Monday, March 3, 2025

WALIYOYAPAMBANIA WANAWAKE WENZETU MATUNDA YAKE TUNAYAONA - MBUJA


πŸ“Œ Asema Wizara ya Nishati inalo la kujivunia kutokana na uwepo wanawake katika nafasi za uongozi.

***

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano  Serikalini Wizara ya Nishati,  Neema Mbuja amesema kile ambacho wanawake walikipambania  katika majukwaa mbalimbali ikiwemo ya Kimataifa ili kuwa na  haki, usawa na uwezeshaji kwa wanawake matunda yake yanaonekana hivi sasa.

Mbuja ameyasema hayo alipokuwa akieleza safari ya mwanamke katika kudai haki, usawa na uwezeshaji kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo nchini kitaifa yatafanyika mkoani Arusha.

"Wanawake wengi walipambana kuhakikisha kunakuwepo na usawa wa kijinsia, usawa wa utendaji kazi na ushiriki katika nafasi mbalimbali za uongozi na tangu kufanyika kwa Mkutano wa Beijing  mwaka 1995 mambo yote ya usawa kwa sasa yanaonekana kwa vitendo",amesema Mbuja.

Ameeleza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imekuwa kinara katika kuhakikisha haki kwa mwanamke inapatikana.

Ameongeza  kuwa, Wizara ya Nishati inajivunia kwa uwepo wa wanawake katika nafasi mbalimbali za uongozi.


 


Source

KATAMBI AKEMEA WATUMISHI WA SERIKALI KUPANDISHA MABEGA




Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu,amekemea baadhi ya Watumishi wa Serikali kupandisha Mabega na kutoa huduma mbovu kwa wananchi.

Amebainisha hayo leo Marchi 2,2025 wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Kambarage kwenye mkutano wa hadhara, wa kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

Amesema kwenye maeneo ya kutolea huduma za wananchi,yamekuwa yakilalamikiwa sana na wananchi kuwa na huduma mbovu,kutokana na baadhi ya Watumishi kupandisha Mabega.
"Kwenye mikutano yangu nimekuwa nikipokea kuwapo kwa huduma mbaya kwenye hospitali zetu, na leo nimepokea tena malalamiko katika shule ya Msingi Kambarage, nawaomba Watumishi wa Serikali fanyeni kazi kwa uaminifu msipandishe Mabega kwa wananchi wahudumieni vizuri,"amesema Katambi.


"Watumishi wenye lugha chafu kwa wananchi,na wapandisha Mabega hatuwataki hapa Shinyanga,Mheshimiwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan anahangaika kutafuta fedha kuboresha huduma za afya na elimu, lakini kuna Watumishi wachache wanataka kumkwamisha hilo sikubaliani nalo,"ameongeza.
Aidha,akizungumzia mambo ya maendeleo kwenye Kata hiyo ya Kambarage,kuwa wameboresha huduma za Afya katika kituo cha Afya Kambarage, ikiwamo upatikanaji wa vifaa tiba vya kisasa na sasa wanajenga uzio.


Amesema pia kwa sasa ujenzi unaendelea wa barabara kiwango cha Lami kwenye Kituo hicho cha Afya Kambarage na pia hivi karibuni watajenga Soko kubwa la kisasa.
Awali wananchi wa Kambarage wakiwasilisha kero kwa Mbunge Katambi,akiwamo Suzana Balele wamelalamikia Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kambarage, kuwa ana nyanyasa wazazi kwa kuwatolea lugha chafu,pamoja na kuwaambia wahamishe watoto katika shule nyingine kuwa shule imejaa na wakitaka kumpatia ushauri ana waambia wasimfundishe kazi.


Mwananchi Mwingine Pili Shija,amelalamikia wazazi wanapokwenda kujifungua kwenye Kituo cha Afya Kambarage, hua wanatozwa pesa kuanzia sh.300,000 mpka 600,000 kwa wale wa huduma za upasuaji,na wakati serikali ilishasema huduma za uzazi ni bure.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Peres Kamugisha,awali akitoa majibu kwenye mkutano huo, amekiri kwamba huduma uzazi ni bure na kwamba hata yeye ameshitushwa kusikia wanatozwa pesa na kwamba atalifuatilia.


Akijibu juu ya Malalamiko ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kambarage nalo amesema atalifuatilia sababu lipo kinidhamu zaidi na siku ya jumanne atampatia majibu Mbunge katika juu ya hatua ambayo itachukuliwa.
Mbunge Katambi ameendelea na ziara yake ya Kata kwa Kata, ambapo leo alikuwa Kata ya Lubaga na Kambarage, kesho atakuwa Kata ya Ndala na Masekelo.


TAZAMA PICHAπŸ‘‡πŸ‘‡
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu akizungumza na wananchi wa Kata ya Kambarage.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Peres Kamugisha akitoa majibu kwenye mkutano kujibu kero za wananchi.
Wananchi wakiuliza maswali na kutoa kero zao.

Sunday, March 2, 2025

UWT KYERWA KUFANYA KONGAMANO LA KUMPONGEZA RAIS SAMIA

 

Na Lydia Lugakila - Kyerwa

Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera unatarajia kufanya kongamano maalum la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan  kwa namna alivyosimamia miradi mbalimbali ya Maendeleo hapa nchini.

Kauli hiyo imetolewa Katibu wa Umoja  wa Wanawake Tanzania UWT Wilaya ya  Kyerwa kutoka chama cha Mapinduzi CCM Bi, Sekunda Silidioni kwa niaba ya Katibu wa chama hicho Wilaya  katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.

Sekunda amesema kuwa Rais Samia amepambana sana katika kuwaletea Maendeleo Watanzania hivyo wao kama UWT wameamua kufanya kongamano hilo maalum la kumpongeza litakalofanyika Marchi 4,2025 katika kata ya Nkwenda Wilayani Kyerwa ambapo amewaomba viongozi mbali mbali wa Wilaya hiyo wakiwemo Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa kuhudhuria kongamano hilo na kulipa ukubwa wa aina yake.

Aidha amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa pamoja na Watumishi wa Halmashauri hiyo kwa kazi wanazofanya kuhakikisha ilani ya  Chama cha Mapinduzi CCM inatekelezwa kwa asilimia kubwa.

Sekunda amempongeza pia Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Bahati Henerico kwa utendaji wake wa kazi ulisababisha mabadiliko makubwa na kufanya Wilaya hiyo inasonga mbele kwa kipindi cha miaka mitano.

Hata hivyo amempongeza mbunge wa Jimbo la Kyerwa Innocent Bilakwate kwa kuisemea vizuri  Wilaya hiyo hadi kupata miradi mikubwa ya Maendeleo

Rais Trump Amtaka Rais Zelensky Aombe Radhi Hadharani....





Rais wa Marekani Donald Trump amesema anataka Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amuombe radhi hadharani ndipo atakubali kurudisha upya uhusiano kati ya Marekani na Ukraine baada ya Viongozi hao wawili juzi kuzozana mbele ya Waandishi wa Habari katika Ikulu ya Marekani (White House) kitendo ambacho Trump anaamini Zelensky ameidharau Marekani.

Mtandao wa Bloomberg umeripoti kuwa Afisa mmoja wa Ulaya amevujisha taarifa kuwa baada ya malumbanonya Trump na Zelensky, Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer aliwapigia simu Viongozi hao wawili na kuwashawishi warejee mezani kumalizia maongezi lakini Trump alisema anahitaji aombwe radhi hadharani na Zelensky na pia nchi ya Marekani kwa ujumla iombwe radhi kwa kilichotokea.

Source

BALOZI NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA DK. SAM NUJOMA NAMIBIA


Picha mbalimbali zikimuonesha Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akishiriki shughuli ya mazishi ya kitaifa ya aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Namibia, Baba wa Taifa hilo na kiongozi wa mapambano ya kupata uhuru wa nchi hiyo, Dkt. Sam Shafiishuna Nujoma, yaliyofanyika katika eneo la makaburi ya mashujaa, jijini Windhoek, na kuhudhuriwa na maelfu ya waombolezaji, kutoka ndani na nje ya Namibia, wakiongozwa na Rais wa Namibia, Nangolo Mbumba, pamoja na viongozi wengine wa Chama na Serikali wa Namibia, tarehe 1 Machi 2025.

JACKLINE WOLPER aumwaga ukweli wote kuhusu sakata la ndoa yake, MWIJAKU aliniomba msamaha

 JACKLINE WOLPER aumwaga ukweli wote kuhusu sakata la ndoa yake, MWIJAKU aliniomba msamaha



Source

VIJANA WA KIKE FEDHA MNAZOPATA MZITUMIE PIA KATIKA UWEKEZAJI- MKURUGENZI UTAWALA NISHATI


πŸ“Œ Asema inaongeza  kujiamini


πŸ“Œ Asema Wizara ya Nishati inaiishi kaulimbiu ya  Siku ya Wanawake Duniani 2025

***

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Nishati,  Bi. Ziana  Mlawa ametoa rai kwa Vijana wa Kike kuwa fedha wanazopata watumie pia katika kufanya uwekezaji hali itakayowajengea uwezo  kujiamini zaidi ikiwemo katika maeneo ya kazi.


Bi. Mlawa ameyasema hayo alipokuwa akieleza kuhusu nafasi ya Msichana katika kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo nchini yatafanyika kitaifa mkoani Arusha.


" Pamoja na majukumu yetu tuliyokuwa nayo tukijiwezesha na sisi kwenye uwekezaji itatujengea sana kujiamini kwenye kufanya kazi, ukiwa na uhuru wa kifedha kujiamini kunaongezeka kwenye kazi yako." Amesisitiza Bi. Mlawa


Amesema Wizara ya Nishati inaitekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya "Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji" kwa namna mbalimbali ikiwemo suala la usawa kwani katika Wizara watumishi wanawake wapo 82 na wanaume 145 na kueleza kuwa kwa uwiano huo anaamini kauli mbiu hiyo imefanyiwa kazi.


Ameongeza kuwa hata kwa viongozi wa Menejimenti ya Wizara ambayo idadi yao ni 12 wanawake ni watano na wanaume ni 7.

 

Kocha Fadlu Ataja Mechi Mbili za Kuipatia Simba Ubingwa...




Kocha wa Simba Fadlu Davids amesema mechi mbili zijazo zinaweza kutoa picha halisi ya ubingwa kwa timu yake msimu huu.

Fadlu amesema kama watapoteza mechi hizo basi timu yake itakuwa imejiweka kwenye hatari kubwa ya kupoteza ubingwa, kwani itakuwa imepoteza pointi nyingi na itakuwa ngumu kumfikia aliyeko kileleni.

"Mechi kubwa zilizopo mbele yetu ni hizi za sasa dhidi ya Yanga na Coastal, hizi zingine tumeshamalizana nazo, lakini napata wakati mgumu kutokana na rekodi za mzunguko wa kwanza.

"Kwa sasa akili zipo katika mbio za ubingwa kwani bado ziko wazi na mwanga unaonekana ila tukifanya makosa mechi mbili zijazo nuru itazima kabisa.

"Hizi kwetu ni mechi zinazobeba ajenda ya ubingwa na hatutacheka nazo kabisa, kwani tunahitaji alama sita za nguvu zitakazotuweka katika nafasi nzuri." -Amesema Fadlu davids

Saturday, March 1, 2025

Jonathan Ikangalombo Silaha ya Maangamizi Kwa Ajili ya Kumuua Simba



Jonathan Ikangalombo ni shida nyingine katika ligi yetu. Ana speed, ana touch nzuri, anapiga chenga, akipata uwanja mzuri kama Benjamin Mkapa kuna mtu anaweza kutema ulimi, anatukumbusha enzi za Kisinda ila yeye anaonekana anayo finishing nzuri.

Hapa tunaambiwa hana match fitness yuko hivi, hiyo fitness ikikaa sawa itakuwaje? Naambiwa hajacheza mechi ya kiushindani kwa miezi minne sasa, inaogopesha sana. Huendi ni silaha ya maangamizi iliyohifadhiwa Kwa ajili ya kumtungua mtani Simba.

Yanga wamekuwa na jicho zuri sana la usajili kwa kipindi kirefu sasa na huu ni miongoni mwa sajili bora kabisa.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...