Wednesday, September 5, 2018

Griezmann aipiga vijembe FIFA kuhusu tuzo za Ballon d’or na UEFA ashangazwa Messi kutolewa

Mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madid na timu ya taifa ya Ufaransa Antoine Griezmann amefunguka kuhusu tuzo za mchezaji bora wa Dunia Ballon d’or na kusema kuwa ni za ‘ajabu’ Mshambuliaji huyo amefunguka hao wakati anaongeza na jarida la Globoesporte kuhusu tuzo mbali mbali zinazotolewa kwa wachezaji wanaofanya vizuri duniani. Griezmann licha ya kuzisaidia timu zake kutwaa …

The post Griezmann aipiga vijembe FIFA kuhusu tuzo za Ballon d’or na UEFA ashangazwa Messi kutolewa appeared first on Bongo5.com.


Source

Faiza Amtolea Povu Zito Mwanamke wa Sugu "Koma Kupiga Picha na Mwanangu na Mungu Akufanye Uwe Tasa For Rest of Your Life "

Faiza Amtolea Povu Mwanamke wa Sugu "Koma Kupiga Picha na Mwanangu "
Mwanadada Faiza Ally ambaye ni mzazi wa mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu amemjia juu mwanamke wa sasa wa sugu baada ya kuona picha za mwanadada huyo aliyepiga na Sasha ambaye ni mtoto wa Faiza.

Kupitia ukrasa wake wa instagramu Faiza amemtolea povu mwanamke huyo kwa kumpiga stop asipige naye picha mwanaye na akitaka hivyo abebe mimba azae  wake.

"Koma kupiga picha na mwananguzaa wako ...na michezo yenu hiyo sijui unapataje mtoto ....baba sasha mkataze huyo mtu mwenye sura mbaya kutafuta kiki mwanangu ...HIVI UNASHINDWA NINI KUMPA MIMBA KAMA ULIVYO NIPA MIMI AU NYIE HUWA MNAFANYAJE??????????"

Ikumbukwe kuwa hii si mara ya kwanza kwa Faiza kumshambulia mzazi mwenzake kwani siku chache sasha alienda kwa baba yake kwaajili ya mazishi ya bibi yake ambaye ni mama mzazi wa Sugu na alimshambulia kwa kumtaka awahi kumrudisha mtoto kwakuwa amefungua shule.

''Unachotaka Niku mtenganisha sasha na baba sasa umefaulu ! Sasa mtaishia kuona picha zake insta tu ....na Mungu akufanye uwe tasa for rest of your life ! Tuone sasa kama kupiga picha na sasha ndio kutafanya awe mwanao! We ni mtumbaya mama hataki na mwanae una n'gan'gania nini ? Au unataka roho yake ? Nenda kaadapti mtoto umlee kama huzai ! Niachie mwananguuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu''
Faiza alitoa maneno makali na leo pia amekuja na jambo lingine na kumsihi Sugu ampe mimba Mkewe kama alivyompa yeye.
Source

VIDEO: Mambosasa Aongelea Mgambo waliompiga Mfanyabiashara, na Kukamtwa pikipiki ya wizi


Kamanda kanda maalum ya Dar es salaam SACP Lazaro mambosasa Amelikemea vikala sakata la askari mgambo kumpiga mfanyabiashara na kudai kuwa ni kinyume cha sheria za nchi ambapo ameongezea kusema kuwa mgambo hao wameshakamatwa na kuchukuliwa hatua kufikishwa mahakamani.


TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI..........USISAHAU KUSUBSCRIBE............


Source

Dodoma roads, airport, bus terminal undergoing facelift to meet city status

The government has expressed its commitment toward improving infrastructure in Dodoma to match the Capital City status, with airport expansion and refurbishment of road high on the agenda.
Source

Matukio ya Instagram Yamchosha Steve Nyerere Amuomba Rais Magufuli Aizime

Matukio ya Instagram Yamchosha Steve Nyerere Amuomba Rais Magufuli Afunge Mitandao ya Kijamii
Msanii wa filamu za kibongo Steve Nyerere amejikuta akimuangukia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli akimtaka afunge mtandao wa instagram kwakuwa watanzania utandawazi.

Steve nyerere ameonekana kukerwa na yanayoendelea mitandaoni kwakuwa vijana na baadhi ya watanzania wameacha kufanya kazi za maana kwaajili ya kuleta maendeleo ya nchi bali wamekalia umbeya na majungu ya kuchafuana mitandaoni.

Kupitia mtandao wake wa kijamii steve ameandika maneno haya;
''MH RAIS MAGUFULI hakika unapenda kuona vijana wanakuwa nguvu KAZI kwa TAIFA lao,Naamini vijana wa kitanzania wakijua kuwa wana deni na TANZANIA basi watabadilika kitabia , TAIFA letu la TANZANIA lina kila sababu ya kumshukuru MUNGU,maana tumebarikiwa vingi ambavyo wenzetu hawana,Mh karne hii inaangamia kwa utandawazi tu Zimaaaaa BABA japo wiki Zimaaaaa BABA uku istagram amna cha kujifunza zimaaa baba ni shidaaa uku.Zimaaaaaa baba japo wiki BABA zimaaaaaaaa''.

Acacia starts fresh retrenchments as concentrate export ban bites

Acacia Mining Company is executing what it terms as 'organisational changes' process for its Bulyanhulu Gold Mine that will culminate into retrenchments of employees as the company cuts costs to remain afloat in the wake of the government's ban on concentrate exports.
Source

News Alert : HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA MASOMO CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM -UDSM 2018/2019


Majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga UDSM mwaka wa masomo 2018/2019 

Tuesday, September 4, 2018

Faida za Utumiaji Samadi Mashambani


Samadi ni aina ya mbolea ambayo hutokana na vinyesi vya wanyama mbalimbali kama ng'ombe, kuku, mbuzi, kondoo na wengine. Hii ni miongoni mwa mbolea ambazo wakulima wengi wanaweza kumudu kirahisi.

Vilevile mbolea zingine ambazo wakulima wanaweza kuzipata kwa urahisi ni masalio ya mimea shambani (mabiwi). Mfano wa masalio hayo ni kama mabua ya mtama, mahindi na mimea ya jamii ya kunde au kitaalamu hujulikana kama (leguminas). Masalio haya yakishaoza hurutubisha udongo kwa kurejesha chumvichumvi za madini zilizokuwa zimechukuliwa na mimea wakati inastawi.

Hata hivyo mbolea yenye manufaa zaidi ni samadi, kwani wataalamu wanakadiria kuwa tani moja ya vinyesi vya fahali (madume ya ng'ombe) huwa na thamani karibu kilo 6.3 za chumvichumvi za nitrates; tani moja ya samadi ya vinyesi vya ng'ombe majike huwa na kilo 5.1 za chumvi za nitrates.
Mbolea zinazotokana na masalio ya mimea kwa mfano, mabua ya mahindi tani moja hutoa mbolea inayoweza kurejesha ardhini karibu kilo 4.0 za chumvi za nitrates.

Hivyo samadi yenye mchanganyiko wa vinyesi vya ng'ombe majike na madume wanaofugwa kwa pamoja (wanaolala katika zizi moja) huwa na thamani kubwa.

Ili upate kustawi na kutoa mavuno mengi na bora, mimea huhitaji chumvichumvi za madini ya nitrates, phosphate na potash pamoja na kiasi kidogo sana cha chumvi za nitrates, phosphate na potash pamoja na madini ya boron, copper, manganese, zinc na nyinginezo.

Kwa hiyo rutuba ya udongo huwa inategemea sana kiasi cha chumvichumvi zilizomo udongoni.
Ubora wa samadi hukadiriwa pia kwa kiasi cha chumvi za madini zinazopatikana mathalani ng'ombe 50 wanaweza kutoa karibu tani 600 za samadi kila mwaka. Kiasi hiki cha samadi kinaweza kurejesha ardhini karibu kilo 3048 za chumvichumvi za nitrates, kilo 544 za phosphate na kilo 2722 za Potash, pamoja na kiasi kidogo cha Boron, Copper, Manganese na Zinc.

Wakulima au wafugaji wengi hufuga ng'ombe hata zaidi ya 50, lakini kwa wastani wengi huwa na idadi hiyo kama ni wastani wa ng'ombe ambao kila mkulima anaweza kuwa nao.

Mbolea yenye kilo 3048 za nitrates, kilo 544 za phosphate na kilo 2722 za potash kwa uwiano huo haziwezi kutengenezwa kiwandani kwani itakuwa ghali sana kiasi kwamba hakuna mkulima anaweza kununua.

Samadi kiasi hicho italeta manufaa mengi kwani licha ya kuongeza rutuba ardhini vilevile itaubadili udongo uwe katika hali nzuri zaidi kwa kustawisha mimea.

Kadhalika samadi unaufanya udongo ushikamane kwa nguvu zaidi hata usiweze kupeperushwa na upepo au kumomonyolewa na maji ya mvua.

Manufaa mengine ya mbolea ya samadi ni kuwa inaufanya udongo kuwa katika hali nzuri ya kuweza kuyashikilia maji au unyevu kwa muda mrefu.

Minyoo waishio udongoni ambao husababisha kuwepo nafasi kwa ajili ya hewa kupenya kwa urahisi na vijidudu vya bakteria ambavyo huozesha mbolea na kubadili hewa kuwa katika hali ya chumvichumvi zinazotumiwa na mimea, hupata mazingira mazuri kwa maisha yao katika udongo uliotiwa samadi.

Wataalamu wanasema kuwa ubora wa samadi inategemea jinsi ilivyokuwa imetunzwa zizini au kibandani kwani chumvi nyingi hasa zile za nitrates huwa zinapotea kwa urahisi kwa maji ya mvua, kutokana na kitendo chake cha kuyeyuka mara tu zinapolowa maji.

Ili tuendelee kuwa na thamadi kubwa ni muhimu zizi liwe na paa lisilovuja kusudi maji ya mvua yasilowanishe, la sivyo ng'ombe wafugwe katika vibanda.

Jack Pemba asaini dili nono na Roc Nation ya Jay Z


Likitajwa jina la Jack Pemba najua wengi mtakuwa mnakumbuka matukio yake kwenye kumwaga fedha kipindi ameiteka vyema Bongo. 

Sasa habari njema ni kuwa, mfanyabiashara huyo maarufu nchini ambaye kwa sasa anafanya biashara zake Uganda amesaini dili nono na kampuni ya michezo ya Roc Nation (Roc Nation Sports Company) ya rapper Jay Z. 

Kwa mujibu wa mtandao wa Big Eye wa nchini Uganda umeeleza kuwa Jack Pemba na kampuni yake ya ku-promote ngumi 'Pemba Sports International' amesaini dili hilo ambalo litasaidia kukuza mchezo wa ngumi nchini humo na kuwapeleka wachezaji kimataifa. 

"I have signed a deal with Jay-Z's sports company, and with support from the Ministry of Education and Sports, we shall be promoting boxing in Uganda." amesema Jack.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...