Thursday, April 30, 2020

Watu milioni 30 wanaomba mafao ya kupoteza kazi Marekani

Zaidi ya wafanyakazi milioni 3.8 walioondolewa kazini wameomba mafao ya kutokuwa na kazi wiki iliyopita wakati uchumi wa Marekani ukiporomoka zaidi katika mzozo ambao umekuwa wenye athari kubwa zaidi tangu miaka ya 1930.

Takriban watu milioni 30.3 wamejiandikisha kupata msaada wa kutokuwa na kazi katika wiki sita tangu kuzuka kwa virusi vya corona na kulazimisha mamilioni ya waajiri kufunga milango yao na kupunguza wafanyakazi.

Hawa ni watu wengi zaidi kuliko wanaoishi mjini New York na Chicago kwa jumla, na kwa kiwango kikubwa ni wimbi baya zaidi la watu kuachishwa kazi kuliko wakati mwingine.

Wakati waajiri wengi wanapunguza matumizi kwa kuwaachisha kazi wafanyakazi , wataalamu wa uchumi wanatabiri kwamba kiwango cha ukosefu wa ajira kwa Aprili kinaweza kwenda juu zaidi hadi asilimia 20.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...