Jonathan Ikangalombo ni shida nyingine katika ligi yetu. Ana speed, ana touch nzuri, anapiga chenga, akipata uwanja mzuri kama Benjamin Mkapa kuna mtu anaweza kutema ulimi, anatukumbusha enzi za Kisinda ila yeye anaonekana anayo finishing nzuri.
Hapa tunaambiwa hana match fitness yuko hivi, hiyo fitness ikikaa sawa itakuwaje? Naambiwa hajacheza mechi ya kiushindani kwa miezi minne sasa, inaogopesha sana. Huendi ni silaha ya maangamizi iliyohifadhiwa Kwa ajili ya kumtungua mtani Simba.
Yanga wamekuwa na jicho zuri sana la usajili kwa kipindi kirefu sasa na huu ni miongoni mwa sajili bora kabisa.