalishaji wa bidhaa hii mpyaitazo enda kusaidia uchumi kwa kutoa ajira kwa watanzania 200 katika ajira rasmi, na zaidi ya watanzania 50 katika ajira zisizo rasmi kama wakulima wadogo na wa kati wanaojishughulisha na kilimo cha mtama katika mashamba yaliyopo wilayani Mwanga na wilaya za jirani.
Kilimanjaro Biochem inashirikiana na jamii inayoizunguka kwa kushiriki kuimarisha huduma za jamii na kuchangia kupitia programu ya uwajibikaji wa huduma za kijamii ( CSR ) kwa kutoa kiasi zaidi ya 24 Milioni kila mwaka kuwekeza kwenye elimu, afya na maji.
Mkuu wa usambazaji na mauzo kutoka Kilimanjaro Biochem Eng Herman Mathias aliongeza kuwa kinywaji cha Kiwingu kinapatikana kwenye chupa ndogo yenye ujazo wa mililita 250 na usambazaji wa kiwingu utaanza katika mkoa wa Dar es Salaam na mikoa yote ya kanda ya ziwa na akawashukuru mawakala wote waliokuwa wamehudhuria uzinduzi huo.
Mkuu wa masoko aliongeza "Wananchi wote wana weza kupata taarifa mbalimbali kuhusu Kiwingu na kuzungumza moja kwa moja na wasaidizi kupitia mitandao yao ya kijamii, kupitia Whatsapp namba 0737 72 7 182 ili kujua zaidi kuhusu Kiwingu.
Kuhusu Kilimanjaro Biochem
Kilimanjaro Biochem Ltd iliyo katika kijiji cha Kifaru wilayani Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro ni Kampuni ya Uwekezaji wa Kigeni ya 100% iliyoanzishwa mnamo 2008.
Kilimanjaro Biochem ltd hutengeneza bidhaa za Extra Neutral Alcohol (96.4%) na liquid LCO2 (99.99+% purity) ambazo hutumika katika viwanda vya vinywaji na pombe na ambayo hutumiwa katika tasnia ya Medical Spirit na Hand Sanitizer.
Ni kampuni ya kwanza ya utengenezaji wa kemikali ya BIO-Chemicals nchini Tanzania.
Kilimanjaro Biochem LTD ni kampuni ya ISO 9001: 2015 na FSSC 22000: 2013 iliyothibitishwa. Sisi kama kampuni tunatumia rasilimali zinazopatikana hapa nchini kama Molasses, na kadhalika.
KBL inaajiri karibu Wafanyikazi 200 moja kwa moja chini ya mishahara yetu na wengine 50 chini ya Mkataba wa moja kwa moja kazi ya kawaida kulingana na mahitaji.
Mawasiliano
Tel: 0769905692 or 0272974148
Email: info@kbl.co.tz