Friday, July 31, 2020

Meneja wa Harmonize afunguka kumng'oa msanii huyo

Meneja wa msanii Harmonize Dr Sebastian Ndege maarufu kama Jembe ni Jembe, amesema alikuwa anatuhumiwa na watu suala la kumchukua Harmonize kwenye menejimenti aliyokuwa ili aweze kufanya naye biashara.

Akizungumza kwenye Show ya SalamaNa inayoruka kila siku ya Alhamisi saa 3:00 usiku kupitia East Africa TV, Sebastian Ndege amesema kuna hisia tatu ambazo watu walikuwa na mashaka naye wakati anamchukua Harmonize.

"Kuna hisia tatu ambazo watu walikuwa wana mashaka mimi kuwa meneja wa Harmonize, moja ni kumfelisha dogo, mbili ni kumpoteza tatu ni kumtoa WCB, lakini ukweli ni kwamba mimi nilisubiri muda wake uishe ili niweze kufanya naye kazi" amesema Meneja wa Harmonize Dr Sebastian Ndege 

MWANAMKE AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUWANYANYASA KINGONO WATOTO 7 WA KIKE


Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Irene James mwenye umri wa miaka 36 amefikishwa mahakama ya hakimu mkazi Tabora akituhumiwa kuwafanyia unyanyasaji wa kingono Watoto saba wa kike  jirani zake wenye umri kati ya miaka 4 hadi 7 kwa kuwaingizia vidole sehemu za siri.

Akisoma maelezo ya kosa jana Julai 30,2020 Wakili upande wa Jamhuri Gladness Senya ameieleza mahakama kwamba mtuhumiwa anadaiwa kutenda makosa hayo saba ya udhalilishaji wa kingono wa hali ya juu kinyume cha kifungu cha 138 C (1) (a)na kifungu kidogo cha 2(b) cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019,Kitendo ambacho amekifanya kwa Watoto hao saba ambao majina yao yamehifadhiwa.

Mbele ya hakimu mkazi mkoa wa Tabora John Mdoe Wakili huyo wa Jamhuri Gladness Senya alidai kuwa mtuhumiwa aliwatendea makosa hayo watoto hao saba wa majirani zake kwa nyakati tofauti majira ya mchana terehe zisizojulikana kati ya mwezi Januari hadi Julai mwaka huu huko katika Kata ya Kanyenye manispaa ya Tabora.

Hata hivyo mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Tabora imemnyima dhamana mshitakiwa huyo kwa madai ya usalama wake na kwamba amepelekwa mahabusu mpaka pale kesi hiyo itakapotanjwa tena tarehe 13 mwezi Agust.

Kizimbani Kwa Kuwaingizia VIDOLE Sehemu za Siri Watoto Wadogo 7


Irene James (36) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora akituhumiwa kuwafanyia unyanyasaji wa kingono watoto 7 wa kike wenye umri kati ya miaka 4 hadi 7 kwa kuwaingizia vidole sehemu za siri

Mtuhumiwa huyo aliwatendea makosa hayo watoto wa majirani zake kwa nyakati tofauti majira ya mchana kati ya Januari hadi Julai mwaka huu katika Kata ya Kanyenye

Makosa hayo ni kinyume cha Kifungu cha 138 C (1) (a) na Kifungu kidogo cha 2(b) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019

Kutokana na Sheria hiyo Mtuhumiwa akipatikana na hatia atawajibika kwa kifungo kisichopungua miaka 25 na kisichozidi miaka 30 na pia atalipa fidia kwa kiwango kitakachoamriwa na Mahakama

Aidha, Mahakama hiyo imemnyima dhamana mshtakiwa kwa madai ya usalama wake na kwamba amepelekwa mahabusu mpaka pale kesi hiyo itakapotajwa tena Agosti 13

Wednesday, July 29, 2020

walinzi wa pwani wa Italia waokoa wahamiaji nje ya Libya

Walinzi wa pwani wa Italia wamesema leo wamewaokoa karibu wahamiaji 100 katika boti la mpira ambalo lilikuwa limejaa upepo nusu nje ya pwani ya Libya baada ya maafisa katika nchi nyingine kushindwa kuingilia kati.

Walinzi hao wa pwani wamesema boti hiyo ya mpira inayojazwa upepo ilionekana na ndege jana mchana katika kanda ya Libya ya utafutaji na uokoaji, SAR, bila ya injini na ikiwa na imejazwa upepo nusu.

Mamlaka ya Libya inayohusika na shughuli za utafutaji na uokoaji baharini haikuchukua uratibu wa operesheni za uokoaji kutokana na uhaba wa vifaa vya baharini, kikosi cha ulinzi wa pwani kimesema katika taarifa.

Wahamiaji 84, ambao ni pamoja na wanawake sita na watoto wawili walisafirishwa alfajiri ya leo kutoka katika boti yao ambayo ilikaribia kuzama kwenda katika meli ya Italia, ambayo ilikuwa inaelekea katika kisiwa cha Lampedusa.

Whozu Amuomba Tunda Msamaha Kwa Kumfumani Kitandani na Mwanaume Mwingine "Pokea Simu Rudi Nyumbani"


Sakata la Whozu Kumfumani Tunda Akiwa na Young D Kitandani Linaendelea, Whozu Amuomba Tunda Msamaha Kwa Kumfumani Kitandani na Mwanaume Mwingine "Pokea Simu Rudi Nyumbani"



VIDEO:

Picha : RAIS MAGUFULI AONGOZA WATANZANIA KATIKA MAZISHI YA RAIS MSTAAFU BENJAMIN MKAPA, LUPASO - MTWARA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka udongo kwenye kaburi la Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa katika Mazishi yaliyofanyika katika Kijiji cha Lupaso Masasi Mkoani Mtwara.

Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia Mjane wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa Mama Anna Mkapa akiweka udongo kwenye kaburi la Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa katika Mazishi yaliyofanyika katika Kijiji cha Lupaso Masasi Mkoani Mtwara.
Wanajeshi wa JWTZ wakiwa wamebeba Jeneza lenye Mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa kuelekea eneo la Makaburi kwa ajili ya Mazishi yaliyofanyika katika Kijiji cha Lupaso Masasi Mkoani Mtwara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Viongozi mbalimbali pamoja Wananchi wa Lupaso waliohudhuria katika Mazishi hayo ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa Lupaso Masasi mkoani Mtwara.
Mabregedia Jenerali wa JWTZ wakishuhudia Jeneza lenye Mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Marehemu Benjamin William Mkapa likishushwa kaburini Lupaso Masasi mkoani Mtwara.  PICHA NA IKULU.

KATIBU MKUU KILIMO KUSAYA AIPONGEZA TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA


Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya,akizungumza wakati wa kikao cha Makamishna na watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kilichofanyika Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya,akisisitiza jambo kwenye kikao cha Makamishna na watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kilichofanyika Jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt. Titus Kamani,akitoa neno kwenye kikao cha Makamishna na watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kilichofanyika Jijini Dodoma ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya.

Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Dkt.Benson Ndiege,akitoa taarifa wakati wa kikao cha Makamishna na watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kilichofanyika Jijini Dodoma ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya.
Afisa Ushirika Mkuu Bi.Veneranda Mugoba,akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya mara baada ya kumaliza kikao cha Makamishna na watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kilichofanyika Jijini Dodoma
Sehemu ya Watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika wakifatiliwa Hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya wakati wa kikao cha Makamishna na watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kilichofanyika Jijini Dodoma
.............................................................................................
Na.Alex Sonna,Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya ameipongeza Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kwa kuendelea kuimarisha na kuendeleza Sekta ya Ushirika nchini katika Nyanja za Kilimo, ufugaji, uvuvi, madini kwani sekta hizo zimeendelea kuchangia uchumi wa Taifa. 

Umuhimu wa Sekta hizo umetokana na kuwaunganisha wanachama katika uzalishaji, ukusanyaji mazao na upatikanaji wa masoko.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa kikao cha Makamishna na watumishi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika kilichofanyika Jijini Dodoma.

Kusaya amesema kuwa Serikali kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirika imefanya na inaendelea na jitihada mbalimbali za kuimarisha Ushirika nchini. 

Serikali imejikita katika kuimarisha Usimamizi na Utawala Bora katika Vyama vya Ushirika, kupitia Sheria ya Ushirika Na 6 ya Mwaka 2013 na Kanuni za mwaka 2015. 

Aidha Kusaya amesema kuwa usimamizi wa vyama unaanzia kwa mwanachama mwenyewe, juhudi zimeelekewa kwenye Mafunzo kwa viongozi wa vyama vya ushirika na wanachama wao kupitia mpango kazi uliotolewa naTume ya Maendeleo ya Ushirika.

 Pia serikali imeendelea kuchukua hatua kupitia vyombo vya usalama pale ambapo kuna wizi na ubadhilifu kwenye vyama. 

Nia ya serikali ni kurudisha Imani ya wananchi juu ya ushirika.

"Kwa hatua hizi kumekuwepo na mabadiliko chanya kwenye ushirika ambapo wananchi wameendelea kuanzisha na kujiunga katika vyama vya Ushirika wa aina mbalimbali ikiwemo vyama vya Ushirika wa Kilimo na Masoko (AMCOS) hatua ambayo itawezesha kupanua shughuli zao za uzalishaji mali na kuongeza kipato na hatimaye kupunguza umasikini. 

Pia, kwa sasa wakulima wanauza mazao yao kupitia mfumo wa Ushirika. Mfumo ambao umesaidia kuimarisha ubora wa mazao, kupatikana kwa bei za ushindani, uhakika wa vipimo vya mazao," alisistiza Bw.Kusaya

Mfumo wa Ushirika umesaidia upatikanaji wa takwimu sahihi za uzalishaji na uhakika wa mapato ya Halmashauri za Wilaya husika. 

Kwa kushirikiana na Soko la Bidhaa(TMX) na bodi za mazao, masoko ya mazao ya kimkakati na mazao mchanganyiko yameendelea kuimarika kama vile mazao ya tumbaku, choroko, kahawa, pamba, ufuta, kokoa na mbaazi yaliuzwa kupitia mfumo wa ushirika katika msimu wa 2019/20 kwa thamani ya Shilingi trilioni 2.7.

Awali akiwasilisha Mafanikio na changamoto za Tume, Mrajis wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Dkt. Benson Ndiege, ameeleza kuwa Vyama vyama vya Ushirika wa Akiba na Mikopo (SACCOS) vimeongeza mikopo kwa wanachama wake kutoka Shillingi Billioni 854 mwaka 2017 hadi kufikia Shillingi Trillioni 1.5 mwaka 2019 sawa na ongezeko la asilimia.

 Ushirika ni Sekta ambayo imekuwa na mchango mkubwa katika kutoa ajira kwa vijana na wananchi kwakuwa ni sekta ambayo inagusa maisha na uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
 
"Tume imeendelea kusimamia masuala ya ajira na kuwezesha wananchi Zaidi ya 90,090 kupata ajira katika vyama vya Ushirika zikiwemo ajira za kudumu, mkataba na za msimu hadi kufikia Juni 2020 ikilinganishwa na ajira 32,668 mwaka 2018," alisema Dkt. Ndiege

Kwa upande wake Kamishna Salome Tondi, amesema Sekta ya Ushirika inaweza kuendelea kukua na kuimarika kwa kuhakikisha elimu ya Ushirika inawafikia wengi katika jamii. 

Tondi alifafanua kuwa elimu ni moja ya nyenzo muhimu inayoweza kuwakomboa wanaushirika akitoa mfano wa masuala ya haki na wajibu wa wanaushirika, taratibu za uendeshaji wa Vyama vya Ushirika, taratibu za uchaguzi wa viongozi wa Vyama vya Ushirika na masuala mengine mengi.

Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kilikuwa ni fursa ya Makamishna kukaa kwa pamoja na watumishi wa Tume kufanya tathmini ya masuala mbalimbali ya Ushirika katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2017 baada ya uteuzi wao kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Ushirika Na.6 ya mwaka 2013.

Viongozi, Wananchi mbalimbali wajitokeza kuaga mwili wa mzee Mkapa


 Viongozi mbalimbali na wananchi wakipita kwa utaratibu maalum kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa hapa kijijini kwao Lupaso,Masasi mkoani Mtwara.



Tuesday, July 28, 2020

KIFO CHA MKAPA KIMENIUMIZA SANA –MWANA FA


MSANII wa muziki wa Bongo Fleva nchini Hamisi Mwinjuma alimaarufu Mwana FA amesema kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa kimemuumiza na ni pigo kubwa kwa wasanii kutokana na mchango wake wa kuanzisha Cosota.

Mwana FA aliyasema hayo leo wakati akizungumza katika wa ibada maalumu ya maombolezo iliyofanyika wilayani Muheza kwenye viwanja wa Jitegemee na kuongozwa na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo  na wananchi wakiwemo viongozi wa dini.


Alisema kutokana na msiba huo mzito ndio maana akaamua kuungana na wananchi wa wilaya ya Muheza katika halfa hiyo kwa sababu katika kipindi chake ndio miongoni mwa taasisi aliyonzisha katika kusimamia haki za wasanii. 


Msanii huyo alisema Cosota ni taasisi inayoshughuli na haki miliki za wasanii tokea ilipoanzishwa 1996 na imekuwa na mchango mkubwa kwani kabla ya hapo kazi za wasanii zilikuwa huwezi kumpeleeka mtu mahakamani.

Hata hivyo alisema kutokana na hilo wana mshukuru Hayati Mkapa kutokana na mambo makubwa aliyowafanyia wasanii hapa nchini ambayo yamekuwa na tija kubwa kwao .

Sunday, July 26, 2020

Live : MISA YA KUAGA MWILI WA HAYATI BENJAMIN WILLIAM MKAPA

Tazama Matangazo ya moja kwa moja Misa ya Kuaga mwili wa Hayati Benjamin William Mkapa.

Rich Mavoko Acha Unyonge Maisha ni Vita, Amka


UNAPOTAJA jina la Q-Chillah kwa mashabiki na wadau wote wa Bongo Fleva na hata ambao siyo wapenzi wa muziki huo hapa Tanzania wanalijua vizuri jina hilo na hata muhusika mwenyewe.

Chillah ni mmoja wa wasanii wenye vipaji vikubwa hasa katika suala la sauti na utunzi, alikuwa anakuwa vizuri kisanii lakini hapo kati anajua mwenyewe alichokifanya kikamfanya apotee kwenye 'game', kwa sasa anapambana kurejea lakini bado inaonekana ana mtihani mkubwa mbele yake.

Mtihani huo unatokana na sababu kadhaa ikiwemo yeye mwenyewe kusababisha mvuto wake kisanii kupotea na changamoto ya vijana wapya kwenye muziki, licha ya kuwa bado ana kipaji cha hali ya juu lakini huyo pekee haiwezi kumfanya kurejesha heshima kama aliyokuwa nayo miaka ya nyuma.

Pamoja na lawama nyingine kadhaa lakini ukweli ni kuwa kwa asilimia kubwa Chillah ni mfano mzuri wa wasanii wengi wenye vipaji vya ukweli vya kuimba ambao wamechangia kujipoteza wao wenyewe au wamejiwekea vizingiti vya kushindwa kupiga hatua kubwa kimafanikio.

Najua siyo lazima wasanii wote wawe kama Diamond Platnumz kimafanikio lakini kuna levo fulani ambayo mtu unamuona fulani anastahili kuwa sehemu fulani kisha anakuwa hayupo hapo unapoona anastahili.

Watu wengi wa aina hiyo wakishaanza kupotea aku wakipata wakati mgumu wanaanza kutoa lawama, fulani na fulani ndiyo waliosababisha wakafeli kimuziki wakati wanasahau kuwa muziki ni kama vita.


Kiuhalisia muziki ni vita kama ambavyo maisha ya kawaida yalivyo ni vita, bila kupambana utaishia kuwa mtu wa lawama kila siku.

Kwenye maisha usipoamka na kupigana ni rahisi kupoteza mwelekeo na mwisho wake ni kuanza kulaumu fulani ananibania au kanikwamisha. Pambana ili kizazi chako kije kikusifie kuwa ulipigana kwa ajili yao.

Bila kuzunguka sana Richi Mavoko ni bonge moja la msanii ambaye kama utafatilia miaka kadhaa ya nyuma alikuwa akifananishwa na levo za kina Diamond na Ali Kiba, hata kama alikuwa hajafikia ubora wa juu kimafanikio lakini kipaji chake kilikuwa wazi na kilionekana.

Mavoko alikuwa akitoa video kali, nyimbo kali na hata kwenye jukwaa alijua kazi yake vizuri.7

Ninaposema Richard Martin au Mavoko anajua kuimba ninamaanisha, ndiyo maana hajawahi kuharibu 'chorus' hata moja ambayo ameshirikishwa.

Aliposainiwa na WBC wengi wakaona kama anajimaliza kwa kuwa bosi wake anakuwa ni yule ambaye alikuwa akifananishwa naye, bahati mbaya mambo hayakwenda kama alivyotarajia.

Kipindi anasainiwa WCB niliamini halikuwa jambo sahihi, bali mtazamo wangu niliamini alitakiwa kutafuta timu sahihi nyuma yake imuongoze katika tifina na mipango yote ya muziki, levo aliyokuwa nayo haikuwa ya kusainiwa na WCB ambapo wengi wao kimuziki ni kama alikuwa amewazidi au wapo levo naye moja.

Lakini kusaini kwake WCB haikuwa kosa sana kwa kuwa kwenye maisha kuna njia nyingi za kutokea. Sasa baada ya kuondoka hapo, inaonekana kuna sababu za kimkataba zimembana ikiwemo kutumia akaunti ya YouTube aliyokuwa akiitumia na vitu vingine kadhaa.

Akafungua akaunti mpya ya YouTube alitoa nyimbo kadhaa ambazo nazo hazijafika mbali, ghafla amepotea kusikojulikana kwenye uso wa Bongo Fleva.

Sijui kilichopo nyuma ya pazia kwake kwa sasa lakini kiuhalisia anaon yesha unyonge sana wa kushindwa vita mapema, kwa picha ya nje inaonyesha ni kama Rich Mavoko amekata tamaa baada ya gia zake kutofanikiwa.

Mavoko ni mzoefu, amepitia milima mingi kabla ya kuwa staa mkubwa, kabla ya kusainiwa na WCB alikuwa ameshakuwa msanii mkubwa, najua lengo la kusainia lilikuwa ni kutoka daraja moja kwenda lingine, kama imeshindikana arudi nyuma na kutafakari alipokosea ili ajipange.

Ukitazama nyimbo alizokuwa akizitoa kabla ya kusainiwa na hawa wakati yumo ndani ya lebo unaona ni mtu ambaye anatoa nyimbo zinazoeleweka na zinazohitajika sokoni.

Lakini ukipitia akaunti yake mpya ya YouTube ya Billionea Kid ukasikiliza na kutazama nyimbo zake zilizomo humo na kisha kwenda kufananisha na zile alizokuwa akiimba huko nyuma utakubaliana nami kuwa 'stresi' za muziki zinampelekea pabaya.

Ushauri wangu ni kuwa hawezi kufanikiwa akiwa peke yake, atafute watu sahihi nyuma yake ili wamuonyeshe njia sahihi ili yeye aongeze nguvu kwenye kutengeneza muziki, ajitafute tena arejee kwenye ubora wake.

Tofauti na hapo namuona anaelekea kuwa kwenye kundi la wale wasanii ambao kila siku huwa tunasema ni wakali lakini hawana 'impact' kwenye Bongo Fleva, yaani wapowapo tu kawaida!

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKAGUA MAANDALIZI YA KUAGWA MWILI WA MZEE MKAPA UWANJA WA UHURU


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi ya Mazishi ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu , Benjamin William Mkapa wakati alipokagua maandalizi ya Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam  Julai 25, 2020 ambapo  kutafanyika Ibada ya kumwombea marehemu na  kuaga mwili kitaifa kuanzia kesho. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)




Faida za kuishi bila michepuko katika maisha


Kama wewe ni mtu ambaye huchepui, nakupongeza sana na hamna ambacho unakikosa kutoka kwa mweza wako. Watu wengi wanafikiri kuna amani au furaha ambayo wataipata wakichepuka, ukweli ni kwamba kila siku wanazidi kukimbizana na wanawake wapya na hawakipati wanachokipata. Baki njia kuu, hata kama kuna foleni utafika unakoenda kwa amani na bila magonjwa.

Zifuatazo ndizo faida za kubaki njia kuu.
 Utapata amani moyoni
·Utaepukana na magonjwa
· Utakuwa na Furaha isiyo elezeka
·Utajimini zaidi
 Mke wako atakupenda zaidi (atajua umeacha kuchepuka hata usipomwambia)
· Utafurahia tendo la ndoa zaidi (Michepuko haina chochote cha zaidi ambacho
·mkeo au mumeo hana)Utasonga mbele kimaendeleo
·Utapata muda mwingi wa kuwa na familia yako

Saturday, July 25, 2020

Madhara ya kukaa na mkojo kwa muda mrefu

Utakubaliana na mimi kwamba, kitendo cha mtu kubanwa na haja ndogo siyo kitu cha hiyari kwamba sasa mtu anaamua ngoja nibanwe na mkojo, hili ni jambo la asili na ni matokeo ya vyakula, matunda au vinywaji tunavyotumia. Kwa lugha nyingine tumekuwa tukiita kuwa ni wito wa asili au nature's call.

Yawezekana mtu akawa katika mkutano, safarini, akawa katika mitandao ya kijamii anachati au popote pale akiwa anafanya jambo fulani na kutokana na jambo hilo, mtu akaendelea kujibana na kutokwenda kuyapunguza maji haya kutoka katika kibofu cha mkojo kwa kutoa kipaumbele kwa shughuli anayoifanya kuliko kusikiliza kwanza wito huu wa asili. Mambo haya tunayafanya sana, utasikia, mkojo umenibana kweli, ila ngoja nimalizie hii kazi halafu niende kujisaidia, hivi ndivyo watu wengi wanafanya.

Kutokana na vyakula na vinywaji tunavyotumia, kibofu cha mkojo huanza kujaa mkojo, mkojo unapofikia karibu mililita 50 mpaka 500 mtu huanza kuhisi hitaji la kwenda kukojoa. Kibofu cha mkojo kimezungukwa na vigunduzi asili (Receptors) vinavyopeleka taarifa katika Ubongo kuonyesha kuwa kibofu cha mkojo kimekaribia au kimejaa, baada ya taarifa hizi kufika katika ubongo, ubongo unatoa taarifa katika kibofu cha mkojo ili kiweze kushikilia mkojo huo kwa kuikaza misuli maalumu (Sphincters) mpaka hapo muda wa wewe kwenda kukojoa utakapofika.

Kibofu cha mkojo hufanya kazi kwa mfumo wa kujiendesha wenyewe yaani, automatic, kitendo cha mtu kupuuzia kwenda kukojoa husababisha Ubongo upate usumbufu wa taarifa za kujaa kwa kibofu cha mkojo na kwa kuwa Ubongo nao hutuma taarifa katika kibofu cha mkojo kusema kuwa mkojo uendelee kushikiliwa mpaka muda muafaka utakapofika, itafika kipindi uwezo wa ubongo kutoa taarifa hizi na pia uwezo wa vigunduzi asili (Receptors) vilivyoko katika kibofu cha mkojo kupoteza uwezo wake tena wa kufanya kazi hizo au uwezo kuwa mdogo. Matokeo yake ni mtu siku kweli anahitajika kuvumilia kidogo ili afike sehemu inayostahihi kujisaidia, lakini hawezi tena na kujikuta muda mdogo tu….mtu tayari kaloanisha nguo yake.

Mpenzi msomaji, mtu kujibana na kupuuzia kwenda kukojoa husababisha uwezo wa kibofu cha mkojo kujitawala (control) upotee. Pia kama uwezo wa neva zinazopeleka taarifa kwenye ubongo kuhusu mabadiliko/ujazo wa kibofu cha mkojo zitaharibika, basi misuli maalumu ya kubana mkojo (sphincter) itashindwa kuachia na matokeo yake mtu ataendelea kukaa na mkojo katika kibofu chake kwa muda mwingi zaidi kitu ambacho ni hatari kwa afya yake. Endapo mkojo huu utashindwa kutoka, utatengeneza mazalia ya bakteria na kukusababishia magonjwa ya kibofu (bladder infection). Magonjwa ya kibofu cha mkojo ni pamoja na U.T.I (Urinary Tract Infections), pia huweza kusababisha magonjwa ya figo na mchafuko wa damu, bacteremia.

Kuna hali huwa inajitokeza kwa baadhi ya watu, yawezekana alikuwa kabanwa na mkojo au alikuwa hajahisi kwenda kukojoa, ila akinywa maji au akisikia sauti ya maji yanachuluzika mfano maji yakitoka bombani, basi atahisi kwenda kukojoa.

Mpenzi msomaji, ni vyema tukawa wasikivu pale mtu unapobanwa na mkojo, hii ni kwa ajili ya afya ya kibofu chako cha mkojo lakini pia ni kwa ajili ya afya yako kwa ujumla. Kama unalo tatizo, usisite kuonana na wataalamu wa afya.

Watu wapatao 20 wameuawa katika jimbo la Darfur

Watu waliojihami kwa bunduki wamewauwa watu wasiopungua 20, wakiwemo watoto nchini Sudan. Watu hao walikuwa kwenye mashamba yao katika jimbo la Darfur linalokumbwa na machafuko.

Kwa mujibu wa kiongozi wa kikabila Ibrahim Ahmad, idadi ya vifo inaweza kuongezeka kwasababu watu wengine waliojeruhiwa wamo katika hali mbaya.

Kiongozi huyo wa kikabila ameeleza kwamba miezi miwili iliyopita serikali iliandaa mkutano kati ya wamiliki asili wa ardhi na watu walioyachukua mashamba yao wakati wa vita vya muda mrefu katika jimbo la Darfur ambapo makubaliano yalifikiwa kwamba wamiliki halali wa ardhi hiyo wangerejea kwenye mashamba yao lakini kilichofuatia ni mauaji hayo.

Mauaji hayo yalitokea katika kijiji cha Aboudos, kilomita 90 kusini mji mkuu wan jimbo la Darfur Kusini.

Picha Hii Inazima Uzushi Kwamba Mwanamuziki Meek Mill Anatoka Kimapenzi na Kim Kardashian

Wiki hii Kanye West aliweka wazi kwamba yupo kwenye mchakato wa kumpa talaka mkewe Kim Kardashian, akidai kwamba alitoka kimapenzi Meek Mill kipindi wamekutana kwenye mchakato wa mabadiliko ya sheria za magereza.

Usiku wa kuamkia leo imesambaa picha hii (Picha Juu) ikiwaonesha Meek Mill na Kim Kardashian wakiwa pamoja na watu wengine kwenye kikao, hivyo kuonesha kuwa hakukuwa chochote kati yao.

Waandamana Kupinga Mshindi Kura Za Maoni Ubunge


Mbunge wa Jimbo la Magomeni akabidhi Basi Jimboni - ZanziNewsIkiwa zimepitia siku kadhaa baada ya kunalizia kwa uchaguzi wa ngazi ya jimbo wa kupendekeza majina ya wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) watakaogombea ubunge na uwakilishi kwenye uchaguzi ujao mapema mwezi Oktoba.

Wakazi wa jimbo ka Magomeni visiwani Zanzibar wameandamana mpaka nyumbani kwa mshindi wa uchaguzi huo Jamal Kassim kwa lengo la kupinga ushindi wake baada ya uchaguzi  uliofanywa na wa wajumbe chama.

Waandamaji walioandama na ngoma na mabango wamesema hawezi kukubari Jamali kupewa nafasi ya kuongoza tena kwenye jimbo hilo aliloliongoza kwa miaka kadhaa.

Bado mchakato wa ndani ya chama wa kutafuta wagombea unaendelea mpaka pale majina kutoka hamashauri kuu ya chama hicho yatakapoletwa kwenye ngazi za awali za chama kwa ajili ya kutagaza kwama wagombea rasmi wa chama hicho.

CHANZO: JamiiForums
Source

Hizi ndizo Sababu Za Uke Kutoa Harufu Mbaya

Ni matumaini nyote mnaendelea vyema, nami alhamdulillah ala kul Hali naendelea vyema
Leo naona ni bora tukazungumzia tatizo la kutokwa na harufu mbaya ukeni maana watu wengi hudhani kuwa na harufu mbaya itokayo ukeni ni matokeo ya uchafu tu na ndio maana wanaume huwachamba wake zao kuwa hawajuhi kujisafisha na kufanya wanawake kuongeza jitihada katika kujisafisha ukeni, leo napenda kuzungumzia tatizo hili linalowasumbua wanawake wengi na kuwaumiza kichwa kutokana na kwamba lina athari kubwa sana kwani hufanya ndoa zao kudumaa NK,


~Kitaalamu Hali ya mwanamke kutokwa na maji yenye rangi nyeupe au njano ni Hali ya kawaida na sio tatizo Lakini endapo maji yanatoka yapo katika Hali ya ute mzito wenye rangi nyeupe au kahawia na yanatoa harufu kali au kuwasha hapo una tatizo
~Majimaji au ute unaoteleza kutoka sehemu za siri ni njia inayowezesha viungo vya uzazi vya mwanamke kujisafisha au kutoa uchafu wa seli zilizokufa na mabaki ya damu ya hedhi nnje ya mwili pia huvikinga viungo vya uzazi dhidi ya maaambukizi ya bacteria
~Kwa kawaida huwa hayatoi harufu na huwa hayawashi na huwa na rangi nyeupe au njano pia huwa na asidi ya LACTIN ambayo huzuia bacteria kuzaliana
~Mwanamke hutoa kiasi cha grams 2 za seli zilizokufa kutoka kwenye mji wa kizazi na grams 3 za ute mwepesi kila siku, kiwango hicho kinaweza kuongezeka au kupungua kutegemeana na mzunguko wa hedhi pia Kuna wakati ute huwa mwepesi na unaovutika na Kuna wakati pia huwa mzito wa rangi ya njano hautoi harufu


VISABABISHI VYA TATIZO HILI
Sababu za kutokwa na uchafu ukeni una vyanzo vingi sana vifuatavyo ni vyanzo vya tatizo hili

1. BACTERIA VAGINOSIS
Chanzo halisi cha ugonjwa huu hakijafanikiwa kuwa wazi,kinachotokea ni kuongezeka kwa ghafla kwa idadi ya ya bacteria hawa na kubadilisha uwiano wa kawaida katika mazingira ya uke, wanawake wenye wapenzi wengi na wanaofanya mapenzi kwa njia ya mdomo Wana hatari ya kupata tatizo hili

2. TRICHOMONAS
Maambukizi haya hutokana na Aina ya protozoa wa seli moja, trichomonas mara nyingi huambukizwa kwa njia ya ngono, protozoa huyo huweza kukaa kwenye unyevu unyevu kwa Muda wa saa 24 Bila kufa hivyo kufanya taulo na chupi zisizokauka kuwa chanzo kingine cha tatizo hili

3. YEAST INFECTION
Kwa kawaida Kuna kiwango kidogo cha yeast (candida albicans) katika uke, huwa tunasema Kuna maambukizi pale kiwango kinapozidi Hali ambayo inatokana na kubadilika kwa Hali ya hewa ukeni (Change in the PH balance of vagina)

Maambukizi ya yeast hayatokani na tendo la ndoa.

Mambo ambayo huchangia tatizo hili ni:

MATUMIZI YA DAWA ZA KUZUIA MIMBA,
MAWAZO,
UJAUZITO,
KISUKARI
MATUMIZI YA ANTIBIOTICS


4. VAGINAL OR CERVICAL CANCER,
Mtu anapokua na kansa ya uke, hutokwa na maji ya harufu mbaya, hivyo ni heri uwe unafanya check up ili kujua Afya yako na kwakuwa cancer ya kizazi inapona hivyo ni vema ukatambua mapema uanze tiba

5. SEXUAL TRANSMITTED DESEAS (STDs)
Kuna baadhi ya magonjwa kama vile KASWENDE NA KISONONO yanasababishwa na ngono na kuwa chanzo cha tatizo hili.

6. POOR HYGIENE
Tatizo la kutokwa na maji wakati mwingine husababishwa na muhusika kua mchafu yan mtu unaoga kwa siku mara moja, chupi moja ndio hiyo hiyo mwaka mzima, pads unakaa nayo saa 24, ukienda kukojoa ujitawadhi na maji masafi hivyo unategemea utakua salama kweli??? Zingatia usafi mrembo

DALILI ZA TATIZO HILI
Kutokwa na uchafu ukeni unaoambatana na kuwashwa au kutokewa na vipele, hii hutokana na kuharibika kwa uwiano wa bacteria hivyo kuwa na madhara na uchafu hutoka wa aina tofauti hapa chini nitaelezea kila Aina ya uchafu na dalili zake.

1. UCHAFU WENYE RANGI YA KAHAWIA AU DAMU
Huu uchafu huonyesha dalili ya kuwa mzunguko wako wa hedhi umevulugika na wakati mwingine ni dalili ya kansa ya kizazi, mwanamke anayepata tatizo hili hutoa damu nyingi kuumwa sana nyonga

2. UCHAFU WENYE RANGI YA NJANO /KIJANI WENYE HARUFU MBAYA
Endapo uchafu huo utatoka kama povu na wenye rangi ya kijani au njano na ukiambatana na harufu mbaya huwa ni dalili ya ugonjwa wa trichomonas, maambukizi ya parasite yanatokana na ngono zembe, dalili Yake nyingine ni maumivu na kuwashwa wakati wa kutoa haja ndogo.

3. UCHAFU MWEUPE MZITO KAMA JIBINI
Mara nyingi hii huwa ni dalili ya maambukizi ya fangasi(YEAST INFECTION) na dalili nyingine huwa ni kuvimba sehemu ya nje ya siri, kuwashwa na kupata maumivu makali wakati wa tendo la ndoa.

4. UCHAFU MWEUPE/KIJIVU WENYE HARUFU YA SAMAKI
Uchafu wa Aina hii ni dalili ya maambukizi ya bacteria vaginosis, mara nyingi mwenye tatizo hili husikia muwasho na maumivu sehem ya nnje ya uke.

5. MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KUEPUKA TATIZO HILI NA TIBA YAKE
Matibabu ya tatizo hili hufanyika baada ya kugundua chanzo cha tatizo na mara nyingi tiba Yake ni tiba ya dawa za antibiotics kitu ambacho si tiba nzuri zaidi kwasababu tatizo huweza kujirudia kila wakati na kusababisha matatizo zaidi hivyo tiba nzuri ni kuepuka hili tatizo kwa kufanya yafuatayo

👉EPUKA KUJIINGIZA VIDOLE MARA KWA MARA UKENI
👉EPUKA MATUMIZI YA DAWA ZA ANTIBIOTICS MARA KWA MARA
👉PUNGUZA KULA VYAKULA VYENYE SUKARI NYINGI
👉TUMIA PADS ZENYE ANIONS NI SALAMA KWA AFYA YAKO
👉SAFISHA VIZURI NGUO ZAKO ZA NDANI NA UZIANIKE JUANI NA HATA                   KUZIPIGA PASI
👉KUNYWA JUICE YA APPLE,STRAWBERRY, NANASI KWA WINGI
👉EPUKA KUFANYA NGONO ZEMBE
👉HAKIKISHA UNAJISAFISHA KILA UNAPOMALIZA KUJISAIDIA
👉EPUKA KUTUMIA DAWA ZA KUZUIA MIMBA
👉EPUKA KUTUMIA SABUNI AU VITU VYA MANUKATO UKENI,

NOTED :
Wanawake wengi mnapenda kutumia baadhi ya dawa kwa lengo la kuongeza vionjo  kwenye mapenzi pia kufanya uke kunukia vizuri, au kukaza uke rafiki uke una harufu nzuri sana ambayo haipatkan kokote hivyo haihitaji kuwekwa pafyumu Wala kusafishwa kwa sabuni za kemikali kwani huwa panajisafisha hivyo ni heri ukaacha kutumia kwani madhara Yake hayaonekani sasa ila baada ya Muda huonekana.

Mkapa Azuia Membe kupokelewa Lindi

Kiongozi mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe ametangaza kusitishwa kwa shughuli za kumpokea mtiania ya kugombea wa urais wa chama hicho  Bernard Membe mkoani Lindi kutoka na kifo cha Rais msaafu Benjamin Mkapa.

Zitto ametangaza maamuzi hayo kupitia ujumbe aliotuma kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter leo Julai 25, 2020 na kusema chama hicho kinaendelea kutoa pole kwa familia ya Mkapa na taifa kwa ujumla.

"Tumeahirisha shughuli yetu ya kisiasa Leo ya Wananchi wa Lindi kumkaribisha Bernard Membe nyumbani ili kupisha shughuli za maombolezo ya Rais Mstaafu Benjamin W Mkapa. Tunaendelea kuwapa pole Watanzania na Famiia ya Rais Mkapa kwa msiba mzito huu. Maisha ya Mkapa kiuongozi ni Mafunzo" ameandika Zitto.

Rais Mkapa alifariki usiku wa kuamkia Julai 24,2020 akiwa hospitali jijini Dar es salaam alikikuwa akipatiwa matibabu na anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatano julai 29,2020 Mkoani Mtwara.

Friday, July 24, 2020

Serikali Yatoa Ratiba Ya Mazishi Ya Mzee Mkapa......Waziri Mkuu Asema Ataagwa Kitaifa Uwanja Wa Uhuru Julai 28


WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa ataagwa Kitaifa Jumanne Julai 28 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na atazikwa kijijini kwao Lupaso, Masasi mkoani Mtwara Jumatano, Julai 29, 2020.


"Mwili wa mzee wetu, kiongozi wetu Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu utaanza kuagwa kuanzia Jumapili, Julai 26, 2020 katika Uwanja wa Uhuru ambapo saa 4.00 asubuhi kanisa Katoliki litaongoza ibada na baada ya ibada waombolezaji wataanza kuaga."


Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Ijumaa, Julai 24, 2020) wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Makazi ya Waziri Mkuu Oysterbay jijini Dar es Salaam. Ametumia fursa hiyo kuwasihi wanafamilia na Watanzania waendelee kumuombea marehemu kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu yote ni mapenzi yake.


Amesema zoezi la kuaga mwili litafanyika kwa muda wa siku tatu ambapo wakazi wa jiji la Dar es Salaam pamoja na wananchi kutoka maeneo mengine wataanza kuaga kuanzia Jumapili, Julai 26 hadi Jumanne, Julai 28 siku ambayo mwili utaagwa Kitaifa.


Waziri Mkuu amesema kwa siku ya Jumanne, Julai 28, 2020 zoezi la kuaga mwili litanyika kuanzia asubuhi hadi saa 6.00 mchana na ifikapo saa 8.00 mchana mwili utasafirishwa kwenda Masasi kwa kupitia uwanja wa Ndege wa Nachingwea na mazishi yatafanyika Jumatano, Julai 29, 2020.


Mapema, Waziri Mkuu alikwenda nyumbani kwa aliyekuwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa Masaki jijini Dar es Salaam na kutoa pole kwa Mama Anna Mkapa mjane wa marehemu pamoja na familia, kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Serikali.


Amesema "Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Serikali tumepokea taarifa za msiba wa mzee wetu, kiongozi wetu Rais wa Awamu ya Tatu kwa masikitiko makubwa. Nawasihi muendelee kuwa watulivu na wavumilivu katika kipindi hiki kigumu kama alivyosema Rais wetu Mheshimiwa Dkt. Magufuli."


Kufuatia kifo hicho kilichotokea usiku wa kuamkia leo, Rais Dkt. Magufuli ametangaza siku saba za maombolezo ya Kitaifa kuanzia leo Ijumaa, Julai 24, 2020 na katika kipindi chote cha maombolezo bendera zote zitapepea nusu mlingoti.


Akitangaza kifo hicho kwa Watanzania kupitia vyombo vya habari usiku wa kuamkia leo Rais Dkt. Magufuli kwa masikitiko makubwa alisema Rais wa Awamu ya Tatu, Mhe. Benjamini William Mkapa amefariki dunia hospitalini jijini Dar es Salaam ambako alikuwa akipatiwa matibabu.


Rais Dkt. Magufuli amewataka Watanzania wote wawe watulivu na wastahimilivu baada ya kupokea taarifa za kuondokewa na mpendwa wao Mhe. Benjamin William Mkapa. "Kwa masikitiko makubwa tumepata msiba mkubwa, Mzee wetu Benjamin William Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu amefariki dunia."


Aliongeza kuwa " Amefariki dunia katika hospitali jijini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa, niwaombe Watanzania tulipokee hili, tumepata msiba mkubwa na tuendelee kumuombea Mzee wetu Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa, ambaye ametangulia mbele za haki."


Mwisho.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU


China yalipiza kisasi kwa Marekani, yaiamuru kufunga ubalozi wa Chengdu


China hii leo imeiamuru Marekani kuufunga ubalozi wake mdogo katika mji wa magharibi wa Chengdu, ikilipiza kisasi cha kufungiwa wake ubalozi mdogo wa mjini Houston mapema wiki hii.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya China Wang Wenbin, amesema Marekani ndiyo ya kulaumiwa.

Utawala wa Rais Donald Trump uliamuru Jumanne kufungwa kwa ubalozi huo mdogo wa China mjini Houston katika saa 72, ukidai kwamba maafisa wa China walijaribu kuiba data kutoka katika Taasisi ya sayansi ya Matibabu ya Chuo Kikuu cha Texas A&M.

 Marekani imeishutumu China kwa wizi huo wa taarifa za kitaaluma, siku moja baada ya wizara ya sheria kuwafungulia mashtaka raia wawili wa China kwa madai ya kudukuwa kampuni kadhaa za Marekani na kujaribu kuiba utafiti wa chanjo dhidi ya virusi vya corona.

Pumzika kwa Amani huku ukitambua ulipanda Mbegu njema maishani mwangu- Makonda

Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Poul Makonda naye ameoneshwa kuguswa na kifo cha Rais Mstaafu Benjamin Wiliam Mkapa na kusema kuwa yeye ni mmoja ya vijana walionufaika na maisha yake wakati alipokuwa hai.

"Mimi ni mmoja wa vijana tulionufaika na Maisha yako hapa Duniani, Pumzika kwa Amani huku ukitambua ulipanda Mbegu njema maishani mwangu. REST IN ETERNAL PEACE BABA"-Aliyekuwa RC DSM, Paul Makonda

ATUPWA JELA KWA KUMTUKANA MAMA YAKE INSTAGRAM

MKAZI wa Mbuyu Zanzibar, Daurat Salum Suleiman amehukumiwa kulipa faini ya Sh milioni tano au kutumikia kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya kumtusi mama yake mkubwa kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.

Suleiman alihukumiwa kifungo hicho katika Mahakama ya Ilala jijini Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Martha Mpaze.

Hakimu Mpaze alisema upande wa mashitaka ulipeleka mahakamani hapo mashahidi sita kuthibitisha mashitaka ya udhalilishaji kwa njia ya mtandao na kwamba wameweza kuthibitisha mashitaka hayo bila kuacha shaka lolote.

Alisema baada ya kusikiliza mashahidi wa alibaini maneno aliyoandika mshitakiwa yalikuwa na lengo la kumdhalilisha mlalamikaji Shabaha Said Chondoma maarufu kwa jina la teacher licha ya kwamba Suleiman alikataa kutenda kosa hilo wakati akijitetea.

"Baada ya kupitia ushahidi wa mashahidi sita na vielelezo, mahakama inakutia hatiani kwa   kumdhalilisha kimtandao Chondoma hivyo, utatakiwa kulipa faini ya Sh milioni tano na akishindwa kulipa fedha hiyo atatumikia kifungo cha miaka miwili jela," alisema Hakimu Mpaze.

Source

Thursday, July 23, 2020

Sheikh wa mkoa wa Dar Es Salaam: Makonda amelikoroga mwenyewe, siwezi kumpigia kampeni, ili iweje


Sheikh mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Sheikh Alhadj Mussa Salum amekanusha taarifa kuwa aliwapigia Waislam wa Kigamboni kumchagua aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda kuwa Mbunge katika kura za maoni Jimbo la Kigamboni.


Akiongea na Waandishi wa habari ameeleza kuwa kuna ujumbe ukiokuwa unatembea ukieleza kuwa yeye aliwapigia simu Waislam wote Kigamboni ili kumpigia kura Makonda.


"Mimi siwezi kufanya hivyo nilimsaidia na kumuombea wakati akiwa mkuu wa mkoa, sisi tunafanya hivyo tukijua anamsaidia Mh. Rais na sisi tunafanya kazi na kiongozi yetote, Makonda alilikoroga mwenyewe "


Mbali na hilo Sheikh wa Kigamboni pia amefafanua kuwa yeye akiwa kama kiongozi Kigamboni hakuna taarifa kama hizo.

Waziri Simbachawene: Matukio Ya Uhalifu Nchini Yamepungua

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. George Simbachawene (MB) amesema Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza matukio ya uhalifu ikiwa ni pamoja na kuziba mianya ya uingizaji na usambazaji wa dawa za kulevya, usafirishaji wa binadamu na uhalifu unaovuka mipaka.

Waziri Simbachawene amesema hayo leo jijini Dodoma, wakati akifunga kikao kazi cha Maafisa Wakuu Makao Makuu, Makamanda wa Polisi wa Mikoa na Vikosi kilichofanyika kwa muda wa siku tatu, kikao ambacho kililenga kufanya tathimini ya utendaji wa kazi za Jeshi hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amesema kuwa, Vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga imara kuhakikisha vinaimarisha hali ya usalama hususani kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu huku akiwataka wananchi pamoja na wanasiasa kutimiza wajibu wao kwa kutojiingiza kwenye vitendo vya uvunjifu wa amani.



Source

Tambiko Lamuibulia Zengwe Nasari


SIKIA hii hapa; tambiko limemuibulia zengwe aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joshua Nassari, uhondo wa stori unakuja.

Nassari ambaye hivi karibuni alikihama Chadema na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), alichukua fomu za kuomba uteuzi wa ubunge ndani ya CCM kwenye jimbo lake la zamani ambapo aliipeleka kwa Wazee wa Mila maarufu kama Washili ili ikatambikiwe.

Mbali na fomu hiyo kupelekwa huko, Nassari aliichukua pia hadi kanisani na kuwakabidhi wachungaji nao waiombee apate kushinda kwenye kura za maoni CCM ili baadaye awanie ubunge kupitia chama hicho.

Mara paap, Nassari aliangukia pua kwenye kura hizo za maoni kwa kupata kura 26 na mshindi kuibuka Dk. John Pallangyo.Baada ya matokeo hayo, zengwe la tambiko lilipata nguvu kwenye mitandao ya kijamii ambapo wengi walimponda mwanasiasa huyo kijana kwa kujihusisha na imani za kale.


"Kijana unaamini tambiko kwenye kitu makini kama uchaguzi, huku ni kufilisika kimawazo," aliandika mtu mmoja kwenye ukurasa wake wa Instagram.Hata hivyo, jicho la Amani Mtandaoni limebaini kuwa, Nassari ni miongoni mwa wagombea ubunge ndani ya CCM aliyesemwa vibaya baada ya kushindwa kura za maoni.


Uchunguzi umebaini kuwa, hayo yanatokana na mitazamo kinzani baina ya wafuasi wa Chadema ambao wanamuona Nassari kama msaliti wa chama na CCM ambao wanampa tano kwa uamuzi wake.

Ingawa tambiko na masuala ya mila hayakatazwi kisheria, wengi walimshambulia Nassari kwa kitendo chake hicho wakifananisha jambo hilo na masuala ya ushirikina, kitu ambacho sivyo kilivyo.Julai 17, mwaka huu, mbunge huyo wa zamani alichukua fomu katika ofisi za CCM Usa River, halmashauri ya Meru na kuipeleka moja kwa moja kwa wazee wa ukoo.

Akiwa ameambatana na wapambe wake, Nassari aliikabidhi fomu hiyo kwa wazee hao wa kimila ambao waliitambikia chini ya mti mkubwa ambao hutumiwa kwa shughuli za mila.Aidha, baada ya shughuli ya kimila kumalizika, Nassari aliongozana na wapambe wake hadi kanisani ambako aliangushiwa maombi ili ashinde uchaguzi, jambo ambalo halikuwezekana

Uchebe Amtolea Povu Baba Levo " Sibishani na Mtu Aliyeanza Kuimba Tangu Mimi Sijazaliwa Hadi Leo Anapanda Magari ya Kukodi"


Aliyekuwa Mume wa msaniii Shilole ambaye ni Uchebe1 amefunguka mengi kuhusu mambo Ambayo msanii Baba Levo kuwa anamuongelea mambo tofauti tofauti nakufunguka pia hashindani na mtu ambaye hajamzidi kipato

''Mimi Siwezi Kuwatukana Wasanii Lakini Kama Ningekuwa Naimba Ningekuwa Mbali Sana Kwasababu Tu Hapa Nilipo Nashwai Kumiliki Zaidi Ya Magari Kumi Sasa Ntabishana Na Mtu Tangu Ameana Kuimba Mimi Sijazaliwa Hadi Leo Bado Anapanda Magari Yakukodi Itakuwa Ni Mtihani, Siwezi Kubishana Na Mtu Ambaye Mimi Nikiuza Madumu Mawili Napata Laki Tatu Ambao Ni Mshahara Wake Wa Mwezi, UCHEBE

"Mimi Leo Nikipata Pesa Ninaweza Kumuita Mtu Aje Kunichekesha Ndio Kama Wale(BABA LEVO) , Usiombe Uwe Mwenye Akili Mbovu Ni Bora MUNGU Akunyime Pesa Akupe Akili Kwasababu Huwezi Sehemu Nzuri Watu Wanakuheshimu Ukaongea Speech Mbovu, Hivyo Siwezi Kubishana Nae Mtu Mpuuzi Usimpe Nafasi'' UCHEBE

Yanga Watoa Pole Kwa Mashabiki Waliopata Ajali Morogoro




Monday, July 20, 2020

Mbinu mpya za kumfanya mteja wako kuwa mfalme

Naomba pasipo kupoteza wakati naomba nikukaribishe katika somo letu la leo. Na siku ya leo tutazungumza kuhusiana na  mbinu moja itakatokusaidia katika ukuaji wa biashara.

Moja kati ya changamoto kubwa ya ufanyaji wa biashara ni kule kufanya kazi kwa mazoea, nasema hivi kwa sababu wafanyabiashara wengi husikika wakisema ya kwamba mteja ni mfalme, kakini katika hili kumekuwa na ukakasi ni wateja wachache sana ambao huuona ufalme huo.

Hii ni kwa sababu wafanyabiashara wachache sana ambao wakekuwa wakijua ni nini maaana ya mteja. Wafanyabiashara wengi wamekuwa wakimchukulia mteja pale anapokuja kwenye biashara ambayo anafanyaa tu. Kufanya hivi kutukufanya kuoina ramani ya biashara haina usawa kwani biashara utazidi kuiona ni ngumu siku zote.

Hivyo ili uweze kumfanya mteja wako awe ni mfalme unatakiwa kufanya mambo yafuatayo;

1. Acha mara moja kumsubiri mteja wako aje kukufuata mfanyabiashara mahali ulipo, bali anza utaratibu wa kumfuta mteja wako mahali alipo, kufanya hivyo kutamfanya mteja wako ajisikie huru na pia ajihisi kuwa yeye ni mfalme kweli, na pia kufanya hivi kutamjengea utaratibu mpya na pia kujiona yeye si mteja tu kwako bali ni sehemu ya biashara yako.

2. Tengeneza utaratibu mpya wa kuwa na mawasiliano ya karibu na mteja wako, si umekuwa ukisema ya kwamba mteja ni mfalme, kama ndivyo hivyo basi hakikisha ya kwamba unakuwa na mawasiliano na wateja, mawasiliano haya chochonde naomba yawe ni kwa ajili ya biashara tu, kwani pindi ukiyatumia mawasiliano hayo kivingine basi jiandae kuwafukuza wateja wote ulionao.  Mawasiliano haya yawe ni yale ya kuwajuza wateja kuhusu ujio wa bidhaa mpya.

3. Jifunze mbinu mpya ya kuweza kufanya mazungumzo na wateja. Hivi hujawahi enda katika biashara ya mtu mwingine mpaka ukajuta ni kwanini ulienda mahali hapo, bila shaka kama hali hii imewahi kukutokea basi ni vyema katika biashara yako uweze kujenga utaratibu mpya ambao utakufanya wateja wako wajisiie huru kila wakija wako.

4. Uchawi mkubwa ambao unafanyika katika biashara ni kutoa ofa kwa wateja wako.
Hii ni siri ambayo nakuibia wewe siku ya leo, haijalishi ni biashara gani ambayo unaifanya ila ili uweze kukua katika biashara hiyo ni vyema ukajiwekea utaratibu wa kutoa ofa katika biashara yako, jitahidi kutoa ofa kama yafanyavyo makampuni ya simu kufanya hivi kutawafanya wateja wengi waje kwako.

Asante sana kwa kusoma makala haya, mpaka kufikia hapo sina na ziada nikutakie siku njema na kazi njema.

Na. Benson Chonya.

Sunday, July 19, 2020

Niko Out na Mrembo Mmoja Kavaa Vikuku Miguu Yote Miwili, Eti Inamaanisha Nini?


Wadau hapa niko out na mrembo mmoja tulikutana facebook miezi miwili hivi imepita leo ndio tumeonana live tupo chobingo moja hivi siri yangu tunapata moja moja, kaja  amenivalia kimini na chini amevaa vikuku ama vicheni miguu yote miwili ...eti huwa zina ashiria au kumanisha nini? Huku mtaani midume huwa tuna danganyana sana juu ya hii kitu Wengine husema ukimuona anazo pande zote huyo antoa kotekote, Ebu tupeni ukweli wana dada au ni urembo tu kama heleni....?

Saturday, July 18, 2020

Shepu ya Lulu Diva Gumzo Mtandaoni


HIVI karibuni mwanadada Lulu Abbas 'Lulu diva' aliposti picha kwenye akaunti yake ikimuonyesha ana shepu kubwa, jambo lililofanya baadhi ya mashabiki zake kudai anatumia mchina.

"Mmmh Lulu Diva hii shepu yote umeitoa wapi? Maana hukuwa hivi wewe au umeanza kutumia mchina?" Alihoji shabiki mmoja ambapo Lulu naye alijibu kwa kumwambia hawezi kufanya hivyo bali ni uumbaji wa Mungu tu."Og hiyo baby, siwezi tumia mchina," alijibu msanii huyo.

Tuesday, July 14, 2020

EUNICE WISWA ACHUKUA FOMU KUGOMBEA UBUNGE SHINYANGA MJINI


Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Eunice Jackson Wiswa amechukua fomu ya kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kwa tiketi ya CCM.

Eunice amechukua fomu ya kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini leo Jumanne Julai 14,2020 katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini.

Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Eunice ambaye ni mtaalamu wa masuala ya Jiolojia (Madini, Mafuta na Gesi) amesema muda muafaka wa kuzungumzia vipaumbele vyake jimboni ni pale endapo chama chake kikapompitisha kuwa mgombea kiti cha ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Eunice Jackson Wiswa akionesha fomu ya kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kwa tiketi ya CCM baada ya kuchukua katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Eunice Jackson Wiswa akionesha fomu ya kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kwa tiketi ya CCM baada ya kuchukua katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini.
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Eunice Jackson Wiswa akiwa na ndugu zake baada ya kuchukua fomu ya kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Eunice Jackson Wiswa akiwa na ndugu zake baada ya kuchukua fomu ya kuomba kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...