Na Lydia Lugakila - Kyerwa
Kauli hiyo imetolewa Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT Wilaya ya Kyerwa kutoka chama cha Mapinduzi CCM Bi, Sekunda Silidioni kwa niaba ya Katibu wa chama hicho Wilaya katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo.
Sekunda amesema kuwa Rais Samia amepambana sana katika kuwaletea Maendeleo Watanzania hivyo wao kama UWT wameamua kufanya kongamano hilo maalum la kumpongeza litakalofanyika Marchi 4,2025 katika kata ya Nkwenda Wilayani Kyerwa ambapo amewaomba viongozi mbali mbali wa Wilaya hiyo wakiwemo Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa kuhudhuria kongamano hilo na kulipa ukubwa wa aina yake.
Aidha amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa pamoja na Watumishi wa Halmashauri hiyo kwa kazi wanazofanya kuhakikisha ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM inatekelezwa kwa asilimia kubwa.
Sekunda amempongeza pia Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa Bahati Henerico kwa utendaji wake wa kazi ulisababisha mabadiliko makubwa na kufanya Wilaya hiyo inasonga mbele kwa kipindi cha miaka mitano.
Hata hivyo amempongeza mbunge wa Jimbo la Kyerwa Innocent Bilakwate kwa kuisemea vizuri Wilaya hiyo hadi kupata miradi mikubwa ya Maendeleo