Friday, November 27, 2020

Serikali ya Ujerumani yaweka marufuku ya matumizi ya mifuko ya plastiki



Ujerumani imetangaza kuchukuwa hatua ya kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki kuanzia Januari 2022.

Kwa mujibu wa kanuni iliyopitishwa na bunge la serikali, mifuko ya plastiki yenye unene wa kati ya mikromita 15 hadi 50 itapigwa marufuku ispokuwa mifuko membamba inayotumika kwa ajili ya mboga.

Waziri wa Mazingira Svenja Schulze alisema kuwa badala ya mifuko ya plastiki, vikapu vya ununuzi na mifuko ya nguo inayoweza kuoshwa ni njia inaweza kutumika kama njia mbadala.

Wakfu wa Kulinda Mazingira Asili WWF, umesisitiza kuwa mifuko ni ishara inayoleta maana ya marufuku kwa mtazamo wao.

WWF inadai kwamba mifuko ya plastiki inayotumika katika ununuzi nchini Ujerumani inachukua asilimia moja ya matumizi yote ya plastiki, kwa hivyo matumizi ya plastiki yanapaswa kupunguzwa katika maeneo yote.

Matumizi ya mifuko ya plastiki yalipungua kwa asilimia 64 nchini Ujerumani baada kuanza kuuzwa mwaka 2015.

Mtu mmoja hutumia mifuko ya plastiki 24 ndani ya mwaka kwa kipimo cha wastani.

Plastiki huchukuwa miaka 400 kutoweka majini na miaka 800 kutoweka ardhini.  

 


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...