Tuesday, June 30, 2020
Kanye West Afunguka Haya Baada ya Mke wake Kutangazwa Kuwa ni Bilionea....
NUKUU ; Alichokiandika *kanyewest baada ya mkewe *KimKardashian kuwa Bilionea
"Ninajivunia kuwa mke wangu hongera kwa kuwa Bilionea rasmi, umepitia dhoruba kali na sasa Mungu anakuangaza wewe na familia yetu"
Mastaa wenye hadhi ya Ubilionea ni Jay Z *KylieJenner na *kanyewest.
Ufaransa Yaipatia Tanzania Sh, Bilioni 592.57 Kutekeleza Miradi Ya Umeme Na Maji.
Serikali ya ufaransa kupitia shirika la Maendeleo ya nchi hiyo (AFD) imeipatia Tanzania Euro milioni 230 sawa na shilingi bilioni 592.57 zikiwa ni mkopo wenye masharti nafuu kwa ajili ya kutekeleza miradi mitatu ya kipaumbele ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Akizungumza katika hafla fupi ya utiaji saini wa mkataba huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Doto James, alisema miradi iliyokusudiwa kutekelezwa kupitia fedha hizo ni Mradi wa Usambazaji wa Umeme Vijijini (REA), uliopatiwa Euro milioni 100 (sawa na shilingi bilioni 257.64) na utasambazwa katika mikoa 16 ya Tanzania Bara.
Mradi mwingine utakaonufaika na mkopo huo ni Mradi wa Umeme wa Kuunganisha Tanzania na Zambia unaojulikana kama "Tanzania – Zambia Interconnector Project" ambao utagharimu Euro milioni 100 (sawa na shilingi bilioni 257.64) kwa ajili ya kuchangia uunganishaji wa Mashirika ya Umeme ya Kusini mwa Afrika kwa pamoja yanayojulikana kama "Southern African Power Pool" na Mashirika ya Umeme ya Afrika Mashariki kwa pamoja yanayojulikana kama "Eastern African Power Pool" na Kazi za Nyongeza kwenye Mradi wa Maji Safi na Maji Taka katika miji inayozunguka Ziwa Victoria ambazo zitagharimu Euro milioni 30 (sawa na shilingi bilioni 77.29) na itahusisha maeneo ya Buhongwa, Kisesa na Buswelu katika jijini la Mwanza.
Pia Bw. James alimshukuru Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kudumisha mahusiano mazuri kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Ufaransa, uhusiano ambao umefanikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali zikiwemo sekta za maji na nishati.
Bw. James aliongeza kuwa miradi yote mitatu ambayo imesainiwa mikataba yake inawiana na Dira ya Maendeleo ya Tanzania ya mwaka 2025, ambayo inaongoza juhudi za kuleta maendeleo nchini hadi mwaka 2025 na kwa sasa inatekelezwa kupitia Awamu ya Pili ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (FYDP II) 2016/17 – 2020/21.
''Malengo ya Dira yetu ni kuinua, kuratibu na kuelekeza juhudi za Watanzania, fikra na rasilimali za Taifa kwenye sekta muhimu ambazo zitawezesha nchi kufikia maendeleo na kuhimili ushindani mkubwa wa kiuchumi unaotarajiwa''. Alisema Bw.James.
Alilishukuru Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD) kwa kuwa licha ya kuisaidia Tanzania kiasi cha Euro milioni 230 wameonyesha nia ya kutoa mikopo mingine yenye masharti nafuu na misaada ambayo inafikia jumla ya Euro milioni 721.7, sawa na shilingi trilioni 1.86 ambazo zitatumika katika kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo program ya Maendeleo ya umeme jua, ujenzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza, Uboreshaji wa Huduma za Kifedha kwa ajili ya Kilimo, Mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi Dar es Salaam (BRT Awamu ya Tano), Mradi wa Usafi wa Mazingira jijini Dar es Salaam, Mradi wa Nishati wa Kuunganisha Tanzania na Uganda na Mradi wa Nishati wa Kuunganisha Tanzania na Zambia.
Kwa upande mwingine Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo aliwashukuru wahisani hao na kusema kuwa baada ya kukamilika kwa mchako mrefu wa makubaliano kati ya Tanzania na Ufaransa na kupatikana kwa fedha hizo, Wizara yake itatekeleza mara moja miradi hiyo na kuwahakikishia wananchi kuwa miradi hiyo itakamilika kwa wakati uliopangwa.
Profesa Mkumbo aliongeza kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe.Dkt. John Pombe Joseph Magufuli imekuwa mstari wa mbele kwa kuthamini rasimali za Tanzania hivyo kuamua maji ya ziwa Victoria kutekeleza miradi mbalimbali ya maji katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Awali Mheshimiwa Frederic Clavier, Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania alisema mkopo uliosainiwa pamoja na mambo mengine una madhumuni ya kusaidia uendelelezaji wa mradi wa umeme vijijini na utatekelezwa katika Mikoa kumi na sita na kukamilika kwake kutasaidia kuwaunganishia umeme familia zipatazo 90,000.
Mwisho
Source
Saturday, June 27, 2020
Igp Sirro Aahidi Kuvifutia Vibali Baadhi Ya Makampuni Binafsi Ya Ulinzi
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, ameyataka baadhi ya Makampuni binafsi ya ulinzi kufuata masharti ya vibali walivyopewa na Jeshi hilo pamoja na kufuata maelekezo mengine yanayotolewa huku akiahidi kuvifutia vibali hivyo baadhi ya makampuni ya ulinzi yatakayoshindwa kutekeleza masharti hayo.
IGP Sirro amesema hayo leo jijini Dar es salaam, wakati akizungumza na wamiliki wa Makampuni binafsi ya ulinzi kwenye kikao kazi cha kujadili utendaji wa makampuni hayo.
Kuhusu suala la usafirishaji wa fedha, IGP Sirro, ameelekeza baadhi ya Makampuni ya ulinzi kuacha tabia ya mazoea ya kusafirisha kiasi kikubwa cha fedha na badala yake watumie Jeshi la Polisi kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa fedha hizo huku watakaoshindwa kufanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria.

Molinga Atoa Kauli ya Kutisha Yanga SC
STRAIKA mbabe wa Yanga, David Molinga 'Falcao', amesema kuwa mwishoni mwa msimu huu ataachana na klabu yake hiyo ya sasa na anatarajia kwenda kujiunga na Klabu ya Renaissance Sportive ya Morocco ila anaamini watamkumbuka.
Hadi sasa Molinga ndiye kinara wa mabao ndani ya Yanga, ambapo ameshaifungia klabu hiyo mabao 10 kwenye Ligi Kuu Bara, japo mashabiki na mabosi wa timu hiyo wameendelea kutoridhishwa na uwezo wake.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Molinga alisema tangu alipotua Yanga alikuwa akitamani sana siku moja kuondoka akiwa mfungaji bora wa ligi, lakini anaona uvumilivu umekuwa mdogo kwao hivyo kwa sasa anafikiria kwenda Morocco kujaribu bahati yake.
"Siyo kwamba mimi sina uwezo wa kuwa mfungaji bora kwenye ligi hii, ila kinachonisumbua ni suala la kuwa nje kwa muda mrefu jambo ambalo wengi hawataki kulikubali na kunipa muda, nimecheza timu nyingi kubwa ila niliumia na hiyo ndiyo sababu ya kupungua uwezo.
"Kama ningepata nafasi ya kuchezea Yanga tena msimu ujao basi naamini ningeweza kupata utimamu mzuri na hakika Yanga wangefurahia."Kwa sasa acha niondoke ila najua watakuja kunikumbuka maana ninakoenda nitapata muda mzuri wa kujiweka fiti na kufunga," alisema Molinga.Ameeleza kuwa ameshasaini mkataba wa awali wa miaka mitatu kujiunga na timu hiyo ya Morocco kwa kuwa mkataba wake na Yanga unaelekea ukingoni.
"Unajua mimi sikusafiri kipindi cha Corona kwa kuwa Yanga walitaka kuzungumza na mimi kuhusu mkataba wangu, lakini haikuwa hivyo.
"Mara kadhaa imewahi kujitokeza nikiwakumbusha viongozi kuhusu mkataba wangu lakini nikawa nazungushwa tu, hivyo sikujua hatima yangu, mwisho nikachoka, nikaamua kusaini hiyo timu ya Morocco mkataba wa awali ambapo rasmi nitajiunga nao baada ya msimu huu.
"Sheria ya Fifa (Shirikisho la Soka la Kimataifa) zimeeleza kuwa kutokana na Corona tunalazimika kumalizia msimu kwa muda uliosalia kisha ndio tutaondoka kwenda klabu nyingine kwa wale wanaohitaji kuhama.
AKATAA FEDHA ZA YANGA SC
Mara baada ya mchezo wa juzi Mcongo huyo alionyesha jeuri baada ya kukataa fedha alizokuwa akitupiwa na mashabiki wa timu yake kwa kufunga mabao mawili dhidi ya Namungo FC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika Ligi Kuu Bara.
Molinga aliingia akitokea benchi akichukua nafasi ya kiungo Mapinduzi Balama na kufunga mabao hayo ambayo yaliamsha shangwe nyingi kwa Wanayanga uwanjani hapo kwa kuwa awali walikuwa nyuma kwa mabao 2-0 hadi dakika ya 80.
Baada ya mchezo alipokaribia mlango mkubwa wa kuingilia wachezaji, alikutana na shangwe kubwa la mashabiki waliokuwa wakimsubiria kwa ajili ya kumtunza fedha ambazo alizikataa na kuingia vyumbani.
"Molinga katuthibitishia ubora wake katika mchezo huu, kiukweli amefunga mabao muhimu na kutupatia pointi moja, tunashindwa kuelewa sababu za yeye kuanzia benchi ni nini wakati ana uwezo mkubwa wa kufunga kama leo (jana) ilibakia kidogo tudharirike," walisikika mashabiki wa Yanga.
Kuhusu hicho kilichotokea, Molinga anasema: "Sikutaka fedha zao kwa kuwa nafanya hii kazi kwa mapenzi yangu, kuna muda (mashabiki) hawaeleweki, unapokuwa kwenye hali ngumu lazima wakuelewe.
"Sikutaka fedha wala mazungumzo nao ili wajifunze kuwa hata sisi wachezaji huwa tunaumia wanapotutukana tusipopata matokeo mazuri."
Thursday, June 25, 2020
Lavalava Amka, Hatukuoni Ukitusua nje ya WCB
Ada ya mja hunena, muungwana ni vitendo
Sikia hii, labda kama umezaliwa kuishi na kufa (kimziki) ndani ya WCB. Pengine unalijua hili, na huna cha kufanya kwa maana uwezo wako ndo umeishia hapo.
Madogo wanakuja, madogo wanakua na wanaondoka. Huoneshi kujitanua, ulisikika vema ulipoingia lakini sasa hali ni mbaya.
Usije kusema hujaambiwa, kama kuna wanaokusifia kuwa bado ni mkali basi ujue wanakulamba kisogo. Labda kama una 'ukali' mwingine unaokutetea na kukuongezea mbeleko
Niliwahi kuwa shabiki yako, nyimbo zako kadhaa ziliwahi kunirahisishia 'kazi' mahali fulani. Nalazimika kuendelea kukukubali kama sehemu ya fadhila, ila usipoamka utaona vumbi tu
Siku ukifurushwa hapo ndo akili zitakukaa sawa, kama ni uwezo umegota bora ukimbie kwa visingizio kama yule mwingine kabla ya fedheha ambayo hutoweza kujitetea
Ukibebwa, jishikie
Uchaguzi 2020 Nitamchagua Magufuli Tena Kwani Ametujengea Uthubutu
Ukiacha mafanikio mengi tunayoweza kuyaelezea ya Mheshimiewa Rais Magufuli nimewiwa kuelezea moja ya mafanikio makubwa ambayo yatabaki kwenye mioyo ya Watanzania.
Fanikio hilo muhimu ni ari ya kipekee aliyotujengea Mheshimiwa Rais.
yaani sisi sio wanyonge na kamwe hatutakiwi kuwa wanyonge.
Mh.Rais katika kipindi chake ametuonesha kuwa Watanzania tunao uwezo mkubwa na tunapaswa kiutumia kuijenga Tanzania.
Tunao uwezo
1-kutumia akili zetu ipasavyo
2-Tuna uwezo wa kudhibiti rushwa
3-Tuna uwezo wa ujasilia mali
4-Tuna uwezo wa kuanzisha biashara na kishindana kibiashara
5-Tuna uwezo kuanzisha biashara
6-Tuna uwezo wa kubuni na kusimamia miradi
7-Tuna uwezo wa kufanya kazi au biashara masaa 24
8-Tuna uwezo wa kuilinda nchi dhidi ya mabeberu
9-Tuna uwezo wa kukabiliana na majanga.
10-Tuna uwezo wa kujadiliana na dunia.
HEBU ENDELEA KUWEKA UWEZO WA WATANZANIA KAMA STATE...
Source
Muna Love afunguka kuhusu sebene la Yesu
Mtumishi wa Mungu Muna Love, amesema maana ya sebene la Yesu ni ujumbe wa Mungu ambao anautumia kwa njia ya kucheza nyimbo za masebene na disko, yanayoambatana na maneno ya kumsifu na kumtukuza.
Muna Love amesema atatumia kila njia ili kumtangaza Yesu kwa sababu, hata huko kuna madisko na masebene pia yupo kwa ajili ya kufikisha ujumbe kwa sababu Mungu amemtendea vitu vingi.
"Maana ya sebene la Yesu ni ujumbe wa Yesu unaoambatana na maandiko ya Mungu, nina mapatano yangu na Mungu kwamba nitamtangaza kwa kila njia ili mradi hata asiyesoma atakusikia, kwa Mungu kuna kila kitu kuna vibe, disko, masebene, kuabudu na kusifu mimi nipo kwa ajili ya kufikisha ujumbe kwa sababu amenitendea vitu vingi na hapo bado sijacheza sebene maana nitacheza sana" amesema Muna Love.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobasi Katambi Amsimamisha Kazi Afsa Mipango Miji Jiji La Dodoma Kwa Kudhurumu Ardhi Ya Mjane.
Na Faustine Gimu,Dodoma
KUU wa wilaya ya Dodoma mjini Patrobasi Katambi ametangaza kumsimamisha kazi,Hadson Magomba,ambaye yupo kitengo cha mipango miji katika jiji la Dodoma kwa kushindwa kutenda haki kwa wananchi.
Katambi ametoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko yaliyotolewa na Mdala Mazengo wakati wa mkutano wa hadhara uliohusu kupokea malalamiko juu ya kudhurumiwa ardhi katika kata ya Ipagala Jijini Dodoma huku akitoa agizo la siku saba kwa mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwini Kunambi kuunda tume huru maalum ya uchunguzi dhidi ya dhuruma ambayo amefanyiwa Mdala Anna Mazengo kwa kudhurumiwa viwanja vyake na kupewa mtu mwingine.
Katika mkutano huo Mdala Anna ambaye ni mjane toka mwaka 1985 na mwenye watoto kumi huku watoto wawili wakiwa walishafariki dunia amesema kuwa aliporwa maeneo yake katika maeneo ya swaswa extation yenye ukubwa wa ekari sita.
Mdala Anna amesema kuwa pamoja na kuwa na eneo kubwa lakini afisa kitengo cha mipango miji wa Jiji la Dodoma ambaye alimtaja kwa jina la Hadson Magomba,alimnyanyasa kwa kutompa eneo lake huku akishindwa kumpa haki yake na kubadilisha matumizi na eneo hilo kuwapatia watu wengine.
"Mimi ni mjane tangu mwaka 1985 na mwenzangu aliniachia watoto kumi japo watoto wawili wameisha tangulia mbele ya haki,watoto waliobaki ninawatunza na nilikuwa na maeneo mbalimbali hasa maeneo ya swaswa zaidi ya heka sita.
" Cha kushangaza baadaye maeneo yangu yalitwaliwa na wakati yanatwaliwa nilikuwa na vielelezo vyote na nilijaribu kufuatilia lakini niliambulia vitisho na maneno ya kejeri na matusi.
"Nilienda katika kitengo cha mipango miji ili kuweza kusikilizwa lakini matokeo yake niliambulia kurushiwa barua na kama mbwa na Hadson Magomba jambo ambalo nilishindwa kupata msaada" alisema Mdala Anna.
Aidha Mdala Anna alisema kuwa kinachomshangaza ni kuona maeneo yake ualiyotwaliwa bila fidia anaona nyumba zikijengwa jambo ambalo alidhani labda ni nyumba za walimu jambo ambalo si kweli kumbe ni nyumba za watu binafsi.
Kutokana na malalamiko hayo Katambi ametoa agizo la kumsimamisha kazi Afisa wa kitengo cha mipango miji ya Jiji la Dodoma Hadson Magomba,huku akimwagiza mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi kuunda tume uchunguzi dhidi ya ofisa Huyo ndani ya siku saba.
Katambi alisema kuwa tume hiyo inatakiwa kuundwa na watumishi kutoka ofisi ya mkuu wa Wilaya,Ofisi ya TAKUKURU,Kamati ya ulinzi na usalana pamoja na ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini.

Wananchi Watakiwa Kuiunga Mkono Serikali Kwa Kuboresha Huduma Za Matibabu Ya Kibingwa Hapa Nchini
Wananchi wametakiwa kuiunga mkono Serikali kutokana na maboresho makubwa yaliyofanywa ya upatikanaji wa huduma za kibingwa za matibabu ya moyo zinazotolewa hapa nchini.
Rai hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Godwin Mollel alipokuwa akizungumza na wagonjwa wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa ziara yake ya kikazi aliyofanya katika Taasisi hiyo ya kuangalia huduma za matibu ya moyo zinazotolewa.
Dkt. Mollel alisema miaka ya nyuma huduma nyingi za kibingwa hazikuwa zinapatikana hapa nchini na hivyo kuifanya Serikali kutumia fedha nyingi kulipia matibabu ya wagonjwa nje ya nchi lakini hivi sasa Serikali imewasomesha wataalamu wa kutosha, imejenga Hospitali za kisasa na kununua vifaa tiba vya kisasa na hivyo wagonjwa wengi kutibiwa hapa nchini.
"Hivi sasa huduma za matibabu ya kibingwa hapa nchini zimeimarika, kwa upande wa wagonjwa wa moyo wanafanyiwa matibabu ya upasuaji wa kutumia tundu dogo linalotobolewa kwenye paja na upasuaji mkubwa wa kusimamisha moyo na wataalamu wa ndani huduma ambazo hazikuwa zinapatikana hapa nchini,"alisema Dkt. Mollel.
Naibu Waziri huyo alisema kazi za kuboresha sekta ya afya zinazofanywa na Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli zimevuka hadi nje ya nchi ndiyo maana wagonjwa wanakuja kutibiwa hapa nchini wakitokea mataifa mbalimbali.
Pia kutokana na madaktari bingwa wabobezi kuwa wachache na ili huduma hii iweze kuwafikia wananchi wengi zaidi Serikali imeanzisha program ya tiba mtandao ambayo itawasaidia wagonjwa walioko mikoani kuweza kupata huduma hukohuko waliko bila ya kufuata huduma hizo Dar es Salaam.
"Kipindi hiki ambacho Dunia inakabiliwa na janga la ugonjwa Corona mipaka ya nchi nyingi ilikuwa imefungwa watu hawakuwa wanasafiri kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine, kwa kuwa Serikali ilikuwa imeboresha huduma za matibabu ya kibingwa ya magonjwa mbalimbali huduma zote hizo zilikuwa zinapatikana hapa nchini na wagonjwa walikuwa wanaendelea kutibiwa," alisema Dkt.Mollel.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi alisema changamoto kubwa wanayoipata ni wagonjwa wengi kufika katika Taasisi hiyo wakiwa wamechelewa huku mioyo yao ikiwa imechoka. Wagonjwa hao wakifanyiwa upasuaji mkubwa wa kusimamisha moyo wanatumia chupa za damu sita hadi nane lakini kama wangewahi wangeweza kutumia hadi chupa mbili za damu.
Prof. Janabi alisema Serikali imefanya uwekezaji kubwa kwa kuanzisha Taasisi hiyo kwani kabla haijaanzishwa wakati iko Kitengo cha magonjwa ya moyo ndani ya Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kipindi cha miaka saba mwaka 2008 hadi 2015 walifanya upasuaji wa moyo kwa wagonjwa 604 lakini baada ya kuanzishwa kwa mwaka 2016 hadi sasa wamefanya upasuaji kwa wagonjwa 1537.
"Tumefanya upasuaji mkubwa wa kusimamisha moyo na kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (Coronary Artery Bypass Grafting-CABG) kwa wagonjwa 100 ambapo asilimia 92 walipona na asilimia nane walipoteza maisha. Tunashukuru tumeokoa maisha ya watanzania ambao hivi sasa wanaendelea na majukumu yao ya kazi za kila siku", alisema Prof.Janabi.
Naye Mkurugenzi Msaidizi wa huduma za Umma na Binafsi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii ,Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Vivian Wonanji alisema wakati ambao nchi yetu inaelekea katika uchumi wa kati idadi ya watu wenye magonjwa yasiyo ya kuambukiza inaongezeka, hii ni kutokana na mfumo wa maisha ambao watu wanaishi .
"Mwaka jana Wizara ilizindua mpango wa kukabiliana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza ili kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya ufahamu ya magonjwa hayo. Kwa wale ambao wamepata magonjwa hayo yakiwemo magonjwa ya moyo Serikali itahakikisha wanapata huduma za matibabu na ambao hawana magonjwa hayo wanakuwa na uelewa wa kutosha ili waweze kuepuka kupata magonjwa hayo", alisema Dkt. Wonanji.
Naibu Waziri Mollel akiwa katika Taasisi hiyo alitembelea wodi ya watoto, Cathlab, chumba cha upasuaji , wodi ya wagonjwa walioko katika uangalizi maalum, alizungumza na wagonjwa aliowakuta wanapata matibabu pamoja na wafanyakazi.

Mastaa Wakike Wammezea Mate BILLIONAIRE wa MADINI, Diamond Atia Neno Kwa Kuandika Haya
Mastaa Wakike Wammezea Mate BILLIONAIRE wa MADINI aliyetangazwa leo, Baadhi ya mastaa wamepost na kujiweka karibu na bilionea huyo Laizer, Mastaa hao ni kama Diva Loveness, Batuli wa Bongo movies, Tunda , Lulu Diva na Wengine, Diamond Atia Neno Kwa Kuandika Haya
Tazama VIDEO:
Tazama VIDEO:
Dalili za mwanamke muhuni katika mahusiano ya kimapenzi
Zifuatazo ndizo dalili za mwanamke muhuni kwenye mahusiano ya kimapenzi;
1. Siyo rahisi kupenda
Dalili ya kwanza ya mwanamke kicheche mi kwamba huwa huwa mara nyingi hawataki mambo ya mahusiano na mambo ya kupendana, wanataka siku zote wawe huru hata mtu yeyote mwenye uwezo zaidi ya aliyenaye akitokea, iwe rahisi kwake kujihusisha naye. Utasikia akisema tuwe Marafiki tuu.
2. Anachukulia mahusiano kama njia ya kujinufaisha
Wanawake vicheche huwa hawaingii katika mahusiano kwa sababu wamependa, siku zote wanakuwa na agenda ya siri nyuma yake, unaweza kuita faida, kiujumla kwa kitu chochote atakachokupa katika mahusiano, ujue hapo anatarajia faida yake, utakuta anakuchangamkia na kukufanyia vitu ambavyo hukutarajia, ila lengo lake mwisho wa siku utakuta anaishia kukuomba kitu Fulani kutoka kwako. Yupo tayari kufanya chochote hata kama kinamgarimu ilimradi apate kile anachokitaka.
3. Anategeka kirahisi kwa vitu vidogo na kwa mtu yoyote
Kwa kawaida mwanamke kicheche, pale tu utapomfurahisha na kumpa zawadi, au hela kila akuombapo unamsaidia, ni rahisi sana kukubali chochote utakacho mwambia afanye, haijalishi kuwa unamalengo gani nae ya baadae au la, ilimradi tu unampa anachotaka.
Na hii hutokea kwa kila mwanaume anayemkuta ambaye anaweza kumpa kile anachotaka basi atamfanyia chochote huyo mwanaume anachotaka.
4. Anamarafiki wakiume kwa manufaa
Mwanamke kicheche huwa na Marafiki wengi wa kiume kila mmoja kwa ajili ya faida. Mwanamke kuwa na marafiki wa kiume siyo tatizo, ila tatizo linakuja pale ukute mwanamke ana marafiki wa kiume ambao kila rafiki yake huyo anajukumu lake katika maisha yake, kifaida zaidi na siyo tu rafiki wa story za hapa na pale.
Unakuta Marafiki hao wote kila mtu anahudumia na wote unaambiwa ni marafiki tu, unaweza kusikia huyu wa kulipia saloon, mwingine wa vocha n.k, basi ujue huyo ni kicheche.
5. Ni rahisi kuvunja mahusiano usipompa anachotaka
Mwanamke kicheche anakasirika haraka usipompa kile anachokitaka. Wanawake kama hawa wamezoea kupata kitu chochote watakacho kutoka kwa mwanamme, na ukibahatika kupendwa na mtu kama huyu ujue si bure, ameona kuna kitu utakachoweza kumsaidia, wengine utakuta wanapohitaji kitu wanazunguka na story nyingi ila mwisho wa siku kama mtu muelewa utajua tu anataka nini, tena hata kubembelezwa hashindwi, ila usimpe sasa anachohitaji, unaweza usiongeleshwe wiki nzima hadi pale utapokamilisha hitaji lake.
Ukishindwa kabisa kumpa anachokitaka basi anavunja uhusiano na wewe na kutafuta mtu mwingine anayeweza kumpa anachokitaka.
Tuesday, June 23, 2020
Kaptein wa Zamani wa timu ya Taifa ya vijana ajitosa kuwania nafasi ya Urais
Kaptein wa Zamani wa Timu ya vijana ya Zanzibar na Mchezaji mkongwe visiwani Zanzibar, Hashim Salum Hashim amejitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM.
Hashim Salum Hashim anakuwa mgombea 24 kufika katika ofisi kuu za chama hicho zilizopo kisiwandui mjini Unguja na kukabidhiwa fomu na katibu Katibu wa Kamati Maalumu ya NEC,Idara ya organization Zanzibar Cassian Galos Nyimbo.
Hashim Salum Hashim alivuma kisoka katika miaka ya 90 na timu aliochezea ni Timu ya mpira wa miguu ya Miembeni iliyopo katikati ya viunga vya Zanzibar, Hashim alipata umaarufu kwa kuwa mchezaji mwenye mashuti vusiwani humo.
Mara bbaada ya zoezi la uchukuaji wa Fomu, Hashim Salum Hashim aliwaambia waandishi wa Habari kwamba pindipo chama cha Mapinduzi kitampa ridhaa ya kuwa mgombea pekee wa nafasi ya Urais wa Zanzibar na Wananchi kumchagua ataanza kuboresha michezo hususani katika soka la vijana.
Alisema lengo lake ni kurudisha hadhi ya soka visiwani Zanzibar kama ilivyokuwa awali katika miaka ya 80s hadi miaka ya 90.
Hata hivyo alisema kwamba pindipo atakuwa rais wa Zanzibar, Serikali yake itatoa ufadhili wa michezo kwa asilimia kubwa ili kurudisha hadhi ya Sekta hiyo visiwani humo.
"Mimi kipaumbele kikubwa changu ni kutekeleza masuala ya michezo kutokana na kuwa mimi ni mwana michezo kama Mungu akijalia nikiwa Rais nitahakikisha michezo inapata wadhamini kwa asilimia 100 kutoka katika serikali,"alisema

Monday, June 22, 2020
Faida 8 za kuweka akiba unazopaswa kuzifahamu
Kuweka akiba ni kanuni mojawapo ya matumizi mazuri ya pesa. Hata hivyo kutokana na watu wengi kutokuwa na matumizi mazuri ya pesa, bado wengi wanashindwa kuweka akiba.
Baadhi ya watu hufikiri kuwa ili uweze kuweka akiba ni lazima uwe na pesa nyingi, lakini ukweli ni kuwa kuweka akiba ni maamuzi tu na siyo kuwa na pesa nyingi.
Ikiwa umekuwa ukipuuza suala la kuweka akiba na kuliona kuwa halina maana, basi fahamu faida 8 za kuweka akiba.
1. Uhuru wa kifedha
Uhuru wa kifedha ni zaidi ya kuwa na pesa, uhuru wa kifedha ni kuwa mtu ambaye unatakiwa kuwa maishani na kuweza kufanya au kupata kile unachokihitaji maishani.
Hata hivyo pesa ni muhimu sana kwenye swala la uhuru wa kifedha, ingawa pesa hizi zinatakiwa ziambatane na fikra sahihi.
Kwa njia ya kujiwekea akiba utaweza kujijengea msingi mzuri wa kifedha ambao ukiambatanishwa na fikra sahihi utakuletea uhuru wa kifedha.
2. Matumizi mazuri ya pesa
Kama nilivyoeleza hapo mwanzo kuwa kuweka akiba siyo kuwa na pesa nyingi bali ni maamuzi na mipango stahiki pekee.
Hivyo kuweka akiba kutakufaidisha kwa kukuwezesha kutumia pesa vyema. Ikiwa unapata elfu kumi kwa siku, itakubidi uitumie vizuri ili uweze kutenga fedha ya akiba.
Kama huweki akiba huna haja ya kutumia pesa vyema kwani hakuna sehemu ya akiba inayotakiwa kutengwa.
3. Kujiaandaa kwa dharura
Watu wengi huingia kwenye madeni au kupata uhitaji mkubwa wa pesa mara wapatwapo na dharura. Hivyo kwa kuweka akiba utapata faida ya kukuepushia mahangaiko wakati wa dharura kama vile maradhi, msiba, majanga, n.k.
4. Kuweza kufanya manunuzi au miradi ya gharama kubwa
Kuna manunuzi au miradi ambayo inahitaji pesa nyingi ili kuitekeleza. Maswala kama vile ujenzi wa nyumba, ununuzi wa kiwanja, kununua gari, n.k. ni baadhi ya mambo yanayohitaji fedha nyingi.
Hivyo, kwa kuwa na akiba utaweza kutekeleza mambo haya kwa urahisi zaidi kuliko ungeyafanya bila akiba.
5. Kuweza kumudu wanaokutegemea
Ikiwa kuna watu wanaokutegemea kama vile wazazi, ndugu au watoto; ni vyema kuweka akiba ili uweze kuwa na fedha ya kukidhi mahitaji yao mara wapatwapo na uhitaji.
Kutokuweka akiba kutakufanya uhangaike huku na huko ukitafuta fedha za kukidhi mahitaji ya wategemezi wako kama vile chakula, matibabu au hata ada za shule.
6. Utulivu wa akili
Unapokuwa huna akiba yoyote huwezi kuwa na utulivu wa akili. Kila wakati unahofu na wasiwasi juu ya maisha yako, unajiuliza likitokea tatizo itakuaje? Au hitaji fulani linalokuja hivi karibuni litakuwaje? n.k.
Unapokuwa na fungu fulani la akiba huna haja ya kuwa na wasiwasi kwani unajua hata ukikosa fedha akiba yako itakusaidia.
7. Hukuwezesha kuandaa kesho vyema
Maandalizi ya kesho yanafanywa leo. Kuweka akiba maana yake unajiandaa kwa mahitaji ya kifedha ya baadaye — yaani kesho. Mtu asiyeweka akiba mara nyingi hafikiri kuhusu kesho wala hana malengo kwa ajili ya baadaye yake.
Ili kujenga baadaye au kesho njema, ni muhimu pia kuimarisha msingi wako wa kiuchumi kwa njia ya kuweka akiba.
8. Hukuwezesha kuwahi fursa
Ni mara ngapi umekuwa ukisema au ukisikia kauli kama vile "Ningekuwa na pesa ningenunua hiki kitu", "Ningekuwa na pesa ningejiunga kwenye hii huduma", "Ningekuwa na pesa ningejiunga na huu mradi", n.k.
Hili linadhihirisha kuwa watu hukosa fursa mbalimbali kutokana na kukosa akiba ya fedha. Unapokuwa na akiba ya fedha ni rahisi kuwahi fursa mpya au bidhaa zenye manufaa mara zinapopatikana.
Hitimisho
Fedha ni jambo linalohitaji nidhamu na busara ya hali ya juu; vivyo hivyo kuweka akiba ni swala linalohitaji kufanya maamuzi sahihi ili uweze kulitekeleza.
Baada ya kusoma makala hii, naamini sasa hutopuuza tena swala la kuweka akiba. Hakikisha hutumii akiba yako pasipokuwa na sababu ya msingi; tambua itakusaidia sana mbeleni wakati wa uhitaji.

Justine Bieber akana madai ya ubakaji anayodaiwa kufanya mwaka 2014
Mwanamuziki wa kimataifa wa miondoko aina ya R&B na Pop Justine Bieber amekanusha madai ya ubakaji yaliyojitokeza kwenye mtandao wa Twitter kupitia akaunti ya mtu asiyejulikana.
Watu wawili wasiojulikana walituma ujumbe kwa njia ya Twitter wakidai kwamba unyanyasaji huo ulitokea mwaka 2014 na 2015.
Akaunti ya mshtaki ambaye hajulikani imeondolewa kwenye mtandao wa Twitter lakini Justin Bieber amejibu na kusema: "Madai haya hayana ukweli wowote."
Akaunti ya pili bado ipo kwenye mtandao huo wa Twitter. Akaunti hii mwenyewe anajulikana.
Msemaji wa Justin Bieber amezungumza na Newsbeat ya BBC na kusema kwamba hakuna anachoweza kusema kuhusu madai hayo na kwamba hana cha kuongeza katika akaunti ya mtandao wa Twitter ya mwimbaji huyo.
Justin Bieber alijibu madai hayo baada kuzungumza na mke wake na timu yake ambayo aliyakanusha vikali.
Katika msururu wa ujumbe kwenye Twitter, mwimbaji huyo alituma picha kutoka kwa simu yake na ujumbe kuanzia usiku ambao unadaiwa madai hayo yalitokea 2014, ambao unaonesha mawasiliano yake na aliyekuwa mchumba wake Selena Gomez.
Anasema kwamba wao hawakuwahi kuishi katika hoteli ya Four Seasons lakini alikuwa kwenye makazi ya kampuni ya AirBnB na marafiki zake.
Pia, ametuma picha za ujumbe unaodai kwamba alionekana hoteli ya Four Seasons Machi 10, siku moja baada ya madai ambayo yanasemekana unyanyasaji huo ulitokea. Akaunti hiyo ya Twitter inaonekana kuwa imeondolewa.
Newsbeat imezungumza na hoteli ya Four Seasons kutaka maoni yao.
Justin Bieber pia ameoesha ujumbe kwenye barua yake pepe na risiti za kampuni ya AirBnB na hoteli ya Westin alikokuwa siku ambazo zimetiwa doa.
Anasema alikuwa anatumia majina ambayo sio ya kweli ya Mike Lowery.
Justin Bieber bado hajajibu shutuma za mtu wa pili ambaye anajulikana kwa jina la Kadi, anayedai kuwa alimnyanyasa katika hoteli ya New York Mei 2015.
Newsbeat imezungumza na mwakilishi wake kutaka maoni yake kuhusiana na madai hayo ya pili.

Nabii Shillah ageukia biashara ya nguo ‘Nina mwaka sijafungua kanisa’ (Video)
Nabii Shillah wa Kanisa la BETHEL CHURCH amefunguka kuzungumzia sababu ya kufungua biashara ya nguo wakati yeye ni mtumishi wa Mungu na kuna watu anawaongoza kiroho. Mtumishi huyo amedai mpaka ana mwaka mmoja hajaenda kanisani huku akidai yeye haongozwi na kondoo wake bali anaongozwa na Mwenyezi Mungu.
VIDEO:
MWAKA WA FEDHA WA 2020/ 2021 WIZARA YA MAJI KUFANYA USANIFU WA MRADI MKUBWA WA MAJI KUTOKA ZIWA VICTORIA KWENDA DODOMA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa, Kitila Mkumbo akizungumza mkoani Singida, mwishoni mwa wiki kwenye hafla ya kupokea mabomba ya maji ambayo ni sehemu ya Programu kubwa inayotekelezwa kwa nchi nzima katika mikoa 17, Singida ikiwa ni moja ya mikoa hiyo.
Mkurugenzi wa RUWASA, Clement Kivegalo, akizungumza kwenye hafla hiyo. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa, Kitila Mkumbo.
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Singida, Mhandisi Lucas Saidi, akizungumza.
Meneja wa Kiwanda cha kutengeneza mabomba cha Pipe Industries Company Ltd, Ezra Chiwelesa, akizungumza.
Mabomba yaliyokabidhiwa.
Mabomba yakiwa kwenye gari.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa, Kitila Mkumbo akizungumza na Mkurugenzi wa RUWASA, Clement Kivegalo.
Na Mwandishi Wetu, Singida
WIZARA ya Maji inatarajia kufanya utafiti mkubwa na usanifu wa mradi mkubwa wa maji wa kuchukua maji kutoka ziwa vicktoria kupeleka Mkoani Dodoma kwa kupitia Mkoani Singida katika mwaka wa fedha wa 2020/2021.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Prof.Kitila Mkumbo alitoa kauli hiyo kwenye hafla ya kupokea mabomba ya maji ambayo ni sehemu ya Programu kubwa inayotekelezwa kwa nchi nzima katika mikoa 17,Singida ikiwa ni moja ya mikoa hiyo.
Aidha Katibu Mkuu huyo wa maji alisisitiza kwamba kwa kuwa fedha za mradi huo zimetengwa katika bajeti ya mwaka huu wa fedha,hivyo anaamini katika kipindi cha miaka mitano ijayo mikoa ya Singida na Dodoma inaweza ikapata maji kutoka ziwa Victoria.
"Na utafiti wa awali umeonyesha kwamba jambo hili linawezekana wameshaona wataalamu wetu kwamba maji yakifika pale Meatu wataweza wakayapandisha yakafika katika Kijiji cha Kisana,katika Mji mdogo wa Kiomboi."alifafanua Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya
Maji.
Hata hivyo Prof.Mkumbo aliitaja mikoa ya Dodoma,Singida,Tabora,Shinyanga,Mara pamoja na Simiyu kuwa ni mikoa ambayo kiraslimali ya maji nimikoa kame na ndiyo yenye
changamoto ya kupata mvua kidogo na hivyo kusababisha uhaba mkubwa wa maji.
"Mikoa ya Dodoma,Singida,Tabora,Shinyanga,Mara pamoja na Simiyu hii ni mikoa ambayo kirasimali za maji ni tunasema ni mikoa ambayo ni mikoa kame inachangamoto za kupata mvua kidogo kwa hivyo maji ni kidogo sana na kwa kiasi kikubwa tunategemea maji chini ya ardhi."aliweka bayana Prof Mkumbo.
Hata hivyo Prof Mkumbo alisisitiza pia kwamba kwa bahati nzuri kwa mikoa ya Tabora,Shinyanga,Simiyu pamoja na Mara wamekwishatatua changamoto zilizokuwa zikiikabili mikoa hiyo kwa kutumia raslimali kubwa ya Ziwa Viktoria.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo wa wizara maji ya ziwa viktoria wameyafikisha mpaka wilayani Igunga,Mkoani Tabora yameshakamilika na wananchi wa Igunga tayari wanapata maji kutoka ziwa Viktoria.
Mkurugenzi wa RUWASA, Clement Kivegalo aliweka wazi kwamba kupitia mabadiliko ya kisera ndani ya sekta ya maji hivi sasa wachimbaji wa visima ni sehemu ya RUWASA,ambapo ni kitengo kilicho ndani ya Mamlaka hiyo.
"Kwa hiyo tutataka tupihe kambi katika Mkoa wa Singida kuhakikisha kwamba tunatafuta vyanzo na tunatekeleza miradi kadri inavayowezekana ili wastani wa upatikanaji wa maji katika Mkoa wa Singida uweze kupanada angalau uweze kufikia kama mikoa
mingine."alifafanua Mkurugenzi huyo wa RUWASA.
Aidha Kivegalo hata hivyo aliweka bayana kuwa alitumia fursa hiyo kuwaagaiza mameneja wengine wa RUWASA wa mikoa yote kukimbizana na kasi kama meneja wa Mkoa wa Singida alivyofanya ambapo takribni miradi yote imeshafikia asilimia sabini.
Meneja wa RUWASA Mkoa wa Singida, Mhandisi Lucas Saidi alifafanua kwamba kuna miradi zaidi ya 30 inayotarajiwa kutekelezwa lakini kutokana na mabomba hayo yaliyopo wanatarajia kutekeleza jumla ya miradi tisa iliyopo katika wilaya za Mkoa wa Singida.
Mhandisi huyo wa RUWASA hata hivyo aliitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na mradi wa Wembere na Kyalosangi wilayanai Iramba,mradi wa Ibaga wilayani Mkalama,mradi wa Mughamo na Msisi wilaya ya Singida,mradid wa Dung'unyi wilayani Ikungi na mradi wa Kitaraka,Kikombo na Kashangu wilayani Manyoni.
Kwa mujibu wa Mhandisi Swedi jumla ya watu 63000 wanatarajia kunufaiaka na huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama ifikapo mwishoni mwa mwaka huu na kwamba zaidi ya miradi 40 inatarajiwa kukamilika katika kipindi hicho.
Source
Sunday, June 21, 2020
Majaliwa atangaza dawa kwa wachochezi
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali imewaagiza Makamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) nchini kuwakamata na kuwachukulia hatua watu wote watakaojihusisha na vitendo vya rushwa kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Ametoa kauli hiyo Jumamosi, Juni 20, 2020 wakati akizungumza na viongozi wa mkoa wa Lindi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Nachingwea akiwa njiani kuelekea wilayani Ruangwa kwa ziara ya kikazi.
"Watu wamezoea vitendo vya rushwa kwenye uchaguzi, Serikali tumeagiza kwa kamati za ulinzi na usalama zishirikiane kuhakikisha kwamba hakuna vitendo vya rushwa katika uchaguzi na yeyote ambaye anajihusisha na rushwa asiachwe", amesema.
Vilevile, Waziri Mkuu amewataka Makamanda wa TAKUKURU katika wilaya zote nchini wahakikishe wanawakamata watu wote watakaojihusisha na vitendo vya rushwa wakiwemo na wapambe ambao ndio wachochezi wa vitendo hivyo.
Waziri Mkuu alitoa maagizo hayo ili kuhakikisha Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu unakuwa huru na wa haki, hivyo kuwawezesha wananchi kuchagua viongozi wanaowahitaji na si kwa msukumo wa rushwa.
Katika hotuba yake aliyoisoma Juni 15, 2020 bungeni jijini Dodoma wakati akihitimisha mkutano wa 19 wa Bunge, Waziri Mkuu aliwataka viongozi wa vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi wazingatie katiba, sheria, kanuni na miongozo iliyopo katika uendeshaji wa shughuli za uchaguzi.
Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwasihi viongozi na wanachama wa vyama vyote vya siasa na wananchi kwa ujumla waendelee kulinda amani na kuendeleza mshikamano katika kipindi hiki na wakati wa Uchaguzi Mkuu.
Source
Serikali Yamchunguza Zari! Kisa Kuwatusi Watanzania
Siku kadhaa baada ya mwanamama mjasiriamali na mzazi mwenza wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz', Zarinah Hassan 'Zari The Boss Lady' kuwatusi Watanzania, hatimaye Serikali imesema inachunguza jambo hilo.
Gazeti la IJUMAA limezungumza na viongozi mbalimbali ambao baadhi yao wamesema taratibu zikifanyika, huwenda mwanamama huyo akachukuliwa hatua za kinidhamu."Samahani, mmezaa vitoto vyenye havina akili, havina confidence (havijiamini), haviwezi kuongea, yaani vimekuwa kama vindondocha…"
Hiyo ni sehemu ya maneno kwenye hotuba ya Zari ya takriban saa moja ya kuwachamba Watanzania wanaomfuatilia maisha yake.
Kauli hizo na nyingine nyingi zenye lengo la kuwatusi Watanzania, zilisababisha baadhi ya watu kuja juu kwa kudai amewatukania watoto wao.
"Sisi kama Watanzania, tunatoa malalamiko yetu kama wananchi, haijalishi tupo nchini au hatupo, hivi Serikali inaona hii dharau aliyoifanya mwanamke wa Diamond?
"Kuidhalilisha nchi yetu, kudhalilisha watoto wetu, hata kama alikuwa anatukanwa na baadhi ya watu, lakini siyo Watanzania wote waliomtukana hadi kuita watoto wetu mandondocha.
"Ina maana ni watoto wetu wote, alafu anaiita Tanzania ni shimo la umaskini, kwa nini Serikali isimpe onyo kwa kutokanyaga Tanzania mpaka atakapojirekebisha na kutuomba msamaha Watanzania wote?
"Haiwezekani aidharau nchi yetu, halafu aendelee kuja na kufanya kazi kwenye nchi aliyoiita ina watu mandondocha," aliandika @anifalahmad katika ukurasa wake wa Mtandao wa Instagram.Kufuatia malalamiko na kelele nyingi kuwa, Zari amewakosea heshima Wabongo, Gazeti la IJUMAA lilifanya jitihada za kumfikia Kaimu Meneja wa Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Semu Mwakanjala ambaye yeye kwa upande wake, alisema kuwa hana mamlaka ya kuzungumzia suala hilo.
Alisema kuwa, wapo watu husika ambao wao ndiyo wanaweza kutoa tamko juu ya hilo."Hilo alilolifanya ni kama kosa la jinai, hivyo binafsi siwezi kutoa kauli yoyote kwa sababu kuna watu ambao ndiyo wahusika wa kuweza kuzungumzia hilo, hivyo watafute na ukishawapata, na wao wakafanya uchunguzi na kubaini tatizo, basi watasema ni hatua gani ambazo watazichukua," alisema Semu.
Hata hivyo, IJUMAA halikuishia hapo, kwani liliwafikia Idara ya Polisi ya Makosa ya Mtandaoni (cyber crime) na kuzungumza na Polisi aliyejitambulisha kwa jina moja la Mwangasa ambaye naye kwa upande wake alikuwa na haya ya kusema;"Mimi naona cha kufanya labda nikushauri kwa sababu huyu Zari amewahi kuwa msanii, hivyo ungewatafuta watu wa Idara ya Habari na wao pia wana sehemu yao, wanaweza kuzungumza kwa sababu kwa suala la jinai, nikiangalia sana, inawezekana, lakini ni suala la kinidhamu ambalo hata watu wa habari wanaweza kuzungumza wanalichukuliaje hilo.
Ingawa pia mtu ambaye anaona ameongelewa vibaya, anaweza kwenda kulalamika Polisi."Kutoka hapo, IJUMAA lilimtafuta pia Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, Kamanda David Misime ambaye naye kwa upande wake alihitaji kuiona video hiyo kisha ndipo atoe tamko lake.
"Nadhani mpaka niione hiyo video kisha ndiyo nitatoa tamko langu," alisema kamanda huyo na kutumia video hiyo kwa ajili ya uchunguzi ambapo gazeti hili linafuatilia kitakachojiri.
Stori:MEMORISE RICHARD, Ijumaa
Friday, June 19, 2020
Uturuki na Italia kushirikiana kutafuta amani ya Libya
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu amesema Uturuki itafanya kazi kwa kushirikiana na Italia katika kufanikisha upatikanaji wa amani na mchakato wa kisiasa ambao utatatoa matokeo nchini Libya.
Waziri huyo pia aliongeza kusema washirika wa Umoja wa Kujihami wa NATO watashiriki pia katika jitihada hizo. Uturuki inauunga mkono serikali inayotambulika kimataifa ya mjini Tripoli.
Kwa jitihada za serikali ya Uturuki serikali hiyo ilifanikiwa kuyarudisha nyuma mashambulizi ya miezi 14 yakilenga mji wa Tripoli ya mbambe wa kivita Khalifa Haftar, ambayo yanaungwa mkono na Urusi, Jumuiya ya Falme za Kiarabu na Misri.
Akizungumza na waandishi wa habari, sambamba na mgeni wake waziri wa mambo ya nje wa Italia, Cavusoglu amesema mataifa hayo mawili pia yatashughulikia mahitaji ya nishati kama umeme nchini Libya.

MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA AMSWEKA NDANI MKANDARASI ERASTO KWILASA NA MKEWE
Bw. Erasto Kwilasa
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko amemsweka rumande Mkandarasi anayejenga barabara mbalimbali katika Manispaa ya Shinyanga, Erasto Kwilasa pamoja na mke wake kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kutomaliza kazi ya ujenzi wa barabara kwa wakati.
Inaelezwa kuwa Mkandarasi huyo ameshindwa kumaliza kazi ya ujenzi wa barabara mbalimbali zikiwemo za Ugweto na Kitangiri katika manispaa ya Shinyanga.
Mwandishi wetu wa habari amezungumza na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko ambaye amekiri kumuweka ndani Mkandarasi huyo.
"Siku ya Jumanne nilikagua barabara za Manispaa ya Shinyanga,Jumatano nikakagua barabara za Shinyanga vijijini. Tuliyokubaliana Jumanne kuwa hadi kufikia leo Ijumaa yawe yametekelezeka yeye hajatekeleza,hajafanya ndiyo maana leo nimeamua kumuweka ndani",amesema Mboneko.
"Barabara zote anazotengeneza hajamaliza ndiyo maana nimemuweka ndani yeye na mke wake ambaye naye ni Mkandarasi. Kule Kitangiri anatengeneza barabara hamalizi huko Ugweto kunakolalamikiwa nako hamalizi kujenga barabara",amesema Mboneko.
Source
Jafo awajia juu Kilosa kwa kuuza eneo la Kijiji cha Magole
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kusimamisha mchakato wa uuzwaji wa eneo la Kijiji cha Magole katika halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Ili kubaini uhalali wa uuzwaji wake.
Zoezi hilo ameagiza lifanyike kwa kushirikisha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Mhe. Jafo alitoa agizo hilo wilayani Bahi wakati akizindua Shule ya sekondari ya Kata ya Nondwa iliyojengwa na halmashauri hiyo kwa kutumia mapato yake ya ndani ambalo alisema eneo hilo lina ukubwa wa hekari 200 na linauzwa kwa raia wa kigeni.
Alisema haiwezekani mchakato ufanyike bila ya kushirikisha wananchi wa Kijiji husika na kutaka uchunguzi huo uangalie uhalali wa muuzaji na mnunuaji pia kujua dhamira waliyokuwa nayo.
"Timu hiyo iangalie kulikuwa na uhalali gani wa kuuza mali hiyo,na mnunuaji pia aangaliwe Kama hakuna harufu ya rushwa,haiwezekani eneo hilo liuzwe bila ya wananchi kujua tena kwa raia wa kigeni,huyu aliyependekeza kuuzwa alishawishiwa na nini, na tangu lini mgeni akamiliki ardhi nchi,?" alihoji Jafo.
Alisema Baraza la madiwani katika kikao Chao Cha mwisho lilipitisha uamuzi wa kuuzwa eneo la Kijiji lenye hekari 200 bila ya kuwashirikisha wananchi pamoja na kwamba mkuu wa Mkoa aliwaandikia barua ya Kuzuia wasifanye hivyo.
"Huu ni udhaifu wa hali ya juu wa madiwani ambao katika kikao Chao Cha mwisho Cha kuvunjwa Baraza lao ndio waliidhinisha hili,"
Jafo alisema Hilo eneo ambalo limeuzwa kwa mchina kulikuwa linatumika na wachina kutekeleza miradi ya miundombinu majengo ambayo wangeweza kuyabadili kuwa kituo Cha afya au zahanati.
"Yaani sijui waliuza Ili wapate hela za kuwalipa madiwani viinua mgongo vyao na madeni mengine,hii ni tabia mbaya,nimechukizwa Sana,"alisisitiza Jafo.
Aliipongeza halmashauri ya Bahi kwa kuwalipa madiwani viinua mgongo vyao vyao na kutumia asilimia 40 ya mapato yao ya ndani katika miradi ya maendeleo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Dk Fatma Mganga alisema mashine za ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kielektroniki(Pos)zimewasaidia kupongeza ukusanyaji wa mapato ambapo hadi kufikia mwezi Mei mwaka huu walifikisha asilimia 86 ya ukusanyaji.
"Wewe mwenyewe mheshimiwa Waziri umetuelekeza tuhakikishe mapato tunayokusanya kiasi kirudi kwa wananchi na tumefanya hivyo,na mashine ya Pos ndio zimekuwa msaada mkubwa kwetu,hapa madiwani wetu wamestaafu wakiwa hawana mawazo,pesa zao zote tumeweza kuwalipa,"alisema Mkurugenzi huyo.

Wafanyakazi wa machinjio 730 wapata corona, kiwanda cha nyama chafungwa
Hadi kufikia jana, wafanyakazi wapatao 730 katika machinjio ya jimbo la North Rhine-Westphalia (NRW) nchini Ujerumani wamethibitika kuambukizwa Corona Virus baada ya kupimwa
Mamlaka za Jimbo zimeamuru kufungwa kwa kiwanda cha kuchakata nyama cha Kundi la Toennies kwenye eneo la Guetersloh jimboni humo
Aidha, watu wapatao 7,000 wamewekwa karantini kwenye eneo la Guetersloh. Jimbo la NRW limeanzisha uchunguzi kujua chanzo cha maambukizi hayo
Spika Ndugai: Tulifika mahali ambapo live camera ikaliharibu Bunge
"Tulifika mahali ambapo live camera ikaliharibu Bunge, Watu wakawa wanatukana, wanakuwa na tabia mbaya, unakuta mmekubaliana kabisa kwenye kamati kila kitu, jambo lile lile likiingia Bungeni inakuwa kama mchezo wa kuigiza" - SPIKA NDUGAI
"Live Camera' iliharibu Bunge, watu wakawa wanatukana,kitu hakiingii Bungeni kinapitia kwenye kamati mbalimbali kimechujwa, mnakubaliana likiingia Bungeni tu wanabadilika sio yule, wanafanya maigizo, kamera isipokuwepo anafikiri sawasawa, ikiwepo camera anabadilika"-NDUGAI
"Hata kwa Mabunge ya Nchi zilizoendelea kama Uingezereza si kweli kwamba ni Live kihivyo, wanaicheleweshea kama dakika mbili au tatu kati ya kinachotokea Live na kinachokuwa Live wanajaribu ku-edit kidogo vitu ambavyo ni aibu kwa Taifa"-SPIKA NDUGAI
Mwanamke wa Kwanza Ajitosa Kugombea Urais Zanzibar Kupitia CCM
Mwantum Mussa Sultan amechukua fomu ya kugombea Urais Zanzibar na anakuwa Mwanamke wa kwanza kujitosa kwenye kinyang'anyiro cha Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Mwantuma amechukua fomu Leo Ijumaa tarehe 19 Juni 2020 katika Ofisi za CCM visiwani Zanzibar zilizoko Kisiwandui na kukabidhiwa Cassian Gallo's, katibu wa Kamati Maalumu ya NEC Idara ya Oganaizesheni Zanzibar.
Mara baada ya kukabidhiwa, Mwantumu amesema, amefanya hivyo ili kutoa hamasa kwa wanawake kujitosa katika kinyang'anyiro hicho, kutimiza sera ya haki sawa kwa wote.
Mwantumu anakuwa kada wa 11 wa CCM kujitosa katika kinyang'anyiro hicho, tangu zoezi hilo la siku 15 lifunguliwe Jumatatu ya tarehe 15 Juni 2020.
JOGOO ALIYEFIKISHWA MAHAKAMANI KUWAPIGIA KELELE WANA NDOA AAGA DUNIA
Jogoo Maurice, ambaye alishtakiwa kwa sababu ya kuwika kila asubuhi, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 6.
Jogoo huyo alishtakiwa kwa kupiga kelele na wanandoa waliostaafu ambao walikuwa wakati wakiwa likizoni nchini Ufaransa kisiwa cha Oléron.
Mmiliki wa jogoo hilo, Corinne Fesseau, alisema kile alichokuwa anafanya jogoo wake ni kuwika tu kawaida kama jogoo wengine.
Maurice pamoja na waliomshtaki, hakuna aliyekuwepo mahakamani ana kwa ana wakati kesi hiyo inasikilizwa.
Lakini ogoo maurice alipata umaarufu wa kimataifa na kuwa nembo ya kampeni ya kulinda sauti kote nchini Ufaransa - baada kujipata katika mgogoro wa kisheria juu ya kupiga kelele.
Aliyeshtaki alilalamika kwamba Bi. Fesseau, mmiliki wa jogoo, alianzisha kubisha baada ya kupewa taarifa na kusababisha mgogoro.
Bi. Fesseau, na wafuasi wake kwenye jamii hiyo, walisema kwamba jogoo ni sehemu ya maisha ya watu wa vijijini na haina maana kusema kwamba jogoo huyo anyamazishwe.
Now ikiwa kuna kile ambacho kingehitajika kufanywa kwa Maurice basi mahakama ilihitajika kuingilia kati na kutoa uamuzi wake Septemba.Corinne Fesseau akiwa na jogoo wake
Mwaka 2019, uamuzi wa mahakama ulimpendelea jogoo Maurice na kuishi katika siku zake zote zilizokuwa zimesalia katika kisiwa cha Oléron.
Jogoo huyo alikufa Mei lakini mmiliki wake akasubiri muda mwafaka wa kutangaza kifo chake.
"Nilijiambia kwamba kwasababu ya hatua za kutotoka nje, watu tayari wana mengi ya kukabiliana nayo," Corinne Fesseau alinukuliwa akisema hivyo katika kituo kimoja cha redio cha Ufaransa.
"Tumenunua jogoo mpya na huyo pia tumemuita Maurice - pia nae anawika kama yule wa kwanza tu. Lakini hawezi kuwa Maurice wetu."
Bi. Fesseau alijaribu kumnyamazisha Maurice - ikiwemo kumfunika kwa shuka
Matatizo ya Maurice yalianza pale wanandoa waliostaafu waliokuwa likizo katika nyumba moja ya kuko huko Oléron walipomshtaki kwa kuwasumbua wakati anawika.
Baada ya hapo jogoo huyo alikuwa maarufu nchini Ufaransa kiasi cha kuwa miongoni mwa nembo za kitaifa na malefu ya watu walitia saini ombi la kutaka kumnusuru.
Walalmishi, Jean-Louis Biron na Joëlle Andrieux, walijenga nyumba yao ya kupumzika ambayo ni kama eneo lao la kitalii wakati walikizo katika kijiji cha Saint-Pierre-d'Oléron karibia miaka 15iliyopita.
Walisema kwamba moja ya sabab iliyochangia wao kujenga nyumba hiyo kwenye kijiji hicho, ni utulivu wa eneo. Lakinimambo yalianza kubadilika pale jogoo Maurice alipoanza kuwika kila mara tena kwa sauti ya juu mno 2017.Maurice hatanyamazishwa baada ya mahakama kumuunga mkono
Septemba mwaka jana, jaji alitoa umauzi unaompendelea jogoo maurice na kuagiza aliyeshtaki kulipa pauni 1,000 sawa na (£900; $1,100) kama fidia.
"Ushindi huu ni kila mmoja aliyekatika hali kama hii. Ni matumaini yangu mimi nitaweza kutumika kama mfano," Bi Fesseau amenukuliwa na shirika la habari la AFP akisema hivyo wakati huo.
Chanzo - BBC Swahili
Subscribe to:
Posts (Atom)
-
Baadhi ya raia walioyatoroka makaazi yao baada ya mlipuko wa volkano uliotokea usiku wa kuamkia huko mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kid...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na...
-
Zaidi ya ghorofa 100 jijini Dar es Salaam zilibainika kujengwa kinyume cha taratibu za ujenzi, Bunge lilielezwa. Kwa mujibu wa ripoti iliy...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania November 23, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za ny...
-
Mhamasishaji maarufu wa mitandaoni, Mwijaku, ameandika ujumbe unaotoa ushauri kwa Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Said Hersi, kupitia ukuras...
-
Hii hapa ngoma mpya ya Msanii wa Nyimbo za asili Mama Ushauri ameshirikiana na Ng'wana Ng'washi inaitwa Merimela ,imetengenezwa Lw...
-
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam, imetupilia mbali shauri lililokuwa limefunguliwa na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam October 9, 2024,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na ...
-
Msanii maarufu Ntemi O Mabala ' Ng'wana Kang'wa kutoka Kahama Mkoani Shinyanga anakualika kusikiliza wimbo wake mpya unaitwa M...