Tuesday, June 22, 2021

UWT kufungua kiwanda cha sabuni chenye thamani ya zaidi ya Milioni 117


Na Amiri Kilagalila Njombe

Jumuiya ya wanawake wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Njombe inatarajia kufungua kiwanda cha kuzalisha sabuni mkoani humo chenye thamani ya zaidi ya milioni 117 kitakachoweza kutoa ajira kwa nafasi mbali mbali huku kipaumbele ikiwa ni kwa vijana ili kupunguza changamoto ya ajira kwa kudi hilo.

Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa jumuiya hiyo mkoa wa Njombe Bi,Scolastika Kevela wakati akitoa hotuba na kuwasilisha mpango kazi wa jumuiya hiyo mbele ya kikao cha balaza la UWT mkoa wa Njombe kilichofanyika katika ofisi za chama hicho zilizopo kata ya mji Mwema mjini Njombe.

"Tumepanga kuanza mradi wa kutengeneza sabuni za kuogea,za maji na sabuni za kufulia kwa maana ya vipande.Ghalama za kuanzisha mradi itakuwa ni shilingi milioni mia moja kumi na saba,laki nne kumi na tano na mia mbili ishirini na moja"alisema Scolastika Kevela

Ameongeza kuwa uwekezaji wa kiwanda hicho unaotarajia kuanza ndani ya miezi sita ijayo utakuwa na uwezo wa kuzalisha katoni 200 za sabuni za miche kwa siku,katoni 50 za sabuni za kuogea kwa siku na lita 2000 za sabuni ya maji kwa siku.

Vile vile amesema dhamira ya kufungua kiwanda hicho ni kutokana na juhudi za jumuiya hiyo kujikomboa na kujitegemea kiuchumi pamoja na kutoa fursa za ajira kwa vijana kwa kuwa bidhaa hiyo ina matumizi makubwa na ya kila siku katika jamii.

"Sabuni ni bidhaa ambayo anaitumia kila mt una dhamira ya serikali ni kuiendeleza Tanzania kuwa ya viwanda pamoja na kupunguza changamoto ya ajira kwa watanzania.Sabuni zetu zitaitwa jina la UWT Njombe "alisema Scola Kevela na kuwataka vijana kujiandaa na kupokea ajira.

Kwa upande wake katibu wa CCM mkoa wa Njombe Bi,Amina Imbo amesema Chama hicho kinasisitiza amani,upendo na utulivu katika usimamizi wa miradi iliyopo ndani ya Chama na jumuiya ili kuongeza uchumi.

"Chama cha mapinduzi kinataka kazi za uhakika na sio kazi za kusema,kinataka mapato ili kuongeza uchumi wa Chama na jumuiya.Jumuiya zetu pia ziko nyuma kuongeza wanachama na ulipaji wa ada ,niawombe sana viongozi msimamie kuingiza wanachama na ulipaji wa ada pamoja na kusimkamia miradi ili chama kiwe na mapato kwenye jumuiya zetu"alisema Amina Imbo

Naye katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Njombe Erasto Ngole mgeni aliyealikwa katika baraza hilo amewataka wanawake kuondoa migogoro na kuto kuchukiana ili waweze kufanikisha miradi yao na kuwakabidhi jumuiya ya wanawake wa Chama hicho wilaya ya Wanging'ombe mota yenye thamani ya milioni 1,500,000 kwa ajili ya kufunga kwenye machine yao ya kusaga nafaka huku wanawake wa wilaya yay a Makete akiwakabidhi mifuko 50 ya saruji ili kukamilisha ukumbi wao unaojengwa wilayani Makete.

Baadhi ya wajumbe wa baraza hilo akiwemo Betrece Malekela ambaye ni mwenyekiti wa UWT wilaya ya Njombe na Anaupendo Gombela kutoka Wanging'ombe wameshukuru uongozi wao kwa kuutambulisha mradi uliridhiwa na baraza huku wakiamini kukamilika kwake kutasaidia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi wa jumuiya na kupunguza utegemezi.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...