Wananchi wa Babati mjini mkoani Manyara wakiwa kwenye foleni katika kituo cha kupigia kura kituo cha Shule ya Msingi Osterbay ili kumchagua Diwani na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi unaofanyika leo Jumatano Oktoba 28,2020 nchini kote.
Jimbo la Babati Vijijini na Mjini hakuna wagombea Ubunge baada ya wagombea wake kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi kupita bila kupingwa ambapo kwa sasa wanasubiri kuapishwa.