Sunday, March 2, 2025

Rais Trump Amtaka Rais Zelensky Aombe Radhi Hadharani....





Rais wa Marekani Donald Trump amesema anataka Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amuombe radhi hadharani ndipo atakubali kurudisha upya uhusiano kati ya Marekani na Ukraine baada ya Viongozi hao wawili juzi kuzozana mbele ya Waandishi wa Habari katika Ikulu ya Marekani (White House) kitendo ambacho Trump anaamini Zelensky ameidharau Marekani.

Mtandao wa Bloomberg umeripoti kuwa Afisa mmoja wa Ulaya amevujisha taarifa kuwa baada ya malumbanonya Trump na Zelensky, Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer aliwapigia simu Viongozi hao wawili na kuwashawishi warejee mezani kumalizia maongezi lakini Trump alisema anahitaji aombwe radhi hadharani na Zelensky na pia nchi ya Marekani kwa ujumla iombwe radhi kwa kilichotokea.

Source
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...