Thursday, April 30, 2020

Watu milioni 30 wanaomba mafao ya kupoteza kazi Marekani

Zaidi ya wafanyakazi milioni 3.8 walioondolewa kazini wameomba mafao ya kutokuwa na kazi wiki iliyopita wakati uchumi wa Marekani ukiporomoka zaidi katika mzozo ambao umekuwa wenye athari kubwa zaidi tangu miaka ya 1930.

Takriban watu milioni 30.3 wamejiandikisha kupata msaada wa kutokuwa na kazi katika wiki sita tangu kuzuka kwa virusi vya corona na kulazimisha mamilioni ya waajiri kufunga milango yao na kupunguza wafanyakazi.

Hawa ni watu wengi zaidi kuliko wanaoishi mjini New York na Chicago kwa jumla, na kwa kiwango kikubwa ni wimbi baya zaidi la watu kuachishwa kazi kuliko wakati mwingine.

Wakati waajiri wengi wanapunguza matumizi kwa kuwaachisha kazi wafanyakazi , wataalamu wa uchumi wanatabiri kwamba kiwango cha ukosefu wa ajira kwa Aprili kinaweza kwenda juu zaidi hadi asilimia 20.

Mgumba: Serikali haitopanga bei za mazao ya wakulima

Serikali imesisitiza kuwa haitopanga wala kuingilia bei za mazao ya wakulima nchini badala yake wakulima watajipangia bei na kuuza wenyewe ilihali serikali ikisalia kama msimamizi.

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 30 Aprili 2020 wakati akizungumza na viongozi wa TADCOs Co ltd kuhusu hatua iliyofikiwa ya uagizaji wa mbolea katika ukumbi wa KILIMO IV Jijini Dodoma.

Mhe Mgumba amesema kuwa mfumo wa biashara ulivyo unategemea zaidi ujazo wa mazao sokoni, hivyo bei haitolewi kutokana na gharama alizotumia mkulima wakati wa uzalishaji badala yake bei inaendana na soko.

Amesema kuwa wakulima kama wanavyoruhusiwa kuzalisha kadhalika wakulima hao watauza mazao yao popote watakapotaka wao lakini kwa kufuata taratibu na sheria za nchi.

Kuhusu Mfumo wa stakabadhi ghalani Naibu Waziri Mhe Mgumba amesema kuwa mfumo huo ulianzishwa kwa lengo la kumrahisishia huduma za biashara mkulima hivyo utaendelea kutumika kwa mujibu wa matakwa ya kuanzishwa kwake.

Amesema kuwa zipo changamoto nyingi katika utekelezaji wa mfumo huo unaochagizwa na viongozi wanaosimamia hususani wa vyama vya Ushirika kutotekeleza kwa mujibu wa sheria.

"Mtu akipeleka mazao yake ghalani lengo la serikali kwa sababu mazao yote tunategemea msimu wa mvua na upatikanaji wake ni wa wakati mmoja hivyo kuhifadhi kwa pamoja na kupewa stakabadhi itakayomrahisishia kupata mkopo kwa ajili ya kukidhi mahitaji yake wakati akisubiri gharama za mazao zikipanda aweze kuuza kwa bei nzuri" Alikaririwa Mhe Mgumba

Mhe Mgumba ameongeza kuwa mfumo huo ni mzuri endapo utaendelea kusimamiwa vizuri ikiwa ni pamoja na kuendelea kuuboresha zaidi ili uwanufaishe wakulima kote nchini kwani mfumo huo unapunguza gharama za uendeshaji.

Ameeleza kuwa miongoni mwa changamoto waliyokuwa nayo wakulima ilikuwa ni Tija ndogo katika mavuno yao yaliyosababishwa na matumizi madogo ya mbolea hivyo serikali ilitoa elimu ya kutosha kwa wakulima kuhusu matumizi sahihi ya mbolea hivyo katika kipindi cha serikali ya awamu ya tano tija imeongezeka.

Mgumba amesema kuwa matumizi sahihi ya mbolea yameongeza tija katika sekta ya kilimo kwani uzalishaji umeongezeka na wakulima wamekuwa na kipato kikubwa.

Katika kikao kazi hicho Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba amesema kuwa nchi ina mbolea ya kutosha ambapo ina akiba ya zaidi ya Tani 203,000 iliyotokana na uagizaji wa mbolea uliofanywa kwa mwaka mzima wa kiasi cha mbolea Tani 633,197

Tabia za Mama Mkwe Ndio Tabia za Mkeo..Chukua hiyo Kubali Au Kataaa


Kwa utafiti wangu mdogo niliofanya nimegundua kwamba tabia za mama mkwe ndio tabia za mkeo upende usipende.kwahiyo kama una mpango wa kuoa usiishie kumchunguza mchumba wa kike ambaye wakati wa uchumba anakuwa anaishi maisha ya kuigiza bali pia angaika kumchunguza mama mkwe.

Kwanini mama mkwe?

1. Mama mkwe ndie aliyemlea mkeo mtarajiwa kwahiyo mchumba wako atakuwa ameiga na kufundishwa kuwa na tabia kama mama yake

2.Mara mwanamke anapoolewa Mshauri mkuu ni mama yake mzazi(napenda uamini hili) kwahiyo maisha yake kwenye ndoa yatategemea ushauri wa mamaye

3.ikitokea mfarakano kwenye ndoa na kama mwanamke ndio tatizo mama mkwe ndie mtu pekee anayeweza kumbadilisha mkeo katika njia sahihi.

MAKONDA ATOA MSAADA WA MABATI YA MILIONI 476 KWA AJILI YA KUEZEKA NYUMBA 1,000 ZA WAJANE WALIOKUMBWA NA MAFURIKO DAR


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo April 30, 2020 ametoa msaada wa mabati yenye thamani ya Tsh. 476m kwa ajili ya Kuezeka nyumba 1,000 za Wajane wa mkoa huo ambazo zimeathiriwa na mafuriko. RC Makonda amewataka pia wananchi waliojenga mabondeni kuhama.



RC Makonda amesema hayo wakati wa Ziara ya Kukagua athari za Mvua  na kubaini uwepo wa familia za Wajane ambao Nyumba zao zimechukuliwa na Mafuriko na sasa wanapitia changamoto ya kuhifadhiwa kwa majirani baada ya kukosa makazi ya kuishi hivyo ameona ni busara kutoa msaada huo kama sehemu ya pole kwa adha waliyoipata.

Aidha RC Makonda amewapa siku 10 Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanapitia maeneo ya Mito na Mabonde kukagua athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwashirikisha viongozi wa mitaa ili kwa pamoja watoe mapendekezo ya nini kifanyike kisha wampatie ripoti ya kuonyesha hatua za kukabiliana na Mafuriko ya Mara kwa Mara.

Aidha RC Makonda amesema athari zinazoonekana kwa sasa ni matokeo ya Jamii kuwafumbia macho watu wanovunja sheria kwa kujenga mabondeni, kuchimba mchanga na kuziba mikondo ya maji jambo linalopelekea Mafuriko hivyo ametaka kila mwananchi kuwa mlinzi wa mwenzake.

Pamoja na hayo RC Makonda amesema kwa sasa serikali inaendelea kurejesha miundombinu na madaraja yaliyochukuliwa na Mafuriko ikiwemo ujenzi wa madaraja ya muda mfupi ili kuwezesha shughuli za kijamii kuendelea.


Jumuiya ya Mawakili Zanzibar yatuma rambirambi kufuatia kifo cha Jaji Mstaafu Augustine Ramadhani


Jumuiya ya Mawakili Zanzibar (ZLS) imepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa za vifo vya Majaji Wakuu Wastaafu wawili wa Zanzibar ambao ni Mh.Augustine Lawrence Ramadhan na Mh.Ali Haji Pandu pamoja na kadhi Mkuu Mstaafu wa Zanzibar Shk.Habib Ali Kombo amabao wote kwa pamoja wamefariki ndani ya wiki moja katika mwezi wa April,2020.

Marehemu wote watatu walitoa mchango mkubwa katika kuujenga na kuuimarisha Mhimili wa Mahkama ambao ndio wenye dhamana ya utoaji haki katika nchi yetu.

Aidha waliitumikia Zanzibar kwa bidii na uadilifu mkubwa ambao unaonekana  kwenye hukumu zao mbalimbali na jitihada zao za kusomesha vijana elimu ya sharia na sheria.

Marehemu watakumbukwa kwa kujituma kwao na kusimamia sheria katika utekelezaji wa utoaji haki katika nyakati na mazingira tofauti.

Kufuatia msiba huu Jumuiya ya Mawakili Zanzibar(ZLS) inaomba ikupendeze kupokea rambirambi zake kwako ukiwa Mkuu wa Mhimili wa Mahkama ambao marehemu wote waliufanyia kazi kwa juhudi, busara na maarifa makubwa.

Aidha, Jumuiya inaungana na wanafamilia na Taifa kwa ujumla katika kuomboleza misiba hii pamoja na kuwaombea wanafamilia kuwa na busra katika kipindi hiki kigumu.

Niyonzima Atupa Kombora Simba



KIUNGO mchezeshaji mkongwe fundi, Haruna Niyonzima, amesema kuwa kwa sasa ni bora akastaafi a maisha yake ya soka Yanga na siyo kurudi tena Simba.

 

Niyonzima alirejea kuichezea Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo msimu huu akitokea AS Kigali ya nyumbani kwao Rwanda.

 

Kumbuka kabla ya hapo alikuwa Simba aliyoitumikia kwa misimu miwili.Kiungo huyo kutua kwake Yanga kumeimarisha safu ya kiungo ya timu hiyo na kurudisha matumaini ya kufanya vema.


Mwandishi wa Spoti Xtra, Wilbert Molandi akiongea na Niyonzima.

Akizungumza na Spoti Xtra, Niyonzima alisema kuwa amezichezea klabu zote mbili kubwa na kongwe hapa nchini, lakini kwake alifurahia na anaendelea kufurahia maisha yake akiwa Yanga.

 

Niyonzima alisema ataendelea kuipambania timu hiyo kwa kipindi chote atakachokuwepo Yanga na kati ya vitu ambavyo amevipanga ni kuhakikisha anarejesha heshima ya timu hiyo ikiwemo kutwaa mataji mbalimbali ikiwemo ligi kuu.

 

Aliongeza kuwa kikubwa viongozi wa timu hiyo chini ya wadhamini wao, Kampuni ya GSM kuhakikisha wanafanyia kazi ripoti ya usajili katika kuelekea msimu ujao kwa lengo la kutengeneza kikosi imara kitakacholeta ushindani.

 

"Kwa sasa nisingependa kuizungumzia timu ambayo nimetoka kuichezea kwani nipo kwenye timu yangu ya zamani ya Yanga niliyowahi kuichezea kwa furaha na amani kubwa.

 

"Kiukweli nilikuwa na furaha kubwa nikiwa Yanga kabla ya kwenda Simba, hivyo kwa sasa sifi kirii kabisa mimi kurudi tena huko, akili na nguvu zangu nimepanga kuzitumia nikiwa hapa, nafahamu mashabiki wana hamu kubwa ya ubingwa baada ya kuukosa kwa misimu miwili mfululizo.

 

"Hivyo mashabiki wa Yanga waondoe hofu, mengi nimepanga kuyafanya nikiwa hapa, ninaamini bado wana furaha ya kuwafunga Simba bao 1-0 huku tukipata sare ya mabao 2-2," alisema Niyonzima.

Stori na WILBERT MOLANDI, Dar


Source

Makonda Atoa Msaada Wa Mabati Yenye Thamani Ya Shilingi Milioni 476 Kwaajili Ya Kuezeka Nyumba 1,000 Za Wajane Waliokumbwa Na Mafuriko Dar

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo April 30, 2020 ametoa msaada wa mabati yenye thamani ya Tsh. 476m kwa ajili ya Kuezeka nyumba 1,000 za Wajane wa mkoa huo ambazo zimeathiriwa na mafuriko. RC Makonda amewataka pia wananchi waliojenga mabondeni kuhama.

RC Makonda amesema hayo wakati wa Ziara ya Kukagua athari za Mvua  na kubaini uwepo wa familia za Wajane ambao Nyumba zao zimechukuliwa na Mafuriko na sasa wanapitia changamoto ya kuhifadhiwa kwa majirani baada ya kukosa makazi ya kuishi hivyo ameona ni busara kutoa msaada huo kama sehemu ya pole kwa adha waliyoipata.

Aidha RC Makonda amewapa siku 10 Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanapitia maeneo ya Mito na Mabonde kukagua athari za mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwashirikisha viongozi wa mitaa ili kwa pamoja watoe mapendekezo ya nini kifanyike kisha wampatie ripoti ya kuonyesha hatua za kukabiliana na Mafuriko ya Mara kwa Mara.

Aidha RC Makonda amesema athari zinazoonekana kwa sasa ni matokeo ya Jamii kuwafumbia macho watu wanovunja sheria kwa kujenga mabondeni, kuchimba mchanga na kuziba mikondo ya maji jambo linalopelekea Mafuriko hivyo ametaka kila mwananchi kuwa mlinzi wa mwenzake.

Pamoja na hayo RC Makonda amesema kwa sasa serikali inaendelea kurejesha miundombinu na madaraja yaliyochukuliwa na Mafuriko ikiwemo ujenzi wa madaraja ya muda mfupi ili kuwezesha shughuli za kijamii kuendelea.


VIDEO: RC Makonda atoa msaada wa mabati kwa walioathirika na mafuriko Dar es salaam


TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI...USISAHAU KU SUBSCRIBE

Tangazo La Nafasi Za Kazi Katika Shirika La IFAD




VIDEO: Mkuu wa Mkoa wa Arusha asimulia alivyopata corona


TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI...USISAHAU KU SUBSCRIBE

Video:Nandy ‘Nimepima Ukimwi Mwaka Jana, Nafuatisha Uzazi wa Mpango’



NI Msanii kutokea Bongo Flevani, Nandy ambae time hii amefunguka mbele ya waandishi wa habari kuhusu kupima (VVU) Ukimwi na kueleza Uzazi wa mpango, itazame hii video hapa

VIDEO:

Jonijoo Amkimbia Diamond Wasafi, Atua Katika Redio Hii na Kukaribishwa kwa Staili ya Aina yake – Video


Aliyekuwa Mtangazaji wa Wasafi media @jonijooo ameondoka katika kituo hicho na kukaribishwa #EFM na mkurugenzi wa kituo hicho @majizzo

Ujumbe wa Majizo ukiambatana na Video umesomeka hivi:-

"@jonijooo : Unasema mitaa imekulea, Naomba Nikukaribishe kwetu Waswahili Tuliotumwa na mtaa. Natambua uwezo wako, njoo Tulisongeshe.

Mimi #CEO wa Waswahili nikupe tu taarifa kwamba Hatuna Shughuli ndogo. Kuanzia leo @efmtanzania na @tvetanzania ndio familia yako. Karibu sana."


Wednesday, April 29, 2020

Bibi mwenye miaka 95 apona corona

Kiungo wa zamani wa Arsenal na Chelsea anayecheza AS Monaco ya Ufaransa kwa sasa Cesc Fabregas amethibitisha kuwa mama wa bibi yake amepona corona akiwa na umri wa miaka 95.

MAJAMBAZI WAVAMIA KANISA KATOLIKI PAROKIA YA MODEKO MOROGORO..KANISA LAFUNGWA KWA KUFURU


Na Angela Kibwana, Morogoro Na P. Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.
Mheshimiwa Padre Lazarus Vitalis Msimbe, S.D.S., Msimamizi wa Kitume wa Jimbo Katoliki la Morogoro nchini Tanzania amefunga Kanisa la Parokia ya Bikira Maria Mtakatifu baada ya kuwasiliana na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na Ubalozi wa Vatican nchini Tanzania.

Kuanzia tarehe 27 Aprili 2020 Kanisa la Parokia ya Modeko limefungwa na halitaweza kutumika kwa sasa hadi pale, Tabernakulo mpya itakapowekwa wakfu.

 Ibada hii inatarajiwa kuadhimishwa wakati wa Sherehe ya Ekaristi Takatifu, fursa makini kwa waamini kutangaza na kushuhudia imani ya Kanisa kuhusu Fumbo la Ekaristi Takatifu, yaani uwamo wa Kristo katika maumbo ya Mkate na Divai. 

Mababa wa Kanisa wanathibitisha kwamba, kwa nguvu ya imani ya Kanisa na uwezo wa Neno la Kristo Yesu, na tendo la Roho Mtakatifu, kwamba, mageuzo ya Mkate na Divai yanakuwa ni Mwili na Damu Azizi ya Kristo.

Padre Nikodemas Masong, Paroko wa Parokia ya Modeko, Jimbo Katoliki la Morogoro amesema, watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi tarehe 27 Aprili 2020 walivamia na kuvunja mlango wa Kanisa la Parokia ya Modeko na kufanikiwa kuiba Tabernakulo iliyokuwa inahifadhi Ekaristi Takatifu na kutokomea mahali kusikojulikana. 

Walivunja pia milango ya ofisi za Parokia na kufanikiwa kuiba kiasi cha shilingi laki tatu na nusu, mali ya Chama cha Watumishi wa Altare Parokiani hapo. Walifanikiwa pia kuiba "Mixer" inayotumika kwa ajili ya mawasiliano Parokiani hapo.

 Familia ya watu wa Mungu ndani na nje ya Jimbo Katoliki la Morogoro imesikitishwa sana na kufuru hizi dhidi ya mahali na mambo matakatifu yanayogusa undani wa imani ya watu.


Via Vatican News

Waziri Jafo atoa maelekezo kuhusu mpango wa Ufundishaji Wanafunzi Kielektroniki

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Selemani Jafo amelitaka Baraza la Mitihani Tanzania(NECTA) na Taasisi ya Elimu Tanzania(TET), kuhakikisha utaratibu wa kufanya marejeo ya mitihani ulioanza kwa kidato cha sita uhusishe madarasa yote yanayotarajia kufanya mitihani ya Taifa.

Aidha, amewataka wanafunzi kuzingatia ratiba ya masomo inayotolewa ili wasikose vipindi vinavyorushwa kwenye redio,runinga na mitandao ya kijamii.

Jafo alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utaratibu wa masomo kwa njia ya runinga,redio na mitandao ya kijamii.

Alitaka taassi hizo kuangalia utaratibu huo wa marejeo kwa madarsa mengine kama kidato cha pili,cha nne,darasa la saba na la nne ili nao wawe na umahiri katika kujibu mitihani yao.

Alisema Serikali kupitia wadau mbalimbali imetoa fursa hiyo muhimu ambayo inapaswa kuzingatiwa na watu wote wakiwemo wazazi,walimu na wanafunzi wenyewe.

"Niwatake wanafunzi wote hasa wa kidato cha sita ambao sasa maandalizi ya kufanya marejeo yanafanyika,tutumie fursa hii vizuri ya kujiandaa kwa utaratibu mpya utakaotumika kuanzia mwaka huu wa kupima umahiri tofauti na ule wa awali wa kuulizana maswali tuliouzoea,"alisema Jafo.

Aliongeza kuwa "Wanafunzi tumieni fursa hii iliyoletwa kwenu,zingatia ratiba,jipimeni uwezo wenu ili wenzio wasikuache nyuma pindi mkirudi shuleni,someni kwa bidii kwa maana tunataka kuelekea kwenye Taifa lenye uchumi imara."

Aliwataka walimu kutumia fursa hiyo kujijengea uwezo wao wenyewe pia lakini kuwawezesha kuwa na uelewa zaidi ili wanafunzi wao watakapohitaji msaada pale watakapokwama wawe wanajua nini kinachoendelea.

"Walimu wetu najua mtu huwezi kuwa mkamilifu kwenye maeneo yote,kwa upande wenu hii pia ni fursa ya kujijengea uwezo kupitia walimu waliopo kwenye program hii ili ukirudi shuleni unakuwa umeongeza kitu kipya,lakini mwanafunzi wako anaweza kukupigia simu ameshindwa kuelewa sehemu Fulani hivyo inakuwa rahisi kumuelewesha,"alisema Jafo.

Waziri Jafo alisema kama Waziri anayesimamia elimu ya awali,msingi na sekondari amefarijika kuanza kwa utaratibu huo na ni imani yake kuwa pengo la vijana waliokuwa wanakaa nyumba bila ya msaada wowote wa kimasomo linaenda kuzibika.

"Wazazi wapeni nafasi watoto wenu ya kushiriki vipindi vyote vinavyotolewa, inawezekana vipindi vinaendelea wewe mzazi umempa mtoto wako kazi nyingine anafanya hilo sio sahihi, toa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha watoto wanasoma na kufanya mazoezi yote yanayotolewa na walimu,"alisisitiza Jafo.

Jafo alivitaja vyombo vya habari ambavyo vinashiriki kikamilifu katika mpango huu wa ufundishaji wa vipindi kwa njia ya Televisheni na Radio kuwa ni TBC, ZBC, Azam Tv, Channel Ten, Clouds Fm, Global Tv, Gel Tv na Radio mbalimbali.

Pia aliwakumbusha wazazi na wanafunzi wote kuwa vipindi hivyo vitakua vinarushwa kupitia mtandao wa Youtube kwa ajili ya marudio ili kujenga uelewa zaidi.

"Mitandao ya Youtube itakayokuwa inarusha vipindi hivyo ni ya Baraza la Mitihani – NECTA, Taasisi ya Elimu Tanzania – TEA, Global Education Link – GEL, Global Tv, Azam Tv, ZBC TV na EATV" alisisitiza Jafo.

Alizipongeza taasisi zote binafsi zilizoshirikiana na Serikali kuhakikisha lengo lake linatimia katika kipindi hiki cha mpito cha ugonjwa wa Corona unaosababisha homa kali ya mapafu(COVID 19).

Alizataja Taasisi hizo kuwa ni Mawakala wa Vyuo Vikuu Nje ya Nchi yaan Global Education Link (GEL), UNESCO na Taasisi ya Elimu Solution.

JAMAA AWACHARANGA MAPANGA WAKWE ZAKE BAADA YA KUNYIMWA MKE


Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mwandu Chalya (75) na mke wake Gigwa Kwangu (70) wakazi wa kijiji cha Mwamasololo, kata ya Sekebugoro wilayani Kishapu wamenusurika kufa baada kukatwa na kitu chenye ncha kali 'panga' na mkwe wao 'Mkwilima' Masele Boniface akilipiza kisasi kwa sababu wamekataa asirudiane na mke wake aliyetengana naye kwa kupeana talaka mahakamani.



Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema tukio hilo limetokea leo Aprili 29,2020 majira ya saa nane usiku katika kitongoji cha N'halange, kijiji cha Mwamasololo, kata ya Sekebugoro, tarafa ya mondo, wilaya ya Kishapu. 

Amesema Mwandu Chalya (75) pamoja na mke wake aitwaye Gigwa Kwangu (70) wote wakazi wa Mwamasololo walijeruhiwa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za miili yao na mkwe wao 'Mkwilima' Masele Boniphace wakiwa wamelala ndani ya nyumba yao. 

"Chanzo cha tukio hili ni chuki /kulipiza kisasi baada ya wazazi wa mke wake aitwaye Emiliana Mwandu (31) mkazi wa Mwamasololo kumkataza kurudiana na Masele Boniface baada ya kutengana kwa kupeana talaka mahakamani mnamo tarehe 06/05/2019 kwa sababu za ukatili aliokuwa akifanyiwa na mtuhumiwa kwa kupigwa hadi kupoteza fahamu kipindi hicho 2019",ameeleza Kamanda Magiligimba. 

Amesema majeruhi wanapatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga na hali zao zinaendelea vizuri. 

Kamanda Magiligimba amesema mtuhumiwa alikimbia mara baada ya tukio hilo na juhudi za kumtafuta na kumkamata zinaendelea. 

Kamanda Magiligimba ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Shinyanga kuacha kabisa tabia ya kujichukulia sheria mkononi na inapotokea kutoridhika na maamuzi ya mahakama ni vyema kuchukua hatua ya kukata rufaa dhidi ya maamuzi ya mahakama badala ya kujichukulia sheria mkononi.

Museveni: Hakuna maambukizi ya ndani “visa vipya vinaletwa na Madereva wa Malori”



Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema hakuna maambukizi mapya ya ndani kwa siku nyingi Uganda na kusema huenda hiyo ina ashiria hakuna maambukizi tena ya corona au Watu wana virusi ila hawaugui , Museveni amesema  kwa mujibu wa Wataalamu wake kama Watu wana virusi na hawaugui ni jambo zuri kwakuwa wanapata kinga mwili na hata virusi vikiondoka vikarudi tena watapambana navyo.

"Bado tuna visa 79, wagonjwa wanapona kwa kasi hadi sasa wamepona 52 na hatuna kifo, visa vya ndani tumedhibiti kabisa, tuko vizuri, shida pekee kwa sasa ni visa vya nje vinavyoletwa na Madereva wa Malori, naambiwa Waganda wana hasira nao kweli, tusiwachukie jirani zetu"-MUSEVENI

Spika athibitisha kifo cha Ndasa ahairisha vikao vya bunge


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai leo Bungeni amethibitisha kwamba ni kweli Mbunge wa Sumve Richard Ndasa amefariki dunia.

"Bunge letu limepata msiba mwingine mkubwa wa kuondokewa na Mbunge mwenzetu, mbunge wa jimbo la Sumve, Richard Ndasa ambaye amefariki usiku wa kuamkia leo 29 April 2020 hapa Dodoma"

"Kufuatia msiba huo taratibu za mazishi zimeanza kufanyika, kwa siku ya leo hatutaendelea na kikao cha Bunge badala yake tutakuwa na maombolezo ya msiba wa mwenzetu aliyekua Mbunge wa Jimbo la Sumve kwa vipindi vitano" - Job Ndugai

Ni siku 8 zimepita toka Mbunge mwingine afariki dunia ambaye ni Mama Mch. Gertrude Rwakatare aliyefia Dar es salaam na kuzikwa na kwenye eneo la kanisa lake.

Rais Museveni “Dereva wa lori awe mmoja na asilale hotelini wala kwa mtu”



Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza hatua mpya za kudhibiti mienendo ya madereva wa malori yanayoingia nchini humo kutoka mataifa jirani baada ya zaidi ya madereva 20 kupatikana na ugonjwa wa Covid-19.

Mataifa ya Uganda na Kenya yamekuwa yakiwafanyia vipimo wa virusi vya corona madereva wa malori katika mipaka yao hali ambayo imesababisha foleni ndefu ya magari hayo yaliopiga foleni ndefu

Madereva na wasaidizi wao upande wa Kenya wamelalamikia jinsi walivyosubiri kwa siku kadhaa kufanyiwa vipimo vya Covid-19 kabla ya kuruhusiwa kuvuka mpaka wa kuingia Uganda.

Njia ya usafirishaji mizigo kutoka bandari ya Mombasa nchini Kenya ni muhimu sana katika usafirishaji wa bidhaa muhimu kama vile chakula na dawa hadi Uganda, Rwanda, Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo.

Lakini wasafirishaji wa mizigo hiyo sasa wanahofiwa huenda wakaeneza virusi vya corona katika kanda ya Afrika Mashariki.

Sasa Rais Museveni anasema hatua zaidi zitachukuliwa kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.

Hatua hizo ni pamoja na kila lori kuwa na mtu mmoja – dereva pekee yake ambaye hataruhusiwa kulala hotelini wala nyumbani kwa watu.

Bw. Museveni pia amesema mienendo ya madereva hao itachunguzwa

Katika hotuba yake kwa taifa usiku wa Jumanne Rais Museveni pia aliangazia kuongezeka kwa chuki dhidi ya madereva hao kutoka kwa baadhi Waganda ambao wanahofia wataleta maambukizi ya corona niching humo.

Museveni aliongeza kwamba kusitisha usafirishaji wa bidhaa itakuwa na athari kubwa lakini alikubali kuwa madereva hao ni tishio katika mapambano ya nchi hiyo dhidi ya corona ikitoa mfano wa janga la Ukimwi la miaka ya 1980 na miaka ya tisini wakati ambapo madereva wa malori katika kanda hiyo waliaambukiza watu virus vya HIV katika kila miji waliyopitia wakiwa safarini.

Official Lynn na Tanasha Donna Walikuwa Kama PAKA na Panya Kisa, Lynn Kujiita "JIKE SIMBA"


Chanzo Cha Msanii na Video Vixen Jina Official Lynn KutoKua na Maelewano Mazuri na Tanasha Licha ya TanashaDonna Teyari Amesha Achanana na DiamondPlatnumz, Mpka Leo Hii TanashaDonna na OfficialLynn ni Kama Paka na Mbwa, Endapo Wakikutana Sehemu Yoyote Basi Lazima Wazichape.

Chanzo Ilikua Baada ya Liynn Kupata Show Mbali Mbali za Ku Perform Mikoani na Wasafi Festival, Show Yake ya Kwanza, Mwanza Ilizuiliwa Baada ya LYNN Kupost Picha na Kuandika Caption Yenye Maelezo Ya "JIKE SIMBA"

Hapo Sasa ndipo Kizai Zai kilipo Aanza, Baada ya Muda Mfupi Ile Post Ilifutwa Haikuonekana Tenaa Baada ya TanashaDonna Kufanya Yake, Kwa Nini Ajiandike "JIKE SIMBA"? Yeye ni Nani Kwani?

Baada Ya Tukio Hilo Kufanyika, Siku ya Trh 1/11/2019 Mwaka Jana, Tulimuona Tena OfficialLynn Kupata Show ya Wasafi Festival Ilio Fanyika Mtwala/Tandahimba na Ndio Ilikua Show Yake ya Kwanza Kufanya, "Kapuni" Haijulikani ni Kwa Nini LYNN Alizuiliwe Kufanya Show na Ikiwa alichaguliwa, Wambea Wasema Kua LYNN Alikwenda Kumuomba Msamaa Tanasha na Ndio Maana Mpka Leo Hii Lynn Alitumii Hili Jina la Kujiita "JIKE SIMBA" Nakupata Nafasi ya Kufanya Show.

Mtangazaji DIVA Loveness Abadili Mwelekeo...Ukitaka Kunioa Njoo na Bilioni 1.5

Diva

Diva Loveness aachi vituko, baada ya kutrend sana week mbili hizi zilizopita baada ya kutangaza kuwa alikuwa kwenye uhusiano wa siri wa kimapenzi na Ali Kiba, Sasa Mrembo huyo ametangaza kuwa atakaye taka kumua aje na Bilioni 1.5 Kama mahari

Mwanzoni Diva Alisema yeye ili akubali kuolewa lazima mwanaume aje na dau la milioni Mia tano, kwa sasa dau limepanda zaidi

Idadi ya waliofariki kutokana na virusi vya corona Uturuki yapungua


Idadi ya watu  amabo wamekwishafariki kutokana na virusi vya corona Uturuki yapungua  kwa kiasi cha kuridhisha na kuonesha matumaini.

Ndani ya masaa  24 watu  92 ndio ambao wameripotiwa kufariki.

Idadi ya watu  waliofariki kwa virusi vya corona imefikia watu  2992.

Watu  5018 wamepona virusi  hivyo hatari  na kufikia watu  38 809.

Tuesday, April 28, 2020

NEW AUDIO:Rosa Ree Feat. Rayvanny - Sukuma Ndinga Remix



NEW AUDIO:Rosa Ree Featuring Rayvanny - Sukuma Ndinga Remix

DOWNLOAD HERE

Bonyeza Play Hapa Chini Kusikiliza:

Ligi kuu ya Ufaransa yafutwa

Ligi Kuu ya nchini Ufaransa maarufu kama Ligue 1 pamoja na ile Ligue 2 zimefutwa baada ya waziri mkuu wa nchi hiyo Edouard Philippe kutangaza hakutakua na michezo hata ile itakayofanyika bila mashabiki kabla ya mwezi septemba.

KARIBU EKIE SHINYANGA CAR WASH CENTRE



Karibu Ekie Shinyanga Car Wash Center ipo
 Lumambo ya old Shinyanga karibu na  Japanese kona/ Tanganyika bar . Wasiliana nasi kwa simu namba 0678 863 605



Source

Wagonjwa wa corona kenya wafikia 374


Wizara ya Afya Kenya imesema wagonjwa wengine 11 wa corona wameongezeka leo na kufanya jumla ya visa vya corona kufikia 374 kutoka 363

"wagonjwa wengine kumi wamepona na hii inafanya idadi ya waliopona Kenya kufikia 124 kutoka 114"

ALIYESAMBAZA WHATSAPP TAARIFA YA UONGO KUHUSU CORONA AKAMATWA MBEYA...NI ILE YA MABLANKET YA WAGONJWA WA CORONA CHINA


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia JOYCE KEPHAS AKYOO @ MANKA [31] Mfanyabiashara na Mkazi wa Stereo Jijini Mbeya kwa tuhuma za kusambaza taarifa za uongo kuhusu ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu [COVID 19] katika Mtandao wa Kijamii.

Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 27.04.2020 majira ya saa 13:30 Mchana baada ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kufanya msako huko eneo la Stereo lililopo Kata ya Manga, Tarafa ya Sisimba, Jijini Mbeya.

Ni kwamba mnamo tarehe 30.03.2020 majira ya saa 14:09 Mchana mtuhumiwa alituma taarifa za uongo na zenye lengo la kupotosha kuhusiana na ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu kwenye kundi "Fans of Mwailubi Car Wash" katika mtandao wa WhatsApp kwa kuweka picha za marobota ya nguo akieleza kwa maandishi na kwa sauti baada ya kujirekodi akisema "Mablanket ya Wagonjwa wa Corona ambao wamefariki nchini China na nguo hizo zinaletwa barani Afrika na ugonjwa wa Corona" Mtuhumiwa aliendelea kuongea na kuandika akitahadharisha watu wasikubali msaada huo.

Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Tangu kuanza kwa Janga la Homa Kali ya Mapafu [COVID 19] na kutangazwa kama Janga la Dunia, Serikali kupitia Wizara ya Afya na Viongozi wakuu wa Nchi ndio wamekuwa wakitoa taarifa kuhusiana na ugonjwa huo pamoja na namna ya kujikinga dhidi ya maambukizi yake, hata hivyo Serikali imekuwa ikitoa makatazo mbalimbali kwa wananchi kuacha kutoa taarifa za kupotosha umma na kusubiri kupata taarifa kutoka vyanzo sahihi.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kuimarisha ulinzi katika maeneo yote ya mpaka wa Tanzania na Malawi, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, maeneo ya Karantini na kudhibiti magari ya kubeba abiria kwa kuwataka kupakia abiria kulingana na siti zilizopo [level seat].

Pia elimu inaendelea kutolewa kwa Wananchi katika maeneo mbalimbali namna ya kujikinga na ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona [COVID 19] na kuwataka wananchi kufuata maelekezo yanayotolewa na Viongozi Wakuu wa Nchi, Wataalamu na Wizara ya Afya ikiwemo kuvaa barakoa, kuepuka mikusanyiko, kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono [Sanitizer].

Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


Atiwa Mbaroni Jijini Mbeya Kwa Kusambaza Taarifa za Uongo Kuhusu Corona

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia JOYCE KEPHAS AKYOO @ MANKA [31] Mfanyabiashara na Mkazi wa Stereo Jijini Mbeya kwa tuhuma za kusambaza taarifa za uongo kuhusu ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu [COVID 19] katika Mtandao wa Kijamii.

Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 27.04.2020 majira ya saa 13:30 Mchana baada ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kufanya msako huko eneo la Stereo lililopo Kata ya Manga, Tarafa ya Sisimba, Jijini Mbeya.

Ni kwamba mnamo tarehe 30.03.2020 majira ya saa 14:09 Mchana mtuhumiwa alituma taarifa za uongo na zenye lengo la kupotosha kuhusiana na ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu kwenye kundi "Fans of Mwailubi Car Wash" katika mtandao wa WhatsApp kwa kuweka picha za marobota ya nguo akieleza kwa maandishi na kwa sauti baada ya kujirekodi akisema "Mablanket ya Wagonjwa wa Corona ambao wamefariki nchini China na nguo hizo zinaletwa barani Afrika na ugonjwa wa Corona" Mtuhumiwa aliendelea kuongea na kuandika akitahadharisha watu wasikubali msaada huo.

Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Tangu kuanza kwa Janga la Homa Kali ya Mapafu [COVID 19] na kutangazwa kama Janga la Dunia, Serikali kupitia Wizara ya Afya na Viongozi wakuu wa Nchi ndio wamekuwa wakitoa taarifa kuhusiana na ugonjwa huo pamoja na namna ya kujikinga dhidi ya maambukizi yake, hata hivyo Serikali imekuwa ikitoa makatazo mbalimbali kwa wananchi kuacha kutoa taarifa za kupotosha umma na kusubiri kupata taarifa kutoka vyanzo sahihi.

Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kuimarisha ulinzi katika maeneo yote ya mpaka wa Tanzania na Malawi, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, maeneo ya Karantini na kudhibiti magari ya kubeba abiria kwa kuwataka kupakia abiria kulingana na siti zilizopo [level seat].

Pia elimu inaendelea kutolewa kwa Wananchi katika maeneo mbalimbali namna ya kujikinga na ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona [COVID 19] na kuwataka wananchi kufuata maelekezo yanayotolewa na Viongozi Wakuu wa Nchi, Wataalamu na Wizara ya Afya ikiwemo kuvaa barakoa, kuepuka mikusanyiko, kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono [Sanitizer].

Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


VIDEO: Idadi ya maambukizi ya wagonjwa wa corona yaongezeka


TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI...USISAHAU KU SUBSCRIBE

Mtoto wa jaji Augustino Ramadhani afunguka kifo cha baba yake

Mtoto wa kiume wa Jaji Mstaafu wa Tanzania Augustino Ramadhani, Yakud Ramadhani ameeleza kifo cha Baba yake huyo na kusema kuwa alikuwa anasumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu, ambapo pia hata kabla ya mauti kumfika aliwahi kwenda kutibiwa nchini Kenya.

"Ni kweli amefariki leo mida ya saa 2 asubuhi, alikuwa Aga khan na baadaye akaenda Kenya kwa matibabu zaidi na baadaye akarudi nyumbani lakini akawa bado anaumwa, sasa hivi wana familia wanafanya taratibu kwa chochote kitakachotokea tutawajuza" amesema Yakud.


Aidha kwa upande wa taarifa zilizotolewa na Mahakama ya Tanzania zimeeleza kuwa Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani, amefariki Dunia leo saa mbili asubuhi katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.

TANZIA: Jaji Mkuu Mstaafu, Augustino Ramadhani afariki dunia

Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Augustino Ramadhani amefariki dunia leo asubuhi katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar baada ya kuugua maradhi ya moyo.

Familia yake imesema hali ya Jaji Ramadhani ilibadilika jana usiku na kukimbizwa hospitalini hapo ambapo mauti ilimkuta leo asubuhi.
 
Jaji Augustino Ramadhani pia alikuwa Brigedia Jenerali kabla ya kuitwa katika sekta ya Sheria na kutumikia Mahakama.

Alipostaafu ujaji, alipewa kazi ya ukasisi, akatawazwa rasmi kuwa Mchungaji wa Dayosisi ya Kanisa la Anglikana lililopo Mkunazini Zanzibar na hivyo kuitwa "Mchungaji Augustino Ramadhani"


TANZIA:Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Augustino Ramadhan amefariki Duni


Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Augustino Ramadhan amefariki Duni leo saa 2 asubuhi katika Hospitali ya Agha Khan DSM baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Marehemu Jaji Ramadhan alishawahi kutumikia nafasi mbalimbali na kupata vyeo vya juu kiwemo kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tanzania Bara na Visiwani mwaka 2002 hadi 2007, pia Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar kipindi hichohicho.

Pia ni Brigedia Jenerali ambapo alilitumikia Jeshi na hadi anafariki alikuwa ni Mchungaji wa Dayosisi ya Kanisa la Anglikana lililopo Mkunazini Zanzibar, Mstaafu Ramdhani aliwahi pia kuwa Jaji Mkuu Zanzibar.
#RIPMzeeWetu🙏

Breaking: Jaji mkuu mstaafu Augustino Ramadhani afariki dunia


Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Augustino Ramadhani amefariki dunia leo majira ya saa mbili asubuhi katika Hospitali ya Aga Khan Jijini Dar es salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu

Jaji Ramadhani ni Mtanzania wa kwanza kushikilia kiti cha Urais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu tangu kuanzishwa kwa Mahakama hiyo

Monday, April 27, 2020

Billnass Awatamani Cassper, Drake!



MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, William Lymo 'Billnass' amesema anatamani kufanya kolabo na wasanii kama Cassper Nyovest na Drake.

Akizungumza na Mikito Nusunusu, Billnass amesema kuwa, amekuwa akitamani kufanya kazi na Cassper Nyovest kutoka Afrika ya Kusini na Drake kutoka Marekani ambao wote ni marapa walio na heshima kubwa.

"Mimi naimba na kuchana na nimekuwa nikiwatazama sana wasanii kama Cassper na Drake, kwani wanaujua muziki wa kuchana na wanafanya vizuri sana, natamani siku moja nifanye nao kazi," alisema Billnass.

STORI: Happyness Masunga

Serikali yapokea msaada wa shilingi bilioni 14.9


Serikali imepokea msaada wa shilingi bilioni 14.9 kutoka Global Fund, Airtel Tanzania, Rotary Club Tanzania ambazo sehemu kubwa zitatumika kununua vifaa kinga kwa watumishi wa afya na vifaa tiba kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wenye maambukizi ya COVID-19.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameyasema hayo leo wakati akipokea msaada wa fedha na lita 1,250 za vitakasa mikono ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali za kupambana na maambukizi ya virusi vya Corona.


Waziri Ummy amefafanua kwamba Global Fund imetoa shilingi bilioni 14, Airtel Tanzania shilingi milioni 700 na Rotary Club Tanzania shilingi milioni 250.

"Tumepokea shilingi bilioni 14 kutoka Global Fund, shilingi bilioni 9.6 tumezitoa kwa ajili ya kununua vifaa kinga kwa ajili ya watumishi wa Afya, lakini pia fedha zilizotolewa na Airtel na Rotary Club Tanzania tutazielekeza huko. Kipaumbele chetu ni kuwalinda watumishi wa afya," amesema Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.

"Natumia fursa hii kuwashukuru watumishi wa afya ambao wamekuwa wakijitoa usiku na mchana katika kutoa huduma kwa watu waliopata maambukizi ya virusi vya Corona (Covid-19) pamoja na wale wahisiwa.

"Kipaumbele cha Serikali ni kuwalinda watumishi wa Afya kwa kununua vifaa kinga kwani fedha tulizozipata hapa tutazielekeza kwenye ununuzi wa vifaa kinga. Niendelee kuwaisistiza Watumishi wa Afya wazingatie miongozo ya magonjwa ya kuambukiza," Amesema Waziri Ummy .

Amesema watumishi wa afya ambao wamepatiwa mafunzo katika vituo vya kutoa huduma kwa wenyr maambukizi ya ugonjwa huo, hakuna aliyepata maambukizi kwa kuwa wanazingatia miongozo ya Serikali ya kutoa matibabu kwa wagonjwa wa Covid-19 pamoja na miongozo ya magonjwa ya kuambukiza.

Waziri amesema ushiriki wa kila mdau katika mapambano dhidi ya maambikizi ya virusi vya Corona ni muhimu na kwamba msaada uliotolewa na kampuni hizo ni mkubwa katika mapambano ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

"Napenda kurudia tena kwa niaba Mhe. Rais Dkt. John Magufuli, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, nawashukuru Airtel Tanzania, Serengenti Breweries na Rotary Club kwa hiki mlichotupatia. Asanteni sana," amesema Waziri Ummy.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Airtel Tanzania, Bw. Gabriel Malata amesema Airtel Tanzania imetoa shilingi milioni 700 ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali za kupambana na janga la Corona.

"Sisi bodi ya wakurugenzi wa Airtel na kwa niaba ya Airtel Tanzania, tunatambua juhudi za Serikali katika kupambana na ugonjwa wa Corona, lakini pia tumejitathimini na kutambua kuwa sisi kama Airtel hatuwezi kuendelea bila kuwepo watu wanaotumia huduma zetu. Watu hawa ndio mtaji wa Kampuni," amesema Bw. Gabriel.

Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kampuni ya Bia ya Serengenti, Bw. John Wanyancha amesema kuwa kampuni hiyo imetoa lita 1,250 ya vitakasa mikono nyenye thamani ya shilingi milioni 15 kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za Serikali za kupambana na maambukiza ya virusi.

Mwenyekiti wa Rotary Club, Bi. Agnes Batenga amesema Rotary imetoa shilingi milioni 250 kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa homa ya mapafu (COVID-19).

"Shilingi milioni 183 zitatumika kutoa msaada wa vifaa vya kujikinga (PPE), vifaa vya maji safi ambavyo vitasambazwa katika vituo maalumu vya kuhudumia wagonjwa wa Corona jijini Dar es Salaam, Hospitali ya Amana, Zanzibar, Hospitali ya Mawenzi na Hospitali ya Mount Meru," amesema Bi. Agnes.

Amesema shilingi milioni 67 zitatumika katika kutekeleza miradi ya kudhibiti ugonjwa wa Corona nchini kupitia Club za Rotary.

Mwana FA "Huyu Mdudu Alining'ang'ania Sana, Nimekaa Siku 28 Isolation"


"Nimekaa siku 28 kwenye isolation, nimepimwa mara 8 hadi kupatikana negative, mara zote nilizopimwa nilikuwa napatikana positive na ukipatikana positive wanakaa masaa 72 hadi kukupima tena! Naweza kusema ni kama huyu mdudu alining'ang'ania" -: @MwanaFA


New Zealand yatangaza kuangamiza virusi vya corona


New Zealand inasema kwamba imezuia maambukizi ya Covid 19 katika jamii hatua ambayo inamaanisha kwamba wameangamiza virusi hivyo.

Huku wagonjwa wapya wachache wakiripotiwa katika siku kadhaa - mmoja siku ya Jumapili - Waziri mkuu Jacinda Ardem amesema kwamba virusi hivyo vimeangamizwa kabisa.

Lakini maafisa wameonya dhidi ya kupunguza kasi dhidi ya virusi hivyo, wakisema kwamba haimaanishi kwamba visa vya ugonjwa huo vimeisha kabisa.

Habari hiyo inajiri saa chache kabla ya New Zealand kuondoa masharti yake makali ya kukaribiana miongoni mwa raia wake.

Kuanzia Jumanne , biashara zisizo na muhimu mkubwa , huduma za Afya na elimu zinatarajiwa kufungua milango yake tena.

Watu wengi hatahivyo watatakiwa kusalia majumbani kila wakati na kuzuia kukaribiana.

"Tunaufungua uchumi , lakini haturuhusu mikusanyiko ya watu'' , bi Arden alisema katika hotuba hiyo ya serikali ya kila siku kwa umma. News Zealand imeripoti chini ya wagonjwa 1,500 na vifo 19 .

Mkurugenzi mkuu wa Afya nchini New Zealand Ashley Bloomfield alisema kwamba wagonjwa wachache wanaoripotiwa katika siku za hivi karibuni wanatupatia motisha kwamba tunaafikia lengo letu la kuangamiza ugonjwa huu.

Mahakama Kuu Yatupilia Mbali Kesi ya Tundu Lissu Kupinga Kuvuliwa Ubunge

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kwa mara ya pili, imetupilia mbali maombi ya aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ya kujaribu kupinga uamuzi wa kuvuliwa ubunge.

Maombi hayo yalitupwa mwishoni mwa wiki mbele ya Jaji Yose Joseph Mlyambina, baada ya kukubaliana na pingamizi la awali lililowasilishwa na jopo la mawakili kutoka ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.

"Baada ya kusikiliza hoja za mapingamizi na majibu, mahakama inakubaliana na hoja za Serikali na inaona  maombi hayana msingi kisheria  kwa kuwa sheria hairuhusu rufaa kwa kesi inayofafana na hiyo,"alisema.

Katika maombi hayo namba 42 ya mwaka 2019 ya kutaka ridhaa ya Mahakama Kuu kumruhusu kukata rufaa yaliyofunguliwa Oktoba 10, 2019,Tundu Lissu alikusudia kupinga uamuzi wa yeye kuondolewa ubunge kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kanuni za Kudumu za Bunge kutokana na kushindwa kuhudhuria vikao zaidi ya vitatu vya Bunge pasipo ruhusa ya maandishi ya Spika.

Maombi hayo yalipingwa vikali na mawakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali kwa madai hayakustahili kusikilizwa kwa kuwa yalikinzana na kifungu cha 5(2) cha Sheria ya Rufani kama ilivyorekebishwa na Sheria ya Marekebisho ya Sheria Na. 25 ya mwana 2002.

Upande wa Serikali, ulidai Lissu hakuwa na haki kisheria kupinga uamuzi wa Jaji Sirilius Matupa ulitolewa Septemba 9, mwaka jana wa kumnyima ridhaa kufungua shauri la mapitio ya kiutawala uamuzi ambao uliishia kwa yeye kupoteza  ubunge.

Ilielezwa na mawakili wa Serikali, uamuzi wa Jaji Matupa haukupaswa kupingwa kwa njia ya rufaa kwa  kuwa uamuzi huo haukumaliza shauri kama inavyopaswa kisheria.

Upande wa Serikali uliishawishi mahakama katika kesi mbalimbali, Mahakama iliamua kuwa rufaa haiwezi kukatwa kwa shauri ambalo limeisha katika hatua za awali kama ilivyokuwa kwa kesi ya Lissu ambaye alikuwa akiomba ridhaa ya kuwasilisha maombi ya mapitio na akanyimwa ridhaa kwa kuwa maombi yake hayakuzingatia Sheria.


Daimond kuwalipia kodi za nyumba kaya 500, ataja utaratibu

Staa wa muziki nchini Nasibu Abdul maarufu kama Diamond Platnumz, amesema kuwa atachangia 'kodi ya pango' kwa kaya 500 nchini kwa ajili ya kupunguza makali ya kiuchumi kwa Watanzania katika kipindi hiki cha janga la corona

Leo katika mahojiano na wasafi FM amesema kuwa ameguswa na hali ya sasa na njia moja ya kuunga jitihada za Rais Magufuli kwakuwa watu wamekwama kwenye biashara zao na suala la kodi ni changamoto kubwa kwa watu wengi.

"Najua katika kipindi hiki cha Corona, mambo mengi hayajakaa sawa, hususani upande wa biashara, nyingi zimeshuka na kupelekea hali ya kifedha kuyumba na mambo kuwa kidogo magumu kwa wengi wetu... na mimi ni miongoni mwa walio ndani ya janga hili" alisema daimond.

Daimond aliendelea kusema kuwa wamejipanga ili kuhakikisha figisu hazitakuwepo na tutatumia serikali za mitaa pamoja na timu yetu ambayo itapita mitaani ili kuwafikia walengwa kama wamama wajane, walemavu na wale wote wenye mahitaji kweli na kila mkoa sitaenda katika familia tazo na asilimia kubwa itakuwa hapa Dar es salaam.

 "Misukumo ya kusaidia watu , imetokana na malezi niliyolelewa, maisha niliyotokea na historia yangu ya nyuma. Nikikumbuka shida nilizopitia , napata Moyo wa kusaidia Wengine "

Kuhusu kiwango kipi cha kodi atakacholipia daimond amesema kuwa inategemea kwakuwa mwanzo mwingine alikuwa anaweza kulipa laki laki mbili kwa mwezi lakini kwa sasa amekwama kweli huyo ni lazima asaidiwe.


Tanzia: Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evord Mmanda afariki Dunia





Source

Watanzania wengine wanne wakutwa na virusi vya corona Uganda




Wizara ya Afya Uganda imesema Watanzania wengine wanne (Madereva wa Malori) wamebainika kuwa na virusi vya corona nchini humo na kufanya visa vya corona Uganda kufikia 79, Madereva hao walioingia Uganda kupitia mpaka wa Mutukula ni kati ya ya Watu 1989 waliopimwa jana Uganda.

"Tumewapima Watu 1989 ambapo Madereva wa Malori ni 1578 na kati yao Watanzania wanne wamebainika kuwa na corona, wengine 411 tuliowapima sio Madereva na wote ni wazima"
OPEN IN BROWSER

WATU Wengi Hawamuelewi NYOKA Ndio Maana Wanapanic ,Chukua Tahadhari Hizi Pindi Uking'atwa

Wengi wakimuona nyoka wanaanza kukimbia ,kupiga makelele.Nani kakuambia kuna nyoka ambaye akimuona mtu anaanza kumkimbiza.

Nyoka sio simba au chui ambao tabia zao wakimuona mtu ambaye ni kitoweo kwao wanaanza kumkimbiza kwa nia ya kumla.Kwa nyoka la hasha hakuna nyoka wa aina hiyo awe venomous au non venoumous.Nyoka huwakimbiza rodents tu kama panya sababu ni kitoweo chao.



Watu hawamtizami nyoka kama kiumbe wa porini Bali humtizama kama vile kitu kibaya hilo ndio tatizo.

Nyoka pekee ni kiumbe namba moja ambaye watu humuelewa sivyo ndivyo Africa,hivyo ni mnyama anayeongoza kuuliwa kikatili

Nyoka hupata attention mbaya sababu ya stori ambazo watu husikia pale mtu anapong'atwa

Kung'atwa kwingi panatokea pale mtu anapojaribu kumzuru nyoka na kiumbe huyo anajaribu kujitetea

Majira ya kiangazi nyoka hujificha sana chini ya mawe,miamba majani au kwenye miti kukaa mbali na joto la jua

Mida ya jioni hujitokeza kwa wingi na usiku wakati hali ya joto ipo chini hushamili kwa wingi

Nyoka wadogo sumu yao sio hatarishi sana kama nyoka wakubwa.Mfano Brown snake kila akiwa mzee sumu yake ndio inakuwa kali zaidi


Njia nzuri ya kufanya pindi ukimuona nyoka mwache pekee yake usimbughudhi labda kama atahatarisha maisha ya watoto

Utajiingiza kwenye matatizo pindi ukimsogelea na kuanza kumrushia fimbo ,nyoka ataamua kujilinda na kujilinda kwao ni kutafuta timing ya kukugonga ila kabla ya kufanya hivyo atakupa alarm ya kufungua mdomo wake na kurudi nyuma.

Endapo mtu aking'atwa na nyoka yafuatayo ni yakufanya.

1.Mtulize mgonjwa awe katika hali ya utulivu,asipanic sababu akipanic atasababisha moyo uende mbio hivyo msukumo wa damu utakuwa wa kasi na hivyo kurahisha usambaaji wa sumu kwenda kwenye moyo

2.Kama nyoka yupo sehemu husika usimuue au kumkamata

3.ondoa vitu vyote kwenye mwili wa mgonjwa ambazo zinazuia mzunguko wa damu kama saa,mkanda ,Pete, viatu sababu vitaweza kumletea matatizo

4.safisha eneo lililong'atwa ila usichue au kusugua sababu itaweza kusababisha sumu iliyo nje iweze kuingia.

5.Mzuie ngonjwa asitembee hovyo na mbebe mgonjwa sababu ukimuacha atembee sumu itasambaa kwa kasi sana

6.Funga bandage na weka pressure kwa juu


7.Mchukue mgonjwa na mpeleke kwenye hospitali ya karibu haraka iwezekanavyo lakini kwa kipando


Usimpe chakula chochote au maji mgonjwa haswa pombe

Usiweke barafu kwenye sehemu iliyong'atwa

Usikate sehemu iliyong'atwa na kufyonza hakuna uthibitisho wa kisayansi unaosema hivyo pia hiyo njia inaweza kumletea madhara anayefonza

Usimpe pain killers mgonjwa au dawa yeyote ilei


Mwisho itolewe elimu kwa wachungaji na wakulima na haswa watoto wanaotumwa kuchunga mifugo

Kuna stori ya kusikitisha ilitokea Zimbabwe miaka 3 iliyopita kijana mmoja wa umri wa miaka 13 alikuwa anasoma darasa la 7 moja ya masiku alikuwa anachunga mifugo pamoja na wadogo zake 2 ,katika hali ya taharuki Nyoka aina ya black mamba alimgonga kijana yule mkononi sababu kijana yule alikatiza kwenye mti ambao black mamba alikuwa amejituliza baada ya kung'atwa wadogo zake walimuambia waende nyumbani wakawaeleze wakubwa wao kilichotokea lakini kijana yule alikataa alisema ni nyoka wa kawaida na hali ni ya kawaida akachukua kitambaa na kujifunga na wakaendelea kuchunga.Haikupita muda mrefu 30mins kijana yule akawa anasikia kizunguzungu na kudai haoni na anasikia ugumu kupumua na inavyoelezwa ngozi ya kijana yule ikawa inabadilika rangi na kuwa nyeusi wale wadogo Zake wakambeba kumrudisha nyumbani lakini ikawa too late .kifo cha mtoto yule kilivuta hisia ya watu wengi

Hivyo elimu kubwa itolewe kwa wakazi wa vijijini ,wakulima ,wafugaji njia ya kutumia mawe asilimia ,kukata na kuanza kufyonza sio sahihi.

By undefine
Source

WAZIRI BITEKO AZINDUA VIWANDA VIWILI VYA MFANO VYA UCHENJUAJI WA DHAHABU STAMICO WAKABIDHIWA RASMI



WAZIRI wa Madini Doto Biteko katikati akijiandaa kukata utepe hafla ya uzinduzi wa viwanda hivyo vya Mfano


Waziri wa Madini, Doto Biteko akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kilipojegwa kiwanda cha kuchenjua dhahabu bila kutumia kemikali ya zebaki cha Katente wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho uliofanyika tarehe 26 Aprili, 2020



Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila akiongea jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa viwanda vya kuchenjua dhahabu vya Katente na Lwamgasa uliofanyika Katente mkoani Geita tarehe 26 Aprili 2020


Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idrisa Kikula akizungumza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha kuchenjua dhahabu cha Katente wilayani Bukombe mkoani Geita tarehe 26 Aprili, 2020

Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Stamico Lucas Seleli akizungumza jambo mara baada ya uzinduzi na makabidhiano ya Viwanda viwili vya uchenjuaji wa Madini ya dhahabu kisichotumia kemikali ya zebaki vilivyoko Katente na Lwamgasa mkoani Geita







Viongozi wa Serikali kuanzia kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel akifuatiwa na Waziri wa Madini, Doto Biteko, Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila na mwisho ni Mshauri mwelekezi aliyesimamia ujenzi wa viwanda vya kuchenjua dhahabu Rogers Sezigwa wakiendelea na ukaguzi wa kiwanda hicho kabla ya kukikabidhi rasmi kwa Shirika la Madini la Taifa (Stamico)

Mtaalamu wa kuendesha mitambo ya uchenjuaji wa dhahabu kwa kutumia teknolojia ya Kisasa Gabriel Masanyiwa  akitoa maelezo ya hatua zinazopitiwa mpaka kupata dhahabu
Waziri wa Madini, Doto Biteko (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Geita mara baada ya hafla ya uzinduzi na makabidhiano ya kiwanda cha kuchenjua dhahabu cha Katente na Lwamgasa Mkoani Geita. Kiwanda hicho kimekabidhiwa kwa Shirika la Madini la Taifa (Stamico) ili kukisimamia na kukiendesha.



Waziri wa Madini, Doto Biteko amelitaka Shirika la Madini la Taifa (Stamico) kusimamia ipasavyo Viwanda vya Mfano vya Uchenjuaji wa madini ya dhahabu vya Katente-Bukombe na Lwamgasa-Geita alivyovizindua leo APRIL 26 na kuvikabidhi rasmi kwa shirika la Stamico..


Ujenzi wa viwanda hivyo visivyotumia kemikali hatari ya zebaki ulifanywa na kampuni ya Tan Discovery MineralConsaltancy Limited inayosimamiwa na Rogers Sezigwa iliyoanza ujenzi wa mradi mwezi Disemba, 2016 ikianziaLwamgasanakufuatianaKatentenaItungi- Chunya.



Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa viwanda hivyo vya Mfano,Waziri Biteko amesema, itakuwa aibu kubwa kwa Stamico endapo Viwanda hivyo vitafia mikononi mwao kwani Serikali imetumia gharama kubwa katika ujenzi wa viwanda hivyo.



"Afe Kipa, afe beki ni lazima viwanda hivi vifanye kazi" Biteko alisisitiza.



Aidha,Waziri Biteko amewahakikishia wananchi na wachimbaji wadogo wa madini nchini kuwa, serikali ya Rais John Magufuli inawajali na itawahudumia kwa gharama nafuu hivyo wasisite kupeleka mawe kiwandani hapo ili waweze kuchenjuliwa dhahabu kwa kutumia teknolojia mpya na ya kisasa na hivyo kuepuka kutumia zebaki na kuachana na utumiaji wa matimba kwenye mashapo.



Amesema matumizi ya matimba wakati wa uchimbaji yanasababisha uharibifu wa mazingira wakati zebaki huathiri afya za wachimbaji hivyo waitikie na kuvitumia viwanda hivyo kwa faida zao.



"Tumetengeneza viwanda hivi kuwavutia ninyi fanyebiashara" Biteko alisisitiza.



Pamoja na hayo, Waziri Biteko alimtaka Mwenyekiti wa Bodi ya Stamico kuhakikisha wanasimamia ipasavyo miradi hii pasipo kucheka na watu wasiotimiza wajibu wao kwenye viwanda hivyo.



Sambamba na hayo amewataka Bodi pamoja na Stamico kuhakikisha wananchi wanaozunguka viwanda hivyo wananufaika na uwepo wa viwanda katika maeneo yao kwa kupata ajira ndogo ndogo kwa kufanya hivyo kutainua uchumi wao.



Akizungumzia faida zitokanazo na uwepo wa viwanda hivyo vya mfano, Waziri Biteko alisema ni pamoja na utoaji wa mafunzo na maarifa kuhusu sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali kwa wachimbaji wadogo, kutolewa elimu ya mfumo wa kuthamini mashapo ya madini yaliyopo ilikufanya uchimbaji wenye tija, kuchenjua dhahabu pamoja na kukodishwa vifaa vinavyotumika katika shughuli za uchimbaji kwa gharama nafuu pamoja na kutolewa elimu juu ya uongezaji thamani madini na upatikanaji wa masoko.



Akizungumzia mchakato wa ujenzi wa viwanda hivi vya mfano, Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Augustine Ollal amesema, ujenzi huo nimatokeo ya Utekelezaji wa Sera ya Madini ya mwaka 2009 iliyosisitiza zaidi juu ya uendelezaji wa sekta ya madini hususani wachimbaji wadogo.



Amesema katika kutimiza azma hiyo, Serikali ilianzisha mradi wa Usimamizi Endelevu wa Rasilimali Madini (SMMRP) uliokuwa na awamu mbili, ya kwanza ni kuanzia 2009 hadi 2014 na awamu ya pili mwaka 2015 hadi 2018 ambapo awamuya pili ya mradi ndipo viwanda vitatu vya mfano vya uchenjuaji wa dhahabu vya Katente- Bukombe, Lwamgasa- Geita na Itumbi –Chunya vilipoanza kujengwa baada ya kufanyika kwa utafiti wa kijiolojia chini ya ushirikiano baina ya uongozi wa mradi, Stamico, Taasisi ya Utafiti na Jiolojia Tanzania (GST) na wachimbaji wadogo.



Akizungumzia gharama ya ujenzi wa viwanda hivyo Ollal alisema mradi wa Katente umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.7 na Lwamgasa umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.3 wakati mradi wa Itumba Uligharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.7 na hivyo kufanya miradi yote kutekelezwa kwa kiasi cha shilingi bilioni 4.7.



Ollal ameongeza kuwa, uwepo wa tekinolojia hii kwa wachimbaji wadogo itakuwa na manufaa kama vile; kupunguza kwa kiasi kikubwa ajali migodini kwa kutumia sementi katika kuimarisha kuta, kurahisisha utoaji wa mbale mgodini(Haulage system) kupunguza athari za kimazingira kwa kutokata miti hovyo na kurahisisha ufungaji wa migodi.



Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara y aMadini, Prof. Simon Msanjila amelitaka Shirika la Madini la Taifa (Stamico) kuisaidia jamii inayozunguka viwanda hivyo vya mfano kuondokana na changamoto ya maji kwa kuchimba kisima kiwandani hapo na kuiruhusu jamii kunufaika na huduma hiyo.



Aidha, Prof. Msanjila amewataka Stamico kutoa nafasi za ajira kwa wananchi kutokana na ukweli kwamba wao ndio walinzi wa viwanda hivyo. "Nitashangaa sana kuona wafanyakazi wakawaida wanatoka km 200 kutoka hapa wakati kijiji kimezungukwa na vijana mahiri na wachapa kazi" alisistiza Prof. Msanjila.



Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel ametoa wito kwa watendaji na wasimamizi wa vituo hivyo kuwa wazalendo katika usimamizi wa Viwanda hivyo vya uchenjuaji wa dhahabu.



Sanjari na hilo, ameelezea mikakati ya mkoa wake kuelekea maonesho ya Tekinolojia ya uchimbaji wa madini kwa mwaka huu kuwa ni pamoja na mkoa wake kuandaa uwanja maalum kwa ajili ya maonesho hayo ambapo tayari ujenzi wa jengo la ofisi mbalimbali ikiwepo ya wataalamu wa Sekta ya madini umefanyika.



Mkuu wa Mkoa ametoa wito kwa wataalamu na timu nzima ya Ujenzi wa viwanda hivi kushiriki kikamilifu katika maonesho hayo ili kuachilia utaalamu wao kwa watanzania wengine wenye nia ya kujiendeleza kupitia sekta ya Madini.


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...