Monday, November 30, 2020
Waziri Mkuu Amaliza Mgogoro Wa Ardhi Kilosa
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemaliza mgogoro wa ardhi katika shamba la Chanzuru lenye ukubwa wa ekari 1,598 lililopo wilayani Kilosa, Morogoro kati ya Laizer Maumbi na Ameir Nahad kwa kuagiza likabidhiwe kwa Laizer ili aweze kuliendeleza kwa kulima mkonge.
Hata hivyo, Waziri Mkuu ameagiza eneo wanaloishi wananchi ndani ya shamba hilo kikiwemo kitongoji cha viwanja 60 na Chekeleni lihakikiwe na kupimwa ukubwa wake na kisha mkulima huyo akafidiwe eneo jingine na wananchi hao wasibugudhiwe.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Novemba 30, 2020) katika kikao chake na Makatibu Wakuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Wizara ya Ardhi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Viongozi wa mkoa wa Morogoro, wilaya ya Kilosa pamoja na Laizer. Kikao hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma.
"Viongozi wa Serikali simamieni na mratibu vizuri ili wananchi wanaoishi katika vitongoji vilivyomo ndani ya shamba hilo wasibugudhiwe waachwe waendelee kuishi na eneo lililobaki lisilokuwa na mgogoro apewe Laizer. Sehemu hiyo iliyopungua Laizer atafutiwe shamba jingine ili kufidia."
Amesema awali shamba hilo lilikuwa linamilikiwa na Sadruddin Rajabali ambaye alimuuzia Laizer ambaye aliamua kuachana na shughuli za ufugaji na kuanza kulima mkonge, na alipokuwa katika harakati za kubadilisha umiliki shamba hilo liliuzwa kwa mtu mwingine.
Waziri Mkuu amewataka watumishi wa sekta ya ardhi wilayani Kilosa wahakikishe suala hilo wanalisimamia vizuri ili haki itendeke kwa mkulima huyo kukabidhiwa shamba lake na watumishi waliohusika katika mgogoro huo wachukuliwe hatua.
Pia, Waziri Mkuu ameuagiza uongozi wa mkoa wa Morogoro uhakikishe inabainisha maeneo makubwa yote ambayo hayajaendelezwa na kutoa mapendekezo Serikalini.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Bw. Loatha Sanare ametumia fursa hiyo kumshukuru Waziri Mkuu kwa kumaliza mgogoro huo na kuahidi kwamba atasimamia utekelezaji wa maagizo na maelekezo yaliyotolewa.
Naye, Laizer ameishukuru Serikali kwa hatua iliyofikiwa ya yeye kukabidhiwa shamba hilo ambalo ndilo tegemeo lake kwa sasa, kwani aliuza mifugo yake yote na kununua shamba hilo ambalo amepanda mkonge.
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...