Taasisi ya Kimataifa ya Demokrasia na Usaidizi wa Uchaguzi (IDEA) imesema viashiria vya demokrasia ya Marekani, ikiwemo uhuru wa vyombo vya habari na mahakama, vimefikia kiwango cha chini zaidi katika kipindi cha miaka 50 iliyopita.
Ripoti hiyo imeonya kuwa hali hiyo imewapa nguvu viongozi wenye misimamo mikali na tawala za kiimla duniani.
IDEA pia imeeleza kuwa kupungua kwa imani katika mfumo wa uchaguzi wa Marekani kumeendelea kuwa na athari kwa demokrasia katika mataifa mengine.
