Friday, July 24, 2020

China yalipiza kisasi kwa Marekani, yaiamuru kufunga ubalozi wa Chengdu


China hii leo imeiamuru Marekani kuufunga ubalozi wake mdogo katika mji wa magharibi wa Chengdu, ikilipiza kisasi cha kufungiwa wake ubalozi mdogo wa mjini Houston mapema wiki hii.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya China Wang Wenbin, amesema Marekani ndiyo ya kulaumiwa.

Utawala wa Rais Donald Trump uliamuru Jumanne kufungwa kwa ubalozi huo mdogo wa China mjini Houston katika saa 72, ukidai kwamba maafisa wa China walijaribu kuiba data kutoka katika Taasisi ya sayansi ya Matibabu ya Chuo Kikuu cha Texas A&M.

 Marekani imeishutumu China kwa wizi huo wa taarifa za kitaaluma, siku moja baada ya wizara ya sheria kuwafungulia mashtaka raia wawili wa China kwa madai ya kudukuwa kampuni kadhaa za Marekani na kujaribu kuiba utafiti wa chanjo dhidi ya virusi vya corona.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...