Saturday, October 31, 2020

Nchi za Ulaya zataka WHO iwe na uhuru wa kuchunguza milipuko ya magonjwa


Nchi za Ulaya zimesema Shirika la Afya Ulimwenguni WHO linastahili kuwa na nguvu ya kuchunguza kwa uhuru milipuko ya magonjwa na pia kuweza kuzilazimisha nchi kutoa data zaidi. 


Wito huo umetolewa baada ya kutokea janga kubwa la virusi vya corona ambalo limewezesha kuonyesha mapungufu katika shirika hilo. 


Waziri wa afya wa Ujerumani Jens Spahn amesema WHO inapaswa kuungwa mkono zaidi kisiasa na kifedha kutokana na juhudi zake za kusimamia migogoro ya kiafya. 


Nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya zimetoa mapendekezo kadhaa ya kulirekebisha shirika hilo la afya duniani. Wakati huo huo mkurugenzi mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema wataalam wa Shirika hilo walilijadili janga la corona hapo jana katika mkutano na wenzao wa China.

Ivory Coast: wananchi wapiga kura kumchagua rais


Raia wa Ivory Coast leo wameshiriki katika zoezi la kupiga kura. Taarifa zaidi zinafahamisha kwamba baadhi ya wafuasi wa upinzani walijaribu kuvuruga kura hiyo hatua inayochukuliwa kuwa walifuata wito kutoka kwa wagombeaji wawili wanaompinga rais Alassane Ouattara uliowataka raia kususia uchaguzi huo ambapo kiongozi huyo anawania muhula wa tatu. 


Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters barabara za mji mkuu wa kibiashara Abidjan zilikuwa na kimya bila watu tofauti na wakati mwingine ambapo zilikuwa zinakumbwa na vurugu uchaguzi. 


Ouattara amesema anagombea tena chini ya katiba mpya iliyoidhinishwa mnamo mwaka 2016, na anafanya hivyo kwa sababu mgombea aliyechaguliwa na chama chake alifariki ghafla mnamo mwezi Julai. Kiongozi huyo anatarajiwa kushinda.

Armenia, Azerbaijan zashutumiana kushambulia raia

Armenia na Azerbaijan kwa mara nyingine tena leo zinashutumiana kwa kufanya mashambulizi ya mabomu katika makazi ya raia wa kawaida.


Vitendo hivyo vinavunja makubalaino yao ya awali ya kutowashambulia raia. Mashambulizi hayo yaliripotiwa saa kadhaa baada ya kufikiwa makubaliano ya kumaliza mgogoro huo, katika mazungumzo ya mjini Geneva yaliyojumuisha mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo mbili na wajumbe kutoka Ufaransa, Urusi na Marekani. 


Haya ni majaribio ya nne ya kujaribu kusitisha mapigano tangu yalipozuka mnamo Septemba 27, ambayo tayari yameshasababisha vifo vya zaidi ya watu1,000. Ni mapigano mabaya kuwahi kushuhudiwa katika mzozo uliodumu kwa zaidi ya miaka 25.

Upinzani wataka uchaguzi mkuu kurudiwa



Vyama vikuu vya upinzani nchini Tanzania Chadema na ACT-Wazalendo vinataka kurejewa kwa Uchaguzi Mkuu nchini humo.

Vyama hivyo viwili vinapinga matokeo ya uchaguzi wa Jumatano ambapo rais aliye madarakani John Magufuli amekwishatangazwa mshindi.

Katika mkutano wa wanahabari wa pamoja baina ya viongozi wa Chadema na ACT Wazalendo vyama hivyo pia vimeitisha maandamano ya nchi nzima ili kudai kurejewa kwa uchaguzi huo

Mwenyekitiwa Chadema Taifa Freeman Mbowe ameeleza kuwa: ''kilochofanyika si uchaguzi ni unyang'anyi wa demokrasia uliofanywa na ZEC (Tume ya Uchaguzi Zanzibar) na NEC (Tume ya Taifa ya Uchaguzi) .''

Vyama hivyo sasa vinataka kuvunjwa kwa Tume ya NEC na ZEC.

Vyama hivyo aidha vimewaomba Watanzania kufanya maandamano ya amani.

''Kuanzia Jumatatu, wanachama wa vyama vyetu na wote wasiokubaliana kushiriki katika maandamano ya amani kuanzia Novemba 2 hadi hapo madai yetu yakapotelekezwa'' walisema.

Siku ya Alhamisi Mwenyekiti wa ACT Wazalendo ambaye pia alikuwa mgombea wa urais visiwani Zanzibar, Maalim Seif Seif Sharif Hamad alikamatwa pamoja na viongozi wengine wa chama hicho.

Kamanda wa Polisi Mjini Magharibi Zanzibar Awadhi Juma alisema Maalim Seif alikamatwa akiwa anafanya maandamano ambayo hayana kibali akiwa na wafuasi wa chama chake

Siku ya Alhamisi Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ulizitaka mamlaka za taifa hilo la Afrika Mashariki kushirikiana na wadau mbalimbali kushughulikia kwa uwazi malalamiko yanayotolewa kuhusu uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Ubalozi huyo kupitia tamko lake lililotolewa Oktoba 29, mwaka huu unasema kufanya hivyo kutarejesha imani na kutekeleza azma ya kuheshimu utawala wa sheria na dhana ya utawala bora.

Moja ya malalamiko yaliyotajwa na ubalozi huo ni kuhusu uwepo wa kura feki katika uchaguzi huo.

NEC imesemaje?

Malalamiko hayo yalishatolewa ufafanuzi na kupingwa na Tume ya taifa ya uchaguzi kwamba hayana ukweli kupitia kwa mwenyekiti wake, Jaji Kaijage.

''Kuna taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusu kuwepo kwa masanduku ya kura feki katika majimbo ya Kawe Dar es Salaam, Pangani Tanga na Buhigwe Kigoma", alisema Bw. Kaijage

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imesema haijapokea taarifa ya madai hayo.

RC DSM atoa onyo kwa watakaotaka kuvuruga amani



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge, ametoa onyo kwa watu au vikundi vya watu vilivyopanga kufanya vurugu na kusema kuwa yeyote atakayejaribu kuvuruga amani kwenye mkoa huo atawajibishwa kwa mujibu wa Sheria.



RC Kunenge, ametoa kauli hiyo hii leo Oktoba 31, 2020, wakati wa uzinduzi wa baraza la wafanyakazi wa shirika la uwakala wa Meli Tanzania, na kuongeza kuwa kwa kuwa hali ya usalama ndani ya jiji hilo ni shwari, hivyo asitokee yeyote atakayevuruga hali hiyo.




"Tumeona hali ni shwari, tumemaliza kupiga kura na washindi wametangazwa, kwahiyo kwa lugha inayotumika sasa ni kuwa Dar es Salaam ni ya kijani, naomba tuendelee kuwa watulivu, serikali imejipanga na vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga vizuri, ila yeyote ambaye ataonekana kuhatarisha usalama au atakayefanya matendo yatakayopelekea kuvunjika kwa amani hatutamvumilia aache Jiji letu liendelee kuwa na amani", amesema RC Kunenge.




Wakati huohuo RC Kunenge, ametembelea ujenzi wa stand mpya ya mabasi ya Mbezi Louis na kukuta ujenzi huo ukiwa katika hatua ya upauaji ambapo amemuelekeza mkandarasi kuhakikisha ujenzi unakamilika kabla ya Novemba 30 kama Rais MagufuliValivyoelekeza.

Kaze Atafuta Rekodi Mpya Leo Yanga



LEO Jumamosi, Kocha Mkuu wa Yanga anatarajiwa kuandika historia mpya wakati timu hiyo ikijiandaa kuwavaa Biashara United ya mkoani Mara katika mchezo wa raundi ya nane ya Ligi Kuu Bara.


 


Mchezo huo ni muhimu kwa Yanga ambao kama watashinda, watafi kisha pointi 22, na kuzidiwa mchezo mmoja na Azam ambao jana walitarajia kucheza na JKT Tanzania.




Yanga hadi hivi sasa ikicheza michezo saba, hajaipoteza na imefanikiwa kushinda michezo yake sita mfululizo huku wakitoa sare ya 1-1 dhidi ya Prisons ikiwa ni mechi yao ya kwanza ya msimu huu.Hata hivyo mchezo dhidi ya Biashara hautarajiwi kuwa mwepesi kutokana na ubora wa timu zote.


 


Biashara wanashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi wakiwa wamejikusanyia pointi 16 wakicheza michezo nane.




Rekodi anayoisaka Kaze ni kupata ushindi wa kwanza kwenye Uwanja wa Karume, Musoma ambao tangu Biashara imepanda kucheza ligi, Yanga haijawahi kupata ushindi wowote.Yanga wamekutana na Biashara kwenye uwanja huo mara mbili kati ya michezo hiyo, wamepata sare mmoja huku mwingine wakifungwa bao 1-0 baada ya kupanda daraja.


 


Hivyo katika mchezo wa leo, Kaze atakuwa na jukumu la kuhakikisha anaandikisha historia mpya kwa kuipa Yanga ushindi wake wa kwanza hapo Musoma.Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo, Kaze alisema kuwa: "Maandalizi kuelekea mchezo wetu dhidi ya Biashara yanakwenda vizuri, kikubwa ni kutarajia mabadiliko ya kikosi changu cha kwanza.




"Tunacheza michezo minne katika siku 12, hivyo hakuna mchezaji ambaye ana uhakika wa kuanza mechi zote. Baadhi ya wachezaji hawakuwa wamecheza kwa muda mrefu hivyo ni vyema kuwatumia kwa tahadhari kuwaepusha na majeraha.


 


"Lakini kingine, hali ya viwanja ambavyo tunavitumia havipo katika hali nzuri, nimepata taarifa Uwanja wa Karume upo kama Uwanja wa CCM Kirumba ni tofauti na Uwanja wa Uhuru tuliocheza mchezo uliopita, hivyo upo uwezekano wa kuanza na washambuliaji wawili ili kuhakikisha tunaitumia vema mipira mirefu ya kushambulia."

Si kweli Mzungu ana Akili Kuliko mtu Mweusi



Hivi kwanini watu weusi mnajidharau sana, hivi leo hii ukizaa mtoto wako na ukaanza kumfundisha mzungu ni bora kuliko wewe unamtengenezea future gani, wenda ungempa ujasiri angeweza kuitawala dunia na kuwa prove wrong wazungu, nimesoma comments nyingi kwenye uzi mmoja umeandikwa "je mzungu ana akili kuliko mtu mweusi?" Majibu ya watu wengi yamenisikitisha sana jinsi Waafrika tunavojidharau, kuna kazi kubwa sana ya kubadilisha mitazamo ya waafrika especially watanzania otherwise tutaendelea kutawaliwa, just imagine mzungu anasoma comment zako na unaandika comment za kujishusha thamani tena kwa madaha na kufurahi.

Nahisi hawa ndiyo wakikutana na wazungu wanachekacheka badala ya kuconcetrate kwe conversation na mwisho wa siku wana sign contract ambazo hawazielewi kisa tu kumuona mzungu kama Mungu, na wakati ni watu wa kawaida tu. Na yawezekana kabisa ukawa unamzidi hadi intelligence bila ww kujua kama unamzidi kutokana na imani potofu.

Binafsi nimegundua watu wengi wanajudge akili kutokana na standard za waliowachapa viboko (wazungu).

Kumbukeni utumwa ni coincidence tu, lakini intelligence ya mtu mmoja mmoja ni kitu kingine kabisa, watu weusi wafanya vitu vingi sana lakini dunia haijawahi kuappriciate, why? Na bila shaka hao wote wanaotoa negative comment kuhusu mtu mweusi wapo inferior na mpo weak nyie kama nyie na sio mtu mweusi. Intelligence has nothing to do with colour. Mkienda kusoma na kuspecialize katika psychology mtajua naongelea nini.

Any body can climb to the top amd reach the highest dream of power, colour is nothing but colour.

Tetemeko la ardhi lapiga Uturuki


Tetemeko la Ardhi lililotokea mchana wa Ijumaa ya tarehe 30 Oktoba 2020 katika Ukanda wa Bahari ya Aegean limeharibu miundombinu katika Miji ya Pwani.

Watu katika Mji wa Izmir uliopo Magharibi mwa Uturuki, wamekusanyika katika mitaa baada ya kuyakimbia majengo yao wakitafuta usalama. Meya wa Mji huo amethibitisha kuwa takriban majengo 20 yameharibiwa.

Taarifa zilizotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Suleyman Soylu kupitia mtandao wa 'Twitter' ni kuwa Miji mingine iliyoharibiwa na tetemeko hilo ni Bornova, Bayrakli.

Aidha, Waziri Suleyman Soylu ameongeza kuwa Uchunguzi bado unaendelea katika eneo hilo.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa takriban watu wanne (4) wamefariki huku 120 wakiwa wamejeruhiwa kufuatia Tetemeko hilo.

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Yafungua Awamu ya Tatu ya Udahili wa mwaka wa masomo wa 2020/2021

 Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetangaza kufunguliwa kwa Awamu ya Tatu ya udahili wa Shahada ya Kwanza kwa mwaka wa masomo wa 2020/2021 kuanzia Oktoba 30 hadi Novemba 4.

Katibu Mtendaji wa TCU, Prof. Charles Kihampa amesema, hatua hiyo imekuja kufuatia baadhi ya waombaji kukosa udahili na Jumuiya ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (TAHLISO) na baadhi ya Vyuo vyenye nafasi kupeleka maombi ya kuongezeka muda.

Kufunguliwa kwa dirisha la Awamu ya Tatu kunatoa fursa kwa waombaji ambao hawakuweza kudahiliwa au hawakuweza kuomba udahili katika Awamu mbili zilizopita kutumia nafasi hii ili kupata udahili.

Aidha, amewakumbusha waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja katika Awamu ya Kwanza na wale wa Awamu ya Pili kujithibitisha katika chuo kimojawapo kuanzia sasa.

 



Marapa Matajiri Zaidi Duniani Hawa Hapa



KWA hapa Bongo, inaaminika mastaa wa wanaoimba, ndio matajiri zaidi kuliko wale wa kufokafoka (Hip Hop).


Tofauti na mtazamo huo wa Kibongo, huko Marekani wapo mastaa ambao ni wa hip Hop lakini wana utajiri wa kutisha.


Twende tukaitazame Top Five ya mastaa wa Marekani lakini pia duniani kote wanaotajwa na mitandao mbalimbali kuwa ndio wanaoongoza kwa utajiri:


KANYE WEST


Kanye West ni moja kati ya marapa bora wa muda wote. Mafanikio yake makubwa ya kwenye mitindo na fasheni ndiyo yamechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza utajiri wake. Kingine kilichochangia mapato yake, Kanye ameachia sokoni albamu 9 ambazo karibia zote zimeuza kwa kiwango cha juu (multi-platinum).


Kanye ameuza karibu nakala milioni 100 duniani kote. Miongozi mwa dili zinazomuingizia mapato ni pamoja na ubalozi ikiwemo wa kampuni ya Adidas. Kwa ujumla, Kanye ana utajiri wa Dola Bilioni 3.2 (Shilingi Trilioni 7. 4) .


JAY Z


Mkali huyu kutoka pande za Brooklyn ambaye ni mjasiriamali ndiye rapa wa kwanza kuwa bilionea katika historia. Jamaa ameweka kibindoni Dola Bilioni 1 (Trilioni 2 .3) peke yake. Lakini ukisema uchanganye utajiri wake na wa mkewe ambaye pia ni staa wa muziki Marekani Beyonce, wanakuwa na utajiri wa Dola Bilioni 1.5 (Shilingi Trilioni 3. 4)


Utajiri wa Jay Z unatokana na uwekezaji wake katika timu za michezo, studio za kurekodia kazi za wasanii, mavazi, kumbi za starehe na mambo mengine kibao.


P DIDDY


Mkongwe huyu naye hayupo nyuma kwenye marapa ambao kimsingi wamefanikiwa kutusua kwenye suala zima la utajiri. Kwenye akaunti yake benki kunasoma Dola Milioni 885 (Shilingi Trilioni 2.5) Mwana huyu mzaliwa wa New York ana majina kama yote, unaweza kumuita Puff Daddy, Puff, Diddy au Sean Combs.


Aliunda lebo yake ya Bad Boy Entertainment mwaka 1993. Mwaka 1997 aliachia albamu yake ya No Way Out ambayo iliuza kwa nakala nyingi (platinum) zaidi ya mara saba.


Mkwanja wake pia anautengeneza kupitia ujasiriamali wa mavazi, migahawa, vileo na kampuni ya miamvuli.


DR DRE


Tofauti na marapa wenzake, mwamba huyu amejiongeza kwa kufanya vipaji vingi ikiwemo uprodyuza, uigizaji na fundi wa sauti (audio engineer). Ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni kubwa ya vifaa vya muziki (Beats Electronics), Beats by Dre.


Jamaa huyu ambaye amewasaidia kwa kiasi kikubwa marapa wenzie wenye mafanikio kama vile Eminem, Snoop Dogg na marehemu 2Pac, akaunti yake benki inasoma mpunga usiopungua Dola Milioni 820 (Shilingi Trilioni 1. 9).


EMINEM


Marshall Bruce Mathers II, ndiyo jina alilopewa na wazazi wake kabla ya kujiita Eminem baada ya kujizolea mashabiki lukuki. Huyu ndiye anayekamata nafasi ya tano katika marapa wenye ukwasi wa kutosha kwani anao mpunga usiopungua Dola Milioni 230 (Shilingi Biloni 533.6)


Mafanikio yake yanatajwa kupatikana zaidi kwa kazi zake za muziki ambapo nyimbo zake zimekuwa na mafanikio makubwa sana sokoni duniani kote.

Marekani yafanya majaribio ya kombora lenye uwezo wa kubeba nyuklia na kusafirisha angani


Mamlaka ya Jeshi la Anga nchini Marekani imetangaza kufanya majaribio hapo jana ya kombora aina ya "Minuteman III" linaloweza kubeba nyuklia na kusafirisha angani.

Kwa mujibu wa maelezo yalitolewa na mamlaka hiyo, iliarifiwa kuwa kombora hilo lililojaribiwa kwenye kambi ya jeshi la anga ya Vandenberg iliyoko California, halikubebeshwa nyuklia wakati wa majaribio.

Maelezo zaidi yalibainisha uwezo na nguvu kubwa ya kijeshi iliyokuwa nayo Marekani, na kuthibitisha kuwa tishio kwa kipindi hiki cha karne ya 21.

Chombo cha kilichotumiwa kubeba kombora hilo hewani, kilisafiri kwa masafa ya maili 4,200 angani hadi kufikia kisiwa cha Kwajelin.

Mamlaka ya jeshi pia iliweza kuchapisha picha za urushaji wa kombora hilo katika mtandao wa kijamii.


Friday, October 30, 2020

Pompeo ahitimisha ziara Ukanda wa India-Pasifiki

 


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amekamilisha ziara yake katika nchi za Ukanda wa India-Pasifiki kwa kuitembelea Vietnam leo Ijumaa. 

Tangazo lililochapishwa na wavuti wa serikali ya Vietnam limemnukuu Pompeo akisema Marekani inaunga mkono Vietnam imara, iliyo huru na yenye ustawi. 

Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Vietnam Nguyen Xuan Phuc amesema anatumai kutakuwepo ushirikiano wa kweli baina ya nchi yake na Marekani, katika kudumisha amani kwenye ukanda wa Asia Kusini, na maendeleo yanayotokana na biashara na uwekezaji. 

Si Pompeo wala Phuc aliyeitaja China kwa jina, ingawa kauli zao zimetolewa wakati wa mvutano mkubwa na nchi hiyo katika Bahari ya China Kusini. 

Ziara ya Pompeo ilimfikisha katika mataifa ya Sri Lanka, Inndia, Maldives na Indonesia.


Maelfu ya Waislamu waandamana kuipinga Ufaransa

 


Watu wengi wameandamana katika nchi nyingi za Kiislamu baada ya sala ya Ijumaa leo, kuonyesha hasira zao dhidi ya namna Ufaransa inavyoishugulikia michoro ya vibonzo vya Mtume Mohammed. 

Miongoni mwa miji iliyoshuhudia maandamano makubwa ni Gaza katika mamlaka ya Wapalestina, mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, na mji mkuu wa Pakistan, Islamabad. 

Katika Ukanda wa Gaza, mmoja wa viongozi wa chama cha Hamas Fathi Hammad amewataka waandamanaji kuungana kukabiliana na alichokiita ''mashambulizi ya kihalifu'' yanayomlenga mtume. 

Maandamano mengine yamefanyika baada ya sala katika msikiti maarufu wa al-Aqsa kwenye mji mkongwe wa Jerusalem mashariki, huku waandamanaji wakipaza sauti zao na kusema ''Tunaitikia wito wako mtume.'' 

Maandamano yamefanyika pia katika miji mikubwa ya nchini Pakistan, ambako waandamanaji walizochoma moto picha za rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, na kutaka balozi wao nchini Ufaransa aitwe nyumbani.


Prof. Kitila Mkumbo ashinda Ubunge Jimbo la Ubungo

Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Ubungo, Beatrice Dominic,  amemtangaza Profesa Kitila Mkumbo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mshindi katika jimbo hilo.

Beatrice amesema idadi ya ya wapiga kura waliojiandikisha ilikuwa 349,057 na waliojitokeza kupiga kura ni 89,656 ambapo kura halali ni 88,274 na zilizoharibika ni 1,382.

Msimamizi huyo amesema Prf.Mkumbo amepata kura 63,221 akifuatiwa na mgombea wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniphace Jacob,  aliyepata kura 20,620 huku mgombea wa ACT Wazalendo, Renatus Pamba,  akipata kura 2,188.

 

Maneno ya Bonnah Baada ya Kumdondosha Mrema

 


Mgombea ubunge wa Chama Cha Mapinduzi,(CCM), Bonnah Kamoli, kwa mara nyingine tena amefanikiwa kushinda nafasi ya ubunge katika jimbo la Segerea dhidi ya mpinzani wake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ,CHADEMA,John Mrema.

 

Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi,Bonnah Kamoli, ametangazwa kuwa mbunge mteule wa Jimbo la Segerea kwa kupata kura 76,828 akifuatiwa na John Mrema wa CHADEMA aliyepata kura 27612.


Akizungumza baada ya kupata ushindi huo Kamoli amesema''Miezi miwili tumefanya kampeni za kistaarabu tumemaliza siasa sasa tunaenda kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya jimbo la Segerea kwa hiyo niwaombe muendelee kuniunga mkono'' 


Aidha amelipongeza Jeshi la polisi pamoja na Tume ya uchaguzi kwa kuhakikisha haki inatendeka na kuendesha uchaguzi wa huru na wenye amani


Source

Sita mbaroni kwa kuvunja na kuchoma nyaraka za ofisi ya Afisa Mtendaji

 


WATU sita wamekamatwa wilayani Ukerewe wakidaiwa kuchoma nyaraka mbalimbali za ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Kagunguli.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro alithibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao jana wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuulizwa na gazeti hili kuhusu tukio hilo.

Alisema watu sita bila kuwataja majina, wanashikiliwa na jeshi la polisi wilayani Ukerewe kwa tuhuma za kuvunja mlango wa jengo la ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kata ya Kagunguli na kuchoma nyaraka mbalimbali za ofisi hiyo.

"Watuhumiwa hao walikamatwa baada ya kuchoma karatasi (nyaraka) mbalimbali kwenye ofisi hiyo ya Mtendaji wa Kata kwa hisia kuwa kulikuwa na karatasi za ziada za kupigia kura,kabla ya kufanya tukio hilo walivunja mlango wa jengo hilo lenye ofisi sita,"alisema Muliro.

Alisema kuwa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo utakapokamilika litawafikisha mahakamani kwa mujibu wa sheria ili kujibu tuhuma zinazowakabili.

NYUMBA YA MBUNGE MTEULE SHINYANGA MJINI PATROBAS KATAMBI YANUSURIKA KUCHOMWA MOTO... SALOME MAKAMBA ASAKWA


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akizungumza na waandishi wa habari leo

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga linafanya uchunguzi kuhusiana na tukio la jaribio la kuchoma moto nyumba ya Mbunge Mteule wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi (CCM) iliyopo mtaa wa Ushirika Mjini Shinyanga huku likiwatafuta na kuwakamata Aliyekuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA Salome Makamba na mdogo wake Timoth Makamba wakihusishwa na tukio hilo.

Akitoa Taarifa kwa Vyombo vya Habari leo Oktoba 30,2020 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa sita na dakika 45.

 "Majira ya saa saba kasorobo, Mbunge Mteule Patrobas Katambi akiwa amelala  nyumbani na ndugu zake walisikia kishindo juu ya paa la choo cha nje ambacho kipo katika eneo la uzio wa nyumba hiyo ndipo walipotoka nje na kuona moto ukiwaka juu ya paa la choo pamoja na dumu lenye mafuta aina ya petroli",ameeleza Kamanda Magiligimba.

"Wakati  wakiendelea kuzima moto huo waliona gari aina ya Toyota Klugger lenye rangi ya silver likikimbiliwa na watu wawili na kisha watu wale waliingia ndani ya gari lile na kutoweka",amesema Kamanda Magiligimba.

Kamanda Magiligimba amesema baada ya kufanikiwa kuzima moto huo waliona gari lile lile likipita barabara ya lami ya Shinyanga – Mwanza ndipo walipoamua kulifuatilia na dereva wa gari hilo baada ya kugundua anafuatiliwa aliamua kuingia hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga na kuliacha gari hilo kisha kukimbia.

"Wakati wa kuwaweka chini ya ulinzi watu hao ilitokea purukushani ndani ya uzio wa hospitali na gari ya polisi iliyokuwa doria ilifika mapema na kufanikiwa kuwakamata watu wawili ambao ni Wilson Mhando Suluti (30) mkazi wa Bugweto na Jackson Raphael Peter (27) mkazi wa Bugweto wakiwa ndani gari hilo lenye namba za usajili T.729 DFP aina ya Toyota Klugger rangi ya Silver mali ya Salome Makamba aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CHADEMA",amefafanua Kamanda Magiligimba. 

"Ilibainika kuwa watu hao tuliowakamata wao ndiyo waliokuwa kwenye eneo la tukio kulingana na mavazi waliyovaa. Baada ya mahojiano, watu hao walikiri kuwa gari hilo ni la Salome Makamba na dereva aliyetoroka ni Timoth Makamba ambaye ni mdogo wake Salome Makamba",ameongeza Kamanda Magiligimba.

Amesema polisi walifika nyumbani kwa Salome Makamba na kufanya upekuzi kisha kuwakamata watu wengine wawili ambao ni Justine Owesiga (35) Mkazi wa Ndala Shinyanga na Gibson Mkongwa (31) mkazi wa Iringa waliokutwa kwenye nyumba hiyo.

"Juhudi za kuwatafuta na kuwakamata Salome Makamba na Timoth Makamba ambaye ndiye dereva wa gari hilo lililotelekezwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga zinaendelea. Gari husika linashikiliwa na watuhumiwa hao wanne na watafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika",amesema.

Amesema Salome Makamba aliachiwa jana kwa dhamana baada ya kushikiliwa na jeshi la polisi Oktoba 28,2020 kwa tuhuma za kumshambulia msimamizi wa uchaguzi kituo cha kupigia kura cha Bugweto B, Farida John na kumuumiza ambapo aliomba aone matokeo na baada ya kutoridhika nayo aliyachana na kuanza kumshambulia msimamizi huyo wa uchaguzi akiwa na wafuasi wake.

"Natoa wito kwa wanasiasa na wafuasi wao kuacha mihemko ya kisiasa inayopelekea uvunjifu wa amani badala yake wafuate sheria,kanuni na taratibu z auchaguzi na Jeshi la polisi halitasita kamwe kuchukua hatua kali za kisheria kwa mtu au watu au kikundi chochote chenye nia ya kuvuruga amani nchini",amesema Kamanda Magiligimba.


Soma pia : 

KATAMBI ASHINDA UBUNGE SHINYANGA MJINI....CCM YANYAKUA KATA ZOTE ...SALOME MAKAMBA AKAMATWA






Wapiga kura zaidi ya milioni 80 wamemaliza kupiga kura Marekani



Zaidi ya wamarekani millioni 80 wamepiga kura ya mapema kabla ya uchaguzi wa rais wa tarehe 3 Novemba, kulingana na takwim zilizokusanywa jana na taasisi ya chuo kikuu cha Florida inayofwatilia uchaguzi wa marekani. Kiwango hicho kimevunja rekodi, ni zaidi ya asilimia 58 ya watu waliojitokeza kupiga kura kwenye uchaguzi wa mwaka 2016, na inaonyesha umuhimu wa uchaguzi wa mwaka huu ambapo kinyanganyiro ni kati ya rais Donald Trump, mrepublican na mdemocrat makamo rais wa zamani Joe Biden. Idadi kubwa ya watu walipiga kura kwa njia ya posta au kwenye vituo vya kura, kutokana na hofu kwamba virusi vya corona vinaweza kusambaa siku ya uchaguzi. Wataalamu wanatabiri kuwa idadi ya wapiga kura mwaka huu itazidi millioni 138 waliopiga kura kwenye uchaguzi wa rais wa 2016, alioshinda Donald Trump. Kura millioni 47 pekee ndizo zilipigwa kabla ya siku ya uchaguzi mwaka 2016. Imetayarishwa na Patrick Nduwimana, VOA, Washington DC



Source

Azerbaijan yaharibu mfumo wa kombora la Armenia


Katika picha zilizoshirikiwa na Wizara ya Ulinzi ya Azerbaijan, inaonekana kuwa mfumo wa kombora la Smerch uliharibiwa kwa risasi.

Raia 25 wamepoteza maisha na zaidi ya watu 70 wamejeruhiwa katika mashambulizi yaliyofanywa na jeshi la Armenia na makombora ya Smerch na mabomu katika mji wa Berde, kilomita 60 kutoka sehemu ya mapigano.

Kwa upande mwingine, jeshi la Azerbaijan linaendelea kuwajeruhi wanajeshi wa Armenia, ambao waliwafyatulia risasi wanajeshi wa Azerbaijan na makazi yao katika pande tofauti.

Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Azerbaijan imeelezwa kuwa mapigano hayo yaliendelea haswa katika mwelekeo wa Agdere, Hocavend na Gubadli.

Ndege 2 Su-25 mali ya jeshi la Armenia, mizinga 3 T-72, gari 1 la vita, "Smerch" 2 na 1 makombora mengine vimeangamizwa na jeshi la Azerbaijan.

Azerbaijan imeonyesha kuwa na udhibiti katika eneo la mapigano.

CHADEMA YAPATA MBUNGE WA KWANZA UCHAGUZI MKUU 2020.... NI AIDA KHENANI, AMEMBWAGA ALLY KEISSY


Aida Khenani, mbunge mteule wa jimbo la Nkasi Kaskazini kupitia CHADEMA.

Msimamizi wa Uchaguzi jimbo la Nkasi Kaskazini, amemtangaza Aida Khenani, wa CHADEMA kuwa ndiye mbunge wa jimbo hilo baada ya kupata kura 21,226, na kumshinda Ally Keissy wa CCM aliyepata kura 19,972 na hivyo yeye kuwa mgombea wa kwanza kukitetea chama chake katika nafasi hiyo.

Aida Khenani kabla ya Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuvunjwa, alikuwa ni Mbunge wa Viti Maalum kuanzia mwaka 2015 hadi 2020 kupitia chama chake cha CHADEMA.

Mbali na CHADEMA kupata mtetezi wake wa kwanza Bungeni mpaka sasa tangu matokeo ya uchaguzi yaanze kutangazwa, chama cha CUF pia kinaye mwakilishi kutoka jimbo la Mtwara Vijijini, ambaye ni Shamsia Mtamba, aliyepata kura 26,262, na kumshinda aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia CCM Hawa Ghasia aliyepata kura 18,505.

Katika matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28 mwaka huu, mpaka sasa vyama vya upinzani yaani CHADEMA na kile cha CUF kina wawakilishi wawili pekee wa ubunge ambao tayari wamekwishatangazwa, huku wabunge wengine wa vyama vya upinzani wakishindwa kutetea majimbo yao ambayo kwa asilimia kubwa yamechukuliwa na CCM.

Chanzo - EATV

Kimbunga Molave chaua watu 31



Mchakato wa uokozi unaendelea nchini Vietnam hii leo, baada ya maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na KimbungaMolave.


Death toll in Vietnam from Typhoon Molave reaches 13


Mamia ya wanajeshi wenye vifaa vizito wametumwa katika maeneo ya ndani ya jimbo la Quang Nam kulikotokea maporomoko ya ardhi na ambako watu 19 wameuawa na wengine 48 hawajulikani walipo.


Aidha miili ya wavuvi 12 imeopolewa baharini hii leo na wengine 14 hawajulikani walipo baada ya boti yao kuzama. Kimbunga hicho kinatajwa kuwa ni kibaya kuwahi kushuhudiwa kwa miongo kadhaa.


21 killed, dozens missing after Typhoon Molave lashes Vietnam | Vietnam |  Al Jazeera


Na kimepiga katikati mwa nchi, ambako tayari kumekuwa kukinyesha mvua kali kwa wiki kadhaa zilizosababisha vifo vya watu wapatao 160.


Zaidi ya watu milioni moja wameathiriwa na dhoruba hizo kali ziliozopiga kwa wiki kadhaa. Mashirika ya kutoa misaada nayo yameelemewa kutokana na idadi kubwa ya walioathirika.

Innocent Bashungwa ashinda ubunge jimbo la Karagwe

 


Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Karagwe Godwin Kitonka amemtangaza Innocent Bashungwa kuwa mshindi wa kiti cha ubunmge wa jimbo hilo akiwa amepata kura 68,371.

Thursday, October 29, 2020

Ndejembi atangazwa kuwa Mbunge wa Chamwino

 


Msimamizi wa Uchaguzi Hlamashauri ya Wilaya ya Chamwino amemtangaza Deo Ndejembi kuwa mshindi wa kiti Ubunge wa Jimbo la Chamwino kwa kupata kura 67,092

Abass Tarimba ashinda kiti cha Ubunge Jimbo la Kinondoni

Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Kinondoni na Kawe, Aron Kagurumjuli amemtangaza mgombea ubunge wa CCM jimbo la Kinondoni Abass Tarimba ameshinda baada ya kupata kura 112,014

Tarimba amewashinda wenzake 17 Kati ya hao Suzanna Lyimo wa Chadema amepata Kura 11260 na Said Kubenea wa ACT Wazalendo amepata Kura 5,948.

 

Ester Bulaya apoteza ubunge Bunda Mjini



Ester Bulaya amepoteza jimbo la Bunda Mjini baada ya kushindwa na Robert  Maboto wa CCM  aliyepata kura 31,129 huku Bulaya akipata kura 13,258


Mwamuzi Shomari Lawi afungiwa mwaka mmoja



MWAMUZI Shomari Lawi leo Oktoba 29, 2020 amefungiwa miezi 12 kwa kushindwa kuumudu mchezo namba 50 wa Tanzania Prisons FC na Simba aliochezesha Oktoba 22, 2020 katika Uwanja wa Nelson Mandela Mkoani Rukwa.


Tundu Lissu Apinga Matokeo ya Uchaguzi



MGOMBEA wa urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, ametangaza kutokubali matokeo ya uchaguzi yanayoendelea kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kufuatia uchaguzi mkuu uliyofanyika jana Oktoba 28, 2020 nchi nzima.


Amedai kuwa kuwa uchaguzi huo ulianza kuingia dosari mapema katika kuapisha mawakala ambao ndiyo waangalizi wa uchaguzi kwa niaba ya chama chao.


Aidha amewataka Watanzania kudai haki yao kwa njia ya demokrasia na siyo kwa vurugu yoyote huku akisema jumuiya za kimataifa pamoja na jumuiya za kikanda ziingilie kati taarifa za matokeo ya uchaguzi wa Tanzania.


"EAC, SADC wasitoe taarifa za kuhalalisha uchaguzi huu. Waseme ukweli. Watanzania waingilie kudai haki yao kwa amani kwa njia ya kidemokrasia," amesema Lissu katika mkutano na waandishi wa habari.


 

Lissu ameongeza kusema kuwa chama chake kimeweka wagombea 244 wa ubunge nchi nzima, kati ya hao 63 walienguliwa, udiwani 3,754 kati yao wagombea 1,025 walienguliwa, hivyo takribani 30% walienguliwa- 'haijawahi kutokea tangu tumefanya uchaguzi wa vyama vingi nchini".


Aliongeza kusema kuwa mbali na kuwa kulikua na changamoto ya kutokuwa na fedha, hawakuweka picha za mgombea nchi nzima lakini "Watanzania walituunga mkono". Jana Lissu alisifu zoezi la upigaji kura kuwa limekwenda vizuri baada ya kumaliza kupiga kura katika jimbo lake la Singida Mashariki.


Hata hivyo Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeshakanusha madai hayo ya upinzani na kusema tuhuma zinazotolewa hazijawasilishwa rasmi na sasa inaendelea na zoezi la kupokea matokeo kutoka katika majimbo mbalimbali na kuyatangaza kwa wananchi kupitia vyombo vya habari.

KATAMBI ASHINDA UBUNGE SHINYANGA MJINI....CCM YANYAKUA KATA ZOTE ...SALOME MAKAMBA AKAMATWA

Patrobas Katambi

Na Damian Masyenene, Shinyanga
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Patrobas Katambi ametangazwa mshindi wa ubunge baada ya kupata kura 31,831.

Katambi ametangazwa mshindi wa kinyang'anyiro hicho leo Oktoba 29, 2020 na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini, Geofrey Mwangulumbi, huku mpinzani wa karibu wa Katambi, Salome Makamba wa Chadema akiambulia nafasi ya pili kwa kupata kura 16,608.

Wagombea wengine katika kinyang'anyiro hicho walikuwa ni Godwin Makomba (ACT Wazalendo) aliyepata kura 883, Charles Shigino wa NCCR Mageuzi (133), Abdallah Issa Sube (Demokrasia Makini) kura 99, Yahya Khamis wa UDP kura 69 na Malengo Elias wa TLP kura 65.

Msimamizi huyo wa uchaguzi ameeleza kuwa katika zoezi la upigaji kura Jimbo la Shinyanga Mjini, wapiga kura walioandikishwa ni 120,944, idadi ya waliojitokeza kupiga kura ni 50,453, idadi ya kura halali ni 49,688 na zilizo haribika ni 765.

Katika hatua nyingine, Mwangulumbi amebainisha kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeshinda viti vyote vya udiwani katika kata 17 za jimbo hilo.
Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salome Makamba 

Wakati huo Jeshi Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia Mgombea Ubunge wa Jimbo la Shi nyanga Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Salome Makamba kwa tuhuma za kumshambulia msimamizi wa uchaguzi kituo cha kupigia kura cha Bugweto B, Farida John na kumuumiza.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana usiku na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba  tukio hilo limetokea Oktoba 28, mwaka huu saa mbili usiku , ambapo Makamba aliomba aone matokeo na baada ya kutoridhika nayo aliyachana na kuanza kumshambulia msimamizi huyo wa uchaguzi akiwa na wafuasi wake.

ACP Magiligimba amesema baada ya kupata taarifa za tukio hilo, jeshi la polisi lilimsaka mtuhumiwa na kumkamata na upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

CHANZO - SHINYANGA PRESS CLUB BLOG


Fred Lowassa ashinda Ubunge Monduli


Msimamizi wa uchaguzi katika Jimbo la Monduli amemtangaza Fredrick Lowassa wa CCM kuwa mshindi wa Jimbo hilo kwa kupata kura 72,502 sawa na asilimia 93.23% akifuatiwa na Cessilia Ndossi wa CHADEMA aliyepata kura 4,637 sawa na asilimia 5.96%, Chogga wa ACT 485 sawa asilimia 0.62% na

Kijuu NRA 145 sawa asilimia 0.19%.


Ester Matiko abwagwa, Kembaki ashinda Ubunge Jimbo la Tarime Mjini

 

Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Tarime Mjini, Ester Matiko ameshindwa kutetea nafasi yake baada ya kushindwa na mshindani wake, Michael Kembaki wa Chama cha Mapinduzi.

Msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo, Elias Ntiruhungwa amesema kuwa Kembaki ameshinda kwa kupata kura 18,235 huku Matiko akipata kura 10,873 na mgombea wa NCCR Mageuzi, Ester Nyagabona akipata kura 143.

Reuben Kwagilwa CCM ashinda ubunge jimbo la Handeni

 

Reuben Kwagilwa CCM ametangazwa kushinda ubunge jimbo la Handeni kwa kura 15,241 sawa na asilimia 67 dhidi ya wapinzani wake Sonia Magogo CUF amepata kura 6,713 ADC Twaha Said amepata kura 310, James Stima Chadema amepata kura 296 na Makame Semndili TLP amepata kura 31

Katambi Ashinda Ubunge Shinyanga Mjini



Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini Mkoani Shinyanga amemtangaza Patrobas Katambi wa CCM kuwa Mshindi wa kiti cha Ubunge Shinyanga Mjini.


Kura zilizopigwa 50,453

Kura halali 49,688

Kura zilizokataliwa 765

Patrobas Katambi (CCM) 31,831

Salome Makamba (Chadema) 16,608.


Sebastian Kapufi (CCM) Ashinda Ubunge Mpanda mjini


Mpanda Mjini:  Mgombea wa nafasi ya ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Sebastian Kapufi ameshinda nafasi ya Ubunge kwa kupata kura 24,020, akifuatiwa na Rhoda Kunchela wa Chadema aliyepata kura 13,611.





Mwanamke, jambo hili ni muhimu sana katika mahusiano yako

 

Kama umeolewa wewe, umechaguliwa wewe ndiyo mpenzi wake hebu acha kushindana na watu wengine, acha kushindana na X wake au wanawake wengine ambao unadhani kuwa wanamtaka mume wako. Nilazima ujue kuwa mume wako alikuwa na watu kabla yako lakini pia kuna watu bado wanamtaka na hawatajali kama ameoa au hajaoa.

Lakini yeye hajawachagua wao kakuchagua wewe, iwe ni kwamba ulimtegeshea mimba, ulienda kwa mganga au alilazimishwa na wazazi wake lakini mwisho wa siku ni kuwa yuko na wewe na hao wengine kuna kitu umewazidi hivyo huna haja ya kushindana nao tena. Umeshashinda kazi unachotakiwa kufanya ni kuulinda ushindi wako na si kushindana na wengine.

Kuhangaika kutukanana nao, kuhangaika kuvaa kama wao, kuhangaika kuwafuatilia maisha yao kunakupa hasara kuu mbili.

Kwanza ni kuwa unakuwa huishi maisha yako, unakuwa huna furaha na kazi yako kubwa ni kujilinganisha, kwamba badala ya kufurahia ndoa wewe kazi ni kuangalia wamevaa nini, wanaishije, wana nini hivyo unakuwa huna amani na huna furaha.

Pili ni kuwa unakuwa kero kwa mume wako unachosha, kwamba kama kila siku unakuwa unamuuliza mbona ulikuwa na fulani, nilikuona unaongea na fulani, fulani hivi fulani vile. Huna furaha una kisirani kila siku, unamfanya mwanaume kujiuliza hivi kweli nilifanya uchaguzi sahihi kumuoa huyu mwanamke. Si bora hata ningemuoa fulani labda ningekuwa na amani.

Unamlazimisha mume wako kuenda kutafuta amani huko kwingine, kama mwanaume kila siku akirudi nyumbani hamuwezi kuongea kitu cha maana zaidi ya kukagua simu yake, kuulizia alikuwa wapi na na nani, kumzungumzia X wake basi atatafuta sehemu ya kupumzisha kichwa. Yaani mtu ofisini akutane na kero za bosi au wateja na akirudi nyumbani anakutana na kero za mke ambaye amemuoa, atachepuka tu hamna namna!

Sisemi uvumilie kama mume wako anachepuka au anafanya ujinga huko nje hapana, lakini kama hajakuonyesha dalili yoyote ya kuchepuka, kama hajaonyesha hata kama anawataka hao watu unaowawaza, hebu acha kisirani eti kisa kaongea nao. Mwanaume awezi kuacha kuongea na mtu fulani eti kisa hujiamini na unadhani atakusaliti nao!

Kwanza kama kweli ni mchepukaji mzuri watu anaochepuka nao hata namba za simu zao huwezi kukuta katika simu yake. Hata siku moja huwezi kukuta anaongea nao hivyo kwanini ujipe presha na vitu ambavyo vipo kichwani kwako tu. Acha kuharibu ndoa yako na kama hujui nini cha kufanya basi jifunze jinsi ya kujipa furaha yako. inawezekana unahisi unasalitiwa kumbe unamlazimisha mume wako kukusaliti.

Wednesday, October 28, 2020

Faida ya kutumia mbolea katika kilimo cha maharage

 

Wakulima wengi wamekuwa wakipuuza kutumia mbolea katika kilimo cha maharage huku baadhi yao wakiwa hatambua kama ipo haja ya kutumia mbolea katika kilimo hicho, ila ukweli ni kwamba maharage hayahitaji nitrogen kwa wingi kwa sababu mizizi ya maharage husaidiana na viumbe hai (nitrogen fixing bacteria) waishio kwenye udongo kutengeneza nitrogen.

Hata hivo maharage yanahitaji phosphorus ambayo hupatitikana katika mbolea kwa ajili ya kuboresha mizizi na potassium kwa ajili ya kuuandaa mmea kwa ajili ya kutoa maua mengi na kuzaa matunda bora.

Ikiwa shamba lililimwa zao ambalo liliwekwa mbolea kama vile Urea au CAN basi huna haja ya kuweka tena mbolea za nitrogen badala yake unaweza kuweka TSP au DAP Kg 60 kwa hekta wakati wa kupanda. Au mbolea ya minjingu (Minjingu Rock Phosphate) Kg 250 kwa hekta moja wakati wa kupanda.

Kama shamba limechoka sana au halikuwekwa mbolea za nitrogen msimu uliopita basi tumia NPK katika uwiano wa 5:10:10 kiasi cha Kg 30 kwa hekta, nayo iwekwe wakati wa kupanda. Mbolea zote ziwekwe sentimita tano hadi 10 kutoka kwenye shina/shimo la mmea na urefu wa sentimita 3 hadi 5 kwenda chini.

Pia unaweza kutumia mbolea ya zizi/samadi (tani 5 - 10 kwa hekta) au mbolea ya kijani (green manure, tani 5 kwa hekta). Mwaga/tawanya samadi kwenye shamba lote halafu ichangane vizuri na udongo kwa kulima kwa plau (la tractor au ng'ombe). Maana yake ni kwamba mwaga samadi kabla ya kulima shamba lako kwa trekta/ng'ombe.

Mbolea ya kijani inapatikana kwa kusafisha shamba halafu ukaliacha mpaka majani/magugu yakaota kisha ukalilima kwa trekta au ng'ombe (likiwa na magugu hivyo hivyo) lakini kabla hayajatoa mbegu halafu ukapanda. Mbolea ya minjingu inaweza kutumika pamoja na samadi na mbolea ya kijani.

Lakini lincha ya kueleza ya kwamba maharage yanahitaji mbolea kwa wingi kama ambavyo nimeeleza hapo awali,

Maharage huhitaji mvua ya kutosha kipindi cha kabla ya uwekaji maua (before flowering) na kipindi cha ukuaji wa vitumba vya maharage (podding). Huhitaji unyevu kidogo kipindi cha kuweka maua (during flowering) na ukavu kipindi cha kukomaa (pod maturation) na kukauka vitumba.
Vitumba ni matunda (pods). Ikiwa utatumia njia nyingine yoyote ya umwagiliaji angalia maharage yako yapo katika hatua gani kabla hujapanga ratiba yako ya umwagiliaji (irrigation schedule

Source

Mgombea Aeleza Sababu ya Kumnunulia Magufuli Keki

 


Mgombea ubunge wa jimbo la Ubungo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Profesa Kitila Mkumbo, amesema kuwa mara baada ya kupiga kura, ataenda Mlimani City kumnunulia mgombea Urais wa chama hicho Dkt. John Magufuli, keki ya 'birthday', kwa lengo la kumtakia heri na mafanikio.

 

Kauli hiyo ameitoa hii leo Oktoba 28, 2020, mara baada ya kukamilisha zoezi lake la upigaji wa kura, na kuahidi jambo hilo.


"Katika kutimiza miaka yake 61 nimnunulie keki, nimtakie afya njema na nimtakie mafanikio makubwa katika kuongoza Tanzania kwa awamu yake ya pili", amesema Profesa Kitila.


Zoezi la upigaji wa kura nchini Tanzania limeanza leo Oktoba 28, 2020, saa 1:00 asubuhi na kuhitimishwa saa 10:00 jioni na kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi jumla ya Watanzania Milioni 29 walikuwa wamejiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura.

Viongozi wa Uturki washutumu jarida la Charlie Hebdo kuhusu katuni yake ya Erdogan


Viongozi wa Uturki washutumu jarida la Charlie Hebdo kuhusu katuni yake ya Erdogan
Maafisa wa Uturuki wamelikosoa vikali jarida la Charlie Hebdo la Ufaransa kwa kuchapisha kibonzo kinachomdunisha rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan. 

Wamelituhumu jarida hilo kwa kuchochea chuki.Kibonzo hicho kimezidisha mzozo kati ya Uturuki na Ufaransa ambao ulianza baada ya msimamo wa rais wa Ufaransa Emmanuel Macron dhidi ya Uislamu kuhusu uhuru wa mawazo na kujieleza, baada ya mwalimu aliyewaonyesha wanafunzi vibonzo vya Mtume Mohammed kuchinjwa. 

Vibonzo vya Mtume Mohammed vimewaghadhabisha wengi katika ulimwengu wa Kiislamu. Lakini Erdogan ndiye alikuwa mstari wa mbele dhidi ya Ufaransa na kutilia mashaka hali ya afya ya akili ya Rais Macron. Matamshi ya Macron pia yalichochea maandamano na wito kwa Waislamu kuzisusia bidhaa za Ufaransa.

HII Hapa Faida Ya Kufikiri Kama Tajiri Hata Kama Huna Kitu Mfukoni...!!!


Kuna wakati unakuwa unashangaa kwa nini watu wengine ni matajiri sana na wakati wengine ni maskini. Najua umekuwa na mawazo mengi juu ya hili na kufikiri pengine hawa ni watu wenye bahati sana, wamezaliwa kwenye familia tajiri au pengine watu hawa wana kazi nzuri na wamezaliwa kwenye nchi zenye mafanikio.

Ni ukweli, yote haya yanaweza kuwa majibu kwa namna fulani, lakini hata hivyo kipo kitu kimoja muhimu sana ambacho kinafanya watu wengine kuwa matajiri na wengine kuendelea kubaki kwenye umaskini. Kitu hiki ambacho kinaleta tofauti zote hizo si kingine bali ni mawazo yako.

Badala ya kuendelea kulalamika kwa nini upo kwenye hali ngumu, kwa nini maisha yako yako magumu, kwa nini hufanikishi malengo yako fulani ambayo unayatamani sana karibu kila siku, kitu cha kwanza ambacho unatakiwa kukiangalia, angalia sana mawazo yako hasa linapokuja suala la pesa.

Mawazo yetu mara nyingi sana yana nguvu ya kutupa kitu chocho ambacho tunakihitaji katika maisha yetu. Mawazo yetu yamepewa uwezo wa kuumba fursa na kila hali ambayo tunaitaka ijitokeze kwetu. Kinachotakiwa kufanyika ni kuamua kutumia  mawazo haya kwa ufasaha hadi kuweza kutufanikisha.

Kwa hiyo mpaka hapo unaelewa kabisa faida kubwa ya kufikiri kama tajiri hata kama huna kitu mfukoni inakusaidaia wewe kuweza kupata kile unachokihitaji kwa hatua. Ni suala la kuujaza ubongo na akili yako taarifa za kitajiri, taarifa za mafanikio na hapo utatengeneza mazingira mazuri ya kufanikiwa.

Epuka sana kuwa na mawazo mgando, mawazo ambayo kila wakati  yanalenga kukukwamisha. Ukiwa na mawazo hayo utateseka sana kwenye dimbwi la umaskini na hautaweza kutoka hapo. Kikubwa endelea kuwa chanya mpaka kuhakikisha ndoto zako zinatumia na kuwa kweli.

Source

Rais wa FIFA apata Corona

 


Rais wa shirikisho la soka duniani (FIFA) amethibitika kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona na sasa amejitenga ili kuangalia afya yake.


Infantino mwenye umri wa miaka 50 sasa amelazimika kujitenga kwa walau siku 10 kabla ya kupimwa tena kuhusiana na mwenendo wa afya yake.


Pamoja na Inafantino kujitenga lakini FIFA tayari imesema imewapa taarifa watu wote waliokutana na Infantino siku chache kabla ya kuthibitika kuumwa na kuwataka wachukue hatua stahiki.

Wakazi wa Mji wa Babati wajitokeza kupiga kura, kumchagua Rais na Diwani


Wananchi wa Babati mjini  mkoani Manyara wakiwa kwenye foleni  katika kituo cha kupigia kura kituo cha  Shule ya Msingi Osterbay ili kumchagua Diwani na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi unaofanyika leo Jumatano Oktoba 28,2020 nchini kote.

Jimbo la Babati Vijijini na Mjini hakuna wagombea Ubunge baada ya  wagombea wake  kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi  kupita bila kupingwa ambapo kwa sasa wanasubiri kuapishwa.

Msemaji mkuu wa Serikali apiga kura, asifu amani na utulivu Dodoma


Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, amekamilisha haki yake ya kikatiba kwa kupiga kura katika eneo la Kilimani, jijini Dodoma.

Katika eneo hilo ambapo pia awali na baadaye walionekana viongozi wengine mbalimbali wa Serikali, Chama na taasisi binafsi, Dkt. Abbasi alikaa kwenye foleni kama kawaida na wananchi wengine na alipomaliza kupiga kura akasisitiza:

"Nimekamilisha haki yangu ya kikatiba kwa furaha sana kwa sababu tukiwa pale kwenye foleni tunapiga stori za hapa na pale wananchi walikuwa wanasema sio wote tuliopiga nao kura mwaka 2015 leo wamepata bahati tena kama hii kwa maana ya uhai kushiriki nasi. Hivyo ni jambo si tu la kikatiba lakini lenye hisia kubwa kibinadamu na kiroho mtu anapolitimiza."

Dkt. Abbasi alieleza kuridhishwa na hali ya utulivu kituoni hapo na kusisitiza ambao hawajakamilisha haki yao wajitokeze kuwahi kabla ya muda uliowekwa na Tume kukamilika.

"Kituoni kwetu hapa na kwingine nilikopita hapa Dodoma hali ni shwari. Tume imejipanga hasa utaratibu ni mzuri na wa uhakika kwani kila hatua unaelekezwa wasimamizi na makarani wa uchaguzi na mawakala wa vyama wanajiridhisha kwa kila jina linalotajwa.

"Ukiacha kelele za baadhi ya wanasiasa wachache Watanzania wengi wameitikia wito wa amani na wengi tuliopiga nao kura hapa kila mmoja anasema anarejea nyumbani au kwenye shughuli zake kwa ajili ya kuendelea na masuala mengine atasubiri matokeo kuanzia jioni," alisema Dkt. Abbasi.

Dkt. Abbasi ametumia muda huo pia kuvipongeza vyombo vya habari kwa kazi kubwa waliyoifanya kuripoti kampeni za vyama mbalimbali na kuvitaka kumaliza vyema zoezi hili la uchaguzi kwa kufuata taratibu za Tume hasa katika kutangaza matokeo ya awali hadi yale ya mwisho.

Lulu Michael Ajivunia Kulea

 


STAA wa filamu za kibongo, Elizabeth Michael 'Lulu', amesema anamshukuru Mungu kwa kumsaidia kumlea vizuri mdogo wake Erick mpaka sasa amefanikiwa kuhitimu elimu yake ya msingi Shule ya Feza Boys.

 

Akizungumza na Mikito Nusunusu, mrembo huyo mwenye mvuto wa aina yake, alisema kuwa anatamani kuzungumza ni jinsi gani anavyojisikia vizuri kuona mtoto anayemlea tangu akiwa mdogo anazidi kuwa kijana bora machoni mwa watu.

 

"Namshukuru Mungu kwa hili, kulea sio kazi ndogo kuna muda naweza kusema Erick sio mdogo wangu bali ni mwanangu kwa sababu nimeanza kumlea tangu akiwa mdogo mpaka hapa alipofikia leo, ni jambo jema kuona ameshahitimu elimu yake ya msingi na muda si mrefu ataenda kujiunga na elimu ya sekondari, natamani kulia kwa hii hatua niliyofikia," alisema Lulu anayefanya poa kunako anga la Bongo Muvi.


STORI: MEMORISE RICHARD

Mondi Awafunika Kiba, Harmo Kupiga Mabilioni

 


KWA sasa katika gemu la muziki hasa wa Bongo Fleva, kumekuwa na ushindani mkubwa ambao umekuwa ukitia chachu kwenye muziki wa hapa Bongo.

 

Wasanii wengi wamekuwa wakishindana kwa kuachia kazi kali na kukimbizana kwa spidi kwenye mitandao ya kuuza, kusikiliza, kupakua na kutazama muziki (platforms).


Mabosi wa lebo kubwa hapa Bongo ambazo zinaongoza kwa kufanya poa na hata kunyanyua vipaji mbalimbali hapa nawazungumzia Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' au Mondi, Ali Saleh Kiba 'King Kiba' na Rajabu Abdul 'Harmonize' au Harmo.

 

Lakini katika wote hao, Mondi ameonesha kuwafunika wenzake kwa kuingiza kipao kikubwa kwa mwaka huu japo ni makadirio ya mitandao ambayo inaweka kazi za wasanii na kuuza.


MIKITO NUSUNUSU inakudadavulia kwa kina kazi za wanamuziki hawa kama ifuatavyo:

 

MONDI


Huyu ni bosi wa Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), ameongoza kwa kuwafunika wenzake kwenye mitandao ya muziki kwa kukadiriwa kuingiza kiasi cha pesa si chini ya Shilingi Bilioni 3 kwa mwaka.

 

Mondi anaingiza mapato hayo kwa kupitia ngoma zake ambazo zinasifika kukimbiza mitandaoni huko. Ngoma kali ambazo zimekimbiza sana kwenye mtandao wa YouTube ni pamoja na Jeje yenye watazamaji milioni 35, Hainisumbui yenye watazamaji milioni 1.5, Gere yenye watazamaji milioni 20 mpaka sasa, Ongeza (milioni 1.3), zote zikitazamwa kwa jumla ya milioni 57, kwenye mtandao wa YouTube tu na bado kuendelea kukimbiza mitandao mingine ya kusikiliza na kuuza muziki.


 

Mbali na ngoma hizo pia album yake ya A Boy From Tandale, imechangia kuongeza mapato yake na kufikia kiwango hicho.

 

KIBA


Ali Saleh Kiba almaarufu King Kiba, huyu ni bosi wa Lebo ya King's Music ambayo nayo inasimama katika lebo bora hapa Bongo.


Kiba ni mkongwe kwenye gemu hili la muziki na anasifika kutoa kazi kali japo sio kwa mpigo kama ilivyo kwa wasanii wengine.

 

Kiba anakadiriwa kuingiza mapato si chini ya Shilingi Milioni 139 kwa mwaka kutokana na ngoma zake kutazamwa na kusikilizwa sana mitandaoni.

 

Ngoma zake zilizofanya poa kwa kutazamwa sana kwenye mtandao wa YouTube kwa mwaka huu ni pamoja na Dodo yenye watazamaji milioni 10, So Hot yenye watazamaji milioni 3.2, Mediocre (milioni 3) na Mshumaa (milioni 6). Mpaka sasa zote kwa jumla zikitazamwa na mara milioni 22 kwenye mtandao wa YouTube na kukimbiza pia kwenye mitandao mingine ya muziki.

HARMONIZE


C.E.O wa Lebo ya Konde Music Gang, Rajabu Abdul 'Harmonize' au Harmo, ni mwanamuziki ambaye anasifika kwa kutoa kazi kali tangu akiwa na lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) ambapo alijitoa na kuanzisha lebo yake mwenyewe.


Harmo anakadiriwa kuingiza mapato si chini ya Bilioni 1 kwa mwaka kutokana na kazi zake kukimbiza kwenye mitandao ya kusikiliza, kupakua, kuuza na kutazama muziki (platforms).

 

Ngoma zake zilizoongoza kwa kutazamwa sana kwenye mtandao wa YouTube kwa mwaka huu ni pamoja na, Jeshi yenye watazamaji milioni 4, Fall in Love yenye watazamaji milioni 4, Mpaka Kesho (milioni 3), Wife (milioni 3), Mama (milioni 2), zote zikitazamwa mara milioni 16 mpaka sasa kwenye mtandao wa YouTube.


Album yake ya Afro East aliyoizindua mwaka huu ikiwa imebeba ngoma 18 nayo imetajwa kuingiza mauzo mazuri mitandaoni.


MAKALA: HAPPYNESS MASUNGA

HUSSEIN MWINYI NA MAALIM SEIF WAPIGA KURA ZANZIBAR

 Wagombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Hussein Mwinyi na Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, tayari wamepiga kura hii leo visiwani humo, huku kila mmoja wao akiwaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kupiga kura.

"Nawapongeza Wanzanzibar wote ambao wametumia haki yao ya kupiga kura na niwaombe ambao hawajafika waendelee kujitokeza kupiga kura na hatimaye zoezi liishe kwa amani" Dkt Mwinyi

Kwa upande wake mgombea urais kupitia chama cha ACT Wazalendo, Maalim Seif amesema kuwa masuala ya kuwatoa mawakala katika vituo siyo sahihi kwani wakala anakuwepo mahala pale kwa lengo la kulinda kura za mgombea wake


 


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...