Tuesday, September 22, 2026
MBUNGE AZZA AWATAKA WANANCHI KULINDA MIUNDOMBINU MIRADI YA MAJI, ATOA PESA KUNUNUA KOKI ZILIZOIBWA
Saturday, September 19, 2026
Trump: Nitafanya uamuzi mzito wa kuanzisha upya mashambulizi makubwa dhidi ya Iran
Jarida la Axios limemnukuu mwandishi wake, Barack Ravid, akisema kuwa Rais wa Marekani Donald Trump anasema yuko karibu kufanya uamuzi mzito kuhusu kuanzisha upya mashambulizi makubwa dhidi ya Iran.
Kulingana na Axios, Donald Trump alisema katika mazungumzo ya simu na Bw. Ravid: "Nina uamuzi mkubwa mbele yangu. Je, nichukue hatua na kuwaangamiza [serikali ya Iran] au la? Ni uamuzi mkubwa. Chaguzi zote zipo mezani."
Kauli hizi zinakuja wakati Rais wa Marekani akitarajiwa kukutana na viongozi wa Saudi Arabia, Falme za Kiarabu (UAE), Qatar, Bahrain, Kuwait, na Oman siku ya Jumanne, pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa jijini New York; mkutano unaotarajiwa kujikita katika mustakabali wa mzozo na Iran.
Bw. Trump anasema ana mpango wa kutumia mkutano huo kutathmini misimamo ya mataifa ya Ghuba kabla ya kuamua hatua zake zinazofuata.
Alimwambia Barak Ravid: "Nataka kujua hali yao (nchi za Ghuba) ikoje. Siku zote tumekuwa tukiwaunga mkono na kuwalinda."
Wakati huo huo, ripoti zinaonyesha kuwa Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Pete Hegseth, ameviagiza vikosi vya Marekani katika Mashariki ya Kati kujiandaa kikamilifu kwa uwezekano wa kurejea kwenye mapigano makali kabla ya mwisho wa mwaka.
Alipoulizwa ikiwa ana mpango wa kukutana na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, jijini New York wiki ijayo, Bw. Trump alisema: "Huenda."
Tuesday, September 15, 2026
IDEA: Uhuru wa vyombo vya habari na mahakama umeshuka Marekani
Taasisi ya Kimataifa ya Demokrasia na Usaidizi wa Uchaguzi (IDEA) imesema viashiria vya demokrasia ya Marekani, ikiwemo uhuru wa vyombo vya habari na mahakama, vimefikia kiwango cha chini zaidi katika kipindi cha miaka 50 iliyopita.
Ripoti hiyo imeonya kuwa hali hiyo imewapa nguvu viongozi wenye misimamo mikali na tawala za kiimla duniani.
IDEA pia imeeleza kuwa kupungua kwa imani katika mfumo wa uchaguzi wa Marekani kumeendelea kuwa na athari kwa demokrasia katika mataifa mengine.
Friday, September 11, 2026
Korea Kusini Yatoa Msimamo Juu ya Usalama wa Mlango Bahari wa Hormuz
Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini, Cho Hyun, amemweleza mwenzake wa Iran kwamba Korea Kusini inaunga mkono hatua za kuhakikisha meli zinaweza tena kupita kwa usalama katika njia hiyo muhimu ya kimkakati.
Korea Kusini bado haijafanya uamuzi kuhusu iwapo itatuma vifaa au vikosi vya kijeshi katika Mlango-Bahari wa Hormuz, Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini Cho Hyun amemweleza mwenzake wa Iran, Abbas Araghchi.
Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kusini, kama ilivyoripotiwa na Yonhap News, Cho Hyun alieleza msimamo wa nchi hiyo wakati wa mazungumzo ya simu na Araghchi siku ya Ijumaa. Amesisitiza umuhimu wa kurejesha uhuru wa usafiri wa meli kupitia njia hiyo ya kimkakati haraka iwezekanavyo.
Mawaziri hao wawili wamejadili hali ya Mashariki ya Kati, ikiwemo suala la kuruhusu meli kupita Mlango-Bahari wa Hormuz, wakati huo huo Korea Kusini inakabiliwa na shinikizo kutoka Marekani la kujiunga na operesheni za kijeshi dhidi ya Iran.
Cho Hyun alieleza “wasiwasi mkubwa” kuhusu hali ya kikanda na akatoa wito wa kurejeshwa kwa amani na utulivu wa kudumu.
Amesema Korea Kusini imekuwa ikisisitiza mara kwa mara kwamba usafiri huru na salama wa meli zote kupitia Mlango-Bahari wa Hormuz lazima uhakikishwe.
Shinikizo kutoka Iran na Marekani kwa Korea Kusini
Mazungumzo hayo yalifanyika baada ya Iran kuionya Korea Kusini dhidi ya kujiunga na operesheni za kijeshi za Marekani dhidi ya Iran.
Katika siku za hivi karibuni, Korea Kusini imetoa taarifa kadhaa ikisema kwamba bado haijafanya uamuzi kuhusu kutuma vikosi vyake katika Mlango-Bahari wa Hormuz.
Cho Hyun na Araghchi wamezungumza kwa njia ya simu mara sita tangu kuanza kwa vita hivyo.
Korea Kusini ni mshirika wa Marekani chini ya mkataba wa ulinzi, na kwa mujibu wa Rais wa Marekani Donald Trump, nchi hiyo ina takribani wanajeshi 39,000 wa Marekani wanaowekwa katika Rasi ya Korea.
Wakati huohuo, Korea Kusini inakabiliwa na shinikizo linaloongezeka kutoka Marekani la kuipa Ukraine mifumo ya kuzuia makombora yenye uwezo unaolingana na Patriot, ambayo imetengenezwa nchini Korea Kusini, kwa mujibu wa gazeti la JoongAng Daily.
Ukraine imekuwa katika vita na Urusi tangu nchi hiyo ilipoanzisha mashambulizi yake makubwa nchini humo mwaka 2022.
Tuesday, September 8, 2026
Chama avunja ukimya 'nipo tayari kuweka hadharani mazungumzo yote'
Mchezaji wa Simba SC, Clatous Chama, amevunja ukimya na kutoa onyo kwa watu anaodai wameanza kuvuka mipaka kupitia mijadala inayoendelea kwenye mitandao ya kijamii.
Chama amesema amekuwa kimya kwa muda wa kutosha, lakini sasa baadhi ya watu wameanza kwenda mbali zaidi, akisisitiza kuwa mitandao ya kijamii ina ukweli na pia kuna watu wanaozungumza kwa lengo la kutafuta umaarufu, ‘likes’ na maoni.
Mchezaji huyo amesema kusimama na kusema ukweli hakupaswi kutafsiriwa vibaya au kutumiwa dhidi yake, akidai kuwa ana ukweli pamoja na ushahidi wa kile anachokizungumza.
Ameongeza kuwa endapo ataona chapisho lingine likitolewa dhidi yake, yuko tayari kuweka hadharani mazungumzo yote aliyofanya na wahusika
Saturday, September 5, 2026
KABLA YA PENSHENI DAIMU SALUM MKWAWA ATOA SOMO LA KUWEKEZA MAPEMA KWA AJILI YA MAISHA BAADA YA KUSTAAFU
Hii ndio Royal Woodbridge Hotel iliyojengwa na kuwekezwa na mstaafu Daim Salum Mkwawa Hotel hii ipo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma mkabala na stendi ya Seedfarm njia inayokwenda Songea-Tunduru-Lindi
Muonekano wa ndani wa Hotel ya Royal Woodbridge iliyopo Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma inayomilikiwa na Daimu Salum Mkwawa 
Hapa ni eneo la kupatia chai na chakula katika Hotel ya Royal Woodbridge iliyopo Seedfarm Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma
Na Regina Ndumbaro Songea-Ruvuma
Kustaafu kutoka kwenye ajira hakumaanishi mwisho wa uzalishaji au mchango wa mtu katika uchumi wa nchi, bali kunaweza kuwa mwanzo wa hatua nyingine ya maisha endapo mtumishi ataandaa mapema shughuli za kiuchumi zitakazomsaidia baada ya kuondoka kazini.
Hilo ni miongoni mwa masomo yanayoweza kupatikana katika safari ya Daimu Salum Mkwawa, msomi na mwanazuoni aliyewahi kufanya kazi katika taasisi mbalimbali za Serikali na baadaye kuhudumu katika Umoja wa Mataifa (UN) kwa miaka 18.
Mkwawa, ambaye sasa ni mstaafu, anasema umuhimu wa kujiandaa kwa maisha baada ya kustaafu haupaswi kuanza siku mtu anapomaliza ajira, bali unapaswa kuanza mapema wakati bado ana nguvu, kipato na uwezo wa kupanga maisha yake ya baadaye.
Anaeleza kuwa yeye mwenyewe alianza kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo tangu mwaka 1992, wakati bado akiwa katika ajira, ikiwa ni pamoja na miradi aliyoianzisha Dar es Salaam.
Safari yake ya kikazi ilimfikisha katika Wizara ya Kilimo na Kiwanda cha Sukari Kilombero, ambako anasema alipata pia uzoefu wa namna ya kutengeneza sukari.
Katika upande wa elimu, amesoma katika vyuo mbalimbali, vikiwemo Sokoine University of Agriculture (SUA) na Chuo Kikuu cha Manchester nchini Uingereza, kabla ya kuendelea na safari yake ya kitaaluma na kikazi.
Mwaka 1996, alifanya kazi na Umoja wa Mataifa hapa nchini kwa kipindi cha miaka 18, akihudumu kwa ukaribu zaidi na Serikali za Mitaa.
Baada ya mkataba wake nchini Tanzania kumalizika, Mkwawa anasema Umoja wa Mataifa ulimpa fursa ya kuendelea kufanya kazi nje ya nchi kutokana na uzoefu na umahiri aliokuwa ameonesha kazini.
Hata hivyo, aliamua kubaki Tanzania. Sababu mojawapo ilikuwa uwekezaji aliokuwa ameanza kuujenga nchini, pamoja na kuzingatia familia na umri ambao ulikuwa umeendelea kusogea.
Uamuzi huo ulimfanya aendelee na safari yake ya ujasiriamali, ikiwemo uwekezaji katika sekta ya hoteli.
Moja ya uwekezaji huo ni Royal Woodbridge Hotel, iliyopo Kata ya Seedfarm, Manispaa ya Songea, Mkoa wa Ruvuma.
Kwa Mkwawa, uwekezaji huo siyo tu shughuli ya kibiashara, bali ni sehemu ya namna mstaafu anaweza kuendelea kutumia uzoefu, mtaji na maarifa aliyoyapata katika maisha ya ajira kwa ajili ya kujenga uchumi wake na kuchangia uchumi wa jamii inayomzunguka.
Hoteli hiyo kwa sasa ina vyumba 20, ikiwa na matarajio ya kufikia vyumba 30, pamoja na mpango wa kuwa na eneo la kuogelea na ukumbi wa mikutano.
Pamoja na kutoa huduma za malazi, uwekezaji huo umewezesha ajira kwa vijana wa kike na wa kiume, huku hoteli ikinunua bidhaa za chakula kutoka kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wa sokoni.
Kwa namna hiyo, shughuli za hoteli zinakuwa sehemu ya mnyororo wa kiuchumi unaowaunganisha mmiliki wa biashara, wafanyakazi, wakulima, wafanyabiashara wa masoko, wasambazaji wa bidhaa na Serikali kupitia mapato mbalimbali.
Mkwawa pia anasisitiza umuhimu wa rasilimali watu katika sekta binafsi, akisema wafanyakazi wanahitaji mafunzo ya mara kwa mara ili kuongeza uwezo wao na kuhakikisha wageni wanapata huduma bora.
Huduma zinazopatikana katika hoteli hiyo ni pamoja na chakula, usalama ndani na nje ya eneo la hoteli, CCTV camera, Wi-Fi ya bure, parking ya magari, restaurant na kifungua kinywa cha bure kwa wageni wanaolala hotelini hapo.
Pia, hoteli hiyo ina mazingira yanayovutia kwa ajili ya kupiga picha, hali ya hewa inayovutia na vyumba vinavyolenga kutoa viwango vya huduma vinavyolingana na thamani ya fedha anayolipa mgeni.
Mkwawa anasema usalama, chakula bora, malazi yenye viwango na huduma zinazokidhi mahitaji ya wageni ni sehemu muhimu ya uwekezaji katika sekta ya utalii na ukarimu.
Kwa upande mwingine, anaitaja Serikali kama mshirika muhimu katika mafanikio ya wafanyabiashara, akipongeza ushirikiano uliopo baina ya Serikali na sekta binafsi.
Anaiomba Serikali kuendelea kuangalia mazingira ya wafanyabiashara, hususan biashara changa, wakati wa ukusanyaji wa kodi, ili kuwe na mazingira ambayo Serikali inapata mapato na mfanyabiashara anaendelea kufanya biashara yenye faida na endelevu.
Kwa maoni yake, Serikali inapaswa pia kuwa mshauri wa wafanyabiashara na kuwasaidia kufikia huduma za mikopo kwa urahisi zaidi.
Mchango wa uwekezaji huo unaonekana pia katika mapato ya Serikali kupitia Manispaa ya Songea na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), huku ajira na ununuzi wa bidhaa kutoka kwa wajasiriamali wa eneo hilo ukiendelea kuongeza mzunguko wa fedha katika uchumi wa Songea.
Mkwawa anasema uzoefu wake ni ushahidi kwamba maandalizi ya maisha baada ya kustaafu yanaweza kufanyika hatua kwa hatua, badala ya kusubiri mtu aondoke kazini ndipo aanze kutafuta shughuli ya kumuingizia kipato.
Kwa wastaafu na watumishi wanaokaribia kustaafu, simulizi hii inaweza kuwa ukumbusho wa umuhimu wa kuanza mapema kupanga maisha ya baada ya ajira, ikiwa ni pamoja na kuwekeza katika shughuli halali na endelevu kulingana na uwezo na utaalamu wa mtu.
Hatua hiyo inaweza kusaidia kupunguza utegemezi wa pensheni pekee na kumwezesha mstaafu kuendelea kuwa mzalishaji, mwajiri na mshiriki wa shughuli za maendeleo katika jamii.
Kwa upande wa Mkoa wa Ruvuma, Mkwawa anasema uwekezaji katika huduma za malazi na biashara nyingine unaweza kusaidia kuongeza uwezo wa Songea kuhudumia wageni kutoka ndani na nje ya nchi.
Royal Woodbridge Hotel, iliyopo katika Kata ya Seedfarm, Manispaa ya Songea, kando ya barabara kuu ya Songea–Tunduru–Lindi, ni miongoni mwa uwekezaji unaoonesha namna sekta binafsi inavyoweza kushiriki katika kutoa huduma, ajira na kuchochea shughuli za kiuchumi.
Mkwawa anawakaribisha wananchi wa Mkoa wa Ruvuma, mikoa jirani ya Tanzania pamoja na wageni kutoka nje ya nchi wanaofika Songea kutumia huduma zinazopatikana katika hoteli hiyo na kujionea wenyewe namna huduma zinavyotolewa.
Pia anasema hoteli hiyo inawezesha usafiri wa ndani ya Mkoa wa Ruvuma kwa wageni wanaohitaji huduma hiyo.
Ujumbe mkubwa unaotokana na safari yake ni kwamba maandalizi ya kustaafu yanapaswa kuanza kabla ya kustaafu. Kwa mtumishi mwenye uwezo na mpango, ajira inaweza kuwa chanzo cha mtaji wa kuanzisha uwekezaji wa baadaye, huku uzoefu wa kazi ukiwa rasilimali muhimu katika kusimamia biashara na kutoa mchango zaidi kwa jamii.
Kwa Taifa, simulizi kama hii inaendelea kuonesha umuhimu wa kuimarisha mazingira ya uwekezaji wa ndani ili wastaafu, wafanyakazi na wajasiriamali waweze kutumia maarifa, uzoefu na mitaji yao kujenga biashara, kutoa ajira na kuongeza shughuli za uzalishaji nchini.










BANDARI YA DAR ES ALAAM KUPANUA UWEZO KUPITIA MIRADI MIKUBWA
Thursday, September 3, 2026
Iran yashambulia kambi za kijeshi za Marekani Kuwait
Kumekuwa na ripoti za mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani za Iran kwenye kambi za Marekani huko Kuwait
Saa moja baada ya jeshi la Kuwait kutangaza katika taarifa kwamba mifumo yake ya ulinzi wa anga ilikuwa imeshirikishwa ili kurudisha kutungua mashambulizi ya ndege zisizo na rubani na makombora yanayotoka Iran, shirika la habari la Tasnim, karibu na Walinzi wa Mapinduzi, liliandika: "Kambi za Marekani huko Kuwait zilishambuliwa na makombora na ndege zisizo na rubani za Iran."
Shirika la habari halikutoa maelezo zaidi kuhusu tukio hilo, na CENTCOM - Amri Kuu ya jeshi la Marekani - bado haijajibu ripoti hizo.
Udhibiti mkali katika nchi za Ghuba ya Uajemi umefanya iwe vigumu sana kwa vyombo vya habari kupata ufikiaji wa moja kwa moja kwenye maeneo yaliyoshambuliwa, na Marekani imeweka vikwazo kwenye uchapishaji wa picha za setilaiti za maeneo haya.
Siku ya Jumatano, Tasnim ilichapisha picha za angani zinazohusishwa na mashambulizi yake ya Jumanne kwenye kambi za Marekani huko Jordan, ikidai kuonyesha athari zilizoachwa na mashambulizi haya.
-
Rais Uhuru Kenyatta na viongozi wengine nchini Kenya wametuma salamu zao za rambi rambi kwa familia ya marehemu Yusuf Haji. Rais Uhuru Kenya...
-
WATU saba wamefariki dunia baada ya bajaji waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na lori eneo la Mpemba, Tunduma wilayani Momba, mk...
-
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe asomewa mashtaka matatu ya uchochezi, yenye nia ya kuleta ch...
-
MWANA-mfalme wa Uingereza,. Prince Charles, ambaye ni mtoto wa kwanza wa Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza, na mrithi wa kwanza katika ...
-
Vijana wametakiwa kuwa wazalendo katika nchi yao kwa kukemea vitendo viovu katika jamii na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha Sil...
-
Mfanyabiashara raia wa Kenya, Raphael Ongangi anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana maeneo ya Oysterbay, Dar es Salaam nchini Tanzania am...
-
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko amefunga rasmi mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa maaskofu na wachungaji wa makanisa ya...
-
Zikiwa zimesalia siku chache tu Hoteli Mpya ya Kisasa yenye Ubora wa hali ya juu 'SHY PARK HOTEL' ifunguliwe Rasmi mwezi Agosti 202...
-
Ng'wana Kang'wa ameachia Album Mpya inaitwa MBINA ... Ngoma zote zipo https://www.youtube.com/@ngwanakangwa .. Hii hapa ngoma inai...
-
Mara nyingi wanawake wamekuwa watu wa kukaa kimya bila kusema wanataka nini ili kuridhishwa katika mapenzi na mbaya zaidi katika swala zima ...











