Tuesday, June 23, 2020

Kaptein wa Zamani wa timu ya Taifa ya vijana ajitosa kuwania nafasi ya Urais

Kaptein wa Zamani wa Timu ya vijana ya Zanzibar na Mchezaji mkongwe visiwani Zanzibar, Hashim Salum Hashim  amejitokeza kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM.

Hashim Salum Hashim anakuwa mgombea 24 kufika katika ofisi kuu za chama hicho zilizopo kisiwandui mjini Unguja na kukabidhiwa fomu na katibu Katibu wa Kamati Maalumu  ya NEC,Idara ya organization Zanzibar Cassian Galos Nyimbo.

Hashim Salum Hashim alivuma kisoka katika miaka ya 90 na timu aliochezea ni Timu ya mpira wa miguu ya Miembeni iliyopo katikati ya viunga vya Zanzibar, Hashim alipata umaarufu kwa kuwa mchezaji mwenye mashuti vusiwani humo.

Mara bbaada ya zoezi la uchukuaji wa Fomu, Hashim Salum Hashim aliwaambia waandishi wa Habari kwamba pindipo chama cha Mapinduzi kitampa ridhaa ya kuwa mgombea pekee wa nafasi ya Urais wa Zanzibar na Wananchi kumchagua ataanza kuboresha michezo hususani katika soka la vijana.

Alisema lengo lake ni kurudisha hadhi ya soka visiwani Zanzibar kama ilivyokuwa awali katika miaka ya 80s hadi miaka ya 90.

Hata hivyo alisema kwamba pindipo atakuwa rais wa Zanzibar, Serikali yake itatoa ufadhili wa michezo kwa asilimia kubwa ili kurudisha hadhi ya  Sekta hiyo  visiwani humo.

"Mimi kipaumbele kikubwa changu ni kutekeleza masuala ya michezo kutokana na kuwa mimi ni mwana michezo kama Mungu akijalia nikiwa Rais nitahakikisha michezo inapata wadhamini kwa asilimia 100 kutoka katika serikali,"alisema
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...