Tuesday, September 4, 2018

Jack Pemba asaini dili nono na Roc Nation ya Jay Z


Likitajwa jina la Jack Pemba najua wengi mtakuwa mnakumbuka matukio yake kwenye kumwaga fedha kipindi ameiteka vyema Bongo. 

Sasa habari njema ni kuwa, mfanyabiashara huyo maarufu nchini ambaye kwa sasa anafanya biashara zake Uganda amesaini dili nono na kampuni ya michezo ya Roc Nation (Roc Nation Sports Company) ya rapper Jay Z. 

Kwa mujibu wa mtandao wa Big Eye wa nchini Uganda umeeleza kuwa Jack Pemba na kampuni yake ya ku-promote ngumi 'Pemba Sports International' amesaini dili hilo ambalo litasaidia kukuza mchezo wa ngumi nchini humo na kuwapeleka wachezaji kimataifa. 

"I have signed a deal with Jay-Z's sports company, and with support from the Ministry of Education and Sports, we shall be promoting boxing in Uganda." amesema Jack.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...