Friday, June 19, 2020

Uturuki na Italia kushirikiana kutafuta amani ya Libya

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu amesema Uturuki itafanya kazi kwa kushirikiana na Italia katika kufanikisha upatikanaji wa amani na mchakato wa kisiasa ambao utatatoa matokeo nchini Libya.

Waziri huyo pia aliongeza kusema washirika wa Umoja wa Kujihami wa NATO watashiriki pia katika jitihada hizo. Uturuki inauunga mkono serikali inayotambulika kimataifa ya mjini Tripoli.

 Kwa jitihada za serikali ya Uturuki serikali hiyo ilifanikiwa kuyarudisha nyuma mashambulizi ya miezi 14 yakilenga mji wa Tripoli ya mbambe wa kivita Khalifa Haftar, ambayo yanaungwa mkono na Urusi, Jumuiya ya Falme za Kiarabu na Misri.

Akizungumza na waandishi wa habari, sambamba na mgeni wake waziri wa mambo ya nje wa Italia, Cavusoglu amesema mataifa hayo mawili pia yatashughulikia mahitaji ya nishati kama umeme nchini Libya.

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...