Tuesday, September 8, 2026

Chama avunja ukimya 'nipo tayari kuweka hadharani mazungumzo yote'


Mchezaji wa Simba SC, Clatous Chama, amevunja ukimya na kutoa onyo kwa watu anaodai wameanza kuvuka mipaka kupitia mijadala inayoendelea kwenye mitandao ya kijamii.

Chama amesema amekuwa kimya kwa muda wa kutosha, lakini sasa baadhi ya watu wameanza kwenda mbali zaidi, akisisitiza kuwa mitandao ya kijamii ina ukweli na pia kuna watu wanaozungumza kwa lengo la kutafuta umaarufu, ‘likes’ na maoni.

Mchezaji huyo amesema kusimama na kusema ukweli hakupaswi kutafsiriwa vibaya au kutumiwa dhidi yake, akidai kuwa ana ukweli pamoja na ushahidi wa kile anachokizungumza.

Ameongeza kuwa endapo ataona chapisho lingine likitolewa dhidi yake, yuko tayari kuweka hadharani mazungumzo yote aliyofanya na wahusika

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...