Monday, June 29, 2026
VIJANA WAHIMIZWA KULINDA NA KUDUMISHA AMANI
Sunday, June 28, 2026
TRA YAPANDA MITI 1000 KATIKA SHULE UMMY MWALIMU KUADHIMISHA MIAKA 30 YA KUANZISHWA KWAKE
NA REBECA DUWE TANGA
Katika kuendeleza shughuli za uwajibikaji kwa jamii, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo imepanda miti isiyopungua 1,000 katika Shule ya Sekondari Ummy Mwalimu iliyopo Kata ya Maweni, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwa mamlaka hiyo.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, mgeni rasmi ambaye ni Naibu Kamishna wa Shughuli za Ufundi – Kodi za Ndani, Ted Frank Silkiluwasha, alisema pamoja na jukumu la kukusanya mapato ya Serikali, TRA imeendelea kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii zinazoleta maendeleo kwa wananchi.
Alisema zoezi la upandaji miti linaonesha ushirikiano mzuri uliopo kati ya TRA na jamii, huku akisisitiza umuhimu wa kuitunza miti hiyo ili iweze kukua na kutoa manufaa kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
"Utunzaji wa miti ni muhimu kwa sababu huchangia kulinda tabaka la ozone, kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi na kulinda afya ya binadamu pamoja na viumbe wengine," alisema Silkiluwasha.
Aidha, alimtaka Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga kuendelea kutoa elimu ya kodi kwa wananchi, akieleza kuwa elimu hiyo inapaswa kuwa endelevu. Pia alipendekeza Shule ya Sekondari Ummy Mwalimu kuingizwa katika mpango wa Tax Club, unaolenga kuwajengea wanafunzi uelewa na utamaduni wa kulipa kodi.
"Ukubwa wa taifa haupimwi kwa wingi wa watu au silaha, bali kwa uchumi imara. Uchumi huo hujengwa kupitia ukusanyaji wa mapato ya Serikali ambayo huwezesha kuboresha sekta za elimu, afya, miundombinu na hata kuimarisha ulinzi na usalama," alisema.
Kwa upande wake, Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga, Castrol John, aliwataka wafanyabiashara kuzingatia sheria za kodi na kuacha kutumia njia zisizo halali wanapoingiza bidhaa nchini.
Pia alihimiza wananchi kuwafichua wakwepa kodi, akibainisha kuwa TRA ina utaratibu wa kutoa zawadi kwa watu watakaotoa taarifa zitakazosaidia kuokoa mapato ya Serikali yanayopotea.
Naye Mhifadhi kutoka Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Michael Charles, aliipongeza TRA kwa hatua hiyo na kuzitaka taasisi nyingine kuiga mfano huo.
Alisema miti ina mchango mkubwa katika kuhifadhi mazingira, kuboresha ubora wa hewa, kuhifadhi viumbe hai, kuongeza vivutio vya utalii, kutoa matunda na kuchangia afya bora ya jamii.
Akitoa shukrani kwa TRA, Mkuu wa Shule ya Sekondari Ummy Mwalimu, Asha Kitundu, alisema shule hiyo ina eneo la takribani ekari 700, hivyo miti iliyopandwa itasaidia kutoa kivuli, kuzuia mmomonyoko wa udongo na kuboresha mazingira ya kujifunzia.
Aidha, aliwahamasisha wadau wengine kujitokeza kuisaidia shule hiyo, akieleza kuwa bado ni changa na inahitaji ushirikiano wa jamii katika kuendeleza maendeleo yake.
Shule ya Sekondari Ummy Mwalimu ilianzishwa mwaka 2022 ikiwa na wanafunzi 316 waliohamishwa kutoka Shule ya Sekondari Maweni. Kwa sasa shule hiyo ina wanafunzi 916 na walimu watatu, huku ikitarajia kupokea wanafunzi 83 wa Kidato cha Tano mwezi Julai mwaka huu.
Saturday, June 27, 2026
ZAIDI YA WANUFAIKA 17,000 WA KAYA MASKINI RUVUMA WAFIKIWA NA BIMA YA AFYA KWA WOTE.
Meneja wa mfuko wa bima ya Afya Mkoa wa Ruvuma Hansi John Akizungumza na waandishi wa habari waliomtembelea ofisini kwake kuhusu mipango ya serikali kuzifikia kaya zisizo na uwezo na utekelezaji wake kwa awamu kupitia mpango wa TASAF.
Na Regina Ndumbaro Songea-Ruvuma
Mfuko wa Bima ya Afya Mkoa wa Ruvuma umefanikiwa kuwafikia zaidi ya wanufaika 17,000 kutoka kaya zisizo na uwezo katika utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mpango wa Bima ya Afya kwa Wote unaotekelezwa na Serikali kupitia mpango wa TASAF.
WADAU KILOLO WAJADILI FURSA ZA KUIMARISHA UCHUMI KUPITIA MRADI WA INUA II
Hand in Hand Eastern Africa–Tanzania imekutana na viongozi na wadau wa Wilaya ya Kilolo kwa lengo la kujadili fursa za ushirikiano katika utekelezaji wa Mradi wa INUA II, unaolenga kuwawezesha wanawake, vijana na makundi yaliyo katika mazingira ya uhitaji kujenga uchumi endelevu.
Thursday, June 25, 2026
ALIYEDANGANYA FAMILIA YA MUMEWE KUWA NI MJAMZITO AKAMATWA KWA UWIZI WA MTOTO MCHANGA LUSHOTO.
Na Rebeca Duwe , Lushoto.
Jeshi la polisi Mkoa wa Tanga linamshikilia mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Habiba Seleman Fundi kwa tuhuma za wizi wa mtoto mchanga katika hospitali ya wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga.
Akithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo Kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Almachius Mchunguzi alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa mnamo tarehe 21juni mwaka huu Majira ya saa 1 usiku katika kitongoji cha Garekaya Wiliyani Lushoto akiwa na mtoto huyo.
Kamanda Mchunguzi alisema alisema kuwa manamo juni 19 mwaka huu saa 11jioni mama mzazi wa mtoto huyo Mwanaidi Juma Nyaki mkazi wa Kijiji cha Kwemakame aliripoti kupotea kwa mwanae wa siku moja .
Aidha aliongeza kusema kuwa mtuhumiwa huyo alitumia mbinu ya kujenga urafiki wa karibu na mama mzazi wa mtoto huyo pamoja ndugu waliokuwa wakimhudumia hospitalini hapo.
Alisema baada ya kupata imani yao alichukua fursa hiyo na kumweka mtoto ndani ya beseni lenye nguo kisha kutoweka na mtoto bila kufahamika kwa wakati huo.
Sambamba na hayo alisema uchunguzi wa kina umebaini kuwa mtuhumiwa alikuwa akidai kwa muda mrefu kuwa ni mjamzito na kuwahakikishia ndugu,jama wa mume wake kuwa alikuwa akisubiri kujifungua.
Hata hivyo baadaya muda ameuweka kufika aliamua kufanya mpango huo wa kuiba mtoto ili kuwathibitishia madai yake kwa familia ya mumewe na watu waliokuwa wakimzunguka kuwa alikuwa mjamzito na amejifungua.
mwisho
Wednesday, June 24, 2026
UVCCM SHINYANGA: TUSIHANGAIKE NA MATUSI YA WAPINZANI MTANDAONI, TUWAJIBU KWA MATOKEO YA KAZI
SHILATU AZINDUA MASHINDANO YA KUSAKA VIPAJI KANDA YA KUSINI, SERIKALI YAIMARISHA MKAKATI WA KUKUZA SANAA NA MICHEZO KWA VIJANA
Tuesday, June 23, 2026
SERIKALI YABADILI GIA, SASA KUWA RAFIKI WA BIASHARA NA SIO WADHIBITI-KAPINGA
TBS YATEKETEZA TANI 110 ZA BIDHAA HAFIFU NA ZILIZOPIGWA MARUFUKU ZENYE THAMANI YA SH. MILIONI 394
NA EMMANUEL MBATILO, PWANI
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) Kanda ya Kati limeteketeza tani 110 za bidhaa hafifu na zilizopigwa marufuku zenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 394 katika zoezi lililofanyika Juni 22, 2026, Mkuranga mkoani Pwani.
Bidhaa zilizoteketezwa zinajumuisha tani 26 za bidhaa za mitumba, ikiwemo nguo za ndani na taulo ambazo kwa mujibu wa viwango na sheria za nchi haziruhusiwi kuingizwa nchini kutokana na hatari zake kwa afya ya jamii.
Bidhaa nyingine zilizoharibiwa ni tani 8 za vipodozi vilivyopigwa marufuku, tani 3 za bidhaa za chakula zilizokwisha muda wa matumizi pamoja na kiasi cha bidhaa za rangi ambazo hazikukidhi matakwa ya viwango vya ubora.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa zoezi hilo, Meneja wa TBS Kanda ya Mashariki, Bi. Noor Meghji, alisema bidhaa hizo zilipatikana kupitia ukaguzi wa mara kwa mara unaofanywa na shirika hilo katika masoko na maeneo mbalimbali ya biashara.
Alisema katika baadhi ya maeneo walibaini uwepo wa bidhaa zilizokwisha muda wa matumizi na kuwaagiza wahusika kuziondoa sokoni na kuziteketeza ili kulinda afya za watumiaji.
Bi. Meghji amewataka wananchi kuwa makini wanaponunua bidhaa mbalimbali kwa kuhakikisha wanasoma taarifa zote muhimu zilizopo kwenye vifungashio kabla ya kufanya matumizi.
“Iwapo mtumiaji atagundua tofauti yoyote kwenye bidhaa au kipodozi anachotumia, ni muhimu kutoa taarifa kwa TBS mapema ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa,” alisema.
Aidha, alifafanua kuwa lengo la TBS si kuwaadhibu au kuwaumiza wafanyabiashara kwa kuharibu bidhaa zao, bali ni kuhakikisha sheria na viwango vinazingatiwa kwa manufaa ya umma. Alisema shirika hilo linaendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara na wananchi kuhusu bidhaa zilizopigwa marufuku na zile zenye viambata hatarishi.
Wakati huohuo, TBS imetoa onyo kwa wafanyabiashara wanaouza bidhaa zisizokidhi viwango vya ubora au zinazohatarisha afya ya watumiaji, ikisisitiza kuwa haitasita kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watakaobainika kukiuka sheria kwa makusudi.
Shirika hilo limeeleza kuwa wahusika wanaobainika kuingiza au kuuza bidhaa hizo wanaweza kulazimika kugharamia zoezi la uteketezaji pamoja na kukabiliwa na hatua nyingine za kisheria kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizopo.
TBS imesisitiza dhamira yake ya kuhakikisha bidhaa zote zinazozalishwa au kuingizwa nchini zinazingatia viwango husika kwa lengo la kulinda afya ya wananchi, mazingira ya biashara na uchumi wa Taifa.
Bi. Meghji alisema kuwa endapo bidhaa hizo zingeendelea kusambazwa na kutumika sokoni, zingeweza kusababisha madhara makubwa kwa afya za watumiaji na kuathiri ustawi wa uchumi wa nchi.
“Tunawaasa wafanyabiashara kuacha kuuza bidhaa ambazo hazikidhi matakwa ya viwango, vipodozi vilivyozuiliwa pamoja na bidhaa zilizokwisha muda wa matumizi. Wakaguzi wetu wanaendelea kufanya kazi muda wote na tunashirikiana na wananchi pamoja na vyombo vingine vya dola kuhakikisha bidhaa zote zinazopatikana sokoni zinakidhi viwango vinavyotakiwa,” alisema.

Monday, June 22, 2026
TRA YATOA MSAADA KWA WATOTO NJITI HOSPITALI YA RUFAA BOMBO KATIKA MAADHIMISHO YA. MIAKA 30
Rebeca Duwe Tanga
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa msaada wa vifaa mbalimbali katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo mkoani Tanga kwa ajili ya kuwasaidia watoto wenye changamoto mbalimbali, wakiwemo watoto njiti, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 30 ya mamlaka hiyo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Naibu Kamishna wa Huduma za Kiufundi kutoka Makao Makuu ya TRA, Ted Silkiluwasha, alisema kuwa katika jamii ya Watanzania kuna watu wenye mahitaji maalum wanaohitaji kusaidiwa, hivyo mamlaka imeona umuhimu wa kuwafikia na kuwasaidia.
Alisema Kamishna Mkuu wa TRA, Yusuph Mwenda, amesisitiza kuwa ukusanyaji wa mapato ndio unaochangia maendeleo na kuimarisha uwepo wa taifa, hivyo ni muhimu kuhakikisha hakuna mwananchi anayeachwa nyuma katika juhudi za maendeleo.
“Sambamba na kuimarisha taifa, hatupendi kumuacha mtu yeyote nyuma. Miaka 30 ya TRA imewezekana kutokana na walipa kodi, na mamlaka inatambua kuwa uhai wa walipa kodi ndio uhai wa TRA. Ndiyo maana tumeamua kutoa msaada huu kwa watoto njiti kama sehemu ya kurudisha kwa jamii inayochangia maendeleo ya taifa kupitia kodi,” alisema Silkiluwasha.
Aliongeza kuwa Julai 1 mwaka huu TRA itatimiza miaka 30 tangu kuanzishwa kwake, ikiwa na kaulimbiu ya “Tanzania kwa Pamoja Tunajenga Taifa Letu.” Alisema mamlaka imeona umuhimu wa kufika Hospitali ya Rufaa ya Bombo kwa kuwa inahudumia watu wenye mahitaji makubwa, ili kuwajulisha kuwa wao ni sehemu muhimu ya jamii.
Kwa upande wake, Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga, Castro John, alisema kuwa mamlaka hiyo inaamini kila Mtanzania ni mlipa kodi wa sasa au wa baadaye, hivyo hata watoto waliotembelewa ni walipa kodi wa kesho na pengine watumishi wa baadaye wa TRA.
Alisema mtazamo huo ndio uliowasukuma kushiriki katika shughuli za kijamii na kusaidia makundi yenye mahitaji maalum.
Aidha, alizitaka taasisi nyingine, hususan mkoani Tanga, kujitokeza kusaidia watu wenye uhitaji na kushiriki katika shughuli za kijamii zinazolenga kuwatia moyo na kuboresha maisha yao.
Naye Nuru Hamisi Omari alisema kuwa hospitali hiyo hupokea watoto njiti kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Tanga. Alieleza kuwa watoto hao hupatiwa huduma mbalimbali ikiwemo kuongeza kiwango cha sukari mwilini na kusaidiwa kupumua kwa kutumia mashine maalum hadi wanapofikia uzito unaoruhusiwa.
Alifafanua kuwa mtoto anaporuhusiwa kwenda nyumbani anatakiwa kuendelea kuhudhuria kliniki maalum ya ufuatiliaji wa ukuaji hadi atakapofikia uzito wa kilo tatu, ndipo huendelea na huduma za kawaida za kliniki.
Kwa upande wake, Muuguzi Kiongozi wa Wodi ya Watoto, Sister Rukia Mbega, ameishukuru TRA kwa kuguswa na mahitaji ya watoto njiti na kutoa msaada utakaosaidia kuboresha huduma kwa watoto hao.
Alisema msaada uliotolewa unajumuisha sabuni, nepi (pampers), dawa na makopo ya maziwa ya unga, vitu ambavyo ni muhimu katika kuwahudumia watoto njiti.
Sunday, June 21, 2026
VIJANA WANAOISHI MAZINGIRA MAGUMU WAJITENGA NA MAANDAMANO YA 7/7
TARURA KUENDELEA KUJENGA MADARAJA YA MAWE NCHI NZIMA -SUNGURA
Saturday, June 20, 2026
TBA YATEKELEZA MPANGO WA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU KWA WANANCHI
POLISI WAFICHUA MPANGO WA UHALIFU JULAI 7
Friday, June 19, 2026
JUMLA YA MIRADI 73 YA MWENGE WA UHURU YENYE THAMANI YA SH BILIONI 27.7 KUKAGULIWA,KUWEKEWA MAWE YA MSINGI NA KUZINDULIWA
Na Rebeca Duwe Tanga
Mkuu wa mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian amewataka wananchi wa Mkoa waTanga kutokeza kupoke mwenge wa uhuru ili kuweza kuukimbiza ili kuhakikisha nuru inamulika kila mahali na kuimarisha umoja na mshikamano, ambapo utakimbizwa katika halmashauri zote 11 za mkoa huo na kukagua, kuzindua pamoja na kuweka mawe ya msingi katika miradi 73 yenye thamani ya zaidi ya 27.7
Hayo aliyasema wakati akizungumza na waandishi wa habari ,kuhusu maandalizi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu ambapo alisema Mwenge wa Uhuru utapokelewa katika Viwanja vya Shule ya Msingi Mji Mpya, Kijiji cha Mtoro, Kata ya Tunguli wilayani Kilindi ukitokea Mkoa wa Morogoro.
Alisema baada ya mapokezi hayo, Mwenge utakimbizwa kwa umbali wa kilometa 1,340 kupitia halmashauri zote za Mkoa wa Tanga kabla ya kukabidhiwa Mkoa wa Kilimanjaro Juni 28 mwaka huu katika Uwanja wa Shule ya Msingi Hedaru.
Dk. Burian alisema kati ya miradi 73 itakayofanyiwa kazi na Mwenge wa Uhuru, miradi 34 itawekewa mawe ya msingi, miradi 26 itafunguliwa na kuzinduliwa, miradi 11 ya vijana itakaguliwa pamoja na miradi miwili ya sekta ya maji.
Alifafanua kuwa miradi hiyo ina thamani ya Sh bilioni 27.76, ambapo Sh milioni 300.6 ni nguvu za wananchi, Sh bilioni 1.27 ni michango ya halmashauri, Sh bilioni 10.7 ni fedha za Serikali Kuu na Sh bilioni 15.47 ni mchango wa wahisani.
Akizungumzia kaulimbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu inayosema, “Tanzania ni Yetu Sote, Tushikamane kwa Pamoja Kuleta Maendeleo,” Dk. Burian alisema mkoa umejipanga kuhakikisha wananchi wa makundi mbalimbali wanashiriki kikamilifu katika shughuli zote za Mwenge.
Alisema viongozi wa serikali, watumishi wa umma, viongozi wa dini, wanawake, vijana, watu wenye mahitaji maalumu pamoja na makundi mengine wamehamasishwa kushiriki kikamilifu kuanzia mapokezi hadi makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru.
Aidha, wananchi watapata fursa ya kuushika na kuukimbiza Mwenge huo kama sehemu ya kuimarisha mshikamano, umoja wa kitaifa na ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo.
Mbali na kuhamasisha maendeleo, Mwenge wa Uhuru utaendelea kutoa elimu kuhusu mapambano dhidi ya rushwa, malaria, VVU/UKIMWI, matumizi ya dawa za kulevya pamoja na umuhimu wa lishe bora kwa jamii.
Dk. Burian aliwataka wananchi wa Mkoa wa Tanga kujitokeza kwa wingi katika maeneo ya mapokezi, miradi na mikesha mbalimbali ili kushiriki shughuli za Mwenge wa Uhuru na kufaidika na ujumbe wake.
Alisema mkoa umejipanga kikamilifu kuhakikisha wananchi wanapata burudani na hamasa kupitia ushiriki wa wasanii na vikundi vya sanaa vitakavyoshiriki katika maeneo yote ambayo Mwenge wa Uhuru utakesha.
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga Daktari Daniel Henry Na Isaac Masengwa ******************* Askofu mteule wa KKKT Dayosisi ya Mwanga...
-
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe asomewa mashtaka matatu ya uchochezi, yenye nia ya kuleta ch...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini Richard Kasesela Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini Richard Kasesela amelishauri Kanisa la Kiinjili la Kilutheri ...












































