Sunday, February 28, 2021

Wanaharakati 47 wakamatwa kwa makosa ya kufanya uasi Hong Kong


Polisi mjini Hong Kong imewakamata wanaharakati 47 wa kutetea demokrasia kwa makosa ya njama ya kufanya uasi ikitumia sheria iliyo na utata ya usalama wa kitaifa iliyopitishwa mwaka uliopita.


Wanaharakati hao wakiwemo wabunge wa zamani waliwahi kukamatwa mwezi Januari lakini baadae wakaachiliwa huru. Kulingana na taarifa ya polisi watu hao walikamatwa tena hivi karibuni na watafikishwa mahakamani Jumatatu. 


Wanadaiwa kukiuka sheria mpya ya usalama wa kitaifa iliyowekwa na China kwa kuhudhuria uchaguzi wa bunge ambao haukuwa rasmi katika eneo hilo lililo na utawala wa ndani. Kwa mujibu wa polisi mjini Hong Kong, washtakiwa hao wanajumuisha wanaume 39 na wanawake wanane walio kati ya umri wa miaka 23 na 64

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...