Vyanzo vingi vinasema kwamba Charlie Chaplin alikuwa ni muigizaji na pia ni mtayarishaji wa filamu maarafu wa kingereza.
Pia Charlie Chaplin alizaliwa mnamo tarehe 16 mwezi wanne mwaka 1889 na alifariki mnamo mwezi wa 12 mwaka 1977.
Umaarufu wake ulitokana na uwigizaji wa video zake za kuchekesha ambazo zilikuwa ni za kimya kimya ambazo zilikuwa hamna kuongea wala kutoa sauti na watazamaji walikuwa wanafurahi, kwa miaka ya hivi karibuni tunaweza kumfananisha mchekeshaji huyo na Mr. bean japo Mr. bean yeye hafanyi vichekesho vya kimya kimya pekee kama ambavyo alifanya Charlie Chaplin.
Kama nilivyosema hapo awali kwamba Charlie Chaplin alikuwa ni muigizaji pia muongozaji wa filamu zote zinazomhusu. Charlie Chaplin alifanya kazi hiyo kwa takribani kwa miaka 70.
Sehemu kubwa za filamu ambazo alikuwa akicheza Charlie Chaplin mara nyingi ilikuwa ikiitwa "the Tramp". Uhusika huu ulikuwa ukimuonesha Charlie Chaplin kwamba ni mtu mwenye heshima zake, ambaye alikuwa akivaa koti, suruali kubwa kofia pamoja viatu huku akichekesha.
Huyo ndiye Charlie Chaplin muigizaji maarafu kuwahi kutokea katika sayari hii.
Asante na endelea kutembelea Muungwana Blog kila wakati.